Malupelupe
Member
- Oct 28, 2012
- 55
- 13
Babu yangu aliwahi kunisimulia ndoto yake kuwa,katika kisiwa cha Donge waliishi wanyama na viumbe wengine walioshirikiana sana kwa kila jambo.Mfalme wa kisiwa hicho aliiamini kuwa kila kiumbe amepewa kipqji cha kufanya jambo.
Sikumoja Mfalme aliitisha mkutano mkubwa na kutaka kila kiumbe abuni na.kufanya jambo ambalo litakuwa na manufaa kwa kisiwa hicho.Ajabu sana,wanyama na viumbe wengine walikataa kufanya chochote nakulazimika kuhamia kisiwa jirani cha Ngewe.Waliamini kuwa kisiwa cha Ngewe ndicho bora zaidi japo kulionekana kuwa na neema za kusimuliwa tu,kamavile uhuru wakuzaliana,vyakula visivyo isha,na manoti ya kuokota kwa kila hatua kiumbe apigayo.
Maisha ya kisiwa cha Ngewe yaliwachosha ndani ya muda mfupi sana na hata kutamani tena kurudi walipo toka.Walipo kumbuka safari ndefu ya miguu walokwisha tembea,hawakutamani hata kugeuka nyuma
Walibaki na sintofahamu iliyo waumiza kwa kila pigo la sekunde iliyopita.
Mwisho wa simulizi ya ndoto yake,Babu aliniambia nisiwe nasimulia ndoto mbaya.Kwani ukiota wachawi wamekutembelea na kukusulubu usiku kucha na kisha ukawabaini na kusema,watakudhuru,ama watakuchukua mzimamzima na kukupeleka kuzimu.Huko watakulisha nyama za viumbe usiyo wajua na kukunywesha maji yasiyo fahamika.
Wakuu tuendelee kukaa kimya mara tuotapo ndoto mbaya ili tuwaenzi WAHENGA au tuwe tunasimulia ndoto zote nzuri na mbaya
ili twende na dunia?karibu uchangie simulizi hii toka kwa babu.