Sina Mgogoro na CHADEMA

Sina Mgogoro na CHADEMA

Wakuu,

kwa siku kadhaa nimekuwa nikiandika ushauri na maoni yangu huru kwa chama changu CHADEMA. Yote yamefanyika kwa nia njema na mapenzi makubwa niliyo nayo kwa chama changu. na hakika hata yote mengine yanayotajwa dhidi yangu, yamefanywa nami kwa sababu ya mapenzi na kukilinda chama changu. Sasa wapo baadhi ya watu wameshindwa kuelewa maana ya ushauri na maoni yangu hayo na kwa makosa wameishia kunishambulia tu kiujumla bila kuainisha makosa kwenye hoja zangu.

Baadhi yao, licha ya kuona ukweli kwenye maoni yangu, wakadhani kuna motive behind ambayo ni mbaya, wengine wakaniona nimekuwa insane, wakielezea ninavyojichimbia kaburi. hawa kwa kinyume wanasema kitu cha hatari zaidi kwa chadema kuwa inaweza hata kukolimba, kuchacha watu nk,na wengine baadhi wakiendeleza mitazamo "makengeza" ya kuona kila anayekosoa na kushauri chadema basi ni mamluki na anatumiwa na CCM.

Wapo wengine ambao bila kufuata urari wa hoja wala kufahamu ninachokiongelea wametukana matusi,ama kuchepuka kwenye mada husika na kuingiza mada tofauti kabisa ili kupunguza makali ya ukweli katika maoni yangu. Tena wapo ambao kwa haki kabisa na kwa weledimkubwa wameona mantiki na ukweli wa yale ninayoyaeleza na nia njema niliyo nayo, na mwisho kuna wanaodhani ninatoa maoni na ushauri huu kwa sababu nina mgogoro na chadema.

Kwa kweli WOTE nawashukuru kila mmoja kwa nafasi yake. Niseme tena hapa hadharani kuwa mimi sijawahi kuwa na mgogoro na chadema, na wala sina kinyongo na chama as such.(hii as such, ni muhimu kueleweka vema, kwani ni ontological concept). Na kwa kweli sijawahi kufanya jambo lolote kinyume na katiba,maadili na miongozo ya chama. kwa sababu hiyo, mimi sijawahi kuonywa,wala kupewa karipio wala barua yoyote na chama, sijawahi kupewa adhabu walakusimamishwa/kufutwa uanachama.

Bado ninayo kadi yangu na ninailipia na muhimu zaidi bado naishi misingi na falsafa za chadema. Kwa kuwa viongozi wetu wameongoza maasi ya misingi hii kiasi cha kutoeleweka tena kwa wanachama wetu, hadi chama chetu kuwa sawa na CCM, Nikumbushe tu kwa uchache kuwa tunaamini katika nguvu ya umma, kuchukia ufisadi, uwazi na demokrasia, na kwa kweli tunaamini katika mabadiliko.

Tunapaswa kusema kweli daima hata kama ukweli huo utatuweka matatani. ndivyo hapo kale ilivyokuwa kwa dokta Slaa na Zitto kule bungeni na mwembeyanga tulipotaja orodha ya aibu. tunapaswa kuuchukia ufisadi hata kama unafanyika na viongozi wetu ama chama chetu. mambo kama kufoji risiti za mafuta ili kuiba hela kwenye fungu la mafuta ya magari kama ifanyikavyo na baadhi ya wakurugenzi wetu makao makuu ya chama, ama vitendo kama kujiuzia jengo la mabaraza ya chama na chama kulipa kodi kwa mmiliki ambaye ni afisa wa chama makao makuu, ni ufisadi kama ufisadi mwingine na unapaswa kusemwa bila kujali eti msemaji anakidhalilisha chama, na haya ni kwa uchache.

Kuna wanaopanua midomo humu kuwa chama kilikwisha nitimua,ama kuwa nilishapuuzwa kwa sababu ya matendo niliyofanya. bahati nzuri watu hao ni ama wafagiaji tu wa makao makuu, ama wachumia tumbo waliojazana pale makao makuu, ama ni hawa mashabiki wasioijua chadema kwa ndani lakini wakikariri kila kisemwacho huko bila kuhoji kiasi cha kudhaniwa na watani zetu kuwa tunakunywa viroba au zaidi kwamba sisi ni misukule.

kama chama (as such-ni muhimu kuelewa maana ya neno hili) kimefanya maamuzi tofauti na ufahamu wangu huu, nifahamishwe na watu rasmi ambao tunao humu, na namba zangu za simu wanazo kwani viongozi wa chadema makao makuu, tunawasiliana kila siku, ila huwa hawasemi.iko siku tutaonyesha mawasiliano yetu ya mara kwa mara ili kunyamazishwa wabwekaji wa humu.

Hatimaye, nitaendelea kuipenda chadema kama mwanzo, kuitetea na wapuuzi wote, na kuitenga na kusingiziwa ujinga wowote. nitatumia uwezo na nguvu zangu zote, hadi dakika ya mwisho.ili ikiwa nikiwa hai ama nimekufa historia inikumbuke kama mzalendo wa kweli kwa taifa langu na chama changu. njia hii ni ngumu na wengi wa "vuvuzela" wa chadema licha ya kutoielewa, hawawezi hata kuifuata. kwa sasa waendelee kuniita msaliti, na mamluki.

Baadaye kama taifa letu litaondokana na ukoloni wa CCM, na kama CHADEMA kitaleta kweli utawala wa haki, basi tutakuja kufurahi na kuinuliwa na CHADEMA yenyewe na hawa "Vuvuzela" wa chadema wataimba nyimbo za kutusifu na kusema hatukujua. hofu yangu ni kuwa CHADEMA kinaweza kuja kuwa chama kibaya kuwahi kutawala Afrika. Dalili tumekwishaziona.

Mwl. Ludovick

Ngumu kumeza,Hivi mkuu ile video ya Rwakatare,aliyorekodiwa,wewe ukimuoji,hebu ifafanue kidogo,maana inaonyesha wewe ulikuwa aware,wakati inarekodiwa,ila Rwakatare hakuwa na habari kama yale mazungumzo yanarekodiwa,mi nafikiri ungeanzia hapo kwenye video kama nia yako ni kujisafisha,maana unayoyaeleza hapa,yanatatanisha,unaiponda CHADEMA,wakati huohuo unaisifia,kwanini kama unaushaidi wa ufisadi ndani ya CHAMA,kwanini usiufikishe kwa viongozi husika,au pereka TAKUKURU,acha kulalama huku mtaani,wewe unaonekana kama kibaraka tu wa CCM,
 
Chadema-phobia syndrome.

Pole sana Ludovick ila hakika kwa kurudia kusoma post yako nimegundua huna amani nafsini mwako. Una majuto na mashaka, hasa ya kukataliwa na jamii.

pole sana, ila haya malalamiko peleka kwa uongozi wa tawi lako sio JF au any other social media
 
Wakuu,

Baadhi yao, licha ya kuona ukweli kwenye maoni yangu, wakadhani kuna motive behind ambayo ni mbaya, wengine wakaniona nimekuwa insane,

Tunapaswa kusema kweli daima hata kama ukweli huo utatuweka matatani.

hofu yangu ni kuwa CHADEMA kinaweza kuja kuwa chama kibaya kuwahi kutawala Afrika. Dalili tumekwishaziona.

Mwl. Ludovick
Pasco unaweza kuja hapa na kunijuza ni kwanini huyu bwana hataki kufuata ushauri wako uliompa hapo juzi?

Hivi ni kwanini ktk siku za hivi karibuni amekuwa na matamko mbalimbali kupitia JF akikihusisha Chadema na vijimambo vyake anavyoviandika kila uchao humu ndani? Kubwa ni kujaribu kuwaaminisha watu hapa ndani kwamba yeye bado ni mwanachama wa Chadema na kwamba anamapenzi makubwa na chama hicho?

Kuna ninu kiko nyuma ya Pazia juu ya haya matamko yake kwa chama? Tukumbuke huyu anajamaa mwenzake anaitwa Deus nani sijui...? Aliwahi kuja hapa jamvini na kuanzisha uzi unaosema "WAKATI WA MIMI KUSEMA UMEFIKA"....

Sasa mkuu Pasco naamni kwa namna flani ni fundi wa kusoma Saikolojia za watu unaweza kuniambia lolote juu ya haya yanayopangiliwa na hawa watu dhidi ya Chadema??

BACK TANGANYIKA
Pasco kuja hapa uchukue taka taka yako ukaifanyie counselling
Mkuu Mwalimu Joseph Ludovick, asante tena kwa bandiko jingine lenye some inconsistances ambazo ni proof ya insanity!, amini usiamini if not that "you are insane!", then your are going to be sooner than expected!.

Ila hata wale vichaa wanaotembea na "birthday suit" zao wao wanajijua wako right, kwa sababu hivyo ndivyo binadamu anavyozaliwa na hivyo anawashanga wengine wote wanaovaa nguo!.

The insanity in you iko kwenye "the ill motive behind",

Na kwenye bandiko lako hili, umeiweka kwenye sentensi ya mwisho, kuwa iwapo Chadema kitakuja kufanikiwa kushika dola, then kitakuwa ni chama kibaya kuwahi kutawala Afrika, na kueleza dalili umekwisha ziona, ili tukuulize uzitaje hizo dalili, ufunguke!.

You seriously need help!, ningekuwa nakufahamu in real life, ningekusaidia kiukweli kabisa!.

otherwise, endelea kuusema huo ukweli daima, mimi nausubiria ule ukweli utakaousema mahakamani haswa the motive behind kazi nzuri iliofanywa na "Bukoba Boy!" kwenye ile "bonafide genuine" movi!.

Thanks.

Pasco
 
Kutoka nje ya uwanja wa CHADEMA ni zaidi ya kuugua UKIMWI
 
Joseph Ludovick,

Wacha kuweweseka kwani iache jamii itaona kama u mwema au la, kwani wasaliti siku zote wajiona wapo sahihi kumbe sivyo ndivyo.
 
Sidhani kama unanianjema Nachamachetu wewe nikikusoma katikati ya mistari baado naona Act flani
 
Mkuu Mwalimu Joseph Ludovick, asante tena kwa bandiko jingine lenye some inconsistances ambazo ni proof ya insanity!, amini usiamini if not that "you are insane!", then your are going to be sooner than expected!.

la hata wale vichaa wanaotembea na "birthday suit" zao wao wanajijua wako right, kwa sababu hivyo ndivyo binadamu anavyozaliwa na hivyo anawashanga wengine wote wanaovaa nguo!.

The insanity in you iko kwenye "the ill motive behind",

Na kwenye bandiko lako hili, umeiweka kwenye sentensi ya mwisho, kuwa iwapo Chadema kitakuja kufanikiwa kushika dola, then kitakuwa ni chama kibaya kuwahi kutawala Afrika, na kueleza dalili umekwisha ziona, ili tukuulize uzitaje hizo dalili, ufunguke!.

You seriously need help!, ningekuwa nakufahamu in real life, ningekusaidia kiukweli kabisa!.

otherwise, endelea kuusema huo ukweli daima, mimi nausubiria ule ukweli utakaousema mahakamani haswa the motive behind kazi nzuri iliofanywa na "Bukoba Boy!" kwenye ile "bonafide genuine" movi!.

Thanks.

Pasco

Mkuu Pasco kupitia hapo bolded blue niseme, hapo bolded red kuwa huyo jamaa naamini "unamfahamu" au ungekuwa wale wenzetu Walokole ningesema umeshukiwa au umeonyeshwa kupitia maono na hivyo unamjua/Unamfahamu hii ni kutokana na namna unavyomwelezea (bolded blue).

So ni kweli jamaa anahitaji ushauri nasaha si mpaka uende nyumbani hata kupitia Chumbani (PM) kwa hapa Jamvini unaweza kumshauri naamini kama atakuwa hajachanganyikiwa kupita kiasi atakuelewa. Fanya hima kabla jamaa hajafikia hatua ya kukimbizwa kwenye zile hospital zetu za magonjwa ya Akili yaliyoshindikana (Mirembe) hii naisema kwa dhati ya moyo wangu na wala simkejeli mtu

Kiukweli jamaa yetu bado ni kijana mdogo sana na Kwakweli ndoa yake ingali changa, kuoa mwaka 2012 ni wazi kwamba kama yeye anavyomwitaji mwenzi wake naye ndivyo anavyomwitaji tena akiwa na akili timamu na si kama alivyo hivi sasa Hivyo ukisaidia kutoa ushauri wenye tija kwa ndugu yetu utaona kwamba utakuwa umeweza si tu kumwokoa yeye bali utakuwa umeokoa ndoa yake na familia yake kwa ujumla.

Pasco , Ludovick Joseph

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
huna mpya wewe. Zaidi unazidi kuizalilisha fani ya ualimu. Hakuna mwl. Mwenye akili za kunguru kama wewe. Mbaya zaidi umezidi kujipambanua jinsi ulivyo kigagula wa hao wanaokutumia kama mpira wa condom.

kwa kweli hii taaluma imevamiwa.kuna jingine linaitwa ni mwl kisandu.ni shida tupu kifikira.
 
Unapojianzishia thredi umu na sisi kukujibu ni kukupa promo ya bure tu.

Acha kutafuta cheap kiki ili uendelee kuwepo kwenye chat.
 
Huyu Mtoto nimesoma naye Duce pale alikuwa anakaa kijiweni na mtela maarufu ganzi ya bangi...... Ni mpuuz sana kijana huyu mpuzieni mjinga na mpumbavu sana....... Ludo amegundua ccm inawenyewe sasa anataka msamaha baada ya kuona vi fedha alivyohongwa vimeisha... Na mwigulu hamjali tena.
 
Back
Top Bottom