Simulizi ya kifantasia: Solo king: ancient legacy

Simulizi ya kifantasia: Solo king: ancient legacy

Joined
Apr 18, 2025
Posts
85
Reaction score
220
Kama mtunzi hii ni simulizi yangu ya kwanza kuandika na kuitangaza nje ya jukwaa husika. Mimi ni mwandishi wa simulizi kutoka jukwaa la fasihinet.com ya boss singanojr 😁

Nisielezee sana kuhusu mimi. Mimi ni Samuel jk(jins halisi) lakini nalipenda neno Euphoria kutokana na maana iliyopo na hii ni sImulizi yangu ya kwanza ihusuyo uchawi, mapenzi, mapigano, fantansia n.k inaitwa SOLO KING: ANCIENT LEGACY

Ninaposema uchawi simaanishi kuwangiana usiku😅😅 Ni new fashioned kinda type!

UTANGULIZI

Hapo zamani, kabla ya historia kuandikwa, aliishi mtu mmoja ambaye alivuka mipaka ya asili. Alikuwa mchawi mwenye nguvu zaidi kuwahi kutokea duniani, aliyefikia upeo wa juu lakini jina lake lilisahaulika, na urithi wake ulipotea kwa muda mrefu.

Kitu kimoja kilichobaki ni kitabu cha kale, kilichoandikwa kwa lugha zilizozungumzwa zamani, lugha ambazo sasa ni za kihistoria. Kitabu hicho kilijulikana kama FORBIDDEN GRIMOIRE, na kilikuwa na masalia ya maarifa yake pamoja na nguvu zisizo za kawaida.

Karne zilipita, falme zilikuja na kupita, dunia ilibadilika, na uchawi ukawa ni hadithi tu za kusadikika.

Lakini hatima haikupotea. Kijana mmoja aitwaye Jimmy anakuja kubeba hatima yake bila kujua.

Usikose simulizi hii ya kusisimua, yenye matukio ya ajabu na mabadiliko ya nguvu. Inamhusu kijana machachari aitwaye Jimmy, anavyopitia changamoto na majira, na jinsi anavyotoka kuwa dhaifu hadi kuwa mwenye nguvu kubwa.

°°°°°°°°°°

CHAPTER 01: Normal life(maisha ya kawaida)

Yalikuwa ni majira ya asubuhi jijini dar es salaam chini Tanzania jua likichomoza kutoka mashariki na mwanga hafifu wenye kupendeza macho, upepo wa asubuhi ukivuma taratibu na kufanya hali ya hewa kuwa yenye utulivu. Watu walikwishaamka kuendelea na majukumu yao ya kila siku ya kutafuta ridhiki za kila siku.

Apartment ya hali ya kati yenye ghorofa tatu kwenda juu ipatikanayo maeneo ya Mbezi majirani walikuwa wakiendelea na shughuli zao za hapa na pale. Ndani ya apartment hiyo ghorofa la kati kwenye chumba kidogo cha wastani alionekana mwanaume kijana akiwa amelala fofofo mpaka wakati huo na hakuonyesha dalili yoyote ya kuamka muda huo, ni wazi kwamba usingizi ulikuwa ni mtamu mno.

Wakati bado amelala mlango wake wa chumba uligongwa kuashiria kuna mtu yupo nje ya mlango wa chumba hiko

"ngo! ngo! ngo!' uligongwa tena safari hii kwa sauti kuzidi mwanzo

"We monica acha kunikata stimu basi" aliongea mwanaume huyo kwa sauti ya lawama

"Amka kumekucha"

"Sawa naamka subiri kidogo" alijibu akiwa bado amelala

Mara mlango ukafunguliwa na kuingia mwanamke mrefu wa wastani, mweupe wa ngozi na kwenda kufungua dirisha lililokaribu na kitanda kisha kulivuta shuka alilojifunika mwanaume huyo kwa fujo

"Asee we monica kuna kitu unakitafuta sio?" Hatimae aliweza kuamka akiwa hana furaha kabisa

"amka wewe kumekucha unalala-lala hovyo acha uvivu dogo"

"Si uniache sasa kwani kulala kwangu hovyo unapungukiwa na nini?" Aliuliza na bila kusubiri jibu alirudi zake kulala lakini alikuja kushtuka kwa kifinyo mguuni na kwa hasira alinyanyuka akitaka kumkamata lakini ilionekana monica alikuwa ashajipanga kwani alikimbia nduki kutoka chumbani humo kabla hata hajadakwa

Hehehe na ubabe wote lakini mwisho wa siku unakimbia tu" alijiongelesha na kuamka maana usingizi ulikuwa umekata kabisa

Hao walikuwa ni dada na kaka wa damu walikuwa wakilumbana asubuhi hio monica akiwa ndie mkubwa na mwanaume huyo aitwae jimmy akiwa mdogo

Ndugu hao walikuwa ni kama paka na panya waishio pamoja kwani kila siku ni malumbano tu na ugomvi usioisha muda yaani kifupi ni kwamba upendo wao kama ndugu ulikuwa ukidhihirishwa kwa ugomvi tu, ni bahati sana kuwakuta wakiwa pamoja bila kuzozana.

Mwanaume huyo ambaye kwasasa anatambulika kama jimmy alikuwa kijana ambaye umri wake ulikuwa miaka ishirini ya mwanzoni(early 20s).

Alikuwa ni mwanaume mtanashati na mweupe wa ngozi kama dada yake, alikuwa mrefu wa wastani na asubuhi hio alikuwa amevalia suruali nyepesi ya kulalia rangi nyeusi juu akiwa kifua wazi kuonyesha mwili wake machachari uliojengeka vizuri kuanzia mabegani mpaka kiunoni kama mwanariadha na urefu wake wa wastani

Basi Jimmy kama ilivyo kawaida ya wanaume wengi baada ya kuamka aliupasha mwili joto kwa push-ups na sit-ups kadhaa kabla ya kwenda kuusafisha mwili na baada ya kumaliza shughuli ya usafi wa mwili alivaa nguo za kawaida na kuzichana nywele zake fupi zilizonyolewa mtindo wa low fade na kumfanya azidi kuwa mtanashati haswaa. baada ya kumaliza mdogomdogo alielekea sebuleni

Kufika sebuleni aliwakuta wanawake wawili ambao ni muhimu kwake na kukamilisha familia yenye idadi ya watu watatu ambao ni yeye, dada yake na mama yake mzazi. Baba yao yeye dada yake alikwishatangulia mbele za haki miaka mingi nyuma wakiwa na umri mdogo

"Shikamoo mama" jimmy alimsalimia mama yake kipenzi

"Marahaba, umeamkaje mwanangu"

"Sio salama mama kuna kunguni alikuwa akinipigia kelele"

"Kuwa na heshima dogo nani unamuita kunguni?"

"Wewe unaniheshimu?"

"Dogo......."

"Hey hey mtapasua ngoma za masikio ysngu jamani nimeshachoka makelele yenu ebo! "mama yao alilalama ilioonekana kweli alikuwa na kazi ngumu sana kuwalea hao watoto mpaka kufikia wakati huo

"Angalau kuwe na amani basi tukipata kifungua kinywa ndio muendelee na hizo ngojera zenu" aliendelea na ndugu hao waliamua kutii mara moja

"Enhee asubuhi hii tunakula nini mama nimemisi sana chapati zako tamu kama asili" jimmy aliuliza

"Tena zipo za kutosha tu ni wewe na tumbo lako" monica alidakia

"Haya ndio mambo sasa ndio maana mama yangu nakupenda huwaga huniangushi kwenye misosi hahaha" jimmy alianza kumsifia mama yake

Basi familia hiyo walikula na kifungua kinywa kwa amani mpaka kumaliza na kila mmoja aliendelea na mambo yake jimmy aliondoka kwenda kwenye kibarua chake, dada yake akielekea chuo akibaki jimmy ambaye muda huo alikuwa amemaliza elimu yake ya advance akisubiri kuanza chuo hivyo alibaki peke yake

Licha ya kusubiria "selection" za chuo haikumaanisha akae tu kizembe,hapana kijana huyu alikuwa akifanya kazi ndogo ndogo za u'dayworker angalau apate pesa za kujikimu hapo baadae isitoshe familia yake ilikuwa ni ya hali ya kawaida hivyo kuna mda pesa inakosekana

Hakukaa sana humo ndani aliondoka baada ya kufungo mlango wa apartment yao.

°°°°°°°°°°

Muda ulienda na hatimae kufika saa kumi jioni. upande wa mbezi beach beach ufukweni mwa bahari ya hindi kulikuwa kumechangamka sana mida hio kutokana na watu kuwa wengi wakipunga upepo wa jioni hio ulioambatana na baridi kwa mbali wengine wakiogelea majini wengine wakiwa na wenzi wao wakifurahia mandhari nzuri ya bahari na kadhalika

ilikuwa ni kawaida kwa jimmy baada ya kumaliza mishemishe zake kuja hapo kutulia kabla ya kurudi nyumbani na siku hiyo alionekana kumaliza mapema sana. alienda kwenye chimbo lake pendwa la kila siku na kujilaza kwenye mchanga bila kujali kama atachafua nguo au lah

kabla ya kulala alijifunga kitambaa kichwani ili nywele zake zisiingie mchanga na kuuchapa usingizi.

Moja ya sifa ya jimmy ni kupenda sana kulala na hachagui sehemu yeye popote kambi tu ilimradi ni salama na ana usingizi wa kutosha

ameshalalamikiwa sana kulala mchana lakini yeye wala hajali anadai kwamba usingizi wa mchana na jioni ni mzuri sana kwa afya ya akili huongeza nishati mwilini na kuondoa uchovu na kupunguza msongo wa mawazo n.k

Muda ulizidi kusonga taratibu, jua nalo lilianza kuzama hatimae giza kuingia Jimmy akiwa bado amelala mahali alipokuwa. Muda ulikuwa ukisoma saa moja na dakika arobaini na hakuonyesha dalili ya kuamka muda huo

°°°°°°°°°°

Katika sehemu tulivu yenye bustani nzuri iliyopendeza kulikuwa na watu wawili wamekaa kwenye benchi mmoja akiwa ni mwanaume wa makamo na mwingine akiwa ni mvulana mdogo ambaye kwa kumuangalia tu alikuwa kati ya miaka sita au saba. Muda huo ulikuwa ni jioni, mwangaza wa jua uking'aa kwa rangi yake ya dhahabu na kufanya mandhari waliyokuwa wakiangalia kuzidi kupendeza.

"Jimmy"

"Naam*

" kwenye maisha hutakiwi kukata tamaa ata kama unapitia changamoto pambana mpaka mwisho usikate tamaa sawa? "

" sawa baba nimekuelewa lakini kwanini unaniambia saaahivi" aliuliza

"kwasababu nataka uwe mwenye nguvu, siku zote wenye nguvu huwa hawakati tamaa kirahisi"

"kwahiyo wale wanaokata tamaa ni dhaifu?"

"Ndio, vipi unataka kuwa dhaifu?"

"Hapana"

"vizuri kuanzia sasa nataka uwe 'strong' mwanangu ili ikifika wakati ambao mimi sioo uweze kuwalinda dada na mama yako na wale wote uwapendao*

"Nakuwaje sasa mwenye nguvu?"

"kuhusu hilo usijali mimi nipo nitakufundisha"

Hayo yalikuwa ni maongezi kati ya jimmy na Baba yake kipindi cha nyuma wakati marehemu baba yake alipokuwa hai

°°°°°°°°°°

Mara taratibu jimmy alifumbua macho yake ikionyesha ni wazi alikuwa kwenye kumbukumbu akiikumbuka siku aliyokuwa akiongea na marehemu baba yake na hakutegemea kama siku ile ingekuwa ndio siku yake ya mwisho kumuona baba yake kwenye uso wa dunia kwani siku iliyofuata baba yake alifariki kwa kupatwa na ajali mbaya.

Alinyanyuka mahali pale na kuikung'uta michanga iliyonasa kwenye nguo zake kisha alijinyoosha vizuri na kupiga miayo

"Nina njaa sasa ngoja ninunue chochote kitu angalau nipooze kidogo kabla ya kurudi nyumbani kula" alijiongelesha na kuingiza mkono mfukoni na kutoa kiasi cha pesa shillingi elfu tano kisha kuangaza huku na huko na kugundua kulikuwa hakuna wate wengi na mda ulikuwa umeenda

"ina maana nimelala mda mrefu kiasi hiki" aliongea baada ya kuangalia muda kwenye saa yake ya mkononi na kukuta ni saa mbili na nusu

"Nitasema kulikuwa na foleni kubwa" alijiambia na kuanza kuzipiga hatua kuondoka maeneo hayo.

°°°°°°°°°°

Upande wa mbezi kwenye apartment ya waishio jimmy na familia yake sebuleni alionekana mama yao akiwa peke ameketi kwenye meza ya chakula na chakula kilikuwa tayari kimeandaliwa mezani na alikuwa akiwasubiri wanae warudi waweze kula.

"Hivi hawa watoto mpaka muda huu bado hawajarudi tu" alilalama mwanamama huyo

Alichukua simu yake aina ya Samsung S22 na kufungua kisha kuingia kwenye apo ya 'contact' na kuanza kuisaka namba ya bintiye monica na alipoipata alipiga lakini aliishia kusikia sauti nyororo ikimwambia "namba unayopiga haipatikani kwa sasa* na kuishia kukunja sura

Alipoona hivyo alimpigia mwanae Jimmy na uzuri ni kwamba alikuwa hewani kwani simu ilikuwa ikiita

°°°°°°°°°°

" Twiiii twiiii twiii twi twiiii!!" simu ilikuwa ikiita kwa nguvu kama 'mic' mbovu, Ilikuwa ni kiswaswadu aina ya Tecno zile za zamani

Jimmy alipokea simu baada ya kuona ni mama yake ndiye anapiga

"Hallo ma...."

"Uko wapi?" alimkatisha na swali

"Ndo niko njiani naelekea huko nyumbani" alijibu huku mkononi alikuwa ameshika Ice cream aliyokuwa anailamba huku akiongea na simu

"Mpigie rafiki yake na dada yako umuulize monica alipo maana kwenye simu hapatikani"

"Usiniambie bado hajarudi mpaka muda huu"

"wewe umerudi?"

"lakini si ndo niko njiani"

"utajua mwenyewe fanya ujue dada yako yuko wapi mana kila siku kunitia presha tu"

"usijali nafika naye hapo nyumbani"

"eeh ndio mmefike mapema chakula kinapoa"

"sawa mama" kisha akakata simu na kumpigia simu mtu mwingine

°°°°°°°°°

Ndani ya Bar moja maarufu ya kisasa iliyoko maeneo hayohayo ya mbezi beach watu walionekana wakipata huduma yao ya ulevi, kila mmoja akiwa bize na chupa yake.

Sasa kulikuwa na mwanamke aliyeketi sehemu yake akinywa bia kwa fujo sana huku machozi yakimtoka na pembeni yake kukiwa na mwenzake ambaye alikuwa akimuangalia kwa kumuonea huruma

Wakati akiendelea kunywa kulikuwa na mziki ukilia taratibu kusindikiza huzuni yake

🎶Ila siri ya penzi, siri ya moyoS Siriya nani?🎶

🎶Siri ya chozi ni maumivu ndani kwa ndani🎶

Alinyanyuka mwanamke huyo na chupa yake ya bia lakini kwa bahati mbaya alikosa balance kutokana na kulewa hivyo kudondoka lakini hakuweza kufika chini kwani alitokea mwanaume na kumdaka

Na mwanaume huyo hakuwa mwingine bali ni jimmy

"Sara, asante kwa kunipa taarifa" jimmy alishukuru kwa moyo wa dhati kabisa akimlenga yule mwanamke aliyekuwa amekaa na alikuwa ni rafiki yake na monica

"anytime" akimaanisha muda wowote

Monica baada ya kuona aliyemzuia asidondoke ni kaka yake ndio alizidisha kulia ni kama vile jimmy amefungua maji ya bomba kwani alilia sana kiasi cha jimmy kupatwa na wasiwasi na kumgeukia Sara akitaka maelezo

Sara alimpa ishara ya kwamba amevunjwa moyo yaani mapenzi ndiyo yanayomliza

"Unajua mapenzi ni ya ajabu sana, na sijawahi kuyaelewa. Unatoa moyo wako, uaminifu wako, yaani kila kitu ili mwisho wa siku uje kulipwa na maumivu? Mapenzi ni kama mchezo flani hivi ambao sheria zake hazijawahi kueleweka

Love's a bullsh*t you know?" aliongea monica huku machozi yakimtoka

"I hear you, kila neno, maumivu yatokayo kwenye moyo wako, nayaelewa na siwezi kukaa hapa nikikuangalia tu ni lazima nimshikishe adabu huyo mpuuzi ila unapaswa kujua mapenzi ndivo yalivyo, kuna muda yankuacha na maumivu, maswali na majeraha ya moyo ambayo huchukua muda kupona

Lakini sikia.... Hutakiwi kuwa mnyonge hivi na kulialia unapaswa kujikaza. Sio mapenzi yanayokuumiza bali ni mpuuzi mmoja anacheza na hisia zako. Cha kufanya ni kusahau tu na kuanza upya you're still of worth something true" alimfariji dada yake na kumpa moyo na kwa kiasi flani alifarijika

"Nilidhani labda utaanza kunifokea na kunisema" monica aliongea

*na kweli ningekufokea sema tu muda haukuwa sahii" alijiwazia na kuishia kumpa tabasamu tu

"ata kama ningekufokea kesho ungesahau tu" aliongea na kumfanya monica atabasamu

"Twende nyumbani mama anatusubiri kwaajili ya kula" aliongea jimmy akiwa ameshaanza kupiga hatua na monica alianza kumfata kwa nyuma kama kifaranga, ungedhani labda jimmy ndio kaka mkubwa kutokana na mwili wake pamoja na urefu.

Wakati anakaribia mlango wa kutokea aligongana na mwanamke aliyekuwa akiingia kwenye bar hiyo, haikueleweka ni makusudi ama kutokuwa makini kwa mwanamke yule mpaka kugongana mabega

"Samahani dada" licha ya kosa kutokuwa lake jimmy aliomba radhi na kuuelekea mlango

"Subiri kwanza kijana unaenda wapi?" aliongea yule mwanamke

"Naondoka" jimmy alijibu lakini alipofika mlangoni aliweza kuzuiwa na mabaunsa wawili wakisimama mbele yake

Alikuwa ni aina ya wale wanawake wenye mashauzi sana, maringo meengii na kujiona wa matawi ya juu sana kiasi kwamba aliwadharau binadamu wenzake aliowaacha mbali kimaendeleo

"Si umeombwa radhi na wewe" Monica aliingilia kati ni kama vile sio yeye aliyekuwa akilia dakika chache nyuma

"Haitoshi"

"hehehe eti haitoshi, unajiona nani kwani?"

"Na wewe ni nani wa kuingilia yasiyokuhusu" aliongea mwanamke yule akisindikiza na sonyo kama la jini kabula

"kwa taarifa yako huyo ni kaka yangu hivyo yananihusu bibiye halafu inaonekana wewe ndio mwenye kosa ni wewe ndiye uliyemgonga mwenzio halafu na bado ukaombwa msamaha ety" haitoshi" screw you!

"Inatosha Monica, unatakaje ili tumalizane haraka?" jimmy alimtuliza dada yake kisha kuuliza

"piga magoti"

"Unasema?"

"Nimesema piga magoti kwani we kiziwi?" aliongea na kumfanya jimmy aachie tabasamu ambalo ni monica pekee alilielewa

TO BE CONTINUED..........

Though kuna makosa madogo ya uandishi lakini sio mbaya ninaeleweka na nitazidi kujirekebisha kadri diku zinavyozidi kusonga

Ndugu wasomaji wa simulizi za kusisimua mnikaribishe writer katika ulimwengu wenu nipate nafasi ya kuwaburudisha☺️

NB: Simulizi bado haijakamiliks inaendelea na nitakuwa nashushs kwa vipande vitatu(kipande kimoja kwa siku. J5, Alh na J'mosi)
 
Attachments

  • Screenshot_20250420-201452.png
    Screenshot_20250420-201452.png
    327.8 KB · Views: 57
BY Samuel jk_Euphoria

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 2: Friendship isn't about guarantee it's about willi

Lilikuwa ni tabasamu lenyeafsiri ya ukiburi ndani yake

"Sikia bidada, usinione mnyonge hivi ukadhani labda unaweza nipelekesha utakavyo kwanza sikujui hunijui halafu kama unaona radhi yangu haitoshi hilo si tatizo langu ni lako" Jimmy aliongea na kumpa ishara monica waondoke lakini sasa wale mabaunsa walikataa kupisha mlangoni

"Waache waende" ilisikika sauti ya kiume ikikaribia mahali hapo

Alikuwa ni mwanaume mweusi japo sioo sana ni ule weusi tunaoita maji ya kunde, alivalia suti nyeusi iliyomkaa vyema mwilini, alikuwa ni mrefu wa wastani na rika kama la Jimmy

"Naitwa Cid, samahani kwa usumbufu uliosababishwa na dada yangu mnaweza kwenda" Cid aliongea akiomba radhi kwa niaba ya dada yake

"Lakini....." hakumaliza sentensi kwa jicho alilopigwa na Cid na kuishia kufunga mdomo

Cid aliwapa ishara wale mabaunsa wawapishe Jimmy na monica na walitii bila shuruti

"Hey, mind if we become friends?" Cid aliuliza akimwambia Jimmy kama hatojali wakiwa marafiki na jimmy alitingisha mabega kama ishara kwamba hajali

Cid alitabasamu na kutoa simu mfukoni kisha kumpa jimmy aandike namba ya sjimu na hakukataa aliandika na kumrudishia simu yake kisha akaondoka akitanguliwa na monica

Muda mchache mbele Jimmy na monica waliweza kufika nyumbani na walimkuta mama yao amesinzia sebuleni, ilionekana alikuwa akiwasubiri mpaka kupitiwa na usingizi.

