Singida Ilitakiwa Kuwa Mji Mtamu

Singida Ilitakiwa Kuwa Mji Mtamu

Singida ina potential kubwa sana ambayo bado haijatumika kikamilifu. Imagine katikati kabisa ya mji kuna view ya mabwawa mawili, hali ya hewa ya kawaida, mazingira yenye utulivu na maji yanayoweza ku-refresh akili. Kwa mipango mizuri ya mji, Singida ingeweza kuwa moja ya miji yenye kuvutia zaidi kuishi Tanzania.

Moja ya mawazo muhimu ni eneo la Shule ya Sekondari Mwenge ambalo lipo katikati ya mji na limechukua eneo kubwa sana. Badala ya kuendelea kuwa sekondari tu, serikali ingeangalia uwezekano wa kuligeuza kuwa chuo kikuu kikubwa. Hii ingeongeza population ya vijana, biashara, apartments, cafes, usafiri na mzunguko wa fedha mjini.

Zaidi ya hapo, eneo la hifadhi ya chanzo cha maji chini ya hospitali ya mkoa linaweza kubadilishwa kuwa sehemu nzuri ya mapumziko, walking areas na city attraction bila kuharibu mazingira. Singida ina nafasi ya kuwa mji wa kisasa wenye utulivu, mazingira mazuri na tourism ndogo ya ndani kama ikipewa maono sahihi ya urban planning.
Wenye akili tunasema hivi ....miji yote Tanzania ina makosa ya kimpangilio na kanuni na logic ya maendeleo hivyo ni vyema serikali kuplani miji mipya kila mkoa siyo kuendeleza makosa yaani mikoa ya kusini wangetenga mkoa mpya wa mji wa kisasa kwa mikoa yote ya kusini na kasikazini hivyo hivyo yaani wangeunda NEW MASTER PLAN YA JIJI SHIRIKISHI LA MIKOA ZAIDI YA MMOJA ..Hii miji yetu kama dar ilisha kosewa toka zamani hivyo hata tukifanya vipi its improve ila itakuwa bado mibovu ....hapa dar ilitakiwa kufanya hivyo kwa kigamboni ila serikali pumbavu ya ccm imetukwamisha serikali ilitakiwa kutengeneza mikoa mipya ya majiji ya kisasa kama mitano ambayo kila mkoa ungetakiwa kuwa na km za eneo zisizo pungua km²2000
 
unajua nini kinafanya singida pawe na mzunguko mkubwa tarafa nyingi za sindiga DC zinategemea kufanya manunuzi ya jumla singida mjini na wao pia wana jitosheleza kwa vyakula kuleta singida mjini tofauti na manyara miji yako iko mbali na babati mingine inakwenda karibu na mkoa wa arusha
Hao wachaga wasingida wanabiashara gani za maana maana hapo Singida zaidi ya guesthouse ?
 
Nimekaa huo mji karibu miaka sita hivi; unayoyasema ni kweli. Singida ni mji mdogo lakini uwezekano wa kukua upo. Ule ukanda wa KBH mpaka kule kiwanda cha kukamua alizeti ni potential sana.
 
Singida ni Pazuri sana ,huu ni ukanda wa Kindai kuna ujenzi wa Morena Hotel Singida.
Pichani unaweza kuona mabwawa yote matatu Kindai,Munangi na Singidani
Screenshot_20260415-120317_1.jpg
 
na pale pana hela ukiona wachaga hawaondoki kwenye mji ambao sio wao jua kuna pesa..kwanini wachaga huwakuti manyara,lindi au kigoma ni kwa sababu washaona hakuna mzunguko
Huu ni uongo, manyara wamejaa wachaga wakifuatiwa na masai, hebu andika vitu vya ukweli na uhakika basi, maana kuna mnyaturu mmoja amefanya nipende singida na watu wake wote,
 
Singida ina potential kubwa sana ambayo bado haijatumika kikamilifu. Imagine katikati kabisa ya mji kuna view ya mabwawa mawili, hali ya hewa ya kawaida, mazingira yenye utulivu na maji yanayoweza ku-refresh akili. Kwa mipango mizuri ya mji, Singida ingeweza kuwa moja ya miji yenye kuvutia zaidi kuishi Tanzania.

Moja ya mawazo muhimu ni eneo la Shule ya Sekondari Mwenge ambalo lipo katikati ya mji na limechukua eneo kubwa sana. Badala ya kuendelea kuwa sekondari tu, serikali ingeangalia uwezekano wa kuligeuza kuwa chuo kikuu kikubwa. Hii ingeongeza population ya vijana, biashara, apartments, cafes, usafiri na mzunguko wa fedha mjini.

Zaidi ya hapo, eneo la hifadhi ya chanzo cha maji chini ya hospitali ya mkoa linaweza kubadilishwa kuwa sehemu nzuri ya mapumziko, walking areas na city attraction bila kuharibu mazingira. Singida ina nafasi ya kuwa mji wa kisasa wenye utulivu, mazingira mazuri na tourism ndogo ya ndani kama ikipewa maono sahihi ya urban planning.
Dar ndio Mwanzo mwisho huko aje Nani?
 
Mkuu ungetutumia picha ili tujionee jinsi singida ilivyo nzuri,sio wote tunakujua singida, ahsante.
Nalog off Z
 
Back
Top Bottom