TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA SITINI NA SITA
MTUNZI
Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA SITINI NA TANO: Naam mahamud alijikuta anatoa macho ya mshangao mara mbili, ni mshangao ulio ambatana na tabasamu jipya la matumaini, ni baada ya kumuona kijana mmoja mrefu kiasi mwenye mwili wa mazoezi, ambae leo alikuwa amevalia nadhifu, ni kijana yule yule aliemsaidia mwaka mmoja uliopita siku aliyovamiwa na wezi kwa lengo la kumpora fedha, ni kijana aliemsaidia kubadiri tairi la gari lililotobolewa na mtego wa wezi wale akiwa amesimama mbele yake amashika wallet yake akimnyoonyeshea kwa maana ya kumpa, “amakweli ukiona kiza kinashamiri basi mawio yaja” alisema Mahamud huku tabasamu likiendelea kushamili usoni mwake……ENDELEA……..
Huku akiendelea kumtazama kijana huyu, ambae mara ya mwisho alimuona kwa sekunde kadhaa kule ofisini kwake na kuambiwa kuwa ameondoka ni kijana pekee ambae yeye Mahamud alimuona kuwa anafaa kumuoa binti yake Soraya, kijana ambae sio tu kufurahi kuonana nae, lakini pia alikutana nae katika siku muhimu sana kwake, “assalama Alaykum kijana, habari za siku nyingi” alisalimia mzee Mahamud kwa sauti ya uchangamfu na mshangao ndani yake, huku anapokea ile wallet toka kwa kijana mpole, “waalaykum salaam mzee kumbe bado unanikumbuka, nilidhania umesha nisahau” alisema Higgno kwa sauti yake tulivu lakini ni ile iliyochangamka, “nitakusahau vipi kijana wakati kila siku mimi na familia yangu hatuachi kukutaja, sijui kwanini uliondoka pale ofisini wakati nafasi yako ya kazi ipo wazi kabisa?” aliuliza Mahamud kwa, huku analipia vocha kwa yule dada ambae mpaka sasa alikuwa amekodoa macho kwa mshangao, “nili…” Higgno alisita kuongea kwasababu kama angeongea ukweli lazima angemtaja Laylah, ambae hakujuwa ni kwanini alionekana kwenye ofisi za mzee huyu siku ile, “nilipoona siitwi jina nikaondoka, nikasema nitakutafuta siku nyingine” alisema Higgno akificha siri ile, “sio tatizo, cha msingi ni kwamba leo tume kutana” alisema mzee Mahamud huku ana malizana na muuza duka, “kwa kweli imekuwa bahati kwangu” alisema Higgno, alieshika mfuko wenye vitu alivyonunua mchana ule, akionyesha wazi furaha yake ya kukutana na mzee Mahamud, ambae hakujuwa kuwa ni mkwe wake, “ok! kijana vipi unashughuri gani sasa, yaani muda huu?” aliuliza mze Mahamud, na hapo sio tu yule binti pekee aliewaza kuwa hawezi kusema kuwa alikuwa busy na shughuli fulani mbele ya mzee kama huyu, ambae ni mmoja kati ya matajiri wakubwa hapa Tanzania, hata Higgno ambae alikuwa anahitaji kazi ili aweze kumudu maisha na pengine kuweza kumnunulia mahitaji mpenzi wake Soraya, ambae mpaka sasa hakuwa anajuwa ni mtoto wa nani pale mkoani, “nimesha maliza kununua mahitaji yangu” alisema Higgno akisahau kuhusu baba yake, ambae hakuwa amewasiliana nae toka alipowasiliana nae asubuhi, “ok! basi kijana naomba uambatane na mimi kwa muda huu, maana tuna mambo mawili matatu ya kuzungumza” alisema Mahamud, huku akiongozana na Higgno kutoka nje ya duka lile, “bila shaka mzee wangu” alisema Higgno, ambae alikuwa amebaba mfuko wake huku wanaelekea kwenye gari, huku mzee Mahamud akiwaza na kumtafakari kijana huyu kuwani kijana wa pekee katika nyakati hizi za utakula kwa ujanja wako, kuwa ndie kijana anaweza kumchumbia binti yake Soraya, “vipi kijana unafamilia?” aliuliza mzee Mahamud, mara tu! baada ya kuingia ndani ya gari, akiwa na maana ya kwamba kijana huyu ana mke na watoto, “ndiyo ninayo” alijibu Higgno kwa uchangamfu, akidhania kuwa mzee huyu anauliza kama anafamilia ili kuona kama ana maisha ya aina gani, maana familia ni moja ya picha ambazo umueleze mtu, lakini haina maana kuwa asie na familia ni muhuni.
Lakini jibu ilo lilimshtua kidogo mzee Mahamud, ambae Mahamud alikuwa anaendesha gari huku Higgno akiingiza vocha kwenye simu, mahamud ambae aliamini kuwa kijana huyu ndie kijana wa pekee ambae anaweza kuwa mkwe wake kwa binti yake wa pekee, “hooo! hongera sana kijana, una watoto wa ngapi?” aliuliza mzee Mahamud, huku anampatia Higgno simu na vocha ili awez kuingiza kwenye simu ile na kuondoa gari kuelekea upande wa msikiti wa mkoa, swali lile lilimfanya Higgno acheke kidogo, “hapana mzee sijabahatika kuoa” alijibu Higgno na kumshangaza kidogo, Mahamud, “sasa wewe unaizungumzia familia ipi?” aliuliza Mahamud huku anatabasamu, “nilidhani unaniuliza kuhusu baba na mama” alisema Higgno na wote wakacheka kidogo, “”kwanini hujaoa mpaka umri huo kijana?” aliuliza Mahamud huku anaendesha gari taratibu, “bado sijapata kazi, sasa nikioa nitashindwa kumlea mke na pengine watoto wakizaliwa” alijibu Higgno kwa sauti tulivu na ya upole, kwahiyo ukipata kazi unaweza kuoa?” aliuliza Mahamud kwa sauti ambayo ilijaa urafiki, “ndiyo mzee nikipata kazi nitajitaidi nifanye kazi kwa juhudi huku anajiandaa kimaisha halafu naoa” alijibu Higgno kwa sauti tulivu iliyojaa hekima huku anamaliza kuingiza vocha kwenye simu, “unadhani ni vitu gani unahitaji kuandaa ili uweze kuoa” aliuliza Mahamud, akiwa anagesha gari pembeni ya msikiti, ambao kwa sasa ulionekana kuwa na watu kadhaa waliokuja kwa swala ya adhuhuri, wengi wao wakiwa ni wazee wa baraza la wazee, “ni sehemu nzuri ya kuishi, na uwezo wa kupata mahitaji muhimu ya familia” alijibu Higgno akicheka cheka na kumpatia mzee Mahamud simu yake, tayari alishaiweka vocha.
Baada kusikia jibu hilo bwana Mahamud akatulia kidogo kama vile anatafakari jambo juu ya kijana huyu, kisha akamtazama Higgno kwa macho makini sana, macho ambayo hata Higgno aliweza kuona umakini wake, “ok! sikia kijana, kuna jambo ambalo nililipanga siku ile uliponisaidia kule Msamala, sio kwamba nimelifikiria leo hii, na hili swala ni la mimi na wewe tu, sihitaji mtu mwingine ajuwe” alisema Mahamud huku anatazama kule walipo wenzake, ambao walikuwa wanachukuwa udhu (kujitakasa, kabla ya kuingia msikitini kwa swala) Higgno akimsikiliza kwa umakini sana, huku kifua kikijaa pumzi kwa hofu na shauku, “kijana nipo tayari kukupatia kila unacho hitaji, na nitakupatia zaidi ya unachohitaji, ukiachilia kazi ambayo uliniomba mwenyewe, pia nitakupatia nyumba, gari, fedha na biashara kubwa, kwaajili ya maisha yako, na mke wako, ambae ndie shariti langu kubwa” hapo Higgno akashtuka kidogo, ni kweli alikuwa anahitaji fedha nyumba gari na hata hiyo biashara, lakini kilichomtia shaka ni sharti ambalo bado hajaelezwa, japo aliambiwa lina muhusu binti wa tajiri huyo, sio yeye tu, vijana wengi wa hali yake ya kimaisha hawakuwa wanamfahamu binti huyo, na hawakuwahi kufahamu kama tajiri huyu ana binti.*******
Tayari mzee Frank alisha kutana na Soraya, na kuambatana nae kuelekea mjini kwaajili ya kufanya manunuzi ya duka lake jipya, huku Frank akiambatana na mke wake ambae alibeba chakula kwaajili ya mgonjwa wakimuacha Pale hospital akimueleza ward aliyo lazwa mzee Komba, na mzee Frank akiwa na Soraya na Laylah wakaelekea mjini ambako walimpatia fedha mzee Frank na kumkodia gari dogo la mizigo kwaajili ya kubebea vitu, “sasa binti yangu, umenifanyia mengi sana, na umeniomba niwe mshenga wachumba wako, mbona