Baada ya kumuamsha na kula hawakuongea sana, kila mmoja alikwenda zake kulala na siku ikaishia hivyo

°°°°°°°°°°

Hatimae kukapambazuka na kuwa siku nyingine tena ya jumapili, siku hiyo Jimmy aliamka asubuhi na mapema, akifanya mazoezi ya mwili kuondoa uchovu wa asubuhi akiwa kifua wazi

Alifanya mazoezi mpaka alichoka na kukaa chini kupumzika mara alisikia mlango getini ukigongwa, of course kulikuwa na fensi.

Kwenda kufungua alikuwa ni Sara rafiki yake Monica, alikuwa amevaa akapendeza kisawasawa, gauni fupi la njano lililofunika magoti ni kama alitengenezewa yeye

"Karibu ndani" Jimmy alimkaribisha na tabasamu

"Asante" aliitikia

Licha ya Sara kuwa na urafiki na Monica kwa jimmy haikuwa hivyo, ukaribu wao ulikuwa ni ule wa salamu basi

"Ingia tu ndani utawakuta mwenzako wakimalizia"

"vipi wewe huendi kanisani?" aliulizwa

"kufanya nini?"

"kufanya Ibada na kumtukuza Mungu"

"Nitafanya nikiwa hapahapa nyumbani" Jimmy alijibu

"Sawa" aliitikia huku bado akiwa amesimama mahali pale

Ni wazi alikuwa akiutazama mwili wa jimmy na kuvutiwa na mpangilio wa six pac na kifua bila kusahau jasho ambalo liliongeza mvuto sasa sijui kama alikuwa akiisikia harufu ya jasho ama alikuwa akijisahaulisha.

Hazikupita hata dakika mbili Monica na mama yake walitoka nje wakiwa tayari wamejiandaa vya kutosha kwenda kanisani

"Msisahau kuniombea baraka na mimi"

"kama unataka baraka nenda ukaombe mwenyewe" monica kama kawaida alijibu

"Siongei na wewe kwanza naongea na hawa" aliongea huku akiwanyooshea mama yake pamoja na Sara

"Una pepo wewe sio bure"

"Mama uniombee Mwanao nipate kwenda chuo kizuri si unajua maombi ya baraka ya mzazi kwenda kwa mwanae yana nguvu" jimmy alimpuuza monica

"Nitakuombea mwanangu lakini na wewe siku moja moja uwe unaenda kanisani sawa J?"

"Oh sawa"

"mmmh!" monica aliishia kuguna tu

Tangu Jimmy ampoteze baba yake ndio ilikuwa mara yake ya mwisho kukanyaga ardbi ya kanisa lake akiwa na sababu zake binafsi.

Basi jimmy aliwaaga wanawake hao na kwenda zake ndani kujisafisha mwili na baada ya kumaliza kwa mtoko

Alivaa T-shirt ya mikono mirefu rangi ya kijivu, suruali ya kitambaa iliyofunika vifundo vya mguu ilikuwa rangi ya kijivu iliyokolea kuzidi T-shirt yake, miguuni alivaa sendo nyeusi zifahamikazo kama slides. Alipendeza kwelikweli kifupi alikuwa tafsiri halisi ya neno bishoo!

°°°°°°°°°°

Upande wa Masaki uliyopo wilaya ya kinondoni, mtaa wenye sifa ya kuwa na upepo mzuri kutokana na kwamba sehemu hiyo hupatikana karibu na bahari. Mazingira safi na makazi yake yaliyo katika mpangilio ulionyooka ulizidi kuupendesha mtaa huo

Watu wengi waishio masaki ni wale wenye uchumi mzuri yaani kipato cha kueleweka kuweza kukidhi mahitaji yao

Katika mtaa huo kulikuwa na nyumba kubwa ya kifahari yenye ghorofa mbili, ndani kulikuwa na bustani nzuri yenye kuvutia macho, mazingira safi kila kona.

Pia yalionekana magari mawili yakiwa yamepark nje moja likiwa Range roverEvoque jekundu na Mercedes A-Class jeusi, yote yakiwa ni ya kifahari

"Mkufu wangu uko wapi, we Sam mkufu wangu uko wapi?" ilikuwa ni sauti ya kike yenye lawama na hasira ndani yake

"Mi sijui bhana tangu lini ukanikuta nashobokea vitu vyako? " Cid alijibu na kutupia swali huku akitabasamu na kuzidi kumchochea hasira dada yake

Mwanamke huyo alionekana akipekua kila sehemu akiutafuta mkufu wake bila mafanikio na alienda mpaka kwenye sofa alilokaa nduguye na kumtaka ampishe kufanya upekuzi

" Ebu tulia basi unanikata ujue" aliongea Cid huku macho yake yakiwa yame'focus kwenye runinga ambayo muda huo kulikuwa na tamthilia ya kifilipino ikionyeshwa

"Utanunua mkufu mwingine bhana acha usumbu....." kabla hata Sam hajamaliza sentensi yake TV ilizimwa

"Move your ass bro! Imenigharimu kiasi cha shilling millioni thelathini kuumiliki move!" alifoka kwa hasira lakini Samson wala hakukasirika na badala yake alitabasamu tu na kuyanyuka.

"Eniwei nikatembee tembee kidogo" alijiongelesha mwenyewe na kuchukua hunguo ya Mercedes iliyokuwa kwenye meza ya kioo na kutoka zake nje

°°°°°°°°°°

Muda mchache mbele gari aina ya Mercedes ilionekana ikiegeshwa kwenye maegesho ya magari ndani ya hoteli ya nyota tano iitwayo Golden Tulip Hotel.

Ndani kabisa ya Hotel hiyo kulikuwa na sehemu maalumu ya kupumzika ni kama bar flani hivi lakini haikuwa bar licha ya kupatikana vinywaji mbalimbali

Waweza kusema ni kama sehemu ya watu mbalimbali waliofika hotelini na kukutania hapo na kuzungumza mawili matatu na kujenga urafiki au tuseme ulikuwa mfano restaurant lakini si restaurant anyway sio lazima kuelewa sana maana ata mimi nashindwa kuwaeleza wewe vuta picha tu sehemu yenye mkusanyiko wa watu.

Wengi wa watu hupendelea kuja hapo kwaajili ya kutuliza kichwa kwa kusikiliza nyimbo mbalimbali ambazo huimbwa na band tofauti tofauti kila jumapili na wenhi wao walikuwa ni wazungu na waarabu, ngozi nyeusi zilikuwa ni za kuhesabu na mmoja wao alikuwa ni Cid ambaye aliingia humo muda huo.

Na muda huo mbele ya ukumbi kwenye stage(jukwaa) ndogo kulikuwa na piano kubwa nyeusi pamoja kiti kidogo kwaajili ya mpigaji kikiwa wazi. Sekunda chache alionekana mwanaume akitembea kuelekea kwenye jukwaa dogo na kuketi kwenye kiti akiwa tayari kuwaburudisha wahusika.

Mwaanaume yule alisafisha koo na kutulia kidogo kisha taratibu kwa ustadi wa hali ya juu alianza kucheza piano.

Ulikuwa ni mtindo maarufu wa piano ufahamikao kama clair de lune

Clair de lune ni neno la kifaransa lenye maana ya moonligh kwa kingereza au mwangaza wa mwezi kwa kiswahili. Mtunzi wa mtindo huo alifahamika kwa jina la Claude debussy na aliitunga mtindo huo mnamo mwaka 1890

Ni sehemu ya mkusanyiko wa piano unaoitwa Suite Bergamasque, ambao una vipande vinne, lakini Clair de Lune ndiyo uliokuwa maarufu zaidi, Ni moja ya kazi bora za Impressionism, mtindo wa muziki ambao hujaribu kuonyesha hisia na taswira, Inaanzia na noti za taratibu, mithili ya mwanga wa mwezi unaong’aa juu ya maji, na kisha huingia kwenye sehemu yenye hisia nzito

Clair de Lune imekuwa moja ya nyimbo za piano zinazotambulika zaidi duniani, Imetumika kwenye filamu nyingi kama "Ocean’s Eleven," "Twilight," na "Atonement," mara nyingi ikiwakilisha hali ya utulivu, huzuni,, tafakari n.k

Inapendwa sana na wanamuziki wa piano kwa sababu ni ya kihisia na ya kuvutia, na ugumu wake kwenye kuicheza ambapo ni wataalamu pekee ndio huweza

Mwanaume yule alikuwa akipiga piano kwa utulivu na ustadi wa hali ya juu kiasi cha kuwashangaza watu wengi waliokuwa wakisikiliza kwani iliwavutia sana

"paah paah paah paaah" yalikuwa ni makofi kutoka kwa watu kama pongezi baada ya mziki huo kumalizika, wazungu baadhi hawakutaka unafiki na kwenda jukwaani kumpongeza mwanaume yule kwa dollars kadhaa.

Upande wa Cid alikuwa katika hali ya kumkubali mcheza piano yule na mara akakumbuka kitu na kutabasamu na palepale aliingiza mkono mfukoni na kutoa simu yake ya Iphone na kupiga

Upande wa mwanaume aliyekuwa jukwaani akijiandaa kushuka mara simu yake iliita na kama kawaida sauti ilikuwa ni ya juu.

Ile kuangalia namba ya mpigaji alikuta ni namba ngeni na kuona si mbaya akipokea, alibonyeza kitufe cha kupokelea na kuiweka sikioni

"Hello"

"unaamini kwenye bahati? nani angedhania kama tungekutana kwa mara nyingine tena" upande wa pili ulisikika na kumfanya mwanaume yule kugeuza shingo kuangalia upande wa kulia mwisho kabisa kwenye kona ndani ya ukumbu huo na aliweza muona Cid akimpungia mkono

Of course mwanaume huyo mcheza piano alikuwa ni Jimmy. Alienda moja kwa moja mpaka kwa Cid

"Bro kumbe na wewe ni mtu wa mahoteli ya maanahahaha" aliongea Cid

"Aah wapi nimepewa mualiko tu bro"

"kumbe ila umetisha sana bro yaani unacharanga piano kama Beethoven vile" (Beethoven ni mchezo piano maarufu wa miaka ya 1800s)

"Haha kawaida tu bro ni kuweka juhudi kwenye kujifunza hata wewe unaweza"

"unaonaje ukawa mwalimu wangu nimekuwa nikipenda sana kujifunza kucheza piano kwa mda mrefu"

"sidhani kama nitakuwa na mda huo"

"Usiwe na wasiwasi nitakulipa pesa nzuri tu kuhusu piano nitanunua tu" aliongea kisha kunyamanza kidogo na kuendelea "vipi si kama ile" alinyooshea piano iliyokuwa jukwaani

"Nadhani hiyo ni brand ya Bosendorfer imperial yenye keys 97 gharama yake itakuwa ni kuanzia dollar laki mbili na nusu($230,000) mpaka laki tano($500,000)"

"Duuh mpaka kujua brand na gharama yake kweli utakuwa ni mtaalamu haswa"

"vipi bro uko free?" Cid aliuliza

"Niko free nikishatoka saloon" jimmy alimwambia

"Sio mbaya nitakusindikiza, by the way bro jina lako bado silifahamu"

"Jimmy" alijitambulisha na kumpa mkono Cid (hand shake)

Baadae kidogo Jimmy na Cid waliweza kuingia saloon ambayo ilikuws ikipatikana humohumo hotelini

"Unataka kunyoa mtindo gani?" Jimmy aliulizwa na kinyozi

"Low fade" alijibu kisha kinyozi alianza kumnyoa taratibu na ndani ya dakika ishirini alimaliza na Jimmy alitokelezea haswaa na kuzidi kuwa mtanashati

"Asee bro hapo lazima mademu wakugombanie oya barber fanya na mimi uninyoe kama hivo" Cid hakuwa na mpango wa kunyoa ila ilimbidi tu anyoe isitoshe alikuwa na nywele nyingi

Dakika ishirini nyingine zilipita na Sam alomaliza kunyolewa

"Bei gani?" Cid aliuliza

"Elfu thelathini na tano (35,000) kila mmoja hivyo jumla ni elfu sabini(70,000)"

"What the f*** Yaani kinyozi cha buku unataja bei ya Almasi?" aliwaza jimmy

"Haina shida nitalipa" aliongea Cid na kufanya malipo palepale

°°°°°°°°°°

Muda mchache mbele lilionekana gari jeusi la kifahari lime-park karibu na ufukwe wa bahari na wanaume wawili wakiwa wamesimama mbele ya gari kwa kuagamia boneti la gari hilo mikononi wakishika Ice cream

"Tamu sana hizi Ice cream" Jimmy aliongea huku amefumba macho akisikilizia utamu wa Ice cream

Upande wa Cid yeye alikuwa amekaa kimya tu akilamba Ice cream yake

"Jimmy" Cid aliita

"Naam bro" aliitika

"Tembea nami kama hjtojali"

"Sure" jimmy aliungana nae kutembea pembeni ya ufukwe wa bahari

"Unajua, nimekuwa nikifikiria jambo fulani tangu tulipokutana kwenye baa. Usiku wa jana, nilikuomba tuwe marafiki, na ulikubali bila kusita. Hakukuwa na maswali, hukusita hata kidogo. kwa nini?" Cid alimuuliza

"Kwa nini isiwe hivyo?"

"Hilo siyo jibu bro. Watu wengi husita, hata kama ni kwa sekunde moja. Wanafikiria kwanza. Wewe hukufanya hivyo"

"Nadhani sioni haja ya kusita linapokuja suala rahisi kama kukubali uwepo wa mtu maishani mwangu"

"Vipi kama ningekuwa na nia mbaya? Kama nisingekuwa mtu anayestahili kuwa rafiki?"

"Kama ingekuwa hivyo, ningekuja kugundua baadae. Urafiki siyo kuhusu uhakika, ni kuhusu utayari wa kuungana," Friendship isn't about guarantee it's about willingness to connect" Kama ungenijia na nia mbaya, hilo ni juu yako, . Lakini usiku ule, sikuhisi chochote kibaya kutoka kwako. Ulikuwa tu mtu anayetafuta koneksheni"

"unaamini watu kirahisi sana basi?"

"Hapana. Nachagua tu kutoishi kwa hofu ya kile kinachoweza kwenda vibaya."

"una mtazamo wa tofauti sana"

"yeah it's the only way I know" Jimmy aliongea akimaanisha ndio njia pekee anayoijua, na wakati anaongea alichuchumaa kwani kulikuwa na kitoto cha mbwa kilichokuwa kimetelekezwa

Wakati anamshika manyoya mara Cid alimshiika bega akimshtua

"oya jimmy ona mbele hapo kuna mbwa"

"Amesimama tu, Tulia"

"Sawa lakini.... Mbona anatuangalia sana halafu kama ananguruma hivi?"

"potezea tu hawezi fanya chochote" mara ghafla mbwa huyo mweusi aina ya Doberman alianza kubweka kwa hasira na kuanza kuwafata kwa kasi kama vile ameona mwizi

"oh shit! Kimbia" jimmy alipayuka akimwambia Cid na kukiacha kitoto cha mbwa na kuchomoka nduki pasipo kujua Sam alikuwa ameshamuacha mita kumi mbele ilionekana walikuwa ni waoga wa mbwa

Uzuri gari halikuwa mbali sana hivyo walichomoka na kwenda kujifungia ndani ya Mercedes waliyokuja nayo

Hahaha Siku sio vichaa tu wanaokukimbiza bila sababu ya msingi yaani mimi ndio wa kukimbizwa na mbwa" Cid aliongea kwa masikitiko na kitendo kile huku Jimmy akibaki kucheka tu

"Haha bro kumbe we ni muoga mbwa sikutegemea ungeniacha bila ya kukushtukia"

"Kama unajiona jasiri shuka nje" Cid aliongea na kumfanya Jimmy kuchungulia dirishani na kukutana na sura ya mbwa isiyotaka masihara kabisa

TO BE CONTINUED.........
 
By Samuel jk_Euphoria

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 3: Ulinisaidia miaka miwili iliyopita

Kimya kifupi kilipita baada ya kicheko ndani ya gari hilo na Cid aliamua kuvunja ukimya

"unapaswa kujua sababu ya mimi kuomba urafiki halikuwa jambo la bahati" kauli hiyo ilimfanya jimmy amtazame Cid kwa makini

"una maana gani?"

"uliniokoa jimmy" aliongea kauli yenye utata na kumfanya jimmy amtazame kwa jicho la swali ni kama alikuwa akisema "nilikuokoa? Lini?"

"ilikuwa ni miaka miwili iliyopita, Nilipatwa na ajali mbaya niligongwa na gari kiasi cha kurushwa nisiweze hata kusimama, damu nyingi zilikuwa zikitiririka kutoka kwenye majeraha, watu walinipita tu, wengine wakiniangalia na kupiga simu bila ya kufanya chochote" Cid alinyamanza kidogo kisha aliendelea

"Lakini wewe hukupita ulinisaidia, kwa mazingira yale ambulance isingeweza kufika kwa wakati, ulinifunga majeraha kuzuia damu kisha kunibeba na kukodi bajaji kunipeleka mpaka hospitali"

"Mbona sikumbuki vizuri"

"Nadhani kwako, ulikuwa unafanya tu kilicho sahihi. Lakini kwangu… ulikuwa mtu pekee aliyeniona kama binadamu mwenzie na sio majeruhi tu" aliongea na kumfanya jimmy aanze kuvuta kumbukumbu

"oh kumbe wewe ndio yule jamaa uliyekuwa ukiendesha Duccati kwa mbwembwe barabarani na kupata ajali?" maeneo ya mikocheni sio?" hatimae aliweza kukumbuka

"Ndio ndio ni mimi"

"Sema uso wako ulikuwa unavuja damu ndio maana sikuweza kukumbuka kirahisi ila sikutegemea kama utanikumbuk9a"

"Siwezi kusahau bro, kingine Sura yako haijabadilika ni umeongezeka urefu na mwili basi"

"Oh sikutarajia mtu aliyekuwa akilala pale chini angenikumbuka" jimmy aliongea na kutabasamu kidogo

"Sitasahau siku ile, halafu nina swali..... Unajua kwa hali ile nisingeweza fika hospitali nikiwa bado hai hisia zangu zinaniambia kuna kitu ulifanya ambacho si cha kawadi" Cid aliongea

Jimmy aliishia kutingisha mabega kwamba hajui kabisa na hakufanya chochote

"Anyway sikutaka urafiki wako kwa sababu ya deni au shukrani. Nilihisi tu… mtu ambaye anaweza kufanya hivyo kwa mtu asiyemjua bila kufikiria mara mbili ni mtu wa kipekee. Na nilitaka kuwa na urafiki na mtu kama huyo, kuna ule msemo wa wazungu" a blessing in disguise" nadhani unakufaa"

"Okay bro tuachane na hii mada nina njaa fanya mpango tupate chakula kwanza halafu ndio mambo mengine yafuate" jimmy aliongea huku akipiga miayo

Cid aliwasha gari na kuliondoa mahali pale kwa mwendo wa taratibu akitafuta mgahawa wowote uliokaribu kwaajili ya ckula

°°°°°°°°°°

Mahali pasipojulikana ndani ya jiji, eneo lililokuwa limezingirwa na misitu na hakuku na dalili ya watu kuishi ama kupita maeneo hayo kulikuwa ni a fensi kubwa iliyozunguka mita za mraba elfu hamsini(50,000 meter squares)

Kulikuwa na majengo mbalimbali ndani ya hiyo fensi sasa kwenye jengo moja ndani ya chumba kilichokuwa na mwanga hafifu, hewa ilikuwa nzito na sauti za milio ya kama mapigo na pumzi nyingi zikihemwa zilisikika

Kilikuwa ni chumba cha mazoezi na walionekana watu wapatao nane walikuwa wakifanya mazoezi mazito mazito kwa usahihi kabisa

Mara mlango ulifunguliwa na kufanya watu hao kusitisha kile walichokuwa wakifanya na kuweka umakini wao kwa yule aliyeingia, alikuwa ni mwanaume mweusi mwenye mwili uliotuna kama baunsa akiwa amevalia gwanda nyeusi isizokuwa na nembo uoyote

Bila kusema neno alienda moja kwa moja kuchukua rimoti na kuwasha runinga iliyokuwa ukutani na Taarifa ya habari ya kusikitisha ilionyeshwa kwenye skrini.

Breaking news: Miili ya watu wapatao ishirini na tano imepatikana ikiwa haina uhai kwa kosa damu, mamlaka hazielewi vifo hivyo vya ghafla vimetokana na nini, polisini wanaendelea kufanya uchunguzi kwenye maeneo hayo kubaini tatizo na kukusanya ushahidi hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa vifo vya ghafla ninavyotokea usiku na miili kubaki ikiwa imekauka"

"Vifo vingine tena" aliongea mwanaume yule mweusi tii na sauti nzito kama roboti

Kundi lile la watu walitazamana wao kwa wao kila mmoja na kushusha pumzi nyingi, lilionekana jambo lile halikuwa geni machoni pao

"wale wapuuzi wanywa damu sio?" Mmoja wao mwanamke mwenye asili ya wahabeshi aliongea

"Na leo ndio mwisho wao watake wasitake" aliongea aliyeingia na gwanda ambaye ndio kiongozi wao walimuita "kamanda"

"Nadhani nyote mnajua kwanini mpo mahali hapa kwanini kundi hili lilianzishwa" aliendelea

Kimya kilifuata kisha mwingine mwanamke mwenye nywele fupi rangi ya silver(rangi ya fedha) alidakia "Yeah, by a damn half-breed. An ex-military bastard with Mysterious blood running through his veins" (Ndio yule mwanaharamu, mwanajeshi wa zamani. Chotara mwenye damu isiyo ya kawaida ndani yake) aliongea kingereza kwani alikuwa ni mzungu

"Don't forget that" bastard" saved your damn life from those blood thirsty asshol*s"(Usisahau huyo "mwanaharamu" aliyaokoa maisha yako kutoka kwa wale punda wenye kiu ya damu) alimkumbusha na kuendelea "He also saved yours too before he also saved yours too before he made you guys what you are now(aliyaokoa na yenu pia kabla ya kuwajenga kama mlivyo sasa)

"Lugha tafadhari wengine wengine hatujjaenda shule ujue" aliongea mmoja afahamikaye kwa jina la Ben

"ondoa wengine sema wewe halafu sio kama huelewi hapo" aliongea Caren muhabeshi

"kwani hujui kiswahili ndio lugha yetu ya taifa?" Ben alikazia msimamo wake kwa swali

Mwanzilishi wa kundi hili aliona kile ambacho serikali ilikataa kuona. Alipigana na kile ambacho dunia ya sasa inapinga uwepo wake, aliokoa maisha ya wengi" alinyamanza kidogo na kuwatazama kila mmoja "lakini sasa hatunaye tena lakini haimaanishi tukae tu, hapana tunakwenda vitani kumaliza kila kitu"

Chumba kilijaa ukimya wa hali ya juu na hewa kuzidi kuwa nzito, nyuso za kila mmoja zikikunjamana.

"We are........" aliongea kamanda

"HIDDEN SUPREMACY" wote walijibu kwa pamoja wakiacha sajti ikijirudia mwangwk

°°°°°°°°°°

Upande wa Jimmy na Cid baada ya kumaliza kula walitoka nje mgahawani jua likipiga kwelikweli na joto la jiji kuongezeka. na jimmy wala hakujali na zaidi alitoa pendekezo la kutembea tembea kidogo kunyoosha miguu na kusafisha macho maana alishachoka kukaa sana kwenye gari

Wakiwa wanakatiza kwenye kona za hapa na pale za mitaa yenye pilikapilika alionekana mzee mmoja ambaye alikuwa akihitaji vijana wa kumsaidia kushusha kreti za soda zilizokuwa kwenye lorry na wengi wa ma'dayworker walikuwa bize na shughuli nyingine zakuwaingizia kipato

"Kijana unahitaji pesa za haraka? Nisaidie kushusha hizi kreti za soda" aliongea yule mzee akimlenga jimmy isitoshe alikuwa akijulikana kama dayworker kwenye mtaa huo

"Zote hizo?" aliuliza huku akiliangalia lorry kampuni ya pepsi lililobeba kreti za soda na kwa hesabu za haraka haraka zilikuwa kreti si chini ya 100, kikawaida lorry size ya kati hubeba kreti 500-800

"Ndio nahitaji zote ila wewe shusha kadri uwezo wako unavyoruhusu"

"Ni bei gani mzee"

"kwa kila kreti utakayoshusha na kuingiza mule ndani ni mia mbili" aliongea yule mzee huku akimnyooshea sehemu ya kuzipeleka

"Nisubiri hapa nitamaliza haraka" Jimmy alimwambia Cid

Cid alitingisha kichwa na kwenda kujiegamiza pembeni kwenye ukuta huku akikunja mikono yake kama boss flani hivi

Jimmy alikwenda mpaka kwenye lorry la kreti kisha alinyoosha shingo kwa kuikunja kulia na kushoto kisha alipandisha mikono ya shati kisawasawa na kuanza kazi mdogomdogo

Nusu saa mbele alikuwa amebeba kreti mia tatu na ushee na hakuonyesha dalili ya kuchoka ndio kwanza anachangamka

"Hujachoka tu?" Cid aliuliza

"Vp unataka kunisaidia? Karibu" Jimmy alimkaribisha kupiga mishe za ki'dayworker mtoto wa kishua

"Juhudi nyingi sana lakini maokoto ni kidogo kuliko ulivyojituma"

"Watoto wa kishua hamuwezi elewa, hakuna anayependa kufanya kazi ngumu lakini ni bora kuliko kutofanya chochote Isitoshe nahitaji maokoto"

"ungekuwa nazo za kutosha vipi ungeendelea kufanya kazi ngumu?" Cid aliuliza

"Ndio, kama ni jambo la maana nitajiuma vya kutosha isitoshe hapa nilipo nafanya la maana, kuhangaika kwangu angalau napata pesa ya kukidhi mahitaji yangu na familia yangu" aliongea huku akitabasamu

Cid bila kuongeza neno naye alikunja mikono ya shati lake na kuungana na Jimmy kubeba kreti "Can't let you take all the glory"(Siwezi kukuacha ukibeba utukufu peke yakok alitabasamu

Lisaa likapita na hatimae waliweza kumaliza kushusha kreti zote zikiwa jumla mia saba hamsini(750), Cid akibeba kreti 80 tu lakini alikuwa hoi bin taaban kuliko hata Juimmy na jua lilivyokali waliloa jasho kana kwamba wametoka kubatizwa kwa mwamposa

"Asee vijana mna nguvu sana na ni wachapa kazi" mzee alisifia na mkononi alishika pesa noti nyekundu na kilikuwa ni kiasi cha shillingi lakini moja na nusu

"kama tulivyokubaliana kijana ila sikutegemea kijana kama mdogo kama wewe kuweza kubeba kreti nyingi kiasi hiko" aliongea akimpatia pesa zile jimmy na alizipokea kiroho safi

Alichomoa elfu hamsini na kumpatia Cid "Gawio lako" lakini Cid alitingisha kichwa kukataa na kumwambia abaki nazo tu isitoshe alifanya kusaidia sehemu ndogo tu

°°°°°°°°°°

Usiku wa saa moja Jimmy alionekana akifungua geti na kuingia ndani akitoka kuzurura siku nzima na rafiki yake mpya, alienda moja kwa moja mpaka kwenye apartment yao na kuingia ndani na mkononi alikuwa ameshika mfuko mweupe wanye chata la KFC

Aliwakuta mama yake na dada yake wakiwa bize kufuatilia tamthilia ya kihindi kwenye runinga na aliwapa salamu na kuweka mfuko kwenye meza ndogo iliyoko sebleni hapo

Ile Harufu tu ya kuku wa Kfc ilitosha kumvuruga monica ambaye alikuwa makini kufuatilia tamthilia ile. Macho yake yalitua kwenye mfuko ambao harufu yenye kuisumbua pua yake inatokea

"Nimewaletea zawadi warembo wangu" aliongea jimmy kwa bashasha

Monica kusikia vile ni kama amepewa kibali cha kuvamia mfuko ule kwani slienda moja kwa moja na kutoa viboxi vidogo vidogo jumla vikiwa sita, viwili vikiwa na chipsi, viwili kuku wa kukaanga na viwili vingine vikiwa na kuku wa kuchoma

"Kuleni mshibe tena mmalize kabisa msijali kuhusu mimi nimeshakula na nimeshiba" aliongea jimmy na kuwaaga zake anaenda kulala na waliishia kumshukuru na kumtakia usiku mwema na siku ikaishia hivyo

°°°°°°°°°°

Ikawa siku nyingine tena, siku ya jumatatu siku ambayo haipendwi na watu wengi miongoni mwao wakiwa ni vijana hasa wanafunzi, usiniulize kwanini maana hata mimi sijui licha ya kutoipenda hii siku ya juma

Siku hiyo kama kawaida Jimmy alikuwa amelala fofofo muda huo wa saa mbili asubuhi mara ghafla simu yake iliita na kumuharibia usingizi wake, alipoangalia namba ya mpigaji aliishia kutingisha kichwa kwa masikitiko

"Huyu jamaa anataka nini asubuhi-asubuhi" alijiongelesha huku akijpokea simu na kuiweka sikioni

"Toka nje bro" Ilisikikika sauti kutoka upande wa pili bila hata salamu

"Nitoke nje kufanya nini kaka saizi bado hakujakucha"

"Oh habari za asubuhi aya toka nje bro" alimpa salamu ya asubuhi kama kielelezo cha kwamba kumekucha

Jimmy alijinyanyua kivivu kutoka kitandani na kwenda dirishani kuchungulia nje na alishuhudia gari la kifahari Aston martin DB12 jeupeee kama theluji likiwa limepark nje tena ndani ya apartment
Ni gari la kifahari linalogharimu $269,000 sawa na millioni mia saba za kitanzania

"Bro who did you rob?" akimaanisha hilo gari amemuibia nani

"Haha ebu toka nje bro ninaangaliwa sana kama jambazi"

Ni kweli raia waliokuwa wakiishi kwenye apartment hiyo walikuwa wakikodolea macho gari hilo n zaidi ni mwenye gari na kujiuliza amekuja kufanya nini wengine walienda mbali kwa kuwaza labda anataka anunue eneo hilo

Jimmy alinawa uso haraka haraka alivaa vest nyeusi akibaki na kaptura ileile aliyolala nayo, alichukua mswaki na kuweka mdogo kisha mdogomdogo mpa nje

"Unalala sana bro nilitegemea kukukuta upo macho" aliongea Cid lakini Jimmy alimpuuza na kuelekea gari alilokuja nalo na kuanza kulitazama kutoa ushamba

"Unaendesha hili sio?" jimmy aliuliza

"Yeah" Cid alijibu

"Tunaenda wapi?"

"Umesahau? Tunakwenda kununua Piano then uanze kunifundisha leoleo" aliongea na kufanya majirani kumshangaa

"Jimmy anacheza piano? Mbona ya leo kali" mmoja wa majirani alinong'ona maana Jimmy wanayemjua wao ni mpenda kulala sana na mvivu
Mara monica na mama yake walitoka nje pia

"Oh kumbe mnaishi pamoja" Cid alishangaa alipomuona monica

"Huyo ni dada yangu bro"

"Kumbe mi nilidhani labda........." aliongea na kuacha sentensi iende hewani

"Uliwaza mbali sana bro kama nilivyosema huyo ni dada yangu"

"Sio mbaya eneweii nichukue nafasi hii kujitambulisha tena, naitwa...."

"Cid si ndio?" Monica alimalizia sentensi yake

"Ndio ndio ni furaha kwangu kukumbukwa jina na mtu ambaye tulikutana kwa bahati" alifurahi meno yote yakiwa nje

"Na huyu hapa ni mama yngu mzazi, mama huyu ni rafiki yangu" Jimmy alifanya utambulisho

"Oh shikamoo mama" Cid alimsalimia mama yake jimmy

"Marahaba mwanangu hujambo"

"Sijambo kabisa mama, unajua mwanao ni mtaalamu sana likija suala la kucheza piano" aliongea na kumfanya Monica kuangua kicheko kile kicheko cha umbea na Jimmy kuona hivyo alitoka hapo na kuelekea ndani huku aki-brush meno yake kwa mwaki

"wapi bro? "

"Naenda kujiandaa sikawii sana"

"Unasema Jimmy anajua kucheza piano?" mama yake aliuliza

"Ndio mama au ulikuwa hujui?" Cid alishangazwa kidogo

"Pengine ni siri yake, vijana mna siri nyingi ambazo wakubwa zenu hatujui au nasema uongo?" mama yake jimmy alisema

"Hujakosea mama sisi vijana huwa tuna mambo mengi sana"

"Ni kweli, aya karibu ndani usisimame tu hapo mgeni kuishia nje haipendezi au nasema uongo mwanangu?"

"Haha wasema lakini sikai sana nimekuja kumpitia Jimmy kuna mahali tumepanga kwenda"

"Sawa karibu ndani"

"We Bianca njoo usalimie wakubwa" jimmy aliita na kioo cha gari siti ya abiria kilishuka

TO BE CONTINUED..........
 
BY Samuel jk_Euphoria

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 4: Moonlight sonata

"Usiishie kuchungulia tu shuka umsalimie bimkubwa"

Mlango wa gari ulifunguliwa na alishuka Binti aliyevalia gauni jeupe fupi lililofinka magoti na kuchora umbo lake namba nane sijui sita vuta picha inavyokupendeza ndugu msomaji,, rangi yake ya ngozi ambayo ni nyeupe ilimfanya kuvutia zaaidi, alikuwa ni mrefu wa wastani na nywele zake zilikuwa fupi lainiii, kifupi ni kwamba mwanamke huyo alikuwa ni zaidi ya urembo wenyewe achilia mbali dada zetu wenye nyashi kama viroba vya mpunga

Majirani hasa wanaume walikuwa wakimuangalia kwa macho yaliyojaa uchu Kulikuwa na mbaba mmoja mwenye kitambi akitoka ndani ya chumba chake almanusura ajikwae ni kama vile amemuona malaika

"Huyu ni Bianca mdogo wangu alikuwa akinisindikiza, Salimia" alimtambulisha na kumtaka asalimie

"Shikamoo" Bianca alisalimia, alikuwa ni wale mabinti wenye aibu mbele za watu na idadi ya majirani walioko nje wakimtazama ilichangia.

"Marahaba mwanangu karibu ndani" mama yake Jimmy na monica alimkaribisha na alikubali na kuingia ndani akifuatwa na Cid

Upande wa Jimmy alikuwa akimalizia kupulizia unyunyu na alikuwa amevaa kikawaida sana, T-sheti oversize rangi ya damu ya mzee na suruali nyeusi aina ya Cargo pants.

Alibeba slides zake nyeusi akipanga kuzivalia nje na kutoka zake chumbani kuelekea sebuleni.
Ile anafika sebleni tu macho yake yalitua kwenye kochi lililokaribu na dirisha, aliketi binti asiyemfahamu lakini alivutia macho kwa kumtazama, alikuwa akigeuzageuza shingo akitalii baadhi ya vitu vilivyopo sebuleni kwa utulivu, mwanga hafifu wa jua ulimmulika ngozi yake na kufanya ing'ae kama dhahabu, Jimmy ni kama vile alikuwa kwenye ndoto ambayo hakutaka iishe

Binti yule mara alihisi kuna mtu akimwangalia na alikuwa sahihi kwani alipogeuza shingo hisia zake zilikomuelekeza alikutanisha macho na Jimmy

Jimmy alitoa tabasamu hafifu na kupotezea na kusogea zaidi sebuleni na kumkuta Cid pia akiwa ameketi kwenye kochi
Cid baada ya kumuona jimmy alianza kuongea

"Ndo ushajiandaa? tuondoke sasa na huyu ni mdogo wangu anaitwa Bianca anatusindikiza, Bianca huyu ni rafiki yangu mpya anaitwa Jimmy" alichukua nafasi hiyo kufanya utambulisho

"Ni jambo zuri kukufahamu" Jimmy aliongea pasipo kujibiwa

"Nimesahau kukwambia anashida ya usikivu hivyo ongea naye ukiwa karibu na taratibu" Cid alimueleza

"oh sawa" Jimmy alitingisha kichwa na kumsogelea karibu

"Nimefurahi kukufahamu" alimpa mkono Bianca, na binti huyo hakuongea na badala yalitingisha kichwa kirafiki na kutabasamu kisha aliupokea mkono wa jimmy

"Tuondoke" aliongea Cid

"Subirini kwanza mpate kifungua kinywa kabla hamjaondoka" Aliongea bi mkubwa akiwa ameshika sahani iliyojaa chapati za mayai zikiwa zimetoka jikoni muda si mrefu

"Kwaleo utatusamehe tu mama tumeshiba, tulikula kabla ya kufika hapa ila usiwaze sana siku nyingine tutakuja pia" Cid alijieleza

"Sawa basi vipi na wewe Jimmy utakula kabla ya kuondoka?" alimuuliza Jimmy

"Niwekee kwenye bakuli nitakula njiani" Jimmy aliongea hakutaka kuondoka bila kula kitu na mama yake alichukua kibakuli vile vya mviringo vya kuhifadhia chakula na kuweka chapati za kutosha kisha kufunika na kumpatia

Baada ya hapo waliaga na kuondoka, kwenye gari Jimmy aliketi siti ya nyuma na mbele walikaa Cid na Bianca dereva akiwa Cid
Njiani gari likiwa kwenye mwendo wa wastani huku ngoma ya "Shake it off" ya mwanamziki wa kimarekani Taylor Swift ikidunda na upande wa Jimmy alikuwa bize na chapati zake akitingishwa kichwa kuendana beats

Wakiwa njiani jimmy aligundua kuwa kuna gari mbili aina za land rover defender zilikuwa zikiwaunga mkia tangu watoke kwao

"Hey Cid"

"Naam bro"

"Tunafuatiliwa" Jimmy alimwambia na kumfanya Cid aachie tabasamu

"ondoa wasiwasi hao ni walinzi wetu sikutaka waingie kule kwenu ili kutoleta attention na minong'ono isiyo na maana"

"Walinzi? unataka kusema?"

"Nadhani ni wakati sahihi wa kujitambulisha vizuri kifupi ni kwamba familia yetu ni familia yenye maadui wengi na ndio maana tunalindwa"

"ooh kumbe mbona jana sikuona ukiongozana na hao walinzi?"

"Sikutaka waongozane nami bro ni vile tu nipo na Bianca hapa ndio maana wapo nasi isitoshe ni mtoto wa kike na anahitaji ulinzi zaidi, ila inashangaza umeweza kugundua kama tunafuatiliwa, bro inaonekana upo makini sana"

"Umakini ni jambo muhimu sana mwanaume hupaswi kukaa kiholela holela hata hivyo mtu yeyote angeweza kugundua maana kila kona tunayokata wapo nyuma yetu"

"Hahaha ni kweli bro nilipanga kuja mwenyewe ila kwasababu ya Bianca kuambatana nami wamekataa kutuacha hata hivyo sio mimi ninayewalipa" alimwelezea na Jimmy hakujali sana kuhusu hilo na alibadilisha mada

" Unakwenda kununua piano kweli bro? Mi nilijua unatania"

"Nitanie wapi bro nilikuwa namaanisha"

Muda mchache mbele waliweza kufika kwenye shopping mall kubwa ya kisasa ipatikanayo mjini na gari lilikwenda kupark kwenye sehemu maalumu ya kuegeshea magari.

Ila wanashuka tu walikutana na walinzi sita waliojazia miili yao wakivaa suti wamejipanga ipasavyo kutoa ulinzi na kwa mara ya kwanza Jimmy alijiona kama Don flani hivi mwenye heshima kwa kuzungukwa na walinzi pembe zote nne za dunia

Shopping mall waliyofikia ilikuwa ni ile yenye hadhi ya juu mno, ilikuwa ni shopping mall yenye ghorofa tano kwenda hewani ghorofa la vioo. Na, floor ya chini kabisa ilikuwa ni ya vyombo vya muziki vya kila aina, kuhusu floor zinazofuata hio ni habari nyingine

Waliongozana mpaka ndani kisha Bianca na walinzi wote sita walipandisha juu wakiwaacha Jimmy na Cid chini kwanza Cid hakutaka habari za kufuatana na walinzi kama kumbikumbi kingine wlinzi wataonekana wambea alitaka 'privacy' kidogo

Jimmy na Cid walienda mpaka sehemu ambayo piano hupatikana, kulikuwa na mbalimbali za piano, kulikuwa na piano kubwa(Grand piano) zile ambazo hutumika kwenye maonyesho makubwa na zinatoa sauti ya juu na ni bora zaidi ni kama ile Bosendorfer aliyokuwa akiitumia jimmy kule hotelini, pia kulikuwa na piano za kidijitali ambazo hazikutumia nyaya na hutumiwa kuonganisha vifaa vya muziki vya kielektroniki na mara nyingi hutumiwa studio kutengeneza album, na aina nyingine nyingi

"Karibuni wateja wa nguvu" muhudumu wa kike wa eneo lile aliwachangamkia kwa bashasha na kuwatembeza akiwaonyesha na kutoa maelezo kuhusu piano mbalimbali

"Bro ipi inafaa kwa kutumia nikiwa nyumbani na i bora zaidi?" Cid aliuliza kama vile hakukuwa muhudumu

"Hio si kazi yangu unapaswa kumuuliza muuzaji"

"Miimi nataka maelezo kutoka kwako mtaalamu unadhani nimekuleta uje ushangae? "

"Kwa wewe unayeanza kabisa nadhani hii itakufa" aliongea Jimmy akinyooshea mkono moja ya piano zile za mbao zinazotumia kamba kutoa sauti

"Kwanini hiyo na si zingine? " Ciid aliuliza akitaka maelezo zaidi

"Kwasababu hii ni Bösendorfer 155, sababu ya kiuitwa 155 ni kwa sababu ina urefu wa sentimita 155 sawa na futi tano, Imetengenezwa kwa mbao imara ya spruce, ambayo huongeza usambazaji wa sauti na kutoa sauti ya kipekee kingine ni Inatumia mfumo wa single-stringing, ambapo kila nyuzi ina pini yake ya kushikilia, jambo linalosaidia katika kudumu kwa mlio wa sauti na mwisho kabisa ni "made in Austria" Alimuelezea kwa kifupi na muhudumu alikubaliana kwani alichosema ni sahihi kabisa

"Nadhani kwa maelezo yako inanifaa kabisa haha inaonekana unajua vizurii kuhusu piano vipi kuhusu bei?"

"Bei hubadilika kila nyakati hivyo ni vyema kumuuuliza muuzaji" aliongea akimgeukia muhudumu

"Hili ni toleo la mwaka huu kabisa na kama alivyosema huyu kaka imetengenezwa kwa mbao imara ya spruce hivyo kufanya iwe ghali kidogo" aliongea muhudumu yule

"Wewe taja bei usiwe na shaka hii lazima niinunue" Cid alimtoa wasiwasi

"Ni dollar elfu themanini na tano thamani sawa na shillingi millioni mia mbili ishirini na nne"

"Nitanunua" Cid alijibu bila wasiwasi na kumfanya Jimmy ameze mate kama vile hayataki kupita kooni na aliishia kujiambia ingakuwa yeye hata awe tajiri kiasi gani haweza nunua piano kwa bei kichaa namna hio labda gari

Palepale muhudumu alitoa kifaa cha kielektroniki cha kulipia kwa kadi ya benki akisubiri malipo na Cid alitoa kadi nyeusi ya benki na kuipitisha kufanya malipo

Kwa wale msiojua kadi nyeusi ni kadi za benki ambazo hutolewa na taaisi za kifedha kwa watu matajiri zaidi UHNWIs(Ultra High Net Worth Indibiduals), Ni kadi ambayo huwezi pata hivihivi tu hutolewa kwa mwaliko tu kwa wale waliokishk vigezo vya kifedha vya juu mabillionea, wafanya biashara wakubwa, viongozi wenye maokoto ya uhakika n.k

Vigezo hivyo ni kuwa na kiasi kingi cha pesa na kutokuwa na kikomo cha matumizi unatakiwa kutumia zaidi ya billioni moja kila mwaka. Jimmy hakuwa mshamba kivile na aliweza kuigundua na kujiuliza huyu rafiki yake itakuwa anatoka kwenye familia kubwa inayotambulika nchini na palepale mawazo ya kumchuna pesa mbili tatu yalianza kumjia

"Asante sana unakaribishwa tena muda wowote kununua nidhaa pia tunasafirisha bidhaa mpaka mahali unapohitaji bure kabisa unachopaswa ni kutupa anwani ya unapotaka ifikishwe" aliongea muhudumu na Cid alimpatia address ya anapoishi na mara moja muhudumu yule alianza mchakato wa kusafirisha bidhaa hiyo

"Vipi naruhusiwaku cheza piano kidogo? " Jimmy aliuliza

"Ndio unaweza isitoshe hakuna wateja eneo hili" alimruhusu

Jimmy alinyoosha vidole vyake vizuri kiasi cha kutoa mlio na kuketi kwenye kistuli maalumu cha wacheza piano na kuanza kubonyeza taratibu kwa ustadi

Awamu hii ulikuwa ni mtindo tofauti na aliocheza mara ya kwanza, ulikuwa ni wa tofauti ni mtindo maarufu ufahamikao kama Moonlight sonata ambao mwanzilishi wake alikuwa ni Ludwig van beethoven mcheza piano maarufu wa miaka ya 1800s

Ni mtindo ambao huwakilisha hali ya huzuni na inasemekana beethoven alitunga mtindo huu wakati akiwa anaanza kupoteza uwezo wake wa kusikia na kujikatia yamaa, ni mtindo unaoelezea hisia za huzuni, ina sehemu tatu sehemu ya kwanza ni ile ya taratibu ya pili ni ile ya kawaida na ya mwisho ni ya haraka na kipekee sana

Sasa Jimmy alikuwa akicheza sehemu ya kwanza ya taratibu huku akiimba kufuatana na mziki huo

🎶In the silence I walk alone🎶

🎶Under the skies that are yet unknown🎶

🎶A story untold, a heart unknown🎶

🎶I search the truth in the shadows I have grown🎶.....

Alinyamanza baada ya kuhisi ongezeko la watu eneo hilo maana aliweka umakini kwenye piano

"Mbona umeacha sasa unapaswa kuendelea mpaka mwisho huku ni kukatana stimu bhana" Cid alitoa lawama
Japokuwa urafiki wao ni.wa siku mbili ila walionekana ni kama marafiki wa siku nyingi sana

Jimmy aliishia kutoa tabasamu tu na kumwambia hakuwa akitumbuiza bali alikuwa akijaribu kuona ubora wa sauti.

Kwa watu walioongezeka walikuwa ni wahudumu wa floor hiyo jumla wakiwa sita, Bianca pamoja na msafara wa walinzi, haikueleweka walifika hapo muda gani, na aliweza kumsikia Jimmy mwanzo mpaka alipoishia, unapaswa kuelewa kwamba licha ya Bianca kuwa na shida ya usikuvu haikumaanisha ni kiziwi, hapana, ni kama mfano wa bendera ipeperukayo kutokana na upepo kuwa mkali lakini inaacha kupeperuka upepo ukiwa mdogo ndivyo ilivyo kwa Bianca kuna muda masikio yanakuwa yanasikia vizuri na mda mwingine yanagoma katakata

Kwahiyo hapo alisikia vyema na kuvutiwa na mtindo huo licha ya kutokuonyesha waziwazi.
Kwa nje ya mall hiyo kupitia vioo Jimmy aliweza kuona gari la Toyota Alpha jeusi likipiga breki ya nguvu na walishuka watu kadhaa wamefunika nyuso zao kwa kuvaa vinjago mikononi wakishika siraha za moto aina ya M16 na palepale akili yake ilimuambia kuna ujambazi unaenda kufanyika

"Laleni chini!" Jimmy alipiga kelele na kuwarukia Cid na Bianca wakilala chini na kwenda kujificha chini nyuma ya Piano

Walinzi now walikuwa 'alert' muda wote na kujikinga lakini haikueleweka kwanini hawakuweza kugundua hatari hiyo mapema, upande wa wahudumu walikuwa wamechelewa sana kwani risasi zilianza kumwagwa kwa fujo bila huruma na kuondoka na maisho yao(wapumzike kwa amani)

Basi yalikuwa ni majibizano ya risasi kutoka pande mbili upande wa walinzi na upande wa majambazi hao

"Hawa wapumbavu wanapata wapi ujasiri wa kufanya ukatili namna hii mchana kweupe, Shenzi!" mlinzi mmoja alimaka

"Kuwatusi haitasaidia kitu fanya kuwasiliana na polisi hatuwezi kumalizana nao wote hawa pasipo kuhatarisha maisha ya raia wengine" mwingine aliongea

"Shaw fanya mawasiliano sasahivi" Kiongozi wa walinzi alitoa amri

"Sawa mkuu.... Aarggh" alipiga ukelele wa maumivu baada ya risasi kupenya kwenye mbao kuutoboa mguu

Upande wa Jimmy, Cid na Bianca walikuwa wamejificha nyuma ya piano kubwa yenye mbao nene isiyoruhusu risasi kupenya kirahisi, Bianca alikuwa amepaniki na kutetemeka kwa woga mara baada ya kushuhudia maisha ya binadamu wenzake yakiondoshwa mbele ya macho yake, hakika hambo hilo lilimuogopesha sana na machozi yalianza kumtoka kama mfereji kibaya zaidi harufu ya damu ilimtia kichefuchefu, alikuwa akiogopa kupoteza maisha yake angali akiwa mdogo ndio kwanza alioka kutimiza miaka ishirini wiki chache zilizopita na anatarajia Kuanza Chuo mwezi ujao

Upande wa Jimmy aliishia kusikitika na kufanya ishara ya msalaba kama mapope wafanyabyo wakiaga maiti, ilionekana haikuwa mara yake ya kwanza kushuhudia binadamu akikata roho mbele ya macho yake. Cid naye hakuwa ametulia alikuwa akiwatukana matusi ya kila aina majambazi hao alienda mbali kwa kuwaita majina ya ajabu ajabu ambayo hayakuwa kusikika ulimwenguni, lakini sasa wangemsikia?

"Tukiendelea kuzubaa hapa tunakwenda kuitwa marehemu" aliongea Jimmy kwani risasi zilizidi kutoboa mbao mdogomdogo na suala la muda tu kuweza kupenya

"Tunafanyaje bro una mpango wowote?" Cid aliuliza akiwa hayupo tayari kufa na kumfanya jimmy aangalie huku na huko kutafuta kitu na palepale alitoa tabasamu

TO BE CONTINUED..........
 
BY Ssmuel jk_Euphoria

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 5: "Hivi unajua maisha yana thamani gani"

Alitabasamu mara baada ya kuona kitu kama ngao flani hivi ya chuma umbo la mstatili, na palepale alivua Slides zake nakubaki peku.

"unataka kufanya nini?" Cid aliuliza

"Unataka kufa?" naye badala ya kujibu alimtupia swali

"Hapana" Cid alijibu

"Tulia sasa, kama sikosei wanatumia silaha ya M16 na kila magazini inabeba risasi thelathini nadhani mda si mrefu zinakwenda kuisha lakini hatupaswi kusubiri nani anajua labda wamebeba magazini zingine?" Jimmy alifafanua ilionekana alikuwa amepiga mahesabu ya kimya kimya

"Halafu inaonekana wanalenga kumuua mtu" aliendelea na Cid aliishia kutoa ishara ya "Sio mimi"

"Kama sio nyinyi ni nani si umesema familia yako ina maadui wengi au unaniona fala sio?" jimmy aliwaza kichwani mwake

Mara mlio wa risasi ukakoma na jimmy haraka alitambaa kwa kulala kutumia vifuti na magoti kama mwanajeshi akihama upande mwingine aliokusudia na mara baada ya kujiegamiza kwenye piano nyingine risasi zilianza kurindima tena safari hii zikielekea upande wa jimmy peke yake

"Rafiki yako ni kichaa" Bianca kwa mara ya kwanza aliongea tangu wafike hapo maana hata walinzi wenyewe licha ya kuwa na siraha hakuna aliethubutu kutoka pale alipo, vipi kuhusu jimmy? hakuwa na siraha yoyote ni ujasiri ulioje!

"Nadhani ana mpango"

Upande wa jimmy alishika ipasavyo ngao ya chuma iliyokuwa pembeni yake na kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha, ghafla kwa spidi alichomoka pale alipo akielekea upande wa majambazi wale akijinga na ngao ya chuma

"Bang! Bang! Bang! Bang!" mlio wa risasi na ngao ya chuma ulisikika na mlio wa sirasi ukakoma magazini zimeisha risasi na Jimmy hakutaka kuwapa nafasi pengine labda wana magazini nyingine, na kwa nguvu aliirusha ngao kumlenga mmoja wa wale majambazi kwenye shingo na alikuwa na shabahi, ngao ililenga kichwa kisawasawa na jitu kuanguka chini kama furushi akipoteza fahamu

"Shit! Huyu mshenzi inaonekana ana mafunzo" Kiongozi wao alimaka kwa hasira baada ya kushuhudia tukio hilo na idadi yao kupungua wakibaki watatu kwani jumla walikuwa wanne na mmoja ndio alikuwa amezimia

"Tumeishiwa risasi" mwingine aliongea

"Damn!"

Kwakuwa waliishiwa na risasi Kwenye M16 zao ni Kiongozi wao pekee alikuwa na "back-up plan" nayo ni bastola na wakati anachomoa na kuikoki Jimmy huyu hapa mbele yake

Anakuja kushtuka bastola haipo mikononi mwake ni kitendo cha haraka sana

"Paah! Paah! Paah! Paah! Paah! " Zilipigwa risasi tano Tatu kila moja ilitua kwenye kila goti la majambazi hao wakipiga kelele za maumivu na mbili zilitua kwenye matairi ya gari walilokuja nalo

"Si unaona ninsi inavyouma lakini hayo maumivu hayatoshi kufidia vifo mlivyovisabisha" Jimmy aliongea akimlenga kiongozi wao kwenye paji la uso

"Niue tu hata hivyo maisha hayana umuhimu sana" alifumba macho akiwa tayari kufa

"kwako wewe na hawa wapuuzi wenzako labda vipi kuhusu wale waliokufa kwa mikono yenu? Mliwauliza kama kuishi kwao ni muhimu ama lah? Hivi unajua maisha yana thamani gani? Baba anahangaika kila siku kwaajili ya familia yake, mama anapambana na ku'save kila senti kwaajili ya maisha bora ya baadae kwa bintiye, hao wadada mliowaua ni binti za watu pia pengine hata wao wana familia zao ambazo zinawategemea na wanawasubiri halafu unaniambia kuishi hakuna umuhimu? Wewe ni mpumbavu haswaa na katika wapumbavu niliobahatika kukutana nao nakupa namba tatu" Jimmy aliongea maneno hayo

"lakini mwisho wa siku kifo ni sehemu ya maisha yao kitawakuta tu"

"Hayo maneno nenda kamwambie mama ambaye ametoka kujifungua kwa uchungu na kumshika mtoto wake mchanga kwa mara ya kwanza, kwa mwanajeshi aliyetoka vitani salama kurudi nyumbani, kwa mtu ambaye amepoteza kila kitu lakini akapata sababu ya kusimama tena uone jinsi ulivyo mpumbavu" jimmy aliongea na kumsogelea karibu akichuchumaa na kuendelea

"Maisha hayana thamani kwasababu tunakufa ni kwa....... Kwanza sitaki kupoteza muda kumuelewesha mpimbavu ambaye mwisho wa siku bado anang'ang'ania upumbavu wake na juhudi zangu kwenda bure" kisha alisimama

"Mwisho wa siku na ngojera zako zote lumeshika bastola kutekeleza mauaji" alicheka yule kiongozi

"Unakosea we mpumbavu na siku ukijua ya kuwa wewe ni mpumbavu na kwanini unaitwa mpumbavi basi kumbuka kati ya wale waliokuita mpumbavu mimi ni mmoja kati yao niliyekuita mpumbavu kwa hekima sana ili upate kujitambua kwamba wewe ni mpumbavu" aliongea na kumuongozea risasi ya goti jingine

"Aaarggghh" alipiga kelele kiasi kwamba sauti ilianza kufifia

"Shh shh sshhh!" jimmy alimpa ishara ya kunyamanza

"Mimi sio muuaji" alivyomaliza kutoa kauli hiyo Cid alitoka mafichoni pamoja na Bianca na walinzi wake

"Nyie washenzi mmenisababishia hasara" Cid aliwasogelea na kuwatandika mateke kwa hasira kila neno moja alilisindikiza na teke

Hasara anayozungumzia ni kuhusu piano yake mpya ambayo hata hakuigusa iliharibiwa kisawasawa na matobo ya risasi, karibia vinanda(piano) vyote viliharibiwa na risasi

"Bro wewe ni jasusi?" Cid aliuliza kwa wasiwasi

"Hapana ondoa shaka nilibahatika tu kupitia mafunzo mbalimbali" aliongea ukweli

"Kumbe ulipita jeshini!"

"Sio jeshini ni mzee mmoja myahudi alinifunza mbinu mbalimbali za kujilinda kama shukrani" hakuona haja ya kuficha

"Usiniambie bongo kuna myahudi"

"Kwanini isiwezekane bro mbona kuna wachina wazungu, waarabu halafu akosekane myahudi?"

Kwa jinsi wanavyoongea ni kama vile hakuna kitu kilichotokea Isipokuwa kwa mrembo Bianca ambaye bado alikuwa na hofu licha ya yote kuisha pengine ilikuwa ni mara yake ya kwanza kushuhudia uhai wa watu ukimtoka mbele ya macho yake

Jimmy alimfata Bianca na kumsogelea karibu kabisa akimshika mabega yote mawili "Usiogope kila kitu kimepita sawa? na ni jambo la kushukuru upo salama pamoja na kaka yako kuhusu wengine ni ajali imetokea hivyo tunapaswa kusahau" aliongea kwa sauti ya upole akimtuliza

Mara Bianca alianza kulia tena safari hii akitoa sauti, ni kwasababu ya hatia aliyoihisi moyoni, dada za watu wamekufa kwasababu yao, haikuwa mara ya kwanza kutaka kuuwawa maana alishatekwa sana ila siku hiyo ya watu kuuliwa mbele yake wasiokuwa na hatia na maadui katika familia yake, alijiambia pengine wasingekuja hapo wangekuwa salama na kuendelea kuishi

Ilimbidi kaka mtu aende mwenyewe na kwenda pembeni kumtuliza, Bianca alikuwa ni kama mtoto mdogo tu licha ya umri wake. Madhara ya kudekezwa kupindukia hayo.

Walinzi wale sita mmoja akisaidiwa kusimama kwa kushikwa bega kutokana na mguu wake mmoja kujeruhiwa na risasi

"Wewe ni nani?" kiongozi wa walinzi aitwaye Abdul alimuuliza jimmy

"Nani mimi? Naitwa jimmy wakuu ni rafiki mpya wa....." akimnyooshea kidole Cid aliyekuwa pembeni akidili na Bianca

"Haiwezekani sisi wenye siraha na mafunzo tushindwe kudili ni hawa panya lakini wewe umeweza kuzizima hizi panya nne zenye siraha...... wewe ni nani?"

"Kama nilivyosema mimi ni Jimmy hamjaelewa wapi wakuu"

"Kuna kitu anatuficha huyu isije kuwa ana mpango wake wa siri kwa bwana mdogo" aliongea Shaw akimwita Cid kama "Bwana mdogo"

"Nafsi yangu inaniambia huyu ni jasusi" alidakia mwingine

"Mnawaza mbali wakuu mimi ni raia mwema nilichofanya ni kuokoa maisha yangu na yenu pia je hampaswi kushukuru?"

"Haha ndio ndio tunapaswa kutoa shukrani, mimi Derick natoa shukrani zangu za dhati kabisa" aliongea mlinzi mwingine aliyekuwa akiwatusi wale majambazi walipovamia

Mara mlio wa gari za polisi ulisikika na sekunde si nyingi waliweza kufika eneo hilo

Ifahamike kwamba alichoongea Jimmy kuhusu myahudi kumfunza mbinu mbalimbali ni kweli. Kipindi jimmy anampoteza baba yake alilia sana na kuwa mpweke kwani baba yake ndiye aliyekuwa rafiki yake mkubwa hakuwa na marafiki wengi.

Na kila siku alikuwa akienda mahali ambapo yeye na baba yake hupenda kufika na kuongea mawili matatu wakipunga upepo, alilikuwa akienda mahali pale kila anapomkumbuka baba yake, sasa siku ya siku akiwa shuleni ulitokea ugomvi ambao ulipelekea Jimmy kumuumiza mwanafunzi mwenzake na kutoroka shule kuepuka adhabu na sehemu aliyofikia ni mahali pale

Wakati amekaa katika hali ya mawazo akimkumbuka baba yake aliweza kugundua kuna uwepo wa mtu mwingine mahali hapo. Alikuwa ni mwanaume mzee hivi wa kiyahudi amekonda sana, nguo alizovaa zilikuwa zimechakaa sana na alikuwa amelala chini akipumua kwa chini sana

Jimmy alijiongeza maana kwa kumuangalia alijua atakuwa ni ombaomba alivua begi lake na kutoa bakula kubwa ls kuhifadhia chakula ambacho mama yake kila siku humuandalia kabla ya kwenda shule, kulikuwa na viazi vitamu, chapati za mayai na mayai manne ya kuchemsha bado vikiwa na umotomoto kwa mbali.
Alimkaribia mtu yule mzee akibeba chakula chake ambacho hata yeye hakula ni kuguswa kwake na hali ya mzee huyo ndiyo kulikomsukuma kufanya hivyo, alichuchumaa na kukiweka karibu ya yule mzee harufu ikisambaa puani mwake

"Ukarimu siku hizi ni adimu sana" aliongea mzee kwa kiswahili akifumbua macho taratibu akitazama chakula kile

"Babu amka ule" aliongea jimmy

"Nilikuwa nimeamka muda tu kabla ya wewe kunigundua" aliongea babu yule na taratibu aliamkaa akiketi kitako

"Una miaka mingapi kijana" mzee aliuliza

"Saba"

"Niambie ni nini kilichokufanya udhani labda nina njaa unisaidie?" mzee aliuliza huku akichukua kiazi kimoja na kutafuna

"Ni moyo wa huruma babu"

(mzee alicheka kidogo na kuendelea) "Unaitwa nani kijana?"

"Jimmy"

"Jimmy unaweza niambia kwanni upo hapa peke yako ukiwa na hali ya mawazo?"

"Nimemmisi baba yangu"

"Yuko wapi" aliuliza tena na Jimmy alinyoosha mkono kuelekea juu na mzee alimuelewa

"Koh...Koh...Koh.." mzee huyo alikohoa na jimmy alitoa chupa ya maji na kumpa
Mzee yule alipokea maji yale na kunywa na kuendelea kula huku akiongea

"Umetoroka?"

"Hapana"

"Uongo kwa wakubwa si jambo zuri" alimwambia lakini jimmy alikuwa kimya na hakumuuliza zaidi alikula na kumaliza na alimshukuru sana Jimmy kwa msaada huo mdogo

Basi ikawa kila Jimmy akienda mahali pale alikutana na Mzee huyo na kuwa marafiki wazuri tu bila kujali umri na alikuja kugundua mzee huyo ana siri nyingi sana. Siku aliulizwa swali na mzee huyo "Kijana unataka kukua kijana?" na alipojibu "ndio" mzee huyo alimfunza mambo mengi sana mengine ni siri yake mwenyewe

°°°°°°°°°°

Ndani ya jumba kubwa la kifahari ndani kwenye sebule pana walionekana watu wakiwa wameketi kwenye masofa wengine wakisimama

Mara ilisikika sauti ya hatua za miguu ikikaribia sebuleni humo kwa kasi na alikuwa ni mwanamama mnene kiasi mwenye umbo kama la Hamisa mobeto akiwa na sura yenye wasiwasi

"Bianca uko salama mwanangu?" aliongea kwa kuhema na Bianca aliyekuwa ameketi kwenye sofa alitingisha kichwa kuwa yupo sawa na kwa kiasi mama huyo alipatwa na ahueni

"Huyu ni nani?" aliuliza baada ya kumuona mtu asiyemfahamu ndani kwake

"Mama huyo ni rafiki yangu unapaswa kumshukuru bila yeye tusingekuwa hapa" Cid alimueleza

"Oh kijana asante sana kwa mchango wako mimi kama mzazi nashukuru sana naahidi nitakulipa"

"Shukrani inatosha huna haja ya kunilipa isitoshe nilikuwa nafanya kile nilichoona sahihi kufanywa" Jimmy aliongea kwa tabasamu

"Hicho sahihi ulichofanya kimeokoa maisha ya wanangu ni kitu ambacho siwezi kupotezea"

"Lakini sikufanya nikitegemea kulipwa"

"Ninaelewa lakini vipi unajua ni nini ninachokwenda ku-offer?"

"Pesa labda au kazi au chochote kile cha kubadilisha maisha yangu?"

"Na unaona ni kitu kibaya?"

"Hapana ni vile sio vya lazima"

"Ooh inaonekana una uchumi mzuri sio?"

"Hata robo sifikii"

"Sasa kwanini ukatae? Wanangu wapo hai sababu yako na nina kila sababu ya kukulipa"

"Vipi kama nisingekuwepo unadhani tungekuwa hapa tunaongea bimkubwa?"

"Lakini ulikuwepo" alitulia kidogo kisha akaendelea "aya chukulia sikulipi kwasababu ya wema wako bali ni kwasababu nataka kukusaidia kwasababu moyo wangu umetaka"

"Wapo wanaohitaji huo msaada kuliko hata mimi"

"Haha wewe ni msumbufu sana ila nimekupenda bure, unaitwa nani?"

"Jimmy" Cid aliropoka kana kwamba aliulizwa yeye

"Sasa Jimmy ukiwa unahitaji msaada wowote usisite kuniambia unakaribishwa hapa muda wowote" aliongea na jimmy alitingisha kichwa kukubaliana nae

Mwanamama huyo aliitwa Velora Mwakalebra na ndiye mama mzazi wa Cid na Bianca na ni mfanyabiashiara mwenye mafanikio makubwa nchini Tanzania naweza kusema ndiye mfanya biashara tajiri namba moja nchini akimiliki kampuni ya VELORA GROUP iliyowekeza kwenye sekta mbalimbali kampuni yenye thamani ya dollar billioni mia tano huku yeye akiwa na utajiri wenye thamani ya dollar billioni kumi na tano

Mwanamama Velora aliwageukia walinzi akiwa na sura ya ukauzu na hakuna hata mlinzi mmoja aliyethubutu kumuangalia machoni. Alikuwa amepata taarifa ya kile kilichotokea

"Nyie nitadili nanyi muda ukifika" aliwaambia

Wakiwa sebuleni aliingia mwanamke mwingine na kuongeza idadi alikuwa akitembea kwa maringo sana mkononi ameshikilia mkoba wenye thamani.

"Wewe mpuuzi unafanya nini humu ndani? Nani amekukaribisha" Mwanamke huyo aliongea alipomuona Jimmy

Alikuwa ni yule mwanamke waliyekutana bar siku ile na leo hio wanakutana tena kwa mara nyingine tena

TO BE CONTINUED..........
 
BY Samuel jk_Euphoria

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 6: The kind of knowledge that gets people killed"

"Nani mimi?" Jimmy aliuliza kama vile hakuwa na uhakika kama swali ametupiwa yeye, alikuwa akijiuliza amemfanya nini bidada huyo kiasi cha kumchukia waziwazi lakini hakupata jibu

"Sophia unapaswa kushukuru ndugu zako wako hai sababu ya huyo mtu hapa, mimi sijali kama unafahamiana nae au lah na kwanini unamchukia ila ifike muda tabia yako uweke kando" aliongea mwanamama vero, alikuwa anaijua tabia ya mwanae vizuri sana kuliko mtu yeyote humo ndani

"Jimmy huyu ni Sophia dada mkubwa wa hawa ndugu zake usijali sana kuhusu tabia yake ndivyo alivyo"

Wakati anataka kujibu simu yake iliita na alipoangalia namba ya mpigaji tabasamu lilijichora usoni mwake na hakuipokea aliikata kisha kutuma ujumbe na kuirudisha mfukoni

"Samahani bi mkubwa ninahitajika mahali hivyo inabidi niwakimbie" ilibidi Jimmy aaage

"Oh sawa karibu tena" aliongea mwanamama

"Asante" alijibu kisha taratibu alianza kurmtembea akielekea mlangoni mara ghafla akakumbuka kitu

"Oh nimekumbuka" aliongea na kuingiza mkono mfukoni na kutoa mkufu mdogo wa almasi"Nadhani hii itakuwa ni mali yako uliidondosha siku ile" aliendelea kuongea akiweka tabasamu flani usoni

Sophia aliishia kutoa macho ya mshangao huku akiupokea mkufu huo ambao alikuwa akihangaika kuutafuta nyumba nzima bila mafanikio na sasa upo mbele ya macho yake

Kila mtu mule ndani alikuwa akiwaza yake kichwani walikumbuka ni kwa jinsi gani bidada huyo alivyokuwa akiwasumbua kuhusu mkufu wake uliopotea

Baada ya Ji.mmy kuondoka kimya kilitawala macho yakimuangalia Sophia na kila mmoja alipita njia yake kutoka mule subuleni huyu kaskazini, yule kusine, hawa magharibi na mwisho Cid alipitia mashariki akibakia Sophia peke yake

°°°°°°°°°°

Upande mwingine ndani ya chumba kidogo cha mahojiano chenye mwanga hafifu, meza ya chuma ikiwatenganisha watu wawili

"So Rico kama mchezaji wa man city sio? Unajua Rico Tanzania ni nchi ya amani sana sema washenzi kama nyinyi ndio mnaotuharibia sifa ya nchi yetu"

"Sikia we. Mshenzi usifanye mambo kuwa magumu niambie nina aliyekutuma?" aliongea Inspekta Sabari

"Unadhani nitatoa tasrifa kirahisi tu kwasababu ya mateso mnayonipa huh? Utakuwa mgeni katika hili inspekta"

"Ngoja nikwambie Inspekta naniliu, kuna siri zingine hazifahi kutolewa nikiongea ninauawa nisipoongea bado nitauwawa taratibu tu"

"Unadhani boss wako aliyekutuma anajali kama umeozea hapa? Tangia saa tunayokukamata tayari alishakuona takataka na pengine anapanga kuisafisha hiyo takataka"

"Unadhani najali sana kuhusu uhai? Pengine aliyeniita mpumbavu yuko sahihi, a nikwambie tu hapa unapoteza muda wako bure hutaambulia chochote"

"Damn! wewe mpumbavu!" Inspekta alipiga meza kwa hasira na kumkunja shati mtuhumiwa yule

"Ngoja tuone kama utaendelea kuwa jeuri mpaka saa ngapi" aliongea na kumtandika mtuhumiwa ngumi nzito ya pua kiasi cha kumtoa damu hakuishia hapo tu aliendelea kumshushia kipigo mpaka askari wenzaki wenzake walipoingia kumzuia

"Utaua" askari mwenzake alimtahadharisha

"Nani anajali kama akifa damu za watu wasio na hatia zimemwagwa na mikono ya hawa wapuuzi" alifoka na mtuhumiwa alianza kucheka kwa sauti, kitendo kile kilizidi kumtia hasira Inspekta

°°°°°°°°°°

"You old man... after so long, now you remember that I exist?" (We mzee leo ndo unanikumbuka baada ya kupotea kwa mda mrefu)

"Still sharp with the words, huh? I thought you'd have softened up by now" (Bado tu una mdomo eeh nilidhani labda utakuwa mpole)

"You disappeared like a ghost. No calls, no messages. I almost thought you kicked the bucket." (umepotea ghafla kama mzimu, hakuna mawasiliano kabisa nilidhani labda umekufa)

"Where were you? "(ulikuwa wapi)

"Some things... are better left buried, kid" .(Mambo mengine ni vyema kutoongelewa kijana)

"Then what's the point of you calling me here" (Kulikuwa kuna haja gani sasa ya kuniita)

"Maybe I just missed an old friend." (Labda nimemmisi Rafiki yangu wa kitambo)

"Come on, I know you better than that. You didn’t just disappear for no reason you're hiding something eren’t you" (Nakujua vizuri sana we mzee huwezi kupotea bila sababu kuna kitu unanificha sio)

"Take it." (chukua) alitoa kitabu kidogo cha zamani kilichochakaa sana

"What is this? "(Nini hiki)

"Something I can’t carry anymore, that's no ordinary book kid" (Kitu ambacho siwezi kukibeba tena, hiko sio kitabu cha kawaida kijana)

"What’s inside old man?"(kuna nini ndani mzee?)

"The kind of knowledge that gets people killed"(Yale maarifa ambayo hupelekea watu kuuwawa)

"Scare tactics? Thought you would be more creative" (Unaniogopesha sio? Nilifikiri utakuwa muwazi)

"You're one of the few peoples i trust in this world, guard it with your life kid and be careful, hope you won't disappoint me"(Wewe ni kati ya wachache ninaowaamini kwenye huu ulimwengu kilinde hiko kwa hali na mali pia kuwa makini nacho natumai hutoniangusha)

"Don't confuse me old man you come back out of nowhere, and hand me something like this—expecting me to just accept it?"(usinichanganye mzee yaani unarudi kusikojulikana halafu unanipatia kitu na unategemea nitakipokea?)

"Yes" (Ndio) aliitika na Jimmy alifungua hiko kitabu na kukuta kurasa zikiwa tupu hakuna neno hata moja

"I must admit it you're quite a secretive one" (Inabidi nikubali tu wewe ni msiri)

"Alright am hungry old man got any cash?" aya mzee nina njaa hapa una hela?) jimmy aliuliza na mzee huyo alitoa bakuli ambalo lilikuwa pembeni yake muda wote wanaoongea

"Haha remind me of the first time we met"(Haha unanikumbusha tulivyokutana kwa mara ya kwanza)

Maongezi hayo yalikuwa ni baina ya Jimmy na Mzee myahudi wakiwa xhimboni wamekaa kwenye benchi wakipigwa na jua la mchana lakini hakuna aliyejali. Muda haugandi masaa yalizidi kusonga na hatimae giza kuingia na siku kuishia hivyo

°°°°°°°°°°

Kesho asubuhi Jimmy alikuja kuamka saa nne asubuhi na kama kawaida yake kitu cha kwanza kufanya baada ya kuamka ni kuuchangamsha mwili kwa mazoezi, baada ya hapo alikwenda kujisafisha mwili

Ile anafungua mlango wa chumba chake kwaajili ya kutoka anakutana na sura ya dada yake

"Usiniambie ulitaka kuja kuniamsha saahizi" aliongea Jimmy

"Bro unabahati sana asee mimi dada yako nakupa salute kwa hilo" alijibu kivingine na kumuacha Jimmy katika sura ya maswali

"Unataka kusema nini?" alimuuliza na monica hakumjibu na badala yake aliishia kumpigaigapiga vingumi vya uchokozi

"Asee kuna muda nawazaga nikufunge kamba nikutupe baharani ukaliwe na papa huko unazingua sana dada yangu kila siku hukawii kuniletea vurugu... Umekunywa nini leo wewe"

"Nenda ukajionee mwenyewe bro" aliongea kwa tabasamu na kuondoka zake akimuacha jimmy akikuna kichwa chake

"Kuna muda kuwa na dada ni baraka sana ila kuna mwingine sasa........" alijiambia kichwani mwake na alielekea zake sebuleni

Hapo ndio anaelewa kwanini dada yake alikuwa vile, kulikuwa na ujio wa mtu humo ndani nae hakuwa mwingine bali ni Bianca

Bianca kumuona jimmy alisimama kutoka kwenye kochi aliloketi

"Hatimae umeamka" aliongea Bianca na sauti nyororo ya kumtoa nyoka pangoni iliyosafiri kwenye masikio ya jimmy bila ya kumuangalia usoni

Jimmy alimsogelea Bianca karibu zaidi na kumwambia akae haina haja ya kusimama isitoshe yeye ni mgeni

"Umefika muda sana?" Jimmy alimuuliza

"Hapana ni sasahivi"

"Cid yuko wapi?"

"Sijaja nae yuko busy na mambo yake ya biashara"

"Ooh kumbe ni mfanyabiashara na sijui anyway karibu vipi umekula" Jimmy aliuliza naye alitingisha kichwa kukanusha

"Okay ngoja basi nikaandae kifungua kinywa tule kwanza ndio tuendelee na maongezi" jimmy aliongea na kunyanyuka

"Subiri kwanza......" Jimmy alisimama baada ya mrembo huyo kumtaka asubiri

"Asante" aliongea Bianca akitoa shukrani ya dhati kwa sauti ya upole na Jimmy alitabasamu

"Ni jambo la kawaida kutoa shukrani hivyo usiwaze sana nimepokea shukrani" aliongea kwa sauti ya upole pia

"Japokuwa wewe na kaka yangu ni marafiki lakini haimaanishi mimi na wewe tu marafiki hivyo nataka tuwe marafiki kuanzia sasa" Bianca alikusanya ujasiri na kuongea

"Sawa natazamia urafiki wetu utakapotufikisha" aliongea maneno yenye zaidi ya maana moja

"kweli?" Aliuliza

"Sioni sababu ya kukataa urafiki na mrembo kama wewe" aliongea jimmy na kufanya mrembo huyo kuangalia chini akitabasamu

Monica alitoka jikoni akiwa amemaliza kuandaa kifungua kinywa cha asubuhi hiyo na kukiweka mezani

"Sijui umemfanya nini dada wa watu mpaka anakuonea ila nimempenda" Mony alimnong'oneza Jimmy aliyekuwa akiandaa pamoja naye

"Unadhani sijui unachokiwaza akilini mwako? Sita kama unapanga kumchuna kwa namna yoyote ile hilo sahau"

"Nimekwambia nataka kumchuna shida y....." aliishia njiani na kuweka uso wa tabasamu baada Bianca kusogea kwenye meza ya kula

°°°°°°°°°°

Baadae mchana mida ya saa saba na nusu Jimmy alionekana mitaa ya kariakoo akifanya shughuli mdogomdogo za u'day-worker kujiingizia kipato

Wakati akiendelea na shughuli zake lilionekana gari jeusi aina ya Lexus TX SUV new model likikatiza mitaa hiyo likisindikizwa na macho ya watu wengi, ilikuwa ni nadra sana kwa magari ya kifahari kama hilo kuonekana mitaa hiyo

Lilikwenda ku-park sehemu yenye uwazi na alishuka mwanaume mnene kiasi mwenye upara ung'aao juani na ndevu za mviringo, akivalia suti rangi ya kahawia mkononi akishika simu janja ambayo kwenye skrini ilionekana picha ya watu wawili jinsia moja wamekaa poz la kirafiki

Aliangalia kulia na kushoto kabla ya kuvuka barabara upande wa pili na alienda moja kwa moja mpaka kwenye duka ambalo pembeni kulikuwa na lorry dogo lenye mizigo na watu kadhaa walionekana kufanya kazi ya kuishusha na kuingiza ndani ya duka hilo

Wewe ni Jimmy sio?"

" Ndio ni mimi kiongozi una shida yoyote?" Jimmy aliitika na kuuliza

" Nina ujumbe wako" aliongea

"Ujumbe wangu? Ujumbe gani?" aliuliza tena

Mtu yule alimuonyesha picha iliyokuwa kwenye simu yake ambayo alionekana jimmy mwenyewe na mtu mwingine

"Unamjua huyu kwenye picha hii"

"Ndio ni mzee wangu huyo, amefanya nini kwani?"

"Ninasikitika kukwambia kwamba hatnaye tena"

"Nini?"

"Jana usiku ulikutwa mwili wake ambao haukuwa na uhai umetupwa kando ya ufukwe wa bahari na kitu pekee ni hii picha iliyokuwa kwenye mfuko wa wazi lake"

Jimmy palepale alisitisha kile alichokuwa anafanya na kwenda kukaa pembeni akiwa katika hali ya mawazo sana, Picha hiyo ilionekana kupigwa miaka mitano nyuma kabla ya mzee huyo myahudi kupotea na ni jana aliweza kukutana nae tena lakini cha kusikitisha ni kwamba ameuawa

"Pole sana kwa kumpoteza mzee wako kijani"

"Hakuwa tu ni mzee wangu alikuwa ni kama rafiki yangu na familia yangu, unaweza niambia nini kilichosababisha kifo chake"

"Kwasasa bado hatuna jibu, bado tupo kwenye uchunguzi"

"Vilevile nina maswali pia ya kukuuliza"

"Kabla ya hayo maswali nataka kuuona kwanza mwili wake kudhibitisha kama ni yeye" aliongea Jimmy na mtu yule alimwambia waongozane na hakupinga, walienda mpaka kwenye gari na kuingia kisha kuondoka maeneo yale kuelekea sehemu husika

Nusu saa ilitosha kwao kufika kwenye hospitali ya kuhifadhia maiti na kuingia ndani ya chumba husika

Kulikuwa na mwili umelazwa juu ya meza ndefu ya chuma ya kulazia maiti, mwili ukiwa umefunikwa na shuka jeupe
Jimmy aliusogelea taratibu mwili ule uso wake ukiwa na hisia mchanganyiko, alifunua shuka na kushuhudia mwili wenye alama za kutobolewa na kuchanwachanwa na mapanga kila mahali, mzee aliuwawa kikatili sana na aliweza kudhibitisha ni yeye kweli

Alikunja ngumi kisiri akificha hasira iliyochanganyika na maumivu na alijiambia yeyote anayehusika na kifo cha mzee huyo lazima amkamate

"Nadhani umeweza kudhibitisha kwamba ni yeye sasa ni wakati wa mimi kuuliza maswali muda wa kuomboleza upo wa kutosha" aliongea mtu yule na kauli ile ilimfanya Jimmy amusangalie kwa jicho flani hivi ambalo halikueleweka linamaanisha ni nini

"Unaweza kuuliza"

"Mara ya mwisho kukutana na mzee huyu ilikuwa ni lini"

"Sikumbuki vizuri ila nadhani ni baada ya kupiga picha kipindi kile"

"Una uhakika unachoongea ni kweli?"

"Kipi kinachokufanya utilie shaka maneno yangu?"

"Sawa mara ya mwisho ilikuwa ni kipindi mnapiga picha, je hakukupatia chochote kile kabla ya kupotea au kukwambia chochote kile chenye kutilia shaka?"

"Mimi nakumbuka mara ya mwisho tulipiga picha na kupiga story mbili tatu kabla ya kutokumuona tena na hakuna chochote cha kutilia shaka tuliomgelea kuhusu mademu jinsi ya kutofautisha pisi mbovu, pisi kali na pisi classic" aliongea jimmy na mtu yule alimtazama machoni kumsoms na hakuambulia chochote

"Nikigundua ulichoongesa ni uongo sidhani ka.ma litakuwa jambo zuri kwako"

"Ondoa wasiwasi kamanda nilichosema ni kweli

Mtu yule aliondoka mahali pale akimuacha jimmy peke yake akiutazama mwili wa mzee na kufanya ishara ya msalaba

" Pumzika kwa amani" aliongea kauli hiyo yenye uchungu ndani yake

°°°°°°°°°°

Baadae jimmy alionekana ameketi mahali palipo na utulivu, akiwa katika tafakari nzito, alikumbuka kwa mara ya kwanza alivyokutana na mzee mpaka kuwa marafiki jinsi alivyomfunza kucheza piano, mbinu mbalimbali za kujilinda na mambo mengine mengi ila huzuni kwa.mba mzee huyo ambaye hakulijua hata jina lake zaidi ya kumuita babu na mzee hayupo tena katika uso wa dunia

TO BE CONTINUED..........
 
Daa

Daaah! Story nzuri san
 
BY Samuel jk_Euphoria

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 7: Hazina

Jimmy alijuana na mzee kwa zaidi ya miaka kumi na katika miaka yote hiyo alijifunza mengi kutoka kwake, jimmy hakuwa na ndugu yeyote upande wa marehemu baba yake na mama yake hivyo kumchukulia mzee huyo kama ndugu pekee aliyenaye

Jimmy aligeuza shingo yake kuangalia pembeni kushoto kwake alipokaa, kulikuwa na karatasi lililokunjwa ikionyesha kuna kitu kimehifadhiwa ndani yake

Alichukua karatasi na kuikunjua na yalionekana majani yenye rangi ya ukijani iliyokauka ilikuwa ni bangi(Marijuana) haikueleweka ameitoa wapi lakini mwamba baada ya kukunjua alianza kufanya mchakato wa kusaga majani yale na kuyaweka kwenye karatasi kisha kukunja tayari kwa kuvuta.

Anakuja kugundua kilikosekana ni kiberiti tu cha kuwashia ganja hiyo hivyo mpango wake kusitisha. Alichokuwa akitaka ni utulivu wa akili na aliona pengine ganja ingemsaidia kwa asilimia kubwa lakini mpango wake haukuweza kuendelea kutokana na kiberiti kukosekana. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kutaka kuvuta ganja

Mara alikumbuka kitu na kuangalia pembeni kulia kwake kulikuwa na kitabu kidogo cha zamani sana kutokana kuchakaa kwake, kilikuwa na michoro ya sajabu ajabu isiyoeleweka ni michoro ya aina gani alikichukua na kukifungua kuanzia kurasa ya kwanza hadi mwisho lakini jambo la kushangaza ni kwamba hakukuwa na maneno yoyote zaidi ya karatasi kuwa unjano kwa mbali kuashiria ni cha muda mrefu sana

Jimmy alikigeuzageuza kitabu kukitazama ambapo mwisho wa siku alichoka na kuanza kujiuliza maswali mengi kichwani yasiyo na majibu, machache kati ya maswali aliyokuwa akijiuliza ni je kitabu hiko ni nini? Mbona hakina maandishi? Mzee myahudi alikuwa na maana gani kumpatia kitabu hiki?

Kuliko kuumiza kichwa na maswali yasiyo na majibu aliona apotezee tu na alinyanyuka kuondoka mahali hapo.

Muda mchache alionekana kwenye bar ameketi kwenye kaunta akinywa bia ya Serengeti lager kwa utulivu, hakukuwa na mteja yoyote kwa wakati huo zaidi yake, hata muhudumu pia hakuwepo. Mimi sijui kwanini yuko peke yake, ukisema ameingia kama mwizi mimi sikupingi ndugu msomaji

Wakati ametulia akisikiliza mziki laini uliokuwa ukilia kupitia simu yake ndogo aliongezeka mwanamke mmoja mzungu kwenye kaunta na kuketi

°°°°°°°°°°

Upande wa pili ndani ya gari kulikuwa na watu wawili ndani wakiwa katika hali ya ukimya

"Nadhani kuna kitu anaficha"

"Usipoteze muda toa taarifa yote"

"Kwa nilivyomuhoji anasema hakuachiwa chochote na yule msaliti, Vijana niliowapa kazi ya kumfatilia wamemuona ameshika kitabu kidogo"

"Kinafananaje?"

"Ni kama ulivyosema Sir"

"Hahaha nadhani ni muda muafaka wa kukiweka mikononi mwetu"

"Lakini unaweza kuniambia ni kitabu gani na kinahusu nini? Nimekuwa nikisikia tu ni hazina kubwa"

"Jua mipaka yako"

"Samahani kwa kurupuka kwangu mkuu lakini sidhani yule mwanaharamu atamkabidhi hazina hiyo kijana asiye na uwezo wa kuilinda"

"Hilo linakwenda kujulikana mda mchache mbeleni"

.........

"Nini kinachokuweka kwenye hali ya mawazo mkaka mzuri" aliongea mzungu yule kwa kiswahili fasaha akiachia na tabasamu

"Huna haja ya kuliongelea kama hutaki, nimeshazioona sura kama hizo hapa kabla, Inaonekana umempoteza mtu muhimu sana kwako si ndio?" aliendelea mzungu yule

"Umejuaje?" Jimmy aliuliza

"Uzoefu tu naelewa unavyojisikia"

"Sikutarajia hili lingetokea ile itoshe kusema duniani watu tunapita tu"

"Siku ndefu huh?"

"Ni siku ndefu ndio kiasi cha kumchanganya anyway unaweza niambia wewe na rafiki zako kwanini mlikuwa mkinifuatilia?" Jimmy aliongea huku akigida chupa ya bia

Mzungu yule aliishia kutoa tabasamu na kuongea "Kama nilivyotegemea yule msaliti lazima atafute mwanafunzi wa kurithi mambo yake"

"Msaliti gani huyo unaemzungumzia ebu funguka itoshe kusema nishachanganyikiwa vya kutosha huna haja ya kuendelea kunichanganya"

"Momochi Saizo"

"Ndio nani huyo Momochi unayemzungumzia" jimmy aliuliza

"Inasikitisha sana licha ya Ukaribu uliokuwa naye hukuweza kufahamu hata jina lake"

"Unamaanisha yule mzee aah kumbe anaitwa Momochi Saizo sikujua mana ni msiri sana yule mzee"

"Tusipoteze muda unapaswa kunikabidhi kile ambscho si mali yako"

"Unazungumzia mali gani sikumbuki kama niliwahi kuiba chochote" sekunde anayomaliza kutamka maneno hayo ghafla kisu aina ya "dagger" kutoka mkononi mwa yule mzungu kilikuja kwa kasi kuelekea shingoni mwa Jimmy lakini alikuwa ashastukia mchezo kwani alirudi nyuma kwa kasi na ilibaki kidogo tu kuchanwa koo yake, hakuishia kukwepa naye alimrushia chupa ya bia ambayo ilikwepwa pia

"The book you fool" alifoka yule mzungu na waliongezeka watu wengine kutoka kwenye kona za bar hio kama vivuli vilivyojificha kwenye giza

"Damn! ninyi ni maninja!" Jimmy alishangaa kwa jinsi walivyojitokeza

Licha ya kujua kwamba alikuwa akifuatiliwa tangia atoke kule mochwari lakini hakutegemea kama wangekuwa ni maninja, kuhusu namna alivyogundua kuwa ni maninja ni hiyo mbinu ya kujificha sehemu yenye ugiza pasipo kuonekana

Ni mbinu Ifahamikayo kama Shadow step ni mbinu ambayo mtumiaji hugusa kivuli na kuungana nacho kwa ufanisi ili kujificha. Akiwa ndani ya kivuli, anaweza kusafiri kati ya vivuli vilivyounganishwa kama milango ya kupita kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Ieleweke naposema kivuli namaanisha sehemu yenye hali ya ugiza kupitiliza, jambo linalofanya iwe njia bora ya kusafiri bila kuonekana.

Mwili wake, fahamu, au nishati yake zinaungana na kivuli. anakuwa haonekani au hawezi kuguswa, kulingana na kiwango cha uwezo wake.

Mara nyingi hutumiwa kufanya upelelezi wa jambo flani mbinu hiyo inahusiana na kanuni za Taoismu na Zen ya "being formless like water, adapting seamlessly, and utilizing the natural world rather than forcing one's will upon it. The darkness is not an enemy but a tool, a medium through which one transcends visibility and perception." kwamba kuwa bila umbo kama vile maji, kuzoea mazingira, na kutumia nguvu za asili bila ya kulazimisha. Giza si adui, bali ni chombo cha kujificha na kufanikisha malengo bila kutambulika

Jimmy katika ukuaji wake amekuwa akifundishwa mbinu za kimapigano kutoka kwa Mzee Momochi Saizo myahudi mwenye jina la asili ya kijapani akidai anatafuta mrithi kabla hajafa na uzee wake, ni mbinu nyingi ambazo nyingi tutazijua huko mbeleni

"Nimesema sijaiba mali yoyote kutoka kwenu eleweni" Jimmy alisisitiza

"Swii swiii swiiii" milio ya visu vidogo vyenye umbo la nyota vijulikanavyo kwa jina "Shuriken" vilisafiri kwa kasi hewani vikimsogelea jimmy

Alikwepa kwa kasi kwa kuruka sarakasi moja matata sana na kujivingirisha hewani kama mtaalamu na kutua chini kwa ustadi wa hali ya juu

"Miaka zaidi ya kumi ya msoto wa kujifunza mbinu nyingi sasa nadhani ni muda wa kuzifanyia majaribio, uzoefu ni muhimu sana" alitamka akiachia tabasamu lisilo jema usoni mwake

Palepale jimmy kwa spidi mara tatu ya Hussein Bolt alichomoka na akisindikiza na ngumi yenye ujazo kamili alimlenga kwenye kifua mzungu huyo lakini mzungu naye alikuwa ni mtaalamu sana kwani aliweza kulipangu na jimmy alitegemea hilo, bila kutegemea mzungu alishtukia teke la shingo alilopigwa kwa staili ya "Scissor kick a.k.a kawi chagi"

KIlikuwa ni kitendo cha spidi sana na "timing" ni mbinu ya kawaida tu lakini iliyopigiwa mahesabu kisawasawa, mzungu huyo alianguka chini kutokana na uzito wa teke hilo

Jimmy hajakaa sawa maninja wengine walianza kumshambulia na alikuwa akikwepa mashambulio kama anacheza mziki vile kwa staili matata ya Capoeira akiruka na sarakasi mbili tatu kukwepa visu na mapanga

Ilikuwa ni show moja matata sana na ndani ya dakika tano Jimmy aliweza kuwadhibiti maninja sita kwa kuwazimisha na alibaki mmoja, yule mwanamke mzungu ambaye alikuwa akitazama show mwanzo mwisho bila kuingilia

"Not bad at least his effort was worth it but too bad he ain't here to witness his beloved disciple" aliongea mzungu yule akimaanisha kwamba sio mbaya juhudi zake(Mzee Momochi) Zilistahili lakini kibaya zaidi hayupo hapo kumshuhudia mwanafunzi wake mpendwa"

"So it was you fools who killed him? Who are you fools?" aliongea Jimmy akigundua kwamba hao ndio waliohusika na kifo cha mzee Momochi na kutaka kujua hao watu ni akina nani

"That old man of yours had Something very precious you know?" (Huyo mzee wako alikuwa na kitu cha thamani sana unajua?) aliongea mzungu huyo akitabasamu

"And you're going to hand it over young man by will or forxe" (Na unakwenda kunikabidhi kijana iwe kwa hiari ama kwa kutumia nguvu) aliongea mzungu huyo na kuushikilia upanga vizuri akijiandaa kufanya mashambulio

Jimmy alipandwa na hasira baada ya kugundua hao washenzi ndio wamehusika na kifo cha mzee wake. Aliinama akiokota upanga aina ya Ninjato ulionyooka wenye urefu wa sentimita arobaini na nane(48)

Alianza kutembea kulia na kushoto akinyoosha viungo vya mwili na kukaa mkao wa utayari kwa pambano

"Teng! Teng! Teng! Twing! Zzzzzz!!!" ilikuwa ni milio ya mapanga kugongana na kukwaruzana kiasi cha kutoa cheche, ilikuwa ni vita ya siraha ya ana kwa ana kati ya mbongo na mzungu

"Sikuwahi kufikiria Ipo siku nitafikia hatua hii" jimmy aliongea huku akiendelea kupambana

"Kwamba nitafikia hatua ya kutaka kumwaga damu,.... Yule mzee siku ambayo nakutana naye nilikuwa ni mpweke sana sikutarajia kama tungefika mbali kiasi kile cha kumchukulia kama mwanafamilia....."

"Shut your damn mouth and hand over the book you fool" alifoka yule ninja mzungu

"Teng! Ting! Ting! Teng!"

"Ni jana tu hapo nilipokutana nae baada ya kupotea kwa zaidi ya miaka mitano halafu......"

"..... Halafu nyinyi viroboto mmemuua...."

".......Kwa sababu ya kipuuzi sana, For a fucking book? Is that book worth much than his life?"

"Cut the Crap!" mzungu aliona Jimmy anampigia makelele tu yeye alichotaka ni kitabu tu na sio ngonjera

Mpambano uliendelea kwa takribani dakika nne na katika dakika ya tano Jimmy alifanikiwa kulidondosha panga la mzungu huyo chini na kumchana baadhi ya sehemu ya mwili

(shwaaaaa!) Aaarggh!! " alipiga makelele mwanamke yule baada ya kuchanwa na upanga mkali kwenye goti na kudondoka chini akipiga goti na mguu mwingine

" Any last words miss before going six feet under? " Jimmy alimuuliza kama ana kauli ya mwisho huku akimwekea upanga karibu na koo tayari kwa kuchinja

"To be honest you really are a talent young man you have my respect but have you ever thought about your family?"(Kusema kweli una kipaji sana kijana hilo una heshima yangu lakini je umeifikiria kuhusu familia yako?) aliongea na kutabasamu mzungu yule licha kuhisi maumivu na damu kumvuja

"What did you do to my family you bitch?"(Umeifanya nini familia yangu we malaya?) Jimmy alifoka kwa hasira

"You have a pretty sister oh and your mama too"!(Una dada mzuri sana oh na mama pia)

"Niambie umewafanya nini we malaya kabla sijakutoboa macho" Jimmy aliongea kwa hasira na kumchana shavu lake na upanga na mzungu yule aliishia kuvumilia tu kwa kujikaza

"You dare hurt my face you moron?" Alilaani

"Nishakichoka kizungu chako niambie wako wapi?" Aliongea akiwa sura ya kikauzu zaidi

"Nadhani unapswa kufikiria kwa makini kati ya familia yako na hiko kitabu kipi chenye thamani" aliongea na kuzidi kumtia tu Jimmy hasira

"I think your mama didn't warn you that to never mess with someone's family"

"kama unataka kuiona familia yako ikiendelea kuishi unapaswa kunikabidhi hiko kitabu"

"Sina kwasasa" aliongea Jimmy na mzungu yule alitabasamu na kuingiza mkono wake mfukoni na kumpatia simu ndogo na kumrushia Jimmy

"Sina haraka unapaswa kwenda kukifata mahali ulipokificha baada ya masaa mawili nitakutafuta kupitia hiyo simu ukifanya ujinga nadhani unajua nini kitatokea" aliongea na kwa tabu sana alinyanyuka akiondoka mahali pale akitembea kwa kuburuza mguu mmoja

Jimmy aliishia kumwangalia mzungu huyo kwa macho yenye ukauzu bila kufanya chochote mpaka anatokomea zake mahali hapo

Alienda mpaka kwenye kaunta ambapo aliacha simu yake, aliichukua na kubonyeza-bonyeza kisha kuiweka sikioni

..........

Upande mwingine kwenye refu kwenda hewani lenye floors zaidi ya arobaini ndio makao makuu ya VELORA VROUP OF COMPANIES, kwenye floor ya ishirini na tano ndani ya ofisi kubwa iliyopambwa na vitu vya bei vhali kukiwa masofa na samani zingine kuendana na hadhi ya mwenye ofisi hiyo

Kwenye meza kubwa yenye tarakishi kampuni ya samsung alionekana mwanaume kijana mweusi aliyevalia suti nyekundu ikikosekana tai tu, mwanaume huyo alikuwa bize na tarakishi yake.

Mara simu yake aina ya Iphone ilianza kuita na alipoangalia namba ya mpigaji alikuta imeseviwa "Hero" alitabasamu na kuipokea

"Niambia bro" Cid alianza kuongea

"Upo wapi?" upande wa pili ambaye ni Jimmy aliuliza

"Nipo kazini nadili na mambo ya kampuni unashida yoyote bro?"

"Nipe Location nakuja sasahivi"

"Kuna nini kwani"

"Wewe nipe location nikifika tutaongea hukohuko"

"Poa kaka nakutumia sasahivi" aliongea na kukata simu kisha kutuma location kwa njia ya ujumbe

Dakika ishirini baadae simu ikaita tena na Cid aliipokea

"Nimeshafika uko floor ya ngapi?"

"Chukua lift mpaka floor ya ishirini na tano ukifika utakutana na dada wa mapokezi atakuleta ofisini nimeshampa taarifa tayari"

Dakika chache mbeleni mlango wa ofisi ya Cid ulifunguliwa na dada wa mapokezi akifuatiwa na Jimmy ambaye mkononi alikuwa ameshikilia kitabu kidogo

"Welcome to my workplace brother this is my office feel free" Cid alimkaribisha Jimmy kwa kingereza

ALUTA CONTINUARA........
 
Kama mtunzi hii ni simulizi yangu ya kwanza kuandika na kuitsngaza nje ya jukwaa husika. Mimi ni mwandishi wa simulizi kutoka jukwaa la fasihinet.com ya boss singanojr 😁

Nisielezee ssna kuhusu mimi. Mimi ni Samuel jk(jins halisi) lskini nalipenda neno Euphoria kutokana na maana iliyopo na hii ni Imulizi yangu ihusuyu uchaei, mapenzi, mapigano, fantansia n.k inaitwa SOLO KING: ANCIENT LEGACY

Ninaposema uchawi simaanishi kuwangisna usiku😅😅 Ni new fashioned kinda type!

UTANGULIZI

Hapo zamani, kabla ya historia kuandikwa, aliishi mtu mmoja ambaye alivuka mipaka ya asili. Alikuwa mchawi mwenye nguvu zaidi kuwahi kutokea duniani, aliyefikia upeo wa juu lakini jina lake lilisahaulika, na urithi wake ulipotea kwa muda mrefu.

Kitu kimoja kilichobaki ni kitabu cha kale, kilichoandikwa kwa lugha zilizozungumzwa zamani, lugha ambazo sasa ni za kihistoria. Kitabu hicho kilijulikana kama FORBIDDEN GRIMOIRE, na kilikuwa na masalia ya maarifa yake pamoja na nguvu zisizo za kawaida.

Karne zilipita, falme zilikuja na kupita, dunia ilibadilika, na uchawi ukawa ni hadithi tu za kusadikika.

Lakini hatima haikupotea. Kijana mmoja aitwaye Jimmy anakuja kubeba hatima yake bila kujua.

Usikose simulizi hii ya kusisimua, yenye matukio ya ajabu na mabadiliko ya nguvu. Inamhusu kijana machachari aitwaye Jimmy, anavyopitia changamoto na majira, na jinsi anavyotoka kuwa dhaifu hadi kuwa mwenye nguvu kubwa.

°°°°°°°°°°

CHAPTER 01: Normal life(maisha ya kawaida)

Yalikuwa ni majira ya asubuhi jijini dar es salaam chini Tanzania jua likichomoza kutoka mashariki na mwanga hafifu wenye kupendeza macho, upepo wa asubuhi ukivuma taratibu na kufanya hali ya hewa kuwa yenye utulivu. Watu walikwishaamka kuendelea na majukumu yao ya kila siku ya kutafuta ridhiki za kila siku.

Apartment ya hali ya kati yenye ghorofa tatu kwenda juu ipatikanayo maeneo ya Mbezi majirani walikuwa wakiendelea na shughuli zao za hapa na pale. Ndani ya apartment hiyo ghorofa la kati kwenye chumba kidogo cha wastani alionekana mwanaume kijana akiwa amelala fofofo mpaka wakati huo na hakuonyesha dalili yoyote ya kuamka muda huo, ni wazi kwamba usingizi ulikuwa ni mtamu mno.

Wakati bado amelala mlango wake wa chumba uligongwa kuashiria kuna mtu yupo nje ya mlango wa chumba hiko

"ngo! ngo! ngo!' uligongwa tena safari hii kwa sauti kuzidi mwanzo

"We monica acha kunikata stimu basi" aliongea mwanaume huyo kwa sauti ya lawama

"Amka kumekucha"

"Sawa naamka subiri kidogo" alijibu akiwa bado amelala

Mara mlango ukafunguliwa na kuingia mwanamke mrefu wa wastani, mweupe wa ngozi na kwenda kufungua dirisha lililokaribu na kitanda kisha kulivuta shuka alilojifunika mwanaume huyo kwa fujo

"Asee we monica kuna kitu unakitafuta sio?" Hatimae aliweza kuamka akiwa hana furaha kabisa

"amka wewe kumekucha unalala-lala hovyo acha uvivu dogo"

"Si uniache sasa kwani kulala kwangu hovyo unapungukiwa na nini?" Aliuliza na bila kusubiri jibu alirudi zake kulala lakini alikuja kushtuka kwa kifinyo mguuni na kwa hasira alinyanyuka akitaka kumkamata lakini ilionekana monica alikuwa ashajipanga kwani alikimbia nduki kutoka chumbani humo kabla hata hajadakwa

Hehehe na ubabe wote lakini mwisho wa siku unakimbia tu" alijiongelesha na kuamka maana usingizi ulikuwa umekata kabisa

Hao walikuwa ni dada na kaka wa damu walikuwa wakilumbana asubuhi hio monica akiwa ndie mkubwa na mwanaume huyo aitwae jimmy akiwa mdogo

Ndugu hao walikuwa ni kama paka na panya waishio pamoja kwani kila siku ni malumbano tu na ugomvi usioisha muda yaani kifupi ni kwamba upendo wao kama ndugu ulikuwa ukidhihirishwa kwa ugomvi tu, ni bahati sana kuwakuta wakiwa pamoja bila kuzozana.

Mwanaume huyo ambaye kwasasa anatambulika kama jimmy alikuwa kijana ambaye umri wake ulikuwa miaka ishirini ya mwanzoni(early 20s).

Alikuwa ni mwanaume mtanashati na mweupe wa ngozi kama dada yake, alikuwa mrefu wa wastani na asubuhi hio alikuwa amevalia suruali nyepesi ya kulalia rangi nyeusi juu akiwa kifua wazi kuonyesha mwili wake machachari uliojengeka vizuri kuanzia mabegani mpaka kiunoni kama mwanariadha na urefu wake wa wastani

Basi Jimmy kama ilivyo kawaida ya wanaume wengi baada ya kuamka aliupasha mwili joto kwa push-ups na sit-ups kadhaa kabla ya kwenda kuusafisha mwili na baada ya kumaliza shughuli ya usafi wa mwili alivaa nguo za kawaida na kuzichana nywele zake fupi zilizonyolewa mtindo wa low fade na kumfanya azidi kuwa mtanashati haswaa. baada ya kumaliza mdogomdogo alielekea sebuleni

Kufika sebuleni aliwakuta wanawake wawili ambao ni muhimu kwake na kukamilisha familia yenye idadi ya watu watatu ambao ni yeye, dada yake na mama yake mzazi. Baba yao yeye dada yake alikwishatangulia mbele za haki miaka mingi nyuma wakiwa na umri mdogo

"Shikamoo mama" jimmy alimsalimia mama yake kipenzi

"Marahaba, umeamkaje mwanangu"

"Sio salama mama kuna kunguni alikuwa akinipigia kelele"

"Kuwa na heshima dogo nani unamuita kunguni?"

"Wewe unaniheshimu?"

"Dogo......."

"Hey hey mtapasua ngoma za masikio ysngu jamani nimeshachoka makelele yenu ebo! "mama yao alilalama ilioonekana kweli alikuwa na kazi ngumu sana kuwalea hao watoto mpaka kufikia wakati huo

"Angalau kuwe na amani basi tukipata kifungua kinywa ndio muendelee na hizo ngojera zenu" aliendelea na ndugu hao waliamua kutii mara moja

"Enhee asubuhi hii tunakula nini mama nimemisi sana chapati zako tamu kama asili" jimmy aliuliza

"Tena zipo za kutosha tu ni wewe na tumbo lako" monica alidakia

"Haya ndio mambo sasa ndio maana mama yangu nakupenda huwaga huniangushi kwenye misosi hahaha" jimmy alianza kumsifia mama yake

Basi familia hiyo walikula na kifungua kinywa kwa amani mpaka kumaliza na kila mmoja aliendelea na mambo yake jimmy aliondoka kwenda kwenye kibarua chake, dada yake akielekea chuo akibaki jimmy ambaye muda huo alikuwa amemaliza elimu yake ya advance akisubiri kuanza chuo hivyo alibaki peke yake

Licha ya kusubiria "selection" za chuo haikumaanisha akae tu kizembe,hapana kijana huyu alikuwa akifanya kazi ndogo ndogo za u'dayworker angalau apate pesa za kujikimu hapo baadae isitoshe familia yake ilikuwa ni ya hali ya kawaida hivyo kuna mda pesa inakosekana

Hakukaa sana humo ndani aliondoka baada ya kufungo mlango wa apartment yao.

°°°°°°°°°°

Muda ulienda na hatimae kufika saa kumi jioni. upande wa mbezi beach beach ufukweni mwa bahari ya hindi kulikuwa kumechangamka sana mida hio kutokana na watu kuwa wengi wakipunga upepo wa jioni hio ulioambatana na baridi kwa mbali wengine wakiogelea majini wengine wakiwa na wenzi wao wakifurahia mandhari nzuri ya bahari na kadhalika

ilikuwa ni kawaida kwa jimmy baada ya kumaliza mishemishe zake kuja hapo kutulia kabla ya kurudi nyumbani na siku hiyo alionekana kumaliza mapema sana. alienda kwenye chimbo lake pendwa la kila siku na kujilaza kwenye mchanga bila kujali kama atachafua nguo au lah

kabla ya kulala alijifunga kitambaa kichwani ili nywele zake zisiingie mchanga na kuuchapa usingizi.

Moja ya sifa ya jimmy ni kupenda sana kulala na hachagui sehemu yeye popote kambi tu ilimradi ni salama na ana usingizi wa kutosha

ameshalalamikiwa sana kulala mchana lakini yeye wala hajali anadai kwamba usingizi wa mchana na jioni ni mzuri sana kwa afya ya akili huongeza nishati mwilini na kuondoa uchovu na kupunguza msongo wa mawazo n.k

Muda ulizidi kusonga taratibu, jua nalo lilianza kuzama hatimae giza kuingia Jimmy akiwa bado amelala mahali alipokuwa. Muda ulikuwa ukisoma saa moja na dakika arobaini na hakuonyesha dalili ya kuamka muda huo

°°°°°°°°°°

Katika sehemu tulivu yenye bustani nzuri iliyopendeza kulikuwa na watu wawili wamekaa kwenye benchi mmoja akiwa ni mwanaume wa makamo na mwingine akiwa ni mvulana mdogo ambaye kwa kumuangalia tu alikuwa kati ya miaka sita au saba. Muda huo ulikuwa ni jioni, mwangaza wa jua uking'aa kwa rangi yake ya dhahabu na kufanya mandhari waliyokuwa wakiangalia kuzidi kupendeza.

"Jimmy"

"Naam*

" kwenye maisha hutakiwi kukata tamaa ata kama unapitia changamoto pambana mpaka mwisho usikate tamaa sawa? "

" sawa baba nimekuelewa lakini kwanini unaniambia saaahivi" aliuliza

"kwasababu nataka uwe mwenye nguvu, siku zote wenye nguvu huwa hawakati tamaa kirahisi"

"kwahiyo wale wanaokata tamaa ni dhaifu?"

"Ndio, vipi unataka kuwa dhaifu?"

"Hapana"

"vizuri kuanzia sasa nataka uwe 'strong' mwanangu ili ikifika wakati ambao mimi sioo uweze kuwalinda dada na mama yako na wale wote uwapendao*

"Nakuwaje sasa mwenye nguvu?"

"kuhusu hilo usijali mimi nipo nitakufundisha"

Hayo yalikuwa ni maongezi kati ya jimmy na Baba yake kipindi cha nyuma wakati marehemu baba yake alipokuwa hai

°°°°°°°°°°

Mara taratibu jimmy alifumbua macho yake ikionyesha ni wazi alikuwa kwenye kumbukumbu akiikumbuka siku aliyokuwa akiongea na marehemu baba yake na hakutegemea kama siku ile ingekuwa ndio siku yake ya mwisho kumuona baba yake kwenye uso wa dunia kwani siku iliyofuata baba yake alifariki kwa kupatwa na ajali mbaya.

Alinyanyuka mahali pale na kuikung'uta michanga iliyonasa kwenye nguo zake kisha alijinyoosha vizuri na kupiga miayo

"Nina njaa sasa ngoja ninunue chochote kitu angalau nipooze kidogo kabla ya kurudi nyumbani kula" alijiongelesha na kuingiza mkono mfukoni na kutoa kiasi cha pesa shillingi elfu tano kisha kuangaza huku na huko na kugundua kulikuwa hakuna wate wengi na mda ulikuwa umeenda

"ina maana nimelala mda mrefu kiasi hiki" aliongea baada ya kuangalia muda kwenye saa yake ya mkononi na kukuta ni saa mbili na nusu

"Nitasema kulikuwa na foleni kubwa" alijiambia na kuanza kuzipiga hatua kuondoka maeneo hayo.

°°°°°°°°°°

Upande wa mbezi kwenye apartment ya waishio jimmy na familia yake sebuleni alionekana mama yao akiwa peke ameketi kwenye meza ya chakula na chakula kilikuwa tayari kimeandaliwa mezani na alikuwa akiwasubiri wanae warudi waweze kula.

"Hivi hawa watoto mpaka muda huu bado hawajarudi tu" alilalama mwanamama huyo

Alichukua simu yake aina ya Samsung S22 na kufungua kisha kuingia kwenye apo ya 'contact' na kuanza kuisaka namba ya bintiye monica na alipoipata alipiga lakini aliishia kusikia sauti nyororo ikimwambia "namba unayopiga haipatikani kwa sasa* na kuishia kukunja sura

Alipoona hivyo alimpigia mwanae Jimmy na uzuri ni kwamba alikuwa hewani kwani simu ilikuwa ikiita

°°°°°°°°°°

" Twiiii twiiii twiii twi twiiii!!" simu ilikuwa ikiita kwa nguvu kama 'mic' mbovu, Ilikuwa ni kiswaswadu aina ya Tecno zile za zamani

Jimmy alipokea simu baada ya kuona ni mama yake ndiye anapiga

"Hallo ma...."

"Uko wapi?" alimkatisha na swali

"Ndo niko njiani naelekea huko nyumbani" alijibu huku mkononi alikuwa ameshika Ice cream aliyokuwa anailamba huku akiongea na simu

"Mpigie rafiki yake na dada yako umuulize monica alipo maana kwenye simu hapatikani"

"Usiniambie bado hajarudi mpaka muda huu"

"wewe umerudi?"

"lakini si ndo niko njiani"

"utajua mwenyewe fanya ujue dada yako yuko wapi mana kila siku kunitia presha tu"

"usijali nafika naye hapo nyumbani"

"eeh ndio mmefike mapema chakula kinapoa"

"sawa mama" kisha akakata simu na kumpigia simu mtu mwingine

°°°°°°°°°

Ndani ya Bar moja maarufu ya kisasa iliyoko maeneo hayohayo ya mbezi beach watu walionekana wakipata huduma yao ya ulevi, kila mmoja akiwa bize na chupa yake.

Sasa kulikuwa na mwanamke aliyeketi sehemu yake akinywa bia kwa fujo sana huku machozi yakimtoka na pembeni yake kukiwa na mwenzake ambaye alikuwa akimuangalia kwa kumuonea huruma

Wakati akiendelea kunywa kulikuwa na mziki ukilia taratibu kusindikiza huzuni yake

🎶Ila siri ya penzi, siri ya moyoS Siriya nani?🎶

🎶Siri ya chozi ni maumivu ndani kwa ndani🎶

Alinyanyuka mwanamke huyo na chupa yake ya bia lakini kwa bahati mbaya alikosa balance kutokana na kulewa hivyo kudondoka lakini hakuweza kufika chini kwani alitokea mwanaume na kumdaka

Na mwanaume huyo hakuwa mwingine bali ni jimmy

"Sara, asante kwa kunipa taarifa" jimmy alishukuru kwa moyo wa dhati kabisa akimlenga yule mwanamke aliyekuwa amekaa na alikuwa ni rafiki yake na monica

"anytime" akimaanisha muda wowote

Monica baada ya kuona aliyemzuia asidondoke ni kaka yake ndio alizidisha kulia ni kama vile jimmy amefungua maji ya bomba kwani alilia sana kiasi cha jimmy kupatwa na wasiwasi na kumgeukia Sara akitaka maelezo

Sara alimpa ishara ya kwamba amevunjwa moyo yaani mapenzi ndiyo yanayomliza

"Unajua mapenzi ni ya ajabu sana, na sijawahi kuyaelewa. Unatoa moyo wako, uaminifu wako, yaani kila kitu ili mwisho wa siku uje kulipwa na maumivu? Mapenzi ni kama mchezo flani hivi ambao sheria zake hazijawahi kueleweka

Love's a bullsh*t you know?" aliongea monica huku machozi yakimtoka

"I hear you, kila neno, maumivu yatokayo kwenye moyo wako, nayaelewa na siwezi kukaa hapa nikikuangalia tu ni lazima nimshikishe adabu huyo mpuuzi ila unapaswa kujua mapenzi ndivo yalivyo, kuna muda yankuacha na maumivu, maswali na majeraha ya moyo ambayo huchukua muda kupona

Lakini sikia.... Hutakiwi kuwa mnyonge hivi na kulialia unapaswa kujikaza. Sio mapenzi yanayokuumiza bali ni mpuuzi mmoja anacheza na hisia zako. Cha kufanya ni kusahau tu na kuanza upya you're still of worth something true" alimfariji dada yake na kumpa moyo na kwa kiasi flani alifarijika

"Nilidhani labda utaanza kunifokea na kunisema" monica aliongea

*na kweli ningekufokea sema tu muda haukuwa sahii" alijiwazia na kuishia kumpa tabasamu tu

"ata kama ningekufokea kesho ungesahau tu" aliongea na kumfanya monica atabasamu

"Twende nyumbani mama anatusubiri kwaajili ya kula" aliongea jimmy akiwa ameshaanza kupiga hatua na monica alianza kumfata kwa nyuma kama kifaranga, ungedhani labda jimmy ndio kaka mkubwa kutokana na mwili wake pamoja na urefu.

Wakati anakaribia mlango wa kutokea aligongana na mwanamke aliyekuwa akiingia kwenye bar hiyo, haikueleweka ni makusudi ama kutokuwa makini kwa mwanamke yule mpaka kugongana mabega

"Samahani dada" licha ya kosa kutokuwa lake jimmy aliomba radhi na kuuelekea mlango

"Subiri kwanza kijana unaenda wapi?" aliongea yule mwanamke

"Naondoka" jimmy alijibu lakini alipofika mlangoni aliweza kuzuiwa na mabaunsa wawili wakisimama mbele yake

Alikuwa ni aina ya wale wanawake wenye mashauzi sana, maringo meengii na kujiona wa matawi ya juu sana kiasi kwamba aliwadharau binadamu wenzake aliowaacha mbali kimaendeleo

"Si umeombwa radhi na wewe" Monica aliingilia kati ni kama vile sio yeye aliyekuwa akilia dakika chache nyuma

"Haitoshi"

"hehehe eti haitoshi, unajiona nani kwani?"

"Na wewe ni nani wa kuingilia yasiyokuhusu" aliongea mwanamke yule akisindikiza na sonyo kama la jini kabula

"kwa taarifa yako huyo ni kaka yangu hivyo yananihusu bibiye halafu inaonekana wewe ndio mwenye kosa ni wewe ndiye uliyemgonga mwenzio halafu na bado ukaombwa msamaha ety" haitoshi" screw you!

"Inatosha Monica, unatakaje ili tumalizane haraka?" jimmy alimtuliza dada yake kisha kuuliza

"piga magoti"

"Unasema?"

"Nimesema piga magoti kwani we kiziwi?" aliongea na kumfanya jimmy aachie tabasamu ambalo ni monica pekee alilielewa

TO BE CONTINUED..........

Though kuna makosa madogo ya uandishi lakini sio mbaya ninaeleweka na nitazidi kujirekebisha kadri diku zinavyozidi kusonga

Ndugu wasomaji wa simulizi za kusisimua mnikaribishe writer katika ulimwengu wenu nipate nafasi ya kuwaburudisha☺️

NB: Simulizi bado haijakamiliks inaendelea na nitakuwa nashushs kwa vipande vitatu(kipande kimoja kwa siku. J5, Alh na J'mosi)
Nauliza...Burichela yumo humu kwenye hii hadithi yako?
 
BY Samuel jk_Euphoria

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 8: "Wapuuzi kama niyinyi ndio mnatusababisha tuingie dhambini baada ya toba ya muda mrefu"

Jimmy aliingia na kupokea ukaribisho kwa ishara ya kutingisha kichwa akionekana ana haraka, hakuwa na muda wa kupoteza

"Vipi bro kuna shida gani mpaka ushindwe kuoiambia kwenye simu?" Cid aloiloza akiwa na shauku ya kujua kilichomleta hapo

"Nahitaji gari lako" Jimmy aliongea

"Hilo tu? Mbona ungesema kwenye simu tu ingeeleweka ningekuandalia mazingira kabla hujafika"

"Haina haja pia nahitaji kingine kutoka kwako"

"Kipi hiko?"

"Nahitaji...... " aliongea Jimmy kwa sauti ya kawaida huku akiiacha sentensi ielee na kufanya ishara flani mkononi jambo lililomshtua Cid

"Bro unataka bastola? Ebu kuwa serious bro kwanza mimi naitolea wapi Usiniambie unataka kufanya uhalifu"

"Huna haja ya kuwa na wasiwasi siendi kuua mtu ni kutishia amani tu kuna kenge zinaleta mazoea" Jimmy aliongea hakutaka kufunguka sana kuhusu jambo lililomtokea

"Hata kama kuna watu wamekuchokoza hutakiwi kwenda mbali hivyo"

"Kwahiyo unasemaje bro? "

"Hapana bro sio kama nakataa sina hicho unachokitaka mimi ni mfanya biashara na sio polisi"

"Ishu sio wewe kuwa nayo ishu ni unaipataje"

"Unamaanishaa...." aliongea akiishia njiani baada ya kugundua kitu

"Ndio, hao walinzi weko si wana vibali vya kumiliki siraha ya moto unachopaswa ni kuwaazima tu sidhani kama watakukatalia bwana mdogo" aliongea jimmy akitoa tabasamu

°°°°°°°°°°

Muda mchache baadae Jimmy alionekana ndani ya gari aina ya Range rover jekundu siti ya dereva, akiwa ndani ametulia tuli akisubiria kitu na mara simu ilianza kuita, ilikuwa ni ile simu ndogo aliyoorushiwa na yule ninja mzungu

Aliipokea na kuiweka sikioni akiwa na sura makini isiyo na masihara hata kidogo, alinyamanza kimya akisubiri kusikia sauti upande wa pili nao upande wa pili ukitegemea kusikia sauti kuanza kwake lakini wapii ni sauti ya kiyoyozi cha kwenye gari ndiyo kilisikika zaidi

Upande wa pili aliamua kuvunja ukimya

"Kijana niseme tu umenifurahisha sana sikutegemea kabisa!" ilisikika sauti upande wa pili na ilikuwa ni ya kiume tofauti na alivyotegemea Jimmy kusikia sautki ya mwanamke

"Acha kuzunguka nipe location haraka iwezekanavyo"

"Haha napenda sana watu aina yako kijana yaani ni 'direct' sana hakunaga longolongo"

"Nikuonye tu nikikuta hata alama ya mchubuko kwenye mwili wa ndugu zangu Naapa utakiona kifo ni bora kuliko kuishi"

"Usiwe na wasiwasi kijana japokuwa tumewateka ndugu zako ila tunaheshimu sana wanawake fata location niliyokutumia" aliongea mwanaume wa upande wa pili

"Nataamini vipi kama mpo na familia yangu na kama wako salama?" aliongea Jimmy na kipya kilifata kwa muda kisha sauti yenye ikasikika

"Kaka..... Kaka tumetekwa tusaidi.. ee" ilikuwa ni sauti iliyoambatana na kilio nauoga

"Monica uko sawa? mama yuko sawa?" Jimmy alikurupuka baada ya kusikia sauti ya dada yake na kuuliza maswali

"Niko.... Mama..."

"Hello.... Hello.. Hello??" jimmy aliongea kwa nguvu baada ya sauti ya dada yake kukoma

"Nadhani sasa umeshadhibitisha kile ulichokuwa na shaka nacho"

"Amini nakwambia wewe mpuuzi umegusa sehemu ambayo hukutakiwa kugusa" Jimmy alifoka kwa hasira na baada ya kumalizia sentensi tu simu ilikata na ujumbe kuingia na baada ya kuusoma ulikuwa ukimuelekeza mahali anapotakiwa kufika huku ujumbe ukisisitiza kwamba anapaswa kwenda mwenyewe vinginevyo hataiona familia yake kamwe

Baada ya kumaliza kuusoma ujumbe huo aliangalia pembeni kwenye siti ya abiria kulikuwa na bastola nyeusi aina ya Glock 17 generation 5,ni toleo la mwaka 2017

Ni siraha inayotumia 9mm bullet(size ya risasi) na inabeba jumla ya risasi 17 ambapo bastola nyingi hazifiki idadi hiyo, kama haitoshi kuna "extended magazines" zenye idadi 33 za risasi. Tukiongelea kuhusu reliability Glock hai-jamm Unaweza kuiangusha kwenye matope, mchanga, hata kwenye maji, na bado itafanya kazi kama kawaida. Ndiyo maana jeshi, polisi, na hata special forces wanaiamini.

Frame yake imetengenezwa kwa "polymer" hivyo kufanya kuwa nyepesi na imara isiyo na uzito wa kukuelemea, kingine ni kuhusu mfumo wake, Glock 17 ina mfumo wa "Safe Action System" yaani ilimradi unakaza trigger inafanya kazi bila stress ya system nyingine sijui kukoki na risasi husafiri hadi mita elfu moja(1000 meters)

Jimmy baada ya kuikodolea macho alisafisha koo na kunyosha shingo lake vizuri na kuwasha gari na kuliondoa kwa kasi maeneo hayo

°°°°°°°°°°

MILITARY HEADQUARTERS TPDF (Tanzania People'sDefenseforce))

Makao makuu ya jeshi la taifa nchini Tanzania lipatikanalo maeneo ya Upanga jijini dar es salaam, ndani ya uzio mkubwa wenye ulinzi mkali sana kulikuwa na majengo mbalimbali ya jeshi walionekana wanajeshi wakiwa katika majukumu yao waliyopangiwa

Kwenye jengo moja lenye ulinzi mkali kuzidi maeneo yote,Ndani ya ofisi ya mkuu wa majeshi ya ulinzi alionekana mzee ameketi kwenye kiti cha heshima pamoja na mzee mwingine pia,walikuwa ni majenerali

Ilikuwa ni ofisi kubwa sana yenye kila kinachoitajika ili kuitwa ofisi ya mkuu wa majeshi ya nchi ya Tanzania

Katika kiti hiko cha heshima Aliyeketi alikuwa ni Jenerali John Merizasta akiwa ndiyo mwenye umri kati ya miaka sitini na tano kwenda sitini na nane akiwa amevalia gwanda iliyochafukwa na vyeo vingi pamoja na kofi yenye beji la dhahabu huku upande wa pili uliomtenganisha na meza kubwa ya ofisi aliketi Luteni Jenerali Omary Mwachitete akiwa wa pili kicheo naye akivalia gwanda lake la heshima lenye vyeo vingi pamoja na kofia yenye beji la dhahabu

Walikuwa katika hali ya utulivu wakizungumza mawili matatu kuhusu mambo ya jeshi na usalama wa nchi kwa ujumla

Wakati wakiwa katika mazungumzo ya kina ghafla sauti ya mlango kugongwa ilisikika na Jenerali Merizesta aliruhusu mgongaji kuingia

Mlango ulifunguliwa na aliingia mwanajeshi wa kiume umri wa makamo aliyevalia kombati mwenye cheo cha kanali, baada ya kuingia alitoa heshima kwa wakubwa zake kupiga salute

"Unaweza kunipatia taarifa kanali" aliongea Jenerali Merizesta alionekana kutegemea ujio wa kanali

"Ndio ndio Mkuu nimefanya kama ulivyoagiza hili ndilo faili lenye taarifa kamili" alijibu kanali huyo na kumpatia Jenerali faili hilo kwa heshima

"Sawa kanali unaweza kwenda" Aliongea Jenerali Merizesta baada ya kupokea na kumpa ishara ya kuondoka. Kanali huyo alitoa heshima yake kwa wakuu na kutoka

Jenerali alifungua faili hilo ambalo ndani yake kulikuwa na picha ya mwanaume kijana na taarifa zake kamili

"Huyu kijana ameikoa familia yangu" aliongea jenerali akimwambia luteni mara baada ya kumaliza kupitia taarifa hizo

"Unamaanisha yule kijana aliyewaokoa wanao kutoka mikononi mwa adui" Luteni jenerali aliuliza

"Ndio ndio lakini inashangaza taarifa zake ni raia wa kawaida tu, anaitwa Jimmy Julian Jairo ana miaka ishirini na mbili(22) amemaliza kidato cha sita mwaka huu na ana subiri kuanza elimu ya Chuo" Aliongea Jenerali Merizesta ilionekana alikuwa amepata taarifa kuhusu tukio la kujaribu kuwauwa watoto wake lakini hakuweza kufika nyumbani kutokana na majukumu ya kijeshi

"Hata hivyo ni Jambo la kushukuru pengine bila yeye wanao wangekuwa marehemu sasahivi"

"Hilo nashukuru sana ila huoni hili jambo lina mashaka ndani yake? Mtu wa kawaida asiye na rekodi yoyote kuweza kudhibiti majambazi wanne wenye siraha ambayo ni kazi ya walinzi wenye mafunzo na uzoefu lakini wameshindwa" aliongea Jenereli akimpatia faili Luteni Jenerali

"Haishangazi sana isitoshe baba marehemu yake pia alikuwa mwanajeshi pengine alimjenga mwanae kwenye mazingira kama haya" aliongea Luteni jenerali baada ya kumalizia kusoma faili na kugundua kitu

"Unataka kusema......." aliongea Jenerali akiishia njiani

"Ndio ukiangalia jina la baba yake unakuta ni Julian Jairo rafiki yetu aliyefariki miaka 15 iliyopita, Unamsahauje mtu muhimu kama yule ndani ya jeshi letu?" aliongea Luteni Jenerali na kumfanya sasa Jenerali kurejewa na kumbukumbu

"Asee uzee unanitafuna vibaya mno mambo ni mengi sana kiasi cha kusahau" aliongea Jenerali

"Unazingua sana mzee mwenzangu bila yeye nadhani tusingefika hapa tulipo" aliongea Luteni Jenerali

"Sema yule muhuni hakutuambia kama ana familia" aliongea Jenerali

"Yeah nilishangaa niliposikia jina lake ila inabidi tupate taarifa pia ili kudhibitisha itoshe kusema alijua kutuficha" Luteni Jenerali alidakia

"Hahaha si alisifika sana kwa kutunza siri ndio maana aliaminiwa sana na wakubwa kipindi kile lakini jambo la kusikitisha hatunaye tena"

°°°°°°°°°°

Muda ulikuwa umeenda sana na mpaka kufikia wakati huo saa ilisoma saa kumi na mbili dakika kumi tano, angani kulikuwa na wingu zito jeusi ikionyesha dalili ya mvua

Lilionekana gari jekunde maeneo hayo ya bagamoyo likikatiza sehemu isiyo na dalili ya watu kuishi wala mnyama kuonekana akipita

Ilikwenda kusimama sehemu yenye uwanja mkuubwaaa na Jimmy alishuka nje ya gari na kwenda kusimama mbele ya boneti la gari mkononi akishikilia kitabu.
Kwasababu ya giza na eneo hilo kutoonekana nyumba yoyote wala kifaa chochote cha umeme aliacha taa za mbele ya gari kumulika

Sekunde si nyingi zilisikika ngurumo la gari zikikaribia eneo hilo na kweli zilionekana gari nne nyeusi zote zikiwa SUVs na zilikwenda kusimama mbele ya macho ya Jimmy umbali kama wa mita thelathini hivi

Milango minne yote ya magari yale ilifunguliwa na walishuka watu kumi na nane wawili wakiwa ni ndugu zake jimmy mama yake na dada yake wamefungwa kamba mikononi na vitambaa machoni wasiweze kuona, wengine wote walikuwa ni raia wa kigeni wanaume kwa wanawake wakivalia nguo rangi tofaut-tofauti

"BOOM! BOOM... BROOOM!" sauti ya radi pamoja na mwanga mweupe ulimulika na mvua ilianza kunyesha

"Hatimae umefika kijana, mwisho wa siku udhaifu mkubwa kwa binadamu ni familia" aliongea mwanaume chotara mwenye asili ya kiarabu na kizungu kwa lafudhi mbovu

"Nimeshafanya kama mlivyotaka waachieni ndugu zangu" aliongea Jimmy

"Usiwe na wasiwasi kijana umefanya jambo zuri kuleta hiko kitabu hivyo tukabidhi ndipo tuwaachie"

"Nitaamini vipi maneno yako kama ni ya kweli naomba muwaachie kwanza ndipo niwape kitabu chenu isitoshe sina mpango wa kutoroka hapa" aliongea Jimmy na kumfanya mwanaume yule kutabasamu

"Kama nilivyosema kabla huwa naheshimu sana wanawake...." Aliongea mwanaume yule akiwapa ishara vijana wake wawili wasogee mpaka karibu na Jimmy wakiwa na ndugu zake kufanya mabadilishano na ndivyo ilivyokuwa Jimmy aliwakabidhi kitabu nao walimkabidhi ndugu zake

Jimmy baada ya kuwapokea mama na dadaye aliwafungua kamba na mikono na mara baada ya mama yake kumuona Jimmy ndiye aliyekuja kuwaokoa alitokwa na machozi ambayo hayakuonekana vizuri kwasababu ya mvua

"Mwanangu.....um..."

"Hapana mama huu sio wakati sahihi wa kuongea tutaongea tukiwa mahali salama" Jimmy alimzuia mama yake asiongee zaidi

"Monica unaweza kuendesha gari?" Jimmy aliuliza na Monica alitingisha kichwa kukubaliana nae, naye Jimmy alimpatia funguo

"Ondoka mahali hapa uende mbali na hapa mpaka uhisi upo salama"

"Vipi kuhusu wewe?"

"Wewe fanya kama ninavyokwambia... Ondoka mahali hapa, kuhusu mimi msijali nitatafuta namna ya kutoka hapa" aliongea Jimmy akiwafungulia mlango wa gari nao hawakuwa tayari kuondoka lakini Jimmy aliwalazimisha mpaka kuingia na kuondoka mahali hapo wakimuacha peke yake akiwasindikiza na macho mpaka walipotokomea hapo

"Ooh ni upendo ulioje, Inaonekana tayari ulishajua hatutakuruhusu uondoke hapa haha unanifurahisha sana kijana" aliongea mwanaume yule ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa kundi hilo la watu kumi na tano wanaume kwa wanawake, walikuwa miili iliyoonyesha wamepitia mazoezi makali sana na mafunzo

Jimmy aliishia kutoa tabasamu lenye uovu ndani yake alijiambia leo lazima atoke na roho zao wote, alijiambia kama kuua ni dhambi mbona dhambi anazo nyingi tu, Ieleweke kwamba jimmy katika maisha yake hakuwahi kutoa uhai wa mtu zaidi ya kushuhudia watu wakifa mbele ya macho yake na siku hio ndio ilikuwa mara ya kwanza kwenda kutekeleza mauaji, kama ni kwenda motoni siku ya kihama kwasababu ya hiyo dhambi alishaikubali hatima hio isitoshe hata kama asipoua motoni kunamuhusu kama kawaida. Kuna watu wengine hawafai kuwepo kwenye uso wa dunia ili kutosababisha matatizo zaidi

"wapuuzi kama nyinyi ndiyo mnatusababisha tuingie dhambini baada ya toba ya muda mrefu" aliongea Jimmy ambaye alikuwa ameloa chapachapa macho yake yakiwa serious

Interesting. You’re either fearless… or foolish. I just want to see how you defeated that bitch" aliongea mwanaume yule na kutoa ishara kwa vijana wake tayari kwa pambano

Kufumba na kufumbua maninja hawa hapa mbele ya macho ya Jimmy ulikuwa ni mshikemshike patashika nguo kuchanika, mapambano kwenye mvua weuweeee!! Ilikuwa ni hatari na nusu. Jimmy alikuwa akijitahidi sana kupangua mapigo na kushambulia lakini safari hii haikuwa rahisi kwake maninja hao walikuwa ni wabobezi zaidi ya wale wa mwanzo

Walikuwa wakitumia mbinu ya Shadow step na mbinu nyingine za kininja walikuwa kama wanapoteapotea na kuibuka angle tofauti tofauti kilichomsaidia jimmy ni mafunzo yake ya hisia vinginevyo angekuwa amejeruhiwa vibaya sana

Mapambano yaliendelea ndani ya dakika kadhaa na Jimmy aliona sasa asipofanya kitu muda si mrefu anaenda kuitwa Marehemu.

TO BE CONTINUED...............
 
By Samuel jk_Euphoria

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 9: "At least now I know what losing feels like"

Alijitahidi kadri ya uwezo wake kuweza kupambana nao lakini hali haikuwa shwari kibaya zaidi hakuwa na siraha ya baridi tofauti na wale maninja ambao wanatumia katana(upanga)

Japokuwa Jimmy alikuwa akijua mbinu nyingi za kimapigano ikiwema Ninjitsu lakini mbinu ya Shadow step hakuweza kuitumia licha ya kufundishwa na Mzee Momochi kifupi hakufanikiwa kui-master kutokana kutokuwa serious nayo, na kingine ni kukosa uzoefu wa mapambano. Kuna utofauti mkubwa kati ya mwenye uzoefu na asiye na uzoefu, ni bahati tu mpaka wakati huo alikuwa hai

"Shit!" Jimmy alimaka baada ya kuchaniwa shati lake

Jimmy alipoona anakwenda kuchoka na pambano kuelekea kumlemea aliwatoroka kiustadi sana kwa kujifanya anakwepa mapigo na alipopata nafasi alichomoka na kukimbilia upande wa yale magari waliyokuja nayo, Uzuri bado injini zilikuwa zinanguruma kuashiria bado gari hazikuzimwa

Aliingia kwenye SUV moja na kukanyaga pedeli na kwa spidi sana gari lilichanja mbuga nao hawakuzubaa walipanda yaliyobaki na kumfukuzia kwa nyuma, wahuni wanasema kuunga trela

Sasa ukawa ni mfukuzano wa magari kwenye barabara ya mchanga na majij yanayotokana mvua.

"Bang! Bang! Bang! Bang!" zilikuwa ni sauti za mirindimoya risasi mithili ya ngoma zikifyatuliwa kulenga gari alilopanda Jimmy

Jimmy kuona hivyo hakuona tena haja kuficha siraha yake ya moto aliongoze spidi kisha kwa ustadi alizungusha usukana kama anakata kona na kukaza handbrake kwa wakati mmoja na gari kwenda mtindo kama wakuzunguka na kupitia dirisha alitoa mkono nje wenye bastola na kufyatua kwa fujo kama zote

Ilikuwa ni shabaha ya hali ya juu sana alilenga matairi ya mbele gari mbili na zilipinduka kwenda hewani na kutua chini vibaya sana

Yote hayo alifanya gari likiwa linazunguka kama "merry-go-round" na alipeleka mkono wake kwenye gia na kubadili level D kwenda R na sasa gari lilianza kurudi nyuma kwa spidi uso kwa uso na gari lililokuwa mbele yake lililobaki kumfukuzia

Jimmy na dereva ambaye alikuwa ndio kiongozi na maninja wengine walioko ndani yake walikuwa wakitazamana tu wakiwa kwenye mwendo basi yakawa ni majibizano ya risasi baina ya gari mbili zilizokuwa uso kwa uso zikieleke direction moja, jimmy akiwa kwenye Reverse(gori kwenda kinyumenyume)

Mpaka risasi zinakuja kuisha hakuna iliyompata yeyote.
Kupitia kioo cha mbele Jimmy aliweza kuona nyuma yake kuna mti mkubwa na palepale aliangalia juu ya gari lake na kutabasamu. Ni jopo(panel) la paa juu ya gari ambalo linaweza kufunguliwa kwa mkono au kitufe ili kuingiza hewa ndani

Alibonyeza kitufe na "Sunroof" ya gari hilo kufunguka na kisha kubonyeza kitufe cha "Self drive" na kutokea kwenye dirisha hilo na kusimama juu ya kali huku gari likiwa kwenye mwendo na alijirusha chini akijitahidi asitue vibaya na kuishia kuumia

Wakiwa wanashamshangaa anafanya nini ndio wanakuja kugundua kwanini alijitupa nje ya gari lakini walishachelewa ni boss wao pekee ndiye alishtuka mapema na kuchukua harua

Gari alilopanda jimmy lilikwenda kugonga mti kwa kishindo kikubwa na gari la maadui pia lilikwenda kugonga gari hilo kwa kishindo na kusababisha mlipuko "KABOOM!!"

"Asee huku ni kujitakia kifo sasa" Jimmy alihema kwa nguvu baada ya kutua chini kidogo avunje shingo na kujiongelesha

Upande wa boss chotara naye alikuwa mzima kwani naye alijirushi kupitia mlango wa gari na sasa wakawa wanatazamani

Yalikuwa ni macho yasiyokuwa yakiongea lugha isiyoeleweka ukijumlisha na mvua inayowanyeshea ilikuwa ni balaa

"Young man! I must say you really impress me, that bastard was insightful for sure" (Kijana! Niseme tu unanivutia, yule mshenzi alikuwa na macho kwelikweli) aliongea Boss chotara

Sitaki kusikiliza ngojera zako we chotara na sijui kwanini unaking'ang'ania hiko kitabu kisicho na maandishi yoyote, mi sijali ninachojali nikukupeleka kuzimu"

"Lets see who will be the first to go then!" Aliongea boss chotara na kufumba na kufumbua alikuwa karibu na Jimmy akisindikiza na teke matata sana la roundhouse kick ambalo Jimmy aliweza kulipangua vyema

Walikuwa wakipigana kwa kurusha ngumi na mateke yasiyo na mpangilio maalum yaani ni kushambulia na kupangua mfululizo bila kupumzika

Ukisikia "face to face Combat" ndio huku sasa, walizichapa kisawasawa wakibadili staili mbalimbali za kimapigano kwa takribani dakika kumi bila mshindi kupatikana, kifupi walitoka draw

Mvua nayo ilikata muda huo na kufanya kuwe na hali ya ukimya zaidi, wawili hao wakiangaliana kwa umbali kama wa mita tano kwenye giza la usiku huo uliosaidiwa na mwangaza hafifu wa mbalamwezi, sauti za pumzi zao wakihema zilisikika masikioni mwao

Kila mmoja aliangalia pembeni kwake kushoto, ni wazi walikuwa wakitafuta siraha
Upande wa Jimmy upande wa kushoto kwake kulikuwa na kile kitabu pamoja na mti wenye urefu wa meter mbili ilionekana kitabu kile wakati boss chotara akijiokoa kwa kujitupa kilidondokea mahali hapo

Upande wa kushoto wa boss chotara kulikuwa na upanga ulio chini na palepale kila mmoja alikimbilia upande wake, Jimmy alikuwa na spidi ndogo kutokana na kuchoka kwake lakini kwa boss chotara ninja mzoefu alikuwa tofauti na mwenye spidi

Wakati jimmy anaukaribia mti na kutaka kuuokota alishtuka upanga ukitokezea mbele ya tumbo lake na damu kuanza kumtoka mdomoni na tumboni upanga ulipotokelezea na alianguka chini na damu zilimwagikia kitabu kile kilicho karibu yake

Ilionekana boss chotara baada ya kuufikia upanga ule alitrtsha dizaini kama mkuki na shambulio lake kufankiwa

"Damn... That actually hurts...... But hey, at least now I know what losing feels like... Might as well return the favor soon." aliongea jimmy kwa sauti ya chini sana akiugulia maumivu kwa lugha ya kiingereza akimaanisha kwamba inauma sana lakini vilevile alielewa hisia za kushindwa

"Still trying to act tough? Just stay down and die slowly" aliongea boss chotara akimaanisha "Bado tu unajikuta mgumu? Tulia chini ufie taratibu"

"No.... I can't die here… Not to you… Not today." (Hapana... Siwezi kufia hapa... Sio kwako... Na sio leo) aliongea jimmy huku akijitahidi kuinuka bila mafanikio kutokana na maumivu makali

"You already lost" aliongea boss chotara na kuchomoa upanga ule na kuzidi kumwagika kwa wingi

"Hapana... hapana... Sipaswi kufa kuna.. Wananisubiri" Jimmy alijiongelesha huku macho yake taratibu yalianza kujifumba bila hiari yake

Sekunde ambayo macho yake yanajifunga ghafla kitabu kile kilianza kuelea hewani kama puto huku kikitoa mwanga wa rangi mbalimbali kwa kubadilikabadilika

"What the hell is happening here?"(nini kinaendelea hapa) boss chotara alishangaa kuona tukio hilo

"Aargghh ***! " alipiga makelele ya maumivu baada ya kukishika na mkono wake kuungua

Alibaki akikishangaa tu bila ya kufanya chochote na zile rangi zilisafiri na kwenda kuingia kwenye mdomo wa Jimmy na kitabu kikapotea kichawi

Mara ghafla ilisikika milio ya defenda za polisi ikikaribia eneo hilo na boss chotara alijiongeza na kutokomea kwenye miti akielekea kusikojulikana.

°°°°°°°°°°

Kwenye hospitali kubwa nchini, Hospitali binafsi yenye majengo matatu yote yakiwa ni maghorofa yaliyotofautiana urefu, ilikuwa ni hospitali yenye hadhi ya kuitwa hospitali ya matajiri kutokana na ufahari wake

Licha ya hivyo haikubagua mwenye uhitaji kama ni tajiri au lah, ilimradi pesa unayo utapatiwa huduma ya kiafya kulingana na hadhi yako

Sasa katika chumba kikubwa cha wagonjwa maalumu(VIP) chenye hewa safi ya kiyoyozi alionekana mwanaume amelala kwenye kitanda cha mgonjwa, alikuwa kwenye usingizi mzito

"aahh!!" alishtuka kwenye usingizi huo kana kwamba amemuona shetani ndotoni akiwa bado amelala vilevile, na sauti yake ilimshtua pia mtu aliyekuwa pembeni yake amelala kwa kuketi kwenye kiti huku kichwa akikilaza kitandani karibu yake

"Umeamka!" ilikuwa ni sauti ya kike ambayo ilikuwa ni tamu sana kama asali masikioni mwa mwanaume yeyote rijali

Alikuwa ni Bianca mrembo ambaye ni rafiki mpya wa Jimmy, alinyanyuka haraka na kutoka kumuita daktari.

Upande wa Jimmy alikuwa akijishangaa na kushangaa eneo hilo akijiuliza yupo wapi. Alinyanyuka na kukaa taratibu na kukaa kitako na alijishangaa kujihisi mwepesi mno kuliko kawaida, wakati anajishangaa ghafla kumbukumbu za kilichomtokea zilianza kumjia, kutoka kuchomwa mpaka kufumba macho
Alijipapasa tumboni alipochomwa na kukuta hakuna kitu wala maumivu yoyote na alijishangaa sana na kutaka kujua nini kilimtokea na kwanini yupo hapo na hapo ni wapi

Mlango ulifungulia aliingia daktari akifuatwa na watu wengine nyuma yake, daktari huyo alishalienda moja kwa moja na kumfanyia vipimo na baada ya kuridhishwa aliwapa taarifa kwamba mgonjwa wao yuko sawa kabisa na ndani ya wiki ataweza kuruhusowa kuondoka akiwa na afya tele

"Ebu subiri nini kimenitokea na kwanini niko hapa?" Jimmy alouliza

"Ulipatwa na ajali ndogo tu na ulikuwa kwenye Coma kwa siku kumi ila usiwe na wasiwasi nimefanya vipimo na kukuta uko sawa" aliongea daktari akimweleza kwa ufupi na kumtoa wasiwasi

Coma ni ile hali ya kutokuwa na fahamu kwa muda mrefu na kuonekana kama umelala usingizi, mara nyingi husababishwa na majeraha ya mwili na baadhi ya magonjwa

"Nini? Siku kumi?" alipigwa na butwaa kama haamini hivi na kuwageukia watu waliokuwa nyuma ya daktari

Walikuwa jumla yao ni watatu, Mama yake, dada yake pamoja na Bianca
Mama yake baada ya kumuona Jimmy alibubujikwa na machozi kama bomba la maji haikueleweka kama ni machozi ya furaha kwa mwanae kuamka kutoka kwenye Coma, usingizi wa muda mrefu au ni kitu kingine.

Mama yake alimsogelea jimmy karibu yake na kumshika mabegani kwa mikono yake miwili

"Mwanangu unataka nife kwa mshtuko wa moyo?"

"Hapana kwanini wasema hivyo"

"Kwasababu umeniogopesha mno nimempoteza baba yenu sitaki nikupoteze na wewe hivi unajua ni maumivu kiasi gani nilipokuona kule msituni nikajua umekufa" aliongea mama huyo akimuelezea jimmy alipomkuta amelala chini kama mfu na damu kuonekana mwilini mwake

Wakati mama yake pamoja na dada yake walipookolewa mikononi mwa adui na walienda kuita polisi mpaka kuja maeneo yale lakini walichelewa na kukuta ajali mbaya zilizotokea pamoja na mwili wa jimmy ukiwa chini ya ardhi

Monica alipouona alianguka chini na kulia kwa uchungu sana pamoja na mama yake. Kwa jinsi damu zilivyonyingi pamoja na ajali walizoshuhudia walidhani jimmy amefariki pia. Waliogopa hata kusogelea mwili wake

Ndipo polisi katika kukagua miili yote waliweza kugundua mwili wa jimmy bado ulikuwa na uhai baada ya kuweka kidole karibu na pua kusikilizia pumzi na walibaini bado akipumua tena hali ya chini sanaa na ndipo sasa kuuwahisha katika hospitali ya karibu ya maeneo yale kupata huduma ya kwanza kabla ya kuuhamisha hospitalini hapo ambapo malipo yote yalifanywa na Bianca baada ya kupata taarifa kupitia Monica

"Nisamehe sana mama yangu kwa kuwafanya mjihisi vile wewe pamoja na Monica nilikuwa nikihakikisha mnakuwa salama"

"Sawa mwanangu muhimu upo salama na ni jambo la kushukuru, hayo mengine yashapita" aliongea mama yake jimmy akimkumbatia mwanae

Upande wa monica alikuwa mpole, hakuwa yule monica mkorofi hapo alikuwa ni dada anayemjali mdogo wake, naye taratibu aliungana nao kwenye kumbatio la kifamilia

Bianca alikuwa akitabasamu pembeni akishuhudia familia hiyo ikiungama.

Mara mlango ukafunguliwa na aliingia mtu mwingine mwanaume naye hakuwa mwingine bali ni Cid na kifanya wanadamilia watatu hao kusitisha kumbatio na kugeuza macho yao

"Nimeingia muda mbaya eeh?" Aliuliza

"Hapana umefika wakati sahihi ndiyo ametoka kuamka kutoka kwenye Coma" aliongea mama Jimmy

"Bro umetutisha sana asee hizi siku kumi za usingizi wa pono si ndogo tulidhani utachukua zaidi ya mwaka maana Coma si lelemama" aliongea Cid kirafiki akitabasamu

"Hata hivyo ni jambo la kushukuru, huyu dogo hapa kila siku alikuwa anakuja kukuangalia pamoja na ndugu zako" aliongea Cid na kumfanya Bianca mashavu yake kuwa mekundu kwa kuona aibu na kuangalia pembeni

Jimmy alimwangalia Bianca na kutabasamu kisha akamgeukia Cid na kuongea

"Yeah, ni jambo la kushukuru"

"It's good to be back man" alijibu Cid na kukumbatia kishkaji

Mara ilisikika ngurumo ya helicopter masikioni mwao na kupitia dirishani waliweza kushuhudia helicopter nyeusi aina ya Bell 525 Relentless ikitua kwenye uwanja mkubwa uliokuwa katikati ya majengo ya hospitali hiyo

Bell 525 Relentless ni helikopta ya ukubwa wa kati iliyoundwa kwa ajili ya usafiri wa watu mashuhuri (VIP), operesheni za mafuta na gesi baharini, uokoaji (SAR), na huduma za matibabu ya dharura (EMS). Ina teknolojia ya hali ya juu na injini zenye nguvu.

Mara baada ya kushuhudia helicopter hio Cid na Bianca walishusha pumzi ndefu ikionekana wanajua nani amefika hapo

Dakika chache mbele mlango ulifunguliwa na aliingia mwanaume mzee aliyevalia gwanda lililochafukwa na vyeo nyuma yake kukiwa na wanajeshi watatu wa ulinzi wanaoambatana nae

Hakuwa mwingine bali alikuwa ni Jenerali Johnson Merizesta

"Baba!" aliita Bianca na kwenda kumkumbatia huku upande wa kina Jimmy wakikodoa tu macho na kujiuliza mwanajeshi huyo amekuja kufanya nini hapo na kushangaza zaidi neno "Baba" lilimaanisha huyo ni baba yao mzazi

Upande wa Cid ilikuwa ni tofauti kabisa na dada yake. Alikuwa ametulia tu na sura ya kikauzu isiyo na hisia zozote zile ni wazi kwamba hakupatana na Baba yake

"Kijana, hujanimisi baba yako?" aliongea Jenerali Johnson Merizesta

"Sikujua kama nilikuwa naye" alijibu Cid kikauzu

TO BE CONTINUED..............
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom