missa
JF-Expert Member
- May 24, 2012
- 360
- 193
Habari zenu wana jamvi.
Mwenzenu nasikitika toka siku ya jana sina furaha kabisa, na hata usiku nimeshindwa kulala sina furaha, na hata muda huu naandika sina furaha wala amani moyoni mwangu.
Naona moyo wangu umeinama hivi, halafu nimekuwa na msongo wa mawazo sana, najihisi nina simanzi hata sijui kwa nini, japo siku kadhaa zilizopita tulikwazana na mpenzi wangu lakini tulishayamaliza na kwa sasa tunakwenda sawa lakini najikuta nina mawazo mengi ya maisha likitoka hili linakuja lile.
Nimejaribu kupotezea hata kwa kuangalia filamu lakini najikuta mawazo yanahama kwenye filamu narudi palepale.
Nimejaribu kusali ili nipate faraja lakini bado naona kama roho yangu haiko sawa.
Upande wa pili wa shilingi siku nyingine huwa naamkaga na furaha na huwa sijuagi kwa nini baadhi ya siku nakuwaga hivyo, huwa inanitokea tu, kwa kweli nashindwa kuelewa kwa nini inakuwa hivi.
Jamani kama kuna mtu ameshawahi kukutana na hali kama hii anishauri nifanyeje kuepukana nayo mana inanipa unyonge uliopitiliza siipendi.