TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA KUMI NA TANO
MTUNZI
Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA NNE: Naam kabla Higgno hajajibu , mara akasikia sauti za watu wakisogelea ule mlango wa kibanda chake, zikiwa ni saut za wanaume watu wazima, “ukweli nakuambia bwana Frank, safari hii siwezi kukubali, tukimkuta binti yangu humu namuacha hapa hapa” ilikuwa ni sauti ya mzee Komba, huku sauti nyingine ikidakia, “yaani ndio atakuwa mke wake, si atakuwa anampenda yeye mwenyewe, kwanini atake kumzalisha tena mtoto wa watu bila ndoa” hiyo ilikuwa ni sauti ya mzee Nyoni, hapo Higgno akamtazama Hilda aliekuwepo pale kitandani, akimtazama kwa macho ya tabasamu….. ENDELEA
Tabasamu ambalo Higgno aliliona kama limejaa tafsiri ya usaliti mkubwa, na kabla hata hajasema lolote, Higgno akasikia sauti ya baba yake toka nje, “mwenyekiti, samahani kwanza kabla ya yote kuna jambo nahitaji kupata ufafanuzi, umekijuaje chumba cha Higgno?’ aliuza baba Higgno kwa sauti ya mashaka, “bwana Frank, mimi nimeitwa kuwakilisha upande wa serikali, kuhusu wamekijuaje chumba hilo mimi silijui, labda tumuulize mzee Komba” alisema huyo mwenyekiti, hapo kikapita kimya kifupi kabla mzee Nyoni hajapayuka, “sidhani kama swala la amejuaje lina umuhimu, cha msingi ni kujua kama Hilda yupo humu ndani au laa” ndivyo alivyo jibu mzee Nyoni, ambae alionekana kuwa alikuwa amelewa pombe aina ya ulanzi, “ni kweli, kwani hajui kama watu walichunguza mpaka kulijua hili” alisema Njogopa, na hapo mwenyeiti akasikika akibisha hodi, “Higgno fungua mlango, mimi ni mwenyekiti” hapo Higgno akamtazama tena Hilda pale kitandani na kumuona ndio kwanza analegeza kanga yake pale kifuani, hakika ungemuona usinge weza kukataa kuwa walikuwa wametoka kufanya jambo fulani.
Basi kiunyonge sana, Higgno akaenda kufungua mlango kundi la wazee likazama ndani, “si unaona mwenyekiti, nilikuambia, ukweli sikubali binti yangu aendelee kuzalia nyumbani” alisema mzee Komba kwa sauti ya juu iliyojaa lawama na malalamiko, huku wenzake wakisaidia kutoa maneno ya lawama,
Higgno alimtazama baba yake, ambae alimtazama kwa macho ya mshangao, “Higgno umeanza lini hii tabia?” aliuliza mzee Frank, ambae alishangazwa na swala la kukutwa Hilda mule ndani, “hayo hayatuhusu bwana, sisi tunacho taka, Higgno akabidhiwe mke, sisi tuondoke zetu” alisema mzee Ngonyani na Njogopa akadakia “sio mke pekee akabidhie na mtoto pia”.
Mzee Frank akashusha pumzi nzito, kisha akamtazama mwenye kiti, “sina ujanja mwenyekiti, ifanyike kama wanavyo taka wao” alisema Frank, kauli iliyomuumiza sana Higgno, ambae alishindwa kuelewa kwanini Hilda alifanya vile, maana hata alipokabidhiwa mke na mwenyekiti wakiandikishiana kwenye karatasi na watu kuondoka zao, huku baba yake Higgno akimueleza mwanae kuwa wataongea kesho, yeye apumzike na mke wake, ukweli Higgno hakutaka hata kupanda kitandani, alibakia amekaa kwenyestuli yake huku akijiinamia chini na kuwaza kwanini Hilda amemfanyia hivi, “Higgy kwanini sasa unakuwa hivyo kwani wewe si ulisema unanipenda jamani?” aliuliza Hilda kwa sauti ya kubembeleza, sauti ambayo Higgno alihisi kama vile inatoka kwa jinni, “au ulikuwa unanidanganya ulivyoniambia nikiachana na Talib nije kwako?” aliuliza Hilda huku akijiinua toka kitandani na kumsogelea Higgno pale kwenye stuli, huku akiiachia kanga ikimtoka kifuani na kuachia baadhi ya maungo yake yakionekana wazi wazi, ikiwa pamoja na maziwa yake ambayo kiukweli si vyema kufananisha na vazi la miguuni(ndara) lakini ndio Uhalisia, “Hilda zaidi ya hapo unakumbuka uliyonifanyia?” aliuliza Higgno kwa Hasira, ambazo alikuwa anajitahidi kuzidhibiti, “lakini Higgy ule ulikuwa utoto” alisema Hilda akijifanya kubembeleza, “ulikuwa na utoto gani, mtoto anayafanya uliyo yafanya, mtoto anabeba mimba, mtoto anavuta mabangi na kunywa pombe, mtoto anakuja kujifanya kunitembelea kumbe anakuja kuniletea matatizo?” aliuliza Higgno maswali mfululizo, ambayo jibu lilikuwa moja tu, “jamani basi nisamehe, subiri nipone na wewe nitakupa” alisema Hilda kwa sauti ile ile ya kubembeleza, “kwani nani amekuambia mi nataka, yani nimekusaidia leo hii asubuhi, usiku wake una nifanyia hivi, nimekukosea nini Hilda?” aliuliza kwa machungu Higgno, ambae sauti yake ilikuwa inakaribia kuangua kilio kwa uchungu aliokuwa nao, “kama hutaki sawa, lakini mimi ndio mkeo na nisikuone na mwanamke mwingine, ukigoma naenda kwa mwenye kiti” alisema Hilda, na hapo Higgno akapandwa na hasira kali sana, japo aliona kuwa maneno yale yana ukweli ndani yake, “na kwa taarifa yako kuanzia kesho nataka nguo mpya, mbona wewe unavaa vizuri” alisema Hilda na sasa Higgno aliona akimuachia ni sawa na kulea kidonda, hivyo akimzibua ngumi kadhaa atakuwa amemtia adabu, lakini kabla hajachukua maamuzi hayo, mara wote wawili wakasikia mlango wa chumba kile unagongwa, Hilda alishtuka sana akihisi moja kwa moja kuwa mtu anaegonga mlango alikuwa amewasikia kila kitu, maana alihisi kuwa mtu huyu alikuwa mlangoni anasikiliza wanachoongea, Higgno akainuka na kuufuata mlango, akaufungua kidogo na kuchungulia nje, hakumuona mtu, akatoka nje kabisa akamuona baba yake anamuita kwa ishara kuwa amfuate.******
Kumbe basi, baada ya kutawanyika muda ule, mzee Frank ambae alikuwa anawaza sana juu ya tukio lile ambalo alikuwa anahisi kuwa ni tukio la kutengeneza, hakuamini kuwa mwanae Higgno alikuwa ameanzisha mahusiano na mschana Hilda binti ambae, habari zake hazikuwa nzuri hata kidogo, hivyo akaamua kurudi kimya kimya kwenda kusikiliza maongezi ya mwanae Higgno na mschana Hilda, hivyo basi mzee Frank, alirudi taratibu na kusimama nje ya chumba cha mwanae Higgno, na ndipo alipoyasikia maongezi ya mwanae Higgno na mkwewe mpya kabisa, na kugundua kuwa mwanae hakuwa katika mahusiano na mschana huyu ambae amejitaja kuwa ni mgonjwa.******
Higno alifunga mlango na kumfuata baba yake, ambae alitembea mbali na pale kwenye mlango wa chumba cha Higno, “Higgno kwanini ulirudisha ukaribu na huyu binti?” aliuliza mzee Frank kwa sauti ya chini iliyoonyesha masikitiko makubwa sana kwa mwanae mara baada ya kusimama ubavuni kabisa mwanyumba kubwa, “baba sijui nisemeje, ila kwa kifupi mzee Komba na mtoto wake wameamua kuniharibia maisha yangu” alisema Higgno kwa sauti ya upole iliyojaa masikitiko, “wameamuwa kukuharibia kivipi, wakati wewe mwenyewe ndio umejisogeza kwa yule binti ambae amekuwa wa hovyo kabisa, wanawake wote hawa mpaka unaamua kumsogelea mschana huyu?” aliuliza baba Higno, japo ilikuwa ni ya chini lakini ilionyesha wazi mzee huyu amechukia, “baba kwanza naomba unisamehe kwa kukuletea aibu kama hii, ila ukweli ni kwamba, Hilda na baba yake waeamua kunikomoa” alisema Higgno na kuanza kusimulia ilivyo kuwa.
“Hapo wametupata, lakini nikuambie kitu mwanangu” alisema mzee Frank, mara baada ya Higgno kumaliza kusimulia jinsi ilivyokuwa mpaka Hilda akaja pale nyumbani kwao, “ili litaisha, na muda sio mrefu huyu mschana atakuwa mbali na wewe, ila cha msingi usije ukashiriki tendo na mschana huyu, kwasababu nilimsikia aliposema kuwa hawezi kufanya lolote mpaka apone, hivyo niwazi kuwa anaumwa gonjwa la zinaa, mimi nitaenda kukutana na mwenyekiti nimueleze ukweli juu ya hili, hata likitokea jambo lingine siku za mbele asishangae” alifafanua baba Higgno.
Naam huo ndio ulikuwa mwanzo wa maisha mapya ya Higgno, akiishi na Hilda na mtoto wa Hilda aliezaa na Talib, huku Higgno akiwahudumia kwa chakula na mavazi, na kumfanya Hilda azidi kunawili na kupendeza, kitu ambacho wengi walikuwa hawakijui ni kwamba wawili hawa walikuwa wanaishi kwa ugomvi mkubwa, Higgno akikubari kuwaachia Hilda na mwanae walale kitandani huku yeye akilala chini, siku zote Hilda mchana kutwa angeshinda nyumbani kwa wazazi wake, angetumia fedha aliyoachiwa na Higgno kununua mboga nzuri na kupika kule kwa mama yake na kula pamoja nao, wakati mwingine angewapatia fedha kwaajili ya ulanzi au angekunywa nao na kurudi nyumbani kwa Higgno saa mbili au tatu za usiku.
Mzee Komba na mke wake walifurahi sana kuona mtoto wao akianza kupendeza na kuonekana ni mmoja kati ya wanawake wenye kupendeza pale mtaani, sasa hata ile tabia yake ya kutoa kitumbia kwa aajili ya kupata shilingi mia mbili aliiacha kabisa, Kwasababu hakuwa na sababu ya kufanya hivyo, maana kila kitu alikuwa anakipata kwa Higgno, japo vijana wengi wa pale mtaani walimlaumu na kumdharau Higgno kwa kukubali kurudiana na Hilda, mschana ambae alishapitia kwenye maovu mengi.
wazazi wa Higgno hawakuwahi kuongea neno lolote kwa wazazi wa Hilda, na hawakuwa na maelewano mazuri kutokana na jambo walilolifanya kwa kijana wao, japo walijitahidi kuongea vyema na Hilda na kumchukulia kama vile mkwe wao.*****
Mwaka 2004, ni mwaka toka siku ile ambayo bwana Mahamud alivamiwe na wezi na kusaidiwa na kijana Mpole ambae kwa bahati mbaya hakuwahi kulijua jina lake, japo alikubali lile ombi la kuwa akimaliza chuo angeomba kujiunga kwenye kampuni yake ya usafirishaji kama fundi wa magari.
Ni mwaka mmoja toka Talib na wenzake, washindwe kupora fedha kwa mzee Mahamud, na talib kuendelea kujifanya mtu mwema ndani ya nyumba ya Mahamud, yaani mjomba wake, ambae aliyakubali mabadiriko ya kijana huyu na kumueleza mke wake kuwa, wanahitaji kumpatia mtaji wa biashara kijana Talib, ili aanze kuandaa maisha yake, nao wakakubaliana kumpatia fedha kiasi cha shilingi za kitanzania, million mbili, nae akaanza biashara ya kununua na kuuza samaki na dagaa toka ziwa nyasa, ambazo aliuliza kwa bei ya jumla mjini songea, ni biashara mbayo ilianza vizuri sana kwa upande wa kijana Talib, huku akitumia lile gari dogo aina ya Hyundai, kijana Talib alizidi kuonekana maridadi, Waschana walianza kumpapatikia na yeye hakuwaacha salama, alipita nao kama wote, starehe za pombe na bangi hakuweza kuacha, aliendelea na kuzidisha mara dufu, japo alijitahidi kuficha ukweli huo mbele ya mjomba wake shangazi na wanafamilia wengine kama Soraya na wafanyakazi, japo kwa mlinzi hakuwahi kumficha na ndie aliekuwa mshirika wake mkubwa, maana kuna wakati alilazimika kuingiza waschana kwa kupitia pale langoni.
