Xav Emmanuel
JF-Expert Member
- Jul 12, 2018
- 215
- 316
Safari ya Denis na Maria katika Maisha, walikunywa na kula mvua na jua kila kuchwao.... Riwaya ya Kiswahili "TOKOMEZO"
Starxav
Starxav
SIMULIZI: “TOKOMEZO” (01)
MTUNZI: XAVERY EMMANUEL (Starxav)
Email: Xavemmanuel12@gmail.com
Whatsapp: 0769765748
Namba: 0672493994
Social Net: @star_xav
SEHEMU YA KWANZA
Kelele za hapa na pale ziliendelea kusikika katika kila kona ya baa, hakukuwa na usikilizano kati ya sauti za binadamu na sauti za vifaa vya umeme vilivyoendelea kuburudisha mule ndani. Mwenye sauti nyembamba alisikika, nene ilisikika itaachaje sauti ya kukoroma sasa!. Hakukuwa na kiongozi yeyote mwenye kukeleekwa na kelele hizo, na hakuna aliyethubutu kuchukulia hatua suala hilo, kila mtu alikuwa huru na mambo yake. Mimi nilikaa karibu na mlango wa kuingia na kutoka nje ili iwe rahisi kutoka pindi nimalizapo kinywaji changu. Sikuwa mlevi wa kupindukia kuogopa kuchafua sare za kazi yangu. Nilipenda sana kazi yangu, kwani inahitaji mtu wa heshima, mtu ambaye hana chembe ya skendo. Nilikuwa maridadi kuangaza kila kona ya upande kuona kama kuna tukio nzito naweza kulipata ili kesho liangukie katika vichwa vya habari vya magazeti. Niliambulia tu kuona watu wakiingia na kutoka wengine wakishikana mashati na kuachana, wengine wakikumbatiana na kuachana, wengine walitokomea nisikokujua. Kweli baa ni baani...
Zilinichukua takribani dakika saba kusikia vishindo vya wababe wakiingia ndani ya baa hiyo, niliwapokea na kuwasindikiza kwa macho hadi walipokaa. Hakuna alieagiza kitu chochote kile kati yao, zaidi walikuwa wakilaumiana sana, huku mmoja aliyejaa misuli iliyoshiba akikunja sura na kurusha mikono huku na kule kama mtu aliyechoshwa na tabia mbaya za wenzake.
Wanasema “kiburi ni mwanzo wa kifo” hivyo nikaona vyema kuondoka sehemu ile kabla mambo hayajawa mambo: niliogopa kwa ujio wao. Taratibu nikachukua kinywaji changu na kukimiminia mdomoni, nilivyoshusha tayari kilikuwa kimeisha, nikaangaza kopo kwa sekunde kama mbili hivi kwa kukagua kama kweli nilikuwa nimemaliza. Macho yangu yalithibitisha mwisho wa kimiminika kile, mara baada ya kukutana na maandishi tu ya lebo ya kinywaji kile “Fanta”. Nikasoma na kuliacha kopo ilo taratibu na kutoka ndani ya baa ile.
Nikatoka nje taratibu na kuangaza kila kona ya baa hiyo. Mikono ilikuwa kiunoni na mdomo ukiwa unaendelea kufuta tamu ya mwisho ya soda niliyotoka kuburudika nayo. Macho yangu yakapambana na bango kubwa la baa hiyo lililopo mbele kabisa jilani na mlango wa kutokea; “La Charz Bar” nilijisomea kimoyomoyo huku nikiangaza kuitafuta njia ya kwenda nyumbani. Nilikuwa sina mwendo wa haraka sababu ya kuwa bado ilikuwa ni mapema.
Saa mbili kasoro! Aagh! Bado ni mapema mno. Daladala zipo chungu nzima. Basi niliendelea na mwendo wangu wa maringo kama kinyonga katika mti aupendae. Kichochoro nilichokuwa kilikuwa kimya kiasi na kupisha sauti za pikipiki na magali zikirindima mita chache katika eneo la barabara kuu. Nilisikia tu mihemo ya matairi ya magari hayo katika ngoma za masikio angali bado nipo vichochoroni kuitafuta njia kuu. Kagiza ambako kanaanza kushonana tayari kalianza kukaribisha ule usiku unaoitwa usiku wa manane. Nikazipiga hatua za haraka haraka kuhofu ukimya wa mtaa huo. Toka nilipo na baa ilipo, ni umbali mchache sana kutoka eneo kuu la barabara Napenda sana kuhudhuria baa hiyo kwani ndio baa kubwa na maharufu kwa sasa Songea Mjini, hakuna aina ya watu wanaokosekana sehemu hiyo. Kwa kazi yangu ya Mwanahabari ni pahari panapofaa kuchukua matukio ya siku, kwa maana ‘penye miti mingi hapakosi wajenzi’.
Wakati nafanya jitihada za kuchepukia katika barabara kuu, nilipokea onyo la mtetemeko wa kitu kama ndoo hivi likianguka!, “Alaah!!” nikagutuka mwenyewe na kusimama wima. Mlio niliousikia ni ule wa jaba ya takataka ambalo limeanguka. Woga wa mapema ukanikamata.
“Nani kaangusha?!!.., panya, paka..... anha panya.... No!!, mlio ni mkubwa, Mbwa!, Yes! Mbwa” nilianza kuhisi kwa kutaja kitu ambacho kinaweza kuwa na nguvu za kuangusha ndoo hilo lenye uchafu. Hayo yote yaliendelea kuongelewa moyoni. Nikatoa hatua moja kuelekea mbele lakini nilisikia tena vishindo. Kwa sasa vilikuwa ni vishondo vya binadamu ambao walikuwa kasi kupita maelezo. Na walikuwa nyuma yangu kutokea upande ambao ipo baa niliotoka. Nikahofu kukumbana na vibaka jioni hile takatifu, nikasogea pembeni kupata sehemu ya kujibanza. Nikajificha kuwaruhusu kwanza wao wapite.
“Deo! Umeona unavyozungua mwanangu?, Unazingua wewe, unazingua. Mi nakuambia ukweli. Wapi sasa?, wapi unadhani tunampata?” mmoja ya vijana wanne aliongea kwa uchungu kuwageukia wenzake, walipofika eneo ambalo nipo karibu nimejificha walisimama kwa mda kupisha malalamiko yachukue nafasi. Nilizikumbuka sura zile vizuri kwani ndizo nilizokutana nazo kule baa. Nikaendelea kujibanza sehemu wasije niunganisha bure katika harakati zao. Jambo jema kulikuwa na mwanga usiolidhisha eneo hilo.
“Sikia mzee!, hana pa kwenda, Yule chapu tu anpaap!. Yule!, Yule haoni! Sema kuna sehemu kajificha tu. Hapa hatuna namna tuvamie kila kona bosi hawezi elewa mzee!.” Mwingine ambaye alikuwa hana mwili wa kutisha aliongea. Ilionekana wanamtafuta mtu ambaye kwa makosa yao amewatoroka. Walipewa kazi ya kumshikilia.
“Daaah! tumefanya kosa sana kutokuwa karibu nae, kwa sasa akiingia mikoni mwangu mimi, hakuna cha bosi, namaliza mchezo, kwa bosi napeleka macho tu kama ushaidi, yaani... alaaaah. Shit!” mwingine ambaye yeye alionekana kupagawa kabisa aliongea. Huyu wa mwisho alikua na umbo la miraba minne ambalo alitosha kabisa kuingia katika masumbwi na kupigana kwa niaba ya taifa. Umbo lake ni kama huyu baunsa wa rahisi mmoja hivi nchi jirani hapa!. Nani huyu! Aagh! Ni maharufu sana yani sema basi tu jina lake limenitoka. Jamaa huyo ulikuwa na ghadhabu zilizomfanya kuvua hadi shati na kuegeza begani. Niliendelea kushudia malumbano yao huku wakijongea taratibu sehemu niliyopo.
“Tusitembee kizembe sasa, tuwe tunaangalie hata huku hukutani, kwa jinsi nilivyo na hasira mwanangu.... Me ntaekutana nae tu mda hu, naosha dadeki!.” Kauli, kauli mzee, chunga kauli yako. Kijana wa kwanza Aliongea kauli mbavu ambayo ilinigusa hasa. Kwani mimi ni mmoja kati watu ambao nipo maeneo hayo. Kwa vipi wangeniona?. Lakini nashukuru walipita salama. Walikagua eneo lililofuata baada ya nilipojificha mimi Walipita na kuenda zao nikawa nahakikisha tu kwa macho kama wamesongea mbali nami niokoze karoho kangu kepesi kuelekea makwangu............
ITENDELEA...
Starxav
Imepitaa mbili uckuSAA MBILI USIKU, INASHUKA SEHEMU YA PILI..
Starxav
naweka mkuu Hadi mwisho wa Mkuu wanguutaipeleka mpaka mwisho au unatuonjesha tu
HAKIKA ni Tokomezo
Hapo tupo pamojaHadi mwisho wa Mkuu wangu
Starxav
Mwandishi bado hujui matumizi sahihi ya L na R????![]()
eeMwandishi bado hujui matumizi sahihi ya L na R????![]()
Nipo kozi an kujifunza, zanitesa kweli yani KUNA WATU wanapitia maisha kama ya Abdul Mkuu... da
. uko vizuri,ila ujitaidi tu isiishie njianNDIO simulizi yangu ya kwanza naandika. kwa mapungufu niambieni tu niyafanyie kazi....
Natamani sana niifikishe mbali hii simulizi kwa maana imebeba Moyo na Roho za watu wengi wanaoteseka.
Tafadhali, naombeni ushilikiano wenu
Starxav
Itafika Mwisho