Sema Tanzania
JF-Expert Member
- May 18, 2016
- 251
- 466
Tarehe 6 Oktoba 2019 saa 10:05 Saada alipiga simu kuripoti tukio la mtoto wake mwenye umri wa miaka minne kuchomwa pasi na baba yake.
Huku akitokwa na machozi Bi Sada alieleza kuwa mumewe ni mkatili sana kwa watoto kwani kipigo chake kilisababisha mauti ya mtoto wao mwingine ambaye sasa ni marehemu. Saada alieleza kuwa yuko njiani akitoroka na mwanae na kuwa aliazima simu kwa msamaria mwema ili atupe taarifa hizi. Alikata simu na kuahidi kupiga tena.
Baada ya siku tatu za kusubiri pasi mafanikio, tulimpigia simu na kuambiwa na yule msamaria mwema kuwa tayari Bi Saada ameshahama kijijini hapo na hana tena mawasiliano naye. Tulimsihi atusaidie kujua yu wapi Bi Saada kwani tulitaka kujua hali ya mtoto aliyeunguzwa kwa pasi. Msamaria huyo alikubali kutusaidia.
Muda mchache baadaye tulipata simu toka kwa Bi Saada akitufahamisha kuwa aliondoka kijijini pale. Alituambia mtoto anaendelea vyema kwani jeraha lake linapona vizuri. Pia alituambia alikwenda Dawati la Jinsia na Watoto la Polisi ambako alitoa taarifa juu ya tukio lile kama tulivyomwelekeza. Polisi walimkamata mumewe na kumuweka rumande.
Saada anatoa shukurani kwa Huduma ya Simu kwa Mtoto kwa kufanikisha kukamatwa na kuwajibishwa lea mumewe . Tayari alikwisha omba talaka na kupewa, hivyo sasa yeye yupo huru, hayuko tena kifungoni kwa mume huyo mnyanyasaji na katili wa watoto.
Kukaa kimya na kuvumilia madhila wanayokutana nayo watoto haipendezi. Tupigie namba 116 bila malipo kwa pamoja tuzungumze. It's Possible. Inawezekana!