Mwaka 2014 nilipata safari ya kikazi Mbeya, Baada ya (TBA) kishindwa mradi wa soko la Mwanjelwa ilabidi tuingie mzigoni kukamilisha mradi huo.
Wakati tunaendelea na ujenzi huo ikatangazwa tender nyingine jengo la NHIF Baada ya kukidhi it vigezo tukapewa pia, kwaiyo muda wa kukaa Mbeya ukaongezeka.
Katika pitapita nikajikuta Kwenye mahusiano na bint mmoja wa ki safwa, bint kaenda hewani weusi kiasi alafu sio mtu wa maneno mengi, mapenzi yakapamba moto balaa,,,,,kwake nikawa naenda kama kwangu na yeye mda wowote kwangu anakuja.
Shida ikaanza project zilipokua mwishoni nikajiroga kumuaga mapema kwamba mda si mrefu nitaondoka Mbeya, ikawa ananisisitiza kwann nisibaki tu alafu nitafute kazi nyingine hukohuko sikukubaliana nae kwaiyo visa vikaanza nikaona hapa ishakua balaa Cha kufanya nianze kujiandaa na matukio mapema.
Siku hiyo nimeenda kumuaga rasmi kwamba kuchukua baadhi ya vitu vyangu namkuta kanuna hatari hata Salam hataki kuitikia nikaona isiwe tabu,, wakati niko ndani akatoka sikujua kaelekea wapi nimekusanya PC yangu na nguo chache zilizokuwepo pale nataka kutoka karudi ghafla kasimama mlangoni ananiambia huendi kokote.
Kumbe wakati katoka alienda kufunga geti kubwa la kuingilia ndan, basi mzee ikabidi niwe mpole bembeleza Sana somo halieleweki nikisema nitumie nguvu nitapita wapi na geti ashafunga basi ikabidi nijifanye nimekubali matokeo nikaacha vitu vyangu pale nikamwambia twende tukatafule chakula tukirudi tunalala kwake siku hiyo kweli akaelewa nikatoka akafungua geti hao mpaka cafe tumekula tukarudi hapo mm napiga hesabu tu nachomokaje pale,
Basi tumeru amesha relax geti karudishia tu coz kuna jamaa wa chuo nao walikua wamepanga mle ndan alafu wanarudi mida mibovu, kitendo Cha kuingia ndani tu nikachukua begi langu nikamwambia naondoka tutaonana kesho aisee aligeuka mbogo akanikwida kama mwizi nikaona Sasa heshima inapotea na mtu mwenyewe sio wa pole pole inabidi kula ushibe, ikabidi nitumie ubabe wa kiume, wakati kanikwida Kila nikimwambia aniachie hataki, hasira zikanipanda nikaona Sasa napata kesi mda si mrufu, nikampa kichwi kimoja matata San naona mtu kaniachia kujishika puani damu akatoka mbio pale akawahi getini alafu kaanza kupiga kelele kwamba kavamiwa nikaona Sasa kifo hiki hapa.
Haraka nikamuhi pale getin virangati lake sio kitoto mpaka napenya kutoka pale mbio shati limechanika nimefika sehemu kwanza pumzi ikakata ikabidi nikae chini tu nikaema kama wananifata potelea mbali, nimekaa pale kama dk10 hivi ndio naona afadhali, ikabidi nianze kuondoka taratibu naelekea home nakoishi, kitendo nafika tu naambiwa kuna watu kama wa nne hiv wamekuja kunitafuta alafu wameacha maagizo kwamba nikifika tu niende nilikofanya tukio wao wakirudi hawataki lawama.
Nikaona Sasa ishakua tabu kitu Cha kwanza nikawahi kituo kidogo Cha polisi Mwanjelwa pale nikaripoti nikapewa na rb yangu pale nikachukua na no, ya poti mmja pale in case of emergency nikaondoka nilivyorudi home sijakaa San namuona huyo kafika anagonga nifungue tukayamalize nnje nikamwambia Sina Cha kujadiliana nae kama kuna issue yote saiz Iko polisi so! Kesho saubuhi anahitajika kituoni na rb nimuonyesha ,,, ndo ikawa mwisho wa usumbufu..ila nilikoma sio kwa mbilinge lile..