Clarence Seedorf
Senior Member
- Sep 29, 2019
- 174
- 1,884
Mambo yanazidi kuwa matam.
Shukran mkuu.Karibuni...
CC Litro Daudi Mchambuzi The Hurricane Jael brucella moneytalk saneneto Affet dluv FabreG ndulle Morgan Freeman unprejudiced Mshana Jr Heri Zabron Hamis kisukari totopack lanyese maubusu Minja Ngalason positive is normal Mine eyes popie Mr no bioto yona raphael Bigjahman nyakisese Tanayzer Shupavu Ngoheranga kilambon renason ADK Makandila9090 General Galadudu Said Cosmetics SnowBall binti mapozi kingkimwe BILLIONAIRE 2025 Badar_01 kanonb bweke undeceivable Marcie KigaKoyo Justine_Dannie sir ide Verifier dokta lu langoni makedonia Kudo Queen M jonoma Sangomwile Lovekid The Planner Mbobo Jenseny Shunie Rosicky Drizzle nabali Secret genius mkulima2 mkulungwa02 Breki ya Kenge EnnoMX Galbi Siratheboy irumba1 mjingamimi TAUNO KIDUDU orturoo Mavindozii Sky Eclat Vangigula seeker of knowledge PapaaSide bardizbah Nascent richard Mzimu wa Kolelo boscop kawoli song 16 Mjep asan njau Silencer Kimatu hambiliki mwanangu Sigara Kali The Wolf Melvine Royal Son Edward A chapa chichiboy1 Scofied EINSTEIN112 Oyaaa majomba mwera hao Katavi Semere92 tokenring ilu Wand Mtoto halali na hela dan oseko Jovet Panel Matumbwela saadatmontana Forgotten MAWAZO UJENZI Masking Agent Madame S Stephen Chelu bouy saleh Rukube Covid nineteen marybaby Mama mimi Mlume ndagu kinjeboy Lubebenamawe FabreG Zion jrGong Marley pirate Careem ndulle FabreG Tajiri mpole BETONY manumbu1 dluv saneneto aramika kiletza Shupavu nsharighe Kambaku Iammoshyn song 16 Affet unprejudiced Agent007 enjai ya kyasha Edward A chapa dendaboy Req pwiro aggyd brucella Lengutee nyakisese mtume wawatu mr chopa The Hurricane Puppy Restless mpwisa kikoozi Mirlz B Matthew ASA 1 ndulle Tanayzer sawima manji h kawoli
SanaaaInahuzunisha sana poti
uwiiiii ya lini hii asante mkuu vitu ni vyenyewe sana hiviSIHUSIKI - 4
ILIPOISHIA...
“Unawahi wapi na kesho huna wasilisho. Tuangalie mpira kidogo.”
“Hapana, ngoja nimalizie hii juisi niondoke. Hiyo siwezi kuinywa,” alisema na kushauri kwamba juisi ya boksi iliyoletwa ataichukua Eggy na kuinywa au kuigawa kwa sababu ilikuwa haijafunguliwa.
Wakati anapeleka mkono kuchukua juisi yake ili anywe mafunda mawili matatu kisha aondoke, kijana mmoja mlevi aliyekuwa akicheza pembeni mwa meza yao aliiangukia ile meza na kusababisha vinywaji vyote kumwagika.
ENDELEA...
Bruno alikuja juu na kumkwida shati yule kijana aliyekuwa akijitahidi kunyanyuka akimlazimisha kununua vinywaji vyao.
“Bahati mbaya father,” alisema kijana yule kwa sauti ya kilevilevi huku Bruno aliyekuwa na hasira akiendelea kumkwida na kumtaka Eggy ambaye alikuja haraka pale mezani amwite meneja wa baa.
“Huyo kijana ni mlevi tunamfahamu hapa. Pengine hapo keshalewa gongo huko mitaani ndipo akaja hapa. Ninamjua hana uwezo wa kununua hivi vinywaji lakini akiwa hajalewa ni mkarimu sana,” alisema Eggy akimsihi Bruno amwache kwa sababu atamuua bure. Jackson pia alimsihi amwache.
“Mkuu mimi nakuacha. Lakini ngoja niwanunulie bia mimi,” alisema Jackson huku akisimama.
“Hapana acha tu… Mimi bado kidogo. Hii ndiyo sebule yetu hapa Tanga,” alisema Bruno na kumsihi sana Jackson aendelee kukaa. Lakini alikataa akisema ataenda kumalizia dakika zilizobaki za mpira akiwa chumbani kwake
“Usiku mwema mkuu.”
“Hata hivyo, umejitahidi. Mpaka sasa bado uko hapa?” Alisema Bruno akiangalia saa yake. Ilikuwa inaelekea saa tano na robo usiku.
“Mpira ndio umenichelewesha… Haya kesho.”
“Sawa,” alijibu Bruno.
“Kaka naomba nikusindikize,” alisema Eggy akisimama.
“Binti, wewe bado uko kazini. Kaa na mkuu hapa utamsindikiza yeye.”
“Sasa hivi kazi zimepungua sana, hakuna wateja wapya wengi.”
“Ulikuwa unasemaje?”
“Ah, twende nikusindikize,” alisema Eggy akimshika mkono Jackson na kisha kuongozana naye.
Jackson alishangaa kumwona Andrew Mambo, Meneja Rasilimali Watu wa Tume akiwa pia ukumbini humo, mtu ambaye ndiye alitaka awe naye tangu alipowasili na siyo Bruno. Alikuwa ameketi na msichana mwingine, mmoja wa wahudumu wa klabu hiyo.
“Vipi Andrew sikujua uko hapa. Kwa nini leo umejitenga nami… Lakini nimeshaona sababu!”
“Ah! Nipo na nilikuona wakati unaingia. Bruno alipokuja dakika mbili hivi baada ya wewe kuingia akakuulizia nikamwambia sijui ulipo ingawa nilikuona ulipokwenda kukaa na ilikuwa nikufuate. Nikaona anakutafuta lakini hakukuona, akarudi tena hapa na kukaa. Amekaa hapa akinikera mara nikaona anaamka na kisha nikaona anahamia kwako baada ya kukuona. Nadhani mambo yamekwenda vyema kuona mahasimu mnakaa tena meza moja. Nikaamua kuwaacha. Bruno kwa kweli simpendi na alipotoka hapa nikashukuru. Hata jana alinikera sana alipolazimisha kuja kukaa na sisi.”
“Naona ameamua kubadilika. Nadhani hatuna sababu ya kumtenga kama anataka ushirikiano.”
“Bruno abadilike! Labda pombe tu au anaigiza…”
“Aisee tutaonana kesho,” aliaga Jackson na kuondoka huku Eggy aliyekuwa amesimama pembeni wakati akizungumza na Andrew akijiunga naye tena kutoka nje ya ukumbi huo. Baada ya kupiga hatua kadhaa, Jackson alimgeukia Eggy na kumwambia inaonekana jamaa waliyemwacha pale mezani kwa maana ya Bruno anamtaka. Akasema yeye hana kinyongo na kwamba anamshauri kwa moyo mmoja akaungane naye.
“Ah yule bwana hana nyimbo.”
“Kwa nini unasema hana nyimbo?”
“Anapenda sana wanawake huyo mzee. Hapa anatongoza kila msichana. Mimi sipendi watu wa aina hiyo. Napenda watu wastaarabu kama wewe. Na nikipata bwana wa kunioa wa aina yako hata pombe nitaacha.”
“Kwani unamfahamu huyo bwana?”
“Nimeanza tu kumwona siku mbili tatu hizi lakini hii si mara yake ya kwanza kuja hapa klabu. Mwezi uliopita alikuwepo hapa pia.”
Jackson alijua Eggy anasema kweli kwani kipindi hicho Bruno alikuwa Tanga akishiriki semina nyingine.
“Unataka kusema hujawahi kuondoka naye?”
“Wala simtaki.”
“Acha masihara. Humtaki kwa lipi?”
“Basi tu… Yaani kila mara alikuwa ananikonyeza niondoke naye lakini nimemnong’oneza kwamba nina mtu tayari lakini yeye anang’ang’ana tu. Nimekusindikiza makusudi ili aone picha.”
“Ah! Nakushauri uondoke naye tu wala hamna shida kabisa… Ehe! Ulikuwa unasemaje?”
“Kwani wewe una mtu mwingine?”
“Hapana. Nakwenda tu kulala ila nimechoka sana.”
“Mimi nakutaka wewe na kama umechoka nitakuchangamsha… Ninaomba uniachie shilingi elfu mbili tu kwa ajili ya bodaboda nitakapokuwa ninakuja chumbani kwako.”
“Kama nilivyosema nimechoka sana na hivyo huna sababu ya kuja. Halafu hapo Twiga kama ukiamua kuja, bodaboda ya nini? Mbona mimi ninakuja hapa kwa mguu na kurejea kwa mguu?”
“We’ mwanamume. Unaijua hii mitaa usiku? Vijana wa kihuni wanaweza kunibaka.”
“Sikiliza binti, kwa hayo mazingira magumu unayosema huna sababu kabisa ya kuja. Kwa heri,” alisema na kuanza kupiga hatua.
“Haya kaka.”
Kabla hajafika mbali, yule mlevi aliyeangukia meza alimsimamisha. Inaonekana alikuwa akimfuata kwa nyuma. Jackson alishituka kidogo akihisi amekuja kwa shari, labda ni mpenzi wa Eggy na hivyo anataka kumfanyia fujo.
“Braza nilikuwa nakufuata wewe. Nimekuokoa maisha miye. Nipe pesa ya bia tu,” alisema yule kijana.
Jackson hakumwelewa, sasa akahisi huyo mlevi anataka kumtapeli, akaendelea na safari yake lakini yeye alizidi kumfuata akimsemesha.
“Mimi pale sikuanguka braza, nilijiangusha tu kwa sababu niliona mtu anaweka kitu kwenye kinywaji chako. Wewe si ulikuwa unakunywa juisi halafu ukaondoka kidogo?”
Jackson aliona anamsumbua bure. Akashika mfukoni na kumpa noti ya shilingi elfu moja.
“Haya kaka, lakini ungejua nimekuokoa, ungenipa hata laki,” alisema yule kijana akikimbia kisogo chake kwani alishageuka kuondoka.
Jackson aliingia chumbani huku roho yake ikimuuma sana kwa kitendo chake cha kuwa karibu na yule msichana hadi kumkaribisha kwake. Alishukuru kwamba alimudu kumnyima pesa ya bodaboda na kumshauri asiende chumbani kwake.
“Bila shaka amenielewa kwamba simhitaji,” alijisemea huku akijaribu kuvaa viatu vya mkewe. Kwamba atajisikiaje siku akisikia kuna mtu anatembea na mkewe?
“Bila shaka nitajisikia vibaya sana. Vivyo hivyo na yeye ataumia sana akisikia mimi mumewe kipenzi ninatumia nafasi hii ya kuwa mbali naye kulala na mwanamke mwingine. Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe na shetani huyu aliyekuwa ananishawishi kuwa karibu na huyo msichana. Mwondoe kwangu, ashindwe na alegee,” alizidi kujisemea.
Aliwasha runinga kuendelea kuangalia mpira. Zilikuwa zimesalia dakika 15 na bado timu zilikuwa hazijafungana. Alivua nguo na kuvaa ya kulalia, akakaa kidogo kumwomba Mwenyezi Mungu kwa kumhifadhi mchana huo, kisha akajitupa kitandani akiendelea kuangalia mpira.
Endelea kufuatilia...
CC Litro the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater Bigjahman moneytalk marybaby nipo2 ram kisukari Smart911 Madame S carbamazepine Astelia culture gal Prisoner of hope Mine eyes kuku mweus Thad hearly Shunie Tumosa Mine eyes Kudo swahiba92 ludist Toyota escudo Clkey macson3 boga la kiangazi LEGE Smart911 Richard irakunda skfull popie Krizy Beat hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Mlenge Kacheda mjasiliamali Laki Si Pesa cocochanel kinusikwetu big jambo mludego Shupavu Kacheda mjasiliamali Mweweso Songa Heri esiankiki mnadhimu mkuu wa jf red apple the-sniper MR KUO dan oseko Jackal kuku mweus mtugani wa wapi huyo chiqutitta ndukulusudicho ADK aggyd BAHARI J
Hahahahahnina mashaka na uyu wakili wa jackson isiwe ameshanunuliwa
dah.........................................................................................................................SIHUSIKI - 19
View attachment 1474719
ILIPOISHIA...
"Simu kutoka kwa Kamanda wa Polisi Tanga? Kuhusu nini shemeji?"
"Ni masuala yetu tu haya ya unyanyasaji wa kijinsia. Kuna kesi fulani nimeanza kuifuatilia... Huyo baba Hellen yuko karibu hapo?" Kabla ya kujibu Andrew alijiuliza maswali kadhaa bila majibu na kusababisha Salome amuulize kulikoni amebaki kimya.
"Shemeji kuna mtu ananisemesha hapa na mimi nikawa namsemesha kwa ishara... Kuhusu baba Hellen kapata matatizo kidogo ndio maana nimekupigia."
"Matatizo? Kuna nini shemeji, mbona umenishitua hadi nasikia moyo ukinienda mbio."
"Usiwe na wasiwasi shemeji. Ni matatizo ya kawaida tu."
"Enhe, ni yapi shemeji."
"Aah ni kwamba, Malima amekamatwa na polisi."
"Amekamatwa na polisi? Kivipi?"
SASA ENDELEA...
"Sababu za kukamatwa kwake bado sijazifahamu kwa kweli. Hivi ninajiandaa kwenda polisi kumwona."
“Shemeji una hakika Baba Hallen amekamatwa?” Aliuliza tena.
“Ndiyo shemeji.”
"Yuko kituo gani?" Aliuliza baada ya kukaa kimya kwa muda.
"Central."
"Basi nikitoka hapa nitapitia huko kituoni. Asante kwa taarifa."
* * *
Andrew alitafuta eneo la kuegesha gari lake dogo baada ya kuwasili katika kituo kikuu cha polisi. Tangu ametoka ofisini njiani alikuwa anajiuliza maswali mengi kuhusu namna polisi walivyoweza kumfahamu Jackson na kumkamata. Sasa alihisi kwamba huenda katika hoteli aliyofikia Jackson kulikuwa na kamera za ulinzi (CCTV) zilizotumika na kuwawezesha kumkamata.
Alikumbuka jinsi Jackson alivyojitoa yeye na mkewe katika kuokoa ndoa yake baada ya mkewe kuanza kudai talaka kwa sababu ambazo hata hazikuwa na kichwa wala miguu. Aliona pia atumie muda huo kujadiliana na Jackson namna nzuri ya kukabiliana na mkewe ambaye aliahidi kuja kumtembelea polisi baada ya kuwasiliana na ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga kama alivyoahidi.
Baada ya kuacha gari mahala salama na kuingia katika jengo la polisi, aliomba kuonana na Jackson. Polisi wakamkubalia. Jackson alipojulishwa kwamba kuna mgeni anayeitwa Andrew Mambo alitaka kuonana naye, alimjibu askari kwamba hakuwa tayari kuonana naye. Wakati yule askari anageuka kuondoka, Jackson akamwita tena kwani aliona hakukuwa na sababu ya kutokutana naye na pengine huo ulikuwa wakati mwafaka wa kumweleza anavyomtuhumu kwa kumsaliti.
“Samahani ndugu kwa usumbufu. Mwambie tu aje kuniona,” alisema kwa upole.
"Karibu Mambo. Nini kimeendelea ofisini kwa sababu nimesikia bodi imemteua Mapunda."
"Nilitegemea niwe wa kwanza kukufikishia hizi habari ambazo zimewaudhi wafanyakazi wengi. Yaani kuna ambao morali ya kazi imewaisha hadi wakaamua kuondoka kazini kwa hasira."
"Lakini bila shaka kuna waliofurahia pia, hasa kukamatwa kwangu."
"Uvumi ulianza kuzagaa kwamba umekamatwa lakini nimejitahidi kuuzima.”
“Nashukuru kwa hilo lakini Mr Mambo, unadhani polisi wamekuja kunikamata hivi hivi tu? Labda kama walipiga ramli kwa mganga wa kienyeji! Huoni kama kuna mtu anayenisaliti na ambaye anaijua vyema hii issue?”
“Hata mimi njia nzima wakati ninakuja hapa nilikuwa ninajiuliza kuhusu hilo.”
“Lakini wanaojua suala hili ni mimi na wewe. Lazima mmoja wetu ndiye atakuwa kawaita polisi. Nasema uongo?”
"Haiwezekani iwe mimi au wewe. Nimepata hisia kwamba huenda katika nyumba hiyo ya wageni uliofikia kuna kamera za ulinzi, CCTV. Hukuona kitu kama hicho?"
"Andrew unaleta hadithi gani? Yaani kile kijigesti kiwe na kamera za aina hiyo? Anyway, kwa kujibu swali lako hakuna kitu kama hicho."
"Unajibu kwa hisia tu au kweli ulichunguza ukaona hakuna kamera hizo?"
"Sikujisumbua hata kuchunguza na ninaamini kwa asilimia mia moja kwamba hakuna kitu kama hicho. Labda tujaalie kwamba zilikuwepo, unadhani kama ndivyo ingekuwa haraka hivyo kunikamata. Yaani tukio linatokea Ijumaa halafu leo Jumanne nakamatwa. Huoni ni muda mfupi mno kwa polisi wetu kuweza kuchakata picha za kamera, kutafuta mtuhumiwa hadi kumkamata? Na kumbuka Jumamosi na Jumapili hazikuwa siku za kazi na kwa hiyo kama ni kazi wamefanya jana."
"Umejibu vyema kwamba hukuchunguza lakini kwa tukio kama lile polisi wanaweza kufanya kazi usiku na mchana hadi kumnasa wanayemtafuta. Tuseme wewe unatuhumu kwamba mimi ninaweza kuwa ndiye nimewajuza polisi kuhusu wewe?"
"Nisiwe mnafiki, kwa kweli ndivyo ninavyohisi kwa sababu kila nikiwaza na kuwazua sipati picha. Ni kweli polisi wangeweza kunikamata siku moja lakini si kwa haraka kiasi hicho. Katika nchi hii hatujafikia hapo."
"Mr Malima kweli umefikia hapo? Mimi? Unaweza kweli kunituhumu kukusaliti?"
"Katika mazingira kama haya unadhani ninaweza kumtuhumu nani? Yaani ninajuta hata kukushirikisha. Sijui umefanya hivi ili kunikomoa, kupata maslahi yoyote au kuna mtu unamtumikia. Isije ikawa umenunuliwa na Mapunda?"
"Baba Mchungaji, naomba uwe na hofu ya Mungu. Ninajua mtu ukikumbwa na janga kama hili unaweza kufikia hatua ya kutuhumu ovyoovyo. Ni sawa na mgonjwa anapougua kwa muda mrefu hufikia kuamini kila dawa anayoambiwa. Lakini ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba sijafanya hivyo na wala sitafanya. Nitaanzia wapi?"
"Andrew, naomba uniache niendelee na matatizo yangu kwa sababu ninaweza kusema jambo baya linaloweza kukuudhi zaidi."
"Lakini nilitaka pia kujua mipango yako ya kushughulikia hii kesi, na..."
"Nimesema ondoka tafadhali. Kama kuna anayekutuma kamwambie mwisho wangu umegota. Mmeshanifikisha hapa niache nipambane. Kama nitafungwa kwa kosa si langu ndio majaaliwa aliyoniandikia Mwenyezi Mungu lakini atanilipa siku ya kiama. Haya maisha ya duniani ni ya muda mfupi na yana ukomo. "
Andrew, akiwa amegubikwa na mshangao alibaki mdomo wazi.
* * *
Simu ya mezani kwake iliita Salome alipoipokea. Karani wa mapokezi alimjulisha kwamba ni simu kutoka Tanga aliyokuwa akiisubiri.
"Hapa ni ofisini kwa Mkuu wa Polisi Tanga. Nazungumza na Salome Bakunda wa mtandao wa kijinsia wa Mwanamke Lulu?" Sauti ya upande wa pili wa simu iliuliza.
"Yes, ndio mimi."
"Afande amerejea ofisini punde. Basi nakuunganisha naye ili akupe majibu ya maswali yako."
"Nitashukuru sana dada," alijibu Salome.
Baada ya sekunde chache alisikia sauti nzito ya Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tanga ikiita: "Hallow.
"Naye akajibu: "Hallow."
"Wewe ndiye ulitaka kujua zaidi kuhusu mkasa wa baamedi wa Tanga Raha Club?"
"Ndio."
"Mtuhumiwa, kama tulivyowaahidi wananchi tumeshamkamata tayari na bado anahojiwa. Tumemkamata leo jijini Dar es Salaam na hatua za awali zikikamilika ataletwa hapa Tanga."
"Kama nilivyowaambia awali taasisi yetu imedhamiria kutoa msaada wa kisheria kwa nyinyi polisi na mawakili wa Serikali na pia kusaidia kila hatua zikiwemo za upelelezi ili kuhakikisha haki inatendeka. Kwa hiyo nitakusumbua mara kwa mara kuhusu maendeleo ya shauri hili hadi hapo tutakapoona mahala tunakoweza kuingia ili kutoa mchango wetu. Na kwa vile umenithibitishia hilo kesho tutaandaa mkutano na waandishi wa habari. Tunataka umma wa Watanzania wajue kwamba sasa taasisi yetu haina utani na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia, mauaji ya vikongwe, ubakaji, ukeketaji na mengine kama hayo."
"Tunawashukuru sana kwa hilo na sisi tuko tayari kutoa ushirikiano kadiri itakavyowezekana. Nitakukabidhi kwa mtu rasmi atakayekuwa anashughulikia hili. Wasiliana nami kesho jioni."
"Nashukuru sana. Huyu mtuhumiwa ni nani na sasa yuko kituo gani hapa Dar es Salaam. Bila shaka atakuwa boyfriend wa zamani wa huyu binti."
"Sijui kama ni boyfriend wake wa zamani au mpya. Huyu bwana tumeambiwa na msiri wetu kwamba ni Mwanasheria wa Tume ya Teknolojia na Mawasiliano aliyekuwa semina hapa Tanga, anaitwa eh eh Jackson Jorwa Malima ni..."
"Umesema nani?"
"Anaitwa Jackson Jorwa Malima."Salome alishikwa na bumbuwazi na hajui namna simu ilivyomdondoka kutoka mkononi baada ya mapigo ya moyo kubadilika ghafla.
Kwa vile alikuwa ameanza kusumbuliwa na shinikizo la damu, aliambiwa na daktari akisikia hali kama hiyo atafune tembe za aspirin haraka.
Kwa vile alikuwa anatembea nazo, alizitoa kwenye pochi akazimung'unya kisha akajiegemeza kwenye meza.
Wakati akipambana na hali hiyo alisikia tena simu ya mezani ikiita lakini hakuwa na uwezo wa kuipokea. Alibaki amejiegemeza kwenye meza kwa muda wa dakika kumi hivi na taratibu akaanza kusikia mapigo ya moyo yanarejea katika hali yake ya kawaida.
Baada ya kutulia, alianza kujiuliza kama alichosikia kutoka kwa KPM wa Tanga ni sahihi kwa masikio yake au hakusikia vizuri.
Lakini akakumbuka kwamba Andrew alimpa taarifa za mumewe kukamatwa. Kutokana na Andrew kutomwambia sababu za kukamatwa kwake, wakati ule alihisi kwamba huenda alikamatwa kwa masuala ya kazi. Alihisi huenda kulitokea purukushani baina yake au wafuasi wa Bruno na wa kwake katika suala zima la nani akaimu ukurugenzi wa Tume na ndipo akakamatwa kwa sababu mumewe alikuwa amemdokeza kwamba suala hilo lingeweza kuleta kishindo TTM.
"Kumbe ni mume wangu ndiye mhusika mkuu? Yaani ndiye kamuua binti wa watu hivi hivi," alijiuliza mwanamke huyo huku machozi yakimbubujika kama maji bila kupata jibu. Alijiuliza kama mumewe na binti huyo walikuwa wakifahamiana kabla au la.
"Au ndiye baba wa mtoto wake... Na kwa nini akamuua?" Aliendelea kujiuliza. Alikumbuka usiku ule wa Jumamosi aliposikia habari hiyo ya mauaji ya msichana wa baa walipokuwa sebuleni na mumewe, kisha mumewe akabadilika ghafla hadi akalazimika kwenda kulala.
"Kumbe ndiyo maana akawa vile... Nitafanyaje sasa?" Alijiuliza na kujijibu kwamba angeendelea na harakati zake kwa sababu mumewe kama kweli ndiye mtuhumiwa, ni mhalifu kama wahalifu wengine na kwa mtazamo wake yeye alikuwa mhalifu mbaya zaidi wa kunyanyasa wanawake kutokana tu na jinsia zao.
"Nilimpenda sana mume wangu na nilitegemea kitutenganishe kifo kumbe Mungu amepanga vinginevyo. Siwezi kuendelea kuishi na mwanamume wa aina hii. Nitaishije na mwanamume malaya na muuaji? Hii maana yake ni kwamba hata mimi anaweza kuniua muda wowote akitaka. Itabidi sasa nichukulie kana kwamba nimefiwa na mume. Nijipange mimi na wanangu," alijisemea.
Kitu kilichomwongezea hasira ni kwamba kumbe mumewe alikuwa anamsaliti kwa kutembea na wanawake hadi mabaamedi. Alijihisi uzito kwenda tena kwa mumewe lakini akaona ni vyema aende akamsikilize na kumpasha kwamba katika suala hilo hatoangalia kama alikuwa mumewe bali kuhakikisha analipia makosa yake.
Kwa jinsi alivyokuwa amechanganyikiwa aliondoka bila kumuaga yeyote wala kufunga ofisi yake kwenda kituo kikuu cha polisi. Baada ya kutoka nje alitafuta usafiri wa magari ya kukodi ya Uber na baada ya muda wa dakika tatu hivi, gari dogo liliwasili, akapanda na kumwambia dereva ampeleke kituo kikuu cha polisi.
Wakati gari lile linazidi kusogea kwenye kituo kikuu cha polisi ndivyo hasira zilivyozidi kumsonga kooni. Aliporuhusiwa kuonana na mumewe kwa sekunde kadhaa walibaki wakiangaliana bila yeyote kusema chochote.
"Yaani nakuangalia hata sikumalizi. Hivi aibu hii nitaiweka wapi, yaani mtu mzima na akili zako, mtu na familia yako unakwenda kutembea na changudoa. Kama vile haitoshi unaamua… Unamnywesha sumu na kumuua?" Alianza kusema Salome huku machozi yakianza kumbubujika.
"Mke wangu mpenzi sihusiki na hili abadani..."
"Kwanza koma kabisa kuniita mkeo. Nani mkeo hapa…" Alimkata kauli. Akaendelea "Kama unajua una mke unakwendaje kutembea na msichana wa baa? Hivi ulimuua kwa nini? Wewe ndiye ulizaa naye mwanawe wa kwanza au ulisikia kakuambukiza Ukimwi ukaamua kumuua?" Aliendelea kulalamika huku akiendelea kufuta machozi.
Jackson alijilaumu tena kwa kumpa Andrew kazi ya kumjulisha mkewe kuhusu kukamatwa kwake. Ilionekana mkewe alikuwa na taarifa zote kuhusu kilichotokea. Alizidi kumlaani Andrew na kumchukia.
"Naomba unisikilize mke wangu nikueleze hatua kwa hatua kilichotokea..."
"Kwanza nimekwambia ukome kuniita mkeo. Mimi sina mume mshenzi kama wewe. Mimi ninaweza kuwa na mume malaya na muuaji. Haiwezekani. Kimsingi huna cha kuniambia kwa sababu habari zako nimeambiwa na chanzo ambacho hakina mashaka... Kwanza napoteza muda wangu kuongea na jitu katili, jitu malaya, jitu shenzi kama wewe."
Mwanamke huyo akihisi mapigo ya moyo yanataka kubadilika alisonya na kugeuka kuondoka.
"Mama Hellen mbona unanihukumu bila kunipa nafasi? Nisikilize."Alikiambia kisogo chake.
________________________________
Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu ninalazimika kuikatisha hadithi hii, kwani kitabu tayari kipo mtaani. Unaweza kujipatia nakala yako kwa Sh 12,000, kinapatikana kwa wauzaji mbalimbali au unaweza kuwasiliana moja kwa moja na mtunzi wa hadithi hii kwa simu namba 0758 143457.
View attachment 1474720
CC Litro Daudi Mchambuzi The Hurricane Jael brucella moneytalk saneneto Affet dluv FabreG ndulle Morgan Freeman unprejudiced Mshana Jr Heri Zabron Hamis kisukari totopack lanyese maubusu Minja Ngalason positive is normal Mine eyes popie Mr no bioto yona raphael Bigjahman nyakisese Tanayzer Shupavu Ngoheranga kilambon renason ADK Makandila9090 General Galadudu Said Cosmetics SnowBall binti mapozi kingkimwe BILLIONAIRE 2025 Badar_01 kanonb bweke undeceivable Marcie KigaKoyo Justine_Dannie sir ide Verifier dokta lu langoni makedonia Kudo Queen M jonoma Sangomwile Lovekid The Planner Mbobo Jenseny Shunie Rosicky Drizzle nabali Secret genius mkulima2 mkulungwa02 Breki ya Kenge EnnoMX Galbi Siratheboy irumba1 mjingamimi TAUNO KIDUDU orturoo Mavindozii Sky Eclat Vangigula seeker of knowledge PapaaSide bardizbah Nascent richard Mzimu wa Kolelo boscop kawoli song 16 Mjep asan njau Silencer Kimatu hambiliki mwanangu Sigara Kali The Wolf Melvine Royal Son Edward A chapa chichiboy1 Scofied EINSTEIN112 Oyaaa majomba mwera hao Katavi Semere92 tokenring ilu Wand Mtoto halali na hela dan oseko Jovet Panel Matumbwela saadatmontana Forgotten MAWAZO UJENZI Masking Agent Madame S Stephen Chelu bouy saleh Rukube Covid nineteen marybaby Mama mimi Mlume ndagu kinjeboy Lubebenamawe FabreG Zion jrGong Marley pirate Careem ndulle FabreG Tajiri mpole BETONY manumbu1 dluv saneneto aramika kiletza Shupavu nsharighe Kambaku Iammoshyn song 16 Affet unprejudiced Agent007 enjai ya kyasha Edward A chapa dendaboy Req pwiro aggyd brucella Lengutee nyakisese mtume wawatu mr chopa The Hurricane Puppy Restless mpwisa kikoozi Mirlz B Matthew ASA 1 ndulle Tanayzer sawima manji h kawoli
Piga simu au wasiliana kwa WhatsApp: 0758 143457, unaweza hata kuletewa mahali ulipo...Pamoja sana mkuu tuko pamoja sana unapatikana wapi? na endapo mtu yupo mbali nawe anakipataje hicho kitabu?
Usijali, jaribu kuwasiliana na mtunzi (Hamisi KIbari) kwa simu/WhatsApp: 0758 143457, nadhani anaweza kukutumia softcopy...bahati mbaya sana kwangu sitapata kuimaliza sababu niko nje ya tz
😞😞...dah.........................................................................................................................
Shukran!Piga simu au wasiliana kwa WhatsApp: 0758 143457, unaweza hata kuletewa mahali ulipo...
Nilijua tu wabongo bhanaAisee