bioto
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 1,261
- 2,099
..WIMBO WA AJABU ..
SEHEMU YA KWANZA.
¶¶¶Wanakandia,Wanapondea wanadhani
watafanikiwa¶¶¶. ¶¶¶Nimeshajua,Janet wangu,Ni
bora tufunge ndoa¶¶¶. ¶¶¶Sema basi laazizii,Sema
mpenzi, Nikilala usingizi,Nakuota kipenzi¶¶¶.
¶¶¶Lazizii,Sema basi kipenzi, nikilala isingizi
Nakuota mpenzi¶¶¶.
Chorus. ¶¶¶Janet nampenda,Janet wangu sana, Kuna
watu wanabana, Ni siishi na huyu kimwana,Na bado
nawaambia,Milele hatutaachana, Hatuta tengana iwe
kufa na kuzikana¶¶ Usingizi uliniishia huku nikiwa
nimeiota tena nyimbo hii ya ajabu ambayo
sikuitunga bali kila nikilala inanijia na kuiota
namuimbia mrembo nisiyemjua ndotoni.
Mara nyingi nilikuwa namkimbiza huyo mrembo
ndotoni huku nikimuimbia huyu mrembo hiyo
nyimbo ambaye nilikuwa simtambui ninani na
anatokea wapi. Basi niliamka na nikaipuuza hii
ndoto tena licha ya kujirudia zaidi ya mara tatu.
Nikachukua mswaki wangu na kupiga fasta kisha
kujiandaa kwenda shule.
Kilikuwa ni kipindi karibia na mitihani ya kidato cha
sita huku nami nikiwa ni miongoni wa watahiniwa
wa hiyo mitihani Ila ghafla nimejikuta naiogopa sana
mitihani hii inayokuja ya kidato cha sita kutokana na
majibu ya kukatisha tamaa ya mock. Nisiwafiche
wadau mock nilipata zero hili jambo linanitisha sana
kwasababu kidato cha sita PCM sio sawa na kidato
cha nne kwani mpaka nimefika hapa wadau kidato
cha nne nilipata one ya point Saba lakini hapa
mambo yananiendea vibaya.
Basi siku hiyo ilibidi niwahi shule ili nikajisomee
zaidi na zaidi walau kujinusuru na hili janga. Nilifika
shuleni nikakutana na rafiki yangu anaitwa Salehe
nilitamani tukajadili naye kidogo maana jamaa
mock alipiga two. "Salehe vipi mshkaji"
Nilimsalimia Saleh ambaye alionekana kashika
daftari na peni anaelekea maktaba kujisomea. "Poa
,Vip Musa".
"Safi ,unaelekea wapi". "Library (Maktaba)". "Jana si
uliahidi tutadiscus(Tutajadili) physics Leo".
"Tutadiscus au mnataka niwafundishe mbona mi
sioni mtu wa kudiscus naye kwenye group letu wote
ni maziro tu nyi mnataka niwavute mpaka kwenye
four mpate vyeti alafu mi nipolomoke mpaka
kwenye three nikose mkopo". Saleh aliongea kwa
dharau sana.
"Mmh,Saleh mambo gani hayo , ukidiscuss ndo
unagain zaidi". "Ukidiscuss na watu wenye akili sio
na vilaza kama nyie mtanipumzikia tu" Basi Saleh
alisema maneno hayo kisha kuondoka na kuniacha
nimeduwaa tu. Basi hakuna noma kwakuwa group
letu tuko sita na Salehe peke yake ndo hayupo basi
acha niende kudiscus na washkaji wengine. Basi
nikapandisha mpaka kwenye darasa tuliopanga
kukutana. "Afadhari Musa umefika" John mmoja wa
washkaji zangu alinipokea na kuniingiza moja Kwa
moja kwenye ubishi waliokuwa wakibishana na
mwenzake Nashon. "Eti ,Messi na Ronaldo nani
mkali".
John alinipa mada ya ubishi moja kwa moja mara tu
baada ya kufika . "Mi naona Messi ni mkali".
Nilijibu. "Mkali wapi mtu mwenyewe ahami timu sio
kama fighter Ronaldo". "Kuhama timu sio hoja
Messi kwenye magoli anashindana na
Ronaldo,Suarez na Rwewandoski, Assist
anashindana na Ozil na Di Maria, Dribble
anashindana na Neymar na hazard kwahiyo Messi
anavitu vingi tofauti na Ronaldo".
"Vitu vingi wapi niambie Mesi anataji gani timu ya
Taifa" Alisema Nashon nami nikaona ubishi utakuwa
hauishi hapa ikabidi nivunje mada. "Hoya washkaji
tuacheni maswala ya Ronaldo na Messi vipi kuhusu
discussion Leo". "Tutadiscus nini wakati Saleh
hayupo" Aliongea Nashon "Sasa kama hayupo si
tunadiscus wenyewe"Nilijaribu kuwashauri washkaji
lakini washkaji hawakunielewa wakaendelea
kusisitiza discussion haiwezi kuwepo kwasababu
Saleh hayupo na tuliopo hapo wote ni vilaza hivyo
hatuna cha kudiscuss sanasana tutapotezeana muda
kama vipi kila mtu ajisomee peke yake .
Hii rai ya kila mtu ajisomee peke yake ndo ilipita
hivyo kila mtu akawa anajisomea peke yake lakini
bado Nashon na John waliendelea kubishana
kuhusu Ronaldo na Messi mimi nikaona hilo eneo
sio sahihi Kwa kujisomea Basi ikabidi nitoke
darasani na kwenda kutafuta mahali patulivu zaidi
kwaajili ya kujisomea, Sikutamani kwenda library
(Maktaba) maana kule kuna washkaji wengine
wakikuona wanaanza kuongea maneno ya ajabu
"Eehee mpaka Musa Library Leo kulikoni au ziro
imemnyoosha?".
Basi ikabidi nielekee sehemu ya uwanja wa shule
ambapo kulikuwa na mbuyu mkubwa pia kulikuwa
na utulivu wa kutosha kwani shule nzima tuko sisi
kidato cha sita,Kidato cha tano wamefunga
kutupisha sisi kwaajili ya mitihani kwani ni wiki
moja tu mitihani inaanza na shule yetu haina oleval
(1-4) . Hivyo eneo la uwanjani lilikuwa tulivu zaidi
kwasababu hakuna hata mwanafunzi mmoja
maeneo hayo. Basi mi nikasogelea eneo la mbuyu
pale uwanjani ili kupata kivuli jua lisinipige wakati
najisomea.
Nilifika eneo lile na nikaanza kujisomea mara ghafla
nikaanza kusikia ule wimbo ukiimbwa tena. ¶¶¶
Sauti nzuri,Kama ya gita, hiyo inakuita, Taratibu uje
kwangu,Uje bila kusita¶¶¶. ¶¶¶Sema basi lazizi,Sema
basi kipenzi, Nikilala usigizi nakuota kipenzi ,lazizi
sema basi kipenzi,Nikilala usingizi nakuota
kipenzi¶¶¶. Nilishtuka Kwasababu wimbo huo huwa
nausikia ndotoni iweje uimbwe live ,Nani anauimba
huu wimbo live wakati sio wa msanii yeyote
ninayemjua mimi. Nilishtuka sana nakuanza
kuogopa ikabidi ninyanyuke kuelekea eneo
linaloimbwa hiyo nyimbo. ***...