Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,638
SEHEMU YA 01:
Siku hiyo mvua ilinyesha sana halafu shuleni kulikuwa na mitihani na mama alinitaka nirudi nyumbani kufanya kazi fulani, kwa hiyo nikaamua kumfuata mwalimu mkuu ambaye alikuwa ofisini kwake kwa lengo la kumbadilisha akili aseme wanafunzi wote turudi nyumbani hadi kesho yake.
“Nilisimama nje ya mlango wake, nikainama kwa sekunde chache, nilipoinua uso, nilibadilika ghafla na kuwa mwanafunzi wa kiume wa pale shuleni anayeitwa Juma Amosi.
“Nilishika mlango na kuufungua, nikazama ndani. Mwalimu mkuu alikuwa akitafuta mafaili kwenye kabati kubwa la ofisini kwake. Alishtuka kuona mlango umefunguliwa bila kugongwa.
“Ilikuwa ukitaka kuingia kwenye ofisi ya mwalimu mkuu ni lazima ugonge mlango na ukaribishwe kwa sauti, kinyume cha hapo usimame mlangoni mpaka atakapotoka au kukukaribisha kama una uhakika alikusikia.
“Wewe Juma ni kwa nini umeingia bila kupiga hodi?” mwalimu aliniuliza. Nilisimama katikati ya ofisi kama mwanajeshi, nikamkazia macho badala ya kumjibu, niliulekeza mkono wangu usawa wake, ukamfikia kwa kurefuka, nikamshika kichwani.
“Palepale akaanza kutabasamu huku akisema nikapige kengele ili wanafunzi wakusanyike mstarini kwa ajili ya kuwaambia jambo la dharura.
“Nilipotoka kwenda kugonga kengele, nilisimama mlangoni tena, nikabadilika na kuwa mjusi, nikakimbia chini kwenda mpaka kwenye mti wa kengele, nikabadilika tena na kuwa Yusta yuleyule. Nikagonga kengele.
Kwa kengele ya muda ule kila mtu alijua kulikuwa kuna dharura, kwa hiyo wanafunzi wakatoka kwenda mstarini ili kusikiliza.
Nilikwenda mstarini kwa kuzunguka nyuma ya shule ambako haikuwa rahisi mtu kuniona kama mimi ndiye niliyegonga kengele, nikafika mstarini na kusimama.
Baadhi ya walimu walitoka ofisini kwao na kuja usawa wa mstari huku wakionekana kushangaa.
“Nani amegonga kengele?” aliuliza mwalimu mmoja aliyejulikana kwa jina la Cecilia Kizigo.
“Hatujui,” wanafunzi mbalimbali walijibu huku wengine wakiendelea kushangaa.
Mara, mwalimu mkuu alitoka akiwa ameshika kitabu mkononi. Alitembea mpaka usawa wa walimu wa kawaida, naye akauliza kengele ni ya nini?
Walimu wengine wakamjibu hawajui. Sasa ikawa nani kapiga kengele, nani kapiga kengele. Kumbe mwanafunzi mmoja aliniona nikipiga mimi kama Yusta, akanitaja. Kwanza kabla hajanitaja alinyoosha mkono, mwalimu wa zamu akamuita jina:
“Hamisa unasemaje?”
“Mwalimu mi nilimwona Yusta akipiga kengele.”
“Yusta toka mbele,” yule mwalimu aliniamuru, nikapita mbele nikiwa na wasiwasi, lakini si sana.
“Nani alikwambia ugonge kengele?” yule mwalimu wa zamu aliniuliza kwa ukali.
“Juma.”
“Juma gani?”
“Juma Amosi.”
Niliposema Juma Amosi tu, mwalimu mkuu akatingisha kichwa kama anayekubaliana na mimi.
“Kweli atakuwa Juma Amosi. Alikuja hata kwangu akasema kengele igongwe anataka kuzungumza jambo.”
Walimu walionekana kumshangaa sana mwalimu mkuu kwa kauli yake hiyo, pengine kwa sababu haijawahi kutokea siku mwanafunzi akataka kengele igongwe ili aongee, mara nyingi wafanyao hivyo ni viongozi wa shule.
“Juma Amos,” mwalimu wa zamu alimuita mbele, akatoka.
“Naam mwalimu.”
“Ulitaka kuongea kitu gani wewe mpaka ukaenda kwa mwalimu mkuu na kuomba kengele igongwe?”
Juma Amos alionesha kushangaa, akaniangalia mimi kwa macho ya kunisuta, lakini na mimi nilijikausha.
“Mwalimu mimi namshangaa sana Yusta, sijamtuma.”
“We!” mwalimu mkuu alikuja juu, akaendelea:
“Wewe hukuja ofisini kwangu ukasema unataka ugonge kengele ili uongee jambo?”
“Mwalimu sijaja.”
“Weee,” mwalimu mkuu aliwaka tena. Cha ajabu, Mwalimu Cecilia akamtetea Juma Amosi kwamba, yeye mpaka kengele inagongwa alikuwa darasa la akina Juma Amosi, hajamwona akitoka zaidi ya muda ule kengele ilipogongwa.
ITAENDELEA