kijana mwenyewe simjui na wala sijawahi kumuona?” aliuliza mzee Frank, kabla ya kuondoka zake na kuanza manunuzi, Soraya alichekesha kidogo, “anakaa kule kule Luhila utakuwa unamfahamu, anaitwa Hig…. kabla hajamaliza kuongea Soraya alisita ghafla na kutazama pembeni ya barabara, akikodoa macho kwa mshangao kumtazama mwanamke mmoja mtu mzima aliekuwa anapita pembeni ya barabara, akionekana kuchoka na hali yake, tena mwingi wa mawazo, “Laylah unamuona yule mwanamke” aliuliza Soraya, na hapo sio Laylah peke yake alietazama, hata mzee Frank pia alitazama kule alikoonyesha Soraya, wakamuona yule mwanamke mtu mzima, akiwa anatembea taratibu akija usawa wa gari lao, “ndiyo nimemuona, ana nini kwani?” aliuliza Laylah, huku anageuka kumtazama Soraya ambae alimtazama mzee Frank, “samahani baba, nadhani tutawasiliana wewe unaweza kuendelea na shughuri zako za manunuzi, alisema Soraya akionyesha kuwa mwenye haraka sana, hapo mzee Frank hakuwa na lakufanya, kwasababu aliona kuwa ni mambo yasiyo muhusu, hivyo akaondoka zake na kumuacha Soraya anamtuma Laylah kwenda kumsimamisha yule mwanamke walio muona, “wa nini lakini, mbona mama wa watu kajichokea kwani unamfahamu?” aliuliza Laylah, huku akimtazama yule mwanamke ambae sasa alikuwa analivuka gari lao, “msimishe kwanza asiondoke” alisema Soraya kwa sauti ya ukali na hapo Laylah, akashuka toka kwenye gari, na kumfuata yule mwanamke, ambae tuna weza kumuona vizuri kuwa ni Sinamengi, “mama mama sahamani kidogo?” alisema Laylah, huku anamgusa begani Sinamengi, nae akageuka na kumtazama Laylah, “nani mimi?” aliuliza Sinamengi kwa mshangao, maana hakutegemea kusimamishwa na mschana mwenye hadhi ya huyu aliemsimisha, “ndiyo ni wew unaitwa na mdogo wangu yupo ndani ya gari lile pale” alisema Laylah huku akionyesha gari lao, yaani Land Rover Discovery.
Hapo moja kwa moja mwana mama Sina akapeleka mawazo yake kwenye kupata fedha za kujinunulia meno, ambayo yalikanywagwa na kijana Idd, “ok! twende zetu” alisema Sina, huku ana ongoza mwenyewe kueleka kwenye gari la Soraya.********
Mzee Mahamud akamtazama Higgno, anamuona yupo makini anamtazama akimsikiliza, “kijana nitakufanyia hayo yote endapo utakubali kumchumbia binti yangu, sijui unasemaje kijana?” aliuliza Mahamud akionyesha kuwa amesha maliza maongezi yake, hapo Higgno akatabasamu kidogo, yaani lile tabasamu la huzuni, tabasamu ambalo hata mzee Mahamud aliliona, kabla ya kuongea Higgno alishusha punzi ndefu, yaani ile ya uchovu na kuhemewa na mzigo mzito, “samahani sana mzee wangu, kikweli, nina mchumba tayari, japo tumekutana hivi karibu, lakini ni mchumba ambae kiukweli nime mpenda na yeye amenipenda, itakuwa vibaya sana nikiuumiza moyo wake kwakufanya jambo kama hilo, isitoshe mzee kwa kitendo hicho nitaonekana msaliti mbele ya binti yako, ambae atafikiria kuwa, endapo nitampata mschana mwingine ambae wazazi wake au yeye mwenye anafedha zaidi nitamuacha na kuishi nae, kwa kifupi nitakuwa sijatimiza mapenzi zaidi ya kutimiza tamaa zangu” alisema Higgno kwa sauti tulivu iliyojaa nidhamu.
Naam hapo Higgno aliweza kumuona Mahamud, akiwa ametazamisha kichwa chini kama anatafakari jambo, hapo Higgno akatulia kimya akisubiri kauli ya mzee Mahamud, huku akiwa amejwa na wasi wasi kuwa maneno yake yame mkera Mahamud na kusababisha yeye kupoteza kila kitu, yaani kazi na maelewano na mzee huyu.
Lakini Mzee Mahamud baada ya kutulia kwa sekunde kadhaa, akainua uso wake na kumtazam, ndipo Higgno alipotambua kuwa mzee Mhamud alikuwa anatabasamu, “kweli binti yangu amekosa kijana mwenye kila sifa ya kuwa mume, ok! nitakusaidia kupata kazi, utakuja kesho kutwa ofisini , labda kijana kama kuna kitu kingine ambacho utahitaji nikusaidie nje ya kukupatia kazi?” aliuliza Mahamud kwa sauti ya kirafiki kabisa, japo ilipooza kidogo, hapo kijana Higgno alitulia kidogo akiwaza na kutafakari juu ya nafasi aliyopewa na mzee Mahamud, “mzee mimi na maombi mawili toka kwako kama itakupendeza” alisema Higgno kwa sauti ile ile iliyojaa heshima, “usiwe na wasi wasi kijana, hata kama yangekuwa kumi we nieleze tu, naamini yatakuwa ndani ya uwezo wangu” alisema Mahamud akionekana wazi, alikuwa anamaanisha alichokisema, “mzee wangu, jambo la kwanza naomba usichukulie kama dharau kwa kile nilichosema juu ya kumchumbia binti yako, nadhani hata wewe unafahamu kuwa mimi ni kijana ambae sina lolote, na ni sawa na mtumishi wako, pengine hata kukaa na wewe kama hivi ni bahati kubwa kwangu….” alisema Higgno kabla Mahamud hajamkatiza, “kijana umeenda mbali sana, wala usiwe na shaka juu ya jilo ongea hilo swala jingine” alisema Mahamud, ambae alitegemea kwa kupambwa vile basi sasa unakuja mzinga (kuombwa fedha) kama ulivyo utaratibu watu wengine, hasa watu wake wa karibu hasa wanapokuwa shinda huwa wanaanza kwa kumpamba kwa maneno matamu, “la pili mzee wangu ninaomba msaada wako katika ushawishi wa wazazi wa mchumba wangu ili wasiniwekee kipingamizi chochote wakati wa kupeleka barua ya posa, nahofia wanaweza kunikatalia kutokana na hali yangu ya kipato” alisema Higgno kwa sauti iliyojaa unyonge, “kwanini umewaza hivyo kijana, kwani huyo binti ni mtoto wa nani?” aliuliza mzee Mahamud, akionyesha wazi kufadhaishwa na hali ya unyonge ya kijana huyu, ambae sio siri mpaka sasa hakuwa ameulizia jina lake, “mzee wangu kwa kweli hata wazazi wake siwajuwi, lakini nadhani nikiwajuwa na kukueleza lazima utawatambua, kwasababu ni…” kabla Higgno hajamaliza, tayari Mahamud alishadakia, “basi usiwe na wasi wasi, we kaongee na huyo mschana kisha utanijulisha, tena nikuhakikishie kuwa mimi nitakuwa mshenga wako na nitahakikisha hakuna kinacho haribika” alisema Mahamud, huku anatazama kule kwenye lango la kuingilia ndani ya msikiti ambapo walionekana watu wakiingia, “hooo! kijana hebu twende tuwahi swala, naona muda unaisha” alisema Mahamud, huku anafungua mlango wa gari nakuanza kushuka, “samahani mzee sijawahi kujifunza mafundisho ya dini ya kiislam mimi ni mkristu” alisema Higgno huku nae anafungua mlango na kushuka, hakuweza kuona mshangao wa wazi usoni kwa Mahamud, “hoo! samahani sana, kijana kumbe nimekuleta sehemu sio sahihi kwako” alisema Mzee Mahamud akipoteza ule mshangao wake kwa haraka sana, “hapana mzee wangu, sidhani kama kuna ubaya, maana kila dini inayohubiri amani, upendo, na kumcha mungu muumba, ni dini ya haki, hivyo hakuna ubaya, hata ingekuwa inawezekana ingekuwa ijumaa mtu anaingia msikitini na jumapili anaenda tena kanisani” alisema Higgno, na hapo Mahamud akamtazama Higgno, kwa namna fulani ya kumshangaa huku anatabasamu, “unakipaji kizuri sana kijana, kama ungekuwa mwalimu wa dini katika madrasa fulani basi ingekuwa faida kubwa sana kwa kizazi hiki, toka nimeanza kukuona mwaka jana umekuwa ni mtu wakushangaza kwa busara na wema wako” alisema Mahamud huku anatoa card ya biashara yani busness card, “mawasiliano ndiyo kitu pekee kilicho tutenganisha hapo mwanzo” alisema Mahamud kisha, wakaagana na kisha kila mmoja kutaka kuondoka lakini Mahamud akakumbuka jambo, “kijana, hebu subiri kidogo” alisema Mahamud, na kuanza kumfuata Higgno, ambae kwa kuona hivyo alirudi mbio kumfuata Mahamud, “nimesahau bwana” alisema Mahamud huku anaingiza mkono mfukoni na kutoa wallet yake, “chukuwa hii itakusaidia kwa mambo madogo madogo” alisema Mahamud huku anampatia noti kadhaa za elfu kumi kumi za idadi ya kumi na tano, “hapana mzee wangu nina akiba kidogo, inaweza kunifaa, nikiwa nashida nitakujulisha mzee wangu” alisema Higgno kwa unyenyekevu, huku anakutanisha viganja vya mikono yake na kuinamisha kichwa cheke, ikiwa ni ishara ya heshima kwa Mahamud, ambae sio tu kushangaa ila na kuduwaa pia, “ok! kijana wacha niwahi swala usiache kunitafuta,alisema Mahamud huku akigeuka na kuelekea msikitini, na Higgno akaelekea upande wa pili wa barabara na kuingia kwenye moja ya chochoro,, inayotumika kama njia ya mkato kuelekea soko kuu, huku kijana huyo akikumbuka kuwa anahitaji kumpigia simu baba yake ili ajuwe kama anakuja mjini au vipi.*******
Naam wakati huo wakina Idd, na baba yake walikuwa njiani wanaelekea msikitini kwa upande wa Idd sio kwamba alienda kwaajili ya swala, hapana Idd ambae mpaka mida hii alikuwa ameshalewa, akidai ni starter ya kuweza kumudu maongezi ya kwenye baraza la wazee, alikuwa anaenda mskitini kwaajili ya kushuhudia jinsi wanavyo kubaliwa kumchumbia Soraya, maana waliamini mtego waliouweka unge
saidia kutimiza hayo, hakika wawili hawa walikuwa na furaha ya hali ya juu, hata walipofika eneo la msikiti walikutana na wajumbe wengine wakiwa wamejaa kuliko siku zote, “hapa lazima Mahamud akubali haraka kutoa binti yake kwa maswali atayo tundikwa hapa, mwenyewe atakubali yaishe” alisema Mahadhi Salum, aliekuwa anaendesha gari, na sasa wanaingia eneo la msikiti, “mdingi mimi nakukubali kinyama, yaani hata wakati ule nilipo shuka bondeni (Africa ya kusini) ninge kushirikisha nadhani mpaka sasa tunge kuwa matajiri wakubwa sana hapa Songea” alisema Idd kwa sauti ya kilevi huku ana jitahidi isionekane kama amelewa, japo alikuwa anatafuna big G, yaani banzoka, lakini bado kwa mbali harufu ya pombe iliweza kusikika, “ila tukubaliane ukisha mchukuwa tu Soraya, kwanza unaninunulia gari moja zuri jipyaaaaa, halafu una…” kabla mahadhi hajaongea neno jingine, Idd akadakia mara moja, “hilo jibu baba, kwanza hujasikia kuwa yale mabus mapya yote Mahamud ana mkabidhi Soraya, amemfungulia kampuni yake, hivyo nitakuwa na mkwanja wa maana sana, baba utaoga fedha kama taka taka” alisema Idd kwa majisifu, huku baba yake anasimamisha gari mbele ya eneo la msikiti, ona kule mbele, alisema Mahadhi akimueleza Idd nae akatazama kule alikoonyesha na baba yake, wote wakamtazama mzee Mahamud ambae alikuwa anaagana na kijana fulani, kisha kila mmoja akaekelekea upande wake, yaani kijana akapotelea mtaani huku Mahamud akielekea kwenye kisima kwaajili ya kuchukuwa udhu, “ameisha pumbavu, unadhani hizo mali utazing’ang'ania peke yako mpaka lini” alisema Mahadhi wakiwa bado ndani ya gari, na wote wakacheka kwa pamoja, huku wakimtazama mzee Mahamud analifikia bomba na kuanza kuchukuwa udhu.******
Sina alipo lifikia gari tu! ghafla mlango wa gari ukafunguliwa, na hapo hapo akashangaa kumuona mwanamke alievalia niqab usoni mwake na kubakiza macho, lakini licha ya hayo lakini Sina aliweza kumkumbuka mschana huyu kuwa ni yule ambae alishirikiana na Idd kumuwekea dawa za kulevya kwenye Juice ili akabakwe, na bahati nzuri alikimbia, Sina mengi aligeuka haraka kutazama alikotoka……….. ITAENDELEA HII NI KWAAJILI YA MASHABIKI WA SIMBAAAA!!!