Simulizi za polisi kuua gaidi Arusha

Simulizi za polisi kuua gaidi Arusha

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

Liberatus-Sabas--Agust8-2014%281%29%281%29.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas

Mkazi wa Mianzini, jijini Arusha, Yahaya Sendei (31), anayedaiwa kuwa kiongozi wa watuhumiwa ulipuaji mabomu nchini na umwagiaji tindikali watu, ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati akidaiwa kujaribu kuruka kwenye gari lao kwa lengo la kutoroka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas (pichani), jana alisema kuwa mtuhumiwa huyo aliuawa juzi saa 5:30 usiku katika barabara ya Arusha- Babati eneo la Kisongo, wilayani Monduli, wakati wakimpeleka kijijini alikozaliwa Chemchem, wilaya ya Kondoa, mkoa Dodoma, kuwaonyesha askari bomu jingine aliloficha.

Alidai kuwa, mtuhumiwa huyo ambaye inadaiwa wakati wa uhai wake alikuwa mwalimu wa karate na judo ni mwasisi na kinara wa matukio ya ugaidi yaliyotokea jijini Arusha, Zanzibar, Mwanza na Dar es Salaam.

"Huyu tulimpata kutokana na intelejensia imara ya polisi ya kisasa na ya hali ya juu na tulimkamata mkoani Morogoro Oktoba 6, mwaka huu na kusafirishwa Oktoba 11 mwaka huu kuletwa Arusha na alipohojiwa alikiri kuhusika na kuratibu matukio ya ugaidi na alikuwa akijificha kwenye nyumba tofauti na porini, " alisema kamanda huyo.

Alidai mtuhumiwa huyo alipigwa risasi kwenye mguu wa kulia na kalio la kulia alipojaribu kutumia uzoefu wake wa kuruka judo na kupiga karate kutaka kuwazidi polisi ili atoroke na kwamba alifia njiani wakati akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru kwa matibabu.

Hata hivyo, hakueleza sababu za kumpiga risasi mtuhumiwa huyo ambaye hakuwa na silaha yoyote na kama alijeruhi askari yeyote zaidi ya kudai kuwa maiti yake imehifadhiwa hospitalini hapo kwa uchunguzi zaidi na kusubiri ndugu kuichukua kwa maziko.
Vile vile Kamanda Sabas hakueleza kama hatua ya kuuawa kwa mtuhumiwa huyo muhimu itawakosesha polisi taarifa muhimu katika mchakato wa upelelezi wao.

Awali Kamanda huyo alitaja baadhi ya matukio ambayo mtuhumiwa huyo inadaiwa alikiri kuhusika nayo kuwa ni la Oktoba 25 mwaka 2012 lililotokea saa 5:30 usiku katika mtaa wa Kanisani Paloti, kata ya Sokoini One, jijini Arusha.

Katika tukio hilo, yeye na wenzake inadaiwa walitega bomu kwenye chumba cha Sheikh Abdulkarim Idd Jonjo (52) nyumbani kwake na kumjeruhi baada ya kulipuka.
Inadaiwa tukio la pili na wenzake ambao wamefikishwa mahakamani, lilitokea Mei 5 mwaka jana saa 10:30 maeneo ya Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi lililopo Olasiti jijini Arusha.

Katika tukio hilo inadaiwa kuwa aliratibu kurushwa kwa bomu na kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi 56.

Juni 15 mwaka 2013 saa 11:50 jioni katika viwanja vya Soweto, kata ya Kaloleni, jijini Arusha na wenzake, wanadaiwa kurusha bomu na kuua watu wanne, kujeruhi 60.
Julai 11 mwaka 2013 saa 5:00 eneo la Kwa Mrombo, jijini Arusha na wenzake wanadaiwa walimwagia tindikali usoni Sheikh Said Juma Makamba.

Februari 12 mwaka 2014 saa 3:45 katika eneo la Tindigani, Unga Ltd, jijini humo, kwenye msikiti wa Sawiyatu Qadiria, wanadaiwa kumwagia tindikali usoni Sheikh Hassan Bashir.
Februari 28 mwaka 2014 saa 5:15 alfajiri katika msikiti wa Bondeni, wanadaiwa kumwagia tindikali Mistapha Mohamed Kiago na kumjeruhi usoni na shingoni.

