Simulizi ya maisha yangu

Simulizi ya maisha yangu

Plato

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Posts
420
Reaction score
94
Simulizi ya Ludovick Joseph

---- Kwa wafuatiliaji wa taarifa katika vyombo vya habari na hasa magazeti wanafahamu kuwa nimekuwa nikihusishwa na matukio kadhaa ya kisiasa na hatimaye pamoja na Lwakatare mkurungezi wa ulinzi wa CHADEMA Taifa, Tulifunguliwa mashitaka na kuwekwa gerezani ambapo mimi nilikaa kwa miezi mine Kabla ya kupata dhamana. Hakika yalisemwa mengi na bado yanaendelea kusemwa na labda masimulizi haya yataibua mambo mengine zaidi.

------ -Ingawa habari kuhusu mimi ziliandikwa sana mfululizo kwa zaidi ya miezi mitatu lakini tangu nipate dhamana mwaka mmoja na miezi miwili sasa bado naona jamii haijapata kujua kwa undani wala ukweli wa nini hasa kilitokea. nimeona kwa macho yangu mwenyewe namna ambavyo kuna uwezekano wa jamii kupotoshwa juu ya jambo Fulani na ikajikuta inaamini- tofauti na ukweli.

-------- Ninaandika simulizi hii ili kuelezea uhalisia wa kilichotokea na kile ninachoweza kukiita " simulizi yangu"(the side of my strory).

-- Ni muhimu kuzingatia kuwa bado ninayokesi mahakamani. kwa hiyo simulizi hili halitahusu masuala ambayo yanaweza kuingilia mwenendo wa kesi na uhuru wa mahakama. Hayo tutayaongea baada ya kesi kumalizika. Inshallah!

-------- Kwa hiyo simulizi hili haina lengo la kujitetea- wala kutoa tuhuma kwa yeyote, bali jaribio la kuelezea kilichotokea lakini pia kusahihisha uongo na upotoshaji uliofanywa na watu mbalimbali juu ya matukio niliyohusishwa nayo.

------ Na kwa ufupi tu nimezaliwa bukoba vijijini mwaka 1982, katika familia ya mwl.ludovick Paulo na Savera Telesphor, watoto Sita wote wa kiume, mimi nikiwa mzaliwa wa nne. Nimewahi kuishi Mwanza Morogoro, Songea Daresalaam na Mbeya. Nimeoa na nina mtoto mmoja.

----- --Nimesoma shule ya msingi na Kumaliza darasa la saba mwaka 1997 na kujiunga nyakato secondary iliyopo Bukoba kwa kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 2001. Mwaka 2002 nilijiunga na seminari katoliki ya mt. Francis De sales Morogoro ambapo nilimaliza kidato cha sita mwaka 2004. Baada ya hapo -nilijiunga na malenzi ya upadre katika shirika la mt. Vincent -wa- paulo- na kupokelewa hapo mwaka 2005. Kwa muda kabla ya kuingia shirika hilo, nilifundisha Rugambwa girls, high school – ya Bukoba.

-nilifanya mwaka wa malezi hadi sept,nilipoanza kusoma shahada ya falsafa katika chuo cha wasalvatori (salvatorian Institute of philosophy and theology)chuo hiki ni affiliate ya pontifical university Urbaniana- cha Roma Italia. katika mchakato huo nimewahi pia kukaa kwa muda kibosho- major Seminary Moshi kabla ya kuamua kuacha malezi ya upadre na mwaka 2008 nikajiunga na chuo kikuu kishiriki cha ualimu cha DUCE ,ambako niliondoka mwaka 2011.

Nilipangiwa kufundisha Singida lakini sikuendelea na kazi ya ualimu huko,badala yake nilijikita katika siasa na katika mitandao ya jamii nikiendesha Mjenjwa- blog. nitafafanua zaidi juu ya baadhi ya masuala haya huko mbele.

-

KUJIHUSISHA NA SIASA

Tangu kale nikiwa kidato cha pili mwaka 1999,nimekuwa mfuatiliaji mkubwa wa siasa nikisoma kila wiki magazeti ya RAI enzi hizo likiandika chambuzi mbalimbali.nilichaguliwa kiranja mkuu wa shule na nilikuwa na mahusiano na viongozi kadhaa wa CCM mkoa wa kagera siku hizo,Mzee Senguo,nadhani katibu wa CCM mkoa na ndugu kagashe. pia nilimfahamu kapteni mstaafu kateme diwani wa kata yangu CCM (baadaye mwenyekiti wa halmashauri ya BKB vijijini)

Lakini baada ya kuingia seminari,nilikuwa nimebadilika sana interest kwenye siasa na hapo nilifikiria zaidi malezi ya upadre na mafunzo hayo na kwa kweli hakuna ruhusa kujihusisha na siasa katika seminari

- -Nakumbuka nilikuwa- nikipenda sana makala za padre privatus Karugedo. Nilipata shida kwa sababu Karugendo alikuwa hatazamwi vema -na walezi wangu na kushabikia- makala zake ilitafsiriwa kama kukubaliana na- mitazamo yake hasi -juu ya baadhi ya mafundisho ya kanisa katoliki.

--------- Mwaka 2006, nikiwa nasoma Falsafa, nilifahamu juu ya chama cha chadema kuzaliwa upya. Hapo nikasikia kuwa kina "Falsafa" ya Nguvu ya umma. Nilipenda sna sana kujua msingi wa falsafa hiyo kwa hiyo nilipopata likizo, nikiwa Dar-es-ssalaam,nilitafuata ofisi za chadema -na hapo nilikutana mara nyingi sana na John Mnyika – wakati ule akiwa anaonekana hata kwa macho kuifuata na kuiamini falsafa ya chama.

----- Tulikaa- na mnyika kwa masaa mengi karibia kila siku nilipokuwa Dar-es-salaam tukijadili mambo mbalimbali , nikimsaidia kuelewa baadhi ya maswala ya kikanisa -yaliyokuwa yanamtatiza. Tulikuwa tunakutana na Akani David Kafulila wakiwa wadogo kwelikweli. nakumbuka siku nyingine Mnyika hakuwa na hela ya chakula cha mchana na mimi nilimnunulia lunch.

Lakini hata wakati huo hatukuruhusiwa kufanya siasa seminari -na hakika hilo halikuwa suala la kipaumbe.,hata hivyo mapenzi yangu kwa chadema yaliendelea na nilipoacha- malezi ya upandre na kuanza chuo kikuu pale DUCE, mwaka 2009 nilijiunga na kukabidhiwa rasmi kadi ya chadema na Erasto Tumbo akiwa Afisa wa habari na uenezi na nilikabidhiwa -kadi hiyo makao makuu ya chama .baadaye nilikuwa mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA chuo cha DUCE…itaendelea wiki ijayo…



0752 814961
 
Mpuuzi tupu huyo mchumia tumbo.

Na hilo gazeti uchwara.

Mnatafuta promo?

Tupo busy na Escrow, tunawapuuza!
 
Hivi hili ndo lile li-Ludovick la Ugaidi au? if yes! ni mpuuzi, tupo katika sensitive issues za kitaifa kwa sasa, hii asubiri mwakani aitoe, kwanza sijaisoma lakini najua kilichomo ni rubbish...
 
Nashauri Ludo apewe ulinzi mara moja!, wasije kumnyamazisha hivyo akaikatishia story yake njia!.

Pasco
 
Nashauri Ludo apewe ulinzi mara moja!, wasije kumnyamazisha hivyo akaikatishia story yake njia!.

Pasco

Imeshindwa story ya tezidume kuzima moto wa Escrow ndio itaweza hii ya huyu Kibaraka aliyekwishashindwa mapema kabla hajaianza kazi?
 
Wewe Ludovic jaribu kutumia shule ya seminari ili uendeleze maisha yako! Hapa hakuna chochote na wala hii story haikusaidii kabisa. Ushauri wangu wa bure achana na maswala ya siasa ya maji taka! Rudi ktk taaluma yako ya walimu au fanya shughuli nyingine mbali na haya mambo ya ........
 
Wewe Ludovic jaribu kutumia shule ya seminari ili uendeleze maisha yako! Hapa hakuna chochote na wala hii story haikusaidii kabisa. Ushauri wangu wa bure achana na maswala ya siasa ya maji taka! Rudi ktk taaluma yako ya walimu au fanya shughuli nyingine mbali na haya mambo ya ........
Ludo ana akili nyingi kuliko wewe
 
Ludo.....unavyosema Mnyika akiwa mdogo kweli kweli....unamaanisha kiumbo....kiumri au? wewe umemaliza elimu ya msingi mwaka 1997 wakati Mnyika amemaliza kidato cha nne mwaka 1998.....una jeuri gani ya kumuita "wakiwa wadogo kwelikweli" ......wewe ni bwana mdogo kwa Mnyika acha mbwembwe na kukosa adabu kwa kaka zako .........
 
leo hii ninajutia uamuzi wangu wa kumtetea ludo kwa nguvu zangu zote asichomwe moto pale darajani baada ya kujiingizaa kwenye 18!......
 
Mpuuzi tupu huyo mchumia tumbo.

Na hilo gazeti uchwara.

Mnatafuta promo?

Tupo busy na Escrow, tunawapuuza!
yanatoka mayoni kwake mkuu unatakiwa kuyaeshimu mawazo yake na sio kumtusi mkuu
 
Imeshindwa story ya tezidume kuzima moto wa Escrow ndio itaweza hii ya huyu Kibaraka aliyekwishashindwa mapema kabla hajaianza kazi?
eshimu mawazo ya mtuu mkuu
yeye anasema kilicho mayoni kwake
 
Nashauri Ludo apewe ulinzi mara moja!, wasije kumnyamazisha hivyo akaikatishia story yake njia!.

Pasco
Pasco,
Consequential Destiny ya story yake ilizimwa na Supreme Tundu Lissu mahakamani. Hana madhara tena huyu Ludo
 
Last edited by a moderator:
Hivi hili ndo lile li-Ludovick la Ugaidi au? if yes! ni mpuuzi, tupo katika sensitive issues za kitaifa kwa sasa, hii asubiri mwakani aitoe, kwanza sijaisoma lakini najua kilichomo ni rubbish...

Kama ni upuuzi weka ya kwako mkuu . mawazo ya mtu yaheshimiwe hii ni jf siyo uhuru
 
Ludo.....unavyosema Mnyika akiwa mdogo kweli kweli....unamaanisha kiumbo....kiumri au? wewe umemaliza elimu ya msingi mwaka 1997 wakati Mnyika amemaliza kidato cha nne mwaka 1998.....una jeuri gani ya kumuita "wakiwa wadogo kwelikweli" ......wewe ni bwana mdogo kwa Mnyika acha mbwembwe na kukosa adabu kwa kaka zako .........
halafu Mnyika kazaliwa 1980 huyo ludo kasema kazaliwa 1982, sasa sijui udogo wa mnyika kwake uko wapi? Mungu mkubwa.
 
Ludo ana akili nyingi kuliko wewe

Mkuu ujumbe umefika hata hivyo! Hapa kinachoongelewa siyo kuwa na akili nyingi ila nikutafuta njia nzuri ya kumsadia Ludovic ili aachane na hao jamaa wanao mtumia yeye bila kujua! Bado ana nafasi kubwa ktk nyanja zingine na wala si siasa za ACT+....
 
..........-------- Kwa hiyo simulizi hili haina lengo la kujitetea- wala kutoa tuhuma kwa yeyote, bali jaribio la kuelezea kilichotokea lakini pia kusahihisha uongo na upotoshaji uliofanywa na watu mbalimbali juu ya matukio niliyohusishwa nayo...............
eti lengo sio kujitetea...............
 
Back
Top Bottom