SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

kwakweli alete mapema kabla simba hawajafungwa kesho asije akatususa wiki nzima kufidia maumivu
Punguza sauti kidogo mkuu, maana apa tupo kuburudika na simulizi, hatuhitaji kelele za mashabiki wa timu za kariakoo zihamie hapa, kusoma kunahitaji sehem tulivu.
 
Na nguo za kufua pia hatuna yaan tupo tupo tu
Utumwa bado upo mkuu, kwenye bajeti yako elfu 60 itenge kando kila mwezi, hapo utakua na uhakika wa kumiliki mtumwa, hata hivyo sikuhizi umeme mwingi kuna zile mashine za kuchubua nguo nazo zinasaidia.
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA THEMANINI NA SITA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA TANO : akasimama ghafla mlangoni na kuwatazama kwa zamu watu wote waliokuwepo mule ndani, uso wake ukionekana kuwa makini sana mfano wa robot, kiasi cha kuwashangaza wote waliokuwepo mule ndani, yaani mjomba na shangazi yake, huku Higgno kiroho kikimdunda kweli kweli, ungesema amefumaniwa, kama wange mtazama vizuri ndiyo wange tambua kuwa amelewa, lakini sio mama Soraya wala Mahamud, ambae aligundua swala hilo.
Wakati Talib ameganda mlangoni katika hali ya kutazama kwa umakini watu waliopo mule ndani, ambae sasa alikuwa amemkazia macho Higgno ambae pia hakuacha kumtazama kama wengine walivyo fanya wakimshangaa yeye, Soraya akaingiza mkono kwenye mkoba wake na kutoa simu, haraka kisha akaipiga namba ile iliyoandikwa Talib mwarabu……………. ENDELEA……..
Hakuna aliekuwa anakiona kitendo kile zaidi wote walikuwa wana mtazama Talib, huku kila mmoja akiwa anawaza la kwake, wakati Higgno mwenyewe anawaza kuanza kufanyiwa fujo na Talib ambae anamfahamu vyema kuwa ni mkorofi na ukichukulia mara ya mwisho walimuona bar, hivyo niwazi atakuwa alikuwa anakunywa pombe, Layla yeye alikuwa anawaza kuwa Talib alikuwa anamtathini Higgno kwa uwepo wake pale nyumbani kwao, lakini kilicho mshangaza ni ule usimamaji wa kama robot, kama ambavyo baba na mama Soraya nao walishangazwa na usimamaji ule ulio ambatana na ushangaaji, pia walibaini utofauti wa macho ya kijana huyu ambae wameishi nae miaka mingi sana, leo alionekana wazi kuwa amelewa, licha ya yote walitegemea kuwa Talib angeongea lolote la kutoa ushidi wake wa uongo juu ya Higgno, ambae wao wamesha baini kuwa ni kijana mwema ambae kutoa msaada wa kiusalama ni kawaida yake, “yaani we Soraya na ujanja wako wote, ume… ume…umekuba” kabla Talib hajamaliza kuongea neno lake kwa sauti yake ya kilevi, ambayo iliwashangaza wakina Mahamud, ghafla simu yake ikaanza kuita, hapo akaitoa mfukoni na kuitazama kisha akageuka upande wa nje, huku anapokea simu, “hallow Zido…. hallow” aliita Talib huku anaelekea nje, huku wakina mzee Mahamud wakimsindikiza kwa macho mpaka alipotowekea nje, kisha waka mtazama Soraya aliekuwa anakata simu na kuiweka juu ya meza, “upuuzi huo, unabip bip tu!, ngoja sasa nikupigie” alisikika Talib akiongea kwa sauti ile ile ya kilevi, “umpigie, utajuwa nani mpuuzi” alisema Soraya akiwa ameishika ile simu mkononi, “kwani wewe ndie uliempigia?” aliuliza Mama Soraya kwa mshangao, Soraya akaitikia kwa kichwa kukubali kuwa yeye ndie aliempigia, “sasa mbona kama ameita Zido, halafu anaonekana amelewa sana” aliuliza mama Soraya kwa sauti ya chini, akichelea kusikiwa na Talib mwenyewe, na kabla hata Soraya hajajibu kitu, simu yake ikaanza kuita, bahati nzuri ilikuwa katika ukimya, (silent) hivyo aliitazama tu na kuachana nayo, “mtajuwa kesho, ngoja kwanza pombe imtoke” alisema Soraya, huku anaiweka simu kwenye mkoba wake, hapo mama Soraya na baba Soraya wakamtazamana kwa sekunde kadhaa, kisha mama Soraya akamtazama Soraya, “ila sio siri Talib amelewa” alisema mama Soraya kama vile anataka uthibitisho toka kwa Soraya, “ila mi wala sijui akilewa anakuwaje” alisema Soraya na hapo wazazi wake pamoja na wakina Higgno na Laylah wakacheka kwa namna ambavyo Soraya alikataa, mfano wa mtu asietaka ushahidi, na hapo ni kama Mahamud alikumbuka jambo akamtazama Higgno, “Higgno unafahamiana na Talib sio” aliuliza Mahamud, kwa sauti tulivu iliyotegemea jibu analolifahamu, “ndiyo namfahamu, nilisomanae Luhuwiko, mimi nilikuwa kidato cha kwanza wakati yeye anamaliza kidato cha nne” alijibu Higgno kwa sauti ya upole na tulivu, “ok!” alisema mzee Mahamud, kama vile alitaka kuuliza mengi lakini akaamua kuishia hapo, “mh! Hebu kwanza nikaongee na Talib” alisema mama Soraya, huku anainuka toka kwenye kochi, mahamud akamdaka mkono, “hautoweza kuongea nae usiku huu, bora ungesubiri kesho, sijui kwanini amerudia tabia ya ulevi wakati alikuwa anaendelea vizuri tu!” alisema Mahamud, “kwani aliwahi kuacha tabia zake za ajabu?” aliuliza Soraya ikiwa ni njia ya kuongea ukweli, “Soraya, si vyema kumsingizia mtu mambo mengi, kwa hili moja ambalo tumeliona leo” alisema Mahamud kwa sauti ya ukali kidogo yenye kuonya, “baba Soraya, ni kweli anachosema Soraya, kama huyu mtu amebadilika basi ni kuwa msafi peke yake” alisema mama Soraya na kumfanya Mahamud amtazame yeye, “ina maana Talib hakuacha kuvuta bangi na kunywa pombe?” aliuliza Mahamud kwa sauti ya chini akichelea kuwa Talib atasikia, “kwa upande wa pombe ndiyo namuona leo, ila jana kwa macho yangu nimemuona anavuta bangi ndani mwake” alisema mama Soraya na kumfanya Mahamud azidi kushangaa,
Naam waliongea mawili matatu kabla Mahamud hajawasisitiza kuondoka mapema pale nyumbani, “jamani hebu fanyeni haraka muwahi kuondoka maana, inabidi mumpeleke Higgno kwake, halafu ndio murudi kwa kina Laylah, tena ninge washauri mutumie gari mmoja ili kesho Laylah akimleta Soraya ndipo aende kwa kina Higgno kuwa fundisha gari wakina mzee Frank, na wakati unarudi uje nao pamoja na Higgno” alisema mzee Mahamud, lakini Soraya akatoa wazo lake, “hapana baba, mimi nikisharudi nitachukuwa gari na kumfuata Higgno, kwasababu nataka tupite madukani” hakuna aliepinga, nao wakaagana na watatu hawa wakatoka na kuingia kwenye gari la Soraya na kutoka nje ya geti, huku wakimpita mzee Ndolite pale getini, hawakumueleza chochote, wao wakaondoka na kutokomea zao upande wa soko kuu kwenda kuikamata barabara kuu iendayo mikoani, na wakati wanakatiza soko kuu ndipo walipo liona gari dogo jeupe, aina ya collola likiwa limesimama pembeni ya barabara sambamba na pikipi mbili ambazo pembeni yake walikuwa wamesimama watu saba, akiwemo Idd na wakina Vitus.
Land rover discovery lilienda mpaka njia panda ya NPF na kuingia kulia likielekea Hospital ya mkoa, na lilipo ufikia uzio wa hospital hiyo ya mkoa likakata tena kulia na kufuata njia iendayo OK hotel, mpaka mtini pub na lilipoikamata barabara ya nyuma ya mtini pub, hawakufika mbali Higgno akatoa ushauri wa kusimamisha gari pembeni ya maduka yaliyopo pembezoni mwa barabara, karibu kabisa na kona ya kuelekea kwa kina Soraya, wakibakiza mita kama mia mbili tu! toka kwa kina Soraya, yaani kwenye geti lao, kiasi kwamba hata gari liliposimama wao waliweza kuona vizuri kabisa geti la Kina Soraya.******
Wakati huo huo, nyumbani kwa kina Soraya mara baada ya watoto wao kuondoka tu, wao wakaingia chumbani kwao wakiwaacha wafanyakazi wao wakihakikisha milango kama imefungwa na kuzima taa za ndani, muda ulikuwa unaelekea saa tano kamili, “nina wasiwasi Soraya anaenda kulala kwa Higgno” alisema Mahamud, akiwa anajiandaa kulala, “hilo nadhani sio la kuuliza, kwasababu wanapendana sana, na kama unavyomuona Soraya toka ameanza kwenda huko amekuwa na furaha ya juu sana” alisema mama Soraya ambae ndie wa kwanza kupanda kitandani akiwa amevua nguo zote akibakia na ile ndogo ya ndani pekee, “mapenzi kitu cha ajabu sana, Soraya hakupenda kabisa kukaribiana na vijana lakini sasa hataki kumkosa huyu kijana” alisema Mahamud, nae sasa alikuwa anapanda kitandani akiwa na boxer pekee, maana alijuwa kazi inayofuata kila pale mke wake anapolala akiwa na vazi hilo moja, “cha msingi tuharakishe ndoa, japo hili swala la dini nalo linaleta kizungu zungu” alisema mama Soraya, na hapo Mahamud akakumbuka simu ya mwenyewekiti, “tena umenikumbusha, unajuwa mwenyekiti sijui amejuwaje hizi habari, yaani kabla hata sija waza kuhusu dini tayari yeye amesha nieleza, wakati sijamuambia lolote” alisema Mahamud huku anachukuwa simu yale kwenye meza ndogo na kuanza kutafuta namba ya mwenyekiti, “he! makubwa ina maana ile simu uliyokuwa unaongea nayo ilikuwa ni ya mambo hayo?” aliuliza mama Soraya kwa mshangao, “hata mimi mwenyewe nimeshangaa, eti anasema hujaona vijana wote wakiislam mpaka umuoze binti yako kwa kafiri” alisema Mahamud, huku anabonyeza namba ya mwenyekiti ambayo ikaanza kuita, “hivi mbona wana muandama sana Soraya, utasema ni mschana pekee hapa Songea jamani…” alisema mama Soraya huku mume wake akimkatiza kwa kumuonyesha ishara akae kimya, kisha yeye akaanza kuongea na simu ile, akianza kutanguliza samahani kwa kutokupokea simu yake wakati ule, maana alikuwa katika shuguri wakati huo.
Ni maongezi yalifanyika kwa dakika kadhaa, japo sio nyingi sana, ila walifanikiwa kuongea vizuri tu, huku mwenyekiti akimueleza Mahamud kuwa siku inafuata yaani kesho wakutane baada ya swala ya adhuhuri, walihitaji kuongea nao juu ya swala lile la kumuozesha binti yake kijana ambae sio muislam.*******
Baada ya kuona amepigiwa simu na Zido, ambae alikuwa ameachana nae muda mfupi ulipita pale Mtini pub akiwa na wakina Vitus Idd na vijana wanne, wakiwa wamekubaliana kuwa Talib aende nyumbani kwao akatazame hali ipoje, kisha awajulishe wenzake waje wapige fedha, lakini alipoipokea simu ile nayo ikakatika akajuwa kuwa Zido alikuwa anambip, hivyo akapiga yeye, ambapo simu iliita bila kupokelewa, “itakuwa imejipiga tu mbona hapokei” alisema Talib huku anaeleka kwenye nyumba yake akafungua mlango na kuingia ndani, ambako kama ilivyo kawaida yake, alisokota bangi na kuanza kuvuta huku akitafakari kitendo cha kumuona Higgno akiwa amekaa meza moja na Soraya wanapata chakula cha jioni, “huyu mshenzi analeta dharau, yaani mimi nimempora yule Malaya mchafu kuoga, yeye anakuja kumchukuwa binamu yangu, atakiona cha moto” alisema Talib kwa sauti ya kilevi, huku anaendelea kuvuta bangi yake, leo hakujisumbua hata kuwasha udi kama kawaida yake, “yaani nikisha kamata mkwanja wangu tu, nanunua lita arobaini za petrol kisha naenda kutia moto nyumba yao na duka lao, ili tuone sasa nani mjanja” aliwaza Talib, ambae hakuwa anatania, “tena nasubiri wamelala na nunua kufuri nawafungia kwa nje ndio nawatia kiberiti” hakika ilikuwa ni mipango ya kishetani kweli kweli toka kwa Talib, akipania kuuwa na kuiteketeza familia ya kina Higgno pasipo kuwa na kosa lolote.
Naam baada ya kukaa kwa dakika kama ishirini hivi, akiwa amekaa juu ya kochi, Talib akianza kusinzia, ndipo aliposikia simu yake ikiita tena na alipotazama ilikuwa ni kutoka kwa Vitus, akaipokea haraka “niambie vitus” alisema Talib huku akisogea dirishani upande ambao unatazamana na nyumba kubwa, “naona gari la Soraya linapita hapa” aliongea Vitus wakati Talib anafunua panzia na kuchungulia nje akitazama “atakuwa anaenda kwa basha wake huyo, ila naona wamesha zima taa, nyie kaeni kama lisaa limoja hivi halafu muje, watakuwa wameshalala” alisema Talib, huku anarudi kwenye kochi na kujilaza tena.********
Naam saa sita na nusu baadae mji ulikuwa tulivu kabisa, wakina Soraya wakiwa bado wapo ndani ya gari wakiongea hili na lile ikiwa ni utani na vicheko vya hapa na pale, huku maongezi yao kwa kiasi kikubwa yakiegemea kwenye maisha ya ndoa na harusi yao itakavyo kuwa, na sasa walikuwa wanakaribia kukata tamaa, huku hata Soraya alikuwa ameshaanza kusinzia, “jamani muda unaenda mi naona sio kama tunavyo fikiria, bora tuwahi tukalale” alisema Soraya kwa sauti ya kivivu na yakudeka, huku anaegemea bega la Higgno aliekaanae seat ya kati, “inawezekana eeh, pengine walishatuona wakatustukia kuwa tuna wafuatilia” alisema Laylah akiunga mkono, “lakini mkae mukijuwa kuwa kama wanataka kufanya lolote hawatokuja mapema kama munavyofikiria, kama vipi ngoja mimi niende nikajaribu kuwatazama, kama watakuwa wamesha ondoka basi na sisi tuondoke, ila kama wapo basi lazima tusubiri hapa hapa, hata kama mpaka asubuhi itabidi mulale ndani ya gari” alisema Higgno huku anafungua mlango na kushuka toka kwenye gari, lakini kabla hata hajafunga mlango, Laylah akasema, “kweli jamani waleeee wanakuja” hapo Higgno na Soraya wakatazama mbele na wote kwa pamoja wakaweza kuwaona vijana wanne waliovalia makoti meusi wakisogea kwa tahadhari kubwa kwenye geti la nyumba ya kina Soraya, Kwa wale ambao simulizi nyingine zimewapita kuna huu uzi usikupite... Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui ITAENDELEA
 
Yaani tumewachambua wahusika wote,

Tumechambua dhamira kama zifuatazo:
1. Wivu na chuki ni chanzo mitafaruku
2. Nafasi ya mwanamke kwenye jamii(chombo cha starehe) hapo wahusika ni Hilda, Mama Hilda, sina mengi

3. Tamaa ya pesa (Idd & Twalibu)
4. Uaminifu(Higgyno)
5. Ushirikina (mzee komba na familia yake Vs mzee Mabula?
6. Ulevi- hapa wale wazee lakini nammaindi sana mzee Njogopa
7. Umasikini (familia ya Mzee komba)
8. Dini (kwa namna gani dini inaweza kutumika kuficha au kutekeleza maovu){iddy na baba yake}
 
Kifungua macho kimetengwa mezani saa 10:14 am,
cha ajabu baada ya shibe mumekimbia hata vyombo hamujaosha! mumekaa uko munavizia muje kudai lunch na dinner, yaani sikuhizi naona muna tabia za ki_talib talib nyie watu.
 
Back
Top Bottom