Aprili 13 mwaka 2014 saa 1:30 usiku, eneo la Mianzini kwenye nyumba ya wageni na Baa ya Niht Park, wanadaiwa walirusha bomu na kujeruhi watu 11 na kusababisha kifo cha mmoja.
Aprili 13 mwaka 2014 la saa 5:00 katika eneo la Majengo, jijini Arusha, anadaiwa alirusha bomu kwa kushirikiana na wenzake na kuwajeruhi watu wawili Sudi Ali Sudi (37) ambaye ni Mkurugenzi wa Answar Muslim Kanda ya Kaskazini na mwenzake Muhaji Hussein Kifea (38), mkazi wa Dar es Salaam. Julai 7 mwaka huu, saa 4:15 usiku eneo la
Uzunguni, mgahawa wa Vama Traditional Indian, uliopo jirani na Viwanja vya Gymkhana, wanadaiwa walirusha bomu na kujeruhi watu wanane.

Kamanda huyo polisi alisema wanaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine wanaojihusisha na kikundi hicho ambacho mtuhumiwa huyo alikiri kuendesha mafunzo ya karate na judo kwenye baadhi ya misikiti jijini Arusha.

Hata hivyo, alisema vikundi hivyo vimesambaratishwa na polisi.
Alitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa polisi ili kuendelea kudumisha amani jijini Arusha na maeneo mengine ya nchini.

"Hawa watu hawakuwa wanafadhiliwa nje ya nchi ila walikuwa wanajifadhili wenyewe na kwa faida zao wenyewe" alisema Kamanda Sabas.

CHANZO: NIPASHE
 
Liberatus-Sabas--Agust8-2014%281%29%281%29.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas

"Hawa watu hawakuwa wanafadhiliwa nje ya nchi ila walikuwa wanajifadhili wenyewe na kwa faida zao wenyewe" alisema Kamanda Sabas.

CHANZO: NIPASHE

Sasa kama walikuwa hawafadhiliwi na waliku wanajifadhili! Ilikuwaje wamiliki mabomu ya kijeshi?

Na Je! ni kwanini wafanye mashambulizi katika mazingira tofauti yasiyo na uhusiano kabisa kama:
  • Kushambulia makanisa?
  • Kushambulia mikutano ya siasa?
  • Kuwashambulia mashehe?
  • kushambulia kumbi za starehe?
Huyu Liberatus Sabas atueleze kuwa huyo marehemu na kikundi chake kilikuwa kuina entrance gani katika uhalifu wao.?
 
...huyu mkubwa ndiye anafuga ugaidi...inakuwaje magaidi wanakuwa waislam tuuuuuuuuuu,mie sielewi hapa.Kote ni wao tuuu hii inakuwaje?.Kwa nini kipindi huyu bwana ndo mabomu mabomu,mapadri risasi risasi?
 
Mkuu hapo umekosea kidogo, sio mikutanobya siasa, ni ya CHADEMA. Hakuna mkutano wa ccm umewahi kushambuliwa na mabomu.
kwa mimi ninachoweza kusema ni kuwa jeshi la polisi ni waongo wakubwa, na watachomwa siku ya mwisho. Wanachojua wao ni kuua tu.
Intelijensia gani ya kisasa waliyonayo hao polisi? Kuna ushahidi gani huyo raia waliyemuua ndio mhusika wa ulipuaji mabomu? Tutaaminije wakati wamemuua? Mahakama pekee ndio ina uwezo wa kutia mtu hatiani leo polisi wanatekeleza hadi hukumu? Haiingii akilini mtuhumiwa wa mabomu yuko kwenye gari la polisi saa tano usiku wakienda alikoficha mabomu, yuko chini ya ulinzi eti atake kutoroka kwa kuruka sarakasi, wadanganyeni wajinga. Pingu zinazonunuliwa na kodi zetu mnafungia waandamanaji tu au zina kazi gani. Mtu akifungwa pingu miguuni na mikononi ataruka sarakasi kweli, na je kwa uzembe wenu polisi hamuoni kuwa bado yapo mabomu mtaani na yataua watu kwa ajili ya ujinga wenu. Kwa nini msingemkamata? Si mna mafunzo ya kukamata wahalifu bila kuua? Au na nyie mpo kwenye mtandao huo manaogopa kutajwa. Mliokuwa kwenye tukio hilo mlipaswa kufukuzwa na kushtakiwa kwa mauaji ya raia ili mjifunze kazi yenu. Mmepoteza ushahidi mna la kusema sasa.
Hiyo kauli eti wanajifadhili wenyewe mmmmmh, wanapata wapi mabomu, yanaingizwaje nchini, sio rahisi kudanganya hivyo
 
Huyu jamaaa kwa nn alipue mkutano wa chadema, kanisana ,bar tena aende kwa shekhe uhusiano uko wapi hapo Police tupeni majibu ya uhakika sio ubabaishaji
 
ImageUploadedByJamiiForums1413891766.656216.jpg
Hivi wewe mtu huna hata aibu kutunga maneno kwenye issue ambayo maisha ya watu yamepotea? RPC ni nafasi kubwa sana na ya kuaminika katika ulinzi wa raia na mali zao sasa unapokuja na hadithi za alinacha tukueleweje?
Kazi hiyo ina kiapo na hivi mnapomkebehi MUNGU kwa kutenda tofauti na viapo vyenu hamuoni ni dharau kubwa kwa huyo mliyetumia jina lake kuapa. Kwani mtu ukisema ukweli hata kama hiyo kazi ikapotea ndio mwisho wa maisha yako? Hudhani kuwa mbele ya jamii utaheshimika wewe na kizazi chako?
Kama mnamwogopa MUNGU semeni ukweli ili ile damu iliyopotea ya waume,wanawake na watoto isiwarudie nyie na vizazi vyenu.
 
...huyu mkubwa ndiye anafuga ugaidi...inakuwaje magaidi wanakuwa waislam tuuuuuuuuuu,mie sielewi hapa.Kote ni wao tuuu hii inakuwaje?.Kwa nini kipindi huyu bwana ndo mabomu mabomu,mapadri risasi risasi?
sio lazima uchangie kama huna cha kuchangia. ni busara ukasoma halafu ukapita tu kama wengine. msome mchangiaji wa juu yako halafu jilinganishe na wewe.
 
Swali ni je alichokisema kamanda Sabas ni kweli au ameudangaya umma?amesema huyu jamaa alikua anakimbia ,lakini ukiangalia amepigwa risasi na mtu aliyekua mbele yake
Alisema amepigwa kiunoni ni kweli hapo ni kiunoni?
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1413892820.346667.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1413892820.346667.jpg
    78 KB · Views: 1,240
Ama kweli huyo jamaa ni noumaaaaa! pamoja na pingu mikononi na miguuni na gari ikiwa kwenye speed tena usiku katikati ya maasikari tena gari iliyofunikwa iliweza aliweza kuruka!
kali zaidi risasi ya mkuuni na matakoni imemuua hapo hapo wala hata hakuwahi kufikishwa hosipitalini!
mara alipue mashekh mara makanisa (the same person, contradicting), mara akalipue mikutano ya chadema mara akalipua mabar mara akamwagie mashekh tindikali (the same man)!
to me, it rising many answers than questions!
 
...huyu mkubwa ndiye anafuga ugaidi...inakuwaje magaidi wanakuwa waislam tuuuuuuuuuu,mie sielewi hapa.Kote ni wao tuuu hii inakuwaje?.Kwa nini kipindi huyu bwana ndo mabomu mabomu,mapadri risasi risasi?

kwa hiyo uhuru kenyatta ni mwisilam ndio maana westget na mpeketoni inavamiwa

kumbe goodluck jonqthani ni mwaislamu ndio maana boko haramu wapo

hujui kuwa kule kossovo ni wakristo kama sisi walipanga mauaji ya waislam
 
Ama kweli huyo jamaa ni noumaaaaa! pamoja na pingu mikononi na miguuni na gari ikiwa kwenye speed tena usiku katikati ya maasikari tena gari iliyofunikwa iliweza aliweza kuruka!
kali zaidi risasi ya mkuuni na matakoni imemuua hapo hapo wala hata hakuwahi kufikishwa hosipitalini!
mara alipue mashekh mara makanisa (the same person, contradicting), mara akalipue mikutano ya chadema mara akalipua mabar mara akamwagie mashekh tindikali (the same man)!
to me, it rising many answers than questions!
Khaa!! "Hawa watu hawakuwa wanafadhiliwa nje ya nchi ila walikuwa wanajifadhili wenyewe na kwa faida zao wenyewe" alisema Kamanda Sabas.
 
Watanzania tunasikitishwa sana na serikali yetu iliyokuwa ipambana na umasikini badala yake inapambana na masikini. Matukuo haya ya kusikitisha hayajaanza tz hata jamaa zetu kule ke nao walianza muda. na naamini mafunzo haya ya askari wa tz wameyapata kutoka kwa askari wa ke.. Inawezekana vipi askari 10 wamlinde mtuhumiwa mmoja. na baada ya wao kushindwa nguvu tena akiwa na pingu wampige rissasi ya kumuua. Vp alitaka kutoroka? haingii akilini, na inawezekana vp risasi ya mguuni lkn picha zinaosha damu zinavuja kichwani na kifuani. haiingii akilini mtuhumiwa akiwa na pingu atake kutoroka. ila ndio sheria ya ugaidi hiyo polisi akikuhisi tu anaruhusiwa kukuuwa. mbaya zaidi sheria hii unawakabili zaidi watu wanyonge, wasio na sihala. kwani naamini muziki wa magaidi wa kweli askari wetu hawawezi kuukabili. ikumbukwe huyu jamaa aliakamtwa kwa mashtaka yaliyotengenezwa na BAKWATA mkoa wa arusha katika kisa cha kugombea msikiti kati ya vijana na wazee (masjid qubah) bakwata waliomba wapewe mashtaka ya ugaidi na wenzie.

hii ni fitna . aliyeuliwa ni muislam na miongoni mwa tuhuma ni kutaka kuuwa waislam. tutafakari bila jabza. huyu kauwawa; na kuna mashekhe wetu wako ndani na wanalalamika kuteswa na kulawitiwa. tuamue moja kudhulumiwa au tujipange kupinga dhulma.

justice ni kitu muhimu ktk jamii bila kujali dini, rangi, au anakotoka.. jamii inayokubali extra judicial killings, kwa sababu tu aliyeuwawa amepewa label fulani, si jamii ya kistaarabu.

nadhani imefika wakati kwa watanzania na kudai kuwepo kwa INDEPENDENT COMPLAINTS COMMISSION, ya kuichunguza polisi kwa matukio kama haya.

ni kichekesho polisi inapojichunguza yenyewe, au inapoachiwa bila kuchunguzwa kwa matukion wanayoyafanya ya kutatiza kama haya.

Inasikitisha pia kuoa wanasiasa wetu ambao jukumu lao la kwanza ni walinda raia hakuna hata mmoja aliyenyanyua mdomo wake kutokana na madhila haya wanayofanyiwa wananchi wanyonge na wasio na hatia zaidi kuwataka watz wawachague kwenye uchaguzi ujao eti ili waingie madarakani. shame on you especially u maalim seif, lipumba, slaa, mbowe na huyu wa nccr. shame on you CCM kwa kuuwa na kujisika kuuwa wasio na hatia
 
Tanzania tusikarijishe fujo kama walivyofanya wenzetu wa kenya nchi ikakosa amani, polisi naona inaamua kuwa waendesha mashitaka na majaji, inaamua tu kumkamata mtu na kumtia hatiani na kumpa adhabu ya kumpiga risasi na kumtia lebo ya mgaidi.Nini maana ya mgaidi, kwanini asiitwe mhalifu tu au ni njia ya kuhalalisha kuwa anastahili kuuwawa kwa kupigwa risasi bila kupelekwa mahakamani.Tunaomba polisi watizame wasije wakawasha moto wakashindwa kuuzima, kwasababu mambo kama haya ambayo yanafanya kundi moja la wananchi linaona kama kwamba linaonewa ndiyo yanaleta fujo.
 
Mimi binafsi hii ya RPC kuongea uongo mtupu hainiingii akilini hata kidogo!

Ni kwanini mhalifu akimbie ingali alikuwa katika ulinzi mkali? Ina maana pingu hakufungwa??

Hata mtoto wa miaka mitatu ukimweleza mauaji haya ilivyo hakika hatakubaliana nayo!
 
huwezi kuuliza swali kama hilo kwanza jaribu kutafakuri kidogo juu ya makundi yafuatayo: taliban, boko haram, tamil tigers, alkaeda, al shabab, ISIS, na mengineyo meni utapata jibu hawa ni makundi ya watu gani
 
mtu gaidi ni hatari sana. wananchi tunategemea awe amedhibitiwa toka mlipomtoa morogoro hadi arusha na arusha kwenda dom. iweje aweze kutumia mafunzo ya karate akiwa chini ya ulinzi mkali.mimi nadhani waandishi wa habari wasiwe watu wa kuambiwa taarifa na kuzibeba kama kasuku mbane kamanda na maswali atueleze vizuri
 
Mkuu hapo umekosea kidogo, sio mikutanobya siasa, ni ya CHADEMA. Hakuna mkutano wa ccm umewahi kushambuliwa na mabomu.
kwa mimi ninachoweza kusema ni kuwa jeshi la polisi ni waongo wakubwa, na watachomwa siku ya mwisho. Wanachojua wao ni kuua tu.
Intelijensia gani ya kisasa waliyonayo hao polisi? Kuna ushahidi gani huyo raia waliyemuua ndio mhusika wa ulipuaji mabomu? Tutaaminije wakati wamemuua? Mahakama pekee ndio ina uwezo wa kutia mtu hatiani leo polisi wanatekeleza hadi hukumu? Haiingii akilini mtuhumiwa wa mabomu yuko kwenye gari la polisi saa tano usiku wakienda alikoficha mabomu, yuko chini ya ulinzi eti atake kutoroka kwa kuruka sarakasi, wadanganyeni wajinga. Pingu zinazonunuliwa na kodi zetu mnafungia waandamanaji tu au zina kazi gani. Mtu akifungwa pingu miguuni na mikononi ataruka sarakasi kweli, na je kwa uzembe wenu polisi hamuoni kuwa bado yapo mabomu mtaani na yataua watu kwa ajili ya ujinga wenu. Kwa nini msingemkamata? Si mna mafunzo ya kukamata wahalifu bila kuua? Au na nyie mpo kwenye mtandao huo manaogopa kutajwa. Mliokuwa kwenye tukio hilo mlipaswa kufukuzwa na kushtakiwa kwa mauaji ya raia ili mjifunze kazi yenu. Mmepoteza ushahidi mna la kusema sasa.
Hiyo kauli eti wanajifadhili wenyewe mmmmmh, wanapata wapi mabomu, yanaingizwaje nchini, sio rahisi kudanganya hivyo

Nafikiria upande wa pili wa Shillingi kuwa huenda huyo marehemu aliwahi kutumika na Polisi kama jamaa yetu wa kesi ya Lwakatare (Ludo) hivyo walipoona mbele ya safari anaweza kuwaaumbua basi ikabidi wamrestishe in pisi tu kufuta nyayo zao,

"GAIDI GAIDI GAIDI KUMSAFIRISHA USIKU, USIKU, USIKU BILA PINGU DUH HII NGUMU KUMEZA"
 
Kama kuna mtu ATKAYE AMIN maelezo ya kamanda Sabas, basi mtu huyo ataamini kila kitu hapa duniani, including hata Kamanda Sabas akimwambia mtu huyo kwamba mimi ndiyo Masiah Yesu Kiristu niamini mtu wa aina hiyo ataamini na kumfuata.

Kweli jeshi la Polisi limejaa akina Kova wengi! (ref kesi ya Mulundi/Gwajima/Dr. Ulimboka)
 
View attachment 195157
Hivi wewe mtu huna hata aibu kutunga maneno kwenye issue ambayo maisha ya watu yamepotea? RPC ni nafasi kubwa sana na ya kuaminika katika ulinzi wa raia na mali zao sasa unapokuja na hadithi za alinacha tukueleweje?
Kazi hiyo ina kiapo na hivi mnapomkebehi MUNGU kwa kutenda tofauti na viapo vyenu hamuoni ni dharau kubwa kwa huyo mliyetumia jina lake kuapa. Kwani mtu ukisema ukweli hata kama hiyo kazi ikapotea ndio mwisho wa maisha yako? Hudhani kuwa mbele ya jamii utaheshimika wewe na kizazi chako?
Kama mnamwogopa MUNGU semeni ukweli ili ile damu iliyopotea ya waume,wanawake na watoto isiwarudie nyie na vizazi vyenu.

Kweni RPC Sabas ni kabila gani? nasema hivyo kwa sababu makabila mengine kusema uongo ndio uanaume wenyewe
 
Back
Top Bottom