SINGIDA: Basi la Mohammed Trans lapata ajali, watu kadhaa wafariki dunia

karume kenge

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
568
421
Habari wadau,

Nimepita hapa kidogo kabla ya kufika Manyoni nimekutana na hii ajali mbaya. Inadaiwa watu 3 wamefariki na majeruhi ni 6. Aidha, inasemekana ni walimu ambao walilikodi basi kutoka Tanga.

Chanzo cha ajali ni gari ndogo lililokuwa limeegesha barabarani bila tahadhari, mbele ya basi kulikuwa kuna lori la mafuta hivyo dereva wa lori alipoona mbele kuna gari imepaka na yeye akatanua kwa haraka.

Wakati huo basi nalo lilikuwa linataka ku-overtake hivyo dereva wa basi akashindwa kulimudu kutokana na mwendo kasi na akaligonga roli la mafuta kwa nyuma na kutoboka kitu kilichopelekea kumwagika mafuta barabarani.

Tushukuru Mungu havijatokea vifo zaidi kwa sababu mafuta yaliyotapakaa ardhini hayakushika moto.

Mungu awaweke mahala panapostahili marehemu wote, amina.

20170107_071934.jpg
 
Mohamed trans kwa kuchinja, hawajambo.
Polisi mkamateni Dereva, mpimeni kileo na aseme alikuwa anakimbilia Wapi?

Mwendokasi chanzo huwa ni abiria mara zote mkuu.

Nimesafiri na haya mabasi mara kadhaa dereva akienda mwendo wa kawaida wana-force afunguke barabara ni yake.

Ila yakitokea haya bas dereva chambo
 
Back
Top Bottom