Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinaendelea kumtafuta kada wake Hilda Newton aliyepotea tangu Alhamisi, Aprili 24, 2025, mara ya mwisho akionekana katika viunga vya Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam.
Kupitia mitandao ya kijamii, wanachama wa CHADEMA wameeleza wasiwasi wao, wakidai kuwa Hilda alikamatwa na Polisi akiwa mahakamani. Hata hivyo, taarifa rasmi ya Jeshi la Polisi iliyotolewa na Kamanda SACP Jumanne Muliro imetaja majina ya wanachama watano waliokamatwa, huku jina la Hilda likikosekana.
Soma, Pia: Jeshi la Polisi: Tuliimarisha na kuweka ulinzi mkali Kisutu kutokana na matishio ya kiusalama na vitendo vya uhalifu
Taarifa hiyo imeongeza sintofahamu na hasira miongoni mwa wafuasi wa CHADEMA, wakitaka maelezo ya kina kuhusu alipo Hilda, huku wengine waliokamatwa wakiripotiwa kupatikana wakiwa wamejeruhiwa vibaya pembezoni mwa jiji.