Simulizi

Simulizi

Mokes Junior

Member
Joined
Aug 20, 2022
Posts
7
Reaction score
0
HEKALU LA WACHAWI sehemu ya 01.

Mwandishi,, @NijoSenso

Katika dunia Kuna mambo mengi sana yaliyojificha kuliko yanayoonekana. Mwenyezi MUNGU mwenye uwezo aliumba viumbe wengi sana wanaoonekana na wasioonekana ila cha kustaajabisha, alimuumba binadam kwa mfano na sura yake ambaye baadaye alimuasi na kukaidi maagizo yake pale Eden. Uchawi Kama zilivyo imani nyingine ni mojawapo ya vitendo vinavyofanywa na binadam wengine kwa kujifurahisha na wengine kwa malengo maalum.
Tumeshasoma hadithi mbali mbali za WACHAWI ila nakuahidi hii itakuwa ya tofauti kabisa. Kuna mambo mengi yanayofanyika katika HEKALU hili ambalo lipo uwanjani Kati Kati ila hakuna mtu anayeliona. Mimi binafsi niliweza kulifaham hili HEKALU kwa msaada mkubwa wa bibi tangu. Kwa Mara ya kwanza kuingia ndani ya hili HEKALU kutambulishwa huwezi amini nilizimia. Ilikuwa mwaka 2005 kipindi hicho nikiwa na miaka 10 tu ndicho kipindi ambacho siwezi kukisahau katika maisha yangu kwani nilimpoteza mama yangu kipenzi.
Mama yangu alifariki akiwa anajifungua mdogo wangu wa kike ambaye naye pia alifariki siku tano tu baada ya kuzaliwa. Kifo cha mama yangu kilifungua ukurasa mpya wa maisha yangu nikiwa Kama mtoto wa kiume tena mwanafunzi wa darasa la nne kwa kipindi hicho. Baada ya miaka miwili kupita, baba naye alifatia akafariki katika mazingira ya kutatanisha kwani alianza kulia kichwa kinamuuma baadae alifariki tukimtibia nyumbani kwani bibi alikataa tusimpeleke hospitalini. Itaendelea sehemu ya pili.
 
Hii kali sana endelea mkuu nakufuatilia, nampenda sana hadithi za ulimwengu wa kichawi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom