SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA SABINI NA MBILI
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA SABINI NA MOJA: “anapenda udi kama vile anafuga majini” aliwaza mama Soraya na hapo akakumbuka jambo, “nilimuona kwa macho yangu anavuta bangi ndani kwake huku amewasha udi” yalikuwa maneno ya Soraya yaliyo jirudia kichwani mwake na kupunguza mwendo ghafla kisha akaubadili kabisa mwendo wake na kuanza kutembea kwa tahadhari akiufuata ukuta wa nyumba hiyo wa upande wa kulia na kwenda kujibanza pembeni ya kidogo ya dirisha la nyumba hiyo, kisha akachungulia ndani ya nyumba ile kwa tahadhari kubwa, naam alicho kiona humo ndani kilimfanya aache mdomo wazi………. ENDELEA……..
Maana alimuona mpwa wake mtoto wa pekee wa kaka yake, ambae alimchukuwa kijijini kwaajili ya kumsomesha nae aje kuwa na maisha mazuri amsaidie baba yake ambae kiukweli ni mlevi wa kupindukia ambae kwa sasa yupo huko ziwani nyasa, kazi yake ikiwa ni kuvua samaki na kuelekea kwenye vilabu vya pombe kutumia kile alichokipata kwenye mauzo ya samaki pasipo kubakisha chochote, yaani Talib akiwa amejituliza kwenye kochi ndani ya sebule ya nyumba hii ndogo, huku ameshikilia sigara iliyosokotwa kienyeji mkononi mwake, hata ushikaji wa sigara ile haukuwa wa kawaida, maana alibana kwa ncha za vidole viwili yaani gumba na kile chakati, na kila alipoipeleka mdomoni alimuona akivuta kwa nguvu sana moshi wa sigara ile na kuubana kwa ndani kama vile hakutaka utoke.
Mama Soraya au shangazi yake Talib alivutiwa na vijiti kadhaa vya udi vilivyo wekwa kwenye kikombe klilicho kuwepo mezani, udi ambao ulikuwa unawaka na kutoa moshi taratibu uliosambaa kama ilivyokuwa kwenye sigara bwege ya Talib, “ina mana Soraya hakusema uongo” alijisema mama Soraya huku anajitoa pale dirishani akihisi miguu yake inakosa nguvu, lakini alijitahidi kujikongoja kuelekea ndani ambako hakuweza kuongea lolote mbele ya mume wake, “ina maana Taribu hakuacha kuvuta bangi, maana hii tabia ya kuchoma udi hajaanza leo” alijiwazia mama Soraya, ambae alikuwa amesimama katikati ya chumba chao kikubwa, “vipi Talib amesha ondoka?” aliuliza Mahamud ambae alikuwa amekaa kwenye meza yake ndogo ya chumbani kwake anahesabu fedha alizokuja nazo jioni ile na kuziweka katika mafungu, maana hakuwa ameziweka vizuri, swali hili lilikuwa ni jepesi sana kwa mama Soraya, lakini jibu lake lilikuwa gumu maana kumueleza ukweli ingekuwa ni ghafla sana, kwasababu kila mmoja aliamini kuwa Talib alisha achana na bangi, “mama Soraya vipi mbona kimya nakuuliza Talib amesha ondoka?” aliuliza Mahamud, akimgeukia kabisa mke wake, hapo mama Soraya akajicheksha kidogo, “ha! naona amepitiwa na usingizi, maana nimegonga wee haitiki, lakini taa zinawaka” alijibu mama Soraya, ambae hakukaa sana mule chumbani, baada yake aligeuka na kutaka kutoka nje ya chumba, “sasa fanya kitu kimoja, waambie wafanyakazi wa jiandae kesho kwaajili ya kupika chakula kizuri kwaaajili ya ugeni, maana tunapaswa kuwaandalia chakula kizur na mapokezi ya kueleweka, kwasababu licha ya shuku zetu kwa Higgno lakini pia tukumbuke anaweza kuja kuwa mkwe wetu” alisema Mahamud, na mke wake akaunga mkono na kutoka nje kueleka jikoni, huku anaendelea kuwaza juu ya mpwa wake, “halafu huyu Talib ameanza lini tabia ya kurudi usiku, maana juzi alirudi saa saba” mama Soraya alikumbuka maneno ya mume wake, huku mama Soraya akiendelea kujikumbusha mambo mengi yanayo muhusu Talib, ikiwa na lile la kutoweka nyumbani kwa siku tatu bila kuaga, na kuonekana asubuhi ya usiku aliorudi Mahamud toka dar es salaam.
Unajuwa kuna jambo ambalo lilikuwa linamchanganya mama Soraya, sio lile la uvutaji wa bangi pekee, ila pia kilicho mstua na kumtisha mama Soraya ni jambo moja tu! “hivi kama ameweza kuvuta bangi kwa muda wote huu, pasipo sisi kujuwa, sasa anafanya mangapi kwa siri?” alijuliza mama Soraya ambae alielekea moja kwa moja jikoni kutoa maagizo kama mume wake alivyoagiza.********
Akiwa njiani ndani ya gari Soraya alimsimulia kilichotokea nyumbani kwao kati yake na wazazi wake, na mashaka ya wazazi wake juu ya Higgno, na kuwa mzee Frank ni baba wa Higgno, “kweli huo mtihani Soraya, unajuwa kama Higgno atajuwa hilo atajisikia vibaya sana, si unamuona mtu mwenywe masikini hakuwa hata na tamaa ya kuwa ya nawewe wala kitu chochote toka kwako, halafu Talib amejuwaje kama yule mzee ni baba wa Higgno?” aliuliza Laylah, kwa sauti ya shaka, “Higgno na Talib wanafahamiana vizuri tu, na ndie alie mnyang’anya mwanamke wake kipindi wakiwa form one, na ndio chanzo cha Higgno kutokuwa na mwanamke mwingine mpaka alipokuwa na mimi” alijibu Soraya huku safari ikiendelea, “mh! hapo na wasi wasi, si unakumbuka yule mzee alisema kuwa aliechoma duka lake ni kijana aliemfuata nyumbani kwake na akasema kuwa ana ugomvi na kijana wake?” alikumbusha Laylah, “mh! ni kweli Laylah, na kijana wake mwenyewe ni Higgno, unajuwa swala hilo, linazidi kufanya Talib aonekane mkweli” alijibu Soraya kwa sauti iliyoanza kupooza, lakini Soraya akashangaa kumuona Laylah ana tabasamu, “wala usiwe na wasi wasi Soraya, mualiko wa Higgno na wazazi wake nyumbani kwenu ndio nafasi pekee ya wewe kuwa thibitishia wazazi wako kuwa Higgno hajuwi kama wewe ni mtoto wa Mahamud, na hivyo hakuwa na mpango wowote wa kukuteka kama wanavyo sema” alisema Laylah, kwa sauti yenye uhakika, “kivipi Laylah, hebu nieleweshe” alisema Soraya kwa shahuku na kutegasikio kumsikiliza Laylah, “kwanza kabisa, inabidi umualike mzee Frank, ambae anajuwa kuhusu wewe ni nani, na ni mtoto wa nani, ila umueleze kuwa aje na familia yake yaani mke wake na kijana wake, halafu wewe ujifanye hujuwi mbele ya Higgno, ili akikuona lazima atashtuka, kitu ambacho kitawashangaza hata wazazi wako” alishauri Laylah, na hapo ndipo Soraya alipoachia tabasamu la ushindi, “hapo umeongea point, wacha nimpigie simu mzee Frank” alisema Soraya huku ana chukuwa simu yake na kupiga kwa mzee Frank, huku wakiwa wanakaribia shule ya msingi chemchem, mita mia moja toka mwanzo wa msitu wa Matogoro, simu haikuita sana ikapokelewa.******
Naam akiwa amesha maliza kuvuta bangi yake Talib akatulia ndani ya chumba chake mpaka aliposikia adhana ya inshaa, kisha akatulia kama dakika kumi na tano halafu akatoka mule chumbani kuelekea sebuleni, ambako alipatia malengo yake, maana alikuta wafanyakazi wa jikoni wanamaliza kuandaa chakula mezani, naye akaenda mezani na kukaa mezani kisha akaanza kujisevia chakula na kukikung’uta, bila kukumbuka utaratibu wao kwamba kama Mahamud mwenyewe yupo pale nyumbani ingepaswa mtu yoyote kusubiri kwanza yeye ajulishwe na kufika pale mezani ndipo wangeanza kula.
Na wakati anaendelea kujipakulia chakula kwenye sahani zake mara akatokea mfanyakazi wa jikoni, “kaka Talib mbona unaanza kula wakati baba bado hajafika?” aliuliza yule mfanyakazi, kwa sauti ya chini iliyojaa simango pasipo kujuwa kuwa mzee Mahamud na mke wake wanakuja pale Sebuleni wakitokea chumbani, “haaa! mi na njaa bwana, sina muda wakusubiri….” alisema Talib huku anaanza kula, lakini akashtuliwa na sauti ya shangazi yake, “adabu gani hiyo Talib, njaa yako inatuhusu nini sisi, kuna aliekuambia mchana ukazurule?” aliuliza shangazi yake Talib kwa sauti ya ukali, hapo Talib akageuka kutazama ilikotokea sauti akamuona shangazi yale akiwa mbele ya mjomba wake aliekumbatia mabulungutu kadhaa ya fedha, Talib akakodoa macho kwenye fedha zile huku koo likimkauka kama mwenye kiu ya maji, “hakuna tatizo mama Soraya muache ale maana njaa haiwezi kusubiri, huoni mpaka nimalize kuwekafedha niandike kumbu kumbu” alisema Mahamud huku anaelekea upande ofisi yake ilipo huku amebeba fedha zake, “lakini baba Soraya huu ni muda wa kula kwanini uanze tena kufanya kazi za ofisi, acha kwanza tutafanya baadae, “ alisema mama Soraya huku anamfuata mume wake kule upande wa ofisini huku Talib anawasindika kwa macho, sio kwamba alikuwa anawashangaa wawili hawa ambao anawafahamu vyema, ni kwamba alikuwa anatazama kwa uchu zile fedha, “mbona kesho mtausoma mchezo” aliwaza Talib, huku anageukia sahani yake na kuendelea kula, wakati huo mfanya kazi wa jikoni alikuwa anaondoka kuelekea jikon, “na kesho inabidi niwe mjanja niibe funguo moja kisha niwapelekee wakina Zido, halafu nitulie hapa nyumbani kimya kabisa, ili wakivamia wasishuku hata kidogo” aliwaza Talib, ambae hakujuwa kama kesho kutakuwa na ugeni pale nyumbani.
Naam baada ya kutulia kwa dakika kama mbili hivi akihakikisha kuwa shangazi na mjomba wake wameshaingia ofisini na yeye akainuka na kuufuata mlango wa upande wa nyuma na kwa tahadhari kubwa sana akachomoa funguo moja kati ya mbili zilizo kuwa zina ning’inia pale kwenye kitasa cha mlango, kisha akarudi haraka mezani na kuendelea kula.*******
Mzee Frank, alipokea simu akiwa amesimama nje ya jengo jipya la duka lake, jengo ambalo ni kama lilikuwa limesha malizika kwa asilimia tisini na tisa, likiwa limebakiza kukauka sakafu na lip za ukutani ili waweke flame nakupanga bidhaa ili duka lifunguliwe, na ndipo alipopokea simu toka kwa Soraya, akaipokea mara moja na kuiweka sikioni, “hallow mwanangu habari za jioni” alisalimia mzee Frank, na wakati huo mke wake alikuwa anakuja pale aliposimama yeye, lakini alikaa kimya kumpisia mume wake aongee na simu, japo hakusikia upande wa pili unaongea nini, “ndiyo nina kijana wangu……ndiyo anaitwa Higgno…… hapana hakai hapa nyumbani yeye aliamua kwenda kukaa mashambani huko mahilo, mara tu baada ya kumaliza chuo cha ufundi….. hakuna tatizo naweza kuja nae…. hakuna tatizo hawezi kukataa, tena leo mmepishana kidogo sana kule mjini…. hakuna shida mwanangu nadhani huu ndio mwanzo wa undugu, japo tupo tofauti sana… asante sana, jioni njema” alisema mzee Frank na kukata simu, kisha akamtazama mke wake aliekuwa amesimama anamtazama, huku akifuatilia maongezi ya simu ya mume wake, “naona mualiko huo, ni yule mschana?” aliuliza kwa shauku mama Higgno, “unaulizia mualiko vipi kuhusu nguo nzuri, inabidi upendeze haswa, maana tunaenda kwa tajiri Mahamud kula nao chakula cha mchana” alisema Frank akiingiza na utani, “we subiri uone nitavyo valia mpaka wewe mwenyewe utanisahau” alisema mama Higgno kwa majigambo ya utani, “halafu amesema twende na Higgno, pengine ni nafasi zaidi ya Higgno kuwa karibu na Mahamud, halafu isitoshe leo alikutana nae na alimuomba amuowe binti yake nanidhani binti mwenyewe ndio huyu, maana sidhani kama Mahamud ana binti mwingine” alisema Frank, na hapo mke wake akashtuka kidogo, “lakini unakumbuka kuwa huyu binti anamshenga na mchumba mwenyewe yupo huku huku Luhila” alisema mama Higgno, akimkumbusha mume wake kwa sauti ya tahadhari, “Higgno alishakataa ombi la mzee huyo, kwasababu anamchumba wake mwingine, pia navyojuwa mimi kama Higgno angekubali kumuoa mtoto wa Mahmud ambae ni huyu binti, basi ingeleta majungu makubwa, ingeonekana ameingilia mahusiano ya watu” alisema Frank, huku wakielekea ndani kuandaa nguo za kesho kwenye mualiko, huku mzee Frank akibofya simu yake kupiga kwa Higgno na kweli simu ikaanza kuita.******
Mama Soraya licha ya kushindwa kumueleza mume wake juu ya kile alichokiona ndani kwa Talib, lakini ukweli alijikuta akishikwa na hasira juu ya Talib, maana ameona kitendo cha wazi kilicho endelea kubainisha uvutaji wake wa bangi, alishindwa kuheshimu utaraibu ambao yeye aliuweka kwa heshima ya mume wake, kwamba akiwa nyumbani yeye ndie atakae anzisha kula, labda itokee aseme kuwa atachelewa kula au atokula kabisa.
Hata walipotoka kule ofisini baada ya kumaliza kuweka fedha na kurecord kwenye kitabu, walikuta tayari Talib amesha maliza kula na wao walipoingia tu nae akanawa na kutoka zake sebuleni huku akiwa na funguo mfukoni, “hooo! Talib hebu subiri kidogo, hebu niambie kuhusu huyo kijana na baba yake” alisema Mahamud ambae alikuwa anakaa kwenye kiti cha meza ya chakula pamoja na mke wake, “nilisha muambia shangazi, tatizo Soraya amekurupuka sana, yule dogo mi namfahamu vizuri sana, nilimuacha shule Luhuwiko, tena alikuwa anapenda sana kuongozana na Hilda” alisema Talib kwa kujiachia huku anarudi kwenye kiti na kukaa, “Hilda ndio nani” aliuliza Mama Soraya, ambae alikuwa anamtazama Talib kwa umakini na mashaka, maana alishaanza kumuona ni mvuta bangi, “yule mschana ambae alisemaga ana mimba yangu, kama muna mkumbuka” alisema Talib, ambae ni kama alikuwa amepewa nafasi nzuri na yapekee, ya kummaliza Higgno, ambae hakupenda kabisa apate nafasi ya kuwa na binamu yake kimapenzi, “wewe ndiyo ukaja kumzidi kete” aliuliza mama Soraya, kwa namna fulani ya kutopendezwa na Talib, “nimzidi kete wapi, atakuwa na mtu wake yeye alikuwa mpambe tu, na sasa hivi ni maadui kweli kweli” alisema Talib kwa kujiachia vibaya sana, “ok! kwahiyo unasema kuwa huyo kijana ndie aliepanga mipango ya kumteka Soraya na kuomba hela na baadae kujifanya ana muokoa?” aliuliza Mahamud ambae sasa alikuwa anajipakulia chakula na kuweka kwenye sahani zake, “ndiyo, ndie aliefanya hivyo kwasababu amnase Soraya, hata yule baba yake ni muhuni kweli kweli tena tapeli, usikute aliwatapeli watu ndio wakamchomea duka lake” alisema Talib akionekana anajuwa mambo mengi sana kuhusu Higgno na baba yake, “kwahiyo tunaweza kupata ushahidi wa kumkamata huyo Higgno?” hapo Talib akatulia kidogo, kwasababu alijuwa fika kuwa alicho kiongea ni uongo na kwamba asingeweza kuupata ushahidi wowote wa kuwa Higgno ndie aliefanya mpango wa kumteka Soraya, “ushahidi kama upi labda Anko?” aluliza Talib na hapo shangazi yake akadakia, “si ushahidi wa hicho ulichosema?” ukweli shangazi alionekana kama kuto kumuamini tena Talib, japo alikuwa anashindwa kumueleza wazi wazi.
Hapo Talib akaganda kidogo, akionekana kukosa cha kuongea, “sikia Talib, ni kwamba nahitaji uchunguze taratibu, uwapate hao watu aliowatuma kumteka Soraya, kisha tuwapeleke Polisi wakatoe ushahidi, pia uchunguze anakokaa huyo kijana ili tukihitaji kumkamata tusihangaike” alisema Mjomba na hapo ikawa kama amempooza kidogo Talib, “ilo tu Anko, mbona simple, tena siku sio nyingi nakuletea jibu” alisema Talib akiwa hajuwi pa kuanzia, lakini alikuwa na uhakika kuwa atatengeneza ushahidi wowote wa uongo na kumkamatisha Higno.
Naam baada ya maongezi hayo, Talib aliondoka na kueleka ndani kwake, “hoooo! halafu tumesahau kumueleza Talib kuhusu ugeni wa kesho” alisema Mahamud, baada ya kuwa tayari Talib amesha toka nje, hawakujuwa kama alishachomoa funguo kwenye mlango, “haina haja ya kumueleza kile tunacho kijuwa kuhusu hao watu” alisema mama Soraya, “ni kweli mke wangu unajuwa licha ya yote inatupasa kukubali kuwa yule kijana ni msaada mkubwa kwa Soraya, sidhani kama alipomuokoa kwa mara ya kwanza, alikuwa na nia ya kumlaghai” alisema Mahamud.*********
Naam Laylah aliondoka mara moja baada tu ya kumshusha boss wake, ambae alianza kuchangamka mara tu baada ya kufika pale nyumbani kwa Higgno, “hoo karibu, yaani leo nimekuandalia chakula kizuri“ alisma Higgno, huku anaandaa kigoda kwaajili ya Soraya, “sito kula mpaka unitajie mshenga wako” alisema Soraya kwa sauti ya utani, lakini wenye ukweli ndani yake, “hoooo! nikikutajia hauto amini” alisema Higgno kwa kujisifu, “mh! amekuwa nani huyo mpaka nisiamini” alisema Soraya akionyesha tabasamu la furaha, huku anaptiliza ndani kuweka begi lake, kisha akatoka na kukaa kwenye kigoda, “haya niambie sasa, mshenga atakuwa nani na atakuja lini? Hakutaka kumueleza kuhusu shuku la wazazi wake, “ni yule mzee mwarabu Mahamud, nimekutana nae leo nimeongea nae sana, akasema atakuwa mshenga wangu, kuhusu kuja kwenu kuleta barua amesema nije nikuulize wewe ni moto wa nani…” alisema Higgno ambae alikatizwa na sauti ya mshtuko..... Musilale Kuna Bonus Inakuja... ITAENDELEA
 
Labda muungane team Twalib na team Idd pengine mnaweza kuambulia chochote

Tatizo team Twalib mnafikiri Higgno ni yule mliyempiga akaangukia mtaloni na baiskeli yake
 
Shukrani sanaa mkuu,
 
Tunasubiri bonas
 
Siku ya kichapo kwa Talib inazidi kukaribia, waache wazidi kujaa kwenye mfumo.
Waache wajae kwenye mfumo

Tayari akina Higgno wamepewa mwaliko, lakini kumbuka Soraya ana mpango wa kuchukua ile simu

Talib amepewa kazi ya kumfuatilia Higgno akiwa hajui kesho Higno anakuja hapo kwao, na mzee Frank atamuona kijana aliyemtisha na anayemuhisi kuwa amemchomea duka
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA SABINI NA TATU
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA SABINI NA MBILI: “sito kula mpaka unitajie mshenga wako” alisema Soraya kwa sauti ya utani, lakini wenye ukweli ndani yake, “hoooo! nikikutajia hauto amini” alisema Higgno kwa kujisifu, “mh! amekuwa nani huyo mpaka nisiamini” alisema Soraya akionyesha tabasamu la furaha, huku anaptiliza ndani kuweka begi lake, kisha akatoka na kukaa kwenye kigoda, “haya niambie sasa, mshenga atakuwa nani na atakuja lini? Hakutaka kumueleza kuhusu shuku la wazazi wake, “ni yule mzee mwarabu Mahamud, nimekutana nae leo nimeongea nae sana, akasema atakuwa mshenga wangu, kuhusu kuja kwenu kuleta barua amesema nije nikuulize wewe ni moto wa nani…” alisema Higgno ambae alikatizwa na sauti ya mshtuko...….. ENDELEA NAYO……..
Na mshangao toka kwa Soraya, “unasema!!! nani atakuwa mshenga wako?” aliuliza Soraya kwa mshangao na pasipo kuamini alicho kisikia, sio kwamba alishangaa kuwa Higgno ana fahamiana na Mahamud ambae ni baba yake, ukweli Soraya alikuwa anafahamu fika kuwa Higgno, anafahamiana na baba yake, tena baba yake alikuwa anamuamini na kumkubali sana mchumba wake huyu, ila kitendo alichosema Higgno na kumsimulia Soraya jinsi ilivyokuwa mpaka wakakutana na maongezi yao yote hata lile ombi la kumchumbia binti yake na vitu ambavyo angemfanyia endapo angekubali kufanya hivyo, “nikamuambia kuwa tayari nina mchumba” alisema Higgno wakiwa wamekaa nje ya kibanda chake, Soraya akatabasamu kidogo, “mh! kwanini ulikataa mali zote?” aliuliza Soraya, ambae sasa ni kama alikuwa anamtega Higgno na kutafuta majibu sahihi ya kuwaeleza wazazi wake, “Soraya sijawahi kumpenda mtu nisiemjuwa, halafu utajiri sio chanzo cha mimi kupenda” alisema Higgno, kwa kujiamini, “Higgno, unamfahamu huyo mtoto mwenyewe wa Mahamud?” aliuliza Soraya ambae swali la hili jibu alikuwa nalo na alikuwa anahitaji uthibitisho wa moja kwa moja toka kwa Higgno, “mimi simjuwi, ila nadhani anafahamiana na wazazi wangu, kwasababu baba ameniambia kuwa anamsaidia kufufua duka lake lililoungua mtoto” alisema Higgno pasipo kujuwa anachoongea ni marudio kwa Soraya, “kwanini hukuniambia kuwa duka la baba yako limeungua moto?” aliuliza Soraya, akijifanya kuhuzunika, ungesema ndio kwanza anaisikia taarifa hiyo, “mh! samahani Soraya, lakini niliona kama ni mapema sana kukueleza kuhusu matizo ya huko nyumbani, ila hakuna tatizo mambo yanaenda vizuri, na huyo mschana mwema anamsaidia baba kurudisha duka lake” alisema Higgno kwa sauti ya upole, “ilikuwaje mpaka duka likachomwa moto au kuna watu amegombana nao” aliuliza Soraya ambae tayari alisha dokezwa sababu, ni kama alikuwa anampima Higgno, “baba anasema kuwa kuna jamaa alikuja pale dukani akaagiza sigara, lakini hakulipa baada yake akaniulizia, na baba alipomjibu kuwa siku hizi sipo pale nyumbani akasema kuwa ananitafuta kwasababu nime ingilia na kuharibu mipango yake, lazima atafanya kitu kunikomesha kama alivyonifanyia miaka iliyopita, usiku wa juzi ndio duka lika chomwa moto, baba anahisi ni huyo huyo” alieleza Higgno kwa sauti ya upole, “kwani wewe una ugomvi na nani, au uliingilia mipango ya nani na ni mipango gani?” aliuliza Soraya huku anasogeza kigoda chake karibu na alipokaa Higgno kisha akaegemeza mikono yake kwenye mapaja ya Higgno, ambae sasa alimtazama usoni, “kwa kweli mimi sikumbuki kuingilia mpango wowote, pengine ni ule wa kukusaidia wewe usitekwe, na kwa upande mwingine mtu ambae aliwahi kunipiga miaka mingi iliyopita ni Talib yule mtoto wa Mahamud, nadhani nilisha kusimulia kilichotokea kati yetu” alisema Higgno, ambae alikuwa ni kama anasisimkwa kwa kitendo cha Soraya kukaa mkao ule kwenye mapaja yake.
Kusikia hivyo Soraya akatulia kidogo kama anawaza jambo fulani, kisha akauliza, “kwanini usimuambie mzee Mahamud kama Talib alikufanyia fujo nyumbani kwenu” aliuliza Soraya akimaanisha siku ile alipokuja na Hilda kumuona mtoto wake, “Soraya siwezi kufanya hivyo, kwanza nasikia Talib sio mtoto wa Mahamud, tumezoea tu kumuita hivyo, sasa nikisema hivyo si nitaonekana nina mgombanisha na mjomba wake?” alisema Higgno, na hapo Soraya akatabasamu kidogo, “Higgno jamani unawezaje kuthamini maisha ya mtu mwingine kuliko ya kwako, yaani mtu ambae pengine ndie ana hatarisha maisha yako wewe unawaza kuhusu, maisha yake?” aliuliza Soraya kwa mshangao, na mastaajabu “huwa sipendi kutengeneza maadui, hasa ambao chanzo cha ugomvi sijui” alisema Higgno kwa sauti ya upole iliyojaa busara.
Mpaka hapo ni kama Soraya alikuwa ameshaanza kuhisi kuwa Talib anahusika na uchomaji wa duka la baba yake Higgno, sasa akaanza kutafuta njia sahihi ya kuthibitisha kuwa Higgno siyo mtu mbaya kama wazazi wake wanavyo hisi, “kwahiyo baba yako akimuona huyo Talib anaweza kumkumbuka?” aliuliza Soraya akiwa bado ameegemeza mikono yake kwenye mapaja ya Higgno, “sijajuwa labda nikamuulize, ila tuyaache hayo ngoja niandae chakula tule ni saa tatu kasoro sasa” alisema Higgno huku anajiinua pale alipokaa na kufanya Soraya atoke mapajani mwake, na wakati huo simu ya Higgno ikaanza kuita, “atakuwa baba huyo” alisema Higgno na kuitoa simu mfukoni, “mbona unajiami kwani hakuna mwingine wakukupiga hebu nione” alisema Soraya huku anakwapua simu toka mkononi kwa Higgno, lakini Higgno hakuonyesha wasi wasi wowote, “hoo kweli ni baba yako, halafu nime kumbuka nipe kwanza ile simu ya wale walioniteka” alisema Soraya huku anampatia Higgno simu yake ambayo aliinunua yeye mwenyewe, ni mara baada ya kuona aliempigia ni baba yake na sio mtu mwingine.*******
Yap Baada ya Talib kuingia ndani ya kijumba chake kizuri kidogo, akawasha udi na kuwasha bangi yake, kisha akaanza kuivuta taratibu, “sasa mambo yanaanza kukaa poa” aliwaza Tarib huku anatoa funguo na kuitazama, “yaani nikiukamata ule mkwanja, sijui itakuwaje?” alijisema Talib, huku anarudisha funguo mfukoni na kutoa simu nakufungua upande wa messeji, kisha akaanza kutafuta namba fulani aliyowahi kuitumia sms.
Talib alifanya hivyo kwa sekunde kadhaa mpaka alipo pata namba ya Zido, “yaani kesho ndio mwisho wa umasikini” alijisemea Talib, huku anaandika ujumbe kwenda kwa Zido, “funguo nimeshaupata nawaletea kesho mapema, jitahidini musifanye makosa kama kule shamba” kisha akaituma kwenye namba hiyo ya zido, alipo maliza akaiona sms nyingine aliyowahi kuituma kwa Zido, hapo akajisonya kidogo maana sio kwamba sms hii ilimuuzi, hapana sms hii aliyomtumiaga Zido siku ile ya jumapili iliyosema kuwa, “mjomba anataka kuwaambia polisi, hebu mtishieni” ni sms iliyomkumbusha “khaaa! hii simu si ameipoteza” alijisemea Talib huku ana anza kuandika tena ujumbe na wakati huo huo ikaja stutas report ikionyesha kuwa messeji deriverd, lakini hakujali, sijui ni kutokana na mibangi aliyo kuwa anaivuta au vipi, aliandika ujumbe mwingine na kuutuma kwa Vitus, nayo ikarudisha taarifa kuwa imepokelewa na jibu likaja baada ya dakika mbili, “poa hakikisha mambo yamekaa fresh” lilikuwa jibu la Vitus.*******
“hallow baba” alisikika Higgno mara baada ya kupokea simu huku anaelekea ndani, Soraya aliweza kufuatilia mazungumzo ya Higgno na baba yake, “kweli baba…… kwani anajuwa kama una mtoto mkubwa kama mimi….. hooo! lakini hajui kama mimi na fahamiana na baba yake sio?........ sawa …….. itakuwa saa ngapi?” alisikika Higgno akiuliza huku anatoka nje ya kibanda na simu nyingine mkononi, “sawa lakini nitamuambia na mchumba wangu afahamu asije akanifikiria vibaya” alisema Higgno, huku anampatia Soraya ile simu ya mkononi mwake Soraya, nae akaipokea huku anamtazama usoni kwa macho ya tabasamu la kumsuta, kwamba anamtaja mbele ya baba yake, “ndiyo nilimemsimulia….. si unajuwa na yeye lazima ajuwe kuhusu mshenga wetu” alisema Higgno kisha akakata simu na kumtazama Soraya ambae bado alikuwa anamtazama kwa macho ya tabasamu, “kwahiyo ulisha muambia baba yako kuwa mimi ni mchumba wako?” aliuliza Soraya huku anacheka kwa furaha, “mhhh!!!.... ndiyo ……. ndiyo nilimuambia, kwani wewe bado hujawaambia wazazi wako?” aliuliza Higgno huku anasogeza ndoo yake anayoifanya kama kiti akionyesha kuwa alikuwa anamkwepa Soraya, “ho! bado sijawaambia, inabidi mpaka mukija kuleta barua ya posa” alisema Soraya huku anavuta ndoo kuirudisha pale pale ilipokuwa, yaani karibu yake, “hooo! nimesahau kuchukuwa chakula……” alisema Higgno huku anandoka kurudi ndani, akimuacha Soraya anamtazama kwa macho ya kumcheka, maana Higgno alionyesha wazi bado hajiamini anapokuwa mbele yake, “kweli huyu ajawahi kuwa na mwanamke” aliwaza Soraya huku anatabasamu, na wakati huo huo akaona ujumbe unaingia kwenye ile simu aliyopewa na Higgno, akatazama jina la mtumaji wa ujumbe liliandikwa Talib mwarabu, “mh!” Soraya aliguna mwenyewe kwa mshtuko, huku anafungua ile sms ambako alikuta sms nyingi zimeongozana, yeye akafungua ile ya mwisho, “funguo nimeshaupata nawaletea kesho mapema, jitahidini musifanye makosa kama kule shamba” ndivyo ulivyo someka ujumbe ule uliotoka kwa Talib mwarabu, “mama yangu, Talib !!!!!” alijiuliza Soraya kwa sauti ya chini iliyojaa mshangao.
Naam wakati Higgno anaendelea kuandaa chakula, yaani anaingia na kutoka ndani, Soraya alikuwa kimya akifungua sms ya pili iliyotumwa na Talib Mwarabu kwa mmiliki wa simu ile ambayo yeye Soraya alimuona nayo mmoja kati ya watu sita waliomteka, “mjomba anataka kuwaambia polisi, hebu mtishieni” ndivyo ilivyosomeka sms ya pili, ukweli Soraya akazidi kushangazwa na jambo lile, hapo Soraya akaona bora aanze kusoma sms za mwanzo na ile kuifungua moja alijikuta anahisi kuzimia, maana hakuamini alicho kiona na kukisoma, kwamba kilikuwa ni kwaajili yake, endelea kufuatilia mkasa huu wa TEMBELE LA UWANI hapa hapa jamii forums
 
Hapa naona tayali tushachomoa funguo. Kilichobaki ni kwenda daslam kununua gari, kucheza na watoto wazuri na kuja kufungua bar
 
Back
Top Bottom