Singida: Basi la Kampuni ya KIDIA ONE lateketea kwa moto

Singida: Basi la Kampuni ya KIDIA ONE lateketea kwa moto

Hapo issue ni tairi sio engine
Siku hizi hazipasuki tena. Zinawaka tu na kusababisha basi zima kuteketea.

Swali hapo, je kwenye basi hakuna vifaa vya fire extingusher vya msingi?

Enzi za General Tyre sijawahi kusikia eti gari linateketea chanzo ni gurudumu kushika moto!

Hao matajiri wamiliki wa mabasi wakae watathimini jambo hilo, maana sasa imekuwa ni 'routine' na kuzoeleka masikioni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi Kidia One likiwa safarini kutoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam, limeungua moto maeneo Iguguno shamba mkoani Singida. Hakuna majeruhi wala kifo.

Ajali ya Moto basi la KIDIA ONE eneo LA maluga kona mkoani Singida muda mchache uliopita.

Abiria wote wako salama Hakuna abiria alyejeruhiwa.

Chanzo cha moto ni tairi ya nyuma kupasuka na kushika moto, hivyo juhudi za abiria na wananchi za kuzima moto huo zilishindikana baada ya moto kuwazidi kasi kutokana name upepo
IMG_20180821_162339.png

Yono vibe
 
Dah
Mungu ni mwema.

Angalau roho zimeokoka mauti, kama ni fedha inatafutwa lakini sio roho ya mtu wala uzima wake.
 
Kwa nini mabasi yanateketea sana mwaka huu?
Tairi linapokanyaga lami linakua limebeba uzito wa gari lote pamoja na uzito wa abiria. gari inapotembea kunakua na msuguano wa tairi na lami, kumbuka lami inapigwa na jua kutwa nzima kwa hiyo mida ya jua lami inakua ya moto. wakati huo huo tairi ya gari inakua imewekewa upepo mwingi na tabia ya upepo kukiwa na msuguano unapata joto Kali. sasa basi : tairi yenye upepo mwingi +mzigo iliyobeba +lami iliyopata moto wa jua +msuguano unaotokana na speed = inahitajika tairi yenye ubora madhubuti kukabili hivyo nilivyoorodhesha. Hapa msala ni wa T. B. A. sasa hivi ukinunua tairi mpya ukienda kujaza upepo tu inaota majipu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halaf singida kulivyokuwa na shida ya maji sijui hata mnazimia nn moto hapo[/QUOTE]
Haja ndogo



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Tairi linapokanyaga lami linakua limebeba uzito wa gari lote pamoja na uzito wa abiria. gari inapotembea kunakua na msuguano wa tairi na lami, kumbuka lami inapigwa na jua kutwa nzima kwa hiyo mida ya jua lami inakua ya moto. wakati huo huo tairi ya gari inakua imewekewa upepo mwingi na tabia ya upepo kukiwa na msuguano unapata joto Kali. sasa basi : tairi yenye upepo mwingi +mzigo iliyobeba +lami iliyopata moto wa jua +msuguano unaotokana na speed = inahitajika tairi yenye ubora madhubuti kukabili hivyo nilivyoorodhesha. Hapa msala ni wa T. B. A. sasa hivi ukinunua tairi mpya ukienda kujaza upepo tu inaota majipu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani si T. B. A ni T. B. S

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom