37.
MWISHO C.O.D.EX. 1
(SEASON 1)
Ila sikufanikiwa, "muda wako wa kuishi duniani umwekwisha, kwa heri maana naskia jeshi la nyumbani lishafika kuja kuniokoa" alisema huku akiondoka. Hiyo ndio ikawa nafasi pekee ya mimi kutoka katika kiti hicho, kwa nguvu zangu zote nilijirusha na kuanguka, kiti kilivunjika na mimi bila kuchelewa nikasimama, nilikiteuwa kiganja changu kimoja ili nitoe pingu na nikafanikia japo maumivu yalikuwa makali lakini sikujali. NIlitoka chumbani humo huku nakimbia kumfata, kisha nikatuma kodi kupitia kichwa changu na lile bomu likaripuka. Nilimkuta akiwa kasima huku anacheka, nilimvizia na kumtia kabali kisha nikamvuta ndani na kuingia nae katika chumba kimoja hivi. "leo nataka nikuonyeshe maumivu ya kuungua na moto" nilimwambia huku nikimwagia mafuta ya taa, "tafadhali usinichome,nina familia inanitegemea" alijaribu kujitetea. "unajua saa hivi kama una familia, lakini kipindi ukinitenganisha na familia yangu hukujali kama ningeteseka kiasi hichi" nilijibu huku machozi yakinitoka. "Mungu akuingize katika moto mkali kuliko yote huko unakokwenda, nakutakia safari ya misukosuko iliojaa mateso, manyanyaso na fedheha" niliongea maneno hayo kuwasha kibiriti na kukiangusha kwenye mafuta. Alipiga kelele lakini wala sikujali nilitoka nje na kukuta kumeshaanza kupambazuka, sikutaka kusubiri niliondoka eneo hilo na kutafuta pahali nikajisafisha, mwili wangu niliuhisi umekuwa mwepesi. Nilivaa mavazi ya kiraia kisha nikatoa simu na kumpigia yule kijana aniletee taxi.
Hakukaa sana alifika na taxi, niliingia na kumwambia amwambie dereva anipeleke auwanja wa ndege. Muda huo mawazo yangu yote yalikuwa kwa mwanangu Christina na mke wangu mtarajiwa Tania. Nilifika uwanja wa ndege na kumlipa yule dereva, kisha nikatoa mfuko mdogo nikamkabidhi yule kijana na kumwambia "hizo ni dola elfu tano, anza maisha yako upya na ujiajiri mwenyewe" alifurahi sana. tuliagan na mimi nikaingia ndani na kukata ticket ya kuelekea marekani, masaa kadhaa baadae ndege ilitua. Nilishangaa sana nilipotoka nje baada kuona gari za serekali zikiwa zinanisubiri, ukweli nilijua tayari naenda kuozea jela lakini kabla sijaamua la kufanya nilimuona kija mmoja kati ya wale wanne akija. KIdogo nilikaa sawa, alipofika aliniambia kuwa nahitajika white house. Tuliingia kwenye gari na kuelekea huko, nilikutana na raisi na kuongea mambo mengi lakini nikamwambia siko tayari kufanya kazi ile tena na sasa nataka kuanzisha maisha yangu ili niwe na familia yangu. Alinielewa na kuaguza nipewe ulinzi mpaka Califonia ambako ndipo alipokuwa mwangu Christina. Japo mwanzo hakunijua lakini kwa msaada wa baba mkwe wangu mambo yalikuwa mazuri. Nilitoa simu yangu na kumpigia Tania na kumuuliza yupo nchi gani, alinijibu kuwa yupo London. NIkamwambia apnde ndege aje Califonia nae hakupinga, siku ya pili mapema nilikwenda kuompokea na kumpeleka nyumbani. kwa vile mi sikuwa na wazazi,niliwafanya wake zangu kama wazazi wangu na kuwaeleza kila kitu. Walikubali na baada miezi miwili Tania aliacha kazi ya ndege na tukafunga ndoa. Na mpaka sasa tunaishi pamoja na tuna watoto wanne,Christina ambae anamiaka 22 na ni personal secretary wa rais, Jeff ambae ana miaka 18 na yuko high school, Edward ambae ana 12 na yuko junior school na wa mwisho ni Tatiana ambae ana mika 3 na yuko baby class.
.
NA MIMI SIE DAVID ROBERT MCCANNON KWA SABABU ALIKUFA SIKU ILE NILOMUUA ADUI YANGU MKUBWA.
JINA LANGU NI JAMES ALLEN
MWISHO.
HUU NI MWISHO WA C.O.D.E.X season one.
Kwa Season two, kaa hapahapa.
Tariq Haji anawapa shukrani wote mliokuwa mnamsapoti katika kazi hii kwa hali na mali na kumkosoa kwa makosa ambayo mliyaona.
Bado anajifunza kupitia waandishi wengine, hivyo anaomba zaidi muwe mnamfunza hasa pale mnapoona makosa ambayo yanajitokeza kwake mara kwa mara, yaani yale ambayo yanaonekana kwake ni ubovu na si yale ya bahati mbaya.
Kaa tayari kwa Season Two.
Imedhaminiwa na BURE SERIES