TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA SITINI NA NANE
MTUNZI
Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA SITINI NA SABA: Lakini kabla mzee Mahadh haja ufikia mlango mara wakamuona Idd akirudi ndani kwa haraka, nusu amkumbe baba yake pale mlangoni, ikionyesha wazi kuwa Idd alikuwa anakimbia kitu kule nje, na wakati wanashangaa na kujiuliza kulikoni, mara wanamuona mwanamke mmoja mtu mzima akiingia pale mlangoni, “weeeee! weeeee! we kaka leo hunikimbii, naomba unilipe….” ghafla yule mwanamke alisita na kusimama akionekana kuwa hakutegemea kama ange kuta watu wengine pale ndani, “weye unaingiaje humu ndani namna hiyo hebu toka nje weweee” aling’aka mzee Mahadhi huku akimdaka yule mwanamke mtu mzima na kuanza kumsukumia nje……… ENDELEA……..
Maana tayari Mahadhi alisha hisi kuwa yule mwanamke alikuwa na tatizo na kijana wake Idd,na alipo jaribu kumsukumia nje mwanamke alikuwa mbishi kutii amri hiyo, “hapana mzee wangu huyu kaka lazima leo anilipe, yaani yote aliyo nifanyia halafu asinilipe hata shilingi, na aishie kunivunjia meno yangu” alilalamika yule mwanamke mtu mzima, huku wajumbe wote wakishangaa wasijuwe nini kinatokea, lakini kwa muonekano wa mwanamke yule wa uchovu wa mwili na sura kila mmoja akavutika kumsikiliza kujuwa alikuwa na nini na huyu kijana Idd, “hapana Mahadhi, hebu muache huyo mama aje atuleze shida yake” alisema mwenyekiti, huku yeye na wezake wakimtazama yule mwanamke kwa mshangao, “baba mtimue, ametumwa huyu Malaya, mfukuzeni humu ndani” alipaza sauti Idd, akishindwa kujizuiwa kutamka lugha chafu ndani ya baraza la wazee, “kijana chunga mdomo wako, upo kwenye baraza la wazee” alikemea mmoja wa wajumbe.
Mahadhi aliona kila dalili ya kijana wake kudhalilika, maana zile mbio alizokimbia kule nje ni wazi alikuwa anamkimbia mschana huyu, ikionyesha kuwa alikuwa na kisa nae, hakujuwa atamuokoaje kijana wake ambae alikuwa anazijuwa vyema tabia zake za ulevi na uzinzi, japo hakumuwekea wazo la kuwa atakuwa amefanya zinaa na mwanamke huyu mkongwe, “mama vua viatu vyako hapo mlangoni kisha njoo ueleze unatatizo gani” alisema mwenyekiti, na hapo mschana yule ambae sio mwingine ila ni Sinamengi, alifanya kama aliyo elekzwa na kisha kuingia ndani na kuonyeshwa upande wa kukaa, Mahdhi nae akarudi tena barazani na kukaa, “lakini mwenyekiti tutawezaje kumruhusu mwanamke kama huyu kuingia humu barazani, isitoshe umesha ambiwa kuwa ni mwanamke mwenda ovyo” alisema Mahadhi, ambae aliona wazi mambo yana haribika mbele ya baraza, “kama ni wa hovyo aliwezaje kufahamiana na Kijana wako” alisema mwenyekiti huku wengine wakiunga mkono kasoro wachache ambao toka mwanzo walionekana kumkandamiza bwana Mahamud, walianza kujiona wajinga na kuanza kuyakumbuka maneno ya Mahamud kuwa “bwana Mahadhi nadhani unashindwa kuelewa kuwa huyu kijana wako ni mtu wa aina gani, au pengine unafahamu lakini una wapumbaza wajumbe wa baraza ili wakuunge mkono kwa kile unacho kifanya, nadhani hata wao wange mfahamu wasinge jiuliza ile messeji imetokea wapi” hapo mmoja wao akaingilia kati, “lakini mwenyekiti inawezekana swala lao likawa ni swala binafsi la bwana Idd na huyu mama, kwanini wasiende kuliongea wenyewe faragha na sio hapa hadharani” alishauri mjumbe huyo kwa sauti ya kuhamaki, “mzee wangu naomba hili swala tuliongee mbele yenu, Kwa sababu najuwa hawezi kunisikiliz hata nyie wenyewe mumeona alivyo nikimbia”, alisema mwana mama Sina mengi kwa sauti ya kuombeleza, “sawa hata mimi naona kuwa maadamu swala hili limeingia humu ndani wacha tulimalize humu humu, inaonekana Idd ameshindwa kumalizana nae huko nje” alisema mwenyekiti, ambae alishaanza kuona dalili mbaya toka kwa Idd, ni kutokana na lugha chafu aliyoitumia kwa mwanamke yule bila kuangalia kama yupo na wazee wenye heshima zao.
