Simulizi za Abunuasi...

Senator jr

JF-Expert Member
Apr 3, 2016
367
496
Kufwendaaaaa...
Wakuu ni muda wetu na wakati wa kuandaa nyoyo zetu juu ya vichekesho ndani ya Maisha ya Abunuasi kuwa karibu na thred hii.

HEKAYA ZA ABUNUASI.
Part one 1.
Abunuasi Alinunua Punda Ila Hakuwa Na Sufuria Kubwa La
Kumnyweshea Maji Ikabidi Aende Kuazima Kwa Jirani Na
Akapewa Baada Ya Siku 3 Akalirudisha Kwa Mwenyewe
Huku Akiwa Ameweka Sufuria Nyingine Ndogo Ndani
Yake,
Abunuasi Akamwambia Yule Jirani Wakati Anaichukua Ile
Sufuria Ilikuwa Na Mimba Kwahiyo Imezaa Yule Jirani
Akashangaa Na Kufurahi Kusikia Sufuria Imezaa,
Siku Nyingine Abunuasi Akaenda Kuazima Yule Jirani
Akampa Akijua Itarudi Imezaa Lakini Siku Nyingi Zikapita
Bila Sufuria Kurudishwa Ndipo Alipoamua Kumfata
Abunuasi Akamwambia "Samahani Jirani Ile Sufuria
Imefariki Wakati Inajifungua."
Jirani "Haiwezekani Sufuria Haiwezi Kufa."
Abunuasi "Kila Kinachozaa Pia Hufa."
Yule Jirani Alirudi Kwake Bila Sufuria...

Hope of Jf
Cc
Senator jr
 
Hekaya za Abunuasi
Part two.02
Abunuasi Aliwaambia Watu Ya Kuwa Kila Siku
Anatembelewa Na Malaika Na Taarifa Hizo Zikaenea
Zikamfikia Mfalme,
Mfalme Akamuita Na Kumuuliza Na Abunuasi Akakubali
Mfalme Akamwambia Ataenda Kwa Abunuasi Kumuona
Malaika Na Endapo Anamdanganya Anamtia Gerezani,
Basi Mfalme Akaenda Mpaka Nyumbani Kwa Abunuasi Na
Abunuasi Akampa Masharti Mbele Za Watu "mfalme Usijali
Utamuona Malaika Ila Kuna Masharti Ya Kumuona Kama
Wewe Ni Mtoto Haramu Huwezi Kumuona Kabisa Na Pia
Ukiingia Lazima Uweke Dhahabu Mlangoni" Mfalme
Akakubali Na Abunuasi Akaingia Ndani Akachukua Kiti Chini
Ya Kiti Akaweka Viatu Na Juu Kofia Na Akatandika Vazi
Zuri Yani Kama Mtu Amekaa Halafu Akamkaribisha
Mfalme,
Mfalme Alipoingia Hakumuona Malaika Ila Alishindwa
Kusema Hajamuona Aliogopa Kuonekana Yeye Ni Mtoto
Haramu Hivyo Akatoka Mle Ndani Na Kusema Amemuona
Malaika Na Abunuasi Akawa Amepata Dhahabu Kiulaini

Cc
Senator jr
 
Hekaya za abunuasi ..
Part three.3
SIKU moja alfajiri, wakati wananchi wa mji wenye
wakazi wengi walipokwenda kuchota maji mtoni,
walishangazwa kuuona mkono wa mtu ukiwa katikati ya
mto. Mkono huo wa ajabu ulikuwa umenyoosha vidole
viwili juu, kuonyesha alama ya mbili.
Wananchi walistushwa sana na kitendo hicho, wakaogopa
hata kuchota maji mtoni, kwani hawakuwahi kuona tukio
la kuogopesha kama lile. Wengine waliamini kuwa huo
ulikuwa mwili wa mtu aliyetupwa mtoni.
Lakini ishara iliyoonyeshwa na mkono huo iliwafanya
wananchi waamini kuwa huo ulikuwa mkono wa ajabu.
Katika kiza kinene kilichozunguka ndani ya vichwa vya
wananchi, habari zikamfikia Mfalme wao, naye akafika
haraka eneo la tukio.
Mfalme wa nchi hiyo baada ya kujiridhisha kuwa ulikuwa
mkono wa ajabu na uliwekwa na watu wenye imani za
kishirikiana, alitoa siku tatu mkono huo uwe
umeondolewe, vinginevyo ataleta wataalam kutoka
sehemu mbali mbali duniani kwa ajili ya kubaini wahusika.
Siku tatu zilizowekwa na Mfalme zikaisha, wataalam wa
mambo ya asili kutoka sehemu mbali mbali duniani
wakaanza kuwasili mtoni hapo kwa lengo la kuundoa
mkono huo wakashindwa.
Mfalme akatoa ofa nono, waganga wenye sifa na jeuri ya
mambo ya jadi wakamiminika eneo la mto, wakafanya
mitambiko na mambo yao kwa ufanisi zaidi, wengine
wakalala mtoni kuonyesha umahili wao lakini wakashindwa
na kuuondoa mkono huo wa ajabu...
Mfalme na wasaidizi wake wakakuna vichwa, wananchi
hawana jinsi ya kupata maji. Maji mtoni hayachoteki,
wananchi wanaogopa kutumia maji hayo. Ndipo Abunuwasi
akajitokeza mbele ya Mfalme. Akamwambia Mfamle,
"Mimi naweza kujaribu.
Mfalme akamfukuza Abunuwasi kwa hasira, akamwambia.
"Mpumbavu sana wewe, hapa wameshindwa waganga na
waganguzi, wewe Abunuwasi utaweza wapi, usitupotezee
muda wetu".
Abunuwasi akaondoka, waganga wakazidi kumiminika
mtoni wakitoka sehemu mbali mbali za dunia kutokana na
sifa zao. Kila walichofanya kuuondoa mkono huo
wakachemka na kuondoka eneo hilo kimya kimya.
Abunuwasi akamrudi Mfalme, akamwambia, "Wacha
nijaribu mimi". Mfalme akamjia juu akamwambia.
"Nimesema huwezi Abunuwasi, wameshindwa waganga wa
dunia, utaweza wapi wewe?, Abunuwasi akasisitiza.
"Wacha nijaribu mimi kama walivyojaribu wengine na
kushindwa.
Mfalme kwa hasira akamwambia Abunuwasi, "Haya
jaribu, maana unataka kutupotezea muda tu hapa, lakini
ole wako ukishindwa, nitawaamru askari wakutie ndani".
Abunuwasi akaanza kuuzunguka mto huku umati wa
wananchi ukimwangalia kwa makini, alipita huku na huku
akikimbia kama mtu aliyepatwa na wazimu, Mfalme
akaanza kuchukia, hatmaye Abunuwasi akakaa sambamba
na mkono ule, Abunuwasi akachuchumaa chini na kuinua
mkono wake juu mfano wa mkono ule.
Mfalme na wananchi walikuwa kimya wakifuatilia kwa
makini tukio hilo, Abunuwasi aliuchezesha mkono wake
kushoto na kulia, mkono ule ndani ya maji nao ukafanya
vile, kama alivyofanya Abunuwasi. Wananchi
wakashangazwa mno na kitendo kile.
Abunuwasi akauvuta mkono wake nyuma, mkono huo pia
ukafanya hivyo, Abunuwasi akakunja kidole chake kimoja,
mkono ndani ya maji nao ukafanya vile. Hatmaye
Abunuwasi akaushusha mkono wake chini kama
anaudhamisha, mkono ule nao ukadhama na haukuonekana
tena.
Mayowe, vigelegele na shangwa vikasikika, Mfalme
akasimama akamfuata Abunuwasi, akamuomba radhi,
akamtukuza na kuonyesha kufurahishwa. "Ahsante sana
Abunuwasi, umetuondolea aibu, nisamehe kwa
kukudharau, sikutegemea kabisa".
Wananchi wakaja juu wanamtaka Abunuwasi apewe
Ufalme. Maana ameweza kufanya jambo lililowashinda
waganga na waganguzi. Mfalme akahamaki. Abunuwasi
akaula...
 
ruksa endelea mkuu ila abunuasi aliwahi kupika chakula kwenye sherehe kwa mwanga kaazi kweli kweli
Naaam kwenye majuha wengi chochote chaweza kuwa kweli na hapo mjanja kila siku ndie anaefaidika
 
Hekaya za Abunuasi..
Part 4.
Abunuasi Aliingia Kwa Kinyozi Na Mtoto,
Akasema Anyolewe Nywele Na Ndevu Alipomaliza
Akasema Na Mtoto Naye Anyolewe,
Wakati Mtoto Ananyolewa Yeye Akaaga Anaenda
Kumnunulia Mtoto Juisi,
Masaa 3 Yakapita Bila Abunuasi Kutokea Kinyozi
Akamwambia Dogo "Vipi Baba Ako Amekusahau?"
Mtoto"Yule Sio Baba Angu Alinikuta Njiani Akaniambia
Tuingie Hapa Tunyolewe Bure."
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom