Ustadh Mtu
New Member
- Nov 27, 2011
- 3
- 0
Ni kweli kwamba sintaksia finyizi imekubalika na wataalam wengi kama nadharia ya ya lugha yenye uwekevu zaidi na bado inaendeleza malengo ya sarufi zalishi. Malengo haya ni kuandaa sarufi bia ya lugha ya mwanadamu pamoja na kutafuta uhusiano na taaluma nyinginezo za lugha kama vile fasihi, isimujamii miongoni mwa mengine. Hata hivyo, matumizi ya nadharia hii iliyoanzishwa na Noam Chomsky inahitaji kufafanuliwa kwa udhahiri zaidi na wanaisimu wa Kiswahili.