Simulizi ya Kweli: Jinsi Nilivyoacha Uzinifu

Simulizi ya Kweli: Jinsi Nilivyoacha Uzinifu

hahahaha dah nilitaka ni comment afadhali tumepata ka story endelevu sa kabla ya kusema nasubiri part navoangalia comment za watu nikakuta inaendelea...heekuona ghafla ndio mwisho aisee dah...nilidhani itakuwa ndefu kidogo ......dah
 
Ina potential ya kuwa bonge ya story, ila hujaitendea haki. Umeimaliza kiajabu ajabu tu. Hebu mwandishi mzuri aendelee.
 
Bora umesema mkuu...huyu jamaa sijui anafikiri kuwa kila mtu ni mtoto???
Aise baadhi ya Watanzania ni watu wa ajabu sana. Heading inasema simulizi ya kweli wewe unasema ni uongo!!
 
Kipi kinakufanya udhani hii simulizi ni ya Sungura na Fisi?
Safari yangu ya maisha na mapenzi na uhusiano ilianza mwaka 2008 baada ya kufika chuo na hii ilisababishwa na ukweli kwamba sikuona haja ya kujihusisha na mapenzi kabla sijafika level hiyo. Kuelekea mwishoni mwa mwaka 2008 nilipata mpenzi ambaye tulikuwa tunasoma nae hapo chuoni.

Mwaka 2009 nilishiriki tendo la ngono kwa mara ya kwanza na sababu iliyopelekea kufanya hivyo ni kwasababu marafiki waliniambia nilikuwa na mwanamke mzuri sana hivyo kama nisipofanya nae mapenzi itakuwa rahisi yeye kuniacha.

Baada ya tendo nilitopea katika mapenzi na msichana wangu, maisha ya mapenzi yalikuwa mazuri kwa kiasi fulani na mabaya kwa kiasi chake. Tulikuwa na furaha na mara nyingi tulikula chakula maeneo ya Posta Mpya ( Kuna ule Mghawa upo Kituo cha Mafuta) na wakati mwingine tulikuwa Chef Uhindini kwasababu nilifanikiwa kupata kazi nikiwa mwaka wa pili.

Kwa kiasi fulani ilikuwa ni changamoto kuwa na mrembo yule kwasababu vishawishi vya wanaume vilikuwa ni vingi sana na kuna wakati nilihisi sipo peke yangu. Lakini hadi kufikia mwisho wa masomo yetu tulikuwa pamoja na lengo hasa lilikuwa kuja kuishi pamoja, familia ya binti ya karibu ilifahamu nia yetu isipokuwa baba wa binti tu.

Kipindi hiki kulikuwa na binti wa kitanga akinisumbua tangu mwaka 2011 akihitaji mahusiano nami, lakini kwa penzi nililokuwa nalo kwa mrembo wangu sikumsikiliza abadani.

Sekeseke la lilianza Novemba mwaka 2012 mwaka mmoja baada ya kumaliza chuo wakati huo mimi naendelea na kazi yangu na binti alipata kazi ya kujishikiza katika moja ya makampuni ya Umma. Baada ya ugomvi na confrontation binti aliomba tupeane muda wa miezi 6 kila mmoja ajitafakari kuhusu mahusiano yetu.

Nilikubali kwa shingo upande na nakumbuka siku ile nazungumza nae akiniambia kuhusu jambo hili nilikuwa nimeshika wallet natoka dukani, nusu saa baadae sikuwa na wallet mfukoni na sikujua niliangusha wapi. Baada ya taarifa hiyo akilini mwangu nilitambua kwamba sasa niko mwenyewe na ilibidi kuishi hivyo.

Nilianza maisha ya upweke mwaka 2013 kwa hali ya uchungu na majuto wa hali ya juu, kaka yangu alifahamu mapenzi niliyokuwa nayo kwa binti yule na alinisihi nisije kufanya maamuzi ya kurudiana nae maana lile sekeseke lililotokea Novemba 2012 alilifahamu “ Ole wako nikuone unarudiana na Z” kauli hii aliitoa kaka yangu.

Itaendelea......
angalia hiyo sentesi niliyo ikolezea wino....mtu mzima mwenye nyingi akili hawezi kufanya kitu kwa kushawishiwa. watoto wadogo ndo huwa wanaelekezwa kipi cha kufanya na kipi cha kuacha.
 
angalia hiyo sentesi niliyo ikolezea wino....mtu mzima mwenye nyingi akili hawezi kufanya kitu kwa kushawishiwa. watoto wadogo ndo huwa wanaelekezwa kipi cha kufanya na kipi cha kuacha.

Hivi unataka kuniambia kwa akili niliyokuwa nayo niko chuo mwaka wa kwanza haikuwezekana kuchukua ushauri wa marafiki ukizingatia sikuwa na uzoefu wowote kwenye mapenzi? Sigh...
 
yaan ulivyoanza na ulivyomalizia tofaut khaa yaan wewe umeogopa kunguru tu...
 
yaan ulivyoanza na ulivyomalizia tofaut khaa yaan wewe umeogopa kunguru tu...
Hahaha..nimeogopa kitendo kile kujirudia mara mbili mahali pale pale kwa staili ile ile na muda ule ule wa asubuhi. Lakini pia unapofanya hili tendo kuna wakati you admit you are sinner and you afraid the proceeding. How was it supposed to end?
 
Hahaha..nimeogopa kitendo kile kujirudia mara mbili mahali pale pale kwa staili ile ile na muda ule ule wa asubuhi. Lakini pia unapofanya hili tendo kuna wakati you admit you are sinner and you afraid the proceeding. How was it supposed to end?
fine everyone has his / her own ending but yours its kind strange nweis its good for you...
 
Umeunganisha tu nukta vibaya, acha woga, jichunguze kunguru huwa anakukwarua ukiwa umevaa nguo gani au nywele zikiwa ndefu au fupi huenda kunguru huona km umebeba kitu kichwani, au unaegeshaga miwani kichwani au unajipakaga mafuta gani kichwani ambayo hualika wadudukm vipepeo kufuata harufu na kunguru akaona ajipati shibe kwa wadudu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom