Gnicx_33
Member
- Mar 12, 2019
- 41
- 60
SIMULIZI YA MAISHA: USILIE NADIA.
MTUNZI: GEORGE IRON MOSENYA
SIMU: 0655 727325 na 0757727324
SEHEMU YA KWANZA
Mwendo wa kutoka nyumba ya kulala wageni tuliyolala usiku uliopita haukuwa mkubwa sana hadi kuifikia stendi kuu ya mjini Musoma ambayo ujenzi wake ulikuwa unaendelea bado licha ya kwamba ilikuwa imeanza kutumika. Mara yangu ya mwisho kuingia katika mji huo ambao ni makao makuu ya mkoa wa Mara kituo cha mabasi bado kilikuwa kipo katikati ya mji. TULIPOFIKA kituo cha mabasi tuliangaza huku na kule huku tukikwepa usumbufu wa ‘wapiga debe’ wa kutuchagulia gari la kupanda huku wakitoa sifa kedekede kuhusu gari wanalolipigia debe.“Tupande Zacharia Coach” alininong’oneza binti yule huku akinielekeza mahali zilipo ofisi zao. Tukajongea huku kila mmoja akiwa ametundika begi lake mgongoni.
Nilimsaidia kubeba kifurushi kimojawapo.Baada ya kupata tikiti zetu mbili ambazo zilituruhusu kuketi pamoja katika basi lenye hadhi ya V.IP, tulijongea upesi garini japo muda wa kuondoka ulikuwa haujafika. Lakini hatukuwa na jambo lolote la kutufanya tukae nje.“Naomba nikae dirishani kaka” aliniomba, nikamruhusu nami nikaketi mkono wake wa kushoto, hapa sasa niliweza kumchunguza kidogo kwa macho ya kuibia ibia nywele zake jinsi zilivyokuwa zimenyonyoka, huenda ni kwa sababu ya kukosa matunzo. Uso wake ulikuwa umechujuka na ile rangi yake ya asili ilikuwa imetoweka.
Alikuwa na mabaka mabaka yasiyokuwa rasmi na ambayo nilikuwa sijajua sababu yake.Nikiwa katika kumchunguza mara alinigeukia huku macho yake yakiwa yanalengwa lengwa na machozi. Midomo ikimtetemeka, bila shaka alikuwa anataka kusema kitu, ama la kuna kumbukumbu ilimjia. Ni hicho ambacho nilikuwa nataka kutoka kwake.
Upesi nikafungua begi langu, nikatoa kijitabu changu kidogo na kalamu kisha niitegesha na simu yangu upande wa kunakili sauti. (sound recording).Badala ya kusema neno alitazama nje pale dirishani, nami nikachungulia na kukutana na wauzaji wa bidhaa ndogo ndogo, sikujua hii inamaaanisha nini.Binti yule akageuza kichwa na kunitazama sasa alianza kuzungumza...
Itaendelea .......
Inawndelea...........
poleni kwa subira
AKAANZIA HAPA. Nami nikamrekodi huku kiuandishi nikinukuu mazingira na muonekano wake ili nisipoteze uhalisia.
“Mara ya kwanza kabisa nilikutana naye hapa, alikuwa anauza maji na soda za kopo pamoja na biskuti. Sikuwa na mpango wa kununua chochote lakini ucheshi wake ukanifanya ninunue soda ya kopo, huwa sipendi kula nikiwa safarini. Sipendi kabisa. Sijui nini kilinivuta kwake, nikanunua. Akatabasamu baada ya kuona amefanikiwa kunishawishi, wakati anataka kunipatia chenchi yangu mara gari likaanza kuondoka, nilikuwa nimempatia shilingi elfu mbili tu na alitakiwa kunirudishia shilingi elfu moja. Nikamsikia anapiga mayowe ya kuzuia basi lisiende anipatie pesa yangu, nilitamani kupiga kelele kumwambia abaki na ile pesa lakini sikubarikiwa uwezo wa kupiga kelele. Nilikuwa siti ya dirishani kama leo hii hapa, nikachungulia anapotokea ili kama nikifanikiwa kumuona nimpungie mkono na kumuashiria kuwa sihitaji pesa ile. Na kweli sikuwa na haja na pesa ndogo kama ile, nilikuwa na nyingine nyingi. Lakini mara macho yangu yakashuhudia kitu kibaya sana kijana yule alijibamiza katika basi jingine akapiga mweleka chini, maji na juisi zake zikatapakaa huku na huko. Hapo sasa niliweza kupiga kelele huku nikiwa nimetaharuki. Yule kijana alikuwa amepata ajali.
Safari yangu ikaharibika, nikawa namlilia mwanaume nisiyemjua hata jina na ilikuwa mara ya kwanza kuonana naye. Nililia sana bila kukoma, hakuna aliyeweza kunibembeleza maana ni moyo wangu ulikuwa unalia. Walionitazama nje hawakujua lolote.
Laiti kama ningejua lijalo, nisingethubutu kununua maji yake mwanahizaya mkubwa yule, nisingethubutu kusema naye na nisingedanganyika na ucheshi wake hata kidogo. Yaani nikamlilia nikiwa hat simjui lakini yeye akaja kuniliza huku akiwa ananijua kila kitu nje na ndani.
Itaendelea.......