Sina ndugu mjini

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,208
4,405
SINA NDUGU MJINI(rudio).

1)urafiki siyo hapa,acheni hilo ni nene.
Mwenze nisitoke kapa,mje ruka kisenene.
Vaeni kanda malapa,kimya kimya muuchune.
Mjini mi sina ndugu,kelele ze si za chura.



2)ofisini siyo haba,namba moja siyo nane.
Salamu si marahaba,poa poa chuniane.
Pembe tatu za mraba,tani sote tubanane.
Mjini mi sina ndugu,kelele ze si za chura.

3)pigo la jua tambua,kelele zo uzibane.
Hakika nimegundua,sitamani tudundane.
Mafunzo nilipitia,wataka tutambiane.
Mjini mo sina ndugu,kelele ze si za chura.



4)tamati kimya nyamaza,natamani tuungane.
Japo giza si mwangaza,mwana usiku manane.
Moto hautouweza,labda mwezi wa sa nane.
Mjini mi sina ndugu,kelele ze si za chura.

Shairi-MJINI SINA NDUGU.
mtunzi-Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0624010160
iddyallyninga@gmail.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom