Sehemu ya 22.
Kuna wakati nilikuwa namwangalia shemeji huyu kisha navuta picha siku asikie kuwa mpangaji mwenzake, tena waliyeshibana, anakula mali zake itakuwaje?
Basi tuliendelea kula bia, nyama choma, kusoma magazeti na kupiga stori mbalimbali. Pia nilipata nafasi ya kumsoma vizuri shemeji yangu huyu.
Niligundua ni mwanaume mwenye akili nyingi sana. Hana pupa, hapendi kumsengenya, kumdharau mtu kwani wakati wote tukiwa pale sikumsikia akimsema mtu hata nisiyemfahamu.
Nilipofika bia ya tatu, siyo siri netiweki zilikata kabisa. Safari za chooni nazo zikaanza. Siunajua tena, pombe si chai.
Kuna wakati nilikuwa nakwenda chooni, nikirudi kabla ya kukaa nilijisikia haja ndogo tena, nikarudi.
Nilimokuwa nikipita sasa, salamu kibao, vimeseji sasa ndo usiseme. Wanaume wengine waliniangalia nikipita wakaishia kusonya. Na mimi ndiyo nikazidisha kujilegeza wakati wa kutembea. Na hivi nilivaa suruali ya kubana na umbo langu ni namba nane, yaani we acha tu.
Ukitaka kuamini kuwa baadhi ya wanaume ni wakware sana tena wana hatari, kuna wakati mhudumu mmoja alinijia nilipokaa na kuninong'oneza jambo.
"Kuna kaka pale anasema mpe namba yako, atakutafuta."
"Mwambie yeye ndo anipe ya kwake," na mimi nilimjibu kwa kumnong'oneza kama yeye alivyofanya.
Mhudumu alipoondoka, niliokaa nao wakaniuliza nini kinaendelea?
"Aaah, anasema eti kama ananifahamu," niliwadanganya lakini nikahisi wameishtukia picha, kwa vyovyote vile nao wanafahamu michezo kama ile kwenye mabaa.
Nilitamani kumwambia mhudumu asije tena kwani ndo bomu litalipuka, lakini hiyo nafasi ikawa haipatikani.
Nilipobanwa tena na mkojo, nilisimama kwenda chooni. Ile natoka tu chooni, yule mhudumu huyo.
"Namba yake hii hapa," alinipa kwenye kipande cha gazeti. Nilikipokea haraka na kukitia ndani ya kimkoba changu. Si unajua tena sisi wanawake, tukiendaga chooni, mkoba juu....ukiwa na tishu au toiletipepa kwa ajili ya mambo fulani.
Niliporudi nikaendelea kuagiza bia kadri ya hamu yangu.
Yule rafiki yake shemeji yeye alianza dalili za kuangusha gari. Naamini walianzia mbali.
Aibu zilinitoka nikaanza kummiminia bia shemeji. Nilihakikisha kila baada ya muda bia kwenye glasi yake ilipoanza kwisha nammiminia haraka sana...
Nini kitaendelea...