Simulizi: Wanawake ni wauaji

Simulizi: Wanawake ni wauaji

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Posts
17,177
Reaction score
34,444
WANAWAKE NI WAUAJI
Mtunzi/mwandishi HUSSEIN BAKARI
MTOTO WA BECKER
mtotowabecker@gmail.com
0713 46 26 29
_________________
EPS 01
========

********

“Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa pumzi na afya njema hadi leo hii niko hai japo niko tofauti sana na nilivyokuwa awali hata wasionijua wakiniona hii leo watadhani nilizaliwa hivi. La hasha! Ila leo nitawaambia ukweli wa yote yaliyonisibu na yanayowasibu wanaume wengi katika dunia hii ya leo. Nakumbuka zamani babu aliwahi kuniambia niwe makini sana na wanawake pindi nitapokuwa mkubwa.

Na alinisihi ya kwamba niwaelewe wanawake ni watu wa aina gani na jinsi ya kuishi nao. Lakini sikuwahi kuamini maneno yake hadi yalipokuja kunisibu na ndipo nilipokumbuka na kuelewa kwanini babu alinisihi vile. Aaaaagh! Wanawake ni mama zetu na ni pambo la dunia na ndio maana Mungu aliwaumba ili watufariji na watulee, lakini ukweli bado unabaki kuwa wanawake ni watu hatari sana kwetu wanaume.

Hebu tukumbuke hata kwenye hadithi za watu wa kale kwenye vitabu vya dini tukianzia mwanzo kabisa wa dunia enzi za Adam na Hawa/Eva. Adam alitii kila kitu katika mamlaka aliyopewa na Mungu lakini mwishowe alikuja kumkosea Mungu kwa kutenda dhambi aliyoponzwa na mkewe (Hawa/Eve) mara baada ya kushawishiwa na Shetani, Eeeh, amini usiamini shetani ni vigumu sana kumuingia mwanaume hivyo anamtumia mwanamke kama alivyomtumia Hawa/Eve kwenda kumlubuni mwanaume kama alivyolubuniwa Adam na kujikuta mwanaume anaumia kwaajili ya upendo na kumuamini sana mwanamke pasi na kuelewa kiundani udhaifu mkubwa wa mwanake mwenyewe.

Tuachane na Adam, tukumbuke Samson mtu mwenye nguvu aliyewapa tabu sana Wafiristi enzi hizo lakini mwishoe anakuja kukamatwa na kupata mateso makali baada ya kulubuniwa na Delila aliyetumiwa na Wafirist kubaini siri za nguvu za Samsoni. Eee, Samsoni nae aliponzwa kwa ajili ya mwanamke, na si yeye wala Adam tu tukumbuke hata mtu wa kwanza kufa alikuwa ni mwanaume na sababu ya kifo chake kilitokana na mwanamke!!

Eeeh ni wanaume wengi mno wameponzeka kwaajili ya wanawake na mmoja wao ni mimi na ndio maana leo hii nasema wanawake ni wauaji. Najua wengi mtanielewa vibaya hususani wanawake, lakini naomba msizime tv zenu ama radio ili mnielewe vizuri kwanini hasa nimekazania kusema Wanawake ni Wauaji? Hii ni asili iliyoanza toka kwa mwanamke wa kwanza kabisa kuumbwa na bado ipo na itakuwepo na itawaumiza wanaume wengi sana wasiokuwa makini na ndio maana hata Mungu hakuwahi kushusha nabii wa kike.

Wanawake ni wadhaifu wasiokubali udhaifu wao na ndio maana nawaita Wauaji. Achilia mbali vitabu vya dini tukija kwenye maisha yetu ya kila siku lini ulishawahi kusikia mwanaume katupa katoto kachanga? Naamini kama mimba wangekuwa wanabeba wanaume usingesikia neno kutoa mimba.

Hivi ushawahi kujiuliza mwanamke ana moyo wa namna gani hadi anadiliki kukiua kiumbe alichokibeba tumboni miezi tisa na kujifungua kwa uchungu?!! au unadanganywa na maumbile yake na sauti laini unajisahau na unaacha kuwa makini nae? hivi hujui kwamba simba dume ana muungurumo mkubwa sana lakini jike ndiye jasiri wa kuua. Huo ni mfano tu lakini nataka unielewe na uwe makini kwanini nasema WANAWAKE NI WAUAJI..”

Ilikuwa ni sauti ya bwana mmoja mlemavu wa macho na miguu akiongea luningani katika kipindi cha YA WALIMWENGU LIVE kilichokuwa kinarushwa kupitia kituo cha BECKER TV kila siku za jumapili asubuhi na marudio yake ilikuwa jumamosi jioni.

Nilikaa kwenye sofa kwa hamasiko. Macho na masikio niliyatupa luningani huku mkono mmoja nikiwa na kikombe chenye chai na mwengine ukiwa na rimoti nikiongeza sauti ya luninga. Mada ya yule bwana ilinistua na kunigusa sana hali iliyochochea niwe na shauku kubwa ya kumsikiliza ili nimuelewe vizuri kwanini anasema wanawake ni wauaji.

Nilitulia na kujikuta nashindwa hata kupiga funda moja la chai na kubaki nimekishikilia kikombe kwa kumakinika na yule bwana alipokuwa anazungumza ambapo aliendelea kwa kusema......

“Nakumbuka miaka kumi iliyopita nilikuwa na maisha mazuri kabisa ya furaha, mimi na mke wangu kipenzi baada ya kufunga ndoa. Kiukweli nilimpenda sana mke wangu nae alinionesha mapenzi hasa na kunisahaulisha maumivu niliyopata kutoka kwa mke wangu wa kwanza tuliyeachana muda mfupi tu baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka mitatu na kuanza visa vilivyosababisha nimuache aishi maisha aliyotaka yeye na ndipo baada ya miezi kadhaa nilipompata huyu mwanamke wangu mwengine aliyeonesha kuwa na vigezo vyote nilivyohitaji na mwaka mmoja tu katika mahusiano yetu tuliamua kufunga ndoa kabisa.

Kiukweli mke wangu nilijivunia uzuri aliokuwa nao upole wake na tabia ya kupenda ibada. Na mara nyingi alinibadilisha kwa maneno matamu na kunisihi niache kunywa pombe, na kweli ilifika kipindi niliacha pombe na taratiibu nilipunguza kabisa kuvuta sigara kutoka pakiti moja kwa siku hadi ikafika mahali siku nzima nikavuta sigara mbili tu, hali iliyofanya hadi walionijua kunishangaa na kumsifu sana mke wangu na ndipo nami nilizidisha moyo wa kumpenda na kumpa uhuru wa kila kitu kwani nilimuamini mno…!” Alinyamaza kisha aliendelea…….

“Kila nilichofanya nilihakikisha lazima mke wangu ajue na nilisikiliza sana na kufata ushauri wake kuliko mtu mwengine. Akisema nisifanye kitu fulani nami nilitii, akisema nifanye nami nilitii, hiyo yote nilifanya nikiamini namjenga na kumuonesha kiasi gani namthimini bila kujua kua kuna ugonjwa m baya nilikuwa naufuga.

Awali sikuona tofauti yoyote wala kuhisi kama kuna kitu nakosea zaidi nilianza kusikia minong’ono kutoka kwa majilani na baadhi ya ndugu zangu kuwa napelekeshwa na nimetawaliwa na mke wangu. Kiukweli nilichukizwa na habari zile na kugombana na baadhi ya ndugu zangu waliomsema vibaya mke wangu nikiamini fika wanataka watugombanishe na wananionea wivu kwa kupata mke wa namna ile kwani maisha yetu yalizidi kunyooka siku hadi siku.

Aaaaaagh.. kuna muda huwa nahisi kama ndoto vilee kwani sikujua kabisa kumbe kuna bomu nalitengeneza mwenyewe ambapo baadae litapolipuka litaniletea madhara makubwa na kama si kuniua basi litanipa ulemavu wa kudumu kama ilivyotokea baadae…. Aaaagh, mke wangu!!!...”

Alivyozidi kuongea ndivyo nami nilivyozidi kutulia kumsikiliza kwa umakini huku nikibofya bofya rimoti kuongeza sauti mara kwa mara utafikiri nilikuwa na ubovu wa masikio. Nilimuangalia kwa jicho la shauku ya kujua yaliyomsibu. Uso wake wa jitimai ulitia huruma ukichochewa na ulemavu uliobeba tafsiri ya mazito yaliyomsibu. Kiu ya kujua ilikuwaje ilizidi kuniparua milango yangu ya fahamu. Lakini kabla sijafaidi vizuri hadithi ya yule bwana mara umeme ulikatika na kila kitu kuzimika.

“Aaaagh, Tanesco bwana kama maboya!!!”
Nilinyanyuka kwa hasira kuzima kitufe cha luninga na kuwasha kile cha taa ili umeme utaporudi tu, taa inijulishe mapema.

Wakati huo ile chai kikombeni ilikuwa ya baridi kabisa na sikuambulia kunywa hata chembe. Nilienda imwaga na kurudisha kikombe kabatini na ndipo nilipoikumbuka simu yangu niliyoiacha chumbani kwenye chaji. Haraka niliiendea na kukuta ikiwa na ‘missed calls’ tisa ‘sms’ nne. Nilipofungua zote zilitoka kwa mtu mmoja. Mtu ambae alikuwa zaidi ya uwaridi moyoni mwangu. Mwanamke wa ndoto zangu ambaye tulikuwa na miadi ya kukutana wikiendi hiyo ili tufurahi pamoja. Huyo alikuwa MARIAM ama MAMU kama nilivyopenda kumwita.

Nilizisoma zile ‘sms’ ambapo mojawapo iliandikwa hivi…
MBONA HUPOKEI SIMU WALA HUJIBU MSG ZANGU? KAMA UPO NA MALAYA WAKO SI UNAMBIE TU NISIJE..!!
“hahaa Mamu bwana..”

Nilijisemea moyoni na kuingia sehemu ya ujumbe kujibu lakini kabla sijabonyeza kitufe cha kutuma ujumbe, mara mlango wa sebuleni uligongwa kwa rabsha. Nilipouendea kabla sijaufikia, ulifunguliwa na mgongaji aliyeingia akiwa kashiba ununo. Alikuwa ni Mamu kipenzi changu. Nilifurahi nilipomuona nilimkumbatia na kum-busu lakini aliitoa mikono yangu kiunoni mwake na kunisukuma pembeni huku akiingia na kunipita bila kusema chochote na kwenda kukaa sebuleni.

Nilibaini kuwa amekasilishwa kutokana na kutopokea simu yake na nilijua sasa nina wajibu wa kum-bembeleza ili nimuweke sawa. Nilimjua kipenzi changu ni chakudeka, nami kwa huba nilimdekeza.
“Unakunywa nini bebi” nilimuuliza kwa sauti ya mahaba.

“Sitaki kunywa chochote niache.” Alijibu kwa hasira huku akipandisha miguu sofani na kubetua midomo huku uso wake akiuelekezea pembeni.
Hali ile ilizidi kunihakikishia kuwa nina shughuli pevu ya kubembeleza mtu mzima sasa. Lakini kabla sijafanya hivyo mara taa ya sebuleni iliwaka na ndipo nilipokumbuka kuwasha luninga kwanza niendelee na kile kipindi huku moyoni nikiwa na shauku Mamu nae amsikie yule bwana juu ya hadithi yake iliyowatuhumu kuwa wanawake ni wauaji.

Lakini lol! Mada ya yule bwana hasa kauli yake ya kuwa wanawake ni wauaji ilimchukiza zaidi Mamu na kuamua kuzima luninga kwa hasira.
“Aaag! Wee vipi?” nilitahayuri.
“Vipi nini!!?” Alinijibu kwa kuniswalika.
“Si uache tuangalie sasa unazimia nini?!”
“Hivi Hussein kwa akili zako timamu unaona hiki kitu anachokizungumza huyu mpuuzi ni sahihi!!”
“Kitu gani..?”

“Kusema wanawake ni wauaji.!!”
“Mh! hapo kumjaji moja kwa moja itakuwa ngumu, sasa nitamjaji vipi wakati hata hadithi yenyewe sijaisikia!! anaweza kuwa sahihi au si sahihi inategemea na point zake mwenyewe.”

”Hee! hivi nyinyi wanaume mpoje!!!” Aliwaka Mamu kwa sauti ya juu na kusimama huku akinitazama kwa hasira. Alihema juu juu na kuzidisha povu akinguruma kama moto wa kifuu.

“Hivi mnatuchukuliaje sisi wanawake eeh!!?”
“Kivipi baby.. mbona tunawakiana sasa.”
“Sio Nawakaa.. ila nakwambia ukweli acha kuwa na mitazamo ya kijinga au ndio kashakulisha ujinga huyo mpuuzi mwenzio…! Kwa hiyo na mimi muuaji si ndio, au unanionaje!!”

“Hapana baby sijamaanisha hivyo..”
“kumbe unanionaje..!”
“Unaweza kuwa muuaji au si muuaji inategemea tuu.”
“Aahaa.. kwa hiyo hadi mamaako aliyekuzaa muuaji, dada zako wauaji, shangazi zakoo si ndio..!”
“Sasa Mamu hayo matusi..”

“Matusi nini.. si wanawake ni wauaji! We vipi..?! Hebu nipishe huko nisije nikakuua buree..”
Alichukua mkoba wake kishari pale sofani kwa hasira Mamu alielekea mlango wa kutokea ulipo na kutoka huku akiubamiza kwa nguvu.
“Aaagh!! Sasa huo mlango umekukosea nini..!”

Nilibaki nimebumbazika pale kwenye kiti huku nikiwa nimechanganyikiwa kwa jinsi Mamu alivyonibadilikia siku hiyo kuliko siku zote. Hakuwa cha kudedee tena bali alikuwa mbogo. Nilijilaumu kidogo kwa kubishana nae punde alipozima luninga na kumsababishia mpenzi wangu kuwa na hasira mara tatu zaidi alivyoingia. Niliuendea mlango na kuokota funguo zilizodondoka pindi ulipobamizwa kisha nilirudi na kujitupa kwenye sofa huku akili yangu ikiwa imecheza makida.

Niliiwasha tena luninga safari hii nikiwa sina shauku kabisa wa kuangalia kile kipindi ambacho ndio kilikuwa kinaishia lakini kuna maneno ya mwishoni ya yule bwana yalipenya vizuri masikioni mwangu na kukistua kichwa changu kidogo pindi aliposema.

“Najua wanawake wengi wataobahatika kunisikiliza na kunitazama watanichukia na kuona nimewadhalilisha na kuwatusi. Nami sitoshangaa wala kuogopa hilo kwa sababu najua kuwa wanawake tayari wana ulemavu wa asili ambao Mungu aliwaumba nao kwa dhumuni la kuwa wasaidizi na wafariji kwa wanaume tu.

Mwanaume hajaumbwa kwaajili ya mwanamke ila mwanamke aliumbwa kwaajili ya mwanaume na ndio maana tunaambiwa kuwa mwanamke ametoka ubavuni kwa mwanaume. Lakini udhaifu wao ndio unafanya tuone mpaka leo hii wanawake wakitaka kushindana na wanaume wakisahau kuwa mwanaume ni wa kwanza tu kiasili.

Na hii inatokana na kuwa mwanamke ni rafiki mkubwa wa shetani anayetumiwa katika kuiharibu dunia na hata baadhi ya wasomi wa dini kiimani wanatwambia wanawake wengi sana wataingia motoni.

Mungu ameweka mifano mingi sana ya wazi kuwakumbusha wanawake kuwa mwanaume ni kiongozi na anapaswa kunyenyekewa na mwanamke japo kwa akili mbovu za wanawake wengi wanaona kufanya hivyo ni ujinga kwani hata wao wanaweza kufanya wanayofanya wanaume. Ha ha haa yaani hata mifano ya wanyama hawaioni!! Wazee waliosema Wanawake mwalimu wao kipofu walikuwa na maana kubwa sana ambayo sasa imepuuzwa.

Cha mwisho nakukumbusha wewe mwanaume unayenitazama hususani wewe uliegombana na mkeo au mpenzi wako hivi punde chanzo kikiwa hiki kipindi na hii mada yangu. Nataka ujue kwamba uko katika wakati mgumu sana na huyo mwanamke tena nakusihi uwe makini nae sana.

Ukipuuza siku moja yanaweza kukukuta kama yaliyonikuta mimi hata kama hautakuwa na ulemavu wa viungo kama mimi. Kuweni makini sana na wanawake wanaume wenzangu kwani hata mwenyezi Mungu ametwambia tuishi nao kwa akili.”

Nilistuka kwa maneno yale na kuhisi kama naambiwa mimi moja kwa moja. Muda mfupi baada ya kile kipindi kuisha nikiwa nimemezwa mawazoni nikijiuliza mwenyewe nishike yapi niache yapi haswa nikiambatanisha na kauli za Mchumbaangu kipenzi.

Mara ujumbe uliingia kwenye simu yangu na nilipoichukua kuufungua alikuwa ni Mariam.
Ujumbe ulisomeka hivi…

“Hussein nashukuru sana kwa matusi yako ya kuwa eti mimi ni muuaji haina shida ila kama ulikuwa hunitaki na ulikuwa unatafutia sababu ungenambia mapema tuu kuliko kunipoteza muda wangu.. Nashukuru sana, usinitafute nakutakia maisha Mema..”

Sio siri ujumbe wa Mamu ulinishangaza. Sikutaraji kabisa kama kile kipindi kinaweza kusababisha yote yale. Niliisoma mara mbili mbili ile 'sms' na kuamua kumpigia Mamu lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

Sikuchoka niliendelea kupiga lakini bado haikupokelewa na mara nyengine ilikatwa na mwishoe nikawa nasikia sauti ya huduma kwa wateja wakinambia kuwa namba ninayopiga inatumika.
Niliachana na simu na kuingia bafuni kuoga niliporejea chumbani nikatupia pamba kama kawaida yangu.

Eeeh.. kupendeza ilikuwa kawaida kwangu kutokana na jinsi nilivyojua kupangilia mavazi hadi watu wengi kitaani wakawa wananita bitozi, si unajua tena uswahilini kila 'chocho' unayokata ukiwa 'umejitupia' sana watu macho kodoo.

Nilirejea sebuleni baada ya kujiridhisha kwa nguo nilizovaa siku hiyo na kabla sijatoka nilipiga tena simu ya Mamu lakini jibu lilikuwa lile lile kwamba namba ninayopiga ipo bize.

Sikuwa na jinsi ilibidi nitoke na kuchukua bodaboda kuelekea kwa kina Mariam nikiwa na nia na madhumuni ya kwenda kuomba msamaha ili mapenzi yetu yaendelee kwani nilimpenda sana na nilijua kama nisingeenda muda huo basi ingebidi nisubiri hadi wiki ijayo kwani nisingepata nafasi kutokana na kuwa kazini muda mwingi.

Baada ya mwendo wa dakika kumi tulifika maeneo ya kina Mam na kumlipa ujira wake yule dogo aliyenileta nami moja kwa moja nikaanza kuongoza njia ya kwa kina Mamu huku nikiwazia jinsi ya kuanza.

_________________ITAENDELEA..
 
EPS 02
========

“Karibu baba.” Sauti ya mama mkwe mtarajiwa ilinikarimu nilipomkuta akiwa nje amekaa kwenye kolido ya nyumba yao akiwa anasukwa na mwanaye mwengine wa kike.
“Asante mama shikamoo”
“Marahaba baba za huko”
“Safi tu mama sijui ninyi”
“Sisi kama unavyotuona baba tunamshukuru Mungu. Enhee mbona hivyo baba kwema!”
“ehe!hee..! Kwema tu mama.” Nilijibalaguza kwa kujichekesha baada ya kuhisi huenda mama Mamu kashastukia mchezo ila ananitega. Lakini kabla sijakaa sawa nilishangazwa na swali ambalo nilijikuta nashindwa kulielewa na kuuliza tena.
“Unasemaje mama!!?”
“Nimekuuliza mwenzio yuko wapi? maana alituaga anakuja huko kwako muda mlefu tu aliondoka hapa sasa umenishangaza nawewe umekuja muda huu ukiwa peke yako! ndio maana nimekuuliza awali kwema?”
Nilijikuta nashusha pumzi kwanza mara baada ya kusikia na kubaini kuwa Mamu hajafika kwao tangia muda ule alipoondoka kwangu.
“Vipi baba mbona huongei..! unatutisha wenzako” Sauti ya mshangao ya mama mkwe ilinitoa kwenye dimbwi la mawazo ya ghafla nilipokuwa nafikiria alipoenda Mamu muda wote ule hajafika kwao.
Niliogopa kimtindo ila nilificha machoni. Niliwaza kama kitampata kitu kibaya huko basi namimi nitahusika kwa kiasi kikubwa pia nilivyoelewa kuwa Mamu atakuwa kachanganyikiwa sana na anaweza kujifanyia hata kitu kibaya mwenyewe kutokana na kujua kiasi gani ananipenda na mara nyingi hakutaka nimuudhi kabisa.
“Hah, ni hivi mama kweli Mamu alikuja lakini hakukaa sana akadai kuwa kuna vitu amesahau na alinambia nimsubiri sasa nimekaa na nilipoona anachelewa sana ndipo nikaamua kuja huku kwa lengo la kumfata yeye. Ndio maana ulivyoniuliza yuko wapi nimeshangaa ina maana hujamuona huku kurudi?”
“Hee!! We babaa eeh ina maana awe karudi halafu mi nikudanganye! Mwanangu si mzururaji hebu usitufiche baba nambie umemuacha wapi mwenzio au nini kimetokea huko kwenu..?” Uso wa mama mkwe ulinawiri mseto wa mashaka na hasira hata kumsimamisha mwanae aache kumsuka.
“Hakuna chochote mama, usiwe na wasiwasi.” nilijaribu kumtuliza.
“sasa mbona hueleweki eleweki simu unayo kwanini hukumpigia kujua alipo hadi unakuja kumuulizia?”
“Okeeey, samahani mama nimekumbuka alinambia kabla ya kuja huku kuna sehemu kwa shogaake angepitia kule mwenge. Tena ngoja nimfate huko kabisa nahisi hajatoka”
Ilinibidi kudanganya na kuongea maneno ya matumaini hasa mara baada ya kumuona yule mama akizidi kubadilika.
Kiukweli nilitambua kitambo kuwa Mariam anapendwa sana na mamaye na ukizingatia yule mama alikuwa na watoto wawili tu. Wote wa kike, babayao alishafariki muda mlefu sana hivyo hata jinsi alivyowalea wanae kwa taabu na maadili walikuwa si watu wa kutokatoka ovyo wala kuzurura. Na ndio sababu kitendo cha kusikia mwanae hayupo kwangu kilianza kumchanganya kidogo nami nikatumia akili ya ziada kumtuliza na kumkwepa kwa kujidai naenda Mwenge kwa huyo shoga yake Mamu.
“Baba naomba utavyorejea uje na mwanangu tafadhali, kwanza kisheria na kidini bado hujakabidhiwa. Asilale huko! oohooo”
Aliongea yule mama kipindi nikiondoka kuelekea kituo cha daladala nikiwa na mawazo mara mbili na niliyokuja nayo.

* * * * *

Safari yangu ilinipeleka mpaka pande za fukwe za coco na lengo halikuwa kuogelea wala kufanya mazoezi bali ni kupunguza angalau robo ya mawazo yaliyoandamana kichwani. Niliichukia siku ile kwa kulaumu ni heri tusingekutana tu na Mamu kwani mipango yote ya kufurahi pamoja wikiendi iliyeyuka ghafla kama machozi ya samaki kwenye maji. Niliwazia nitamwambia nini yule mama endapo Mariam asingeonekana siku hiyo kabisa. Niliwaza pia ina maana Mamu anaweza akajifanyia tukio hata la kunywa sumu kwa kajiugomvi kale tuu! Na kama akifanya hivyo nini kitanikuta baadae..! si ndio itakuwa basi tena! Niliwaza mambo mengi sana na kuchukua tena simu kupiga namba ya Mamu lakini bado jibu likawa lilelile ndipo nilipogundua sasa Mamu atakuwa kani-'reject'.
Nilijisonya na kumtumia ujumbe nikimsihi na kumuomba popote alipo basi arudi nyumbani haraka wanamtafuta. Japo nilituma zaidi ya meseji tano lakini hakuna hata moja iliyojibiwa. Nikiwa bado nimekaa juu ya jiwe moja nimening’iniza miguu huku nikiirusharusha na kuangalia watu mbalimbali wakifurahia maisha ufukweni, ndipo nilipoangaza macho huku na kule moyo wangu ulilipuka ghafla nilipomuona binti mmoja akiwa kavaa kipensi chepesi kifupi kilichom-bana barabara huku akiacha sehemu kubwa za mwili wake nje ambapo kifuani alijisitiri na kisidilia kidogo cha kamba.
Macho hayakuamini nikionacho huku mapigo ya moyo yakiongeza mwendo wa msukumo wa damu. Kilichonistua zaidi si uzuri wake wala umbo lake ama mavazi, la hasha! bali nilipouona uso wake ambao niliujua vizuri mno. Nilishindwa stahimili kumtazama binti akiwa kashikwa kiuno na baunsa mmoja ambae kushoto kwake alishika pira kubwa la kuogelea. Hakuwa mwengine yule binti bali kipenzi changu Mariam akiwa na yule njemba wakielekea majini huku wakionesha nyuso za furaha.
Nilijikuta mwili ukinitetema kwa hasira na midomo kunichezacheza huku macho yakiwa hayaamini kile kilichokuwa kinaonekana.
"!!Shiit!!!...?!" Nilihamaki na kuruka pale juu ya jiwe na kukanyaga maji licha ya kuwa nilivaa viatu simpo na suruali ya jeans lakini sikujali wala kufikiria hilo zaidi nilitembea haraka kama mwanajeshi macho yamenitoka nikielekea kule alipokuwa kipenzi changu Mamu na yule baunsa kabla hawajafika kwenye kina cha kuogelea.
“Mamu hapa unafanya nini na huyu boya ni nani yako?” Nililianzisha punde nilipofika kwa kuwaputisha mikono waliyoshikana.
“Boya? Hii we kaka vipi.. Eti baby unamjua huyu!!?” Alijibu kwa taharuki Mariam huku akinishangaa na kujisogeza jirani zaidi kwa yule njemba aliyekuwa ananitazama kwa hasira. Moyo ulinichoma na kujikuta naongea huku midomo ikinicheza cheza kwa kutoamini kama yule ndie Mamu ninayemjua mimi au kivuli chake.
“Mamu !!? hivi umepatwa na nini lakini..!”
“Hivi baby unamuelewa huyu..” Aliongea Mamu kumuuliza yule baunsa kwa kauli iliyonichoma zaidi ya msumali wa moto uliopigiliwa katikati ya kidonda na kubaki natazamana na yule mwamba aliyevimbiana kishari. Alikuwa mtu wa miraba minne aliyestahili kuitwa jitu. Umbo lake komavu lililovimbiana misuli lilitosha kumuogopesha mpenda amani yeyote kama mimi. Jitu jeusi kipara lenye sura iliyobeba alama zote za uvunjifu amani lilinikazia macho na kunikoromea.
“Oyaa wee bwege, usitupotezee muda katika starehe zetu hebu jikatae haraka kabla sijakufanya kitu mbaya sasa hivi, tena usinihamshie wazimu oooohoooo POTEA!” Lilifoka lile baunsa na kunisukumia majini. Haa! nami sikukubali japo sikuwa baunsa wala kuwahi kucheza mchezo wa ngumi, nilijikaza kiume na kumsukuma pia huku nikirusha maneno ya ndaro.
“Oyaa usinitishe wewe hizo nyama tu hata kwenye sambusa zipo. Sikuogopi wala nini! kwan......”
Nilipayuka nikisahau kuwa mdomo huponza kichwa. Ndipo hamadi! Kabla sijamaliza kauli nilistukia napigwa ngumi kali ya meno iliyonipeleka moja kwa moja chini na niliponyanyuka ili nikabiliane naye alinibamiza na lile pira usoni hadi nikaona cheche za moto mbele yangu na nafsi yangu kutamani watu waje kutugombezea haraka kabla uhai haujaniponyoka. Lakini ubaya wa watu wa jiji la Dar ndio kwanza walikusanyika na kuzunguka eneo lile wakitufanya sinema pasipo kuniokoa. Hata kipenzi changu Mamu hakujali wala kusema chochote.
’PWAATCHAAA’
Maji yalichapachika zaidi ingawa yalikuwa ya ugoko lakini kwa nilivyodondoshwa mara ya tatu ilitosha kulowana mwili mzima huku mengine yakiniingia puani na mdomoni kana kwamba nilitupwa kwenye kina kilefu. Kilichonisikitisha zaidi ulinzi eneo la fukwe naweza kusema kama haukuwepo kabisa kwa raia zaidi askari wachache walikuwepo eneo la nyuma za fukwe wakilinda magari yaliyoegeshwa. Nilipiga hesabu za haraka na kuona kama nitazembea zaidi naweza kukata moto mikononi mwa njemba yule aliyenichachamalia kuutafuta ujiko mbele ya Mamu na umati ule.
Nilinyanyuka kwa mbwembwe huku nikijifanya nami namtafuta nimpachike zangu ndipo 'paaap' kwa kwa kasi ya kope niliinama sambamba na kutoa ukelele wa hatari na kumrushia maji sambamba na michanga usoni yule baunsa na alipozubaa tu sekunde zilezile nilipenya kwenye ukuta wa watu na kukimbia eneo lile kwa kasi ya mshale nikiwaacha wakizomea na wengine wakivunjika mbavu kwa vicheko.
Daaah!! katika siku nilizowahi kujisikia vibaya na kupatwa aibu kubwa ambayo sitoweza kusahau na hii pia ni mojawapo. Niliumia sana hususani pale nilipoisikia sauti ya Mamu ikiambaa juu ya sauti zile zilizokuwa zikinizomea pale ufukweni. Sikumbuki kwa kasi niliyotoka nayo kama lile jitu lilinifukuzia ama laa, lakini ninachokumbuka vizuri ni pale nikiwa ndani ya daladala mara baada ya kustuliwa na sauti ya dada mmoja.
“Wee kaka vipi! Simama vizuri unaniloweshaa…!!” Sauti hii ilinifanya nijibane zaidi mlangoni aliposimama konda huku abiria wengi wakinishangaa kwa mwonekano wangu. Nilikuwa zaidi ya kituko nilivyolowa chapachapa mchana ule wa jua kali. Ilinibidi nishuke tu kituo cha mbele kwa aibu. Taratibu mguu mosi mguu pili, nilihesabu hatua macho chini kama mwali wa kimakonde huku njia nzima kila niliyepishana nae akinishangaa si mkubwa wala mtoto.
Kwa mwendo wa sawajiko nilifika 'getto' na kuchojoa zile nguo za masahibu na kuvaa taulo. Ndipo niliduwaa zaidi nilipojitazama kwenye kioo cha 'dressing table' na kubaini kuwa nilikuwa na uvimbe kwenye paji la uso, jicho moja lilivilia damu pia mdomo wangu wa chini ulipasuka na kulikuwa na damu zimegandia sehemu ya kidevu. Nilisonya na kumlaani Mariam kwa uchungu mara machozi yalibisha hodi usoni mwangu na kilio kuniponyoka. Maumivu yaliyokufa ganzi awali sasa yalifufuka upya mwilini mwangu. Nilijikaza na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniokoa kwenye mikono ya jitu lile lililokosa huruma. Nilijikagua vizuri kinywa kilichosheheni uzito wa maumivu na kubaini kumbe hata jino moja la mbele liling'oka na fizi kuvimbiana. Nilidata zaidi kwa uchungu punde taswira iliporudisha tukio lile machoni mwangu na muda uleule niliamuaa kuifuta kabisa namba ya Mamu kwa amri ya nafsi yangu iliyotibuka na kutotamani kuonana nae tena..! Niliiendea ile suruali niliyoivua muda mfupi pale chini lakini nilipotazama mifukoni kutafuta simu nayo sikuiona hata pochi yangu ya fedha pia haikuwepo.
"Dooh! nimepoteza kila kitu shaabash!" Nilisema mwenyewe nilipobaini kuwa lazima nilividondosha kwenye hekaheka ile hasa nilipokumbuka kuwa hata kwenye daladala nauli sikulipa wala konda hakunidai punde niliposhuka kule njiani. Nilishusha pumzi na kumshukuru tena Mungu na kuwazia hata nitaponunua simu sitokuja kuirejesha namba yangu wala sitomtafuta tena Mariamu kivyovyote. Niliwasha jiko la mchina na kuchemsha maji kisha nilielekea moja kwa moja bafuni kwa zoezi la kujikanda na kujisafisha kabla ya kwenda famasi kununua dawa za kutuliza maumivu.

_________________
ITAENDELEA,,,,
 
EPS 03
========

* * * * *

Ilipita wiki nzima nikiwa mnyonge sana kuanzia kazini mpaka mitaani sikuwa na shauku hata ya kutaka kujua maendeleo ya Mamu wala sijapata salamu zozote kutoka kwao. Upande wa pili moyoni nilikubaliana na maneno ya yule bwana kuwa inawezekana kuwa kweli wanawake ni wauaji. Nilijiuliza endapo yule baunsa angenizimisha ama kuniua yote ingekuwa kwa sababu ya Mamu. Pia niliwaza kuwa ina maana Mamu alidhamiria muda mwingi kufanya vile ama alifanya kama kulipa kisasi kwa maneno yangu? Lakini ikawaje iwe mapema vile tena siku ile ile?
Nilichoka na kuendelea kumlaani licha ya ukweli kuwa nilimpenda sana. Miezi ilipita na hatimaye ilikatika miezi nane nikiwa sijawahi kuwa na mahusiano mengine yoyote wala kukutana kimwili na mwanamke. Na katika siku hizo tulipata safari kikazi mkoani Arusha na ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufika Arusha.
Jiji la Arusha lilikuwa tofauti sana na Dar kuanzia hali ya hewa hadi tabia za watu. Sio siri katika kipindi kifupi nilijikuta nalipenda sana jiji lile. Lakini mara kwa mara usiku nilikuwa naandamwa na ndoto kuhusu wanawake. Na kubwa zaidi nakumbuka siku moja usiku nikiwa nimelala niliota kuna sehemu tumeenda kufanya kazi muda wa mapumziko mchana tulizunguka eneo moja ambapo nilikutana na msichana mzuri sana na katika maongezi nilipomuuliza jina alinambia kuwa anaitwa Zai. Nilishtuka usingizini na kuifikiria sana ile ndoto lakini mwishowe niliipuuza nikiamini huenda ni kutokana na kutofanya mapenzi muda mlefu ndio maana ndoto za wasichana ziliniandama. Lakini cha ajabu siku mbili baadae nilishangazwa tulipofika eneo ambalo lilifanana kabisa na lile nililoliota na kilichokuja kunishangaza zaidi na zaidi nikiwa na mshikaji wangu tunatembea tulipishana na msichana mmoja mzuri sana na tuliangaliana huku sura yake ikiwa haina tofauti kabisa na yule niliyemuota.
"ZAI!" Sauti iliita ubongoni baada ya kukumbuka jina la yule niliyemuota na kujikuta nikiliropoka kumwita yule binti tuliyepishana naye.
“Oyaa unamjua au ndio unaleta uroporopo kwenye miji ya watu?”
Aliniuliza rafiki yangu lakini kabla sijamjibu kitu niliita mara ya pili kwa sauti zaidi ya mwanzo na tulipogeuka tulishangaa kuona binti amesimama nae akiwa amegeuka akitutazama kwa mshangao. Nilipiga moyo konde na kumsogelea nikimuacha ndani ya bumbuwazi rafiki yangu.
“mambo Zai.” Nilimsalimu kwa kumhakikishia kuwa sikubahatisha kumwita ingawa nilificha mshangao wangu wa kuona kile nilichokiota kikienda mubashara.
“Poa, ila mbona sikukumbuki na sidhani kama tuliwahi kuonana!” kwa sauti tamu ya malaika binti alijibu kwa mshangao.
“Ni kweli unaweza kuwa sahihi kwa upande mwengine miili yetu haijawahi kuonana ila nafsi zetu ziliwahi.”
“kivipi mbona sikuelewi.”
“Utanielewa tu, kama hautajali chukua namba zangu hizi tuwasiliane kwasasa nina haraka.” Niliongea na kumkabidhi kikadi changu cha mawasiliano huku nae akikipokea akiwa bado ametaharuki nilimuaga na kuondoka. Sijui hata niliutolea wapi ujasiri wa majibu yangu pindi nilipokuwa nazungumza na yule binti. Nilimkimbilia rafiki yangu ambae alibaki ameduwaa muda wote niliposimama na yule mrembo.
“mwanangu mbona sikusomi?”
“hahahaaa hamnaaa utanisoma tuu.”
“heee! Hayaa, sema mtoto mkali kishenzi, umemjuaje?”
“nitakwambia tu usiogopee” Nilimzuga rafiki japo bado alionesha hajaridhika na majibu yangu na kujikuta akienda anageuka nyuma kumtazama yule binti na kunitaarifu kuwa bado alikuwa amesimama akitushangaa. Sikutaka kugeuka zaidi ya kujiuliza sana kichwani imekuaje nimeota ndoto na imetokea vilevile!
Nilihisi ujinga kama nitamwambia mshkaji eti simjui yule demu ila nilimuota na jina lake alinitajia ndotoni. Nilijua huo utakuwa ujinga ambao asingeniamini kabisa kwani si rahisi mtu kumuota mtu asiyemjua akamtajia mpaka jina halafu siku si nyingi wakakutana tena kiukweli na ikawa vilevile.
Tulirudi kuendelea na kazi huku muda mwingi nikiwa na shauku ya kupigiwa na yule mrembo lakini ajabu siku zilipita sikupigiwa simu na Zai wala kupata ujumbe wake na kwakuwa sikuchukua namba yake iliniwia vigumu kumtafuta na hata tulipotembelea tena yale maeneo sikuwahi kumuona. Nilijilaumu kutochukua namba yake lakini muda mwengine niliogopa hasa imani yangu ilipoenda mbali na kuhisi huenda atakuwa jini. Siku zilisonga hali ikiwa ile ile hadi muda wa kuwepo Arusha ulipoisha na safari ya kurejea Dar ilijili na kukusanya vitu vyetu kurudi rasmi pasipo kumuona tena Zai.

* * * * * *

Ilipita miezi minne sawa na mwaka mmoja tangu niachane na Mariam na nilikuwa nimehama kabisa lile eneo nililokuwa nakaa awali na nilipanga sehemu nyengine pembezoni mwa jiji. Maumivu ya kupenda yalisahaulika moyoni na kutamani kupenda tena. Upweke uliutesa mwili na kuhitaji mwenza ingawa hofu ya kutokea kama ya awali haikucheza mbali nami. Niliuvaa umakini machoni ili moyo usiteleze tena.
Siku hiyo nilipotoka kuoga baada ya kurudi kazini nilikuta simu ikimalizia kuita na nilipoitazama namba ilikuwa ngeni na kulikuwa na 'missed calls' nne. Nikiwa bado nina taulo niliamua kuipiga ile namba huku nikiwa nimesimama najiangalia kwenye kioo cha 'dressing table' na haikuchukua muda kuita sana upande wa pili mara ilipokelewa na sauti tamu ya kumtoa nyoka pangoni ilisikika.
‘’’Hallow, samahani naitwa Zai nipo hapa Arusha uliwahi nipa hii namba siku moja japo ni muda kidogo ulipita nilikuwa na matatizo nilisahau kukupigia.. nadhani naongea na mtu sahihi!”
Sio siri nywele zote zilinisisimka kusikia sauti ya mrembo wa ndotoni ambae niliwahi kukutana nae nilipokuwa Arusha kikazi na nilishakata tamaa ya kuonana nae tena. Eti leo kanitafuta mwenyewe baada ya kimya kingi kupita!?.
Kwa hamasiko na furaha nilijikuta namjibu harakaharaka.
“kweli kabisa ni mimi Hussein hapa upo wapi Zai?”
“Mi niko Kijenge na leo asubuhi nilipokiwa napangapanga nguo zangu kwaajili ya safari ndio nikaikuta namba hii kwenye begi langu moja niliihifadhi na nilishasahau lakini nilipoiona ndio nikakukumbuka hivyo nimeona vyema nikuage pia unikumbushe umenijuaje maana maneno yako siku ile yalinichanganya sana kama unaweza tuonane leo maana umenitia shauku ya kujua tulionana wapi.”
“Oooooh, unasafiri kesho..! wapi sasa?”
“naenda Dar”
“Dar!!! Haha Mungu mkubwa mi mwenyewe niko Dar huko nilikuwa kikazi tu.” Nilimjuza Zai na tukaongea mengi sana juu ya safari yake ambapo alinambia kuwa ndio mara yake ya kwanza kuja jijini na safari yake ni kwaajili ya masomo ya elimu ya juu na angefikia kwa shangazi yake huko Kinondoni.
Ingawa alinilazimisha nimwambie tulionana wapi lakini nilimzuga kuwa tutapoonana atapokuja nitamkumbusha.
Na kweli baada ya Zai kufika jijini Dar na ilipopita wiki moja tu alinijuza na siku ya jumapili ilibidi niende pande za Kinondoni kuonana nae hasa aliponiomba kwa madai ya ugeni wake asingeweza kutoka. Nilifika na kukutana nae kituo cha basi kama alivyohitaji. Moyoni nilifurahi japo kichwani sikuamini kama yule mrembo wa ndoto leo niko nae kwa mara ya pili tena hapa Dar. Baada ya salamu ndipo bila mbwembwe nyingi nilijikuta namwambia ukweli kwa fafanuzi kuwa hatukuwahi kuonana kimwili lakini niliposema nafsi zetu ziliwahi kuonana nilimaanisha kuwa niliwahi kumuota na akanitajia mpaka jina.
“hahahahahaaa usinichekeshe bwanaa hebu nambie kweli” Alicheka kwa kuamini yalikuwa maneno ya mzaha. Nilimtazama vyema alivyokuwa anacheka kwa mara ya kwanza niliushuhudia uzuri yakinifu na hata nafsi ilimpigia saluti binti alivyokuwa mrembo hadi nashindwa kuelezea.
“kweli Zai na ndivyo ilivyokuwa ila mi nahitaji tuwe karibu zaidi ya hapa” Nilikazia na kumshika mkono huku nikiivaa sura ya mahaba kama Sharukhan.
“kivipi..?” Kicheko kilimwisha ghafla na kunikazia macho punde nilipomshika mkono aliuputa na kusimama kiumakini baada ya kuniuliza.
“namaanisha tuwe na mahusiano ya ndani kabisa na endapo utakuwa radhi niko tayari kukuoa hata kesho Zai kwani naamini wewe ni mwanamke niliyeelekezwa na Mungu moja kwa moja kwenye maono” Niliongea kwa upole na sauti ya kumaanisha lakini maneno yangu safari hii hayakumfurahisha Zai.
"Lol! kumbe hilo ndilo lengo lako? kujizungusha kote sijui nimekuota sijui nini lol! samahani kakaangu naomba usipoteze muda wako na umwambie huyo aliyekutajia jina langu kuwa siko hivyo. Hiyo ndoto haipo na kutokea usahau...Kwaheri." Aliniaga baada ya kunishua na kuondoka huku kijungu chake mnato kikitingishika kimadoido. Nilijaribu kumzuia ili anisikilize zaidi lakini Zai hakusimama hata nilipomshika mkono aliuputa. Sikuwa na jinsi ilibidi nami nigeuze huku nikijilaumu upande wa pili kwa kuwahi kumwambia vile kabla hata sijamuweka karibu zaidi.
ITAENDELEA....
 
EPS 04
========

* * * * *

Zilipita wiki mbili nikijitahidi kumjenga Zai kwa njia ya simu bila mafanikio. Kila siku nilimtumia ujumbe asubuhi 'umeamkaje' mchana 'umeshindaje' na ile ya 'usiku mwema' kila jua lizamapo. Ingawa sikujibiwa hata meseji moja lakini nilifarijika kuona zinafika na kupokelewa. Sikuchoka kujishusha zaidi na kuomba radhi kama nilichofanya ni kosa kwake hata kumtaka basi tuwe marafiki wa kawaida tu hata kwa kupitia mtandao ingetosha kama hatotaka tuonane tena. Lakini pia niligonga mwamba kwa kukosa majibu. Nilimtumia jumbe mbalimbali za vituko na vichekesho lakini bado alizidisha mikausho mikali.
Baada ya muda nilianza kukata tamaa na kumsahau pole pole. Lakini nakumbuka siku moja majira ya usiku nilipokea 'sms' iliyotoka kwa Zai ambayo aliandika kuwa anahitaji kuonana nami. Nilistaajabu hasa alivyosema safari hii alihitaji aje ninapoishi. Sikuamini nikihisi alikuwa ananikejeli ingawa nilimjibu na kumuelekeza ninapoishi. Aliniahidi asubuhi yake ingefika na kweli keshoye mapema asubuhi alinijuza kuwa yuko njiani. Hapo ndipo nilipoanza kuamini na kumhakikishia angenikuta kituo cha basi namsubiri. Ingawa nilijua nahitajika kazini lakini nilijikuta naua kazi siku hiyo na baada ya kumaliza kuchati na Zai nilituma ujumbe wa uongo kazini na kuwambia kuwa nisingefika kutokana na kufiwa na jirani yetu. Na kweli haikuchukua muda asubuhi ile Zai alinipigia kuwa alishafika kituoni. Nilimuwahi na kumkuta mtoto amesimama kama jike la twiga akiwa kavaa gauni lefu na mtandio uliofunika vyema kichwa chake. Tulisalimiana na kuishika njia ya ninapoishi huku moyoni nikiwa siamini kabisa kama kweli huyu ndie Zai yule yule aliyeninyali siku ile. Nilitamani kumuulizaali muda ule kwa shauku kama ndio nimekubaliwa ombi langu au kuna lengine tena ! Lakini nilijikataza nafsini nikiilazimisha subira ingawa kuna muda nilijiuliza kaswali kengine ka uzushi kuwa hivi huyu binti Zainabu ni binaadamu wa kawaida kweli au isije kuwa ni jini linanifanyia mchezo..!!
Nilimuangalia pindi tunaingia 'ghetto' na kukaa kimagutu sebuleni mara baada ya kumuhudumia kinywaji alichohitaji na kufungua maongezi. Lakini ajabu nilishangazwa zaidi na kile alichokuwa anaongea Zai siku hiyo na kubaki na bumbuwazi zito sana kwa kutoamini nisikiacho Daaah!!... Unajua alisemaje..?
Zai alinsema hivi..
“Kiukweli kwanza naomba nisamehe kwa kutopokea simu yako wala kujibu meseji zako, lakini napenda ujue kuwa nilikuwa nafikiria sana swala lako kwani sijawahi kuwa na mwanaume japo nakutana na majaribu ya kutongozwa mara kwa mara. Na huku Dar nilichofata ni masomo tu na ndivyo nilivyoapa ila sijui imakuaje nimetokea kukufikiria sana na leo nimeamua kuja ili nikuhakikishie kuwa nimekubali niwe wako lakini kwa masharti matatu..”
Alinyamaza nami nikatumia nafasi ile kumeza mate na kukaa vizuri. Niliganda kama sanamu ya bisimini nikimtazama kwa makini nikionesha utayari wa kusikia hayo masharti ambayo nilishafuta pingamizi nafsini ingawa nilitaka tu kuyajua.
“sharti la kwanza naomba tusikutane kimwili mpaka utaponioa..."
Aliongea huku akinikazia macho nami nikatikisa kichwa juu chini juu kwa ishara ya kukubali na kumruhusu aendelee hilo sharti lengine.
"Lapili nipe muda nisome usinipigie simu ovyo hadi nikutafute mimi na kila mwezi tuonane mara moja tu tena maongezi yetu yasichukue zaidi ya nusu saa" Aliniangalia jinsi nilivyokuwa tuli namsikiliza.
"Na la mwisho uniapie kuwa hutokutana kimwili na mwanamke yeyote hadi utaponioa..”
Alimalizia Zai huku akinikazia macho nami bila kisito wala maswali nilimtoa hofu na kumhakikishia.
“Ondoa shaka kabisa mke wangu mtarajiwa niko tayari kufata masharti yote hayo na nakuapia sitokuja kuvunja hata moja niamini. Hata kama kuna mengine we niongeze.”
Alinyanyuka Zai na kunikumbatia lakini ajabu nyengine nilipomtazama machoni nilishangaa kuona anatokwa machozi.
“Vipi mbona unalia tena?”
“hamna ni mapenzi tu.. Nakupenda sana Zungu”
Sauti yake ya huba ilipenya zaidi masikioni mwangu na kunigandisha ubongo pindi aliponiita jina la Zungu. Niliganda staajibikoni kwani lilikuwa ni jina langu la utani enzi niko shule ya msingi sasa sikujua kalijuaje wala sikumbuki kama niliwahi mtajia mtu jina hilo na mbona ni miaka mingi mno hata kazini hakukuwa na mtu aliyenijua kwa jina hilo tena hata mwenyewe nilishalisahau. Nilitaka kumuuliza lakini nilijikuta napotezea na kusahau kwa pumbaziko la kumbato la huba na binti yule lililodumu zaidi dakika kumi. Baada ya maongezi machache ya hapa na pale ndipo aliponiaga nami kumruhusu bila kinyongo nikiwa mwenye furaha isiyo kifani.
Na huo ndio ulikuwa mwanzo wa ukurasa wa kitabu changu kipya cha ulimwengu wa mahusiano. Kitabu kilichopambwa na kasha zuuuuri la mapenzi ya dhati lililonakshiwa kila aina ya mvuto na kumpendeza yeyote akionacho kitabu hiko na kutamani kukisoma bila kujua kuwa ndani yake kuna kurasa zenye maandishi mazuri yenye maana mbaya iliyofichwa na misamiati migumu sana yenye kuumiza. Daaah!! laiti ningejua nisingeendelea kusoma misamiati hii na kuipuuza bila kujua maana yake. Na Laiti ningefunua kwanza nyuma ya kitabu kujua fasiri yake nadhani kitabu changu ningekisoma kwa tahadhali na umakini mkubwa ama nisingekinunua kabisaaa. lakini Mwe! Tafsiri niliyoikuta kwenye kurasa ya mwisho imekuwa matokeo tu ya haya niyaonayo baada ya dharau yangu ya kutosoma hata dibaji na kukimbilia kusoma nisiyoelewa maana kiundani nikifurahia kwa kukodolea picha za michoro mizuri kwenye zile kurasa bila kujua siri na maana yake. Na nilipomaliza kufunua kurasa ya mwisho kulipofafanuliwa maana nikawa nishachelewa saaaanaa. Daaah!! Aaaaaaaaahh!… Amini usiamini baabaaa..... WANAWAKE NI WAUAJI.

*||*||*||*

Sauti ya jitimai ilikinai kusimulia hadithi ile ndefu ya maumivu. Kumbukizi zilimfanya mzee msimuliaji machozi kutabaruku machoni pasipo hiyana. Kimtazamo hakupungua miaka hamsini akiwa ameketi akifarijiwa na kijana aliyeketi jiraniye. Huyo ndiye alikuwa Hussein baada ya miaka mingi kupita. Mengi yalimsibu kwenye maisha yake hata kujikuta akishindwa zuia machozi punde kila aliposimulia mkasa wa kweli wa maisha yake. Ilikuwa kazi kwa kijana msimuliwa kum-bembeleza na kumfariji mzee yule. Walikuwa pembezoni mwa fukwe maarufu ya SUN RISE iliyokuwa Kigamboni jijini Dar es salaam. Lakini alipofikia pale mzee Hussein alinyamaza na uso wake ukizidi lowanishwa na machozi na mwishowe kilio cha kwikwi kilimponyoka.

* * * *
<<<---->
(MIAKA 8 NYUMA)
HATUA ZA
> SHAABAN MWINCHANDE <
----------------------------------
-------------------------------

Ilikuwa ni siku ya furaha kwa familia ya mzee MWINCHANDE baada ya kijana wao wa pekee aliyeitwa SHAABAN kuhitimu elimu ya juu. Baada ya pongezi na sherehe kuisha siku hiyo Shaaban alikaa na mzee wake kwa mazungumzo juu ya hatua itayofata kuhusu elimu aliyoipata huko Nairobi Kenya alipokuwa kimasomo zaidi ya miaka mitatu.
“Mwanangu nimefurahi umefaulu vizuri na umerejea salama lakini bado narudia tena sikufurahishwa na kile ulichoenda kujifunza. Imani yangu ipo pale pale kwa elimu hiyo haitokusaidia hapa nchini kwetu labda ungekuwa ulaya.”
“Kivipi baba? Mimi ndiye mwenye chaguo tena kutoka moyoni. Naipenda sana elimu ya saikolojia na maisha ya viumbe na ndio ilikuwa ndoto yangu ambayo sasa imetimia.” Shabani alisimama kwenye imani yake ambayo ilikinzana na babaye mara kwa mara.
"Sawa baba. Kwa kuwa unaamini hilo basi subiria kazi." Alifunga maongezi mzee Mwinchande na kuingia ndani.
Siku zilipita baada ya tafrija Shaaban alianza mizunguko huku na kule kutafuta kazi juu ya kile alichokisomea lakini mambo yakawa kama vile alivyoambiwa na baba yake. Hakukata tamaa aliendelea kupwiyanga hatimae mwaka ulikatika bila kufanikiwa.
Babaye alijaribu kumshauri ajiunge na jeshi lakini Shaaban alipinga na kuamini taaluma yake ya elimu ya Saikolojia na mahusiano ya maisha ya viumbe. Alipokosa ajira aliamua kujiajiri kwa kufungua ofisi binafsi lakini bado kwa hali ya Tanzania hata hao wahudumiwa hawakuwa na elimu wala imani ya matatizo ya saikolojia. Kwa kipindi kilefu aliweza kujitolea tu mashuleni na kwenye semina kutoa elimu kwa watu kuhusu matatizo ya saikolojia na maisha lakini bado hakukuwa na cha maana kikubwa alichokivuna zaidi ya kupigiwa makofi ya hapa na pale, kula misosi ya semina na kuendelea kuwa tegemezi kwao.
Hali hiyo mwishowe ilimchosha Shaaban na mwishowe alikuwa mpole na kumuomba msamaha babaye.
"Nimekiri baba mawazo yangu hayakuwa sahihi kwa kile nilichokiamini. Niko tayari kukusikiliza baba na kufanya kile nilichopinga mwanzo. Naomba uniunganishie nafasi ya jeshi niirithi kazi yako tu." Maneno ya Shaaban yalimfurahisha zaidi mzee Mwinchande ambaye aliwahi kuwa mtumishi wa jeshi la magereza miaka ya nyuma.
“Usijali mwanangu nilitegemea siku moja utakuwa upande wangu tu. Sasa kutokana na elimu uliyonayo itakusaidia kupanda vyeo jeshini na wiki ijayo nitakupeleka makao makuu kwani mwezi ujao ndio usaili utaanza. Usiwaze naamini pia huko utapata nafasi ya kuitumia kazi yako kwani kuna mengi sana kwa wafungwa.”
Aliongea mzee Mwinchande na safari hii Shaaban hakuwa na pingamizi japo awali hakutaka kabisa kuja kuwa askari magereza kazi aliyowahi ifanya babaye.
Huo ndio ulikuwa mwanzo wa safari ya Shaaban ndani ya jeshi la magereza baada ya kujiunga na kwenda mafunzoni mwishowe akawa askari rasmi. Kutokana na juhudi na elimu yake haikuchukua miaka mingi mbele alipandishwa vyeo na kupanda ngazi kwa haraka hadi akawa Kamishna baada ya miaka mitano tu.
Mwaka mmoja baadae akiwa kamishna alihamishwa na kupelekwa kwenye gereza moja lililohusisha wafungwa wa makosa mazito mazito. Huko alishika wadhifa wa juu kabisa mara baada ya mkuu wa gereza lile kuugua na kufa ghafla. Na huko ndipo alipokutana na kisa cha mfungwa aliyekuwa pale kwa zaidi ya miaka ishirini na tano akijizolea umaaarufu jela kwa jina la HUSSEIN BABU BUBU alilotungwa na wafungwa wenzake kutokana na kuwapo gerezani kwa muda mwingi na kutopenda kuongea. Kituko kikubwa zaidi alichokuwa nacho mbali ya kutopenda kuzungumza wala kujichanganya na wenzake na muda mwingi anapotulia hutumia kuandika maneno ya ajabu ajabu na hata kwenye kuta za jela alitumia mawe kusugua na kuandika japo alishaadhibiwa sana na kuteswa juu ya swala hilo lakini hakukoma kwa miaka yote ile. Yalikuwa ni mazoea yake na aliharibu kuta nyingi kwa michoro yake na maneno ya ajabu kama mtu aliyechanganyikiwa na alihukumiwa pale kifungo cha maisha kilichotokana na kesi iliyomkabili ya mauaji.
Kilichomshangaza zaidi Kamishna Shaaban ni baada ya kufatilia michoro ya huyo mfungwa na alipoichunguza zaidi kwa uyakinifu aligundua kuna maneno ndani yake yaliyosomeka 'Wanawake ni wauaji’ Na huo ndio ukawa mwanzo wa Kamishna Shaaban kumtafiti na kumchunguza huyo mfungwa akianzia historia ya mafaili yake hadi kuhukumiwa na kuletwa pale huku moyoni Shaaban akiapa lazima atafute jinsi ya kuongea na huyo mtu kwani maneno yake yalionesha yana siri nzito na maana kubwa kwenye maisha yake.
ITAENDELEA,,,,
 
EPS 05
========

Alilipitia upya faili la kesi nzima ya Hussein Muhondogwa aliyefungwa pale kwa zaidi ya miaka 25.
Maelezo yalionesha kuwa mtuhumiwa alihukumiwa pale kwa kosa la kuwaua kwa kuwakatakata viungo mkewe na mwanae aliyekadiriwa umri usiozidi miezi sita. Ilionesha wazi mtuhumiwa alidhamiria kufanya tukio hilo kwa shinikizo la imani ya kishirikina ili awe tajiri kama ilivyothibitshwa na shahidi aliyeona na kuyasikia mazungumzo muda mfupi kabla mauaji kutokea. Ingawa serikali haikuamini ushirikina lakini bado aina ya tukio lilitosha kuthibitisha kuwa mtuhumiwa alidhamiria kuua hasa baada ya majibu ya daktari kuthibitisha kuwa alikuwa na akili timamu. Kwa mujibu wa katiba na vifungu vya sheria hakimu alikuwa na uwezo 3wa kutoa hukumu ya kunyongwa mtuhumiwa mpaka kufa, lakini kutokana na kukiri makosa yake mbele ya mahakama na kuonesha majuto ndipo alipunguziwa adhabu kutoka kifo mpaka kifungo cha maisha sambamba na kazi ngumu.
Baada ya kusoma yote yale Kamishna Shaaban alishusha pumzi na kufikiri jambo.
"Lakini kama kweli ana akili timamu na alikusudia kuua kwanini achanganyikiwe na kuandika haya maneno wanawake ni wauaji? Mh! hapa bado kuna jambo limejificha." Aliwaza na kuwazua
kwa kutumia elimu yake na uwezo wake binafsi wa kufikiri ndipo alipokata shauri na kulivalia njuga suala lile apate kutambua huo ukweli alioamini umejificha ndani ya maneno ya yule mfungwa. “Hakikisha Coplo unampiga picha kwa kila akifanyacho na uwe unanirekodia nyendo zake zote huko 'site' sawa..”
“Sawa mkuu.”
Alitoa agizo kwa askari kiongozi wa wafungwa pindi wanapoelekea kufanya kazi ngumu. Paipo kugundua Hussein kila alichofanya alirekodiwa kupitia simu ya yule 'coplo' na video kutumiwa kamishna Shaaban.
Kama kawaida yake Hussein mwili unapochemka akiwa kwenye kazi ya ngumu ya kuvunja kokoto hakutaka soga na yeyote zaidi ya kufanya kazi kwa nguvu sana. Licha ya umri wake kuwa ni mtu mzima lakini bado mwili wake ulikuwa na nguvu huku uso wake ukionesha ni mtu aliyedata. Muda mwengine alitabasamu na kujichekea mwenyewe tena kwa sauti kubwa hata kuwastua wengine wasijue kipi kimchekeshechasho! Na anapokuwa katika hali hiyo ndipo anapoongea maneno yake ya ajabu na mwishoni mwa kicheko husema WANAWAKE NI WAUAJI..
Wafungwa wenzake walishamzoea na walichukulia kawaida. Hakuna aliyethubutu kumzuia wala kumuuliza kwa kujua ni kazi bure kwani wengi waliopita walijaribu na kuambulia patupu na zaidi anapokasilika aliwapiga hata hao waliomuuliza bila kujali ni wafungwa wenzie ama askari. Hali ile ilimjengea usugu ndani ya gereza na kuogopwa. Lakini zile rekodi na picha zilizidi kumpa hamasa Kamishna Shaaban ya kujua nini kimejificha kwa mfungwa yule. Aliwazua na kuona sasa kuna umuhimu mkubwa wa kumfanya huyo mfungwa azungumze nae. Ndipo aliuandaa mchezo kupitia askari wake waliomtii na siku moja majira ya saa mbili usiku mchezo ulianza. Njemba za askari watano waliingia alipolala Hussein na kumkamata kwa nguvu. Walimfunga kitambaa machoni na minyororo ya pingu mikononi na miguuni. Akiwa katika hali ya sintofahamu Hussein alifurukuta na kupiga kulele. Haikuwa kazi rahisi lakini haikuwafanya wale maafande washindwe kumpeleka msobemsobe sehemu husika waliyokusudia. Walipomfikisha walimzimisha kwa kumpiga na kitako cha bunduki nyuma ya kisogo na kukata moto kwa muda.
"Tayari mkuu, tushamuweka kwenye chumba cha mahojiano." Afande aliyeongoza zoezi alimuhabarisha mkubwa wake ambae aliagizwa na kamishna Shaaban. Ndipo nae alipomjuza Kamishna. Ilikuwa ni siri ya kamishna na yule coplo ambae aliwatumia askari wengine pasipo kugundua nini ambacho kamishana wao anafanya.
Baada ya lisaa limoja anakuja kustuka Hussein punde maji baridi yalipotabaruku usoni mwake. Alijikuta amekalishwa kwenye kiti na mbele yake alikaa mtu ambae hakumfahamu ikizingatiwa hakuvaa sare zozote. Alikuwa ni Kamishna Shebby ambae pia aliamuru afunguliwe pingu kwanza. Japo awali coplo alisita kutokana na kumjua Hussein ni mtu hatari mwenye mwili mkubwa alioutengeneza kwa kufanya kazi ngumu, asije mpalua mkuu wao hata kumtia kabali. Aliamini si salama kumuacha aongee na muheshimiwa wao akiwa hajadhibitiwa walau mikono lakini cha ajabu Kamishna Shebby alisisitiza wampe uhuru wamfungue na wawaache wazungumze. Lakini mbali ya kumuonesha kila aina ya amani haikumfanya Hussein ampende yule kijana wala hakumjibu chochote alichomuuliza kwa siku hiyo. Alimuonesha kwa vitendo kwa nini anaitwa babu bubu. Alijaribu Shebby kwa mbinu zake siku hiyo kumfanya aseme walau jina lake lakini kazi ilikuwa bure. Mwishowe alishindwa na kuamuru wamrejeshe.
Baada ya hapo kamishna Shebby hakuchoka kwa kuamini yule mfungwa si bubu wala hajapoteza weledi wa kusema. Siku nyengine tena Hussein alichukuliwa na kufikishwa kwenye kile chumba ambapo safari hii kamishna alitaka wamtoe kule na kumpeleka kwenye nyumba ya mkuu wa geleza ambapo ndipo aliishi. Huko alimpa uhuru zaidi hata ya kumtaka akaoge kwenye bafu zuri na kuvaa nguo mpya ingawa pia zilikuwa za kifungwa. Chini ya usimamizi wa askari waliokuwa wakishangazwa na kamishna wao hasa pale alipokaa nae meza kuu ya chakula na mtuhumiwa yule. Siku hiyo walikula pamoja ingawa Hussein alikula kiujeuri lakini moyoni hakuacha kujiuliza kwanini anafanyiwa ukarimu ule na mtu yule ambae alikuwa mgeni pia machoni mwake ingawa alishagundua ndiye mkuu mpya wa gereza. Siku hiyo Shebby hakumuuliza kitu chochote mzee yule zaidi ya kumuonesha heshima na baada ya chakula aliruhusu arudishwe kule na kusisitiza zoezi lile la kula pamoja liwe endelevu.
Ilikuwa si rahisi kueleweka kwa askari wake nini anafanya ingawa kwa upande wake kamishna Shebby alikuwa na uhakika wa kile afanyacho. Yote hiyo ilitokana na kipawa kikubwa na uwezo wa ajabu aliokuwa nao kwenye kuisoma saikolojia ya mtu. Hakuisha kumchombeza Hussein kwa maneno ya hapa na pale kila alipokutanishwa nae na kumuonesha heshima kubwa hasa kwa kumtunuku jina la 'baba' ambalo Hussein katika maisha yake hadi kipindi hiko akiwa na miaka hamsini na kitu hajawahi kuitwa baba ingawa alishakuwa na mtoto. Alisikia faraja kidogo moyoni Hussein licha ya kuificha machoni lakini zaidi alichanganywa na tabia na ukarimu aliokuwa anaonyeshwa na kijana yule mkuu mpya wa gereza.
"Katika maisha binaadamu tunakutana na matatizo mbalimbali. Na matatizo ndio maisha yenyewe. Maisha bila matatizo bado hayawezi kuwa maisha. Masikini na matajiri wote wana matatizo yao ingawa wengine hudhani pesa ndio mwisho wa matatizo. Si kweli! Hatupaswi kusihi kwa kuwalaumu wengine ama kuwaona hawana maana eti kwa sababu ya matatizo yao ama kutusababishia matatizo. Wala hatupaswi kuomba sana kwa Mungu asitupe matatizo, huo utakuwa ufinyu wa fikra. Kikubwa tunapaswa kumuomba Mungu nguvu na akili ya kupambana na matatizo. Jisikie kawaida wala usijione mpweke kwenye uso wa dunia. Kumbuka baba hakuna aliye huru kwenye maisha uwe gerezani ama uraiani bado hauko huru. Tunaishi kwa sheria na kila sehemu kuna sheria zake na hapo ndipo kuna tofauti ya kimantiki maana ya kuwa huru. Lakini kiundani hakuna aliye huru duniani na hata mbele za Mungu. Sote tunaishi kwenye misingi na kanuni maalum ambazo ukienda kinyume chake lazima adhabu iwe upande wako. Jisikie amani baba. Naitwa Shaaban." Aliongea kamishna Shebby na kujitambulisha kwa mara ya kwanza siku hiyo maneno ambayo yaliugusa moyo wa Hussein bubu ingawa hayakumfanya aunyayue mdomo wake na kusema chochote. Kamishna Shebby nae hakuonesha papala wala haraka. Alizidi kumroga kifikra Hussein bubu. Siku zilisonga na maisha ya jela kuwa tofauti kwa Hussein na hata ifikapo usiku hakuchukuliwa tena msobe msobe kwenda kukutana na kamishna zaidi alisindikizwa tu kwa amani na coplo mwenyewe. Muda mwengine hata Kamishna Shebby alijiuliza kwanini moyo wake una shauku sana ya kujua kilichomkuta yule mzee? lakini kila alipokutana naye moyo ulizidi msukuma kutaka kujua kilichojificha kwenye maisha ya Hussein na kauli yake ya 'wanawake ni wauaji'.
Lakini mbali ya mbinu zote za Kamishna Shaaban (shebby) lakini zoezi la kuzungumza yaliyomsibu Hussein liligonga mwamba. Hapo ndipo kamishna alipoumiza kichwa na kutumia mbinu m'badala ambayo alimtoa eneo tofauti kabisa Hussein tena kwa siri iliyojulikana na askari wachache. Mipango ilianza baada ya kamishana kuagiza Hussein bubu apimwe vipimo vya nguo na kushonewa suti nzuri. Ndipo siku hiyo ikiwa mwisho wa wiki kamishna akiwa amevaa suti kali aligizwa aletwe Hussein bubu ambae naye chini ya ulinzi alioga na kuamriwa avae suti. Hali ile ilimshangaza mno Hussein hasa baada ya kunyolewa vizuri a kuwa katika mtazamo mpya wa kibinaadam. Ndipo mwishowe msafara wa magari mawili yalipotoka nje ya gereza ambapo moja wapo alikuwapo kamishna na Hussein bubu na nyengine walikuwa walinzi waliovaa kiraia pia. Askari wengi hata wa getini hawakujua kama kuna mfungwa mmoja anatoka na kamishna zaidi walidhani ni kiongozi mwengine tu wa jeshi aliyekuwa anatoka na kamishana siku ile. Ukiwa ni mchezo wa kinyume na sheria za magereza kutoka na mfungwa nje ya gereza kinyemela lakini Kamishna Shebby aliamua kufanya yote yale kwa kukata kiu ya moyo wake ili mfungwa yue azungumze kwa mara ya kwanza tangu ahukumiwe. Na moja kwa moja aliamuru msafara kuelekea maeneo ya fukwe ya 'Sun rise'.
Walifika na kupokewa kama wateja wengine wa heshima huku askari aliombatana nao wakichukua nafasi kwenye pembe tofauti wakidumisha usalama wa kamishna na mfungwa. Mazingira ya nje yalikuwa kama lulu machoni mwa Hussein bubu. Ilikuwa ni tofauti na fukwe alizozizoea kabla hajawa ndugu wa gereza. Teknolojia ilikua na mambo yalibadilika na kumfanya akumbuke mambo mengi hasa mara baada ya kuliona jua na wanawake wengi waliomwagika wakifurahia maisha ufukweni. Ni muda mlefu sana ulipita hakuwahi kuuona uso wa mwanamke. Aliwatazama vijana wa kiume wakikumbatiana na wanawake zao kimahaba na hapo alianza kuchefuka taratibu moyoni. Muhudumu wa kike aliwahudumia vinywaji na vyakula walivyoagiza na alipoondoka Hussein alimtazama sana kwa dharau ya hali ya juu.
"ha ha ha ha aaa HAHAHAHAAAAA .." Mwishowe Hussein bubu alicheka ghafla kwa sauti ya juu na kumstua kamishna Shebby.
"Kulikoni baba vipi?" Alimuuliza lakini alichojibu Hussein Babu bubu kilimshtua hata muhudumu yule ambaye alikuwa anarejea akiwa na vinywaji.
"Wanawakeeee... wanawakeeee .. wanawaaaake wazuuuri sana mwananguu ukiwatazama kwa nje tu, ila kwa ndani ni wabaya sanaaaa tena saaanaaaa na ni wauaji wakubwaaaa.. ha ha ha hahaaa.. WANAWAKE NI WAUAJIIII"
Kwa mara ya kwanza kinywa cha Hussein bubu kilifunguka na kunyoosha maneno. Ndipo kamishna Shebby alipobonyeza kitufe cha kurekodi katika simu yake kwani alijua sasa ule wakati alioutafuta na kuusubiri kwa muda mrefu umetimu. Alianza kumuuliza na kumpekecha kujua kulikoni zaidi kilichokuwa nyuma ya pazia! Na kweli taratiiiibu Hussein alijikuta kwa mara ya kwanza akifunguka na kusimulia historia yake yote na masahibu ya maisha yake hadi kufikia vile. Kumbukizi zake zilimrudisha siku ile aliyokuwa anaangalia kile kipindi cha ya walimwengu kutoka BECKER TV na hadithi yake ndio ilianzia pale akimsimulia kamishna Shaaban Mwinchande.

ITAENDELEA....
 
_________________
EPS 06
========

Simulizi iliyoshiba hisia ilimuumiza kila taswira ya matukio ya maisha yake ilivyomjengea picha ubongoni. Na zaidi alipofikia pale alipojuana na Zai msichana mrembo wa ndotoni aliyekuja kuwa dhahiri alikumbuka mengi sana. Msichana aliyemshangaza kwa kumtaja jina lake la utani tena la utotoni pasipo kumtajia mwenyewe. Msichana aliyemuonesha mapenzi na kuwa tayari kuvumilia masharti magumu. Masharti ambayo yalificha siri kubwa ndani yake ambayo alipuuza kuijua. Ndipo alipojikuta akishindwa kabisa kuendelea kusimulia baada ya maumivu ya moyo kuzidi uhimili wa hisia. Wakale walisema, ukimuona mtu mzima analia mbele za watu! ujue kuna jambo. Hapo ndipo kamishna Shaaban alipolivaa jukumu la kumfariji na kumsihi kwa maneno matamu ambayo hayakumfanya atulie mzee Hussein aliyezidi kunung'unika katikati ya kilio akisisitiza kuwa 'wanawake ni wauaji.'

*<>* *<>* *<>*
<EnDeLeA>
_______
Kum bembeleza mtu mzima ilikuwa si kazi ndogo pia muda nao ulienda sana na kutokana baadhi ya watu kuanza kutega masikio kujua kulikoni hasa walipoona kuna mtumzima mmoja alietinga suti kali ya heshima anatokwa machozi hivyo kama unavyojua ukimuona mtu mzima analia mbele za watu ujue kuna jambo na kwa kukwepa kujaza watu ndipo Kamishna Shebby sambamba na vijana wake waliamua kuondoka haraka na kurejea gerezani na baadae baada ya kurudishwa kwenye chumba cha siri na kuvalishwa nguo zake za gerezani aliamuru Hussein ahamishwe toka sero za awali na kupelekwa sero za v.i.p ambako walifungwa watu wenye pesa na viongozi wakubwa.

Ndipo siku nyengine ilikuwa saa sita za usiku Babu bubu (Hussein) alichukuliwa kama kawaida na kupelekwa kwenye chumba kimoja kikubwa kilichokuwa na masofa mazuri huku kamera mbalimbali zilitegwa na kamishna Shebby pasi na kujua yeyote kwenye chumba kile ndani ya makao ya Kamishna gerezani pale ndipo Hussein alijikuta akiendelea kuhadithia ile story ambayo aliapa awali kuwa ingebaki kuwa siri moyoni mwake.

* * * * * *
.......
< MASWAHIBU >
(MIAKA 29 ILIYOPITA)
<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Kiukweli japo masharti aliyonipa Zai yalikuwa magumu sana lakini kutokana na upendo wa ajabu niliokuwa nao nilijikuta navumilia na kusubiri na taratibu miezi ikasonga na nikaanza kuisoma tabia nzuri na ya kipekee aliyokuwa nayo Zai.
Kwanza alipenda dini alikuwa muislam safi sana pili alikuwa ana akili za kipekee mno na zaidi ya yote alijiheshimu tofauti na wasichana wengi niliowajua.

Siku zilisonga na hatimae mwaka mmoja ulikatika na siku hiyo Zai alinipigia simu tena kuwa anakuja getto nami nikafanya usafi harakaharaka na alipofika siku hiyo nilishangaa jinsi alivyokuja huku akiwa na begi kubwa la nguo na zaidi ni mada aliyokuja nayo nikajikuta nabaki mdomo wazi pale aliposema.

“Hussein amini mimi ni wako na sasa nimekuwa wako rasmi. Najua huna kipato kikubwa lakini una uwezo wa kunioa hata kesho, ukweli mi huku sikuja kusoma wala sina ndugu zaidi nilikuja kufanya kazi za ndani tu kwa mama mmoja wa kichaga aliyekuja kuniomba kwetu ila samahani nilikudanganya awali na kukupa masharti yote yale kwa lengo la kukujua vizuri ili uniimanishe kama umenipenda kweli au umenitamani na wanaume wote walionitongoza na kuning’ang’ania niliwakubalia wote na kuwapa masharti hayo matatu na woote walijitahidi kuvumilia lakini walishindwa baadae na hakuna hata aliyefika miezi sita lakini wewe umekuwa wa ajabu kwangu na naamini ndie mume bora kwangu… naomba unipokee kwani kule nimeondoka rasmi kutokana na manyanyaso na tabia za pale nyumbani.”

Nilibaki namuangalia Zai kile alichokuwa anakisema huku nikifikilia kichwani mwangu nimkubalie harakaharaka vile au kuna uongo anauendeleza tu kwani baadhi ya mambo ya Zai yalinistaajabisha kidogo hasa kuniamini na kunambia mi ni waajabu ilihali tulikuwa hatukai wote lakini kiukmweli toka niachane na Mamu sikuwahi kufanya ngono hadi dakika ile.
Na ukichochea upendo niliokuwa nao na uzuri wa Zai nilijikuta namkubalia na kupanga nae safari siku tatu zijazo twende huko kijijini kwao Arusha.

Ulipotimu usiku kwa mara ya kwanza baada ya Zai kusali alipanda kitandani na kulala pamoja na mimi huku akiwa kava gagulo na kiblauz alinibusu na kunambia kuwa nisitamani wala ntusifanye ngono hadi siku tutayofunga ndoa na kuninong’oneza kuwa yeye ni bikra pia.
Moyoni sikuamini hata kidogo alichosema Zai kwani alikuwa mrembo mno si rahisi kudumu na bikra hadi umli ule… niliona kuwa sasa nadanganywa na ktk umli wangu wote ule nilikuwa sijawahi kukutana na mwanamke bikra.

Usiku huo usingizi haukuja kabisa kila mara nilimuangalia Zai alivyolala umbo lake zuri lilivyojichora namba nane nilijikuta paipu yake inasimama na nyege za mwaka zikisisimua mwili wangu baada ya taswira za pepo chafu kutawala hisia zangu nilijikuta najisogeza karibu kabisa na Zai na kuanza kumpapasa kiuno na taratibu nilianza kupeleka mkono ndani ya gagulo lake na kukutana na kufuri lake lililoficha sehemu zake za utamu na kujikuta mate yakinijaa mdomoni kama fisi mwenye njaa aliyekutana na mzoga mbele yake.

Niliendelea kumpapasa taratibu nikiwa makini kabisa ili nisimstue usingizini na hatimae mkono wangu hususani vidole vyangu vile vya kati viliweza kupenya katika pachupachu ya chupi na kukutana na kajoto ka ajabu kutokea kwenye mashine ambayo sikuamini kama kweli ni mpya kabisa na haijawahi kutumiwa hapo kabla.
Katika hali nisiyoitarajia nililazimisha kwa ustadi mkubwa kupenyeza kidole changu kile ambacho ukimnyooshea mtu lazima mgombane,
Sikuamini pindi nilipoona kila dariri kuwa ni kweli ile mashine ilikuwa mpya na nilipolazimisha kupenyeza kidole kwa kuvisukuma vile vijinyama vilivyoziba njia Zai aliruka na kushtuka kwa sauti ya juu name kuutoa mkono haraka na kujigeuzia pembeni kwa speed ya hali ya juu.

“Hussein baby kwanini unataka kunifanyia hivyo?... tuseme huniamini nilivyokwambia!!? Mimi ni bikra kweli sijawahi kuguswa na mwanamme yeyote na niwewe pekee niliyekuamini na nahitaji uwe mume wangu wa ndoa ndio itakuwa raha siku utayonifungulia njia hii ya starehe ya wapendanao… baby najua una hisia lakini naomba vumilia tuu honey”
Maneno ya Zai yaliweza kumrusha ibilisi aliyenishika ghafra na kujikuta Napata moyo na nguvu na kumkumbatia huku nikimuomba samahani na kumuahidi sitamgusa tena mpaka tutapooana.
“So sorry baby.. sitorudia tena ni shetani tu alinipitia nikataka kukujaribu ili nihakikishe but sitorudia tena mpaka siku tutapohalalisha ..”
Niliongea maneno haya kwa busara ya hali ya juu nae Zai bila kinyongo aliniitika kwa kichwa na kunibusu kisha tukalala na sikumgusa tena hadi kulipokucha na mishe mishe ziliendelea hususani kwenda kukata tiketi kwajili ya safari huko kwao na siku mbili baadae niliaga tena kazizni ambapo nilipewa likizo ya wiki moja kwaajili ya kumaliza msiba niliodanganya awali na kutumia fulsa hiyo kusafiri na Zai mpaka jijini Arusha ambapo tulipanda tena gari lililotupeleka vijiji vya ndani ndani kabisa.
ITAENDELEA.....
 
EPS 07
========
Tulipokelewa vizuri pia bibiake Zai alikuwa mcheshi mno baada ya kufika alituandalia chakula cha asili na katika jambo ambalo sikulitarajia ni mara baada ya Yule bibi kuelewa kila kitu kuhusu mimi na Zai na hata kabla sijajitambulisha Yule bibi alinitajia kila kitu na kunambia bintie hakumficha chochote awali kuhusu mimi na tayari wajomba zake waliujua ujio wetu na wiki hiyo hiyo watatufungisha ndoa ili tuwe mke na mume rasmi.

Sikuwa na kiasi kikubwa cha pesa lakini nilishangaa kusikia mahali tutalipana wenyewe zaidi nilitakiwa kutoa elfu hamsini tu kwaajili ya mila zao.
Nilishangaa sana kumpata mke haraka vile tena kwa bei chee namna ile sikuamini kabisa na baada ya ndoa usiku wake tulitengewa chumba maalum kwaajili ya kulala na ndio ikawa mwanzo sasa wa kujilia lile tunda ambapo purukushani ilikuwa kubwa sana kwani zai alibana miguu na kuogopa sana nami nilikuwa jasiri wa kumkamata na kumdhibiti hatimae niliweza kumsongomeka msumari japo haukuingia wote na kwa shida sana Zai alipiga kelele mno za maumivu na chaa ajabu alipopiga zile kelele nilisikia sauti ya vigeregere nje ndipo nilipogundua kuwa kulikuwa na watu walikuwa wanatusikilizia.

Tulikaa siku saba kabla hatujarudi Dar ambapo tulifungashiwa zawadi kibao kwaajili ya kwenda nazo na nilipokuwa njiani niliwasiliana na ndugu zangu baadhi ambao walikuwa wananisubiri kwa hamu kubwa huku wengi wakiwa wamenilalamikia kwa kitendo cha kwenda kuoa pasi na kuwataarifu mapema.
Safari yetu ilifikia kwa Mjomba kakaake na marehem mama kwakuwa sikuwa na wazazi kipindi hiko na tuliwakuta baadhi ya ndugu na kutupokea vizuri tu na kuanza kuwatambulisha mke wangu lakini chaajabu kipindi nawatambulisha nilipofika kwa baba mkubwa ambae alikuwa ni mganga wa kienyeji aliposhikana mikono na Yule bint alimuangalia sana hadi Zai alionesha kusikia aibu na jicho la ba mkubwa kidogo lilinishangaza hata mimi.
Nilipomuangalia zaidi mke wangu alikuwa kainamisha kichwa chini huku baba akiwa bado kamkazia macho na kugeuza shingo kisha kunitazama kwa mshangao hali iliyoanza kidogo kunipa wasiwasi.

Lakini nilijibaraguza na kukenua meno kwa kucheka kidogo huku nikijiiminisha kuwa hali aliyoonesha baba huenda ilikuwa ya masihara na kautani kidogo nikiamini alishangaa kuona nimewezaje kung'oa kifaa kama kile.
Nakumbuka baada ya pongezi na zawadi mbalimbali ambapo napo kulikuwa na sherehe ndogo kwa niaba yangu, usiku uliingia tukalala lakini asubuhi na mapema nilipoamka na kutoka nje nilikutana na Ba mkubwa ndipo aliponiita na kunivutia pembeni.
“Pole sana kwa safari mwanangu”
“asante baba.. vipi kwema”
“kwema, ila naomba nikuulize swali”
“lipi baba”
“hivi huyu bint kabla hujenda kuoa ulishawahi kuishi nae japo mwezi mmoja au miwili?”
Swali la ba mkubwa kidogo lilinibabaisha kujibu na kujikuta nauliza swali badala ya kujibu
“kwani vipi baba..”
“hapana .. nimekuuliza tu mwanangu maana hukutwambia mapema kama unaishi na mtu baada ya yule Mariam aliyekuwa anakuja kwako mara kwa mara pia hukutwambia kama mliachana na umepata mchumba mwengine, lakini pia mwanangu kwanini hukumjulisha ndugu yeyote kama ungekuwa na safari ya kwenda kuoa..? tena mkoa wa mbali kabisa eeh..! hii imenitisha kidogo. ni afadhali ungeoa mtu wa nyumbani mwanangu sidhani kama huyu bint ni chaguo lako sahihi kabisa.”
Maneno ya baba yalininyima raha kidogo kwa kuona kama wananisimanga zaidi ili hali nilishaomba radhi hapo kabla na kauli yake ya kuwa afadhali ningeoa mtu wa nyumbani kidogo ilinichefua kwa kuona sasa wanataka kuanza kumnyanyapaa mke wangu nimpendae mapema ile.
Uso wangu kidogo ulibadilika sambamba na sauti pindi nilipomjibu tena ba mkubwa na kumwambia
“daah! Kiukweli ndio maana niliwaomba msamaha mapema tu baba kuwa nilipitiwa, lakini mimi ni mtu mzima na jua zuri na baya hivyo mkae mkijua namtambua vizuri sana mke wangu na sikukurupuka kumuoa ni chaguo langu sahihi kabisa.”
“Basi vizuri Mwanangu kama unamtambua vizuri, ila kumbuka Mpotea njia mara nyingi si Muulizaji”

Aliongea ba mkubwa na kuingia ndani na kuniacha nimesimama pale nje nikitafakari kidogo maneno yake na methali zake za mafumbo huku nikifikilia picha ya jana yake alivyoonana na mke wangu Zai na jinsi alivyomuangalia, nilijikuta najisonyea mwenyewe na kumpumbaza ba mkubwa moyoni kuwa kumbe bado ana akili za kizamani kabisa na mila potofu za kuchaguliana mke.

Nilipuuzia huku nikijichekesha kupotezea hasira iliyoanza kuubadilisha uso wangu na kurudisha tabasamu bandia ili mtu mwengine asinigundue asubuhi ile japo moyoni nilichefuka kidogo kisha nikaamua kurudi chumbani na baada ya sherehe kuisha siku hiyohiyo niliaga kwa ajili ya kuondoka japo awali mjomba tulikubaliana kuwa tungekaa siku tatu lakini nilieka visingizio kaza wa kaza hasa kuhusu kazini mpaka wakanielewa japo moyoni sababu kubwa ya kutaka kuondoka mapema ile ni baada ya kutibuliwa na ba mkubwa.
Na ndipo tulisindikizwa mpaka kule nilipokuwa naishi na baadhi ya ndugu waliotoka kijijini kwa kina Zai ili kupafahamu tulipoishi na waligeuza asubuhi hiyo na kutuacha wenyewe pale ndani na baadhi ya ndugu wa palepale mjini.
Baada ya nasaha mbalimbali hatimae kila mtu akaondoka na maisha mapya kabisa baina yangu na Zai yakaanza rasmi na yalinoga siku hadi siku.
Siku zote nilimshukuru mungu kwa kupata mke bora na mwema kama yule lakini ujinga mkubwa niliofanya ni kupuuzia swali na maneno ya Ba mkubwa yaani Laiti ningeyatilia maanani japo kidogo maneno ya ba mkubwa nadhani yasingenikuta yoote haya baadae… loh!! Kweli muda mwengine wanaume ujasiri wetu unatuponzaga kwani katika miaka miwili tu ya ndoa yetu ilitosha kabisa kuamini na kukumbuka maneno pia ya yule mlemavu wa kile kipindi kilichorushwa na kituo cha Becker TV nilichoangalia miaka mitano iliyopita hadi kupelekea kugombana na mchumbaangu wa awali kwa sababu tu ya ile mada na kauli ya msimuliaji kuwa Wanaake ni Wauaji.

Ni ngumu kunielewa harakaharaka lakini usijali utanielewa tu.
Ukweli mke wangu alikuwa mtu wa kufatilia ibada sana, alinisihi na kuniasa mara nyingi huku akinionya kwa upole mara kwa mara na kunisomea hadithi mbalimbali kuhusu watu waliomuasi mungu karne hizo na adhabu walizozipata.
Taratiibu nilijikuta nami nikianza kufatilia ibada na ndipo maendeleo yetu yalizidi kuwa mazuri na tulinunua kiwanja huko kigamboni na kuanza kujenga huku mke wangu akiwa msimamizi mkuu.
Mwaka mmoja baadae ikiwa ni miaka mitatu baada ya ndoa yetu nakumbuka siku hiyo majira ya jioni nikiwa ndani ya daladala nikitokea kazini kama kawaida nikiwa nimesimama na kutokana na wingi wa watu waliokuwa wanahitaji huduma ya usafiri jioni ile wakitokea makazini na mashuleni tulijikuta tukiwa tumebanana mno ndani ya daladala ile,
Nakumbuka vizuri tukiwa kwenye foleni kuna mtu alienisalimia akiwa amesimama nyuma yangu na niliitikia pasi na kugeuka kumtazama japo sauti yake sikuifahamu lakini alionesha kunifahamu zaidi kutokana na kunisalimia kwa kunitaja na jina, aliongea nami kwa sauti ya chini na kunambia ana ujumbe wangu.
Nilishindwa kumuelewa hali iliyonifanya nijalibu kujigeuza sasa nitazamane nae lakini kutokana na m banano wa watu nilishindwa kufanya hivyo hadi nilipoona napenyezewa bahasha ndogo kwa juu nami nikaipokea japo sikuelewa ni barua ya nini na inatoka wapi lakini nilijipa imani watu watapopungua mbele nitaongea nae huyo mtu ili anieleweshe zaidi na kilichomo ndani ya bahasha ile japo nilielewa kuwa ni barua lakini sikujua inatoka wapi na ni kwa dhumuni gani.
Gari ilisogea na kweli kituo cha mbele watu wengi walipungua ndipo nikapata nafasi ya kugeuka na kumtafuta yule aliyeniongelesha na kunikabidhi barua lakini cha ajabu kila niliyemtupia macho kuhisi ndie alibaki nae kunikodolea na kunishangaa tu na kujieka bussy na mambo yake,
Nilihisi na kujilidhisha huenda akawa kashuka pale kituoni gari iliposimama lakini nilijiuliza kwanini hata hajaniambia kama anashuka? Niliachana nae na kuendelea na yangu huku nikiwa na shauku ya kufika haraka nyumbani niweze kusoma kile kilichoandikwa ndani ya ile barua.

Nilifika nyumbani na kupokelewa vizuri na kipenzi changu kama kawaida na kumnyanyua mwanangu kipenzi ambae alikuwa anakaa chini kipindi hiko kwani tayari mungu alitubariki mtoto mmoja wa kiume na niliipenda na kuijali sana familia yangu.
Mara baada ya mke wangu kipenzi kuniekea maji bafuni na nilipomaliza kuoga nilitoka kuja sebureni kwa ajili ya kupata msosi lakini niliikumbuka ile barua na kurudi chumbani na kuichukua kwa shauku ya kuisoma kujua dhumuni lake ndipo nilipotulia sebureni nikiwa nasubiri msosi kipindi hiko mke wangu alikuwa busy jikoni ananipakulia ndipo nikaanza kuisoma barua ile ambayo nje haikuwa na anuani yoyote lakini kadri nilivyozidi kuisoma ndivyo mapigo yangu ya moyo yalivyozidi kuongezeka.
aaaagh! Kamishna babaaaa.....
Naikumbuka vizuri ile barua iliandikwa hivi.,………………..
ITAENDELEA,,,,,
 
EPS 08
========

……………………………………………………………………………………………..
NDUGU,
POLE NA MAJUKUMU NA HONGERA KWA KUISHI NA MWANAMKE MZURI NA KUJIMILIKISHA MTOTO.
NISINGEPENDA KUONGEA ZAIDI ILA NIA NA MADHUMUNI YA KUKUANDIKIA HII BARUA NI KUKUONYA NA KUKUTAHADHARISHA JUU YA MKE WANGU UNAYEISHI NAE.
SIKUWA HAPA JIJINI KWA MUDA MREFU KIDOGO LAKINI NIMEPATA HABARI ZOTE JUU YA JANJA YAKO ULIYOTUMIA HADI KUITEKA NA KUILAGHAI FAMILIA YANGU.
SASA KWA USALAMA WAKO NAKUPA SIKU SABA TU.
ANZA KUHESABU KUANZIA KESHO UMRUDISHE HUYO MWANAMKE KWAO ARUSHA NA HUO NDIO UTAKUWA USALAMA WAKO.
ZAIDI YA HAPO UTAJITAFUTIA MATATIZO MAKUBWA YATAYOKUFANYA UJUTE MILELE NAMI NISINGEPENDA YAKUKUTE MAJUTO.
AHSANTE.
WAKO….. MR. X

………………………………………………………………………………………………

Nilishindwa kuielewa ile barua licha ya kuirudia kuisoma zaidi ya mara tatu na mke wangu alinishangaa pindi aliponitengea chakula na kubaki nimeduwaa tu na barua ile huku uso wangu nao ulishaanza kubadilika ghafra hali iliyomfanya anisogelee na kuniuliza kwa upole nami sikumjibu zaidi ya kumpa ile barua ambapo aliisoma nae alianza kushangaa na kuonesha wazi hakuielewa kabisa hasa aliponiuliza kuwa ile barua ya nani?
Nilimjibu nimepewa mimi ni yangu na inanihusu mimi na yeye.
Aliniuliza tena imetoka wapi, hapo ndipo niliposhindwa kuwa na maelezo ya kutosha zaidi ya kuitaka ile barua na kuisoma tena lakini sikuambua chochote zaidi ya mke wangu kuniapia na kunisihi kuwa ule ni ujinga wenye uongo wa kutupwa wala haumlengi yeye inawezekana muhusika amekosea.
Nilikubaliana na mke wangu lakini pia nilijiuliza mbona amepataja Arusha? ilihali kweli mke wangu nimemuolea huko?
Na atasemaje yule ni mke wake wakati nimemuoa takribani miaka mitatu? Na kwa maelezo ya ile barua niligundua kuwa mwandishi alimaanisha kuwa nilimchukua yule mwanamke akiwa ana mtoto mdogo…
hahahaha hapo nilijikuta nikicheka mwenyewe moyoni kwani mke wangu nilimuoa akiwa m bichi kabisaaaa na bikra yake na alikuwa hajawahi kuguswa wala kujihusisha tendo na mtu yeyote zaidi yangu hadi anapata ujauzito na kurudi kwao kwa miezi minne ya mwisho walipomuhitaji akaugulie huko na baadae alijifungua salama mtoto wa kiume na niliwaacha mpaka mtoto alipotimiza miezi miwili ndipo nilipowafata kuwachukua na kuendelea na maisha.
Niliamini wazi hiyo barua imekosewa tena si kidogo na nilitamani sana kumuona yule aliyenipa ile barua.

Lakini swali lililonishangaza tena mbona yule mtu alinitaja kwa jina langu kabisa akionesha kunifahamu kabla ya kunipa ile barua?
Hapo nilikosa jibu kamili lakini niliamua kupotezea na siku zilienda ambapo zilipita siku nne tangu nipate ile barua ndipo siku nyengine tena nikiwa kwenye daradara safari hii nilipata siti sikuwa nimesimama kama siku ile na wala watu hawakuwa wengi sana kutokana na kuwahi kutoka kazini siku hiyo ndipo nikiwa ndani ya ile daradara mara simu yangu iliita na nilipoitoa mfukoni kuangalia aliyekuwa ananipigia ilionesha ilikuwa namba ngeni machoni mwangu ndipo nikaipokea kujua nani aliyekuwa ananipigia lakini nilipopokea tu kabla sijasema 'hallow' nilianza kuisikia sauti ya aliyenipigia ikinikumbusha kuwa zimebaki siku tatu na kuniasa nisije kupuuza nilichoambiwa kwenye ile barua kisha simu ilikatwa.
“HALOOW!! NANI WEWE??”
Nilipayuka kwa sauti ya juu hadi nikawastua abilia wenzangu na kunishangaa ambapo nilionesha kuchanganyikiwa kwa hasira na ndipo nilipojaribu kuipiga ile namba lakini cha ajabu haikupatikana kabisa hata niliporudia zaidi ya mara tano ndipo nilipoamua kutuma msg lakini nayo haikuleta majibu kama imefika.

Nikiwa nimepagawa ndani ya daradara nikitafakari cha kufanya mara simu iliita tena kwa mara nyengine na nilipoiangalia namba nayo ilikuwa ngeni lakini ilikuwa tofauti na ile niliyopigiwa muda mfupi na mtu nisiyemfahamu.
Nilishusha pumzi na kuipokea kwa sauti ya upole lakini nilijikuta nastaajabu nilipoisikia sauti ya aliyenipigia ilikuwa tofauti na ya yule wa mwanzo lakini mada ilikuwa ileile hasa aliponambia.
“Usipanick ndugu yangu na kuwastua watu kwenye daladala ila nakupenda sana ndio maana nakusihi na kukukumbusha kuwa zimebaki siku tatu na hujatekeleza maagizo ya kwenye barua nakusihi tafadhali fanya hima sasa kwa usalama wako’’’

Nilibaki nimeganda safari hii pasi na kujibu chochote hadi simu ilipokatika nilibaki nimeduwaa huku kichwa kikijawa mawazo lukuki nikihisi sasa kuna uwezekano wa kile nilichodhalau kikawa na ukweli ndani yake lakini ni ukweli upi huo kama sio udanganyifu na kutaka kuporwa mke wangu kinguvu?
Niliangaza kona zote ndani ya gari ile nikihisi waliokuwa wananifanyia kale kamchezo huenda niko nao ndani ya gari ile lakini sikuambulia chochote zaidi ya watu nao kunishangaa tu kwa kuchanganyikiwa kwangu.
Nilijisikia aibu sana kwa mara nyengine nikikumbuka aibu iliyonipata kipinde kile baada ya kupigwa na baunsa niliyemfumania na mchumbaangu Mariam.
Gari ilifikia kituoni na taratiiiibu nilishuka na kuelekea nyumbani ambapo siku hiyo mke wangu alinigundua kuwa siko sawa tangia aliponipokea nje na kuingia ndani ambapo nilijibwaga kitandani bila kuzungumza chochote.
Haikuwa kawaida yangu kurudi bila kumkumbatia mke wangu na kumnyanyua mwanangu kwa furaha huku nikimchekesha chekesha na kucheza nae na ndipo kwa mshtuko mke wangu aliniuliza kulikoni lakini nilizuga kwa kudanganya kuwa naumwa na alipohoji kuhusu kwenda hospitali nilidanganya kuwa nishakunywa dawa za maralia kazini na ningependa kupumzika muda huo.
Nililala kitandani huku mke wangu akiwa pembeni akinifariji sambamba na mwanangu aliekuwa akinichezea chezea mikono.
Moyo uliniuma sana na kumlaani shetani aliyekuwa ananiandama kutaka kuisambaratisha familia yangu.

Nilifikilia kupiga simu polisi na kutoa taarifa zile lakini kabla sijafanya hivyo nilinijia wazo la kumtafuta babaangu mkubwa ambae alikuwa mganga wa kienyeji na moyo ulinisukuma kumtafuta yeye moja kwa moja pasi na mtu mwengine kutokana na lile tukio lililojili miaka mitatu iliyopita na maneno yake ya mafumbo aliyoniambia nilihisi huenda kuna kitu ambacho alikijua mapema kuhusu mke wangu.

Safari hii sikutaka kumwambia ukweli moja kwa moja mke wangu juu ya kilichonikuta tena nikihofia kumtisha pia nilijipa mda wa kutafakari kitu cha busara cha kufanya na akili bado ilinituma moja kwa moja niwasiliane na ba mkubwa tu nimuhadithie kila kitu huenda yeye akawa na msaada mzuri wa kiushauli na cha kufanya.
Takriban siku mbili nilishindwa kwenda kazini na nilipopata nafasi ya kuwa pekeangu baada ya mke wangu kuniaga kuwa anaenda bombani kuchota maji ndipo nilimpigia simu ba mkubwa na kumuelekeza yaliyojili ambapo hakuonesha kushangaa sana wala kustushwa na habari zile ila alinionya nisithubutu kutoa taarifa polisi wala kwa mtu yeyote kwanza kabla sijaonana nae na aliniomba na kunisihi sana nifanye hima niende kwake haraka ikiwezekana kesho au jioni ya siku hiyo ambapo kwa mujibu wa ile barua ndio ilikuwa siku ya saba.
Nami sikutaka kuremba japo nilijua safari ya kwa bamkubwa ilikuwa mbali kando kando ya mkoa wa pwani mpakani mwa dare s salaam lakini niliona niondoke na familia yangu jioni ile ile kwa kuhofia tusije kuvamiwa usiku bure na watu wa huyo Mr.X kwani namba yangu tu ya simu waliijua sembuse nilipokuwa naishi?

Mke wangu aliporudi kuchota maji nilimsihi ajiandae kwa safari haraka ambapo nae alishangaa mno lakini hakupinga hivyo tulijiandaa pamoja na lisaa limoja baadae tayari tulikuwa tupo safarini kuelekea kwa ba mkubwa.
Moyo wangu kidogo ulianza kupata amani na kupata shauku ya kuonana na ba mkubwa kwani alisaidia na kuaminika na watu wengi mno hivyo niliamini kama tatizo letu kuna nguvu za giza ndani yake basi litakuwa limeisha kabisa kwani ba mkubwa nae alikuwa ni nooooowmaa ktk maswala ya kwechekweche na tunguli.
ITAENDELEA………
 
EPS 09
========

Saa tatu kasoro usiku tulishuka eneo husika na kuchepuka kukifata kibarabara chembamba kilichoelekea huko alipopatikana ba mkubwa ambapo kulikuwa na umbali wa kilometa kama mbili kukifikia hiko kijiji.
Kwa kuwa ulikuwa usiku na giza lilishaingia huku kukiwa na kijimbaramwezi kwa mbali ilibidi tutumie tochi kumulikia na njia nzima kulikuwa kimya sana.

Nakumbuka baada ya mwendo kidogo tukiwa tumebakiza kama kilometa moja na nusu kufika mke wangu aliniomba ajisaidie haja ndogo kwani alibanwa mno na asingeweza kuendelea mbele nami nilimuonya ajisaidie palepale njiani asiingie polini kwani kuna wadudu wengi kwenye majani na ndipo nilipompokea mtoto na kusimama kumsubiria.

Nikiwa nimesimama mke wangu anajisaidia ghafra nilisikia chakala chakala na nilipogeuka nilishangaa kumuona mtu aliyevaa kininja akininyang’anya mtoto kwa nguvu na kabla sijafanya lolote kujitetea mara kwa nyuma nilipigwa na kitu kizito bila kumuona aliyenipiga na kujikuta naanguka chini huku kwa mbali nilisikia ukulele wa mke wangu kipenzi Zai akisema.

‘’’’’’Jamaaniii iiiinatoshaaaaa Nilishawaaambiaa msimuuueeee..’’’’’

Sitoweza kuisahau kamwe kauli ile ya Mke wangu Zai.. Zai wangu kipenziii msichana wa ndoto yangu niliyeamini nimeoneshwa na Mungu lakini leo hii anatoa kauli iliyoniaminisha na kuniumiza moyo wangu kupelekea kupoteza fahamu pindi nilipoanguka baada ya kugundua kuwa kumbe mchezo wooooooootee nae alihusika na aliujua vizuuuuri. looh!
Ama kweli adui wako mkubwa ni mtu wako wa karibu na Udhaniae ndie sie ila sie ndie.
Nilijihisi nakaribia kufa huku nikijiuliza kumbe Zai aliishiii kwa kuniigiziaa?!! aaaaaghh!!!!!… Ni vigumu sana kuaminilll! lakini Chunga sana baaabaa Kamishnaaa usiombe kabisa yakukute kama yaliyonikutaaaa.
Siku hiyo ndio kwa mala ya kwanza niliikubali thabiti ile kauli kuwa Wanaake ni Wauaji, nami nakazia kabisa leo hadi siku ya kufa kwangu nitasema kuwa WANAAKE NI WAUAJIIIIII.

*<>* *<>* *<>*

Kilifuata tena kilio cha sauti ya juu na kwikwi kutoka kwa Hussein na kazi ikabaki kwa Kamishna Shaaban Mwinchande kum bembeleza na kumtuliza ili apate kuelewa na kubaini kilichoendelea ktk hadithi yake baada ya kurudiwa na fahamu.
Safari hii sasa hata Kamishna Shaaban mwenyewe alijikuta nae machozi yakim bubujika kwa jinsi alivyokuwa anasikiliza kisa kile cha Hussein na zaidi alipomtazama uso wake wa kiutuuzima uliokuwa unatiririkwa machozi kama mtoto kadri alipokuwa anasimulia na alionesha dhahili kuwa ana ghadhabu kubwa juu ya wanaake kwani ktk hadithi yake ile hadi muda huo ilibeba maumivu tu na mateso yote ameyapata sababu ya mwanamke aliyempenda na pia kwa uzoefu wake wa kusoma saikology za watu Kamishna shebby alizidi kumuamini na kubaini kuwa kweli mfungwa yule alionewa na hakuwahi fanya ubaya wowote.
Lakini maswali bado yalibaki kichwani mwa Kamishna Shebby na alitaka kujua zaidi ilikuaje hadi kukawa na uthibitisho wa maiti hizo mbili ya mkewe na mtoto? na iweje huyo Zai mke wa Hussein afahamiane na hao watu na kueka mbinu kisha wamgeuke pia na wamuue sambamba na mtoto? ilikuwaje kuwaje hapo... na huyo Mr. X ni nani kwa mujibu wa barua ya kutatanisha aliyoipata Hussein.
Japo alikuwa mtaalamu sana Shaaban na alijaliwa ubongo mwepesi ktk kufikiri na kufumbua jambo lakini kwa maswali yale yaliyosumbuka kichwa chake muda ule juu ya hadithi ya Hussein hakuweza kupata majibu ya haraka zaidi ya kumsihi mfungwa wake (Hussein) ajikaze ili aendelee kumsimulia kilichotokea baada ya kurudiwa na fahamu mpaka kukamatwa na kuhukumiwa.

Siku hiyo Hussein japo maumivu yalikuwa mazito mno moyoni mwake kwa kukumbuka mapito yaliyoinyamazisha ndoto zake na kujikuta anazeekea jera akisubiri kifo tu lakini alijitahidi na alipania kuwa aweke kila kitu wazi kwa kijana yule ambae awali hakutambua kama ndio kamishna lakini sasa alijua na hakuwa na jinsi zaidi ya kumuelezea kila kitu hasa baada ya kugundua ni askali kiongozi mwenye moyo wa kipekee sana.

Huku akifuta mafua baada ya kimya cha zaidi ya dakika arobaini Hussein aliendelea kusimulia ilivyokuwa mara baada ya kupigwa na kitu kile kichwani hali iliyompelekea kuanguka na kupoteza fahamu.

*<>* *<>* *<>*
..........

Nilistuka mara baada ya kuhisi hali ya ubaridi na unyevunyevu na nilipotaka kuamka nilijihisi kichwa kuwa kizito sana lakini nilijitahidi na kukaa kitako pale njiani huku nikitazama huku na huko kuangalia kama kuna watu wanakuja niombe msaada ama sivyo nikusanye nguvu nipige mayowe raia waje wanisaidie japo nilijua kuwa pale nilipo kuna zaidi ya kilometa moja kufika kwenye makazi ya watu ambako ndiko pia alipatikana babaangu mkubwa yule mganga wa kienyeji na ndio nia ya safari ile tulikuwa tunaelekea kwake.
Sikujua ilinichukua muda gani mpaka niliporejewa na fahamu kwani nilijikuta niko mwenyewe pale chini.

Lakini niliponyanyua mkono wangu na kutokana na mbalamwezi kuchomoza muda ule nilishangaa kuona umetapakaa damu halkadhalika na mkono mwengine.
Nilijikagua haraka haraka kuona wapi nimeumia lakini bado sikuhisi jeraha lolote mwilini mwangu zaidi ya jeraha dogo kichwani ambalo lilikuwa halivuji damu kivile.
Lakini pia nilipoangalia chini vizuri nilishangaa kuliona panga usawa ule nilipolala likiwa limeloa damu pia kulionekana michilizi ya damu kuelekea kwenye kichaka kimoja eneo lile.
Nilijikuta nikilishika lile panga kwa mshangao na kuligeuza geuza kuhakikisha kama ni kweli au macho yangu yalikuwa bado yana mawenge,! lakini nilipofanya vile akili iliniaminisha kuwa kile nikionacho ni kweli wala si mawenge na hapo ndipo nilipogutuka na kulitupa haraka chini lile panga na kujikuta nimepata nguvu za kusimama na kuanza kunyata kwa umakini kufatilia ile michilizi ya damu kujua nini kilichopo pale kwenye kichaka.
Lakini kabla sijakifikia kile kichaka mara nilianza kusikia kelele kelele za watu wengi waliokuwa wanakuja kwa mwendo wa kasi wakitokea ile njia iliyoelekea kijijini na punde tu nilipogeuka niliona mianga ya tochi ikinimulika huku kwa mbali nikisikia baadhi ya maneno waliyokuwa wanaongea wale watu.

"Mwanaharamu mwenyewe si ndio yuuleeee.."
"Enheeeee yule yule si unaona midamu ilee.."
"Aliyeua auaweeee hebu tupisheni sie mbona hamtembei tutamkosaaa.."

Zilikuwa ni moja ya kauli nilizozisikia toka kwa wale watu huku wengine wakianza kukimbia kuja pale niliposimama nami nikabaki nimeganda kwanza nikiwashangaa na nilipokaza macho kutazama vizuri niliwaona wengine wakiwa wamebeba silaha za jadi na macho yao wote wakinilenga mimi hasa baada ya kunionaa.
"Uuuuuaaaa Huyooooo.."
"PIGA UUAAA.."
Ukelele huu ambao uliambatana na kurushwa kwa mkuki ambao kwa bahati nzuri ulinikosa na ndipo akili ikanicheza na kunionya endapo nitachelewa sekunde kadhaa watu wale wataponikaribia zaidi wataniua kwani walionesha wazi walikuwa hawaji kwa wema wala huruma hata chembe juu yangu.
Nilijikuta naruka na kuanza kutimua mbio huku upepo mkali ukinipitia ghafra karibu na kichwa baada ya kurushwa kwa rungu moja kubwa ambalo niliamini lingenipata huenda ningezima pale pale kama sio kufa kabisa.

Nilikimbia kwa speed ya kunusuru maisha yangu huku nikifata kile kibarabara kilichoelekea barabara kuu kule tulipotoka na nyuma yangu bado niliandamwa na watu wale wenye hasira kali ambao sikuwa na uhakika wa moja kwa moja kuwa ni wanakijiji au ni miongoni mwa wale walionivamia awali!?
Lakini kabla sijafika mbali mbele yangu kulisikika mlio wa gari sambamba na mwanga mkali wa taa zilizonizuia kuona vizuri na kujikuta naingia porini lakini mara ile gari ilisimama ghafraa na nilisikia vishindo vya watu wakiruka na kunizunguka huku ukelele wa mlio wa risasi ukisikika kuwatuliza wananchi waliokuwa wanakuja ndipo nilipotulia hasa baada ya kusikia kauli zao na kugundua kuwa walikuwa ni polisi.
"tulia hivyo hivyo usikimbie zaidi mikono juu sisi ni maafsa wa polisi.."
Ilikuwa ni sauti ya mmoja wa watu walioruka kwenye gari akinisihi na kunisogerea pale niliposimama huku nami nikitii na kuona sasa afadhali msaada umepatikana.
ITAENDELEA….
 
EPS 09
========

Saa tatu kasoro usiku tulishuka eneo husika na kuchepuka kukifata kibarabara chembamba kilichoelekea huko alipopatikana ba mkubwa ambapo kulikuwa na umbali wa kilometa kama mbili kukifikia hiko kijiji.
Kwa kuwa ulikuwa usiku na giza lilishaingia huku kukiwa na kijimbaramwezi kwa mbali ilibidi tutumie tochi kumulikia na njia nzima kulikuwa kimya sana.

Nakumbuka baada ya mwendo kidogo tukiwa tumebakiza kama kilometa moja na nusu kufika mke wangu aliniomba ajisaidie haja ndogo kwani alibanwa mno na asingeweza kuendelea mbele nami nilimuonya ajisaidie palepale njiani asiingie polini kwani kuna wadudu wengi kwenye majani na ndipo nilipompokea mtoto na kusimama kumsubiria.

Nikiwa nimesimama mke wangu anajisaidia ghafra nilisikia chakala chakala na nilipogeuka nilishangaa kumuona mtu aliyevaa kininja akininyang’anya mtoto kwa nguvu na kabla sijafanya lolote kujitetea mara kwa nyuma nilipigwa na kitu kizito bila kumuona aliyenipiga na kujikuta naanguka chini huku kwa mbali nilisikia ukulele wa mke wangu kipenzi Zai akisema.

‘’’’’’Jamaaniii iiiinatoshaaaaa Nilishawaaambiaa msimuuueeee..’’’’’

Sitoweza kuisahau kamwe kauli ile ya Mke wangu Zai.. Zai wangu kipenziii msichana wa ndoto yangu niliyeamini nimeoneshwa na Mungu lakini leo hii anatoa kauli iliyoniaminisha na kuniumiza moyo wangu kupelekea kupoteza fahamu pindi nilipoanguka baada ya kugundua kuwa kumbe mchezo wooooooootee nae alihusika na aliujua vizuuuuri. looh!
Ama kweli adui wako mkubwa ni mtu wako wa karibu na Udhaniae ndie sie ila sie ndie.
Nilijihisi nakaribia kufa huku nikijiuliza kumbe Zai aliishiii kwa kuniigiziaa?!! aaaaaghh!!!!!… Ni vigumu sana kuaminilll! lakini Chunga sana baaabaa Kamishnaaa usiombe kabisa yakukute kama yaliyonikutaaaa.
Siku hiyo ndio kwa mala ya kwanza niliikubali thabiti ile kauli kuwa Wanaake ni Wauaji, nami nakazia kabisa leo hadi siku ya kufa kwangu nitasema kuwa WANAAKE NI WAUAJIIIIII.

*<>* *<>* *<>*

Kilifuata tena kilio cha sauti ya juu na kwikwi kutoka kwa Hussein na kazi ikabaki kwa Kamishna Shaaban Mwinchande kum bembeleza na kumtuliza ili apate kuelewa na kubaini kilichoendelea ktk hadithi yake baada ya kurudiwa na fahamu.
Safari hii sasa hata Kamishna Shaaban mwenyewe alijikuta nae machozi yakim bubujika kwa jinsi alivyokuwa anasikiliza kisa kile cha Hussein na zaidi alipomtazama uso wake wa kiutuuzima uliokuwa unatiririkwa machozi kama mtoto kadri alipokuwa anasimulia na alionesha dhahili kuwa ana ghadhabu kubwa juu ya wanaake kwani ktk hadithi yake ile hadi muda huo ilibeba maumivu tu na mateso yote ameyapata sababu ya mwanamke aliyempenda na pia kwa uzoefu wake wa kusoma saikology za watu Kamishna shebby alizidi kumuamini na kubaini kuwa kweli mfungwa yule alionewa na hakuwahi fanya ubaya wowote.
Lakini maswali bado yalibaki kichwani mwa Kamishna Shebby na alitaka kujua zaidi ilikuaje hadi kukawa na uthibitisho wa maiti hizo mbili ya mkewe na mtoto? na iweje huyo Zai mke wa Hussein afahamiane na hao watu na kueka mbinu kisha wamgeuke pia na wamuue sambamba na mtoto? ilikuwaje kuwaje hapo... na huyo Mr. X ni nani kwa mujibu wa barua ya kutatanisha aliyoipata Hussein.
Japo alikuwa mtaalamu sana Shaaban na alijaliwa ubongo mwepesi ktk kufikiri na kufumbua jambo lakini kwa maswali yale yaliyosumbuka kichwa chake muda ule juu ya hadithi ya Hussein hakuweza kupata majibu ya haraka zaidi ya kumsihi mfungwa wake (Hussein) ajikaze ili aendelee kumsimulia kilichotokea baada ya kurudiwa na fahamu mpaka kukamatwa na kuhukumiwa.

