Iramba: Wamuua baba yao kisa kuoa mke wa pili (Mama Mdogo Wao)

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,775
Unakuta waliofanya upumbavu huu ni Watoto wa kiume ambao nao hawako exceptional na ghasia za Wanawake.

Matoto ya hivi Huwa ni mapumbavu sana.Polisi funga hao waizee huko huko jela.

---
WATU sita wa familia moja wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida kwa tuhuma za kumuua baba yao kwa kile kilichodaiwa kukerwa na kitendo cha kuongeza mke wa pili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Stella Mutabihirwa aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 30 mwaka huu katika Kijiji cha Kinalilya wilayani Iramba mkoani hapa.

Alisema, watuhumiwa hao ambao hata hivyo hakuwataja majina kwa kuwa uchunguzi bado unaendelea, walimuua Daudi Kitonka (68) kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababisha kutoka damu nyingi.

Kamanda Mutabihirwa alisema uchunguzi wa awali ulibaini kuwa kabla ya mauaji kutokea, kulikuwa na ugomvi wa kifamilia baada ya baba kumhamishia nyumbani kwake mwanamke aliyezaa naye watoto wawili nje ya ndoa, kitendo ambacho kilitafsiriwa kuwa ni manyanyaso kwa mke mkubwa.
 
Mmoja alimtandika baba yake mzazi kisa kaoa mke wa pili.

Baba alitandikwa mama wa pili alipigwa nusura kufariki.

Mitoto mingine ya hovyo sana
 
Back
Top Bottom