Tabia hiyo ilifanya biashara ya kijana huyu ianze kushuka taratibu, kwa maana ya kupoteza mtaji mwingi kwenye starehe na anasa, akajikuta ana anza kuingia kwenye madeni, hali ilikuwa ngumu, alihitaji fedha nyingi ya kufanyia starehe zake, kutokana na matumizi mabaya ya fedha na tamaa akajikuta anaitamani nafasi aliyokuwa nayo soraya, kiasi cha kumchukia na kumuona kuwa ndie kauzibe, anae sababisha yeye asipate nafasi nzuri kwa mjomba wake.
Ni mwaka pia toka Soraya alipogunduwa kuwa binamu yake bado anavuta bangi, tofauti na watu wanavyo muona, japo yeye aliamua kukaa kimya, Soraya pia licha ya kuzidi kukuwa na kupendeza, akisumbuliwa na wanaume kila kukicha, lakini bado hakuwa na mwanaume wala mchumba, alisema bado hakumuona mwanaume wa kuendana nae, pangine alidanganyika na filamu za kihindi, “ni miezi miwili toka Soraya amalize chuo na baba yake kumpatia kazi ya kusimamaia baadhi ya miradi, ambayo aliiandaa kwa aajili ya binti yake huyu, ambae hakuwa tayari kuona anaajiriwa na mtu au kampuni yoyote, mmoja kati ya mirad ambayo Soraya alipewa kuisimamia ilikuwa ni miradi ya mashamba huko mahiro, kando kando ya milima ya matogoro ambako mwenye Soraya alikuwa anapenda kutembelea huko kila mwishoni mwa week, hasa siku ya ijumaa anapokuwa ametoka msikitini, mara nyingi aliongozana na dereva wake yaani Laylah.
Ni mwaka pia toka Higgno akabidhiwe Hilda kama mke wake na kuanza kuishi maisha yaliyojaa maudhi na ukosefu wa amani, maana Hilda alizidi kuwa mwenye tabia mbaya kila kukicha, ukiachia tabia ya kulewa na kuchelewa kurudi huku akimuacha mtoto wake nyumbani kwa kina Higno, pia alianza tena kutoa kitumbua chake bila kukiheshimu, na safari hii hakukitoa kwa aajili ya kutafuta fedha kama ilivyokuwa zamani, ila kwaajili ya hulka aliyokuwa nayo na mara nyingi alifanya hivyo akiwa amelewa ulanzi, na wakati mwingine hutokea akamkosea adabu Higgno nae kushindwa kumuadhibu, maana kauli iliyotawala ni kwamba, “we nipige kama kweli mwanaume, kama sijaenda kwa mwenyekiti” hapo Higgno angekuwa mpole.
Zilikuwa zime pita siku chache toka zitangazwe nafasi za kazi kwenye kampuni ya tajiri Mahamud, nae akaandika barua ya kuomba kazi, ambapo alipewa majibu ya kuja pale kwenye ofisi za kampuni hiyo week tatu zijazo mbele, ikiwa ni jumatatu ya kwanza ya mwezi wa tisa, katika kufanya usaili, yaani interview, Higgno alitamani kupata kazi hiyo na alipanga kuwa endapo ataipata kazi hiyo basi ange mueleza boss wake yaani mzee Mahamud, ampange kwenye gari linalo safiri mbali, ili asiwe anashinda pale nyumbani kwao kuepukana na maudhi ya Hilda, mwanamke ambae ni kama alizaliwa kumnyima raha.*****
Naam siku tatu mbele, ikiwa ni siku ya juma nne, Hilda alienda mjini kukuangalia nguo zake na za mtoto, kwa fedha aliyoachiwa na Higgno ambae hakuwa na namna ya kumkwepa na kumnyima matumizi, na Hila akiwa ameshaingia mjii ana elekea majengo mitumbani, mara akashangaa kuona gari likisimama pembeni yake, “Hilda mambo vipi?” kwanza Hilda hakujua kama anasalimiwa yeye, pengine kulikuwa na Hilda mwingine, lakini alipotazama lile gari akaliona ni lile gari ambalo lilikuwa linamfuata Talib shuleni miaka ile, “na alipotazama vizuri akamuona Talib akimtazama kwa uso wa tabasamu” kwanza Hilda hakujua kuwa na yeye atabasamu au atulie, maana anakumbuka kuwa mara ya mwisho kijana huyu alimkataa mbele ya wazazi wake, “poa mambo Talib” aliitikia na kusalimia Hilda, “mbona mbali mbali ingia kwenye gari twenzetu” alisema Talib ambae kwenye gari alikuwa peke yake, …. ITAENDELEA.