Single momz tunashida sana katika mahusiano

Single momz tunashida sana katika mahusiano

Status
Not open for further replies.
ukiona wanakukimbia, tatizo si mtoto peke yake, kuna jingine ...
Kwa wanaume wengi ambao hawajapata watoto ni ngumu sana kuoa mwanamke mwenye mtoto na mara nyingi tatizo kubwa ni mtoto na si kingine. Of coz exceptions zipo kwa baadhi.
 
Aisee afadhali umekiri maana juzi kati hapa eti wenyewe mnajifariji, proud to be singo mamz!!! Mimi nilisema na ninasema hupaswi kuwa proud kuwa single mom kwa sababu sio sawa japokuwa hii haina maana kwamba ni laana au tiketi ya kudharauliwa. Kinachotakiwa ni kukubaliana na hali halisi, kumpenda mtoto, kuangalia mbele na kumtegemea Mungu.

Hebu fikiria tunakutana na wewe sehemu uniambie I am a single mom and I am proud of it. Hivi hata kama nafikiria kukuoa unadhani hayo mawazo yatabaki kichwani mwangu tena.
 
Huyu Morg Pasua kichwa ndio Vaislay???? Kweli nimeamini kwenye kuoa unahitaji kuwa makini, maana Morg bad girl Halafu Vaislay good girl lakini Wote wanashare something in common they are single momma

yaaani sikuwaza kabisaaaaaa kwamba ni two in one
 
Nakuletea list yote kama sever haitajaa

Ijae tuu kwa maana ntajakuta bwanangu mokoyo ana jina lingine Kaizer bi araundi nikiletewa hii list ya fake ID lolote laweza kutokea
 
Last edited by a moderator:
jamani mbona sielewiiiiiiiiiiiiiiiiiii! mleta thread kawa nani tena?

ndio maana baada ya kupost anatoka online anaingia kwa ID nyingine?

JF inaumiza kichwa aisee! hahahaaa!!
miss neddy umeona huyu mtu wangu?
 
Last edited by a moderator:
Huyu Morg Pasua kichwa ndio Vaislay???? Kweli nimeamini kwenye kuoa unahitaji kuwa makini, maana Morg bad girl Halafu Vaislay good girl lakini Wote wanashare something in common they are single momma

halafu kumbe ni mtu mmoja

heehe
 
Watu wengi wanachukulia single momz kama hawana umuhimu tena na hawafai katika mahusiano. Siku hizi wanaume wengi ambao hawajakuwa na watoto utasikia wakisema "Mimi mwanamke wenye mtoto simtaki amechoka na amekongoroka kabisa huyo"

Kumbuka hapa kuna wanawake wengine hata ukikutana nae na asipokuambia ana mtoto huwezi jua, anajipenda na ni mrembo wa kuvutia na mwenye maendeleo.

Wanaume wengi sana wanaona hana thamani, na wengine kusema ni wameshindikana walikotoka yaani na jaamaa aliyezaa nae.Tukumbuke NOT EVERYMAN MEANT TO BE A DADY, kuna wengine ni waharibifu tu, pengine pia tofauti za maisha zinazotokea zinapelekea yote hayo kutokea, Watu hawaelewi...

Single moms haimaanishi hawatakiwi kuwa na mahusano mengine mapya labda na mwanaume ambaye hana mtoto, wengi hudhani ukijitumbukiza hapo basi utalea mtoto.

Jamani kuna watu wanauwezo wa kutake care ya watoto wao bila msaada, jiulize kabla yako nani alikuwa anamsaidia kama sie mwenyewe. Ni faraja na upendo tu anahitaji kutoka sehemu nyingne.

Hawa watu haimaanishi waolewe au wawe na mahusiano na wanaume ambao nao wanawatoto...eti sababu wasaidane kulea... Tena na zile familia zikisikia kijana anasema "nina mwanamke ila ana mtoto" moto unawaka, jamani jamani? Huu si ubaguzi lakini?

Mwenye mawazo hayo wewe ni katili na mbinafsi kabisa. Na ndo maana inafikia hatua wanaume mnafichwa mnakuja kutambua kwamba ana mtoto imepita hata miaka 10, halafu unalaumu oooh hakuniambia. Hakukuambia kwasababu anajua mtazamo wenu kwao...

Mimi naomba tu niwaambie ndugu Kaka zangu, wadogo zangu, Mwanamke aliyezaa ni sawa na wengine tu, tena bora yeye kazaaa anajua ana kizazi, kuliko hao wasiozaa na wanaokesha kila siku kutafuta watoto kwa waganga..

Mimi mwenyewe ni mfano mzuri, nimepata unyanyasaji sana na wanaume, pale nilipokuwa nawaambia nina mtoto, wengine walishia kimya kimya, wakidai eti tuna kawaida ya kupasha kiporo na mzazi mwenza HIYO NI UONGO NA FIKRA MBOVU ZA WATU
Na kamwe sikuweza kuficha kama sina mtoto kwasababu najua nini maana ya mtoto. Mtoto ni zaidi ya thamani ya vitu ulivyonavyo ndani...
Tena wanawake ambao mmekutana na haya wala msifiche ukweli, Mwanaume akikimbia ujue mungu kakuepushia jambo.

WANAUME HEBU TOENI NA MBADILIKE NA HIZO IMANI AMBAZO SIO...

Swali lolote linakaribishwa... Asanteni
Vaislay ni kwamba umemshikia morg ama ni wewe kabisa?

samahani kwa swali lakini... OMBA RADHI KWA ULIOWAKWAZA KWA ID YA MORG...
 
Last edited by a moderator:
Unaoa mwanamke mwenye mtoto/watoto kwani wasichana wameisha au hawapo? Mpango wa Mungu kijana aoe msichana na waanze wao kuzaa kama Baraka ya ndoa ndio maana hata Mungu akaweka bikira ili maisha ya ndoa kati mvulana na msichana yaanze kwa damu ya msichana kumwagika (kutoa bikira). Watoto wakikua wanaenda zao na wao wanabaki wawili kama walivyoanza hadi kifo kinapowatenganisha. Tatizo la watanzania wanapenda kuingiza siasa katika kila jambo. Kwa nini ukompromise values. Afadhali kama kijana kampa mimba msichana na anamuoa huyo huyo japo atakuwa amefanya kinyume na makusudio ya Mungu lakini watoto wao watakuwa direct product ya ndoa. Suala kuwa kijana akimkimbia single mother ati Mungu kamuepusha single mother ni maneno ya kujifariji kwani Mungu huyo huyo inaweza kuwa kamuepusha kijana ingawa Mungu hasaidii mtu katika uzinzi wake. Aidha hao single mother karibu wote huwa wanaishia kuvuruga ndoa za wanawake wenzao waliochagua maisha safi ya ndoa. Kama mtu ameamua kuwa single mother basi aheshimu vilevile uamuzi wa mwanamke mwingine aliyeamua kuwa katika maisha safi ya ndoa badala ya kuzengea waume za watu. Kila mtu huwa anakuwa na nafasi ya kuchagua maisha yake yaweje ndio maana kuna wazazi, waalimu, maafundisho ya dini haya yote ni kwa ajili ya kumfanya mtu awe well informed.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom