SIMULIZI: Zafeera

SIMULIZI: Zafeera

TAECOLTD

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2013
Posts
1,051
Reaction score
1,844
Story : ZAFEERA
Mwandishi : Gerald Mtenga
Mawasiliano : 0625600802
Barua pepe : gmtenga@gmail.com

UTANGULIZI :
Bila shaka hakuna binadamu anayependa kuishi maisha ya kimasikini na ya kujidhalilisha mbele ya jamii lakini tukatae au kukubaliana na ukweli kuwa uwezo wa watu umetofautiana sana. Umasikini uliokithiri ndiyo chanzo cha matatizo mengi katika jamii zetu kama ujambazi, ukahaba, utapeli, uchawi n.k na vijana wanahangaika usiku na mchana kuweza kujikomboa na mkono wa jinamizi wa umasikini anayewakaba koo ,na wengine wakikimbia maisha ya mjini na kuelekea vijijini na kuishia kwenye tufani la umasikini mkubwa. Hii ndiyo sababu kubwa iliyomfanya kijana Gerald anayetokea katika maisha ya kimasikini kujiapiza kwamba atahakikisha anaukamata utajiri kwa nyanja yoyote na kufanikiwa kupindua historia ya ukoo wao ambao haujawahi kuwa na msomi wala tajiri yeyote. Katika kitabu hiki utaona namna Zafeera anavyomsababishia kijana Gerald kuharibu njia zake hapa ulimwenguni na kuishia kwenye majuto makubwa.

Ilikuwa vipi mpaka akafanikiwa kufikia ndoto zake na hatimaye kuziharibu mwenyewe? Fuatana na mimi katika kitabu hiki mwanzo hadi mwisho ili uweze kuburudika na kujifunza mambo mengi ambayo yatakusaidia wewe kuweza kutambua mambo ambayo yalikuwa kama ukungu mzito uliokuwa umetanda katika mboni za macho yako. Ikumbukwe majina yote yaliyotumika katika kitabu hiki ni ya kusadikika na kumrathi kwa yeyote atakayekuta jina lake hapa, atambue ya kwamba sijamlenga yeyote katika stori hii.

SEHEMU YA 1:
Ilikuwa ni siku ya jumamosi tulivu kabisa ya mwaka 2006 nikiwa nimepumzika pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya Hindi jijini Dar es salaam, na kutafakari mahala maisha yangu yalipotoka mpaka hapa nilipo na kujaribu kupanga na kutafakari mambo yangu ya maisha tangu awali hadi huko siku za usoni. Nikiwa nimezama katika wimbi la mawazo ghafla lilinijia wazo zuri ambalo ilinibidi kulitekeleza ipasavyo, kutokana na hali ya maisha yangu kuwa ya kawaida sana hivyo wazo langu ilikuwa ni kuanzisha banda la kuuza nguo na mashuka ya mtumba.

Nilitafakari kwa muda mrefu na jua lilikuwa limekwishapata usingizi na kufumba macho yake barabara, hivyo ilinilazimu kujinyanyua mahala pale kwani hata wasimamizi wa ufukwe ule walikuwa wakiwaondoa watu eneo la ufukwe kwa muda ule hivyo kuamua kutafuta usafiri wa kurudi nyumbani. Kwa kuwa nilikuwa ufukwe wa koko maeneo ya msasani na maskani yangu yalikuwa ni pande za manzese, niliamua kupanda gari za masaki-kariakoo na gari ilipofika magomeni hospitali niliteremka na kuanza kutembea kuelekea kituo cha usalama ili nipande gari za ubungo.
ITAENDELEA...

SEHEMU YA 2:
Ilikuwa ni mida ya saa moja usiku nikiwa natembea taratibu kuelekea kituo cha basi ambapo ningepanda gari na kufika nyumbani. Nilikuwa na shauku ya kufika mtaani ili niende kwa rafiki yangu Regan ambaye alikuwa ni rafiki na pia kaka yangu mkubwa, nilitaka nimdokeze wazo langu ambalo kwa wakati huo niliamini lilikuwa wazo zuri kupita mawazo yangu ya awali. Nikiwa nakunja kona ya magomeni kwenye ukuta wa hospitali ya magomeni niliona kitu ardhini kikiwa kinang’aa sana.

Nilipiga hatua kadhaa za haraka haraka na kukiinamia kile kitu na kukiokota haraka sana kisha nikaanza kutazama kushoto na kulia kama mwizi aliyetoka kuvunja nyumba na kuiba vito vya thamani. Simu yangu ya kichina iliyokuwa na tochi kali ilinisaidia barabara kuweza kukitazama kile kitu nilichokiokota na maneno yakawa wazi yakisomeka "Zafeera" na maneno mengine ya kilugha ambacho sijawahi kukiona labda sababu sikuwa na elimu kubwa hivyo lugha ile ilinipiga chenga. Kichuma chenyewe kilikuwa na rangi ya dhahabu huku kikiwa kinang’aa sana kikiwa na muonekano wa tofauti na vyuma nilivyowahi kuviona iwe kwenye televusheni au magazetini.
ITAENDELEA...

SEHEMU YA 3:
Baada ya kujirithisha kwamba kile kichuma nilichokiokota kilikuwa na uashiria wa asilimia kubwa kuwa ni dhahabu niliangalia tena pande zote safari hii nikiwa na mashaka kama kuna mtu yeyote aliniona wakati nikikiokota kitu kile. Nilipojiridhisha ya kwamba hakuna aliyeniona niliamua kukihifadhi vizuri kwenye mfuko wa ndani ya suruali yangu (si unajua sisi masikini nguo zetu zinakuwa na mifuko mingi hadi ya ndani ya nguo ili kuhifadhi akiba zetu zisipotee kirahisi).

Baada ya kuhakikisha nimekihifadhi vyema mfukoni nilianza kutembea kwa madaha huku nikiachia tabasamu la ushindi na kuamini kuwa ndio mwanzo wa mafanikio yangu. Niliamini kuwa iwapo ningeenda kukiuza basi ningepata fedha nyingi ambazo zingeniwezesha kufanya biashara kubwa, niliamua kumpigia simu mshikaji wangu Regan kwa migoko mikubwa ili kujua kama yupo chumbani kwake ama kijiweni tunapopenda kukaa jioni baada ya shughuli za kutwa nzima.
“Oyoo, niaje mwanangu mwenyewe?”

“Freshii tu kaka Gerald, vipi?”
“Poa poa mwana, umejiachia pande zipi wewe?”
“Nipo geto tu nimejinyosha kitandani maana najisikia hovyo sana kaka na ndio maana leo maskani nimeshindwa kupanda”
“Aaaah unaumwa wapi wewe, utakuwa umeshapata dawa zako ndio maana umeamua kuvutia stimu magetoni kama kawaida yako”
“Unanirushia njiwa mwana, leo sijapata dawa kabisa maana sijapanda maskani na kama nilivyokuambia najihsi mwili mzima naumwa.”

“Hah hah hah hah hah hah wewe huyo siku ipite hujapata dawa? Labda unataka kuanza kuniuzia chai kama sikujui vile”
ITAENDELEA...

SEHEMU YA 4:
“Hah hah hah hah haya bwana, tuachane na hayo nipe habari zingine”
“Poa poa mimi nipo magomeni hapa nakuja maskani hapo maana nina bonge la dili na wazo la msingi mtu wangu”

“Aaah we Gerald nimeshakuzoea siasa kibao mshkaji wangu, unanirushia stimu tu”
“Mwana we ngoja nije dakika kama kumi hivi nitakuwa hapo, maana hata salio lenyewe linakata sasa hivi”
“Haina kwere kaka, nakusubiria”

Nilivuka barabara na kuelekea upande wa kituo cha magari ya ubungo na kusimama maeneo yale kungojea usafiri. Kama ilivyo kawaida ya usafiri wetu wa jijini ulivyo mgumu, kila basi lililokuja kituoni pale lilikuwa limeshiba abiria mpaka pomoni. Usafiri unapokuwa mgumu ni kawaida kwa wenye magari yao binafsi kusimamisha magari yao kituoni na kutangaza kwa uchu mkubwa bei zao wanazopendezwa nazo. Kwakuwa nilikwishasimama pale kituoni zaidi ya nusu saa hivyo nilikata shauri na kuamua kupanda gari za watu binafsi kwa bei mara tatu zaidi ya nauli za mabasi ya kawaida.

Gari ilikata vituo kadhaa kwa mwendo wa wastani kuashiria kwamba dereva alikuwa mstaarabu na mjuzi, ilipofika tip-top niliomba kushushwa na dereva bila hiyana alisimamisha gari na nilimlipa haki yake kisha nikateremka na kuanza kuelekea nyumbani. Nilinyoosha na ile barabara moja kwa moja mpaka kuifikia njia ya mabibo kisha nikakunja kona na kupiga hatua kama ishirini nikawa nimefika maeneo anayoishi mshakaji wangu Regan. Nilibisha hodi pale mlangoni na nilisikia sauti kwa ndani ikiniashiria niingie ndani, niliingia ndani na kumkuta jamaa akiwa amejilaza kitandani huku akitazama luninga.

“Yani jamaa yangu tangu saa moja umenipigia simu na kuniambia dakika kumi utakuwepo lakini hapa saa zima limepita ndio dakika kumi za siku hizi?”
“Aaah usafiri mizinguo kinoma noma yani magari yameshona mbaya, si unajua leo wikiendi watu kibao wametoka kula bata”
“(Akinicheka) na wewe mmoja wao umetoka kula bata au siyo?”
ITAENDELEA...

SEHEMU YA 5:
“Aaaaaah hilo sio la kuuliza, nimetoka kujiachia mbele mbele kula bata kama vigogo wanavyofanya vile”
“(Akiendelea kucheka kwa nguvu zaidi)”
“Sasa kinachokuchekesha ni kitu gani haswa, kwani kipi kigeni hapo?” “Unanichekesha sana, umetoka kula bata au umetoka kutangaza shida zako huko na umasikini wako”
“Kwa sasa kweli ni masikini lakini nakuapia mbele za Mungu lazima niwe tajiri mkubwa sana hapa nchini na duniani lazima wanitambue”
“Wapi wewee, mwenye nacho ataendelea kuongezewa na yule asiye nacho hata kile kidogo alicho nacho kitaondolewa”
“Hayo unasema wewe ila sio mimi na napozidi kupata adha ya usafiri wanazidi kuntia hasira za kupambana na maisha mpaka na mimi nifike juu sana zaidi yao”
“Freshi ndio maisha hayo si unajua jiji lenyewe limeshona watu kibao mpaka kero”
“Tuachane na hayo, duuuh kweli mwana utakuwa unaumwa maana madudu yako hujayaleta leo? Maana daily unaleta mwanamke na unabadili kama nguo, utakufa na mizoga yako kaka”

“Ushaanza porojo zako, wanawake wamewekwa ili watumike sio kama wewe mzinguaji. Halafu jamaa yangu sijui kama wewe ni mzima au rijali kweli maana tangu umeachana na Patricia miaka kibao iliyopita sijawahi kusikia hata shemeji wa kusingiziwa?”

“Hivi kaka unaona maisha tunayoishi yanavyotuzingua na ndio maana jamaa yangu hupigi hatua, kila siku ni wanawake, pombe na ganja zako Jirekebishe ushakuwa mtu mzima wewe”
“Ndio maana huwa nakuambia wewe Gerald siasa nyingi, yani unaongeeeea kama upo kwenye kampeni bwana. Enhee nipe michongo ya maana achana na siasa zako”

“Sio siasa bali nakuchana uhalisia wenyewe hivyo, tatizo lako hupendi kuambiwa ukweli hata siku moja”
“Tuachane na hayo nipe habari uliyosema utaniambia ukifika hapa, maana naona unamwaga sera sijui ili nichague chama gani cha siasa mshkaji wangu”
ITAENDELEA...

SEHEMU YA 6:
“Poa haina noma kaka mkubwa, Sasa leo nimepata wazo zuri sana, unaona pande hizi zote za mabibo na manzese? Wakitaka kununua nguo au mashuka hawaendi kariakoo au posta bali kwakuwa maisha yao ni ya chini kama ya kwetu hulazimika kwenda mahakama ya ndizi au karume kupata mahitaji yao”
“Naelewa hilo we nenda kwenye point husika acha kuzunguka mbuyu”
“Hata hivyo ndiyo nilikuwa naenda kwenye point, nimekueleza hayo ili uweze kunielewa barabara. Si unajua kuwa mimi napenda sana kumuelezea mtu hadi anielewe?”

“Sawa ndio nakusikiliza hivyo”
“Sasa mimi nimekuja na wazo la kufungua biashara ya duka la nguo na mashuka ya mitumba kaka”
“Ahah hah hah hah hah hah hah hah hah hah (kicheko cha nguvu)”
“Sasa mbona unanicheka kabla hata sijamaliza? (nikikunja sura kuashiria nimekasirishwa na kitendo kile)”
“Mwana umeongea siriazi nikajua booonge moja la wazo kumbe ni suala la kuwa “machinga”?!”

“Umetafakari ndivyo s..............(akanikatisha)”
“Haina haja ya kuendelea kunipa elimu nimeshakupata vizuri kabisa, unataka tufanye biashara ya machinga wa nguo za mitumba. Hah hah hah hah hah hah hah hah masuala ya ‘za leo leo bei nzuri, bei poa anabeba anabeba mia tano, mia tano, mia tano’ hahahaha basi kaka hilo wazo sijaliafiki kabisa.”
Nilipata ghadhabu sana hadi sura ikabadilika kwa maana sikutegemea jamaa angelipuuza wazo langu kiurahisi vile tena kwa dharau kama aliyekuwa anaongea ni mtoto mdogo. Lakini nilifanikiwa kutuliza hasira zangu kisha kwa upole nikamuuliza. “Poa nimekuelewa kaka mkubwa kwa maelezo yako, sasa basi nipe wewe wazo unaloona ni zuri na imara kuliko nililolisema mimi basi”
“Nilishakuambia tukikaza kwenye fani hii ya muziki lazima tutoke yaani wewe kama kawaida unachana na kutengeneza midundo ya ukweli na mimi naimba mwanzo mwisho, lazima tung’ae maana one day yes”

“Lakini kaka huu ni mwaka wa ngapi tunajihusisha na muziki bila mafanikio na hata kwenye kata yetu hatujulikani?”
“Wee tambua hata mbuyu ulianza kama mchicha, tukikaza one day lazima uwe zaidi ya wana profesa Jay na mimi bongo fleva watangoja sana si unajua ninavyojua kuipanga sauti yangu ya ukweli”
“Aaaahah hah hah hah hah hah hah hah unajidanganya sana ndugu yangu, huu mwaka wa sita unajidanganya tu hivyo. Yani kama usingekuwa pusha na kucheza kwako kamari basi ungeshauliwa kwa wizi, maana huo muziki hauna manufaa yoyote kwako”

“Sawa upusha wangu na kamari vinaniingizia sana hela lakini suala la kuwa machinga hapana kaka. Nilijua unaniletea wazo la maana kwamba umepata dili la kusukuma kete za poda (madawa ya kulevya) ambalo ndilo dili ninaloliwinda badala yake unaniletea ishu za kuuza mashuka bwana”
“Ila nimeshakuzoea jamaa yangu, ukiendelea kuwa na mawazo yako mgando utakuja kuishia mahali pabaya sana na ukipona pona utakuja kujutia njia zako za sasa unazozipitia”

“Utaishia na ushauri wako hivyo hivyo huku wenzio wanapiga mtonyo. Ila mwana nikitoka sitakusahau ili uwe unanipa mahubiri na ushauri wako vizuri hah hah hah hah hah hah”
“Hah hah hah hah hah endelea kujidanganya hivyo hivyo. Poa bwana haina noma namna gani vipi naenda kuegesha mwili kitandani si unaona mida nayo imesogea saa nne sasa hivi Kwahiyo usiku mwema kaka nitakucheki kesho basi”
“Haina noma askari wangu nimekuelewa vizuri kabisa, usiku mwema pia ila leo nalala mpweke sana shemeji yako hajaja bwana”

“Haha hah hah hah hah kumbatia mto. Poa bwana kesho”
Baada ya kumaliza kuzungumza na Regan nilimuaga kisha nikaondoka nikiwa na mawazo tele na nilijiamini sana kwani nikikumbuka nina dhahabu mfukoni basi niliona tayari ulimwengu ni wangu na nilitamani kukuche haraka niweze kwenda kwa sonara nikachukue hela yangu na nikaanza kupanga mipango mingi.
ITAENDELEA...
 
Yaan anaweka fupi fupi halaf ukuje makapuku nilisahau kukuita nimeweka story kule mpaka episode ya 10
Mniwie radhi jaman, mwanzo nilijaribu kuweka ndefu saaana ikanigomea ikabidi nianze kuedit kufupisha sababu ipo katika mfumo wa kitabu ambacho ni rasmi nachofanya na-copy na kuja kui-paste hapa wakuu
 
Mniwie radhi jaman, mwanzo nilijaribu kuweka ndefu saaana ikanigomea ikabidi nianze kuedit kufupisha sababu ipo katika mfumo wa kitabu ambacho ni rasmi nachofanya na-copy na kuja kui-paste hapa wakuu
Sawa mkuu tumekuelewa
 
SEHEMU YA 7:
Hapakuwa mbali na nyumba ninayoishi hivyo hatua zilihesabika kuweza kufika lakini nilitembea taaratibu yaani kibosi kama wengi wasemavyo, nilifika chumbani kwangu kisha nikaingia ndani ya chumba changu nikiwa nimechoka kupita maelezo. Nilijitupa kitandani kwa lengo la kujinyoosha dakika kadhaa kisha nikaoge na baada ya hapo nirudi na kuanza kula chakula nilichokuwa nimekipika mchana. Kutokana na uchovu niliokuwa nao sana nilipitiwa na usingizi bila kujitambua, usiku wa manane niliota njozi ya ajabu sana. Nipo kwenye jengo kubwa na refu sana kwenda juu na kileleni mwake limeandikwa nembo kubwa sana ikisomeka "Gerald & Zafeera Company Limited" nikiwa ndani ya hilo jengo nilishangaa kupishana na watu wengi sana wakinisalimu
“habari yako boss”.
Nilipofika ghorofa ya juu kabisa ile natoka tu kwenye lift msichana mmoja aliyekuwa mzuri sana na nadhifu wa kuvutia alinifuata na kuniambia ;
“Boss mke wako anakusubiri ofisini kwako”
“(Nikishangaa shangaa kisha akanichukua mpaka alipokuwepo yule mtu aliyekuwa akinisubiria) Nashukuru sana”
Wakati nafungua mlango tayari kuingia ofisini akanyanyuka kwenye kiti mule ofisini mwanamke mmoja hivi mweupe, mrefu wastani, mwenye nywele ndefu na mzuri sana sijui mfano wake hapa duniani. Akaja mpaka niliposimama na kunikumbatia kwa nguvu na kunong’ona masikioni mwangu kwa sauti ya mahaba
“nimekumisi mume wangu” huku akinibusu. Mwili mzima ukasisimka na ghafla nikastuka usingizini huku jasho likiwa linanitiririka na nilipoitazama saa yangu mishale ililenga saa nane za usiku. Wakati nimekaa kitandani natafakari ndoto niliyoiota niliyatupa macho yangu kila kona ya chumba changu na ghafla yakatua mezani nikaona kitu kinang’aa sana taratibu nikanyanyuka na kuisogelea meza ndipo nilipogundua kile kitu ni kama kile nilichokiokota maeneo ya hospitali ya magomeni. Nikakumbuka kuwa nilikiweka mfuko wa ndani wa suruali yangu, nilipojisachi sikukiona kile kitu mfukoni mwangu nikazidi kuchanganyikiwa. Nilianza kurudisha kumbukumbu zangu nyuma na kumbukumbu zilinijia sawia kwamba wakati naingia chumbani na kuufunga mlango (Nikahakikisha kutazama mlango) vizuri sikutoa chochote mfukoni na hata simu bado ilikuwa mfukoni, sasa inawezekanaje hicho kitu kutoka mfuko wa ndani wa suruali mpaka kufika mezani?! Mapigo ya moyo yalianza kunienda mbio nikaanza kukiogopa chumba changu mwenyewe ambacho siku zote ndicho huifadhi mwili wangu. Nilianza kumpigia simu rafiki yangu Regan na simu iliita mara nyingi bila mafanikio. Kwa uoga mkubwa niliwasha luninga yangu na kuanza kujipooza kwa kuangalia filamu nikiwa kitandani na hata njaa sikuihisi tena. Sikumbuki ni mida gani nilipitiliza usingizini na safari hii nikaota ndoto ya kuogofya sana, niliota nipo na watu wengi nawaaga (kuwakumbatia kisha kuwapungia mkono) huku nikiwa nimebeba begi jeusi mgongoni kisha mbele yangu kukiwa na vichochoro vingi sana. Basi nikaanza kutembea kufuata vile vichochoro, nilitembea umbali mrefu sana huku nikiwa nimechoka ghafla nilitokea sehemu yenye majengo marefu sana kwa upana na pembeni kulikuwa na mto mpana sana unaotiririsha maji yake. Milango ya majengo yote ilikuwa imefungwa kasoro mlango mmoja tu uliokuwa karibu na ule mto, ndani ya chumba kile alikuwepo mama mmoja aliyekuwa amekaa kwenye meza yenye vitabu vingi sana na huyo mama alikuwa amevaa miwani huku akisoma vitabu vile bila wasiwasi wowote. Kwa mbali upande wa pili wa ule mto niliona kijana anavuka ule mto, alipofika katikati akasombwa na maji lakini akafanikiwa kushikilia mti uliokuwa katikati ya ule mto. Nilipoangalia vizuri pembeni ya ule mto nikaona joka kubwa sana lililokuwa limejiviringisha na lilikuwa kubwa kuliko hata ghorofa nililowahi kuliona katika maisha yangu, kichwa chake alikuwa amekilaza kwenye ule mto uliokuwa unatiririsha maji. Nilipomuangalia vizuri yule mtu aliyekuwa anavuka awali na safari hii akiwa ameshikilia mti ule ili asisombwe na maji, niligundua amefanana na mimi kila kitu. Wakati nikiwa nimepigwa na butwaa pale ghafla kwenye kile chumba alimokuwamo yule mama akinitazama na kuita
“Gerald”
sauti yake ilikuwa nzito sana mithili ya sauti ya radi nzito inavyopiga. Ndipo akaniambia
“Tazama umeyashuhudia haya yote kwa macho yako mawili, umechaguliwa kuingia kwenye ukoo wa kifalme ila kamwe usijaribu kumsimulia mtu yeyote"
ndipo nikapata ujasiri wa ajabu na kumuuliza
“Nimechaguliwa vipi kuingia kwenye ukoo wa kifalme ilihali maisha yangu ni ya duni sana?!”
Akanijibu kwa msisitizo
“umechaguliwa hata kabla hujazaliwa na hii itabaki kuwa siri yako hutatakiwa kumuambia yeyote na chochote kitakachoanza kukutokea usiogope kwa kuwa siku zako za kuishi katika maisha ya kimasikini zinaelekea ukingoni”.
Alivyomaliza aliniamuru nigeuze na kuondoka kwa barabara niliyokuja nayo na ghafla nikashtushwa na sauti ya mtu aliyekuwa akigonga mlangoni mwangu kwa nje. Nilijinyanyua pale kitandani na kwenda kufungua mlango na kumbe alikuwa ni mpangaji mwenzangu wa chumba cha pili aliyekuwa akiitwa Balbina ni rafiki yangu na pia shemeji yangu kwa rafiki yangu aliyeitwa Crispin. Alipanga chumba na sebule huku mimi nikiwa na chumba kimoja tu eneo lile, alinisalimu kwa bashasha tele
ITAENDELEA...
 
SEHEMU YA 8:
“Habari za asubuhi Gerald?”
“Nzuri tu, mbona mapema sana?”
“Aaaah mapema wapi wewe, sasa ni saa kumi na mbili na si unajua leo jumapili hivyo tunataka kwenda kanisani hivi”
“Aiyaaaaah daah yaani Balbina hata sijaandaa nguo za kanisani, nguo zangu zote chafu ndo nataka nifue zote leo”
“Yaani wewe mwanaume huishiwagi visingizio kila jumapili mara nguo chafu, mara unaumwa visingizio vingi au wewe mwanaume umelogwa nini?”
“Hah hah hah hah hah hamna sijalogwa bwana ila kweli wiki ijayo nistue twende wote ila leo kaniombee tu mtu wangu”
“Mmmmh nimeshakuzoea wewe kwa uvivu wako huo, namuonea huruma sana wifi yangu. Poa mida basi mimi nawahi misa ya kwanza hivyo”
“Freshi basi ila ukirudi si utanisaidia kusuuza nguo na kuzianika kama kawaida maana nitakuwa nazifua halafu najisikia hovyo leo”
“Pole sana, usijali nitakusaidia nikirudi (Akiondoka nami nikamsindikiza kwa macho mpaka nikahakikisha ameishia)”
Balbina alivyoondoka nilirudi ndani na kurudishia mlango wangu kisha nikarudi kukaa kitandani huku nikiwa nimeinamisha kichwa kama mtu aliyekuwa na mawazo sana. Nikiwa katika mawazo yangu nikakumbuka ya kuwa mida ya saa nane usiku nilipogutuka usingizini niliamua kuangalia muvi mpaka usingizi uliponipitia tena bila ya kuzima luninga, cha ajabu nilipoitazama luninga yangu ilikuwa imezimwa kabisa kana kwamba haikuguswa tangia jana mchana nilivyoiacha. Nilipoyatupa macho yangu pale mezani kwa uhakika wa kukiona kile kitu nilichokiona usiku nilishtuka baada ya macho yangu kutoona chochote pale mezani, nilipigwa na butwaa na kuanza kujiuliza kimekwenda wapi? Nilipojikagua nilishangaa kukikuta mfukoni kama nilivyokiweka awali nilipokiokota pale magomeni, nilikurupuka mbio na kuacha nyumba kadhaa kisha nikafika kwenye chumba cha jamaa yangu Regan nikiwa nimechanganyikiwa, nilidhani nipo ndotoni kumbe ndio mambo yaliyokuwa yanatokea katika ulimwengu wa macho yangu. Regan aliufungua mlango wake huku akionekana amechoka sana kama masaa kadhaa ametoka kufanya kazi ya kupasua kokoto, alivyofungua mlango tu nikataka kuingia ndani
“Kaka mbona asubuhi asubuhi hivi, kuna kitu cha maana ulikisahau humu ndani ulipoondoka jana usiku nini?”
“Hapana kaka ngoja kwanza niingie ndani maana nahisi kichwa changu kizito sana mtu wangu naweza kuanguka ujue”
“Aaaah ngoja kwanza kaka tukae hapa nje maana ndani shemeji yako Antonia kajipumzisha, unielezee nini hasa tatizo?”
“Antonia??? (nikihema kwa nguvu) Hivi kaka una wanawake wangapi hasa maana wengi sana mpaka wengine naanza kuwasahau mara Aquilina, Domitilla, Habiba, Blandina, Faustina, Cassia, Fadhila, Swaumu, Gratiana, Pili na sasa Antonia. Una malengo gani hasa na hao wanawake wengi hivyo ndugu yangu???”
“Ssssssssh!!!! (akiniziba mdomo) Ongea taratibu Antonia asije akakusikia maana utakuwa ugomvi na anavyonipenda ni hatari. Halafu sina mpango na yeyote kabisa, mimi nawatumia kwa haja zangu nikijirithisha haja zangu basi lakini sina future na yeyote kati yao kwani hujui ya kwamba “mwanamke ni kama udongo wenye rutuba hivyo rutuba ikiisha mkulima uhama na kutafuta ardhi yenye rutuba tena?!”
“Mmmmmh silitambui hilo kaka na hongera kwa ushujaa wako huo ila tambua ulimwengu huu ni tofauti na enzi za babu zetu, magonjwa mengi sana kama kaswende, ukimwi, gono, pangusa na mengine mengi sana jihadhari tusije tukakuzika kilo tano mshkaji wangu”
“Siwezi kufa kifala hivyo wewe (Kwa mbwembwe), mimi nawachapa nao lakini afya yangu naijali kupita maelezo, hivi una habari kwamba shemeji zako wote kabla sijawagonga mwanzoni huwa tunaenda kupima afya kwanza?”
“Silitambui hilo lakini pia kupima afya sio kigezo cha kutopata maradhi, wewe una wanawake wengi hivi na kila mmoja anajijua yupo peke yake je una uhakika gani kuwa na wewe kwao upo peke yako?”
“Hamna kitu kama hicho kaka, mimi kiboko yao nawapagawisha na ndio maana nina uhakika nipo peke yangu kwao”
ITAENDELEA...
 
SEHEMU YA 9:
“Hahahahahahaha nicheke mie asubuhi ya leo niongeze idadi ya miaka ya kuishi, kila mwanaume hujiona shababi kuliko mwenzake lakini ukweli hakuna nguli wa ngono. Akija kwako unampagawisha vivyo hivyo akienda kwa mwenzako nae anajituma na anapagawa vile vile, acha kujiwekea dhana mbovu kichwani mwako ndugu yangu”
“Hivi kaka unataka niweje maana kila nikikaa na wewe unanihubiria na siasa zako, unataka niwe hanidhi au? Akyamungu ukiendelea hivyo nitaanza kukukwepa, ila freshi tu niambie kulikoni asubuhi yote hii na mapema?”
Ile nataka kuanza kuongea tu mara kwenye chumba cha Regan akatoka mwanamke alikuwa mzuri kiukweli bila kupaka mate chini alivutia kwa kumtazama. Alibeba ndoo yenye maji mkononi akiwa amejifunga kanga moja iliyochora maungo yake sawasawa na mkono mwingine alikuwa amebeba jagi lenye maji na mswaki kuashiria alikua akielekea bafuni kuoga na pia kusugua meno. Alinisalimu kwa sauti nzuri ya kutoka kuamka nami bila hiyana nilimuitikia huku nikiwa namkazia macho mpaka alipoingia bafuni.
“Unaona mtoto huyo? Halafu ndio unaniambia niache mademu, watoto wazuri kama hawa nani awagonge kama sio mimi?”
“Duuuh kaka unafaidi maana mtoto mzuri utadhani hajazaliwa maana hana kasoro”
“Mimi sichagui manung’aembe kaka, shemeji zako wote viwango”
“Mmmmh haya bwana mkubwa heshima zako kwa raha unazozipata ila kwa hali hii ndugu yangu Ukimwi unakuita kabisa maana kwa msichana mzuri namna hii awe na masikini kama wewe tu bila kuwa na mibaba inayompa uwezo wa kuishi hapa mjini ni jambo ambalo haliwezekani kabisa na tena usijidanganye eti upo peke yako”
“Maneno yako tu hayo mimi ukimwi hauwezi kuniondoa kwani mimi ni chuma cha reli na pia kumbuka mimi ni mwisho wa matatizo nachapa ilale mpaka wanapagawa”
Baada ya maongezi ya muda mrefu na kucheka mara simu ya Regan iliita na alinyanyuka na kwenda kuongea pembeni, mimi niliinamisha kichwa chini na kuanza kutafakari yote yaliyonitokea usiku na asubuhi lakini sauti ikanikumbusha onyo nililopewa kuwa
“umechaguliwa hata kabla hujazaliwa na hii itabaki kuwa siri yako hutatakiwa kumwambia yeyote na chochote kitakachoanza kukutokea usiogope kwakuwa siku zako za kuishi maisha ya kimasikini zinaelekea ukingoni”
ilijirudia rudia kichwani mara kadhaa. Nilishusha pumzi ndefu kisha nikamwambia jamaa yangu aliyekwisha maliza kuzungumza na simu, niliamua kumuambia uongo tu ili kupotezea uhalisia.
“Kaka naona missed call zako kibao za jana usiku, kulikoni tena?”
“Haswaa ndicho kilichonileta hapa baada ya kuona hukupokea simu”
nilipomwambia vile akanikazia macho kuashiria ya kwamba ananisikiliza kwa makini.
“Kaka jana usiku nimefika home nikakumbuka kuwa leo ni jumapili na kuhusu sherehe ya ndoa ya jamaa yetu Azizi wa kibamba, sasa usiku ndio nikawa nakupigia simu kukukumbusha kuwa ni leo na inabidi uende. Mimi sitaweza maana nguo zangu zote ni chafu na inabidi nikapige usafi wa maana leo”
“Nakumbuka vizuri kabisa na nilishaandaa nguo na kila kitu, nilishakuambia tafuta mwanamke awe anakufanyia usafi na kukufulia pamoja na kupika kaka. Si unaona mimi hadi raha nafuliwa, nafanyiwa usafi na kupikiwa na zaidi ya hapo nawagonga kama kawa, poa nitakuazima zangu kwa leo”
“Hapana ndugu yangu ngoja leo nikomae nifue na kufanya usafi mpaka nimalize kila kitu leo, wewe nenda ukaniwakilishe mwanao huko mtie kamba jamaa mwambie Gerald anaumwa kinoma noma na ameshindwa kuja bila shaka nitaeleweka tu”
Wakati nikiongea vile Antonia akawa ametoka bafuni huku ameshikilia ndoo mkononi na jagi lake, safari hii kanga ilikuwa imeloa loa maji ya mwilini mwake hivyo ilimchora barabara. Alinitazama kwa jicho la wizi kuashiria kama alivutiwa na mimi kisha akafungua mlango na kuingia ndani, niliishia kuingiwa na tamaa lakini nilijizuia na kuendelea na stori na Regan.
“Hivi kaka Antonia amekuja saa ngapi? Maana kwa kumbukumbu zangu hapa nimeondoka mida ya saa nne usiku”
“Hah hah hah hah hah hah hah alikuja kwenye mida ya saa tano alivyomaliza kufunga biashara yake mbezi, nikampigia simu aje lakini kwakuwa ilikuwa usiku nikamwambia apande bajaji mpaka hapa maana usiku usingizi uligoma kabisa kuja bila mchuchu pembeni”
ITAENDELEA...
 
SEHEMU YA 10:
“Duuuh umekwisha athirika na wanawake kaka inabidi ufanye mchakato wa kupunguza maana hiyo hali itakutesa siku zote na itakusababishia uishie kupata magonjwa ya zinaa”
“Aaaah wapi siwezi kupunguza nitawachapa nao mpaka nguvu ziniishie kabisa, ila mwana yule Balbina jirani yako pale ni wa ukweli kinyaama hakika penye miti mingi hakuna wajenzi”
“Hapana kaka yule ni rafiki yangu tu halafu si unajua jamaa yake ni mwanetu pia?”
“Urafiki nchi za watu, kuna urafiki kati ya mwanamke na mwanaume Tanzania hii ya leo? Kweli mjini ulikuja na rambo na gari la mkaa kama gunia, mtoto mzuri vile kajaza kinoma noma wewe unamchukulia rafiki tu”
“Urafiki kati ya mwanaume na mwanamke upo iwapo ni urafiki wa nia njema lakini hakutakuwa na urafiki kati ya mwanaume na mwanamke iwapo mmoja kati yao anamuwazia mwenzie mabaya yani kumtamani n.k . Mimi ninamuheshimu kama rafiki yangu na si vinginevyo”
“Acha upumbavu wewe mchangamkie mtoto yule kabla sijamuingiza kumi na nane zangu maana kitambo tu namtamani ila namkaushiaga tu”
“Hahahahahaha usinichekeshe wewe watambua namna yule binti asivyokupenda na tabia zako mbovu halafu leo akajae kwako kiurahisi kama unavyosema? Labda ukamloge asikutambue ni wewe”
“Unacheza wewe nafahamu fika kwamba ananichukia lakini nikimuhangaikia yule hata simuendei kwa babu bali atajaa mwenyewe”
“Aaaaah wapi hujanishawishi bado, sasa mimi ngoja nisepe zangu nikachote maji ya kufua na kufanya usafi mwana”
“Poa poa kaka mimi naenda kunywa chai na shemeji yako kisha nikaoge na nielekee kibamba kwa mshkaji. Pia nitaenda na shemeji yako yeye atashukia mbezi kwenye duka lake na mimi nitapitiliza”
“Haina noma kaka niagie kwa shemeji ndani na pia mpe hongera Azizi, nitampigia simu baadaye niongee naye vizuri. (nikiwa nanyanyuka tayari kuondoka)”
“Usijali kaka nitakuagia kwa shemeji yako na pia salamu zako zitafika”
akiwa naye ananyanyuka na akaingia chumbani kwake. Niliondoka nikiwa na mawazo tele kichwani mwangu, ukweli nilitamani kumsimulia mtu lakini niliogopa kwakuwa nilishakatazwa kwenye njozi nisithubutu kumwambia mtu. Nilikuwa najiongelesha mwenyewe
“hivi inawezekana vipi niogope ndoto na kushindwa kumsimulia mtu kisa nimekatazwa kwenye njozi na wakati ni njozi kama njozi zingine tu?”
nikiwa najiongelesha vile ili kupooza moyo wangu mara sauti ilisikika masikioni mwangu kama inajibu mawazo yangu
“hii sio njozi kama unavyodhani bali ni uhalisia wa mambo yajayo na yatakayotukia katika maisha yako”
niliogopa sana kusikia jibu lile na kujawa na hofu ingawa ile sauti iliendelea kunisisitiza nisiwe na hofu yoyote. Nilifika nyumbani nikakuta mlango upo wazi kwakuwa nilipokimbia chumba sikukumbuka hata kurudishia, niliingia ndani huku uoga na mapigo ya moyo yakizidi kuongezeka. Niliingia ndani nikajipa moyo kwamba hali ile imeshaisha, nilikagua vitu mule ndani na kila kitu kilikuwa sawa hakuna kilichopotea. Nilitoa ndoo zangu zote na majaba ya maji kwaajili ya kujaza maji kisha nikatoa nguo zote, mapazia na mashuka yaani kwa ufupi chochote kilichokuwa kichafu nilikitoa rasmi kwa ajili ya kufua. Nilienda nyumba ya pili na kuanza kuchota maji ambapo kila ndoo moja ilikuwa inauzwa shilingi hamsini (50), nilipomaliza kujaza ndoo zangu na majaba yote nilienda dukani kununua sabuni itakayotosheleza kufua kila kitu. Niliporudi toka dukani nilimkuta Balbina ameshafika kwani ilikuwa ni saa tatu, aliingia ndani huku akiniambia atanisaidia nikianza kufua yeye atakuwa anasuuza na kuanika. Nilianza kufua nguo zangu nilipofika katikati Balbina alitoka akiwa amejifunga kanga mbili yani moja aliifunga kifuani na nyingine kiunoni, kweli alinisaidia kusuuza na kuanika mpaka nikamaliza kabisa hapo ikiwa ni mida ya saa tano na nusu. Ukweli nilikuwa nikimuangalia anavutia sana na pepo la tamaa likaanza kuwaka moyoni mwangu, kila alivyokuwa akienda kuanika nguo nilikuwa namuangalia jinsi alivyoumbika na tamaa ikazidi kunikaba lakini nikajikaza. Nilimshukuru sana kwa msaada wake mkubwa maana ingekuwa peke yangu ningemaliza jioni, alifurahi pia akaingia chumbani na mimi pia nikaendelea na shughuli zangu za kufanya usafi chumbani. Nilimaliza mida ya saa sita na nusu mchana nikatoka nje kupumzika nikamkuta Balbina naye yupo nje.

Nini kitaendelea katika maisha ya Gerald? Je historia ya Balbina itamkatisha tamaa Gerald? Vipi Regan atafanikiwa kumuweka kimiani mtoto Balbina? Kwa hayo na mengine mengi ungana nami mwandishi wako nguli Gerald Mtenga katika stori hii ya kusisimua, kuelimisha na kuhuzunisha ya ZAFEERA
ITAENDELEA...
 
I
SEHEMU YA 6:
“Poa haina noma kaka mkubwa, Sasa leo nimepata wazo zuri sana, unaona pande hizi zote za mabibo na manzese? Wakitaka kununua nguo au mashuka hawaendi kariakoo au posta bali kwakuwa maisha yao ni ya chini kama ya kwetu hulazimika kwenda mahakama ya ndizi au karume kupata mahitaji yao”
“Naelewa hilo we nenda kwenye point husika acha kuzunguka mbuyu”
“Hata hivyo ndiyo nilikuwa naenda kwenye point, nimekueleza hayo ili uweze kunielewa barabara. Si unajua kuwa mimi napenda sana kumuelezea mtu hadi anielewe?”
“Sawa ndio nakusikiliza hivyo”
“Sasa mimi nimekuja na wazo la kufungua biashara ya duka la nguo na mashuka ya mitumba kaka”
“Ahah hah hah hah hah hah hah hah hah hah (kicheko cha nguvu)”
“Sasa mbona unanicheka kabla hata sijamaliza? (nikikunja sura kuashiria nimekasirishwa na kitendo kile)”
“Mwana umeongea siriazi nikajua booonge moja la wazo kumbe ni suala la kuwa “machinga”?!”
“Umetafakari ndivyo s..............(akanikatisha)”
“Haina haja ya kuendelea kunipa elimu nimeshakupata vizuri kabisa, unataka tufanye biashara ya machinga wa nguo za mitumba. Hah hah hah hah hah hah hah hah masuala ya ‘za leo leo bei nzuri, bei poa anabeba anabeba mia tano, mia tano, mia tano’ hahahaha basi kaka hilo wazo sijaliafiki kabisa.”
Nilipata ghadhabu sana hadi sura ikabadilika kwa maana sikutegemea jamaa angelipuuza wazo langu kiurahisi vile tena kwa dharau kama aliyekuwa anaongea ni mtoto mdogo. Lakini nilifanikiwa kutuliza hasira zangu kisha kwa upole nikamuuliza. “Poa nimekuelewa kaka mkubwa kwa maelezo yako, sasa basi nipe wewe wazo unaloona ni zuri na imara kuliko nililolisema mimi basi”
“Nilishakuambia tukikaza kwenye fani hii ya muziki lazima tutoke yaani wewe kama kawaida unachana na kutengeneza midundo ya ukweli na mimi naimba mwanzo mwisho, lazima tung’ae maana one day yes”
“Lakini kaka huu ni mwaka wa ngapi tunajihusisha na muziki bila mafanikio na hata kwenye kata yetu hatujulikani?”
“Wee tambua hata mbuyu ulianza kama mchicha, tukikaza one day lazima uwe zaidi ya wana profesa Jay na mimi bongo fleva watangoja sana si unajua ninavyojua kuipanga sauti yangu ya ukweli”
“Aaaahah hah hah hah hah hah hah hah unajidanganya sana ndugu yangu, huu mwaka wa sita unajidanganya tu hivyo. Yani kama usingekuwa pusha na kucheza kwako kamari basi ungeshauliwa kwa wizi, maana huo muziki hauna manufaa yoyote kwako”
“Sawa upusha wangu na kamari vinaniingizia sana hela lakini suala la kuwa machinga hapana kaka. Nilijua unaniletea wazo la maana kwamba umepata dili la kusukuma kete za poda (madawa ya kulevya) ambalo ndilo dili ninaloliwinda badala yake unaniletea ishu za kuuza mashuka bwana”
“Ila nimeshakuzoea jamaa yangu, ukiendelea kuwa na mawazo yako mgando utakuja kuishia mahali pabaya sana na ukipona pona utakuja kujutia njia zako za sasa unazozipitia”
“Utaishia na ushauri wako hivyo hivyo huku wenzio wanapiga mtonyo. Ila mwana nikitoka sitakusahau ili uwe unanipa mahubiri na ushauri wako vizuri hah hah hah hah hah hah”
“Hah hah hah hah hah endelea kujidanganya hivyo hivyo. Poa bwana haina noma namna gani vipi naenda kuegesha mwili kitandani si unaona mida nayo imesogea saa nne sasa hivi Kwahiyo usiku mwema kaka nitakucheki kesho basi”
“Haina noma askari wangu nimekuelewa vizuri kabisa, usiku mwema pia ila leo nalala mpweke sana shemeji yako hajaja bwana”
“Haha hah hah hah hah kumbatia mto. Poa bwana kesho”
Baada ya kumaliza kuzungumza na Regan nilimuaga kisha nikaondoka nikiwa na mawazo tele na nilijiamini sana kwani nikikumbuka nina dhahabu mfukoni basi niliona tayari ulimwengu ni wangu na nilitamani kukuche haraka niweze kwenda kwa sonara nikachukue hela yangu na nikaanza kupanga mipango mingi.
ITAENDELEA...
Inakuwa fupifupi mkuu acha hizo
 
SEHEMU YA 11:
“Jamani pole sana Gerald, umechoka sana eeeh?!”
“Akhsante mtu wangu yaani nimechoka mpaka sitamani kwenda kuoga”
“Hahahahaha kama kawaida yako wewe mwanaume ni mvivu kupita maelezo yaani kazi hizo mbili tu umechoka kiasi hicho??”
“Weeeee!!! Huu sio uvivu kazi ni nyingi sana aisee halafu zinachosha kupita maelezo Balbina”
“Hamna kitu wewe ni mvivu tu mwanaume wewe loooh!! Hapo bado hujaoga na kupika tena hahahahahahaha utakoma”
“Daaah noma kweli, kwani wewe unapika nini?”
“Napika pilau kisha niandae kachumbari”
“Mmmmh shemeji anakuja nini?! (Nikionesha sura ya wivu)”
“Aaaah wapi nimeamua tu nipike hivi leo, halafu unajua ya kwamba Crispin nimeachana naye nina kama mwezi sasa hivi?!”
“(Kwa mshangao) Eeeeeh maajabu kwasababu gani mmeachana??”
“Mwanaume hana malengo ya maana, akipata hela ni starehe tu yani clubs na bar mpaka hela zinaisha. Nilijaribu sana kumshauri namna ya kuwekeza hela zake vizuri kwa manufaa ya baadaye lakini hakutaka kunielewa yeye anawekeza kwenye starehe tu, nikamwacha na maisha yake”
“(Nikionesha tabasamu la furaha na la ushindi) mmmmh makubwa kwahivyo sasa hivi ni nani aliyepata bahati ya kuwa na wewe?”
“Sina mwanaume yeyote na nahitaji kupumzisha akili yangu kwanza nifanye biashara zangu kariakoo maana nataka kufungua duka la vipodozi maeneo ya sinza”
“Waaaaow umejipanga, mwanamke una akili sana (Nikishangilia moyoni)”
“Hamna mbona kawaida sana bwana, we nenda kaoge acha uvivu wako halafu pilau nimepika nyingi hivyo basi usipike leo tutakula wote na usiku labda ukanunue soda tu za kushushia”
“Daaaah Balbina nashukuru sana yani nilishapanga nikitoka bafuni niende kwa mama Jally kununua chakula kama kawaida”
“Usijali mtu wangu leo mama Jally ni mimi (tukacheka kwa pamoja)”
Niliingia chumbani kwangu nikiwa na tabasamu la ushindi kwani niliamini Balbina lazima awe wangu kwa vyovyote vile. Nilipotoka kuoga nikaingia chumbani kisha nilipomaliza kuvaa nikarudi pale nje ambapo tayari Balbina alikwishamaliza pika, hivyo nilienda dukani kwa mangi Mushi nikachukua soda mbili za baridi na haraka nikarudi mpaka pale nje kwenye mkeka tayari kwa kuanza kula. Ilikuwa ni jumapili ya kipekee kwangu kwani niliona kama njozi maana wikiendi zote tunakuwa kwenye pilika pilika za kuyasaka maisha, Balbina huenda kuwasalimia ndugu, jamaa na marafiki zake hivyo kwa siku ile niliiona ya kipekee kwangu kupata kukaa nae kutwa nzima. Ukweli Balbina alikwishaniingia akilini na moyoni hivyo nikaanza kutafuta mbinu za kumuingia mpaka akubali niwe mwanaume wake, ingawa sikujua nianzie wapi. Tulianza kusali na kukiombea chakula kisha tukaanza kula huku tukitaniana hapa na pale mpaka tukamaliza kabisa na baada ya pale tukafunga kwa sala na kumshukuru Mungu kutupatia chakula kile. Baada ya kumaliza kula tulitoa sahani na kuziosha kisha tukarudi kwenye mkeka na kuanza kupiga stori za hapa na pale ilimradi kusogeza masaa mbele na kuifanya jumapili iishe na ije jumatatu tuanze pilika pilika za kila siku tena.
“Hivi Gerald unajua kweli tumeishi hapa muda mrefu lakini sijui unajishughulisha na kitu gani?”
Balbina alianza kwa kunitandika swali ambalo kwangu niliona kama bahati kwani nilitegemea muda kama huo ili niweze kujizolea sifa kutoka kwa binti yule
“Aaaaaah ila usijali leo nitakuambia kila kitu na wewe pia ningependa unieleze maana hata mimi sifahamu chochote kuhusu wewe”
Niliongea kwa mikogo kibao ilimradi niweze kunasa ndege tunduni na hakika nilikamatika vilivyo
“Haina shida haya nielezee basi...”
Bila hiyana akajiweka tayari kunisikiliza na alionesha sura ya umakini kidogo na moyoni nikajisemea
“Huu ndio wakati wenyewe uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu”
“(Nikajikoholesha kiuongo na kweli ili kusafisha koo na sauti itoke vizuri maana ndio nilikuwa nataka nichukuwe point tatu kamili kwa muda huo)...ninajishughulisha na uandishi wa muziki na pia kutengeneza midundo kwaajili ya wasanii mbalimbali, pia kuna duka la vifaa vya simu na kutengeneza simu ndio langu lipo pale ubungo. Kwasasa nataka niitanue biashara nianze mpaka kutengeneza simu kwa kutumia vifaa imara vya kompyuta na kuuza simu mbalimbali.”
Nilimaliza stori yangu fupi huku nikijigeuza huku na kule kama vile nilikalia misumari
“Waaaaaaow Gerald unajitahidi sana kujipanga, kwani kwa sasa una miaka mingapi?”
Balbina alichanua tabasamu la haja kisha akatoa sauti murua iliyoambatana na sifa zilizofanya kichwa kiongezeke ukubwa kwa sifa, kisha akaendelea kwa kunitandika swali papo kwa hapo
“Kwasasa nina miaka 26”
nilijibu pasipo kupepesa macho wala maneno huku nikiachia tabasamu mwanana nikimtazama usoni
“Aaah safi nimependa hiyo na sina tena maswali, labda wewe uendelee na maswali yako nami nipate wasaha wa kukujibu.”
Balbina alimaliza kwa kusema hivyo kisha akawa ananitazama kama nina swali au maswali ya kumuuliza yeye.
“Aiseee unaniruhusu nianze kuuliza maswali mimi kweli?! Maana mimi nauliza maswali mpaka ninakera mtu wangu hivyo usinichoke kwa maswali yangu unaweza ukakereka bure”
Nilijigamba kama vile nimemaliza chuo kikuu hivyo ni mtaalamu wa kudadisi vile kumbe hamna lolote mlalahoi tu
“Haina shida wewe uliza tu maana mwenzio huwa napenda sana kujibu maswali kuliko kuuliza maswali.”
Bila hiyana Balbina aliniruhusu kuuliza maswali na sikungoja hata sekunde nikamtandika swali
“Poa mtu wangu, jina lako kamili ni nani?”
alinijibu bila kusita
“Naitwa Balbina Justine Fungakamba”
jambo la kujibu vile lilinipa urahisi wa kuuliza swali lingine haraka haraka kama mwandishi wa habari vile
“Anhaaa na umezaliwa mwaka na tarehe ngapi?”
Balbina pia alinijibu huku akitabasamu kidogo
“Nimezaliwa tarehe 07/02/1984 kwahiyo kwa sasa nina miaka 22 bila shaka umenizidi miaka minne (sote tukacheka)”
kama niliyapangilia maswali yangu vile kwani kabla hata hajameza mate nikamtandika swali lingine ambalo lilimfanya agune kidogo
“Na ilikuwaje mpaka ukaja Dar es salaam na historia yako kwa ujumla?”
ITAENDELEA...
 
