Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,627
Alibaki mwenye mshangao huku machozi ya uchungu yakimbubujika kutokana na kutotarajia kama atajifungua watoto wanne, ikiwa ni ongezeko la wawili kati ya aliokuwa akiwatarajia.
Matarajio yake, ilikuwa ni kujifungua watoto wawili kwa mujibu wa majibu ya kipimo cha Ultra Sound yalivyokuwa baada ya kupima mara ya kwanza na kuamua kujiridhisha kwa mara ya pili.
Kuzaliwa kwa watoto hao, kunakamilisha idadi ya watoto wanane alionao mjane Ashura Shaibu (37), anayekabiliwa makali ya maisha na hajui namna atakavyowahudumia peke yake.
Ashura anasema ni jambo ambalo hakulitegemea, lakini Mungu ndiye amempatia watoto hao hivyo hana budi kuwatunza kwani ni zawadi ya pekee iliyoweza kuziba pengo la mume wake.
“Mume wangu alifariki Desemba 25 mwaka jana, nikiwa na ujauzito wa miezi mitatu na kuniachia watoto wanne wa kike, ipo nyumba ya vyumba vinne ninayoishi na watoto wangu,” anasema.
Baada ya kujifungua Mei 22 katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke, alilazimika kubaki chini ya uangalizi maalumu kutokana na watoto hao kuzaliwa chini ya uzito unaotakiwa.
Hata hivyo, Juni 7 Ashura aliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya hali za watoto kuimarika. “Mimi na wanangu tunaendelea vizuri, tutakuwa tunahudhuria kliniki ya watoto njiti kila tarehe tutakayopangiwa, ili wauguzi waangalie maendeleo ya watoto na kunishauri njia sahihi za matunzo,” anasema Ashura.
Licha ya kuwa na furaha ya kuungana na familia yake, katika hali isiyokuwa ya kawaida, Ashura amejikuta mwenye changamoto nyingi hasa upande wa malazi yake na watoto.
INAENDELEA UK 24
INATOKA UK 23
Ashura anasema kwa sasa wanalazimika kulala kitanda kimoja na mama yake, ili amsaidie katika uangalizi wa watoto wakati wa usiku kwani muda mwingi wanakuwa wanasumbua.
“Katika kitanda cha futi sita, tunalala watu sita ili tugawane watoto wawili wawili na mama, ili kuwapatia uangalizi unaostahili,” anasema Ashura na kuongeza: “Tulipokuwa hospitalini tulipewa vitanda vitatu yaani kimoja kwa ajili yangu, kingine kwa wanaonisaidia na kingine kwa ajili ya watoto.”
Anasema vitanda vilivyopo nyumbani kwake vyote vinatumika jambo linalosababisha kushindwa kuongeza kitanda, ili kukidhi mahitaji.
Licha ya kuwa Ashura anaishi na ndugu zake nyumbani hapo wakiwa kama wasaidizi, ukweli ni kwamba kila mmoja alikotoka ana matatizo.
“Wameacha familia zao na watu wanaowategemea wamekuja kuishi na mimi, hawana namna lakini inawabidi kwa sababu wao wakisema wasije hakuna mtu mwingine wa kunisaidia,” anasema Ashura.
Anasema hali hiyo inamfanya kuwa mwenye hofu na mawazo mengi kwa kuifikiria siku watakayoondoka kurudi Newala mkoani Mtwara, kuungana na familia zao namna atakavyoweza kuishi na watoto hao.
“Nitabaki sina usaidizi kwa sababu watoto wangu wakubwa wote wanasoma, anayebaki nyumbani ni mdogo ana miaka mitatu hawezi kufanya chochote,” anasema Ashura.
Anasema mtoto wake wa kwanza anaingia kidato cha nne na mpaka sasa hajamlipia ada ya kumalizia muhula, jambo linalofanya maisha kuwa magumu na asielewe kitu anachoweza kufanya.
Maisha yake
Anasema ugumu wa maisha ulianza ujauzito ulipofika miezi minne, tumbo lilionekana kumuelemea jambo lililomfanya ashindwe kuendelea na biashara zake zilizokuwa zikimpatia kipato kwa ajili ya matunzo ya familia.
Anasema kwa sasa misaada anayoipata kutoka kwa wadau mbalimbali ndiyo inayomsaidia katika matunzo ya watoto na familia yake.
“Mimi ndiye mama na baba, kazi sina misaada mbalimbali inayotufikia ndiyo inayotusaidia katika mahitaji ya nyumbani na watoto shuleni,” anasema.
Wadau waliojitokeza.
Anasema wakati yupo hospitalini watu wengi walimtembelea na kumjulia hali, kumpatia misaada na wengine kutoa ahadi mbalimbali hali iliyomtia moyo.
Ashura anasema watu wa ustawi wa jamii walimwambia kuna mfadhili amejitokeza yupo tayari kulea watoto hao hadi watakapokua, lakini kwa sharti la kuishi katika kituo chao cha kulelea watoto.
Anasema anatambua mtu huyo alikuwa tayari kumpa msaada, lakini kukaa mbali na familia yake ndiyo jambo ambalo asingeliweza mzazi yeyote.
Anaongeza kuwa ushiriki wa wananchi katika kumsaidia, umeendelea kuonekana hata aliporuhusiwa kutoka hospitalini.
“Kuna watu wanaendelea kuja, ninaowafahamu na nisiowafahamu na hii ni kutokana na kuguswa kwao,” aanasema Ashura.
Maombi kwa wananchi
Ashura anasema hapendi kuwa mtu wa kuombaomba kila wakati na kuishi kwa misaada ya watu, bali anataka kujishughulisha ili aweze kujiingizia kipato chake mwenyewe.
Anawaomba Watanzania wamsaidie kupata mtaji utakaomwezesha kufungua biashara ya kukaa sehemu moja, siyo kusafiri sehemu mbalimbali.
“Siwezi nikasema kwa sasa naweza kuanza kufanyabiashara, hapana. Lakini watoto watakapofikisha umri wa miezi angalau mitatu, naweza kusimamia biashara itakayoweza kunikwamua na familia yangu,” anasema Ashura.
Anasema anaamini uzoefu alionao wakati anafanya biashara za kukopesha, anaweza kuutumia na kujiingizia kipato kinachoweza kukidhi mahitaji ya familia.
“Biashara kama duka la vitu vya nyumbani, au genge ni rahisi kuiendesha tofauti na biashara ambazo bidhaa zake lazima ufuate sehemu fulani ndani ya nchi au nje,” anasema Ashura na kuongeza:
“Serikali na wadau watakaoguswa wanisaidie hata kusomesha watoto, kwa sababu sina urithi wa kuwapa zaidi ya elimu.”
Wasaidizi wanena
Mama yake Ashura, Fatuma Kuhadaika (65) anasema anatamani kukaa na mwanaye maisha yake yote lakini naye anakabiliwa na ulezi wa mjukuu wake mwenye matatizo ya akili aliyekataliwa na wazazi wake, hivyo kuamua kubeba jukumu hilo.
“Yule mtoto ananitegemea kila jambo, alipozaliwa mama yake akamtelekeza, baba yake hatujui alikoelekea,” anasema Fatuma.
Anasema hata alipoondoka alimuacha na mtoto wake mdogo, lakini kila siku aanapigiwa simu na kuombwa kurudi kwa kile kinachodaiwa mjukuu wake (mwenye matatizo ya afya ya akili), amekuwa akitoroka kila mara na kumsumbua mwangalizi.
“Hata mimi nashindwa nifanye nini sijui nimsaidie nani nimwache nani na wote ni damu yangu. Naomba Watanzania walione hili na watusaidie peke yetu hatuwezi,” anasema Fatuma.
Wifi yake Ashura, Fatuma Mohammed (39) anasema atakaa mwezi mmoja wa kumsaidia baadaye atarudi nyumbani ili kuangalia familia yake.
“Nilikuja huku siku mbili kabla ya kujifungua kwake, umekuwa muda sasa tangu nitoke nyumbani sijui watoto wangu wanaendeleaje,” anasema.
Anasema alipoondoka alimuacha dada yao mwenye miaka 19 awaangalie wadogo zake, Dar es Salaam amekuja na mtoto wa mwaka mmoja.
“Hata huyu mtoto mdogo niliyenaye ananipa wakati mgumu katika kumsaidia wifi yangu, kwani kuna wakati hata yeye anahitaji kuangaliwa kwa ukaribu,” anasema Fatuma.
Anasema Watanzania wamsaidie apate wasaidizi wa nyumbani angalau wawili wataokidhi mahitaji, kwani watoto wake wakubwa wanasoma na muda mwingi wanautumia shuleni.
Jirani hawajamtupa mkono
Mama Jerry anasema Ashura ameishi na majirani vizuri tangu alipomfahamu, jambo linalosababisha waguswe kumsaidia katika mambo madogo ambayo yamo ndani ya uwezo wao.
“Awali alipotoka hospitalini alioneka bado hajawa vizuri kiafya, lakini kadiri siku zinavyozidi anaimarika, jamii iendelee kumsaidia na kumkwamua isimuache peke yake, hawezi!” anasema.
Muuguzi Hospitali ya Temeke
Katika kuhakikisha mama huyo anapata huduma sahihi na kuendelea kuwa chini ya uangalizi hata baada ya kutoka hospitalini, Muuguzi Mkuu Hospitali ya Temeke, Deodata Msoma anasema kwa sasa Ashura yupo chini ya ustawi wa jamii.
“Ustawi wa jamii ndiyo wenye dhamana, sisi kama wauguzi tunazidi kumsisitiza kuwalisha vizuri watoto na kuhudhuria kliniki kwa tarehe anazopangiwa ili tujue wanavyoendelea,” anasema Deodata.
Kama umeguswa waweza kumsaidia Ashura kwa namba 0783 287 929