TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,844
- Thread starter
- #21
SEHEMU YA 14:
“Mmmmh (niliguna moyoni kusikia maneno yake nikajikuta nimeropoka tu) sina cha kuongea zaidi ya kukupongeza tu Balbina kwa yote uliyoyapitia na bila shaka ni fundisho kwa vijana wengine wanaopitia changamoto nyingi wasikate tamaa na daima wamtangulize Mungu awaongoze katika mipango yao.”
Niliongea kama mtu mwenye busara kubwa kumbe moyo wangu naujua vyema namna ulivyojaa tamaa ya kupata pesa kwa namna yoyote ile hata ikiwezekana kwa kutoa uhai wa mtu
“Kabisa kikubwa watu wanakata tamaa mapema na kutegemea nguvu zao binafsi huku wakisahau kwamba Mungu ndiye anayepanga riziki ya kila kiumbe wake.”
Balbina alizidi kuuteka moyo wangu kwa maelezo yake ya kishujaa na yaliyokwenda shule
“Kweli maisha pande mbili mana unalijua la leo tu ila la kesho hulijui, pole na hongera sana kwa moyo ulionao.”
Nilimpa hongera kwa changamoto kubwa alizokutana nazo katika maisha yake lakini bado akapambana na kuzishinda na hatimaye akaweza kufika hapo alipo.Tuliendelea kupiga stori mpaka mida ya saa kumi na moja akawa anahisi usingizi hivyo akaniomba akalale nami nikamwambia haina shida akajipumzishe tu na mimi nikajinyanyua tayari kuingia mtaani pande za kijiwe ninachopenda kukaa. Tunapenda kukaa kijiweni hapo kubadilishana mawazo na kupeana mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto za maisha na pia kunywa kahawa. Nilikaa pale mpaka mida ya saa moja jioni kisha nikarudi nyumbani nikaoge na kujipumzisha maana sikupumzika tangu nilipoamka na pia kumwona Balbina maana tayari alikwishaniingia mazima moyoni. Nilirudi mpaka chumbani kwangu kisha nikajiandaa kwenda kuoga, baada ya kumaliza kuoga niliwasha luninga na kuanza kuangalia tamthiliya huku nikipitia magazeti ambayo tayari nilikwishayasoma ila nilikuwa nikiyapitia kwaajili ya kusogeza muda mbele tu angalau usingizi unipitie. Ilipotimu mida ya saa mbili za usiku nilibadili chaneli na kuanza kuangalia taarifa ya habari ya siku nzima kwani katika ratiba yangu hakuna siku inayoweza kunipita bila kuangalia taarifa ya habari, ilipofika mida ya saa mbili na nusu nilisikia sauti ya Balbina mlangoni mwangu akiwa ananiita. Nilipoenda kufungua lahaula nikapigwa na butwaa kumkuta mtoto wa kike ndani ya kanga moja tu huku akinitazama kwa umakini na macho yake malegevu nusura uzalendo unishinde mdomo ubaki wazi kwa kushangaa ila nikajizuia kiume tu, kwa sauti yake nyororo akasema
“Samahani kwa usumbufu nilitaka kujua kama upo ndani, umeshakula chakula cha usiku?”
alipouliza vile sijui hata ni muda gani nilijibu maana ghafla nilijikuta nimesharopoka
“bado bado kabisa (kwa msisitizo mkubwa”
mpaka nikajishangaa imekuwaje nimeongea pasipokujua kwamba naongea ila bila hiyana akaniambia
“Basi mida ya chakula hii jiandae tuje kula basi”
“Ooooh (Mapigo ya moyo yakinienda mbio) nipo bwana, ukimaliza kuvaa utanishtua ili tule basi.”
Niliongea macho yakiwa yamenitoka kwelikweli kuona namna Balbina alivyovaa na sielewi alitambua nilichokuwa nawaza hivyo akasema
“Usijali nitabadilisha lakini huwa nalala hivi hivi maana si unajua joto la mji wetu hatari tupu?”
Kwa sauti tulivu na iliyojaa kila aina ya hamasa. Aliponena vile niliachia mguno wa haja
“Mmmmmmmh ni kweli ila poa tunalia chakula nje au ndani?”
sielewi hata kwanini niliuliza swali la kipuuzi vile ilihali nilijua kabisa ni usiku hakika nilichanganyikiwa, ila kwa ustaarabu Balbina alinijibu
“Wewe usiku sasa hivi wee njoo ndani kwangu kisha tukimaliza kula utarudi chumbani kwako kulala.”
Aliponijibu vile hakika nilijihisi mpumbavu kwani hata kama sikusoma ila nilianza kujiona mpumbavu kuuliza maswali ya kijinga vile na kwa upole na sauti ya chini nikamjibu
“Poa basi wewe andaa kabisa msosi mimi naenda kwa mangi kuchukua soda kama mchana kisha nakuja sasa hivi.”
Nilivyoongea vile akanielewa haraka kisha akasema
“Sawa mtu wangu nakusubiria basi (Akiondoka kuelekea chumbani kwake)”.
Nilimuangalia mpaka alipoingia ndani kwake huku uzalendo ukiwa umenishinda namna alivyokuwa ameumbika na ndani ya kanga moja, nilirudi chumbani kwangu kisha nikaanza kutafakari namna nitakavyoanza
ITAENDELEA...