SEHEMU YA 12:
“Mmmh una maswali kweli kweli Gerald”
“Aaaahahaha (nikicheka kidogo nikiona sifa) hapo mbona bado hata sijaanza mtu wangu bado utanichoka tu”
“(Alinitazama kidogo kisha akatabasamu na akaendelea) Haina shida lakini, nimezaliwa hapa hapa Dar maeneo ya Pugu mwisho nikiwa mzaliwa wa kwanza na wa mwisho kwa wazazi wangu ambao walikuwa wana uwezo sana. Ila Mungu sio Athumani kama wengi wasemavyo hivyo ana mipango yake, mwaka 1997 nikiwa kidato cha kwanza pale shule ya Kifungilo iliyopo Tanga wazazi wangu wote walipata ajali wakati wakija shuleni kwangu kunitembelea. Ajali ilikuwa mbaya sana na kwa bahati mbaya hakuna abiria aliyepona maeneo ya korogwe Tanga na wazazi wangu walipoteza maisha. Maisha yalianza kubadilika kwani ndugu walianza manyanyaso sana na nilipofika kidato cha pili mvutano ulianza kabisa na kupelekea kushindwa kunilipia ada na hatimaye nikashindwa kusoma kabisa. Mwaka 1998 ilinibidi kuacha shule na kurudi nyumbani Pugu ambapo baba mkubwa alishikilia mali zote na kudai ni zake na sikuwa na haki kabisa, iliniuma sana kuwaona watoto wake wakisoma shule nzuri na za gharama kubwa na pia kuhudumiwa vizuri kwa mali zilizokuwa za wazazi wangu huku mimi nikiwa sina matumaini ya kurudi shule tena. Niligeuzwa mtumwa pale nyumbani, nikawa nafua na kupika bila kusahau kufanya usafi wa nyumbani na kuwa mlinzi wa nyumba pindi wanapoondoka na kuelekea kwenye matembezi yao ya starehe. Mwaka 2000 kuna rafiki yangu nilikuwa nikisoma naye kifungilo alikuwa akiitwa Judith alinitafuta kisirisiri bila yeyote pale nyumbani kufahamu kwa maana ningepigwa sana iwapo wangetambua nawasiliana na yeyote nje ya ile nyumba. Yule rafiki yangu alinitaka nikafanye kazi katika duka lao kubwa la bidhaa za jumla na kiukweli nilikuwa nakubalika sana kwenye mahesabu hivyo aliamini ningeweza kujiendeleza iwapo nitaweza kusimama kwa miguu yangu miwili, sikumpinga lakini nilimuuliza nitaweza vipi kuondoka pale wakati nimewekwa kama mfungwa hapa nyumbani? Ndipo aliponiambia nitoroke siku wakiniachia uhuru au kunituma dukani na kuhakikisha nafika kwao mbagala mwisho ambapo ningepokelewa na kuanza maisha mapya. Alinipa maelekezo mengi sana na njia zote za kufika nyumbani kwao kwani tayari ameshaandaa mazingira ya mimi kufika pale, tuliafikiana kwa pamoja kwamba nitatoroka na kuja huko moja kwa moja bila hiyana. Nakumbuka ilikuwa ni siku ya ijumaa ambapo waliniaga kama kawaida yao kwenda matembezi ya kifamilia na kuniacha mimi nyumbani kuilinda nyumba mpaka watakaporudi, niliafikiana nao huku moyoni nikiwa na wazo kwamba ndio siku haswa ya mimi kutoroka. Waliondoka mida ya saa kumi jioni nami nikaingia chumbani kwangu na kujiandaa kisha nikachukua fedha za kutosha kabisa kuondoka pale, sikutaka kuchukua chochote pale ndani. Mida ya saa kumi na mbili nilitoka na kufunga nyumba na kisha kufunga geti kubwa na ufunguo nikaupeleka kwa jirani iwapo wangerudi awape ufunguo, nilipohakikisha kila kitu tayari nilipanda gari na kuondoka na kuelekea mbagala. Nilipofika pale mbagala mwisho nilipanda pikipiki na ikanipeleka moja kwa moja hadi nyumbani kwa kina Judith kwani walikuwa ni watu maarufu hivyo haikuwa shida kufika pale. Nilipokelewa vizuri pale nyumbani kwao na nilishangaa kukuta familia iliyokuwa ikiishi kwa furaha na amani vile, nilioneshwa chumba changu na nikaenda kuoga kisha nikarudi chumbani ambapo Judith alinifuata kwa furaha na kunitaka niende mezani kwaajili ya chakula. Ukweli nilipoiona ile familia roho iliniuma sana na kuwakumbuka wazazi wangu lakini sikuwa na la kufanya. Nilinyanyuka pale na kwenda kujumuika wote mezani, walinipenda sana kwa ucheshi wangu kwani meza ilichangamshwa kwa stori zangu za kuchekesha sana. Kesho yake yule baba na mama walinipeleka duka lao kubwa lililokuwa wazo hill tegeta rasmi kwa kuanza kazi, waliniambia kuwa ningekuwa nikifanya kazi pale asubuhi hadi usiku na wangekuja kunipitia na kurudi wote nyumbani. Nilianza kazi pale nikiwa na usongo wa kuhakikisha nafikia mafanikio niliyokuwa nayataka katika maisha yangu, nilianza kazi pale mwaka 2000 kama msaidizi tu na miezi sita baadaye nikakabidhiwa mimi ndio niendeshe hilo duka. Miaka miwili baadaye yaani 2002 duka liliingiza faida kubwa sana bila wao kutarajia na kweli walinipenda sana wakanifanya nisimamie na bar yao iliyopo bunju pamoja na duka lingine la vifaa vya umeme maeneo hayo ya tegeta. Mwaka 2004 rafiki yangu alikuwa mwaka wa pili chuo cha mlimani akichukua shahada ya sheria, biashara ilikuwa na kutanuka sana na wazazi wao kwa pamoja waliamua kunifungulia biashara kariakoo ya duka la jumla pia na kunijengea nyumba maeneo ya kimara stop over. Walinipa Baraka zao na kuniacha niendelee na maisha yangu lakini kwakuwa nilikuwa na mipango yangu mingi niliwaomba nyumba waliyonikabidhi niipangishe kisha fedha za kodi nizidi kuziwekeza kwenye miradi na hatimaye kufikia malengo yangu. Walifurahi kwa pamoja na kunitaka nipatapo tatizo nisisite kuwajulisha au kuwatembelea mara kwa mara walinifanya kama mtoto wao wa damu. Ndipo nilianza maisha yangu maeneo ya kimara huku nikisimamia biashara yangu kariakoo, nilipangisha nyumba yangu na ndipo nikaja hapa kupanga na fedha zangu kuzidi kuongeza vitu vingi dukani kwangu.”
Balbina alimaliza stori yake na nikahisi kitu kimeuchoma moyo wangu mpaka nikaanza kuumwa ila nikajikaza bila yeye kujua ila hakika simulizi yake iliniumiza sana nikajikuta nikimuonea huruma sana
ITAENDELEA...
 
SEHEMU YA 13:
“Duuuuuh (nikitingisha kichwa kwa masikitikiko makubwa) sikutegemea kama umepambana kiasi hicho mtu wangu, yaani umeongea hadi mwili umesisimka jinsi ulivyopambana kuyaweka maisha yako yakae sawa. Kweli Mungu sio Gerald au Balbina, sasa vipi kuhusu nyumbani kwenu Pugu umekwishawahi kwenda au ndio tangu uondoke mpaka leo hujagusa huko?”
Nilimuuliza huku nikijiweka sawa kupata stori ile ambayo ilishauteka moyo wangu kabisa
“Mwaka jana mwezi wa kumi na moja nilienda kutembea na ukweli nilisikitika nilichokikuta (akimeza funda la mate kwa ajili ya kulainisha koo lake)”
“Ulikuta kitu gani?”
niliuliza kwa shauku kubwa kutaka kujua kulikoni
“Nilimkuta baba mkubwa akiwa anaumwa vibaya sana matatizo ya moyo na sukari ikiwa inamsumbua sana, mke wake alikuwa na presha hivyo alifariki miaka mitatu iliyopita. Watoto wake waliokuwa wakifurahia mimi kunyanyasika wote walikuwa wamepoteza ramani ya maisha, kaka yao mkubwa alikamatwa na madawa ya kulevya na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela hivi navyoongea yupo segerea mwaka wa tatu sasa toka 2003. Dada aliyefuata amezalishwa na akafukuzwa shule na sasa analea mtoto wake nyumbani na ndio anamuhudumia baba yake, mdogo wao wa mwisho amejiingiza kwenye uendeshaji wa pikipiki maarufu kama bodaboda. Waliponiona walianza kulia na kuniomba msamaha kwa mabaya yote waliyonifanyia, baba mkubwa aliniomba msamaha sana na kunikabidhi hati ya nyumba ya wazazi wangu huku akinitaka niwasamehe kwa yote waliyonifanyia akidai waliingiwa na shetani wa tamaa. Niliwaambia nimekwishawasamehe na wasiwe na wasiwasi kwani hakuna mkamilifu katika ulimwengu huu, nilimrudishia baba mkubwa hati ya nyumba ile na kumuambia ni nyumba yake rasmi hivyo asiwe na shaka na mimi tena kwani nilikwishawasamehe tangu siku naondoka pale.”
Balbina alimaliza kuongea alishusha pumzi kama mtu aliyetua kitu kizito mgongoni kwa huzuni na hakika ilikuwa ni stori inayoweza kukutoa machozi hadharani
“Mmmmmh (Nikaguna kwanza) hongera sana mtu wangu maana una moyo wa kipekee katika ulimwengu huu, watu wengi wangekuwa wameshapoteza ramani ya maisha na wangeharibikiwa kabisa maisha yao. Uliwezaje kupambana na hali iliyokukumba mpaka kufanikiwa kufika katika hatua hiyo kubwa hivyo?”
Stori yake ilinipa funzo kubwa sana la kutokata tamaa kwa lolote lile kama umeweka malengo yako hata kama hayakwenda kama ulivyotarajia basi hutakiwi kukata tamaa bali yakupasa upambane mpaka ufikie mafanikio yako kuna msemo husemwa Dhahabu haiwezi kuwa Dhahabu yenye dhamani pasipo kupitishwa kwenye moto mkali.
“Kikubwa ni kuwa na kiasi na pia imani na Mungu, huwa naamini kila jambo huwa linatokea kwa mpango wa Mungu pekee. Nililia sana lakini kuna kitu kilikuwa kikinena na mimi moyoni kwamba Balbina usijali kila jambo limeshapangwa mlango mmoja unapofungwa yakupasa kufumbua macho yako na kuona mlango mwingine ulio wazi kikubwa mtangulize Mungu wako na usimuwekee mtu kinyongo na daima muheshimu na kumpenda adui yako. Upendo ndio uliopelekea mipango yangu yote kutimia kwani huwa napenda kuishi na watu kwa upendo mkubwa sana.”
Balbina aliongea kwa upole na hakika alipangilia kile alichokuwa akikiongea na alionekana binti mwenye busara sana
ITAENDELEA...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom