Singida Black Stars imewasilisha rasmi malalamiko TFF kufuatia mechi dhidi ya Simba SC

Singida Black Stars imewasilisha rasmi malalamiko TFF kufuatia mechi dhidi ya Simba SC

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Klabu ya Singida Black Stars imewasilisha rasmi malalamiko kwa mamlaka za soka nchini, ikiwemo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa mchezo wao dhidi ya Simba SC uliochezwa jana Mei 28 kwenye Uwanja wa KMC Complex.

Katika mchezo huo, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0, bao pekee likifungwa na mshambuliaji Steven Mukwala dakika ya 42. Ushindi huo umeiwezesha Simba kufikisha alama 72 na kuendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC, ikiwa pointi moja nyuma ya vinara Yanga SC walio na pointi 73. Timu zote zimecheza michezo 27.

Kwa upande wao, Singida Black Stars wamesalia katika nafasi ya nne wakiwa na pointi 53 baada ya mechi 28.

Afisa Habari wa klabu hiyo, Hussein Massanza, amethibitisha kuwa wamechukua hatua hiyo ili kutafuta haki kufuatia kile walichokieleza kuwa ni vitendo vilivyoathiri ushindani wa haki katika mchezo huo.

1748526031145.png
 
Watu wa msimbazi mko na makasiriko sana.Kama ubingwa hamtopata sasa makasiriko ya nini?waacheni black stars wakalalamike
 
Ndio wajue maana ya ubaya ubwela, walidhani 200m zinapatikana kirahisi tu.
 
Mbuzi wa bwana Heri amekula mahindi kwenye shamba la bwana Heri na kesi ya mbuzi hao imepelekwa kwa bwana Heri.
 
Wanatakaje wapewe penalty? Warudi dimbani wakapige penalty...
Hao wanadanganywa na wapwa zao mwiko nyuma ...
Malalamiko FC
Naskia waliahidiwa milioni 200 kuifunga Simba ...😂
Ila nimeamin msemo mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe
 
Ukisikiliza mawazo kutoka UTO utapata hasara ya hela na muda. Presha nayo itakuandama
 
Back
Top Bottom