Hivi kwanini watu mliofanikiwa mnawatendea vibaya ndugu zenu?

Street brain

JF-Expert Member
Oct 24, 2022
486
606
Habari za wakati huu wanajf kuna hope mko powa? Niende moja kwa moja kwenye mada maana hili suala huwa naona kama ndugu waliofanikiwa hawatumii akili.

Miaka ya nyuma sana takribani kama miaka 12 enzi hizo sina mbele wala nyuma yaani hohehahe nilikuwa sina kazi yoyote ile but nilikuwa nimehitimu kidato cha nne, so nikaona sina mishe yoyote ile kitaa na kwenye ukoo wetu kuna ndugu waliofanikiwa kweli kimaisha kama mipesa wanayo.

Nikapiga simu kwa uncle fulani hivyo nikimuomba anisaidie kutafuta kazi maana mimi nilitafuta mishe mpaka nikaona sasa kazi yangu sasa yangu ni kutafuta kazi. Nilipompigia akanicheki akaniambia niende pale kwake niuze duka lake na atakuwa ananilipa hela ili nami nipate mtaji nifungue biashara yangu.

Basi mimi nikafunga safari kutoka Mtwara mpaka Geita kuuza duka, nikakuta uncle ana wafanyakazi wengine kama 4 hivi. So nikafika pale akasema atakuwa ananilipa 20,000 kwa mwezi, japo hiyo pesa nilikubali kishingo upande nikasema powa kwa sababu sikuwa na option nyingine nikajua na wale wafanyakazi wanalipwa hiyo hiyo.

Tukafanya kazi na wale jamaa zangu mi nikawa mtu wa fedha yaani nakaa kwenye droo kila kitu kinachouzwa mi ndio nahusika kupokea pesa na kutoa chenji maana uncle alikuwa bize nashughuli zingine za migodi pale GGM tukafanya kazi kwa muda wa miezi 10.

Biashara iliendeshwa vizuri sana siku moja uncle akaja pale dukani mara wale jamaa wakaanza kudai waongezewe mishahara, mimi nikawauliza kwani nyie mnalipwa shilingi ngapi, jamaa akanijibu analipwa laki 1 kwa mwezi na kula, kulala ni kwa uncle na mimi pia hivyo hivyo.

Hapo sasa nikaanza kujiona kama vile mimi siyo kitu pale na wale jamaa, ndiyo anawapendelea zaidi kuhusu mishahara, nikaona isiwe kesi nikamfuata nikamuuliza kwanini mimi ananilipa elfu 20 halafu wale jamaa anawapa laki 1?

Akanijibu kwa mimi ndugu yake kwaihyo sifai kupewa hiyo laki 1, nikamuuliza tena kwani kati ya hao outsider na mimi nani mwenye umuhimu zaidi, akanijibu ni wewe, kwanini unawalipa vizuri halafu mimi unanifanyia ni harsh akajibu kama kama nimechoka naweza kuondoka!

Daah, niliondoka siku hiyo hiyo asubuhi, sikujua hata naenda wapi ila na laki 150,000 mfukoni nikapanda gari mpaka Mwanza kesho ya asubuhi mpaka DSM. Nilipofika Dar nikakutana na washikaji ninaofahamiana nao, kama unavyojua vijana wengi hukimbilia Dar. Basi nikafika pale nikaanza biashara ya kutembeza mikate kwenye maduka, I mean kwa small retail, ulipofika mwezi wa nane kwa sababu nilifaulu form 4 vizuri nikaaply chuo cha uhasibu Bahati Manyara.

Nimesoma kwa mazingira magumu sana, yaani sup zilikuwa ni ndugu yangu, maana nilikuwa siendi chuo nashinda kitaa napiga day worker kila siku ili nipate hela ya ada na kulipia kodi. Duuh sitosahau shida nilizozipata chuo, mpaka nilijilaumu kwanini nimekuja chuo bila kuwaza nitatoa wapi ada.

Nimesoma hivyo hivyo kwa kuhangaika mwisho wa siku nikamaliza elimu yangu ya Diploma YA Uhasibu nikiwa na GPA 3.9 nokaomba sehemu ya kujitolea camp fulani ivi ipo Arusha nikapata pale nimejitolea kwa miezi 12 nilipotoka pale nikaaply kazi za uhasibu katika kampuni fulani nikakosa, but nilikuwa nishatuma maombi kwenye taasisi mbalimbali so nikaitwa nikafanye interview Mungu siyo Athumani nikafaulu interview nikaajiliwa rasmi.

Nikasoma Open University kuongeza elimu till now nina masters na CPA na ni incharge of Accounts Department, sijigambi ila siwezi pesa ya kula.

Kilichonipelekea kuongea hayo yote leo kuna mtoto wa ndugu yangu fulani hivi kanipigia simu kuniomba mtaji nimsaidie au kama nina kijisehemu nimuajiri akanikumbusha maisha ya miaka 12 huko nyuma yule ndugu alivyonitreat nikaumia sana, maana kama angelijua asingelifanya vile maana hujui nani atavisaidia vitoto vyake.

Chamsingi ni kwamba ndugu mnazingua sana. Kwanini msiwasaidie ndugu wa ndugu yako ambao hawajiwezi na pia ukiwasaidia ni kama unajitengezea heshima na jina na hakuna kizazi chako kitakachoteseka kama huku nyuma ulijijengea uhusiano mzuri.

Ndugu yako mthamini usimnyanyase, munazingua sana.
 
Habari za wakati huu wanajf kuna hope mko powa ,,,
Niende moja kwa moja kwenye mada maana hili suala huwa naona kama ndugu waliofanikiwa hawatumii akili...

Miaka ya nyuma sana takribani kama miaka 12 enzi hizo sina mbele wala nyuma yaani hoehae nilikuwa sina kazi yoyote ile but nilikuwa nimehitimu kidato cha nne, so nikaona sina mishe yoyote ile kitaa na kwenye ukoo wetu kuna ndugu waliofanikiwa kweli kimaisha kama mipesa wanayo, nikapiga simu kwa uncle fulani ivo nikimuomba anisaidie kutafuta kazi maana mimi nilitafuta mishe mpaka nikaona sasa kazi yangu sasa yangu ni kutafuta kazi, nilipompigia akanicheki akaniambia niende pale kwake niuze duka lake na atakuwa ananilipa hela ili nami nipate mtaji nifungue biashara yangu.

Basi mi nikafunga safari kutoka mtwara mpaka Geita kuuza duka nikakuta uncle ana wafanyakazi wengine kama 4 ivi so nikafika pale akasema atakuwa ananilipa 20,000 kwa mwezi, japo hiyo pesa nilikubali kishingo upande nikasema powa kwa sababu sikuwa na option nyingine Nikajua na wale wafanyakazi wanalipwa hiyo hiyo.

Tukafanya kazi na wale jamaa zangu mi nikawa mtu wa fedha yaani nakaa kwenye droo kila kitu kinachouzwa mi ndo nahusika kupokea pesa na kutoa chenji maana uncle alikuwa Bize nashughuli zingine za migodi pale GGM tukafanya kazi kwa muda wa miezi 10, biashara iliendeshwa vizuri sana siku moja uncle akaja pale dukani mara wale jamaa wakaanza kudai waongezewe mishahara mi nikawauliza kwani nyie mnalipwa shilingi ngapi jamaa akanijibu analipwa laki 1 kwa mwezi na kula, kulala ni kwa uncle na mi pia hivyo hivyo.

Hapo sasa nikaanza kujiona kama vile mimi siyo kitu pale na wale jamaa ndiyo anawapendelea zaidi kuhusu mishahara nikaona isiwe kesi nikamfuata nikamuuliza kwanini mimi ananilipa elfu 20 halafu wale jamaa anawapa laki 1 akanijibu kwa mi ndugu yake kwahyo sifai kupewa hiyo laki 1, nikamuuliza tena kwaani kati ya hao outsider na mimi nani mwenye umuhimu zaidi akanijibu ni wewe, kwanini unawalipa vizuri afu mimi unanifanyia ni harsh akajibu kama kama nimechoka naweza kuondoka,,, daah niliondoka siku hiyo hiyo asubuhi sikujua hata naenda wapi ila na laki 150,000 mfukoni nikapanda gari mpaka mwanza kesho ya asubuhi mpaka DSM, nilipofika dar nikakutana na washikaji ninaofahamiana nao kama unavyojua vijana wengi hukimbilia dar basi nikafika pale nikaanza n biashara ya kutembeza mikate kwenye maduka I mean kwa small retail ulipofika mwezi wa nane kwa sababu nilifaulu 4m4 vizuri nikaaply chuo cha uhasibu bahati manyara,,,,,, nimesoma kwa mazingira magumu sana yaani supp zilikuwa ni ndugu yangu maana nilikuwa siendi chuo nashinda kitaa napiga day worker kila siku ili nipate hela ya ada na kulipia kodi duuh sitosahau shida nilizozipata chuo mpaka nilijilaumu kwanini nimekuja chuo bila kuwaza nitatoa wapi ada,,,
Nimesoma ivo ivo kwa kuhangaika mwisho wa siku nikamaliza elimu yangu ya diploma YA UHASIBU nikiwa na GPA 3.9 nokaomba sehemu ya kujitolea camp fulani ivi ipo Arusha nikapata pale nimejitolea kwa miezi 12 nilipotoka pale nikaaply kazi fula ivi za uhasibu katika kampuni fulani nikakosa, but nilikuwa nishatuma maombi kwenye taasisi mbalimbali so nokaitwa nikafanye interview Mungu siyo athumani nikafaulu interview nikaajiliwa rasmi nikasoma open university kuongeza elimu till now nina masters na CPA na ni INCHARGE OF ACCOUNTS DEPARTMENT sijigambi ila siwezi pesa ya kula.

Kilichonipelekea kuongea hayo yote leo kuna mtoto wa ndugu yangu fulani ivi kanipigia simu kuniomba mtaji nimsaidie au kama nina kijisehemu nimuajiri akanikumbusha maisha ya miaka 12 huko nyuma yule ndugu alivyonitreat nikaumia sana maana kama angelijua asingelifanya vile maana hujui nani atavisaidia vitoto vyake,,
Chamsingi ni kwamba ndugu munazingua sana kwanini msiwasaidie ndugu wa ndugu yako ambao hawajiwez na pia ukiwasaidia ni kama unajitengezea heshima na jina na hakuna kizazi chako kitakachoteseka kama huku nyuma ulijijengea uhusiano mzuri ...
Ndugu yako mthamini usimharas......munazingua sana
Maandishi mengiii, inaonyesha wewe ndio tatizo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom