Singida: Walimu mbaroni kwa kusababisha kifo cha mtoto wa miaka 5

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,017
9,885
JESHI la Polisi Mkoa wa Singida linawashikilia Mwalimu Regina Laurent, (28) wa Shule ya Msingi Mang'onyi na Mathias Marmo (30) kwa tuhuma za kumuua kwa kipigo mtoto mwenye umri wa miaka 5 aitwaye Joyce John, mkazi wa Kijiji na Kata ya Mang’onyi, wilayani Ikungi mkoani hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi wa Polisi ( ACP) Stella Mutabihirwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa watuhumiwa hao walikuwa ni walezi wa mtoto huyo na kuwa uchunguzi zaidi ukikamilika wote wawiliwatafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalowakabili.

Mutabihirwa akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuhusu tukio hilo alisema Agosti 11/2021 majira ya saa 1:30 usiku katika Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu iliyopo maeneo ya Puma, Wilayani Ikungi, Mkoa wa Singida mtoto huyo alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu hospitalini hapo ambapo wauguzi wa hospitali hiyo walitilia mashaka kifo hicho kutokana na majeraha aliyokuwa nayo marehemu na ndipo waliamua kutoa tarifa kwa Jeshi la Polisi.

Alisema Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida lilipata taarifa hizo siku hiyo majira ya saa 2:00 usiku ambapo lilifanya uchunguzi wa awali na kubaini kuwa majeraha aliyoyapata marehemu yalitokana na kupigwa na vitu vinavyodhaniwa kuwa ni fimbo na kitu butu sehemu mbalimbali za mwili wake na wazazi wake walezi ambao ni Mathias Marmo, (30), Mwalimu wa Shule ya Msingi Mang'onyi na Regina Laurent, (28), wote wairaq na wakazi wa mang'onyi.

Aidha Mutabihirwa alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtoto huyo alikuwa akipigwa na kufanyiwa ukatili mara kwa mara na walezi wake hao na kuwa mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kukabidhiwa kwa ndugu kwa hatua za mazishi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linaendelea kukemea vitendo vya kikatili vinavyofanywa na baadhi wazazi na walezi na linawaomba wananchi kuachana na vitendo hivyo vikiwemo kutoa adhabu zisizokuwa na mipaka kwa watoto na kusababisha unyanyasaji wa kijinsia na wazazi wameaswa kuwalea watoto wao katika maadili mema.

Michuzi Blog
 
Ndio mana yule mtoto alesoma bora kupelekwa jela kuliko kusoma, wengine tulishauri uchunguzi uanzie shuleni isije kuwa kuna mambo ya ajabu yanafanyika huko, na n yie walimu kama mnastress za kazi zenu kuweni makini na wanafunzi mnaowafundisha.
 
aisee yaani inasikitisha,umri wa mwanangu Jasmine huo,

Hao wauaji inatakiwa wapigwe risasi adhalani
Tukisema binadam ni ni viumbe hatari ujue ni pamoja na wewe unaesema wapigwe risasi
😀
Mimi naona sio makosa yao kwa sabab
Mpaka unaua
Ujue kwenye akili kuna kitu hakijakaa

Sawa
Kila kitu ni akili
Sasa hivi yamekuja magonjwa mengi ya akili
 
mtoto wa miaka mitano mbona mdogo sana unaanzae kumpa kipigo cha mbwa mwizi ? au wanatoa kafara ?
 
Kwanini kichwa cha habari kimesema walimu ilihali walikua walezi kwake na hakuna mahusiano ya moja kwa moja je wangekua wanasheria , madereva... ungesema MADEREVA MBARONI ?
 
JESHI la Polisi Mkoa wa Singida linawashikilia Mwalimu Regina Laurent, (28) wa Shule ya Msingi Mang'onyi na Mathias Marmo (30) kwa tuhuma za kumuua kwa kipigo mtoto mwenye umri wa miaka 5 aitwaye Joyce John, mkazi wa Kijiji na Kata ya Mang’onyi, wilayani Ikungi mkoani hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi wa Polisi ( ACP) Stella Mutabihirwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa watuhumiwa hao walikuwa ni walezi wa mtoto huyo na kuwa uchunguzi zaidi ukikamilika wote wawiliwatafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalowakabili.

Mutabihirwa akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuhusu tukio hilo alisema Agosti 11/2021 majira ya saa 1:30 usiku katika Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu iliyopo maeneo ya Puma, Wilayani Ikungi, Mkoa wa Singida mtoto huyo alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu hospitalini hapo ambapo wauguzi wa hospitali hiyo walitilia mashaka kifo hicho kutokana na majeraha aliyokuwa nayo marehemu na ndipo waliamua kutoa tarifa kwa Jeshi la Polisi.

Alisema Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida lilipata taarifa hizo siku hiyo majira ya saa 2:00 usiku ambapo lilifanya uchunguzi wa awali na kubaini kuwa majeraha aliyoyapata marehemu yalitokana na kupigwa na vitu vinavyodhaniwa kuwa ni fimbo na kitu butu sehemu mbalimbali za mwili wake na wazazi wake walezi ambao ni Mathias Marmo, (30), Mwalimu wa Shule ya Msingi Mang'onyi na Regina Laurent, (28), wote wairaq na wakazi wa mang'onyi.

Aidha Mutabihirwa alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtoto huyo alikuwa akipigwa na kufanyiwa ukatili mara kwa mara na walezi wake hao na kuwa mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kukabidhiwa kwa ndugu kwa hatua za mazishi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linaendelea kukemea vitendo vya kikatili vinavyofanywa na baadhi wazazi na walezi na linawaomba wananchi kuachana na vitendo hivyo vikiwemo kutoa adhabu zisizokuwa na mipaka kwa watoto na kusababisha unyanyasaji wa kijinsia na wazazi wameaswa kuwalea watoto wao katika maadili mema.

Michuzi Blog
Aaaagh, Jesus, hao watu sijui wafanywe nini, kama mtoto umeshindwa kumlea mrudishe kwa ndugu zakenau kabidhi ustawi wa jamii, daaah 😭, hivi mtu ukapata hasira ukaua hao watu itakuwa ni kosa la nani?!
 
Soma vizuri,acha kukurupuka. Huyo mtoto kapigwa na wazazi walezi wake(ambao wana taaluma ya waalimu) na sio walimu wake shuleni

Hata angekataa shule bado home angekumbana na hao walezi wake. Suluhisho lilikua kurudi kwa wazazi wake(kama wapo)

R.I.P mtoto

Back
Top Bottom