Xav Emmanuel
JF-Expert Member
- Jul 12, 2018
- 215
- 316
- Thread starter
- #21
SIMULIZI: “TOKOMEZO” (04)
MTUNZI: XAVERY EMMANUEL (Starxav)
Email: Xavemmanuel12@gmail.com
Whatsapp: 0769765748
Namba: 0672493994
Social Net: @star_xav
“Ndugu! Nitaeleza ayo yote hadi mpenzi wangu awepo hapa. Kwa maana miaka yote niliyokaa na msichana huyo sijawai mwambia sababu ya mimi kutafutwa kwa namna hii, kila siku nampiga chenga tu kwa maana ilifikia hatua hata kumwamini mtu ilikuwa ni sumu. Siri hii naijua mimi tu peke yangu, labda kwa uchache ni hao wanaonitafuta kwa sababu wanaogopa kutolewa kwa siri yao. Mwenyezi mungu wa rehma kesho mapema pindi afikapo mpenzi wangu basi nitaweka kila kitu hadharani...... aaaagh! Ndio samahani kwa hilo mama!” alimaliza kwa kumtaka mke wangu radhi..
SEHEMU YA NNE.
Hatukuwa na lingine zaidi ya kumwandalia sehemu ya kulala pamoja na chakula, kila mda sikusita kumpa pole kwa magumu aliyopitia, ingawa sikuyafahamu bado.
Kwa kweli ukimwangalia Abdul kwa sura ya karibu unapata kila aina ya majibu ya shida duniani, sura na umbo lake limebeba maswaibu yote ya ulimwengu kabla hujapata mkasa wake. Kwa kumwangalia tu utajua kuwa kweli Abdul ni mwamba na shupavu kwani mifupa yake imegangamaa kwa michosho na maangaiko ya dunia.
Alikuwa ni mrefu kiasi, urefu uliomtosha mwenyewe kujiingizia kipato, alikuwa ni mweusi ambae rangi yake alipatikana baada ya vita kati ya rangi nyeusi na maji ya kunde, nani awe mtawala rasmi wa mwili, na hatimaye weusi ulizidi shapavu kwa majikunde na kutawala mwili mzima, yaani alikuwa mweusi wa matatizo mwili mzima. Alikua mwembamba kwa kukosa lishe ya mwili kwa mda mrefu takribani milongo tisa na ushee. Hiyo tisa, kumi alikuwa ni kipofu, lakini uzuri wa hapa; kipofu chake kilikuwa ni cha macho tu lakini sio kuona. Kweli alikuwa hana uwezo wa kuona kabisa, lakini alikuwa na uwezo wa kufanya vitu vikubwa vinavyoonekena kumshinda hata alievalia miwani maarufu kama macho manne.
Kosa kumpeleka au kumwelekeza kitu kwa mara moja, mara ya pili anafanya mwenyewe. Hivyo hatukupata shida kumwelekeza mazingira ya chumba kilivo, sehemu ya maliwato na pembe nyingine za chumba. Kila kitu kilichofuata kuhusu chumba hicho alijua yeye jinsi ya kupanga na kuweka kwa ustadi asipate shida kukitafuta. Kilikuwa ni chumba kwaajili ya wageni.
Basi tuliagana baada ya chakula na kumtaka alale salama huku mimi na mke wangu tukiliendeleza valangati la kutatua mgogoro wa mawazo kuusu mgeni wetu mpya na wapi pa kuanzia kuhusu kumpata Rose ambaye ni mpenzi wa Abdul.
“Baba eh!! kama unavyojua bhana... ‘Abilia chunga mzigo wako’, unakoenda kesho, unaenda kumchukua Rose na kurudi, marafuku tamaa!” hicho kilikuwa ni kijembe cha mke wangu kilichotokana na wivu, mke wangu amabaye tulizoea kuishi kwa matani kila kinapokutana lakini jambo jema la kumshukuru Mungu ni kwamba hakuwai kunivunjia heshima hata siku moja, toka nimtoe kwao undendeuleni.
Tuliongea kidogo na mpango wa kuwahi kwenda kumchukua Rose kwani siku iliyofuata ilikuwa sio siku ya kazi; ni jumamosi. Na hatimaye tukalala kwani kila upande ulikuwa bize kuwaza historia kali ya maisha ya kijana ambaye yupo hatihani kutolewa roho kwa sababu ambazo hakuna anayejua zaidi ya msimuliaji mwenyewe, ambaye kwa wakati huo tayari neno Fofofofo Liliendelea katika chumba chake.
“Kokolikooooo!, kokokoko kokoli…” kama ilivyo majogoo ya kila siku, siku pendwa katika historia nyingine ya maisha ikaanza. Tukajuliana hali kila mmoja, na kwa mara ya kwanza jua la asubuhi liliniwezesha kuona kabisa uso wa Abduli ukiwa na tabasamu.
Baada ya kifungua kinywa nikaaga kwenda sehemu ambayo kila mtu aliifahamu, Abduli alinipa maelezo sehemu ambayo wanaishi kwa siri na mpenzi wake Rose, niliwasiliana na Rose kujua sehemu gani tunakutana, na kwa vile nilikuwa na namba yake ya simu haikunipa shida.
Nilianza safari kwa kuchukua daladala moja kwa moja hadi Bombambili stendi, sehemu ambayo tuliahidiana kukutana. Nilishuka stendi ya Bombambili na kuanza kutafuta namba ya mwanamke ambaye Abdul alimjaa kinywani, kila kichwao yeye ni Rose, Rose, Rose hadi kero! sijui ndio mzimu wake alaaah!. Niliendelea kuongea mwenyewe kimoyomoyo kwa muda kabla maada haijabadilika kichwani mwangu na kuanza kuwaza ni aina gani ya mwanamke ambaye bwana Abdul ametunikiwa, mke mjasiri ambaye amekubali kuishi na Kipofu kwa umaskini na matokomezo kadha wa kadha, hakika nilipata msisimko sana na kupongeza baadhi ya jitihada wafanyazo wanawake katika kupigania mapendo yao. Nilipofika nikafungua simu yangu kwa kutoa nenosiri, nikatafuta namba za Rose kupitia missed call na kuipiga.
“Hallo!, hallo,... eh wapi, wapi!!, ehh hallo!” bila maelewano simu hiyo ilikata, nikaipiga tena na nikajibiwa na muhudumu ambaye alikuwa zamu siku hiyo,
“Namba unayopiga haipatikani, Jaribu tena baadae”, nikakata na kupiga tena lakini mchezo ukawa vilevile, uso wangu ukaanza kuchukia na kuendelea kuangaza uku na uko kumtafuta mtu nisie mfahamu, niliangaza sana lakini sikufanikiwa kupata nilichokitaka, mshituko wa mayo ukanipata palepale nilipokuwepo mara baada ya macho yangu kuona mwanamke ambaye kwa mbali rangi yake ya maji ya kunde ilimulika mboni ya macho yangu.
Picha ya mke wangu ikafutika kichwani kwa kuanza kutoa sifa sisizostaiki kwa mwanamke ambaye sio mke wangu.
“Jamani Mungu fundi... Lo!” nikapaza ukuu wa mungu na nikajikuta namsogelea msichana huyo, kama tujuavyo wanaume sifa zetu pindi tumuonapo mwanamke ambaye maumbile yake ni mfano tosha wa kuamsha sehemu ambazo zimelala kwa mda. Alikuwa ni mchana mwenye rangi yake, sikumbuki kama kipodozi cha kemikali kishawahi pita katika uso wake; hakika anavutia. Alikuwa na nyele ndefu nyeusi ambazo alizifunga tu kwa kamba kichwani mwake upande wa juu, utadhani anazitumia kama ngata katika kubebea mizigo mizito. Nilimsogelea kuendelea kufahadi japo mapozi tu, alikuwa anakata kucha za mkono wake kwa kutumia meno huku mkono mwingine ukiangaika na simu ndogo kabisa ambaye ilikuwa haiendani na umbo lake. Nilipoganda kuendelea kumchora ghafla alinishtua na swali.
“Kaka naweza azima simu yako mara moja?” Swali hilo halikuwa na majibu kichwani kwangu, kwani aliendelea kunichanganya kabisa kwa kutumia sauti yake iyo ambayo kama wataalam wa utengenezaji wa simu wangeigundua basi wangeinyunyiza katika teknologia ya mlio wa kuitia katika moja ya kampuni zinazofanya poa duniani. Kweli niliongeleshwa ila nilibaki nimeduwaa kwa kukosa jibu, kwani hata kilichosemwa nilikikumbuka?, nikabaki kuishia tu aah!, Ah!... na kabla sijaangaika sana kijigonga gonga akarudia kile alichosema.
“Samahani lakini.... simu!, Naazima!” Hapo kilichozungumzwa kilikaa kichwani, haraka nikatoa simu yangu na kumpa mrembo yule, macho yangu bado hayakuchomoka usoni mwake.
“Kaka mimi siwezi tumia hizi! Naomba niandikie namba....” aliongea na kunizidishia mawazo. Inakuaje kwa kizazi hiki mtu mrembo na mwenye miaka yake duniani anashindwa tumia smartphone. Nikabaki nashangaa tu. ‘Jamani kwa lika kama ya huyu dada halafu anasema eti hawezi kutumia “Smartphone” Laulaaa!’, nilipigwa na butwaa la moyomoyo ambalo hakuna alieliona zaidi ya moyo wangu wenyewe.
“Mhhh namba!” nikajikwakwamua kutoa msaada.
“0757.. 9947....” kabla hajamalizia kuitaja namba hiyo, nikainua macho yangu na kumtazama kwa makini, nilikutana na uso wa tabasamu wa mrembo yule, kilichonishangaza ni kuwa namba hizo alizokuwa anazitoa kichwani. Yaani bila kuangalia sehemu yoyote ile jambo ambalo lilinishangaza sana. Sikumbuki kama alimalizia kutaja namba za mwisho au la, lakini tukabaki tu kuangaliana, huku mimi nilimshangaa yeye na yeye akishangaa mimi kwa mshangaa yeye.
“Unamtafuta nani?” Nikajikuta namtupia swali rahisi kwake.
“Abdul..... A....” likalirudia mara mbili lile jina la Abdul, hapo nikastuka katika dimbwi la mawazo na kuanza kumkazia tena macho mrembo yule. Nilikuwa kama sijaelewa alichozungumza kwa mara nyingine. Lakini alitaja bila kusita, tena mara mbili. Kitu ambacho kilinifanya niamini ni yeye Rose ni kuwa alipotaja namba alitaja namba zangu kabisa ambazo nilitumia kuwasiliana na yeye. Nikataka kupingana na macho yangu kama yule ndio kweli mwanamke ambaye ametekwa na kijana kama Abdul. Kwa kweli baada ya jina hilo, kilichofuata ni maswali na majibu tu ambayo nilikuwa najiuliza mwenyewe bila kupata nafasi ya kujijibu.
“We ni rose?” naaam, nikamtwanga swali ambalo lilimwacha kinywa wazi!, niliuliza kutaka kuhakikisha tu. Akainamisha kichwa chini kwa hofu ya kujibu. Alikuwa anaogopa.
“Okey mimi ni Xavery!, Xav... kama unamtafuta Abdul basi hapa ndipo sehemu sahihi na muafaka kabisa, nipo nae kwangu!”. Nikamwaminisha.
“Kaka samahani, nilikuwa naitaji huduma ya simu tu basi, kama hapatikani naomba mimi niende” akainua kichwa chake chenye aibu na kuongea, hakuchukua sekunde akaanza kugeuka tayari kuondoka.
“Rose ni mimi bhana, nimeagizwa na Abdul, nimepatwa na mshangao mara baada ya kusikia namba iliyotaja ni yangu. Mwishoni ni 87! Si ndiyo?, Abdul yupo salama na anakuitaji, na mguu huu ulikuwa kwako. Sikufahamu na nisingeweza kukufahamu kwa mapema namna hii, utambulisho pekee ambao nilikuwea nao mkononi mwangu ni namba yako tu ya simu. Nimepiga sana lakini hupatikanai” nilijitahidi kutokwa na maneno ya ukweli kwa mfurulizo kwa kumwaminisha binti yule, akageuka tu na kutoa chozi jembamba lililotililika hadi mashavuni mwake, lakini hakuharibu kitu katika kung’aza uzuri wake, alipendeza hadi wakati analia. Alinisogelea na kunitaka radhi.
“Kaka angu, ni vigumu kumwamini kila mtu kwa sasa, tunatafutwa sana, sio mimi wanaoniitaji, ni Abdul, kwa maana hata tukiwa wawili mimi na yeye, basi wataanza na yeye. Nampenda sana mume wangu jamani, naomba nikamwone” alitoa ombi la mwisho kwa kilio, nilimwonea huruma kwa kweli, nikawaza shida anazopata kwa kuishi na kipofu angali yeye ni malaika namna ile, vipi kelo za wanaume wanaomsumbua kumtaka kimapenzi?. Basi nikachukua nafasi ya kumbembeleza hadi kutulia.
Tukachukua usafiri wa pikipiki, niliwaza sana tunapandaje pikipiki moja na hali ya nyuma ilivyo nzuri ya binti yule. Rose alibeba kila kitu sehemu zake za nyuma, alikuwa mwemabamba wa kukonda kwa maisha tu ila mwili ulimkaa vizuri sana, mbinuko wake wa nyuma na shepu yake ya uchanga vilionekana.
Sasa nawezaje kupanda nae pikipiki moja? Nani atakaa mbele na nani nyuma? Mwanaume nikae mbele, hapana, nikae nyuma! Lo! Na ilo sebene ya matuta njiani ikuru yangu itaweza vumilia kweli ikigusana na mlima Rose? Na akiniona mke wangu huo ni ugomvi mwingine, nikatabasamu na kuchukua pikipiki mbili, kila mmoja aliapanda yake na kuanza kuingoza njia kuelekea nyumbani.
Hatukuchukua mda mrefu tayari tulishaingia mlangoni, sikuwa na mlinzi wala haouse girl nyumbani mwangu, nikafungua mlango mwenyewe na kuingizana ndani na Rose ambaye roho yake tayari ilianza kuweuka mara baada ya kuona amekaribia sehemu ambayo roho yake imefia mazima.
Ile kuingia tu.. tukakalibisha vilio vya furaha vilivyosindikizwa na machozi. Si kwa furaha ya Roze, vipi upande wa Abdul?, kwa mara ya kwanza nikaona nyuso ya tabasamu kwa Abdul huyu jamaa ukimwangalia kwa makini unaweza sema sio kipofu. Kwa maana hakuna anachokosea yaani kila kitu anafanya sahihi utadhani ana macho yote mawili!!!
ITAENDELEA...
Starxav