Siku hiyo Hussein japo maumivu yalikuwa mazito mno moyoni mwake kwa kukumbuka mapito yaliyoinyamazisha ndoto zake na kujikuta anazeekea jera akisubiri kifo tu lakini alijitahidi na alipania kuwa aweke kila kitu wazi kwa kijana yule ambae awali hakutambua kama ndio kamishna lakini sasa alijua na hakuwa na jinsi zaidi ya kumuelezea kila kitu hasa baada ya kugundua ni askali kiongozi mwenye moyo wa kipekee sana.

Huku akifuta mafua baada ya kimya cha zaidi ya dakika arobaini Hussein aliendelea kusimulia ilivyokuwa mara baada ya kupigwa na kitu kile kichwani hali iliyompelekea kuanguka na kupoteza fahamu.

*<>* *<>* *<>*
..........

Nilistuka mara baada ya kuhisi hali ya ubaridi na unyevunyevu na nilipotaka kuamka nilijihisi kichwa kuwa kizito sana lakini nilijitahidi na kukaa kitako pale njiani huku nikitazama huku na huko kuangalia kama kuna watu wanakuja niombe msaada ama sivyo nikusanye nguvu nipige mayowe raia waje wanisaidie japo nilijua kuwa pale nilipo kuna zaidi ya kilometa moja kufika kwenye makazi ya watu ambako ndiko pia alipatikana babaangu mkubwa yule mganga wa kienyeji na ndio nia ya safari ile tulikuwa tunaelekea kwake.
Sikujua ilinichukua muda gani mpaka niliporejewa na fahamu kwani nilijikuta niko mwenyewe pale chini.

Lakini niliponyanyua mkono wangu na kutokana na mbalamwezi kuchomoza muda ule nilishangaa kuona umetapakaa damu halkadhalika na mkono mwengine.
Nilijikagua haraka haraka kuona wapi nimeumia lakini bado sikuhisi jeraha lolote mwilini mwangu zaidi ya jeraha dogo kichwani ambalo lilikuwa halivuji damu kivile.
Lakini pia nilipoangalia chini vizuri nilishangaa kuliona panga usawa ule nilipolala likiwa limeloa damu pia kulionekana michilizi ya damu kuelekea kwenye kichaka kimoja eneo lile.
Nilijikuta nikilishika lile panga kwa mshangao na kuligeuza geuza kuhakikisha kama ni kweli au macho yangu yalikuwa bado yana mawenge,! lakini nilipofanya vile akili iliniaminisha kuwa kile nikionacho ni kweli wala si mawenge na hapo ndipo nilipogutuka na kulitupa haraka chini lile panga na kujikuta nimepata nguvu za kusimama na kuanza kunyata kwa umakini kufatilia ile michilizi ya damu kujua nini kilichopo pale kwenye kichaka.
Lakini kabla sijakifikia kile kichaka mara nilianza kusikia kelele kelele za watu wengi waliokuwa wanakuja kwa mwendo wa kasi wakitokea ile njia iliyoelekea kijijini na punde tu nilipogeuka niliona mianga ya tochi ikinimulika huku kwa mbali nikisikia baadhi ya maneno waliyokuwa wanaongea wale watu.

"Mwanaharamu mwenyewe si ndio yuuleeee.."
"Enheeeee yule yule si unaona midamu ilee.."
"Aliyeua auaweeee hebu tupisheni sie mbona hamtembei tutamkosaaa.."

Zilikuwa ni moja ya kauli nilizozisikia toka kwa wale watu huku wengine wakianza kukimbia kuja pale niliposimama nami nikabaki nimeganda kwanza nikiwashangaa na nilipokaza macho kutazama vizuri niliwaona wengine wakiwa wamebeba silaha za jadi na macho yao wote wakinilenga mimi hasa baada ya kunionaa.
"Uuuuuaaaa Huyooooo.."
"PIGA UUAAA.."
Ukelele huu ambao uliambatana na kurushwa kwa mkuki ambao kwa bahati nzuri ulinikosa na ndipo akili ikanicheza na kunionya endapo nitachelewa sekunde kadhaa watu wale wataponikaribia zaidi wataniua kwani walionesha wazi walikuwa hawaji kwa wema wala huruma hata chembe juu yangu.
Nilijikuta naruka na kuanza kutimua mbio huku upepo mkali ukinipitia ghafra karibu na kichwa baada ya kurushwa kwa rungu moja kubwa ambalo niliamini lingenipata huenda ningezima pale pale kama sio kufa kabisa.

Nilikimbia kwa speed ya kunusuru maisha yangu huku nikifata kile kibarabara kilichoelekea barabara kuu kule tulipotoka na nyuma yangu bado niliandamwa na watu wale wenye hasira kali ambao sikuwa na uhakika wa moja kwa moja kuwa ni wanakijiji au ni miongoni mwa wale walionivamia awali!?
Lakini kabla sijafika mbali mbele yangu kulisikika mlio wa gari sambamba na mwanga mkali wa taa zilizonizuia kuona vizuri na kujikuta naingia porini lakini mara ile gari ilisimama ghafraa na nilisikia vishindo vya watu wakiruka na kunizunguka huku ukelele wa mlio wa risasi ukisikika kuwatuliza wananchi waliokuwa wanakuja ndipo nilipotulia hasa baada ya kusikia kauli zao na kugundua kuwa walikuwa ni polisi.
"tulia hivyo hivyo usikimbie zaidi mikono juu sisi ni maafsa wa polisi.."
Ilikuwa ni sauti ya mmoja wa watu walioruka kwenye gari akinisihi na kunisogerea pale niliposimama huku nami nikitii na kuona sasa afadhali msaada umepatikana.
Ajabu aliponifikia cha kwanza nilipigwa pingu na kugongwa mabega na kitako cha bunduki hali iliyonistaajabisha na kunikosesha kabisa nguvu.
ITAENDELEA….
 
EPS 10
========

"Wananchi tunaomba mtulie, mshatoa taarifa kwetu hampaswi tena kuchukua sheria mkononi. kwa pamoja naomba mtusaidie kuona eneo lenyewe la tukio hasa ni lipi na jee mtuhumiwa husika ndie huyu mliyekuwa mnamfukuzaa?"

"Ndioooooo Afande tuachieni tuliue kabisaaa linyamaa hiloo"

Sauti hizi zilizidi kunishangaza na kunishtua kwani mpaka muda huo sikujua nini hasa nilichofanya yaaani badala ya kupewa msaada ndio kwanza nataka kuuawa?
Nilikamatwa suruali na kuanza kutembezwa mpela mpela na wale askali wakiwafata wananchi ambao nao waliongozwa na mtu mmoja kuelekea kule niliposhambuliwa hususani eneo lile la kichaka ambako sikubahatika kuona kilichopo na ndipo mara baada ya askali kufika pale huku wakiwa na matochi makubwa yenye mwanga mkali tulishuhudia maiti mbili ya mama na mtoto mdogo zikiwa zimekatwa katwa vibaya.
Nilijihisi kuchanganyikiwa hasa baada ya kuona nguo za kale katoto ndio zilezile alizovaa mwanangu siku hiyo.
Nilipiga kelele kwa kumlilia zaidi mwanangu nikiamini nae wamemuua sambamba na mke wangu lakini chaajabu ndio kwanza nilizidi kuchezea vitasa na maneno makali kutoka kwa wale mapolisi huku wengine wakinipiga picha.

"Afande Jacobo sogeza gari pia afande Dula weka hilo panga vizuri hapo mbele hakikisha mtu yeyote asilishike direct bila groves pia inabidi turisachi hili liuaji vizuri tuone kama kutakuwa na ushahidi zaidi.. hakikisheni kila tukio linapigwa picha"
Aliongea afande mmoja alioonekana mkubwa wao, wakati huo wote mi nilikuwa nalia sana huku wananchi wakinitazama kwa hasira mno.

Ajabu kilichonistua zaidi na kufanya nipoteze fahamu kwa mara nyengine ni mara baada ya kuanza kusachiwa kabla ya kupandishwa kwenye difenda.
Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni kwani kwenye mifuko yangu ya mbele ya suruali nilikutwa na kipande cha kiganja cha mkono wa mtoto kikiwa kimezungushiwa hirizi.
Aaaaaghhh!!!!!!!!! sikuaminiiii hata chembe nikionacho na mara ndipo nilipojihisi kizunguzungu cha ghafra na network zangu zilizima palepale.

Nilirejewa na fahamu mara baada ya kustuliwa kwa kumwagiwa maji mengi ambapo nilikuwa nimelala kifudi fudi ndani ya bodi la difenda iliyokuwa imesimama na nilipoinua kichwa niligundua nilikuwa peke yangu lakini nilipogeuka sasa kutazama vizuri ndipo nilipoona gari nyingi za polisi zikiwa zimepaki huku askali wengi sambamba na waandishi wa habari walikuwa wamesimama wakinipiga picha nikiwa kwenye ile Difenda hadi walipopanda askali wengine na kunishusha mkuku mkuku huku wakinisukuma na kuniongoza kwenye jengo moja ambalo niliponyanyua uso niliona maandishi makubwa yaliyosomeka KITUO KIKUU CHA POLISI KINONDONI

Nilijua sasa kumbe hatukua kule polini bali tupo mjini na ni katika kituo kikubwa cha polisi ambacho awali nilizoea tu kukisikia na kukiona kwa mbali huku sikuwahi kuwaza hata siku moja kama nami ningekuja kuingia eneo lile kama mtuhumiwa tena kwa kesi mbaya mno.
Sikujua tulichukua mda gani kutoka kule porini kutokana na kupoteza kwangu fahamu na mpaka muda ule akili zangu hazikukaa sawa kabisa na kila kilichokuwa kinaendelea niliona kama ndoto ama sinema tu na si kitu halisi japo ukweli ulibaki kuwa haikuwa ndoto wala sinema.
Nakumbuka baada ya kuvuliwa mkanda na viatu nilisongomekwa katika selo moja huku nyuma yangu nikiandamwa na virungu mfululizo hasa pale nilipotaka kusimama kuongea chochote lakini nafasi hiyo sikuipata.
Niliingia ndani ambapo kulikuwa na mahabusu wengine wakinishangaa kwa jinsi nilivyokuwa, nilijituliza na kukaa kitako kwenye kona ya kuta ya selo ile na kujikuta naanza kulia kwa uchungu mkubwa hasa nilipokumbuka maiti zile ambazo nilikuwa na uhakika kuwa ni za familia yangu hususani nilimlilia sana mwanangu kipenzi kwa kuuawa bila kosa lolote.

"Oyaaa M baba mbona unaleta uduanzi sasa... hebu tukaushie usituchulie hapaa tutakunjenga ooohooo.."

Ilikuwa ni sauti ya kiteja iliyondamana na kofi lililonikuta kichogoni na kunistua kwenye dimbwi la huzuni na mawazo na kunifanya nipunguze mdadi wa kulia kwa sauti na kubaki machozi yanaendelea kububujika yenyewe huku nikiomba kupambazuke haraka.
Asikwambie mtu selo pabaya sana hakuna hata chembe ya raha, harufu mbaya ya kinyesi tulichokuwa tunalala nacho kikiwa kwenye ndoo mpaka asubuhi ndio mtu anaenda kumwaga, hakukuwa na vigodolo wala shuka ya kujifunika na siku watu wakiwa wengi unakosa hata sehemu ya kukaa na kubaki umesimama daaah!! ni afadhali walau maisha ya huku jera japo nayo si mazuri.
Nakumbuka baadae asubuhi yake nilichukuliwa na kuingizwa katika chumba maalum cha mahojiano na mateso na huko nilikutana na askali watatu mmoja wao alikuwa mrefu mtu wa milaba minne ambae ndie alienikalisha kwenye kiti cha chuma na kuanza kunihoji huku wengine wakiandika na kurecord.

"Taja lijina rako upesi.."
Alianza kuniuliza kwa ukali kidogo yule afande baunsa.
"Naitwa Hussein afande.. hus..sein.." Nilijibu huku nikiwa na hofu.
"Taja vizuri bwana Lihuseni nani?"
"Hus..sein.. Bakari..kaka."
"Nani likaka lako wewe?! sina dogo likatiri na Riuaji kama wewe Ebo!.. haya sema kwanini uliua familia yako?"
"Familia yangu!! hapana.. afande sijaua yeyote mbona..!!"
"KELELE.. Tuna ushahidi wa kutosha na tumekukamata eneo la tukio. Unataka kudanganya chombo cha dora wakati vielelezo vyote tunavyo?..! lichawi likubwa wewe ngoja nikupe chai kwanza.."
Aliongea kwa hasira yule afande huku wenzake nao wakinikandamiza zaidi kwa tuhuma za ukatili ambao sikuwahi hata kuuwaza kama kuna binaadam anaweza kufanya vile kwa familia yake mwenyewe aliyoipenda.
Nilifungwa barabara kwa kuinamishwa nikiwa nimekaa kwenye kiti kile cha chuma kilichokuwa na mfano wa kisturi (hakina uegemeo) huku viwiko vya mikono yangu vikiwa sambamba na magoti yangu na kubananizwa pamoja hali iliyofanya nibaki nusu nimekaa nusu nimeinama na ndipo mateso makali yalipoanza sambamba na mijeredi.

Niliumia sana na kulia mpaka sauti ikaanza kunikauka kutokana na mateso yale makali asubuhi ile. Niliwaambia na kuwaapia kadri nijuavyo kuwa sijahusika na tukio lolote baya zaidi ya kwamba mimi na familia yangu ndio tulivamiwa lakini maneno yangu ndio ilikuwa kama chachu ya kufanya mateso yaongezeke zaidi.
Nilitamani hata kifo kije muda ule lakini nacho kilikuwa mbali na mimi. Oooh! sikuamini kama Hussein mimi ambae sikuwa na rekodi hata ya kushtakiwa kwa mjumbe tu ktk makuzi yangu wala kuwahi japo kumtishia mtu na kiwembe achilia mbali kumkata, lakini leo hii nateswa vikali kwa kosa la kuwakatakata na kuwaua vibaya mwanamke na mtoto mdogo? tena eti ni familia yangu? yaani mke wangu na mwanangu mwenyewe!!? aaaaaghhhhh!!!!! kwa mara nyengine nilizimia tena katikati ya mateso yale makali.

ITAENDELEA...
 
EPS 11
========

Nilizinduka baada ya siku mbili na kujikuta nipo hospitali nikiwa nimetundikiwa madripu huku mkono mwengine ukiwa umefungwa pingu sambamba na kona ya kitanda nilicholalia na pembeni yangu bado kulikuwa na ulinzi mkali.
Sikuwa na cha kuongea zaidi ya kububujikwa machozi tu huku moyo wangu ukiniambia kuwa ndio nishaangamia tena sitoweza kubadilisha ukweli labda utokee muujiza.
Baada ya kupata ahueni nilichukuliwa tena mkuku mkuku na askali kisha nikapandishwa kwenye difenda na ndipo mlio wa toori toori (king'ora) ulisikika na safari ilianza kutokea pale hospitali mpaka tulipofika kwenye jengo moja ambalo nililijua vizuri tu kwa nnje kwani ilikuwa ndio njia yangu kubwa ya kupita pindi niendapo na nirudipo kazini, aaaah! ama kweli usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Leo hii hussein mimi naletwa sehemu hii!!? tena kwa staili hii..? Nilijiuliza pindi niliposhushwa na kuzungukwa na askali wenye bunduki na kuanza kuelekea kwenye jengo lile huku eneo zima kukionekana watu wengi hasa waandishi wa habari.
nakumbuka nilinyanyua kichwa kwa mara nyengine na kuyasoma vizuri maandishi yale makubwa yaliyokuwa kwenye lango kuu la lile jengo yaliyosomeka MAHAKAMA KUU YA TAIFA.
Nilishusha pumzi na kichwani niliisikia sauti ikinambia 'Umeangamia Hussein'

Sikuwa na chaguo zaidi ya kutii kila nilichoelekezwa mule ndani ambapo zamu yangu ilipofika niliongozwa na askali wawili na kufikishwa kizimbani kusikiliza kesi inayonikabiri.
Niliangaza huku na kule ndani ya mahakama ile huku kila niliyemtazama alinitazama kwa jicho baya tu na hali iliyoniashiria kuwa nina kesi nzito sana na mbaya mno, nilibaki nimeinamisha kichwa na masikio yangu kuyaelekeza kwa hakimu pale juu japo akili zangu tayari zilishanambia kuwa Nimekwisha.
Hakimu yule ambae alikuwa ni mwanamke alianza kusoma kesi yangu kama ifuatavyo.....

.............
'' Ndugu Hussein Bakari, Unashtakiwa na jamhuli kwa kesi inayohusu mauaji ya kikatili na ya kinyama kama ifuatavyo;.......
Mnamo tarehe kumi mwezi wa pili mwaka huu majira ya saa tatu usiku makao makuu ya jeshi la polisi kitengo cha mawasiliano ya dharula ilipokea simu kutoka kwa msamalia mwema iliyotoa taarifa kuhusu mauaji ya kinyama yaliyokuwa yanaendelea pembezoni mwa jiji maeneo ya Kibamba karibu na kijiji cha Hakipo.
Taarifa ilidai zaidi kuwa huyo kijana (msamalia mwema) akiwa anatoka kijijini kwa mbali aliona mwanaume akiwa na panga mkononi wakibishana na mkewe huku wakinyang'anyana mtoto mdogo ambapo alimsikia mwanamke akimlalamikia mumewe kuwa waachane na ushauli wa mganga wasimuue mtoto wao ni heri wafe masikini, lakini mwanaume alikuwa m bishi na kumtishia mkewe kuwa kama ataendelea kubisha basi atawaua wote na ndipo hapo msamalia yule alishuhudia mwanaume yule akimrushia mapanga mfululizo mkewe na kuanza kumkatakata na kwa kuwa yule msamalia hakuonwa na yule muuaji na alishindwa kusaidia chochote kuzuia mauaji yasiendelee ndipo alipokimbilia kijijini kutoa taarifa kwa wanakijiji wenzake baada ya kupiga simu polisi na hapo ndipo vijana wa polisi walipotoka haraka kuelekea eneo husika ambako walimkuta mtuhumiwa bwana Hussein Bakari akikimbizwa na raia wenye hasira kali huku akiwa katapakaa damu mwili mzima.
Kwa uzoefu na mbinu za kiusalama, polisi waliweza kuwashawishi wananchi watulie baada ya kumkamata mtuhumiwa na kisha kupelekwa eneo husika ambako ilikutwa miili ya marehemu ikiwa imekatwa katwa vibaya sana na walilikuta panga lililogandiwa damu lililoaminika kuwa lilitumiwa kwa mauaji na kama hiyo haitoshi pia walipomsachi mtuhumiwa walimkuta na kiganja cha mkono wa mtoto kikiwa kimezungushwa kwenye kitambaa chekundu kilichofungwa kwa hirizi ikisadikika kuwa mtuhumiwa Hussein alifanya mauaji hayo kwa imani ya kishirikina.
Mwisho wa kunukuu .. ''
..............

Nilinyanyua macho na kumtazama yule mama hakimu kipindi ananisomea kesi yangu huku mwili wote ukiwa umekufa ganzi nilijikuta napiga kelele kwa sauti ya juu sana ambayo sikuwahi kuitoa toka kuzaliwa kwangu
"HAPANAAAAAAA.... HUO NI UONGOOOOOOO"

Hakimu aligonga nyundo baada ya kuanza minong'ono kutoka kwa mawakili na watu waliokuwepo pale mahakamani kutokana na kitendo changu cha kupiga kelele huku nikiambiwa kuwa ni kosa kisheria kwa mujibu wa katiba sikupaswa kuongea mpaka niruhusiwe na baada ya hapo ndipo mahakama ikabaki tena kimya na hakimu aliendelea kwa kusema kuwa sitakiwi kujibu chochote siku hiyo ilikuwa ni kusomewa shtaka tu ila kesi itakuja kusikilizwa rasmi baada ya miezi miwili na dhamana juu yangu ilifungwa kutokana na aina ya kesi iliyonikabiri hivyo ikalazimika nifikishwe segerea kusubiri tarehe nyengine ya kesi.
Sikuamini hadi muda naingizwa kwenye karandinga na safari ya Segedansi (segerea) ilianza huku nikiwa nimepoteza kabisa matumaini ya kuishi na kumuomba mungu akilete kifo upesi kije kinichukue lakini bado kifo kilikuwa mbali nami.
Nilijikuta naongea na mungu mithili ya binaadam mwenzangu ninayemuona huku nikimlaumu kwanini hanitendei haki au muujiza wa kuniokoa kwenye matatizo yale mazito yaliyonikumbuka ilihali anajua fika kwamba sijatenda kosa lolote?
Pia nilimlaumu sana mke wangu ambae hadi muda huo imani ya kuwa nae amefariki sikukubaliana nayo kwani maiti ya yule mwanamke haikufanana na alivyokuwa mke wangu ila niliamini kuwa nimechezewa mchezo mchafu na watu walioshilikiana na mke wangu mwenyewe na kuniulia mwanangu aaaaaah!! nini kilimsibu mama watoto wangu hadi akawa tayari kuacha mwanae anauawa na yeye kuondoka na mwanaume mwengine akiniachia majanga mwanaume niliyempenda na kumthamini siku zote?
Ina maana Zai alikuwa msaliti..!? aagh.. lakini mbona sikuwahi kuona walau chembe ya tabia yake mbaya? Daah niliishia kujiuliza maswali ambayo yalizidi tuu kuniongezea maumivu na sikuwa na chaguo zaidi ya kukubali kuwa sasa mimi ni mtuhumiwa wa kosa la mauaji na hapa segerea ndio makazi yangu mapya mpaka pale nitapohukumiwa.

Nikiwa nimeshaanza kutumikia maisha ya kukosa uhuru ndani ya segerea nikisubiri hukumu yangu, Kumbe upande wa nje kona zote za jiji na mikoa ya jirani kesi yangu nayo ilikuwa moja ya gumzo midomoni kwa watu.
Vyombo vya habari hususani magazeti ya udaku yaliandika na kuchapisha picha mbalimbali zilizohusu tukio langu la mauaji ya kinyama tena kwa familia yangu kwa sababu tu ya kutaka utajiri.
Kila aliyenifahamu alishangazwa na kustushwa sana na habari zile na kutokana na mazingira niliyokutwa na vithibitisho vya uhakika vilivyoolozeshwa kwa mujibu wa habari vilifanya hata walionijua kuamini habari zile na kunilaani kuwa kumbe upole na ustaarabu niliokuwa nawaonyesha ulibeba siri nzito moyoni mwangu tena za kishirikina....!!
Ilinichoma sana na haya niliyapata toka kwa rafiki yangu kipenzi aliyejitolea kuja kuniona segerea mara baada ya ndugu na marafiki wengine kunisusa na kutotamani kuniona huku wengine wakihofia kujitokeza na kuthibitisha kuwa wananijua huenda ikawaponza kukamatwa na wao kuisaidia polisi juu ya ukatili wangu.
Niliangalia baadhi ya vichwa vya habari vya magazeti aliyokuja nayo rafiki yangu yule japo niliishia kuyaona kwa mbali kupitia kidirisha kidogo cha nondo kilichokuwa katikati ya ukuta uliotutenganisha huku nikiwa bado chini ya ulinzi na uangalizi mkubwa tofauti na watuhumiwa na wafungwa wengine waliokuwa pale segerea kwa muda ule.
Sikujua ni kwa sababu tuu ya uzito wa kesi yangu ama ndio taratibu za pale kwa mtuhumiwa mpya au laah.
Rafiki yangu hakunificha kitu kuhusu kazini na maagizo ya bosi kuwa nishafutwa kazi wala nisitegemee msaada wowote wa kiofisi. Daah!! yaani kwa jinsi nilivyoitumikia kwa moyo mmoja ile ofisi na kujituma kwangu kote tena kwa uaminifu wa hali ya juu sikuamini kama leo hii wameshindwa hata kuja kuniona na kunisikiliza ili walau waniekee hata wakili wa kunitetea juu ya tuhuma zile lakini loh! wao pia wamekuwa mstari wa mbele kwa kunitenga.
Niliishia kutokwa machozi tu kila habari niliyokuwa naipata kutoka kwa rafiki yangu yule wa kweli na pekee aliyekuwa na moyo wa kumfariji mtuhumiwa wa kesi mbaya ya kutisha kama yangu lakini hakusita kuniamini nilichomuelekeza na kunipa moyo kuwa nisichoke kumuomba mungu kwani hakuna linalomshinda na haki yangu itasimama tu nisihofu.
Muda mfupi baadae askali walikuja kuniondoa baada ya muda kuisha na kuwapisha watu wengine ktk kidirisha kile na nilimshuhudia rafikiangu akinitazama kwa jicho la kunisikitikia na kukata tamaa hadi nae machozi yalianza kumdondoka.
Nilirudi ndani ya jengo lile la kujichanganya na mahabusu wenzangu lakini haukupita muda mrefu tena niliitwa na askali wawili walinichukua kwenda kuongea na mtu mwengine ambae sikujua ni nani harafu tayari muda wa kuongea na watuhumiwa ulishakwisha.
Niliongozwa na kuelekea tena pale kwenye kidirisha na niliponyanyua macho kuchungulia ni nani mwengine aliyekuja kuniona nilijikuta napata faraja na kuangusha kilio cha matumaini baada ya kumuona mtu yule na kugundua ni baba mkubwa.
Nilielewa wazi ni ba mkubwa pekee ndie aliujua ukweli juu ya tatizo langu na ni yeye tu ndie nilimpigia simu kumuelezea matatizo yote na vitisho vilivyokuwa vinaniandama hadi ukweli juu ya safari yetu aliujua kwani tulikuwa tunaelekea kwake.

"Usilie mwanangu Hussein, huu ndio ukubwa baba huwezi kujiita mkubwa bila kukupitia mitihani mwanangu na unapopata mtihani inabidi utulize akili ujue jinsi ya kukabiliana nao usijiferishe kabla hujajaribu kuufanya mtihani wako hata kama utauona mgumu kiasi gani. Lakini kumbuka kauli yangu miaka ile nilikuonya kwa kukwambia kuwa 'Mpotea njia mara nyingi si muulizaji'
laiti ungeifanyia kazi kauli yangu ile tu nadhani ungeniuliza mapema na pengine haya yote yasingekufika leo hii.
Lakini sikulaumu sana kwa kupotea kwako kwa kuwa bado niko hai nitahakikisha nakutetea kadri niwezavyo kuhakikisha haki inatendeka kwani najua wazi huna kosa mwanangu, wewe si muuaji, wamekupakazia tuu na hata mkeo nina imani kabisa yuko hai.
Usilie wala usihuzunike amini mungu yu nawe na ataweza kukuokoa kama utamuamini kwani kumbuka tatizo lako si kubwa mbele ya matatizo makubwa yaliyowahi kuwakuta watu na mungu akawaokoa. Usijali baba tuko pamoja nami nishajiandikisha kama shahidi wako siku ya kesi nitakupigania. "

Maneno ya Ba mkubwa yalinitia nguvu sana na faraja lakini hayakuzuia machozi yaliyokuwa yananidondoka yaache.
Nilishangaa pia kuona hisia zangu zimelingana kabisa na maneno ya ba mkubwa kuwa Zai si yule mwanamke aliyeuawa siku ile na kubaini kuwa kumbe ba mkubwa alikuwa na siri nyingi kuhusu mke wangu Zai..! ina maana alimjua hapo kabla ama vipi? na jee sasa hivi yuko wapi? hapo nilikosa jibu kabisa pia nilitamani kumuuliza Ba mkubwa kuhusu huyo Mr. X kama anaweza kuwa anamtambua lakini muda wa kuendelea kuongea haukuturuhusu mara baada ya askali kumtoa ba mkubwa kule nje nami kurudishwa ndani kabisa ya gereza.
ITAENDELEA......
 
EPS 12
========

Siku zilienda hatimae ilipita miezi miwili nikiwa segerea na ilifika tarehe ya kesi yangu ambapo siku hiyo asubuhi na mapema niliingizwa kwenye karandika sambamba na watuhumiwa wengine wenye kesi tofauti tofauti na safari kuelekea mahakamani ilianza tukiwa chini ya ulinzi mkali.

Tulifika kwenye viwanja vya mahakama kuu na kutelemshwa ambapo siku hiyo niliushuhudia umati mkubwa ulifurika huku wengi wao wakinyoosheana vidole kuelekezea kwangu ndipo nilipobaini kuwa ni kweli kesi yangu ilikuwa ni moja ya habari iliyotikisa.
Zamu yangu ilipofika nilifikishwa kizimbani na siku hiyo sikuwa nalia kama ilivyokuwa siku ile ya kwanza.
Nilimudu kutazamana na watu waliokuwepo mule ndani ya mahakama japo wengi wao walinitazama kwa jicho baya lakini niliwapuuza na kuwasikitikia kwa kutojua walitendao.

Macho yangu niliyaelekeza kila pembe ya mahakama kwa umakini mkubwa nikimtafuta ba mkubwa na kweli nilimuona nae alikuwa ananitazama na kunipa kwa kuinamisha kichwa kuwa yupo pamoja nami na nilitegemea pia ushahidi wake pekee kuwa ndio utetezi mkubwa kwangu.
Niliendelea kuangalia kona nyengine kwa makini kujua kama kuna mwengine ninayemfahamu kaja kusikiliza kesi yangu na kipindi hiko hakimu alikuwa ndio anaanza kuisoma tena ile kesi nami ktk kupepesa pepesa macho huku na kule nilimuona rafiki yangu kipenzi yule aliyenitembelea segerea na tulipokutanisha macho alitabasam kwa kunionesha ishara kuwa yuko pamoja nami.
Nilijisikia faraja kwa namna furani na kumshukuru mungu kwa kuwajua rafiki na ndugu wa kweli kwangu kwani ni vigumu kumtambua rafiki wa kweli au ndugu wa kweli kama hujapatwa matatizo makubwa.
Siku hiyo ndio nilizidi kuielewa na kuimbuka misemo mingi ya wahenga ambapo awali nilichukulia kama burudani tu kwa watoto lakini baada ya majanga nikakubali kuwa Akufaae kwa dhiki ndie rafiki pia umdhaniae sie ndie, kwani sikuamini kama mjombaangu aliyetoka tumbo moja na mamaangu angeweza kunisariti na kutofika ilihali nilimthamini na kumsaidia sana huku nikimpuuza ba mkubwa kuwa ana mila za kizamani lakini leo hii niliyempuuza ndie kaja kunifariji jera na mahakamani yupo ila yule niliyemtegemea awali hata salamu zake za kunifariji sikuzipata. Ina maana ameamini mimi ni muuaji na katili kwa kiasi kile? aaah kweli binaadam hukukimbilia pindi mungu anapokupa neema lakini hukukimbia pindi anapokupa mitihani.

Lakini wakati nilipogeuza shingo upande wa kushoto karibu na alipokaa rafiki angu nilishangazwa mno na kile nilichokuwa nakiona safari hii.
Aaaagh!! moyo wangu uliripuka na kupiga paah! huku nikiwa siamini pindi nilipokutanisha macho na mtu ambae nilimtambua vizuri sana tena sana nae alinitambua vizuri tu nilivyo.
Mtu ambae niliamini ni adui yangu lakini macho yake hayakuonesha kuwa yana uadui na mimi kwani yalipokutana na yangu tu yalianza kutoa machozi na kunihurumia akionesha kuwa eti ameumizwa na kesi yangu nae kaja kuniunga mkono.
Machozi yake ndio kwanza yalinichefua zaidi kwani akili yangu ilinambia kuwa 'Huyu nae anahusika kwa haya yaliyokukuta'
Msschhhhhh...!!! Na ndipo nilipojikuta natoa sonyo kali sana lililosikika vizuri mahakama nzima kutokana na utulivu uliokuwepo na muda ule kumbe Hakimu alikuwa ananiuliza swali juu ya shtaka langu lililopaswa nijibu kweli au si kweli lakini kutokana na kuhama kwa mawazo yangu nilijikuta nasonya wakati mahakama imenitegea sikio mimi kusikia jibu langu kama nakili au nakana shtaka..!?
Aaaaaaaaaaaaaagh!!!!
Ama kweli ulimi unaponza Kichwa

" Kutokana na kifungu namba 279 sheria ya mahakama iliyopitishwa na kuhakikiwa upya mwaka 1972 kuwa mtu yeyote hata akiwa mtuhumiwa endapo ataonesha lugha yoyote inayoashilia aidha matusi au dhalau ndani ya mahakama hilo ni kosa la jinai na adhabu yake ni kuisimamisha kwanza kesi husika na kupitisha kifungo cha miezi kumi na mitatu jera sambamba na kazi ngumu na bakora kumi. tano siku ya kuingia na tano siku atayotoka na kama muhusika alikuwa mtuhumiwa inapaswa kutorudi uraiani ila baada ya hapo atarudishwa mahakamani ndipo kesi yake husika itatajwa tena na kusikilizwa.
Nami kwa kufata kanuni na sheria hiyo nakuhukumu bwana Hussein Bakari kwenda jera kwanza mwaka mmoja sambamba na adhabu hizo nilizozitaja ili ukajifunze kwanza adabu na heshima ili utaporudi tena mahakamani uoneshe utiifu na adabu nzuri..."

Nilistushwa mno na maneno yale toka kwa hakimu yule wa kike licha ya kwamba niliomba msamaha tena kwa kupiga magoti mara baada tu ya kusonya na kukumbuka kuwa nipo mahakamani lakini hakimu hakuonesha hata chembe ya kujali kile nilichokisema na baada tu ya kutamka maneno yale aligonga nyundo mezani mara tatu ndipo askali wakaja kunitoa pale kizimbani na kunifunga pingu ambapo nilimgeukia tena yule hakimu kwa uchungu nikamuangalia na yule mtu alieniponza ambae alikuwa ni mwanamke amemshika mtoto mdogo nae wa kike wa umli wa miaka kama mitatu hivi.
Hakuwa mwengine yule mwanamke bali ni Mariamu yule mwanamke wangu wa kwanza kumpa moyo wangu na kumthamini nikitegemea atakuja kuwa mke wangu lakini kwa alichonitendea na kunisariti huku akinikana mchana kweupeee na kunisababishia maumivu makubwa ya kutendwa kwa mara ya kwanza.
Nilimuangalia kwa jicho baya sana Mariam aliyekuwa analia machozi ambayo niliamini kuwa ya kinafki kwani kama kweli alikuwa ananipenda na kuniulumia mbona hakulia siku ile niliyokuwa nachezea kichapo kwa baunsa wake hadi almanusura ninyofolewe roho lakini ndio kwanza alivunjika mbavu kwa kicheko pale nilipotimua mbio kujinusuru..
Eti leo hii anajifanya kunisikitikia na kunililia kwa lipi hasa yaani nipo ktk mkondo wa sheria anajifanya kunililia ila nilipokuwa kwenye mkondo wa mtu aliyekuwa anajichukulia sheria mkononi alinicheka..! kama si unafki nini? Nilimuangalia zaidi kwa jicho baya kila mwanamke niliyemuona mbele yangu muda huo nikiona wote ndio wale wale na hapo ndipo ilipokuja sauti ya yule mlemavu kichwani mwangu kanakwamba ananinong'oneza na kuisikia kwa mara ya kwanza kabisa ikinipa pole na kunambia hivi...

' ' 'Usimshangae hakimu wala yule aliyekufanya usonye kwa sababu wote ni wanaake Hussein.
Wengi hawawajui walivyo lakini ni wazuri tu kwa nje ila mioyo yao mibaya sana japo ina huruma na imezungukwa na hofu lakini inaponzwa na vichwa vyao wanavyoviacha wazi ambavyo vina ubongo wenye kiza ambao shetani hupendelea sana kujificha ndani yake na kuwaongoza anavyotaka na kuwafungia milango ya kufikiria katika maamuzi yao na ndio maana wanafanya vitu vya ajabu mara nyingi hata wanapojidhalilisha wao wenyewe hawajioni na wanachukulia sawa tu.
ona Mwanaume una ubongo mng'avu unaoweza kummulika na kuusaidia ubongo wa mwanamke na kumuongoza vizuri lakini kwa kuwa shetani hataki hilo na amejiekea makazi kiurahisi kichwani kwa mwanamke huyo ndio sababu utapomwambia ukweli huu lazima kwanza akasilike na kukuchukia akidhani hata yeye ana haki ya kukutawala na kukuongoza pia hataki kuongozwa akiziamini akili za kichwani mwake zinazoongozwa na shetani kuwa wanaake na wanaume wote sawa na wapo ktk daraja moja hivyo ujue Hussein wanaake wote wenye imani hii wasiotaka kujishusha mbele ya wanaume hao ndio miongoni mwa wauaji na waliopotea na hawana soni wala haya kwenye nyuso zao...
lakini utapoona umemwambia haya mwanamke nae hajakasirika wala kukuchukia na akakili kuwa yuko chini ya mwanaume basi huyo mwanamke ni miongoni mwa wanaake wa peponi waliobarikiwa na mungu ambao wamefanya jitihada kubwa binafsi za kumfukuza shetani vichwani mwao na aina hii ya wanaake hupenda sana kujishusha na hawajifanyi kujua zaidi mbele ya wanaume na wanaake hawa hupenda kufunika vichwa vyao si kwa nguo tu bali nyuso zao zimejaa soni na haya hata wanapokutana njiani na wanaume basi huwapisha huku vichwa vyao wakiviinamisha chini.
Lakini kwa karne hii ya sasa wanaake hao wamekuwa hadimu na ni wachache mnooo Hussein wengi waliobaki ni Wauaji watupu hata wale wanaojifanya wanapenda dini karne hii lakini ona tabia zao tofauti kabisa na mafundisho ya hizo dini, ona Hussein ona wengine wanaenda makanisani wakiwa wamevaa viguo vifupi na visuruali vya kuwatega wanaume na kufanya waharibu ibada zao hawana haya si kwenye makanisa tu hata kwenye misikiti na madrasa huoni Hussein wanaake wanavaa mahijabu kama mapazia? vigauni kama vyandarua pamoja na kanga nyepesi kama karatasi? yoote hii kuwaponza wanaume tu na kuwaharibia ibada zao kwa kuwasababishia dhambi kimakusudi lakini bado ukiwaambia watakukasilikia.
Na mwanaume ataposhindwa kuutumia vizuri ubongo wake akiwa na mwanamke na kujifunza jinsi ya kuishi nae basi ndio hutokea majuto mwishoni kama haya ya kwako Hussein.
Kumbuka wanaake huwa hawafikirii kwanza kabla ya kunyanyua midomo yao na siku zote wanajiona wao wanaonewa na kuhisi wanaume wanapendelewa bure tu hivyo wanapopewa nafasi au wadhfa kama wa yule hakimu hupenda kujionesha kuwa nao wanaweza kwa msukumo wa shetani na ndio wanapoonesha makucha yao wakitaka ushindani kwani amini laiti hakimu yule angekuwa mwanaume kwanza angekuonya kwa maneno tu kesi ingeendelea na kama ungerudia tena ndipo angekupa hiyo hukumu lakini ndio hivyo Hussein usishangae sana wala usiumie kwa sasa kwani hao ndio wanaake bwana nilikwambia usiwaamini sana uwe makini nao ukapuuza.... wanaake ni wauajiii Hussein usiogope kusema haya maneno popote ili uwaokoe na wanaume wengine wasikie na waelewe wakajifunze jinsi ya kuishi nao .
ITAENDELEA.......
 
EPS 13
========

Hussein waambie ... waambie sasa... waambieeee kwanguvu wasikiee waambieee usiogopee .. usiogopee usiogopeeeeee.... ' ' '

Baada ya kusikia maneno haya ktk fahamu zangu nilijikuta napata ujasiri na kupayuka kwa nguvu pindi napandishwa kwenye karandinga na kusema
WANAAAAAAKEE NI WAUAJIIIIIII
Na hii ndio ikawa mara yangu ya kwanza kutamka maneno haya hadharani.

* * * *

Siku zilienda ambapo muda wote toka nianze kutumikia kile kifungo cha mwaka mmoja sikuwa na rafiki jera wala sikutaka urafiki na yeyote yule nikiamini rafiki angu ni mmoja tu yule aliyekuja kunitembelea na ndugu yangu ni mmoja tu nae ni ba mkubwa tu basi lakini hawa wengine wote wataniongopea kwa kuwa tupo ktk hali moja tu wakitoka kila mtu atafata yake kwani niliokuwa nao uraiani nao walinisapoti kwa kuwa tulikuwa ktk hali moja ila leo nimepata matatizo mabaya tena ya kusingiziwa lakini wote wamenigeuka na kuniacha peke angu hivyo baada ya hapo ndio nikaanza kuwa na tabia ya kukaa peke angu na kufanya kazi kwa nguvu muda wote na inapofika wakati nikikumbuka matukio yaliyonikuta na hadithi za yule bwana ambazo zilikuwa zinanijia kichwani mara kwa mara huku nikiisikia sauti yake na hapo ndio nasemaga makusudi kuwaambia wengine kuwa 'Wanaake ni Wauaji' japo wengi waliishia kuniangalia na kudhani kuwa nimerukwa tu na akili.

Siku zilipita hatimae kifungo changu kiliisha na baada ya kufanyiwa vipimo nilikung'utwa bakora zangu tano zilizobaki na siku chache mbele baada ya kupata uwezo wa kusimama nilifikishwa tena kizimbani.
Eee.. asikwambie mtu zile bakora heri uzisikie tu kwa wenzako usiombe zikukute kwani ziko tofauti na bakora za shule nilizozizoea yaani fikiria bakora tano tu mtu wa mazoezi kama mimi nilishindwa kusimama, kama una afya mgogoro unaweza kukata upepo kabisa (kufa).

Basi baada ya kufika kizimbani na hakimu alikuwa yuleyule mama kesi ilianza tena kuunguruma ambapo kwa upande wa mashtaka ambao ilikuwa serekali wenyewe ulileta ushahidi mbali mbali zikiwemo zile nguo nilizovaa za tukio panga na kiganja cha mtoto ambacho kilihifadhiwa muda wote na nilipoulizwa kuhusu kuvitambua vile vitu ambapo nilikubali kuzitambua nguo tu kuwa ni kweli zilikuwa za kwangu lakini vile vyengine vyote nilikataa ndipo alipopanda daktari aliyenichukua alama za mikono baada ya kukamatwa na kuleta majibu ambayo yalikuwa yamefanana na alama za mikono ya mtu aliyelitumia lile panga hali ile ilinishangaza pia kwani nilishasahau kuwa kweli niliwahi kulishika lile panga lakini sikulitumia kudhuru chochote.
Ushahidi wote na maswali ya mawakili yalizidi kunibana na nilichoka zaidi baada ya kupanda dogo aliyethibitisha kuuona ugomvi baina yangu na mke wangu tukigombania mtoto huku nikiwa na panga mkononi ambapo yule dogo alikuwa chini ya miaka kumi na nane na alihesabika kama mtoto kwa mujibu wa sheria iliamini hasemi uongo.
Niliumia sana na kumtazama yule dogo alivyovuka mipaka kuongea kitu ambacho hakikutokea hadi akawa anatoa machozi pale mahakamani kukazia uongo wake.

Niliamini kuwa nimekwisha na nilishindwa kupiga kelele kumstopisha yule dogo nikihofia yasije kunikuta yale ya mwanzo na kumuacha anikandamize tu lakini baada ya yule dogo nilistuka pindi niliposikia anatajwa shahidi upande wa mshtakiwa na moyo ulipata faraja kidogo mara baada ya kumuona ba mkubwa akisogea kizimbani nami nilimtazama kwa jicho la kushukuru kwani nilijua yeye ndie tumaini pekee kwa muda ule lakini alipopanda na baada ya kuapishwa akaanza kuzungumza ba mkubwa maneno yaliyosafirishwa kwa sauti yake mwenyewe na yalipenya vizuri masikioni mwangu na kuingia ktk milango yangu ya fahamu kabla hayajaenda kutua kwenye moyo wangu na kuufanya ustuke kupita maelezo huku nikijihisi viungo vyangu vyote vimeshindwa kufanya kazi hadi macho yalishindwa kupepesa na kubaki yameganda kwa ba mkubwa kwa kutoamini kama ndie yeye au..? aaaaah!!!!! sikuamini hata kidogo kile nilichokisikia.

Nayakumbuka vizuri maongezi yale baada ya kuapishwa ba mkubwa na wakili yule wa serekali alisimama na kumuuliza kama ananitambua nae akasema ananitambua kisha wakili akamuuliza tena.
"Unamtambua tambua vipi mtuhumiwa hebu ifafanulie mahakama.."
"Ndio namtambua bwana Hussein Bakari kama mwanangu kwani ni mtoto wa marehemu mdogo wangu wa tumbo moja.."
aliongea ba mkubwa kisha wakili aliendelea kuhoji..
" Sawa, kumbe Hussein ni mwanao kwa namna moja je una lipi la kuiambia mahakama juu ya kesi inayomkabiri mwanao ?"
" Nipo hapa kwa ajili ya kutoa ushahidi kwa kile ninachokijua kuhusiana na tukio zima na kesi inayomkabili mwanangu"
Aliongea Ba mkubwa maneno yake ya awali ambayo yalinipa moyo kuwa amekuja kunitetea na kuongea ukweli lakini mara baada ya hakimu kumruhusu aongee kile alichokijua ndipo nilipostaajabu kumsikia ba mkubwa akisema....

" Muheshimiwa hakimu nakumbuka miezi miwili kabla ya tukio mwanangu Hussein alikuja katika kijiwe changu kwani mimi ni mtaalam wa tiba asilia na alionesha hali ya kuchanganyikiwa kidogo ambapo nilipomuuliza kulikoni hakunambia ukweli zaidi ya kusema maisha yanamchanganya kisha akaniuliza ktk dawa zangu hivi sina dawa ya kumfanya mtu awe tajiri? hapo nilicheka na kumwambia mwanangu kuwa hutajiri hauletwi kwa dawa bali ni juhudi tu binafsi ktk kazi na kujituma kimaisha bila kusahau kumuomba mungu . Aliondoka siku hiyo lakini miezi miwili baadae wiki moja kabla ya tukio nilipigiwa simu na mkwe wangu marehemu mkewe mwanangu Hussein na alinambia kuwa wana matatizo makubwa na ugomvi baina yao kuhusu mtoto ... Na nilipouliza zaidi kulikoni ndipo mkewe alinambia kuwa kutokana na kuchoshwa na ugumu wa maisha mumewe alienda kwa mganga mmoja ambae hakunitajia ni wapi na anaitwa nani lakini alichosema ni kuwa alienda kwa lengo la kupata dawa ya kuweza kuwa tajiri ili wajikwamue na maisha magumu waliyokuwa nayo.
Na mganga wake alimwambia masharti ya dawa hiyo ili itengenezwe inapaswa amtoe kafara mamaake mzazi au mtoto wake mwenyewe na apeleke kiganja chake ndipo atafanyiwa hiyo tiba na kuwa tajiri hivyo kwa kuwa mamaake alishafariki na pia alikuwa na mtoto pekee ndipo alipomfikishia mkewe habari zile na kumshauli wamuue tu mtoto wao ili watajirike na baadae watazaa wengine lakini mkewe alimkatalia na ndipo ugomvi ukaanzia pale. Nami kwa busara zangu siku moja kabla ya tukio mapema nilipiga simu ambapo nikasikia ugomvi mkubwa baada ya simu kupokelewa na baadae ndipo alipoanza kuongea mkewe ambapo niliwaomba waje kwangu nia na madhumuni nimuonye mwanangu Hussein kwa kile anachotaka kukifanya kwani safari ile nilimsikia kwa masikio yangu na kwa bahati nzuri nilimrekodi.
Lakini cha ajabu alimlazimisha mkewe na kuamua kuja kesho yake usiku na kutokana na mazingira ya kule kuwa polini ndipo alipata nafasi ya kufanya tukio.
Ki ukweli muheshimiwa Hakimu na wazee wa baraza inauma sana kuusema ukweli huu kwani Hussein ni mwanangu lakini nikiongopa kwa ajili ya kutetea nitakuwa nimejiekea mzigo wa dhambi tu mbele za mungu... na nina ushahidi wa record ktk simu niliyopiga siku hiyo. ila ninachoomba cha mwisho muheshimiwa mumsamehe tu mwananguu...uuuuh..."

Aliongea ba mkubwa na kumalizia kwa kilio kisha ilitegwa kwenye mike ile simu yake aliyosema kuna hiyo record na kweli mara spika zilizokuwa kwenye mahakama zilianza kutoa sauti na kweli ulisikika ugomvi wa mwanaume na mwanamke wakigombania kumuua mtoto wao ambapo nilizidi kustaajabu kwani sauti ya mwanamke kweli ilikuwa ni ya Zai wangu na pia sauti ya mwanaume ilifanana kabisa na yangu japo kiukweli hatukuwahi hata siku moja kuzozana na Zai lakini daaah!!! mchezo niliofanyiwa pale ulinichosha sana na kuamini kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni ina maana hawa watu waliikopi hadi sauti yangu na kuiigizia?
Imekuaje ba mkubwa nae ameshirikiana nao kuniangamiza ilihali awali aliapa kunisaidia?

Basi ba mkubwa alipomalizia kunipigilia msumali wa moto kwenye utosi sikuwa na cha zaidi zaidi ya kukubali kuwa sina jipya hata nikitolewa kuwa huru sitokuwa na manufaa yoyote ulimwenguni hivyo nikamuomba mungu ipitishwe hukumu ya kifo juu yangu ili nikapumzike kwani maisha ya dunia ndio basi yameshanisariti.
Lakini hakimu aliisogeza kesi tena kwa kutakiwa nikafanyiwe vipimo vya ubongo kama sikuwa na tatizo lolote la kiakili kwani kwa mujibu wa katiba serekali haikuamini uchawi na imani za kishirikina na majibu ya daktali ndio yataongoza na kuisaidia hukumu husika.
ITAENDELEA,,,,,,
 
EPS 14
========

Kesi iliahilishwa na kufanyiwa vipimo na mwezi mmoja baadae nilirudishwa tena kizimbani ambapo daktari alithibitisha kuwa sikuwa na tatizo lolote la ubongo linaloweza kuafect akili zangu kwa hiyo vipimo vya kichwa vilionesha niko safi kabisa.
Na hapo ndipo hakimu aliponigeukia na kuniuliza kama nina lolote la kujitetea..?
Nilimuangalia hakimu yule ambae safari hii hakuwa yule mama na nilistaajabu sana kwani haikuwa kawaida japo nilipokuwa gerezani baadae ndipo nilisikia habari kuwa yule mama wiki moja kabla ya kesi alipatwa ajali mbaya iliyomfanya alazwe wiki nzima i.c.u na siku niliyohukumiwa nae alifariki siku ileile....
Basi, nilimuangalia yule hakimu na kumwambia kuwa..
"Ndugu Hakimu, mimi ni mkosaji niliepoteza nafsi za watu, sina chochote cha kujitetea kwa kuwa tayari nipo mikononi mwa sheria. Ninachosubiri tu nilipwe ujira sawa kama nilivyoifanyia familia yangu ili niwafate huko walipo.
Naiweka nafsi yangu mikononi mwa mahakama hii tukufu niko tayari kuhukumiwa."

Maneno yangu yalimshangaza kila mtu aliyekuwa pale mahakamani mpaka hakimu mwenyewe nilimshuhudia akishusha miwani yake ya macho chini kidogo na kuniangalia vizuri kisha akaipandisha tena kuwaangalia wazee wa baraza na baada ya kimya kama cha dakika tano ndipo hakimu aliposoma hukumu yangu.

......
"Bwana Hussein Bakari, baada ya mahakama hii tukufu kufanya uchunguzi yakinifu kwa kuzingatia sheria na taarifa za mashahidi mbalimbali na vipimo vya madaktari juu ya tukio lililotokea la mauaji.
Mahakama inakutia hatiani moja kwa moja bwana Hussein Bakari kwa kosa la mauaji ya mke na mtoto.
Na kupitia kifungu namba 94 sheria ya mahakama iliyopitishwa mwaka 1981 kuwa endapo mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ikaonekana dhahili aliua kwa makusudi basi hukumu yake ni ya kifo moja kwa moja.
Lakini pia kifungu hiki kilihakikiwa upywa mwaka 1990 kuwa endapo mtuhumiwa huyu akakili na kuonesha kutubia kosa lake kabla ya hukumu basi mahakama itaangalia chaguo juu ya hukumu yake aidha ahukumiwe kifo anyongwe ama ahukumiwe kifungo cha maisha jera na kazi ngumu.
Nami kupitia kifungu hiki cha mwaka 1990 nakitumia kukuhukumu bwana Hussein kutokana na majuto uliyoyaonesha mbele ya mahakama kwenda jera kwa maisha yako yote yaliyobaki sambamba na kazi ngumu. Na hii iwe fundisho kwa watu wote wenye tabia kama hizi kutaka mafanikio kwa njia haramu na kusababisha vifo vya watu wasio na hatia.
Mwisho wa kuhukumu... Askari mchukueni kufungo chake kimeshaanza sasa. "
............

Aliongea yule hakimu nami sikulidhishwa na hukumu ile huku nikisisitiza kwanini nisingehukumiwa kifo.?

" Hapanaa Hakimu umekoseaaa.... kumbuka aliyeua anapaswa auaweee.... niueni tuuu... Niueniii tuuu hiyo sio hakiii.."

Nilipiga kelele hadi walionichukia wakawa wananishangaa na kunihurumia ndipo nilipoingizwa kwenye karandinga na muda mfupi baaadae safari ilianza kwenda kutumikia kifungo changu.
Lakini nikiwa nachungulia kwa nje ndipo nilishangaa kuna mtu alikuwa akilikimbilia gari lililotubeba na kulisimamisha huku mkononi mwake akiwa na barua.

Askali walijaribu kumzuia lakini alilalamika huku akiinyoosha juu ile barua japo sikumsikia alichokuwa anaongea lakini nilimtambua vizuri mwanamke yule ndie alikuwa ni Mariam aliyenitenda hapo awali na sikujua alikuwa na jipya gani na kama barua ile ilinilenga mimi ni kwa nia na dhumuni gani hasa.
Nilipotezea na kuzungusha shingo yangu ndani na kuinamisha kichwa chini kwani sikupenda kabisa kuendelea kuuona uso wa mariam kule nje na hatimae gari iliingia barabara kuu na safari ya kwenda kumalizia ngwe iliyosalia ya maisha yangu ikaanza huku kichwani mwangu nikilaumu kwanini sikuhukumiwa kifo moja kwa moja.

Nilifika kwenye hili gereza kwa mara ya kwanza na baada ya kupewa namba na kukabidhiwa sale maisha mapya yakaanza rasmi lakini siku chache tu tukiwa tunavunja mawe eneo moja niliitwa na afsa magereza mmoja na kunikabidhi barua ambayo ilinitonesha zaidi na kuniliza pia na siku hiyo niliapa kuwa sitozungumza na yeyote kuhusu yaliyonikuta kwani sikupenda niendelee kujitonesha maumivu haya ya kihistoria kwenye maisha yangu.
Kwa muandiko tu wa ile barua nilijua fika imetoka kwa Mariam kwani hati yake niliielewa vizuri ndipo nilipobaini kuwa huenda hii ndio barua aliyoikimbizia siku ile nilipohukumiwa na kuna askali mmoja aliichukua kati ya wale waliomzuia.
Nilitulia kwenye kivuli na kuanza kuisoma ile barua ambayo ilikuwa imeandikwa pande zote mbili za karatasi kutokana na urefu wake sitoisahau hii barua ambayo ilikuwa ya mwanzo na mwisho ktk makazi yangu mapya haya ya jera na ilianza kwa kusema...
.............
" ''Najua sikustahiri kusogea mbele ya macho yako kutokana na yale niliyokutendea siku za nyuma lakini naomba unisamehe ndani ya nafsi yako ili hata nitapokufa niwe nimejipunguzia walau uzito kidogo ndani ya mzigo wangu mkubwa wa dhambi.
Ukweli nilikupenda lakini sikuwa mke mwema kwako.
Nilikuwa msariti wa penzi lako kwa kufata maneno na ushauli wa shoga zangu kuwa mwanaume mmoja hatoshi kwa mwanamke mrembo mwenye kuhitaji mambo mazuri kama mimi na hivyo ndivyo ilivyokuwa hata pale nilipokukasirikia nilimpigia simu na kumfata bwana mwengine ambae nae aliamini mimi ni wake pekeake na ndie yule mliyepigana kule beach.
Madhumuni ya barua hii si kukuumiza kwa kukukumbusha yaliyopita bali ni kukutaka ujue kuwa una damu yako inayoishi uliyoitumbukiza tumboni kwangu miezi michache kabla hatujatengana.
Na hata siku ile ya mwisho niliyokuja kwako nilipanga kukufanyia suprise ya kukwambia swala hili lakini habari ile ya kwamba wanaake sisi ni wauaji ilinikera mno kwa kuwa alichokuwa anaongea yule bwana kilinirenga kweli na kuna mengine yalinigusa kabisa na kuniumbua moyoni.
Nilikuchukia na kujaribu kuitoa ile mimba baada ya kuachana lakini ajabu ilishindikana na kuendelea kukua hali iliyofanya kuachwa na mabwana zangu wengine baada ya kila niliyemsingizia kuikataa kwa kugundua hesabu ya miezi.
Ukweli mwezi ule nilionasa sikutembea na mwanaume yeyote zaidi yako na hata ukipiga hesabu mwezi niliojifungua na umli wa mtoto utakumbuka kila kitu.
Najua imekuwa too late na laiti ningejua awali ningekwambia ukweli tu lakini baada ya kusikia majanga yaliyokukuta nafsi imeniuma sana na mimi ni mmoja kati ya watu wasioamini kabisa kama kweli ulifanya mauaji yale.
Niliisikia sauti yako siku ile mahakamani uliposema kuwa Wanaake ni Wauaji nami moyoni sikuchukia kama siku ile na nilikubaliana nawe kwa namna frani nahisi hata kesi yako umeponzwa na mwanamke.
Nasikitika ninapomuangalia huyu mtoto ninayemuacha katika hali ya uyatima kwani hapa nilipo nimegundulika nina kansa ya koo na sitoweza kupona kwa mujibu wa ripoti ya daktari kuwa imesababishwa na uchafu mwingi wa mbegu mbovu za kiume uliokuwa unapenya kwenye vijitundu vya ulimi wangu na kwenda kurundikana kooni na kutengeneza wadudu wabaya walioanza kushambulia koo pasi namie mwenyewe kujua.
Usishangae Hussein huo ndio ukweli, na hii yote ilisababishwa na tabia yangu ya muda mrefu kupenda kunyonya tupu za wanaume tofauti mara kwa mara kwa lengo la kuwachanganya kimapenzi ili nipate kuwachuna vizuri lakini leo hii najuta kwa kukiona kifo changu kikiwa kimenisimamia nikiwa kwenye umli mdogo bado na kumuacha mtoto ambae najua hatomuona tena babaake kutokana na hukumu uliyopewa.
Nilikuwepo nae siku ile ya kesi yako na alilia sana pindi ulipotolewa kwa kusukumwa huku ukipigwa kuingizwa kwenye karandinga baada ya kusonya mahakamani...
Nakuombea mungu akunyooshee mkono wa kheri na atende muujiza kifungo chako kiwe chepesi.
Mtoto huyu anaitwa Asha na kwaajabu ya mungu nyuma ya shingo yake karibu na sikio amezaliwa na alama kama ile uliyokuwa nayo na sasa ana miaka mitatu na miezi sita.
Japo nae ni wa kike lakini huko ulipo naomba umuombee ili asije potezwa katika mkumbo na kuwa miongoni mwa Wanaake Wauaji.

Ahsante kwa kuisoma barua yangu....
Ni mimi mfu mtarajiwa MARIAM

...............
ITAENDELEA....
 
EPS 15
========

Nilitetemeka na kukakamaa mithili ya mtu aliyepatwa homa ya ghafra kwenye mazingira ya baridi kali au mtoto aliyebanwa na degedege na kujikuta machozi yananitoka huku nikiikunjakunja ile barua ya Mamu na kuanza kugugumia kwa uchungu.
Moyo uliamini wazi kuwa huyo kweli ni mwanangu hasa baada ya kusikia kazaliwa na alama kama ile niliyokuwa nayo shingoni mwake kwani hata mwanangu wa kiume waliyemuua nae alizaliwa na alama hiyo pia na mimi nilizaliwa nayo nikiirithi toka kwa babaangu.
Lakini sikuwa na cha kufanya zaidi ya kumuachia mungu ajuae yote na sikuweza kumlaumu kwanini sikujua mapema kumbe nilikuwa na mtoto mwengine aliye hai.
Lakini nililia tena kwa kumsikitikia mwanangu ambae nilijua fika kwa mazingira atayolelewa hatokuja kuwa kati ya wanaake wachache wema zaidi niliona kuna muuaji mwengine anaandaliwa aliyetoka kwenye mifupa yangu.
Nilinyanyuka na kucheka kwa sauti kubwa sana kicheko ambacho hakuna aliekielewa tafsiri yake na nikaendelea kutumikia kazi na kifungo changu kwa staili ile ile.
Na hapo ndio nikazidi kuwa sipendi kuzungumza lakini kila mwezi nilipenda kuandika sehemu mbalimbali hadi kwenye miti maneno kuwa 'wanaake ni wauaji' ili hii iwe kumbukumbu na ujumbe mzuri kwa wanaume wengine wataokuja na kutoka jera hata kama nitakuwa nishakufa wakawasimulie wenzao kuwa kuna ujumbe uliachwa na mfungwa mmoja kuwa wanaake ni wauaji kwani niliamini kwa kufanya hivyo itatokea siku moja wanaume watatafuta maana ya huu usemi na watauelewa ukweli hivyo watajifunza jinsi ya kuishi na wanaake hadi shetani atapohama vichwani mwao na kutokea kizazi cha wanaake wema na walezi na maumivu yote yataisha.
Lakini kwa sasa bado naona na naamini wanaake ni wauaji Kamishna.
Mimi si chizi wala bubu kama wanavyosema ila kama watapuuzia haya na kuendelea kufuta maneno yangu kwenye kila kuta niliyochora basi wajue fika wanaume wengi watazidi kuumia na wanaake wachache wema watazidi kuteseka kwa kuponzwa na hawa wauaji ambao ndio wengi sana.
Na hiyo ndio hadithi yangu juu ya kisa kilichonifanya niwe hapa miaka yote na niwe hivi mwanangu. Nakushukuru kwa kuniita baba kwani sikuwahi kuitwa jina hilo wala kutegemea.. tena kutoka kwa mtu mkubwa kama wewe.. Mungu akubariki sana mwanangu pia naomba ujifunze sana usije pata matatizo kwa sababu ya wanaake kwani namkumbuka yule mlemavu alisema 'sio lazima hadi uje uwe kilema kama mimi bali yanaweza kukukuta kwa mtindo tofauti na ukajuta'
Ona mimi yamenikuta hivi... Je wewe ukizembea yatakukutaje ..? Kwa hiyo uwe makini mwanangu, sisemi kwamba uwachukie wanaake kama mimi la hasha!! kwa kuwa hayajakukuta unapaswa kuwapenda na kuwaonesha thamani kwa kukumbuka fadhila kuwa hawa ni mama zetu na tulikulia kwenye matumbo yao lakini usije kuwaamini sana na hii utie akili kichwani mwako ukae na ukumbuke kuwa WANAAKE NI WAUAJI.

______________
______

<*> *<>* *<>* <*>

______
______________

Naam, baada ya Hussein kumaliza kumuhadithia mkasa wake Kamishna Shaaban ilikuwa tayari ishatimu saa kumi alfajiri ndipo Kamishna alipomuomba Hussein asimame na kukumbatiana nae huku akimfariji kwa kumwambia kuwa jera haimaanishi sawa na kutokuwa duniani anachopaswa amshukuru mungu na amtumaini yeye kwani hajui kilichopo mbele yake na kama amemuandikia kutofia jela basi akae akijua hatofia jela.
Maneno ya Kamishna Shebby yalimfanya Hussein atoe machozi ya furaha kwa kutoamini faraja ile anayoipata tena kutoka kwa askali mkubwa ambayo hakuwahi kuiota wala kudhania huku nae Kamishna Shebby alijiapiza moyoni mwake na kueka naziri ya kumsaidia Hussein na kuutafuta ukweli wote uliojificha nyuma ya pazia juu ya matatizo ya Hussein huku zaidi akitaka kujua habari za Mr.X alikuwa nani hasa? pia je Zai yuko hai kweli? na kama yuko hai mwanamke aliyeuawa ni nani? na kwanini ba mkubwa alibatirisha ahadi yake na kumsariti Hussein dakika za mwisho?

* * * * *

Baada ya kupita miezi sita toka Kamishna Shaaban kujua kisa kizima cha mfungwa Hussein Babu bubu na sababu za kuandika kwake kwenye kuta na miti kuwa wanawake ni wauaji, ndipo Kamishna Shaaban au Shebby aliamua rasmi kujiingiza kwenye mission ya kuutafuta ukweli ambao hata Hussein mwenyewe hakuujua kwa lengo la kumtafutia msaada mfungwa wake yule kwani ndani ya moyo wake aliapa kufanya kadri awezavyo ili kumsaidia walau atoke tu jera Hussein asiendelee kutumikia kifungo ambacho hakimuhusu kabisa.

Hakujua kwanini moyo wake ulimsukuma sana kumsaidia mfungwa yule lakini bado alijiona wazi anapaswa kufanya hivyo kwa hali na mali.
Aliamua kupitia tena mafaili yote yaliyomuhusu Hussein huku akisikiliza rekodi ya hadithi ya Hussein mara kwa mara na kuingia mtandaoni kutafuta kwenye google habari za miaka zaidi ya ishirini iliyopita hususani kesi zilizowahi kutikisa nchi miaka hiyo.
Na kweli kutokana na teknolojia kukua sana vitu vingi vilikuwepo mtandaoni na hapo ndipo alipoziona habari mbalimbali zilizowahi kutikisa nchi miaka hiyo na kuanza kuitafuta habari iliyomuhusu Hussein babu bubu.
alisukuma mouse ya computa yake taratibu huku akishusha chini kuendelea kutafuta habari alichoihitaji ndipo alipoziona na kuvutika na habari mbili zilizotikisa za mauaji ambapo moja wapo ilikuwa na kichwa cha habari kilichoandikwa..

AMUUA MUMEWE NA KUMFUKIA KISIMANI KWA MIAKA SABA;

Kamishna Shaaban alijikuta anaguswa pia na habari hii japo sio aliyokuwa na kusudi nayo lakini aliamua kuifungua na kuisoma kwa ufupi ambapo ilisema kuwa,
' ' Mwanamke mmoja huko Bagamoyo inadaiwa alimuua mumewe kwa sumu na kumtumbukiza kwenye kisima kilichokuwa ndani ya uzio wa nyumba yao kisha asubuhi yake aliwaita mafundi wakakisakafia hiko kisima akidai eti alitumbukia mmbwa.
habari zilisema zaidi mama huyo alienda kutoa taarifa polisi wiki moja baadae akidai juu ya kupotea kwa mumewe ambapo polisi walifanya jitihada zote za kumtafuta na kutofanikiwa.
lakini miaka saba baadae mtoto wake pekee aliezaa na marehemu ambae alikuwa nje ya nchi kipindi tukio lilipotokea, aliporejea na kukuta habari zile alianza kufanya utafiti juu ya kupotea kwa babaake ndipo alipoingiwa na wasiwasi na mashaka juu ya kusakafiwa kisima kile mwaka huo aliopotea babaake na kuwaita polisi na mafundi kuomba kivunjwe kile kisima kuhakiki kama ni kweli alitumbukia mbwa au lah!! na hapo ndipo siri ilipovuja baada ya kuukuta mwili wa mtu ulioharibika vibaya na alipobanwa yule mama na maaskali ndipo alipokili kuwa yule alikuwa mumewe na alifanya vile kwa msukumo wa wivu na tamaa ya mali hasa baada ya kusikia mumewe alikuwa na mpango wa kuongeza mke wa pili hivyo aliona endapo angezaa na huko basi mwanae pekee aliyekuwa nje ya nchi kipindi hiko angepunjwa mali kwa kuwa asingekuwa mrithi pekee wa mali za marehemu.. ' '

kwa taarifa zaidi #ingia_hapa >>>

"Daaah!! kweli wanaake bwana mmh hawafikirii kabisa ktk maamuzi yao. sasa huyu mamaa dah!! ndio mana Hussein anawaita wauaji."
Alitikisa kichwa kamishna Shebby baada ya kusoma habari ile na kujikuta akijiongelesha mwenyewe moyoni.
Aliachana na habari ile na kuitazama habari ya pili ambayo iliandikwa...
INASIKITISHA MUME AUWA FAMILIA YAKE KWA KUWAKATAKATA KINYAMA KWA TAMAA YA KUWA TAJIRI;

Naam, alipoitazama habari hii ilikuwa imeandamana na picha iliyomuonesha Hussein enzi hizo akiwa chini ya ulinzi mkali na hapo ndipo alipoanza kuisoma mpaka mwisho ile habari na katika kuisoma kuna kipengele kilimvutia kilichomuhusu baba mkubwa wa mtuhumiwa alipokiri kuwa mwanae alihusika na suala hilo ambapo ndani ya habari ile pia aliyapata maelezo kwa urefu kidogo sambamba na jina maarufu la yule Baba mkubwa wa Mtuhumiwa na kuliandika pembeni kwenye notebook yake kisha alizima computa muda uleule na kutoka.
ITAENDELEA...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom