SINGIDA : Basi lagonga nyumba, abiria wawili wajeruhiwa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
bbec7757cf1ca6a37f0ef110eda8072e.jpg
Wakazi wa Kijiji cha Njirii Wilaya ya Manyoni, Singida, wakiangalia basi la kampuni ya Tabora Moja Express, ambalo liligonga nyumba ya Amina Hamisi baada ya basi hilo kuacha njia

Basi hilo lilikuwa likitokea Tabora kwenda Dar es salaam juzi, lilisababisha kujeruhiwa kwa abiria wawili.

My take : Poleni abiria wote ambao mmenusulika kufa, na majeruhi mungu awape nafuu

Na mwenye nyumba kama nyumba yako haiko katika hifadhi ya barabara.. basi tegemea nyumba mpya kulipwa.
 
Siku zote kama nyumba yako ipo pembeni ya bara bara ni bora upande miti pembeni ya bara bara
Nadhani kujenga karibu na barabara ni kuhatarisha maisha kwa sababu lolote linaweza kutokea ama kubomolewa au ajali kama hizi..!
 
Dahh yaani hilo basi linakimbia kama nini? Linaondoka dar SAA moja asubuhi na wanataka kuwahi mapema tabora na linazunguka njia ya singida
 
Wizara ya Ardhi, ndo pekee wenye mamlaka ya kugawa matumizi, ifiki wakati wa Wizara hii kusimama kidete kwa kuweka alama maalum sehemu husika ya Makazi ya Watu.
Tanroad imeshindwa kabisa, inaweka alama yake na hata ukiisogelea wao hawana habari na wewe!!!!!!
 
Back
Top Bottom