Hapo idadi ya watu wengi ikaunga mkono uamuzi wa mwenyekiti, japo Mahadhi na wenzake hawa kuonyesha kuridhika na maamuzi yale na ndipo Idd alipoona kuwa anaenda kuumbuka live live, na pengine mchezo mchafu aliotaka kuufanya kwa Soraya ungethibitishwa mbele yake, hapo akainuka ghafla,“jamani kama munamsikiliza huyu changu mimi natoka nje” alisema Idd huku ana anza kutembea kuufuata mlango, “hivi huyu ndie kijana ambae tunahitaji amchumbie binti wa Mahamud, mbona nidhamu yake ni sawa na wala madawa ya kulevya wa huko mtaani, anafanya nini sasa, hebu kaa hapa” alisema mmoja wa wajumbe kwa sauti iliyojaa hasira, lakini Idd hakusimama wala kugeuka akaendelea kutoka nje, “hebu mzuieni asitoke” alisema mwenyekiti, na hapo ndipo Idd aliposimama na kuwageukia wale wazee ambao walikuwa wanamtazama kwa mshangao, “nani anizuie? kama mumeshindwa kuongea na huyu mwarabu koko nimuoe binti yake sasa munataka nini kwangu, kaeni na huyo changudoa muongee nae” alisema Idd, kwa sauti ya kibabe, kisha akaelekea nje, “sasa naanza kuamini kuwa huyu kijana ni muovu, hata ule ujumbe mchafu aliuandika yeye mwenyewe” alisema mwenyekiti na wajumbe wengine wakamuunga mkono kasoro mzee Mhadhi na wenzake wachache ambao walikuwa wanahisi kufedheheka mioyoni mwao, maana kabla hata hawajatoka mule ndani tayari maneno ya Mahamud yalishaanza kutimia kwa muonekano wa matendo ya Idd.****
Talib alifika kule mwembechai moja kwa moja nyumbani kwa Zido na kuwakuta wakina Vitusi Zido na wale wengine wanne, ambao hali zao zilikuwa zimesha tengemaa kasoro yule alievunjika mkono, “oyaaa! yule fala anazidi kunipanda kichwani” alisema Talib, huku anasogelea Vitus na kumpokea kipisi cha bangi, “duh! fala yupi tena?” aliuliza Zido, huku ana chakua majani ya bangi mengine na kuanza kuyasokota kwenye karatasi lake maalumu, “ni yule boya Higgno, et ndie mtu anaemgonga Soraya” alisema Talib kama vile anasimulia kituko cha ajabu sana, huku wakina Zido wakiangua kicheko cha mwaka, “kumbe yule boya ni shemeji yako?” aliuliza Vitus, huku wakiendelea kucheka kwa sauti kubwa, hapo Talib akawasimulia jinsi alivyo gundua jambo hilo na yeye kuongea uongo kwa shangazi yake, “dah! dogo anazali kweli, lakini kwa ubabe alio uonyesha mbele ya Soraya lazima demu aingie mtego” alisema mmoja kati ya wale vijana wanne, “lakini tayari nimeshampa kesi, nimepakaza kuwa yeye ndie aliepanga mchongo wote” alisema Talib na kuwaeleza wenzake jinsi ilivyo ongea na shangazi yake, “sema kama alianza kunishtukia hivi, ila hakuna ubaya, kinachotakiwa ni sisi kumaliza mchezo, wao wakimkamata mpaka sijui wagundue kuwa sio yeye tayari sisi tumesha fika mbali na mambo yetu” alisema Talib akiendelea kuvuta bangi, “mh! talib una uhakika na unacho kisema, maana michongo miwili yote imefeli” alisema Vitus, akionyesha mashaka juu ya swala hilo, “nyie musiwe na wasi wasi, cha msingi pale mukivuka muna mfunga kamba mlinzi, kisha nawapa funguo munazama ndani munakomba mkwanja kisha munatoka zenu, wao mpaka washtuke ni kesho asubuhi” alisema Talib kwa sauti ya dharau, sauti ambayo kwa vyovyote vile ungejuwa kuwa alikuwa na uhakika wa kufanikiwa mpango ule, “basi poa, sasa mchongo lini?” aliuliza Zido akionyesha kukubali mpango ule, “kesho usiku, inabidi tufanye faster kabla hawaja muuliza yule boya” alisema Talib, hapo wakina Vitus wakatazamana, kisha wakamtazama Talib huku wana kubali kwa kichwa.********
Wakina Soraya wakiwa ndani ya gari waliweza kumuona Idd anatoka kwenye ukumbi wa baraza akiwa mbio mbio na kuelekea ndani ya gari la baba yake na kutulia ndani yake bila kuondoka, “huyu atakuwa amekimbia au wamemtoa ili waongee na yule mwanamke?” aliuliza Laylah, “sijui hebu kwanza tuendelee kutazama” alisema Soraya, huku wote wakiwa wanatazama kule mbele yao.
Ukweli licha ya kuwa alikuwa anatazama kule msikitini ambako Sinamengi alikuwa ameshaenda, lakini Soraya bado mawazo yake yalikuwa kwa Higgno, “Higgno amesema kuwa na yeye ametafuta mshenga” alisema Soraya, “lakini Soraya, huyo mwanaume atawezaje kutafuta mshenga wakati sehemu ya kukaa haieleweki?” aliuliza Laylah, “mimi ndie niliemueleza kuwa inabidi tufuate utaratibu wa kunichumbia, sidhani kama swala sehemu ya kuishi itakuwa ni tatizo kwetu” alisema Soraya, huku wakiendelea kutazama kule msikitini, “una maanisha unataka kumfanyia kila kitu Higgno?” aliuliza Laylah, akionyesha mshangao kwa mwanamke kuandaa maisha ya ndoa yeye na mwanaume wake, “hapana sitofanya kila kitu peke yangu ila tutasaidiana” alisema Soraya macho yake sasa yalikuwa kwenye gari alilo ingia Idd, “lakini huoni kwamba yeye atakupendea mali na sio mapenzi ya kweli?” aliuliza Laylah, akionyesha mashaka juu ya uamuzi wa Soraya, swali ambalo Soraya nadhani hakulipenda, “nipo tayari kumfanya chochote ili Higgno azidi kunipenda, halafu Higgno sio mwenye tamaa, kama angekuwa na tamaa basi angekuwa amesha mzonga zonga baba toka zamani, si unajuwa kuwa anamfahamu?” aliuliza Soraya akiendelea kutazama kule kwenye gari, “lakini kweli yule kaka anaonekana mwenye mapenzi ya kweli” alisema Laylah.*******
Ukweli mama Soraya kutwa nzima ya siku ile alikuwa ametulia nyumbani kwake akiwaza na kutafakari juu ya kile alichoambiwa na mtoto wa kaka yake yaani Talib kwamba yule kijana mpole ndie aliepanga utekaji wa Soraya, na kisha kwenda kumuokoa, “kwa lengo gani haswa?” alijiuliza mama Soraya, “lakini huyu huyu ndie alie muokoa Soraya siku chache zilizopita toka kwa Idd, na kama angekuwa na nia ya kumteka si angemteka siku ile ambayo alikuwa amelewa” aliendelea kuwaza mama Soraya, ambae kwa upande mwingine aliona kuwa maneno ya Talib yalikuwa na ukweli ndani yake, Kwa sababu ni kweli Soraya alikuwa anamfadhiri baba wa kijana huyo kujenga duka lake ambalo lilikuwa limeunguwa moto, “na kama hivyo basi wawili hawa wanafahamiana muda mrefu, na vipi kuhusu Talib ameyajuwaje yote hayo, na Soraya ndiyo kusema tayari amesha fanya mapenzi na yule kijana?” aliwaza mama Soraya ambae alikuwa anatamani sana kumueleza mume wake juu ya hilo lakini alikuwa ameshaishiwa salio.*******
Baada ya kuhakikisha ukumbi umetulia mwenyekiti alimruhusu mwana mama yule aanze kuongea, “haya mama unaweza kujitambulisha na kutuleza una shida gani na Idd, maana sisi ndie wazee wake na tunaweza kukusaidia” alisema Mwenyekiti akimtazama Sinamengi, kwa maana ya kumpa nafasi ya kueleza shinda yake, ili wamsikie na kumsaidia, “mimi naitwa Sina mengi, ni mfanyakazi wa kuchile bar” kusikia hivyo tu! tayari watu wote mule ndani wakajuwa binti huyu anataka kuongea nini, “jamani kama ni muhudumu wa bar mimi sipo tayari kusikiliza upuuzi wake, wacha niondoke” alisema Mahadhi huku anainuka , “bwana Mahadhi naomba labda nikuambie kitu, endapo utatoka ndani ya baraza hili basi kuanzia leo hauto ruhusiwa kuswali kwenye msikiti wowote” alisema Mwenyekiti na hapo Mahadhi akakaa chini na Sina mengi akaendelea kueleza, “siku ya alkhamis saa nne asubuhi nikiwa kazini alikuja yule kijana alietoka nje na kunikabidhi juice kweny chupa, akinieleza kuwa ameweka dawa za kulevya na kwamba atakuja na mschana ambae ataagiza juice na mimi nimletee hiyo, akiwa na lengo la kumuingilia kimwili mara baada ya kulewa, pia aliniomba nimchukulie chumba kwenye hoteli ile ile ya kuchile, chumba ambacho tungemuingiza yule mschana baada ya kulewa ili yeye akamuingilie kimwili, akiahidi kunilipa fedha mara baada ya kumaliza kazi hiyo” alieleza Sinamengi, huku wote wakimsikiliza kwa umakini, na bila kubakisha neno Sinamengi akasimulia kila kitu kilichotokea jioni ya siku ile, kwamba yule mschana mrembo wa kiarabu alifanikiwa kukimbia, “na yule kijana kuamua kulala na mimi” alisimulia mwana mama Sina mengi, na kueleza mchezo mchafu uliofanyika usiku ule, Idd akimwingilia kwa njia ya kinyume na maumbile, “na mbaya zaidi Asubuhi akavunja meno yangu ya bandia na kuondoka bila hata kunipa shilingi moja, mimi ninacho omba ni hela ya kwenda kununulia meno mengine” alimaliza kusema Sinamengi na kumuacha kila mmoja akisisimkwa na simulizi ile, “huu ni mpango mwingine wa kumchafua Idd, hakika huyu mwanamke nampeleka polisi” alisema Mahadhi kwa sauti ya Jazba, “nipo tayari hata kuongea polisi, lakini kumbuka yule mschana pia anafahamu kuwa aliwekewa dawa kwenye Juice, na yeye atathibitisha” alisema Sinamengi kwa sauti ya kujiamini, “Mahadhi niwazi kabisa unafahamu kila anachofinya kijana wako Idd na bila shaka unaweza ukawa una ushirikiana na kijana wako kujaribu kufanya uovu huu na kumchafua bwana Mahamud ili upate fulsa ya kumchumbia binti yake” alisema Mwenyekiti, “tena hawana nia nzuri katika swala la kumchumbia Soraya binti Mahamud, nadhani ni tamaa za utajiri ndizo zilizo walazimisha kufanya hivyo” alisema mwingine na Mahadhi uzalendo ukamsinda, “hapo sasa munanikosea adabu, nitashirikiana nae vipi katika swala kama hilo, na vipi kama huyu mwanamke ametumwa kuja kuchafua” alisema Mahadhi kwa jazba, “inawezekana ametumwa kuja kuchafua kwa kueleza kila kitu, lakini bado swala linabakia pale pale Mahadhi, kuwa kijana wako alikuwa na mpango mbaya na binti yangu, kwa kweli kabisa ninajuta sana kukuweka karibu na mimi” alisema Mahamud kwa sauti ya msisitizo, ilyoonyesha kuchukizwa, “basi yaishe bwana Mahamud, umefanikisha nitamuambia Idd aachacne na Soraya” alisema Mahadhi huku anasimama na kutaka kutoka nje, “Mahadhi kuhusu Idd kuachana na Soraya hilo nilisha lipanga toka siku nilipogundua maisha ya Idd alipokuwa nje ya nchi, tunachokifanya hapa ni kuhakikisha watu wanafahamu tabia halisi ya kijana wako na wewe unalipia gharama za meno za huyu mama, na pia nakusanya ushahidi ili nikufikishe mahakamani kwa kosa la kuandika ujumbe wa kunichafua” alisema Mahamud, kisha akasimama na kusogea mbele kwa mwenyekiti, “samahani naomba niwahi nikaswali halafu nikafanye makusanyo, maana ni alaasiri sasa, alisema Mahamud na wote wakashtuka na kutazama saa zao, “kweli saa tisa, lakini kabla hatujaondoka ni muhimu kufahamu kiasi cha fedha anachotakiwa kukipata huyu mwanamke, pia bwana Mahamud tutahitaji kukutana tena na kulizungumzia swala hili vizuri, maana haipendezi kuona sisi wenyewe tuna pelekana polisi kwa mambo kama haya” alisema mwenyekiti na mzee Mahamud akakubali swala la kukutana, pia Mahadhi akatakiwa kutoa kiasi cha fedha elfu ishirini kwaajili ya Sinamengi.
Hakika wapo walio mpongeza bwana Mahamud kwa jinsi alivyoweza kujiondoa kwenye ile kashfa na tuhuma kubwa ya ajabu, pia wapo walio shindwa hata kumtazama usoni kutokana na kushadadia kitu ambacho hawakujuwa kuna nini nyuma ya panzia.*******
Naam Soraya na Laylah wakiwa bado wametulia pale pale ndani ya gari wanatazama kule msikitini, mara wakamuona Sinamengi akitoka kwenye ukumbi wa baraza la wazee na kuanza kuja upande wao, “huyoooo! anatoka, msubiri kwanza apite halafu tutamfuata nyuma” alishauri Soraya huku wakimtazama Sinamengi aliekuwa anakuja kwa mwendo wa haraka haraka na uso wake ukionyesha dalili ya furaha huku nyuma yake wakianza kuonekana wazee wakitoka kwenye ukumbi na kuelekea kwenye bomba la maji kuchukuwa udhu maana tayari adhana ilianza kusikika, “mh! muda umeenda eeh! saa tisa hii” alisema Laylah, huku anatazama saa yake ya kwenye simu na wakati huo tayari Sinamengi alikuwa anakatiza pembeni ya gari lao, huku mawazo yake yakiwa huko anakoelekea.
Baada ya Sinamengi kupita na kupotelea mbele kidogo na wao wakawasha gari na kumfuata nyuma mpaka walipomfikia, wakamchukuwa kwenye gari na kuelekea nae NPF kwenye hospital ya meno, huku njiani Sinamengi akiwasimulia kila kitu jinsi kilivyo kuwa kuanzia Idd alipomuona na kukimbilia ndani, na kule ndani jinsi mambo yalivyo kuwa mpaka maamuzi na msimamo wa Mahamud.
Baada ya kumfikisha Hospital na kumuacha Sinamengi, wakina Soraya wakaelekea nyumbani ambako walimkuta mama Soraya akiwa anatoka kuswali, “assalam alaykum” alisalimia Soraya, mara baada ya kuingia ndani akiwa amemuacha Laylah nje ana egesha gari vizuri, “waalaykum salaam naona unatembea vizuri sasa?” aliuliza mama Soraya, huku akimtazama mwanae kwa jicho la shaka, “ndio mama nimeshapewa dawa” alisema Soraya kwa sauti ya wasi wasi, huku akijichekesha chekesha, “ulimueleza nini doctor mpaka akakupa dawa na umepewa dawa gani kwa kitu kama hicho? kwani umeambiwa huo ni ugonjwa?” aliuliza mama Soraya huku akiachia tabasamu la kusanifu, Soraya akatazama chini kwa aibu, “anaitwa Higgno, ni mtoto wa mzee alieunguliwa na duka sio?” aliuliza tena mama Soraya, hapo Soraya akainua uso wake kumtazama mama yake kwa mshangao……….. ITAENDELEA
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA SITINI NA TISA
MTUNZI
Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA SITINI NA NANE: waalaykum salaam naona unatembea vizuri sasa?” aliuliza mama Soraya, huku akimtazama mwanae kwa jicho la shaka, “ndio mama nimeshapewa dawa” alisema Soraya kwa sauti ya wasi wasi, huku akijichekesha chekesha, “ulimueleza nini doctor mpaka akakupa dawa na umepewa dawa gani kwa kitu kama hicho? kwani umeambiwa huo ni ugonjwa?” aliuliza mama Soraya huku akiachia tabasamu la kusanifu, Soraya akatazama chini kwa aibu, “anaitwa Higgno, ni mtoto wa mzee alieunguliwa na duka sio?” aliuliza tena mama Soraya, hapo Soraya akainua uso wake kumtazama mama yake kwa mshangao………..SONGA NAYO ……..
Kitu ambacho mama yake akajuwa ni kweli alicho ambiwa na Talib, “mama kwahiyo unanifuatilia?” aliuliza Soraya ambae ni kweli mpaka dakika hiyo alikuwa amemdanganya mama yake kuwa ameumia goti lakini ni kwamba yalikuwa ni maumivu ya kitumbuani kutokana na kupewa dudu kwa mara ya kwanza, “kwahiyo ni kweli unae msaidia ni baba yake Higgno sio?” aliuliza mama Soraya akionekana kuwa makini sana bila dalili ya utani au mchezo, mara nyingi huwa hivi wakati anapokuwa na jambo lililomkera, “hapana mama, sio baba yake Higgno, ila pia wazazi wa Higgno wanakaa…” alisema Soraya kwa mshangao, kabla hajasita kidogo na kukumbuka jambo fulani, ni kwamba licha ya Higgno kumueleza kuwa wazazi wake wanaishi Luhila pia mzee Frank alimueleza kuwa anakijana wake na hata siku ya jana asubuhi alikutana na mzee Frank kule chem chem alimueleza kuwa anaenda kumpa taarifa kijana wake, na hata leo Higgno amekuja mjini na amesema yupo na baba yake na wana toka mjini na alikuwa kwenye gari ambalo lilionekana kuwa ni gari la wazi, kwahiyo inawezekana kuwa ni kweli Higgno ni mtoto wa mzee Frank, “mh! inawezekana mama, lakini mimi nilikuwa sijui, nadhani hata Higgno hajui kuwa namfahamu baba yake” alisema Soraya kwa sauti ya mashaka akionyesha bado anajiuliza mama yake amelijuwaje jina la Higgno, wakati miaka yote hii walikuwa wanahangaika kumtafuta kijana huyu bila mafanikio, “inawezekana vipi, kwahiyo hujawahi kukutana na Higgno nyumbani kwa wazazi wake?” aliuliza mama Soraya, akionyesha wazi kuwa anahisi Soraya anadanganya, maana alishaanza kuamini maneno ya Talib kuwa mchezo huu ulipangwa na kuratibiwa na Higgno ambae alijifanya anatoa msaada kumbe anahitaji kumnasa Soraya, kisha kujichumia utajiri, “mama kama nilivyo kuambia, yule mzee tulimsababishia ajali siku ile nilipokuwa na Idd, na kuhusu Higgno nadhani hakuna asiejuwa, kwani kuna tatizo gani juu ya Higgno?” aliuliza Soraya kwa sauti ya kuhamaki, ni baada ya kuona kuna dalili za kumshuku vibaya Higgno, ambae yeye ana uhakika wa asilimia nyingi kabisa kuwa Higgno ni mvulana pekee mwenye mapenzi juu yake, ukiachilia kuwa kijana mwema na mpole kupata kumuona, “kwa taarifa yako huyo mwanaume sio mtu mzuri, na anashirikiana na baba yake kujifanya ni watu wema kwako ili wapate wanacho hitaji” alisema mama kwa sauti iliyojaa jazba na hasira, “we mama muogope mungu na maandiko yake, kijana wa watu hata hanijuwi nakaa wapi, ni mtoto wa nani, leo hii aanze kupanga mipango hiyo, tena kwa miaka yote hiyo, mbona basi angeweza kunipata toka ni kiwa form two au angekubali kuongozana na wewe siku ile nilivyoleweshwa madawa” alisema Soraya kwa sauti iliyojaa busara na mshangao kwa mama yake, “unajuwa pengine alipanga na Idd kufanya hivyo” alisema mama Soraya kwa sauti ya jazba, “kwahiyo baba anahusika katika mpango huo, maana yeye ndie alieniambia kuwa nimsindikize Idd kule bomba mbili?” aliuliza Soraya kwa jazba pia, si unajuwa mtu akishapenda, “baba yako alidanganywa tu ule mpango ni wa Idd na baba yake” alisema mama Soraya kwa sauti ya jazba na Hasira pia, “lakini yule mwanamke alie tuhudumia amesema kuwa ulikuwa ni mpango wa idd ili aniingilie kimwili na nilimwambia aende akaseme barazani kwenye kikao, sasa Higgno anahusika vipi?” aliuliza Soraya, hapo mama Soraya akatulia kidogo kabla ya kuongea kwa upole, “lakini Soraya, hukupaswa kukufanya nae chochote mpaka tumchunguze kwanza” alisema mama Soraya kwa sauti ya upole, hapo Soraya alijuwa mama yake anamaanisha nini, akatazama chini kwa aibu, “lakini mama sikujuwa kama tutafanya hivi, mimi nilikuwa namjaribu kama anaweza kuzalisha” alisema Soraya kwa sauti ya upole, “mama yangu Nanyoni, nani alikuambia mwanaume anajaribiwa? na kwanini uliamua kumjaribu?” aliuliza mama Soraya kwa sauti ya chini yenye mshtuko na mshangao, huku akikaribia kucheka kwa upuuzi wa binti yake, “niliona mtu mwenyewe haonyeshi dalili za…” alisita Soraya alieongea kwa sauti ya uoga, huku bado akitazama chini, “dalili kama zipi Soraya?” aliuliza mama Soraya kwa sauti ya chini, bado ikiwa na mshangao, “za kuwa na uwezo, kwasababu hakuwahi kuwa na mwanamke, pia hata nilipolala nae siku ya kwanza alikuwa anaogopa kunigusa” alisema Soraya kwa sauti ya uoga kama mwanzo iliyojaa aibu, “mh! sasa umeuona urijali wake, haya subiri uthibitisho wa mimba” alisema mama Soraya huku anataka kuondoka, “lakini mama jujaniambia umejuwaje, kuhusu higgno na kwamba yule mzee ni baba yake, kwasababu nilimuomba awe mshenga wa Higgno?” aliuliza Soraya huku anamtazama mama yake ambae alisimama na kutulia kidogo kama anawaza amtaje au asimtaje.******
Hakuna siku Mzee Mahadhi alijona kuwa na bahati mbaya kama siku hii ya leo, hata alipokuwa anaswali alaasiri alikuwa akifanya vile vitendo, vya takbira kufunga swala kurukuu na kusujudu, ni sababu aliwaona wenzake wakifanya hivyo, lakini kiukweli mawazo yake haya kuwepo kabisa mahali pale, alikuwa anawaza fedheha aliyoipata, maana hata mambo ambayo hakutegemea kuwa yange fahamika yamefahamika, “sijui amejuwaje huyu mshenzi kuwa Idd alikuwa hivyo huko msumbiji?” hilo ni moja ya swali ambalo lilimsumbua , na swali la pili lilikuwa ni vipi ataongea na bwana Mahamud kumuomba msamaha juu ya yale yaliyotokea, “nitamwambia kuwa sihusiki na jambo hilo, ni kwamba Idd ameniingiza kwenye mkenge” aliwaza Mahdhi akiwa katika swala.
Naam sio kwamba alimaliza kuswali ni kwamba alitoka nje baada ya kuwaona wenzake wanamaliza na kutoka nje, na alipofika nje aliweza kuwaona wenzake wakimfuata Mahamud na kumuomba radhi kwa kile walichokifanya ndani ya ukumbi wa baraza la wazee na kumpa pole kwa kashfa aliyozushiwa, “kwa niaba ya wazee wote tuliopo hapa na tulioshiriki kikao hiki, nikutake radhi bwana Mahamud kwa hii dhahama, lakini imekuwa vyema tumelizungumza na kubaini ukweli, maana tungebaki na viulizo huku kashfa inasambaa, nadhani kwenye swala ya ijumaa nitalizungumaza swala hili na kuliweka sawa” alisema mwenyekiti, ambae ni kama aliongea baada ya wenzake waliokuwa pembeni wanasikiliza majibu ya Mahamud juu ya msamaha wao, toka kwa Mahamud ambae alikuwa pembeni ya gari lake, “hakuna tatizo mwenyekiti, ila nitahakikisha nampata mtu aliefanya hivi, na nitampeleka mahakamani ushahidi wa sms ninao” alisema Mahamud ambae alikuwa ameonyesha kukasirishwa na jambo hilo japo alishukuru kufanikiwa kuwaelewesha wajumbe wa baraza, huku akimshukuru Sinamengi kwa ujio wake pale msikitini, japo hakuelewa ilikuwaje mpaka akafika pale msikitini, alitamani kumuona tena ili ampe zawadi, “nashukuru sana bwana Mahamud kwa kuelewa jambo hili na kutusamehe kwa ujumla wetu, maana kila mmoja alikuwa ana hasira za wazi kabisa juu yako, akiamini kuwa ule ujumbe ni wa kweli, pia tunaomba utualike kwenye harusi ya mwanao, na kwa heshima ndoa ifungwe kwenye msikito huu” alisema mwenyekiti wote wakacheka kwa furaha, “siwezi kuacha kuwa karibisha kwenye siku hiyo muhimu na yakipekee kwenye familia yangu” alisema bwana Mahamud akionyesha kuondokewa na hasira yote kisha wakaagana na kila mmoja akaelekea kwenye gari lake, na wasio na magari ambao idadi yao ilikuwa kubwa wakaondoka zao kwa miguu huku kila mmoja akikiri kuwa Idd sio kijana mwema, hata wao waliapia kuwa wasinge weza kukubali binti zao au wajirani zao au wandugu zao wachumbiwe na Idd.
Mahadhi ambae muda wote alikuwa mbali anawatazama wenzake, sio kwamba hakutaka kwenda kuungana na wenzake kuomba msamaha, ila yeye hakujuwa ataanzaje kujieleza mbele ya Mahamud kwa kile alicho kifanya, yeye alichokifanya ni kumvizia mwenyekiti mara tu baada ya kumaliza kumuomba msamaha bwana Mahamud, na alipomuona mwenyekiti ana chanja mbuga kuelekea mtaa wa shule ya mfaranyaki akamkimbilia haraka, hakujuwa kama kijana wake Idd alikuwa amejibanza ndani ya gari akiwatazama wazee waliokuwa wanatawanyika kuelekea makwao.
“Kumradhi mwenyekiti, ninahitaji muda wako kidogo” alisema mzee Mahadhi, kwa sauti ya kinyonge, mara tu baada ya kumfikia mwenyekiti, “bwana Mahadhi kabla hujaongea naweza kujuwa nini unataka kuongea, lakini kiukweli huwezi kusema ulikuwa hujuwi hila za mwanao Idd, kiukweli umetumaanisha vibaya sana, na nina kuambia ukweli bwana Mahadhi kama hauto mfuata mapema Mahamud na kumuomba msamaha basi utaozea jela, na hakuna atake kusikitikia, maana umefanya vibaya sana, kuhusu kijana wako hilo hata mimi sijui” alisema mwenyekiti akionyesha kuwa amechukizwa kweli kweli, “mwenyekiti, ukweli shetani alinipitia, nakuomba tafadhari nisaidie juu ya hili, siwezi kurudia tena ujinga kama huu” alisema Mahadhi kwa sauti ya kuomboleza, kitu ambacho mwenyekiti hakukijuwa ni kwamba, sio kuwa Mahadhi alikuwa anajutia alicho kifanya ila alikuwa anaogopa kupelekwa mahakamani.
Hapo mwenyekiti akatulia kidogo kama anawaza atoe jibu gani, kisha akamtazama bwana Mahadhi, “sawa bwana Mahadhi nadhani tutahitaji muda wa kukaa na kuona namna ya kwenda kwa Mahamud” alisema mwenyekiti na kisha wakaagana na kila mmoja akaelekea upande wake, wakati mwenyekiti akiendelea na safari yake huku Mahadhi akirudi kule msikitini ambako aliliacha gari lake.
Mahadhi alishtuka sana baada ya kumkuta Idd ndani ya gari, lakini aliingia ndani ya gari na kuondoa gari na safari ikiwa ni ya kimya kimya, hakuna hata mmoja aliemsemesha mwenzake mpaka walipofika nyumbani na kuingia ndani, “hivi we mpuuzi uliwezaje kulala na bibi kama yule?” aliuliza Mahadhi kwa hasira huku akimtazama Idd aliekuwa anachukuwa chupa ya pombe kali na kumimina kwenye glass, kisha bila kumjibu baba yake akajimiminia ile glass kwa mkupuo mmoja akiimeza ile pombe kwa kukunja sura na kuiweka glass tupu mezani, “baba hayo maswali sio mahala pake, huu wakati inabidi tukomalie mpango wetu” alisema Idd huku anachukuwa sigara yake na kuiwasha, “baradhuri mkubwa, yaani hiyo mipango yako nuksi bado unaiwazia?” aliongea Mahadhi kwa sauti iliyojaa hasira, huku anaelekea chumbani kwake, “bwana hee kama wewe umegwaya mimi nitakomaa mwenyewe” alisema Idd, huku anamimina pombe kwenye glass, “utakomaa nayo ukiwa jela” alisema Mahadhi huku anaingia chumbani kwake.*******
Naam kule nyumbani kwa Mahamud, mama Soraya baada ya kujiuliza akaona hakuwa na budi kumtaja mbea wake, “ameniambia Talib, ni baada ya kusikia maongezi yetu asubuhi” alisema mama Soraya kisha akataka kuondoka, “mh! unamsikiliza huyo mvuta bangi?” aliuliza Soraya kwa sauti ya mshangao, hapo mama Soraya akasimama na kugeuka kumtazama mwanae, sura ameikunja kwa hasira, “we! Soraya, acha kumuita mwenzio mvuta bangi, na tunapaswa kuheshimu na kuyathamini mabadiliko yake, kama bangi alishaacha siku nyingi” alisema mama Soraya kwa sauti ya ukali yenye kuonya, “mama unajidanganya, kwa taarifa yako nimemuona kwa macho yangu anavuta bangi ndani mwake huku amewasha udi ili harufu isitoke nje” alisema Soraya kisha akatoka na kuelekea chumbani kwake..... ITAENDELEA MUWE NA USIKU MWEMA