Simulizi: Sihusiki

Simulizi: Sihusiki

SIHUSIKI - 11

ILIPOISHIA...

“Tulipomaliza kazi Eggy aliniaga kwamba amepata buzi anakwenda kulichuna. Mimi nilisepa zangu lakini huyo mwanaume hakuwahi hata kunitajia jina lake,” alisema na kuongeza kwamba anaamini hiyo ilikuwa ni siku ya kwanza kwa Agnes kuondoka na mwanaume huyo.

Alipoulizwa kama akimwona mwanaume huyo anaweza kumfahamu alijibu pengine anaweza kumtambua kwa sababu alimwona Agnes akiwa naye hadi walipokuwa wanakaribia kufunga huduma.

SASA ENDELEA...

Mariamu alipoulizwa kuhusu familia ya marehemu, akajibu: “Eggy ana mtoto mmoja anayelelewa na bibi yake. Hilo lilikuwa linamuuma sana marehemu na alikuwa keshajifunza ususi wa nywele akiwa mbioni kufungua saluni yake ili aachane na kazi ya baa. Alikuwa anasema kazi ya baa, licha ya kipato kuwa kidogo itamnyima muda wa kutosha wa kukaa na mwanawe endapo atamchukua. Ukiingia chumbani kwetu utadhani saluni kwani Eggy keshanunua takribani kila kitu kinachofaa kwa ajili ya saluni. Hata mabaamedi wote pale kazini tulishaacha kwenda saluni zingine. Yeye ndiye anatutengeneza nywele na alishakuwa mzuri sana katika hilo,” alisema Mariamu.

“Yaani wanaume! Huu ukatili wa kijinsia utakwisha lini?” Alisema Salome kwa hasira baada ya habari ile ya baamedi kumalizika na kuingia taarifa nyingine. Akaongeza “Yaani wanawake tunauliwa tu kama kuku pale mpenzi anapojisikia. Ni lazima tuzidishe elimu na vita dhidi ya mfumo dume.”

“Hizi tulizosikia ni tuhuma tu, hupaswi kuzichukulia kama kweli,” alidakia Jackson

“Tuhuma? Unasemaje ni tuhuma wakati kila kitu kiko wazi? Tena huyu mwanaume aliyekuwa na huyu binti wa watu anaonekana ni mhalifu mzoefu. Kampa sumu binti wa watu, kisha akanyofoa taarifa kwenye kitabu cha wageni. Kinachonisikitisha ni jinsi ambavyo huyu binti alivyokuwa na mipango mizuri ya kulea mwanawe lakini mwanaume mmoja mshenzi, kwa ukatili na ushetani wake anamuua hivi hivi tu. Dunia haiwezi kuendelea kulea vitu kama hivi,” alisema Salome akionekana mwenye hasira maneno yaliyomchoma sana Jackson. Alibaki kimya akitafakari.

Mkewe akazidi kuongea: “Kesho nitamwambia mkurugenzi wangu kuhusu hii kesi. Kama mhalifu atapatikana ofisi yetu itajitolea kutoa msaada wa kisheria mahakamani ili haki itendeke. Hii inaweza kuwa kazi yangu ya kwanza kama wakili kusimama mahakamani kumkaanga huyu mshenzi. Lazima huyu criminal alipie dhambi zake. Wanawake tumechoka.”

“Lakini unapandisha hasira bure kwa kusikia upande mmoja. Unaweza kusikia upande mwingine ukashangaa. Pengine huyo dada akawa kafa natural death.”’

“Hivi ulikuwa unasikiliza vizuri? Hapo imetajwa hadi sumu aliyowekewa na huyo mwanaume mshenzi… Yaani wanaume wote ni walewale tu. Na huyu mshenzi kama ulivyosikia alikuwa mwanasemina mwenzenu huko Tanga, isije hata ikawa mnatoka naye ofisi moja. Jumatatu ipeleke hii hoja ofisini kwenu,” alisema mkewe. Jackson alizidi kujisikia vibaya. Baada ya sekunde chache za ukimya, akanyanyuka kwenda chumbani.

Alijitupa kitandani na kujikuta katika mawazo makali. Alikumbuka jana yake Ijumaa alipokuwa kwenye basi, Andrew alipimpigia simu na kumjulisha tena kwamba askari na watu anaoamini wanatoka Twiga Executive Lodge walipita tena kwenye vyumba vya semina kwa kushitukiza kutafuta waliyekuwa wakimtafuta.

“Itakuwaje siku nikigundulika? Itakuwaje siku mke wangu akisikia kwamba mtu anayetuhumiwa kuua ni mimi. Hivi, mimi kama mwanasheria kwa nini nimejiweka katika mtego mbaya? Kwa nini sikutoa taarifa polisi baada ya kifo cha yule binti pengine tusingefika huku.”

Aliitwa kula chakula cha usiku na mwanawe Hellen, lakini akasema bado moyo unamwenda mbio na hana hamu ya kula. Tumbo lilikuwa limejaa ghafla na alikuwa hasikii hamu ya kula. Mkewe alimfuata na kumshauri waende hospitali kama anajisikia vibaya lakini alikataa.

Usiku huo usingizi wake ulikuwa mgumu sana kupatikana. Muda mwingi alibaki macho akiwaza na pale alipopata usingizi ndoto na jinamizi la Eggy lilikuwa likimtokea na kujikuta akishtuka ghafla huku jasho likimtoka hadi mkewe akamuuliza kulikoni.

* * *

Saa tatu na dakika 10 siku ya Jumanne, wajumbe wote kasoro wawili waliokuwa na udhuru walikuwa wameshawasili kwenye Ukumbi wa Bodi, ulioko katika ofisi za TTM.

Dakika tano baadaye, yaani saa tatu na robo, kikao cha dharura cha Bodi kilifunguliwa na Mwenyekiti wake, Profesa Aboubakar Mwinchumu kwa kuwashukuru wajumbe waliofika akisema kulikuwa na ajenda chache za kujadili na ambazo alisema anaamini isingechukua muda mrefu.

“Katibu wetu anayemaliza muda wake atakapotusomea muhtasari wa kikao kilichopita, tutakuwa na agenda kubwa moja, nayo ni ya kupitisha mtu atakayekaimu nafasi ya ukurugenzi wa Tume kabla Rais hajateua mkurugenzi mwingine. Na huyu tunayempitisha leo, kama mnavyojua ndiye atakuwa katibu wetu wa muda katika vikao vijavyo,” alisema Profesa Mwinchumu.

Akaendelea: “Sasa hivi ni saa tatu na dakika… inaelekea 16 hivi. Sitegemei kama saa tano itatukuta hatujamaliza hii ajenda na kuendelea na shughuli zetu zingine. Kama mambo yatakwenda kama ninavyotarajia huenda hata saa nne na nusu isitukute hapa.”

Aliendelea kusema kwamba mchana huo, saa sita kamili, wafanyakazi wote wa Tume hapo makao makuu wanatakiwa pia kukutana katika ukumbi huo huo kuagana na bosi wao, Matakwali na kutajiwa kaimu mkurugenzi wao.

“Wafanyakazi wameshatangaziwa hilo na hivyo ni muhimu sana sisi kikao hiki tukimalize mapema,” alisisitiza Mwenyekiti.

Alipomaliza kusema hayo alimkaribisha Mkurugenzi wa Tume, Ibrahim Matakwali, ambaye kwa nafasi yake alikuwa katibu wa bodi, kusoma muhtasari wa kikao kilichopita.

Siku hiyo ndiyo Matakwali alitazamiwa kustaafu rasmi kutokana na umri baada ya kutumikia Tume kwa miaka 18 akiwa Mkurugenzi mwanzilishi. Na hiyo ilikuwa ni baada ya kuongezewa miaka mitano na Rais ambayo sasa ilikuwa imekamilika. Yeye mwenyewe alikuwa ameshachoka kazi akitaka kuendeleza miradi yake binafsi bila kuongeza siku hata moja.

Kama kawaida, muhtasari huo ulisomwa, wajumbe wote wakaafiki kwamba yote yaliyosomwa ni sahihi. Mwenyekiti alipouliza kama kuna yatokanayo hakuna aliyenyoosha mkono. Wengi walikuwa wanataka kwenda kwenye ajenda kuu kisha waondoke zao.

Mwenyekiti alisimama na kumpongeza Mkurugenzi aliyekuwa akimaliza muda wake, akimwelezea kama mtu mwenye weledi, mwaminifu, mbunifu, mtiifu, mwadilifu na aliyeiongoza Tume kwa mafanikio na umahiri mkubwa.

“Kama mtakumbuka mwenzetu ilikuwa astaafu miaka mitano iliyopita lakini Rais akamwongezea muda kwa sababu ya kazi yake nzuri. Tumejaribu sana kumshawishi abaki hata kwa mwaka mmoja mwingine baada ya Rais kukubali pia lakini mwenzetu anasema ni vyema akalee wajukuu.

“Kwa hiyo hatuna namna nyingine isipokuwa kumwachia akapumzike. Alikoitoa Tume kama mkurugenzi mwanzilishi hadi sasa inafanya makubwa kwa kweli ataendelea kukumbukwa daima kwa mchango wake na utumishi uliotukuka,” alisema mwenyekiti wa bodi.

Baada ya maelezo hayo mafupi, mwenyekiti alimkaribisha Matakwali kuwaaga wajumbe wa bodi kabla ya kuingia kwenye ajenda ya kuchagua na kupitisha jina la mtu ambaye angekaimu nafasi yake.

Matakwali aliwashukuru wajumbe wa bodi kwa ushirikiano waliompa na maelekezo mazuri aliyokuwa akipata kutoka kwao ambayo alisema ndiyo hasa msingi wa kile kinachoonekana kama ni ufanisi wake.

Alikiri kwamba bodi ya sasa inayoongozwa na Profesa Mwinchumu ilikuwa ndio bodi bora na makini zaidi kuwahi kutokea kulinganisha na bodi zilizotangulia. Akasema ndio maana mwaka uliokuwa umepita, Rais alikuwa ameamua kuiacha yote na kuiongezea tena muda wa miaka mitano.

“Kwa umakini wenu huo, ninaamini pia mtapitisha mtu makini ambaye atakaimu ukurugenzi na kuongoza menejimenti kwa umahiri mkubwa pengine kuliko hata mimi. Mimi kwa kweli sikuwa ninajua kila kitu. Nilikuwa nina upungufu mwingi tu lakini niliwatumia vizuri wasaidizi wangu ambao wengine ninakiri kwamba wana uwezo mkubwa wa uongozi kuliko hata mimi,” alisema Mhandisi Matakwali.

Endelea kufuatilia...
 
SIHUSIKI - 12

Baada ya shukrani hizo aliketi na ndipo ajenda ya kuchagua jina la mtu atakayekaimu ukurugenzi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wajumbe wa bodi ikawadia. Mwenyekiti alirusha tena mpira kwa Matakwali akisema kwamba kwa vile yeye amekuwa mkurugenzi mwanzilishi na anawajua watu wake vizuri, ni vyema akamtaja mtu anayeona anafaa kukaimu nafasi yake na kama bodi itakubaliana naye basi itampitisha.

“Kwa bahati nzuri, katika kipindi hiki ambacho tumekuwa wajumbe wa hii bodi na kisha kuongezewa muda na Mheshimiwa Rais, tunawajua pia baadhi ya wasaidizi wako. Tunatazamia utatutajia jina ambalo kila mmoja wetu ataridhika nalo. Kama hatutaridhika nalo hatutakubali,” alisisitiza Mwenyekiti.

Matakwali aliposimama, akamtaja Jackson Malima, Mwanasheria Mkuu wa Tume, kwamba alikuwa na sifa zote, siyo tu za kukaimu, bali hata kuwa mkurugenzi kamili wa TTM.

“Ni mtu makini, mchapakazi, mwadilifu na mkweli na anayejifunza haraka sana. Yeye kitaaluma ni mwanasheria lakini huwezi kuamini, amejifunza haraka sana kivyake vyake teknolojia ya habari na mawasiliano na hivyo sasa anaweza kuwa mahiri kuliko hata baadhi ya wahandisi tulio nao hapa kwa nadharia.

Mimi huwa ninamwambia anatakiwa kwenda tu chuoni kupewa cheti siyo kusoma kwa sababu huwezi kumdanganya kitu. Niliwahi kupata dharura wakati nikitakiwa kuwasilisha mada kwenye moja ya semina muhimu huku mhandisi mwenzangu, Bruno Mapunda akiwa pia ana dharura, huwezi kuamini namna alivyoiwasilisha vizuri kwa niaba yangu pengine vizuri zaidi kuliko ambavyo mimi ningeliiwasilisha.

“Mwenyekiti amenisifia hapa kama mbunifu, basi huyu ndiye mbunifu halisi. Mengi ambayo ninasifiwa kwamba nimebuni na kuifanya Tume kila siku ionekane inapiga hatua ni ushauri wake kwangu kwa asilimia 70. Zilizobaki 30 ndizo ninazoshauriwa na watu wengine,” alisema.

Baada ya kusema hivyo aliketi na mwenyekiti akataka kusikia wajumbe wanasemaje kuhusu pendekezo hilo. Mjumbe wa kwanza alisimama na kutaka kukumbushwa ni mtu gani ambaye amekuwa mara kwa mara akikaimu nafasi ya ukurugenzi pale Matakwali anapokuwa hayupo, yaani pale anapokuwa yuko safari au likizo.

Matakwali alisimama na kujibu kwamba huko nyuma aliyekuwa akikaimu nafasi yake anapokuwa hayuko ofisini alikuwa Mhandisi Hassan Majura ambaye alihamishiwa wizarani na kwamba katika siku za karibuni aliyekuwa akikaimu zaidi ni Mhandisi Bruno Mapunda na kwamba Jackson Malima naye alishamkaimisha nafasi hiyo mara kadhaa.

Baada ya jibu hilo mjumbe huyo alisimama tena na kuhoji: “Kama Bwana Mapunda ndiye amekuwa akikaimu mara nyingi nafasi ya ukurugenzi, kwa nini asiendelee kukaimu wakati huu hadi hapo mkurugenzi mpya atakapoteuliwa na Mheshimiwa Rais, iwe ni yeye Mapunda, Malima au mtu mwingine kutoka nje ya TTM?”

Matakwali alisimama na kujibu kwamba amekuwa akimwachia Mapunda ofisi anapokuwa hayupo kwa sababu ya uwepo wake wa muda mrefu kwenye Tume na siyo uwezo.

“Naweza kusema hizo mara chache nilizomkaimisha Bwana Malima, alifanya vizuri zaidi,” alijibu Matakwali.

Mjumbe mwingine alisimama na kuzidi kumpinga Matakwali akimtaka Mapunda kwa madai kwamba kwa vile kampuni ile inahusiana na masuala ya teknolojia ya mawasiliano ilitakiwa mkurugenzi awe mwenye taaluma hiyo kwa maana ya Mhandisi Mapunda kama ilivyo kwa Matakwali kuliko kuweka mtu mwenye taaluma nyingine tofauti.

“Tumeambiwa hapa kwamba huyo anayependekezwa ni mwanasheria ingawa tumeambiwa pia kwamba masuala haya ya kiteknolojia pia anajifunza, lakini huyu hawezi kuwa sawa na mhandisi halisi kama Bw. Mapunda,” alisisitiza mjumbe huyo.

Matakwali alisimama tena kujibu hoja hiyo akisema kwamba uongozi wa Tume ulikuwa haumhitaji mtalaamu wa masuala ya teknolojia bali uwezo wa kuongoza, kutoa maelekezo sahihi, kubuni miradi, umakini, uchapakazi na uadilifu.

“Sisemi kwamba Bw. Mapunda hana sifa hizo, lakini kwa kuwalinganisha, Bw. Malima anafaa zaidi. Isitoshe, kama nilivyodokeza awali, Bw. Malima ni mtu wa kujifunza sana, humdanganyi kitu,” alisisitiza Matakwali.

Mjumbe mwingine alisimama na kusema yeye anaungana na wanaotaka nafasi hiyo ikaimiwe na Bruno kwa maelezo kwamba ana uzoefu kuliko Jackson.

“Siku zote uzoefu ni mwalimu mzuri sana. Nashangaa kwa nini tuache mzoefu, tena mhandisi kitaaluma, halafu tuchukue mtu asiye na uzoefu wa kutosha na ambaye taaluma yake siyo inayohusiana na core business ya Tume,” alifafanua mjumbe huyo.

Mjumbe mwingine tena alisimama na kuunga mkono Bruno ndiye akabidhiwe madaraka ya kukaimu akidai hoja za wale wanaoona kwamba anafaa yeye kupewa nafasi hiyo zina nguvu kuliko mkurugenzi anayestaafu kwa kumpendekeza Jackson kisha akataka ipigwe kura.

Huku akijua kwamba wajumbe wale, wengi wao kama si wote walikuwa bila shaka wameshanunuliwa na Bruno, Mwenyekiti alisimama na kusema hakukuwa na sababu za kupiga kura isipokuwa kuzingatia nguvu ya hoja.

“Tukubaliane kwamba kama kuna mtu anawajua vizuri watu hawa wawili ni Matakwali. Tukubaliane pia kwamba tuko hapa kwa sababu ya kushauri na kuhakikisha Tume inafanya vyema zaidi na siyo vinginevyo.”

Mwenyekiti akakohoa kidogo kusafisha koo lake, akaendelea: “Mkurugenzi amejitahidi sana kumwelezea vizuri Malima. Binafsi pia nimefanya utafiti wangu kwa siku mbili hizi kuona ni nani atatufaa na hivyo ninaungana na Mkurugenzi moja kwa moja kwa mapendekezo yake.

“Ngoja nisimung’unye maneno kwa kusema ukweli kwamba katika utafiti wangu unaonesha kwamba Mapunda si mwadilifu sana. Mimi amenitafuta sana ili nimuunge mkono katika hili lakini ninajua hafai. Na waswahili wanasema kweli kwamba kibaya chajitembeza lakini kizuri chajiuza.

“Isije ikawa pia kapitapita huko kwenu wajumbe wenzangu. Tuambizane tu ukweli kwa faida ya Tume. Rais ametubakiza hapa ili tuisaidie Tume na siyo vinginevyo… Naona makamu wangu naye anataka kusema kitu,” alisema akimwangalia makamu wake, Josiah Mafumu, aliyekuwa kanyoosha mkono.

Makamu huyo mwenyekiti aliposimama akaunga mkono mapendekezo ya Matakwali na ya Mwenyekiti akisema kulikuwa wala hakuna sababu ya kupiga kura kwani kinachotafutwa si uwakilishi wa watu bali kuangalia sifa ya anayefaa kuongoza Tume kwa muda kabla Rais hajafanya uteuzi wake.

“Profesa alijipa kibarua cha kuchunguza ni nani anaweza kuvaa viatu vya Mhandisi Matakwali katika kuipeleka mbele Tume na mimi pia nimefanya kazi hiyo. Nimehoji wafanyakazi bila wao kujua ninachokitafuta na mwisho wa yote nikagundua kwamba hata kama tulizoea kuona Bw. Mapunda akikaimu ofisi lakini katika hili si Mnyamwezi tunayemtafuta. Kwa sababu Waswahili wanasema mzigo mzito mpe Mnyamwezi basi ninawahakikishieni wajumbe wenzangu kwamba hapa Mnyamwezi anayeweza kubeba huu mzigo ni Malima.”

Endelea kufuatilia...
 
SIHUSIKI - 13

Jackson Malima alikuwa ofisini kwake akiendelea na kazi huku tukio la Tanga likiendelea kumsumbua kisaikolojia. Kilichomharibia siku yake mapema asubuhi hiyo ya Jumanne ni habari katika moja ya magazeti yaliyokuwa mezani kwake.

Alijilaumu hata ni kwa nini alikimbilia kusoma magazeti ya siku hiyo baada ya kuwekwa mezani kwake na mhudumu. Katika gazeti hilo kulikuwa na mwendelezo wa habari ya ‘Baamedi wa Tanga Raha Club’ aliyedaiwa kuuliwa na mpenzi wake kwa kunyweshwa sumu.

Ndani ya habari hiyo mwandishi aliwakariri polisi wakisema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kwamba wanakaribia kabisa kumkamata muuaji. Jackson alijiuliza sana kuhusu dhana ya sumu na dhana ya kukaribia kumkamata muuaji zilimaanisha nini.

Kwanza hakuamini tuhuma za sumu. Alihisi kwamba ama polisi wanadanganya au daktari aliyemfanyia uchunguzi hakupima sawasawa. Yeye aliamini kwamba Eggy aliumwa ghafla. Alijilaumu sana kwa nini hakuchukua hatua haraka ya kumkimbiza hospitali pale msichana huyo alipoanza kulalamikia tumbo.

Wakati akiendelea kutafakari tukio hilo lililomwachia maswali mengi, Andrew Mambo aliingia ofisini kwake na mara moja aligundua kwamba Jackson hakuwa sawa.

“Vipi Malima, unaumwa au bado unasumbuliwa na tukio la yule binti?” Aliuliza Andrew.

“Kwa nini unasema hivyo?” Jackson naye aliachia swali.

“Ninakuona tu. Uso wako hauna bashasha. Yaani mtu yeyote anayekufahamu akiingia hapa ofisini kwako anajua hauko sawa,” Andrew alimfafanulia vizuri huku akimtazama.

“Kwa kweli ndugu yangu, tukio la kifo cha yule msichana linanikosesha raha sana. Yaani ninajiona kama muuaji. Laiti ningelimwahisha hospitali, haya yote yasingetokea. Nina hakika yule binti alikuwa anaumwa lakini nashangaa wanavyosema alinyweshwa sumu,” alisema Jackson akimsukumia gazeti.

“Nitaisoma hiyo habari baadaye lakini nimekuja kukupa nyepesi nyepesi kwamba kikao cha bodi kinaendelea na makamu mwenyekiti amenijulisha mapema asubuhi hii kwamba Mapunda keshahonga wajumbe karibu wote ili wampitishe.”

“Mimi sioni shida kama wakimpitisha, lakini ninachoomba ni awe mwepesi tu kupokea ushauri wowote mzuri kutoka kwetu kwa ajili ya maendeleo ya Tume, basi,” alisema Jackson.

“Hiyo ndio shida kubwa ya Mapunda. Huwa anadhani kwamba anajua kila kitu. Yaani kumkabidhi Mapunda kuendesha taasisi ni sawa kumkabidhi fisi mwenye njaa akulindiye ndama. Ni fisadi, hasidi na mtu mwenye roho mbaya kweli kweli. Ninajua hata wafanyakazi wengi watasikitika sana akipewa yeye uongozi wa Tume.”

“Ninajua hilo… Lakini makamu mwenyekiti kakuambia yeye anaonaje?”

“Ameniambia kwamba wameshaweka msimamo na mwenyekiti kwamba hawawezi kukubali kumpitisha Bruno.”

“Kama wajumbe wengi watamtaka Bruno, wataweza kuzuia?” Kabla Andrew hajajibu swali lile, askari wawili wakiwa wamevaa sare za polisi waliingia ofisini pale.

“Hamjambo mabwana?” Alisalimia mmoja wao.

“Hatujambo,” alijibu Jackson akishangaa askari wale walipitaje mapokezi hadi ofisini kwake bila hata kupigiwa simu na karani wa mapokezi. Huo haukuwa utaratibu wa kawaida.

“Tuwasaidie nini ndugu?” Akauliza Jackson.

“Bila shaka wewe ndiye Jackson Jorwa Malima?” Aliuliza askari mmoja wapo akimwelekea Jackson aliyekuwa amekaa kwenye kiti rasmi ofisini humo.

“Ndio mimi, niwasaidie nini?” Alijibu huku moyo wake ukimlipuka. Akakumbuka habari ya kwenye gazeti ambayo Kamanda wa polisi alikaririwa akisema wanakaribia kabisa kumkata muuaji.

“Sisi ni askari polisi… Kuanzia sasa uko chini ya ulinzi. Unahitajika kituoni,” alisema mmoja wao.

“Ninaweza kuona vitambulisho vyenu?”

“Kwani haya mavazi hayakutoshi?” Alihoji askari yule kwa hasira.

“Ndio, wakati mwingine hata majambazi wanavaa sare,” Jackson alijitahidi kujibu kwa upole huku hofu ikizidi kutanda moyoni mwake. Yule askari alitoa kitambulisho na kuonesha.

“Haya, kosa langu ni nini?”

“Utajua mbele.”

“Yaani hata katika zama hizi bado kuna askari wanakamata watu bila kuwaambia makosa yao? Tafadhali nijulisheni kosa langu. Hiyo ni haki yangu,” alijibu kwa upole Jackson.

“Inaonekana unajifanya mjuaji… Haya unatuhumiwa kumuua changudoa Tanga. Nadhani unajua,” alijibu.

“Kwa hiyo mnataka nini kwa sababu hilo unalosema sihusiki?”

“Tunakuheshimu ndugu. Tumeshakwambia uko chini ya ulinzi na umetaka tukuambie kosa. Sasa tunakuomba unyanyuke twende kituoni.”

Wakati akinyanyuka kwa sababu hakutaka kufanya ubishi, Jackson alikuwa anajiuliza haraka haraka ni nini hasa kiliwaongoza askari hao kuja kwake. Wale askari walitaka kumtia pingu baada ya kunyanyuka lakini akawaomba wamwache.

“Ndugu zangu, mmesema ninyanyuke, nimenyanyuka. Sasa kupigana pingu kwa sababu gani tena?” Alihoji Jackson. Andrew naye akaamua kuingilia kati akisema anaamini wamekuja kumkamata kama walivyodai na si kumfedhehesha.

“Huyu ni mtu anayejiheshimu na siyo kibaka. Chonde ninawaomba mabwana acheni kumfunga pingu,” alisema na wale askari wakaamua kumwacha bila kumtia pingu.

“Andrew, nadhani umeshuhudia kila kitu, basi utatoa taarifa kwa wengine kwamba nimekamatwa. Sipendi niwe wa kwanza kumjulisha mke wangu kuhusu hili. Naomba umjulishe wewe,” alisema kisha akamtajia namba za simu za mke wake baada ya Andrew kusema alizipoteza baada ya simu yake ya awali kuharibika na kununua simu mpya na hivyo kupoteza namba nyingi ikiwemo ya Mama Hellen.

* * *

Salome Bakunda au Salome Malima kama alivyojulikana zaidi kazini kwake kutokana na jina la mumewe huku wengine wakimwita Mama Malima na mtani kwake wakimwita Mama Hellen, alimaliza kusoma habari ya mauaji ya baamedi wa Tanga Raha Club na kuzidi kupata hasira.

Alishukuru gazeti hilo kumkumbusha habari ambayo mpaka anafika ofisini siku hiyo ya Jumanne alikuwa hajaanza kuandaa mpango kazi wa namna ya kushughulikia tukio hilo. Sasa alidhamiria kuacha shughuli zake za siku hiyo alizokuwa anafanya ili kwanza kujikita katika suala hilo na hatimaye kumshawishi bosi wake ili ofisi yao ianze kulifuatilia mara moja.

Alipomfikiria mtoto wa marehemu, aliwakumbuka pia wanawe. Akajiuliza ingekuwaje ni yeye ndiye kauawa na kuwaacha wanawe bila mama. Maelezo ya binti aliyekuwa akiishi na marehemu ndio yaliyomtia huzuni zaidi na hasira kila alipofikiria namna ndoto za Agnes zilivyokatishwa kinyama na mwanaume aliyemuua kwa sumu.

“Mshenzi mmoja anakatisha maisha ya binti wa watu aliyekuwa na ndoto nyingi za maisha kwa sababu tu yeye ni mwanaume. Anasababisha mtoto wa marehemu ambaye mama yake alianza kujiandaa kuboresha maisha yake kuendelea kulelewa na bibi ambaye pia pengine anatakiwa kulelewa… ni mbaya sana,” alijisemea.

Kutokana na gazeti alilosoma kuonesha kwamba ulikuwa ni mwendelezo wa habari ya jana yake, aliona umuhimu wa kutafuta gazeti la Jumatatu ili kujua mengi zaidi kuhusu mkasa huo. Salome alimpigia wakala wa magazeti akimuuliza kama anaweza kupata gazeti lolote la Jumatatu lililokuwa na mkasa wa baamedi wa Tanga Raha Club kwa kina.

“Mama, ungechelewa kidogo tu usingelipata kwa sababu ndio nilikuwa ninapanga kurejesha mabaki ya magazeti ya jana,” alisema wakala huyo wa magazeti aliyekuwa akiwaletea nakala za baadhi ya magazeti ofisini kwao.

Kwa kuwa ofisi yao haikuwa mbali sana na mahala wakala huyo alikokuwa akifanyia shughuli zake za kusambaza magazeti, maeneo ya Kariakoo, baada ya dakika kumi Salome alikuwa anakabidhiwa gazeti alilokuwa akilihitaji.

Alikuwa anataka kuchukua maelezo zaidi ili apate pa kuanzia kwa sababu alidhamiria ofisi yao ifuatilie kwa karibu suala hilo hadi mwisho na kutoa msaada wa kisheria utakaohitajika ili kuhakikisha kwamba mhusika wa mauaji hayo analipia uhalifu wake.

Endelea kufuatilia...
 
SIHUSIKI - 14

Kitu kizuri ni kwamba mfadhili wa asasi yao ya kiraia alikuwa ameshatoa fedha za kutosha kwa ajili ya masuala ya aina hiyo na hakukuwa na sababu yoyote ambayo ingekwamisha taasisi yao kushindwa kufuatilia. Baada ya kusoma magazeti yote mawili, alichukua daftari lake dogo na kuanza kuandika mambo muhimu kuhusu sakata hilo.

Aliandika jina la msichana aliyeuawa kwa sumu, umri wake, klabu aliyokuwa akifanya kazi, sumu inayodaiwa kumuua ambayo kwa mujibu wa habari alizosoma ilionekana pia kwenye chupa ya bia iliyokutwa chumbani alimokuwa na jina la nyumba ya kulala wageni alimofia.

Alichukua pia majina ya watu ambao wanaweza kuwa mashahidi muhimu katika kesi hiyo ambao ni pamoja na mlinzi katika nyumba ya wageni alimofia Agnes, mhudumu wa mapokezi, rafiki aliyekuwa akiishi na marehemu pamoja na meneja wa klabu ya Tanga Raha.

Maswali ambayo yalitakiwa kujibiwa ni nani alifanya uhalifu huo na sababu za kufanya hivyo. Ingawa sababu zilikuwa hazijatajwa lakini kutokana na uzoefu wake, kwa asilimia zaidi ya 70 alihisi zitakuwa zinatokana na masuala ya mapenzi.

Alihisi kwamba huenda mwanaume aliyekuwa na baamedi huyo ni mpenzi wake wa siku nyingi na huenda alitaka kumbinafsisha lakini msichana huyo mrembo ambaye picha yake ilikuwa kwenye gazeti akawa mgumu kukubaliana naye. Alihisi pia kwamba huenda mwanaume aliyemuua ndiye alizaa naye mtoto wake wa kwanza na pengine alitaka warejeane lakini msichana huyo akawa hataki.

“Kama waandishi hawa wangekuwa makini wangelimtafuta huyu baba wa mtoto wake au pengine wanamtafuta. Anaweza kuwasaidia,” alijisemea.

Ofisi yao ilikuwa pia imewahi kushughulikia matukio ya akina dada kuuawa na watu waliozaa nao au wapenzi wao wa zamani waliokuwa wanalazimisha kuwaoa au kuwamiliki tena bila mafanikio na ndio maana akapata hisia hizo.

Lakini pia miongoni mwa kesi walizowahi kuzifuatilia ni za mtu mmoja ambaye alikuwa akichukizwa na uwepo wa machangudoa mitaani. Mtu huyo akadhamiria kuwamaliza kwa kuwaua ambapo alikuwa anawachukua kama mteja na kwenda nao kwenye nyumba za kulala wageni ambako aliwaua kwa kuwanyonga, wengine kwa sumu na wengine kuwachoma visu kutegemea na mazingira. Mtu huyo kila alipokuwa akiua aliacha ujumbe usemao ‘Makahaba mjiandae’. Hata hivyo, mtu huyo aliwekewa mtego na kukamatwa akijiandaa kuua msichana wa saba.

Jambo moja lililokuwa limemtia faraja Salome katika gazeti la siku hiyo ni kauli ya Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Tanga kwamba jeshi lake linakaribia kabisa kumnasa muuaji. Lakini pia alihisi hayo yanaweza kuwa maneno tu ya kuwatia moyo wasomaji na wananchi ili walione jeshi kwamba liko kazini na siku ipite!

Baada ya kuandika mambo muhimu kuhusu kesi hiyo, Salome alinyanyuka kuelekea ofisini kwa bosi wake, Dk. Jumanne Marijani. Huyu udaktari wake haukuwa wa uzamivu (PhD) bali udaktari bingwa wa tiba za binadamu, hususani magonjwa ya akina mama.

Alimkuta pia akisoma gazeti na Salome alihisi bila shaka atakuwa anasoma habari hiyo hiyo ya baamedi wa Tanga Raha Club. Kutokana na shughuli zao zilizojielekeza katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia wanaofanyiwa akina mama na watoto, kila aliyekuwa akishika gazeti anaanza kwanza kutafuta habari za aina hiyo kabla hata ya kusoma habari inayoongoza kwa siku hiyo.

“Bosi, bila shaka unasoma habari ya mauaji ya msichana wa Tanga,” aliuliza Salome baada ya kumjulia hali bosi wake ambaye walikuwa hawajakutana asubuhi hiyo.

“Ndio. Salome, inasikitisha sana. Ninaifuatilia tangu Jumamosi nilipoiona ikitangazwa kwenye vyombo vya habari,” alijibu Dk. Marijani.

“Kilichonileta ni habari hiyo hiyo. Jana nilitingwa na shughuli nikasahau kuizungumzia. Ninataka tuifuatilie kwa karibu na huyu mtuhumiwa atakapokamatwa tuongeze nguvu za kisheria. Ninataka ikiwezekana hii iwe kesi yangu ya kwanza kusimama mahakamani kama wakili wa marehemu na kwa mantiki hiyo kusaidiana na Serikali ili kukomesha haya mauaji. Ninataka huyu mwanaume aliyefanya haya tumshikishe adabu,” alisema Salome aliyekuwa akiongea kwa hisia kali akijitahidi kuzuia machozi.

“Bila shaka Mama Malima. Hata wakati ninasoma hii habari nilikuwa ninafikiria wapi sisi tunaweza kuingilia ili kutoa mchango wetu katika kukomesha mauaji ya wasichana wasio na hatia,” alisema.

“Ninashukuru bosi kwa hilo. Kwa hiyo mimi ninaanza kufuatilia. Nataka kuwasiliana na Kamanda wa Polisi wa Tanga kujua maendeleo ya hii kesi na kisha nimweleze nia yetu ya kulisaidia Jeshi la Polisi.”

“Utaniandalia tu mpango kazi wako na bajeti. Kama utataka kusafiri kwenda Tanga utaonesha kwenye mpango kazi wako. Lakini nadhani mpango mzima utaanza baada ya mtuhumiwa kukamatwa na hapa nimeona askari wakijigamba kwamba wanakaribia kumkamata.”

“Ndio Bosi. Ndio maana nimesema nataka kuwasiliana na polisi Tanga.”

“Ninakutakia kila heri Mama Malima. Kama kesi hii utaisimamia vyema hadi mwisho kwa kushirikiana na mawakili wa Serikali na mhusika kupewa adhabu anayostahili, wafadhili wetu watafurahi sana. Usisahau kuwashirikisha waandishi wa habari hasa wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake kwa kila hatua utakayochukua.”

“Sawa bosi.”

* * *

Wakati vuta nikuvute ikiendelea ndani ya kikao cha Bodi huku wajumbe wakikubali kwa shingo upande msisitizo wa mwenyekiti kwamba mtu atakayevaa viatu vya Matakwali ni Jackson Malima, karani wa Matakwali aliingia kwenye chumba cha mkutano ghafla na kumfuata mezani alikokuwa amekaa bosi wake.

Alipofika akamnong’oneza kwamba Jackson alikuwa amekamatwa muda ule na polisi. “Wameshuka naye sasa hivi na pengine watakuwa getini,” alisema karani yule.

“Inakuwaje mtu anakuja kukamatwa hapa ofisini bila mimi kutaarifiwa?” Alihoji kwa hamaki Matakwali.

“Walianzia ofisini kwa bosi Mapunda. Nadhani bosi Mapunda, aliona kwa kuwa upo kwenye kikao kizito ndio akaamuru waendelee na kazi yao. Ndiye pia kanituma nikuletee huu ujumbe,” alijibu yule karani.

“Kama hao askari hawajaondoka naye kawaambie wanisuburi. Fanya haraka. Ondoka,” alisema Matakwali aliyeonekana kushitushwa na habari hizo. Wakati karani anaondoka, Matakwali alisimama na kuwaambia wajumbe wa bodi alichoambiwa na karani wake.

“Tafadhali mnisubiri mara moja niongee na hawa askari, ninakuja mara moja,” alisema Matakwali akinyanyuka na kutoka haraka.

Alishuka ngazi kutoka ghorofa ya tatu walikokuwa kwenye ukumbi wa mikutano kueleka chini haraka na kukuta askari wale wakiomba wafunguliwe geti waondoke kwa sababu walikuwa hawana sababu ya kusubiri mtu huku karani aliyetumwa na Matakwali akiwaambia askari wa getini wasifungue kwanza hadi Mkurugenzi afike.

Matakwali alipofika alikwenda hadi kwenye gari lao na kuwasalimia kisha akajitambulisha. “Ndugu zangu, mnafika kwa mtu, mnachukua familia yake bila kujitambulisha kwake?” Alihoji.

“Kuna bosi mmoja alishatupokea na kutupa baraka zote. Isitoshe sisi tukija kukamata mhalifu si lazima tupate ruhusa ya mtu,” alijibu mmoja wao mwenye cheo cha sajini.

“Haya niambieni, mmemkamata ofisa wangu mwandamizi kwa kosa gani?”

“Mtuhimiwa anajua lakini kwa faida yako ni kwamba kaua baamedi aliyekuwa naye gesti kule Tanga Ijumaa iliyopita.”

Usikose kufuatilia mkasa huu wa kusikitisha...
 
Karibuni...

CC Litro Daudi Mchambuzi The Hurricane Jael brucella moneytalk saneneto Affet dluv FabreG ndulle Morgan Freeman unprejudiced Mshana Jr Heri Zabron Hamis kisukari totopack lanyese maubusu Minja Ngalason positive is normal Mine eyes popie Mr no bioto yona raphael Bigjahman nyakisese Tanayzer Shupavu Ngoheranga kilambon renason ADK Makandila9090 General Galadudu Said Cosmetics SnowBall binti mapozi kingkimwe BILLIONAIRE 2025 Badar_01 kanonb bweke undeceivable Marcie KigaKoyo Justine_Dannie sir ide Verifier dokta lu langoni makedonia Kudo Queen M jonoma Sangomwile Lovekid The Planner Mbobo Jenseny Shunie Rosicky Drizzle nabali Secret genius mkulima2 mkulungwa02 Breki ya Kenge EnnoMX Galbi Siratheboy irumba1 mjingamimi TAUNO KIDUDU orturoo Mavindozii Sky Eclat Vangigula seeker of knowledge PapaaSide bardizbah Nascent richard Mzimu wa Kolelo boscop kawoli song 16 Mjep asan njau Silencer Kimatu hambiliki mwanangu Sigara Kali The Wolf Melvine Royal Son Edward A chapa chichiboy1 Scofied EINSTEIN112 Oyaaa majomba mwera hao Katavi Semere92 tokenring ilu Wand Mtoto halali na hela dan oseko Jovet Panel Matumbwela saadatmontana Forgotten MAWAZO UJENZI Masking Agent Madame S Stephen Chelu bouy saleh Rukube Covid nineteen marybaby Mama mimi Mlume ndagu kinjeboy Lubebenamawe FabreG Zion jrGong Marley pirate Careem ndulle FabreG Tajiri mpole BETONY manumbu1 dluv saneneto aramika kiletza Shupavu nsharighe Kambaku Iammoshyn song 16 Affet unprejudiced Agent007 enjai ya kyasha Edward A chapa dendaboy Req pwiro aggyd brucella Lengutee nyakisese mtume wawatu mr chopa The Hurricane Puppy Restless mpwisa kikoozi Mirlz B Matthew ASA 1 ndulle Tanayzer sawima manji h kawoli
 
Shukran mkuu.
 
Naona sijasahaulika
 
Dahhh siri inataka kuvuja sasa
SIHUSIKI - 14

Kitu kizuri ni kwamba mfadhili wa asasi yao ya kiraia alikuwa ameshatoa fedha za kutosha kwa ajili ya masuala ya aina hiyo na hakukuwa na sababu yoyote ambayo ingekwamisha taasisi yao kushindwa kufuatilia. Baada ya kusoma magazeti yote mawili, alichukua daftari lake dogo na kuanza kuandika mambo muhimu kuhusu sakata hilo.

Aliandika jina la msichana aliyeuawa kwa sumu, umri wake, klabu aliyokuwa akifanya kazi, sumu inayodaiwa kumuua ambayo kwa mujibu wa habari alizosoma ilionekana pia kwenye chupa ya bia iliyokutwa chumbani alimokuwa na jina la nyumba ya kulala wageni alimofia.

Alichukua pia majina ya watu ambao wanaweza kuwa mashahidi muhimu katika kesi hiyo ambao ni pamoja na mlinzi katika nyumba ya wageni alimofia Agnes, mhudumu wa mapokezi, rafiki aliyekuwa akiishi na marehemu pamoja na meneja wa klabu ya Tanga Raha.

Maswali ambayo yalitakiwa kujibiwa ni nani alifanya uhalifu huo na sababu za kufanya hivyo. Ingawa sababu zilikuwa hazijatajwa lakini kutokana na uzoefu wake, kwa asilimia zaidi ya 70 alihisi zitakuwa zinatokana na masuala ya mapenzi.

Alihisi kwamba huenda mwanaume aliyekuwa na baamedi huyo ni mpenzi wake wa siku nyingi na huenda alitaka kumbinafsisha lakini msichana huyo mrembo ambaye picha yake ilikuwa kwenye gazeti akawa mgumu kukubaliana naye. Alihisi pia kwamba huenda mwanaume aliyemuua ndiye alizaa naye mtoto wake wa kwanza na pengine alitaka warejeane lakini msichana huyo akawa hataki.

“Kama waandishi hawa wangekuwa makini wangelimtafuta huyu baba wa mtoto wake au pengine wanamtafuta. Anaweza kuwasaidia,” alijisemea.

Ofisi yao ilikuwa pia imewahi kushughulikia matukio ya akina dada kuuawa na watu waliozaa nao au wapenzi wao wa zamani waliokuwa wanalazimisha kuwaoa au kuwamiliki tena bila mafanikio na ndio maana akapata hisia hizo.

Lakini pia miongoni mwa kesi walizowahi kuzifuatilia ni za mtu mmoja ambaye alikuwa akichukizwa na uwepo wa machangudoa mitaani. Mtu huyo akadhamiria kuwamaliza kwa kuwaua ambapo alikuwa anawachukua kama mteja na kwenda nao kwenye nyumba za kulala wageni ambako aliwaua kwa kuwanyonga, wengine kwa sumu na wengine kuwachoma visu kutegemea na mazingira. Mtu huyo kila alipokuwa akiua aliacha ujumbe usemao ‘Makahaba mjiandae’. Hata hivyo, mtu huyo aliwekewa mtego na kukamatwa akijiandaa kuua msichana wa saba.

Jambo moja lililokuwa limemtia faraja Salome katika gazeti la siku hiyo ni kauli ya Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Tanga kwamba jeshi lake linakaribia kabisa kumnasa muuaji. Lakini pia alihisi hayo yanaweza kuwa maneno tu ya kuwatia moyo wasomaji na wananchi ili walione jeshi kwamba liko kazini na siku ipite!

Baada ya kuandika mambo muhimu kuhusu kesi hiyo, Salome alinyanyuka kuelekea ofisini kwa bosi wake, Dk. Jumanne Marijani. Huyu udaktari wake haukuwa wa uzamivu (PhD) bali udaktari bingwa wa tiba za binadamu, hususani magonjwa ya akina mama.

Alimkuta pia akisoma gazeti na Salome alihisi bila shaka atakuwa anasoma habari hiyo hiyo ya baamedi wa Tanga Raha Club. Kutokana na shughuli zao zilizojielekeza katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia wanaofanyiwa akina mama na watoto, kila aliyekuwa akishika gazeti anaanza kwanza kutafuta habari za aina hiyo kabla hata ya kusoma habari inayoongoza kwa siku hiyo.

“Bosi, bila shaka unasoma habari ya mauaji ya msichana wa Tanga,” aliuliza Salome baada ya kumjulia hali bosi wake ambaye walikuwa hawajakutana asubuhi hiyo.

“Ndio. Salome, inasikitisha sana. Ninaifuatilia tangu Jumamosi nilipoiona ikitangazwa kwenye vyombo vya habari,” alijibu Dk. Marijani.

“Kilichonileta ni habari hiyo hiyo. Jana nilitingwa na shughuli nikasahau kuizungumzia. Ninataka tuifuatilie kwa karibu na huyu mtuhumiwa atakapokamatwa tuongeze nguvu za kisheria. Ninataka ikiwezekana hii iwe kesi yangu ya kwanza kusimama mahakamani kama wakili wa marehemu na kwa mantiki hiyo kusaidiana na Serikali ili kukomesha haya mauaji. Ninataka huyu mwanaume aliyefanya haya tumshikishe adabu,” alisema Salome aliyekuwa akiongea kwa hisia kali akijitahidi kuzuia machozi.

“Bila shaka Mama Malima. Hata wakati ninasoma hii habari nilikuwa ninafikiria wapi sisi tunaweza kuingilia ili kutoa mchango wetu katika kukomesha mauaji ya wasichana wasio na hatia,” alisema.

“Ninashukuru bosi kwa hilo. Kwa hiyo mimi ninaanza kufuatilia. Nataka kuwasiliana na Kamanda wa Polisi wa Tanga kujua maendeleo ya hii kesi na kisha nimweleze nia yetu ya kulisaidia Jeshi la Polisi.”

“Utaniandalia tu mpango kazi wako na bajeti. Kama utataka kusafiri kwenda Tanga utaonesha kwenye mpango kazi wako. Lakini nadhani mpango mzima utaanza baada ya mtuhumiwa kukamatwa na hapa nimeona askari wakijigamba kwamba wanakaribia kumkamata.”

“Ndio Bosi. Ndio maana nimesema nataka kuwasiliana na polisi Tanga.”

“Ninakutakia kila heri Mama Malima. Kama kesi hii utaisimamia vyema hadi mwisho kwa kushirikiana na mawakili wa Serikali na mhusika kupewa adhabu anayostahili, wafadhili wetu watafurahi sana. Usisahau kuwashirikisha waandishi wa habari hasa wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake kwa kila hatua utakayochukua.”

“Sawa bosi.”

* * *

Wakati vuta nikuvute ikiendelea ndani ya kikao cha Bodi huku wajumbe wakikubali kwa shingo upande msisitizo wa mwenyekiti kwamba mtu atakayevaa viatu vya Matakwali ni Jackson Malima, karani wa Matakwali aliingia kwenye chumba cha mkutano ghafla na kumfuata mezani alikokuwa amekaa bosi wake.

Alipofika akamnong’oneza kwamba Jackson alikuwa amekamatwa muda ule na polisi. “Wameshuka naye sasa hivi na pengine watakuwa getini,” alisema karani yule.

“Inakuwaje mtu anakuja kukamatwa hapa ofisini bila mimi kutaarifiwa?” Alihoji kwa hamaki Matakwali.

“Walianzia ofisini kwa bosi Mapunda. Nadhani bosi Mapunda, aliona kwa kuwa upo kwenye kikao kizito ndio akaamuru waendelee na kazi yao. Ndiye pia kanituma nikuletee huu ujumbe,” alijibu yule karani.

“Kama hao askari hawajaondoka naye kawaambie wanisuburi. Fanya haraka. Ondoka,” alisema Matakwali aliyeonekana kushitushwa na habari hizo. Wakati karani anaondoka, Matakwali alisimama na kuwaambia wajumbe wa bodi alichoambiwa na karani wake.

“Tafadhali mnisubiri mara moja niongee na hawa askari, ninakuja mara moja,” alisema Matakwali akinyanyuka na kutoka haraka.

Alishuka ngazi kutoka ghorofa ya tatu walikokuwa kwenye ukumbi wa mikutano kueleka chini haraka na kukuta askari wale wakiomba wafunguliwe geti waondoke kwa sababu walikuwa hawana sababu ya kusubiri mtu huku karani aliyetumwa na Matakwali akiwaambia askari wa getini wasifungue kwanza hadi Mkurugenzi afike.

Matakwali alipofika alikwenda hadi kwenye gari lao na kuwasalimia kisha akajitambulisha. “Ndugu zangu, mnafika kwa mtu, mnachukua familia yake bila kujitambulisha kwake?” Alihoji.

“Kuna bosi mmoja alishatupokea na kutupa baraka zote. Isitoshe sisi tukija kukamata mhalifu si lazima tupate ruhusa ya mtu,” alijibu mmoja wao mwenye cheo cha sajini.

“Haya niambieni, mmemkamata ofisa wangu mwandamizi kwa kosa gani?”

“Mtuhimiwa anajua lakini kwa faida yako ni kwamba kaua baamedi aliyekuwa naye gesti kule Tanga Ijumaa iliyopita.”

Usikose kufuatilia mkasa huu wa kusikitisha...
 
SIHUSIKI - 15

ILIPOISHIA

Matakwali alipofika alikwenda hadi kwenye gari lao na kuwasalimia kisha akajitambulisha. “Ndugu zangu, mnafika kwa mtu, mnachukua familia yake bila kujitambulisha kwake?” Alihoji.

“Kuna bosi mmoja alishatupokea na kutupa baraka zote. Isitoshe sisi tukija kukamata mhalifu si lazima tupate ruhusu ya mtu,” alijibu mmoja wao mwenye cheo cha sajini.

“Haya niambieni, mmemkamata ofisa wangu mwandamizi kwa kosa gani?”

“Mtuhimiwa anajua lakini kwa faida yako ni kwamba kaua baamedi aliyekuwa naye gesti kule Tanga Ijumaa iliyopita.”

ENDELEA...

“Haiwezekani,” alisema na kumwangalia Jackson aliyekuwa ameketi kiti cha nyuma cha gari lile ambalo alipochunguza vizuri lilikuwa gari la kiraia. “Hawa wanasema nini Malima, mbona siwaelewi?”

“Wananituhumu hivyo bosi, lakini nakuhakikishia sihusiki abadani na hilo. Nakushauri wewe kachape kazi, niache nao lakini Mwenyezi Mungu akipenda ukweli wa hili utajulikana,” alisema Jackson kwa utulivu.

Mkurugenzi Matakwali aliondoka kwa masikitiko kurudi chumba cha mikutano cha bodi huku akiwaza namna atakavyowaambia wajumbe.

Alipofika, huku akionekana mnyonge, Matakwali aliwajulisha wajumbe wa bodi kilichotokea na kuwataka wajadili la kufanya. Mwenyekiti wa Bodi alionelea kwamba waahirishe kikao wakisubiri mustakabali wa Jackson.

Ushauri huo ulipingwa na wajumbe ambao walisema kama Jackson anatuhumiwa kwa mauaji, kesi inaweza kumaliza miaka hata mitano, kitu ambacho hawawezi kuendelea kusubiri na Tume haiwezi kuendeshwa bila kuwa na kaimu mkurugenzi.

“Malima ninayemfahamu mimi hawezi kufanya kitu kama hicho, lakini na mimi naungana na mjumbe kwamba tuangalie tunafanyeje ili ikiwezekana kesho awepo mtu wa kukaimu,” alisema Matakwali.

“Makamu mwenyekiti alisimama: Mimi nilikuwa nafikiria kwamba kikao hiki kimpitishe, Andrew Mambo ambaye ni ofisa rasilimali watu, akaimu haya madaraka bila kupitishwa na bodi, yaani iwe kama kaachiwa tu ofisi na Mkurugenzi hadi tutakapokutana tena na kuona kama tumpitishe yeye au mtu mwingine. Pengine Malima atakuwa keshamalizana na polisi muda huo.”

Wazo hilo liliungwa mkono na Matakwali lakini wajumbe wengine walilipinga vikali. Wakahoji ni kwa nini meza kuu ilikuwa haimtaki Bruno hata katika mazingira kama hayo?

“Kwani Mapunda kawafanyia nini kibaya? Hapa tulikuwa tuna majina mawili tunayoyajadili, Mapunda na Jackson. Kama Mwenyezi Mungu ametuonesha mbele ya macho yetu kwamba huyo mnayemtaka kumkabidhi ofisi hafai kwa nini tusimpe huyu mwingine? Kwa nini makamu aje na jina lingine?” Alihoji mjumbe mmoja wapo.

Matakwali alijibu hoja hiyo akisema jina la mtu aliyependekezwa, kwa mtazamo wake alikuwa anafaa kuliko Bruno na kujaribu kueleza wasifu wake lakini wajumbe wakampinga. Mwenyekiti kwa kuhisi ataonekana ana lake jambo kuendelea kumpinga Bruno, akajikuta anakosa hoja na kukubaliana na wajumbe wengi kumpitisha Bruno kukaimu nafasi ya Matakwali.

Hata hivyo, moyoni aliapa kwamba angeharakisha kujadiliana na waziri pamoja na Rais kumpata mkurugenzi mpya ambaye si Bruno hata kama anatoka nje ya taasisi kama Jackson ataendelea kung’ang’aniwa na polisi.

* * *

Jackson alifikishwa kituo kikuu cha polisi na kutakiwa kuandika maelezo. Aliwaambia askari waliomkamata kwamba asingeandika maelezo hayo kabla ya kukutana na wakili wake na hivyo akaomba awasiliane naye kwanza.

Askari hao bila shaka walidhani mtuhumiwa yule mbele yao ni mtu wa ‘kusukumwa sukumwa’ tu. Wakataka kumshurutisha kuandika maelezo kwa nguvu lakini akawaambia yeye ni mwanasheria kwa hiyo anachokiomba ana haki nacho kisheria na kikatiba.

Akaonya kwamba anaweza kuandika kwa kushurutishwa lakini askari hao pia wajiandae kwa kile atakachowarejeshea kisheria. “Madhali niko mikononi mwenu hampaswi kuwa na haraka yoyote, tekelezeni tu yale ambayo nina haki nayo.”

Akaendelea: “Nitafanya mtakachonilazimisha mkitaka lakini nina matumaini kwamba mtanipa haki yangu ya kuwakilishwa kwenye shauri hili. Kwanza mliponikamata mlitakiwa kunieleza kituo mnachonipeleka na muda huo ningeshampigia wakili wangu. Lakini nilikuwa sijui mnanipeleka wapi, hivyo mtalazimika kusubiri aje. ”

Wale askari walikubali kuchukua ushauri wake na kumpa wasaa wa kumwita wakili wake. Alimpigia simu wakili Hussein Magabhanya, mtu aliyesoma naye sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye wakati huo alikuwa wakili maarufu wa kujitegemea katika jiji la Dar es Salaam. Mbali na kusoma pamoja, chuoni walikuwa wakilala chumba kimoja na kushirikiana mambo mengi.

Baada ya kuongea naye, Jackson aliwajulisha askari wale kwamba wakili wake alikuwa na kesi kadhaa mahakamani mchana huo na kwamba angekuwa na nafasi ya kuja pale kituoni baada ya saa 9:00 alasiri. Askari mmoja aliona kama huo ni muda mrefu kwa sababu maelezo yake yalikuwa yanahitajika mapema.

“Maelezo yangu yanahitajika mapema kivipi na nani anayeyahitaji? Kama sikosei muda wenu wa kusubiri kisheria ni saa nane na kama muda huo ukipita nitakuwa hiari kuandika maelezo bila wakili wangu. Hili ni shauri ambalo haki inapaswa itendeke pande zote, kwa mimi ninayeshtakiwa na anayenishtaki kwa maana ya Jamhuri mnayoiwakilisha. Natumaini busara itawatuma msubiri tu hadi muda huo ambao umeelezwa na sheria.”

“Wewe shauri lako liko Tanga. Unatakiwa baadaye usafirishwe kwenda Tanga na hatujui itakuwa lini lakini inabidi utakapohitajiwa maelezo yako yawe tayari. Kwani huwezi kupata wakili mwingine? Wewe si mwanasheria, unawajua wengi?”

“Kumbe kama ni Tanga basi hata huko ninaweza kuandika maelezo. Ninaweza kuwa ninawajua wanasheria wengi lakini si wanasheria wangu. Katika hili mtapaswa tu kusubiri huo muda wa kisheria uliowekwa,” alisema Jackson ambaye kutokana na kutoshughulikia kwa muda mrefu masuala ya kesi za jinai, alikuwa hakumbuki vyema mambo mengi ya kipolisi ikiwa ni pamoja na muda ambao mtuhumiwa anaweza kupewa kuwasiliana na wakili wake kabla ya kuandika maelezo.

Maofisa wale wa polisi ambao inaonekana, walikuwa hawafanyi kazi waliyofundishwa chuoni isipokuwa ubabe na kutumia udhaifu wa wananchi kutojua sheria kufanya wanayotaka, wakakubali kusubiri kwa shingo upande.

* * *

Saa sita mchana wafanyakazi walianza kuingia kwenye ukumbi wa mikutano wa bodi ya Tume. Dakika saba baadaye ukumbi ulikuwa umejaa wafanyakazi wa Tume ya Teknolojia na Mawasiliano, baadhi wakilazimika kusimama kwa kukosa viti.

Takribani wote walikuwa wanajua ajenda ya kikao kile kwamba ilikuwa ni kuagana na bosi wao, Ibrahim Matakwali ambaye wao walizoea kumwita ‘Mzee’. Ukisikia mfanyakazi anasema ‘Mzee anakuita’, ‘Mzee kasema hivi’ na kadhalika basi ujue walimaanisha Mhandisi Ibrahim Matakwali.

Lakini hamu yao kubwa ilikuwa ni kujua ni nani atakayekaimu nafasi yake au kama tayari Rais alikuwa keshateua mkurugenzi mpya. Kutokana na malalamiko mengi ambayo walikuwa wakiyatoa dhidi ya Bruno, mtu ambaye kwa nafasi na uzoefu wake alipaswa kukaimu madaraka hayo, walikuwa wanajua fika kwamba ‘Mzee’ asingefanya kosa la kumwachia ofisi yake kama Rais alikuwa hajachagua mkurugenzi mwingine kutoka nje ya Tume.

Kwa muda wa wiki nzima, kulikuwa na uvumi kwamba Jackson ndiye alikuwa anatazamiwa kukaimu madaraka hayo ingawa hakukuwa na mfanyakazi hata mmoja aliyekuwa amethibitisha habari hizo. Kwao zilikuwa habari njema kutokana na mahusiano mazuri aliyokuwa nayo na wafanyakazi wenziye na uadilifu wake. Mara chache alizoachiwa ofisi, Jackson alionekana kuwa msaada mkubwa kwa wafanyakazi wenzake, akishughulikia hata matatizo yao binafsi na wengine kuwatembelea majumbani.

Endelea kufuatilia...
 
SIHUSIKI - 16

Kuanzia kipindi hicho, Matakwali alikuwa akimtegemea sana hata katika kusuluhisha migogoro ya baadhi ya wafanyakazi na wenzi wao. Kwa mfano, kuna huyu aliyekuwa ameitelekeza familia yake na kuhamia kwa hawara huku muda mwingi akishinda kwenye mabaa. Jackson alikwenda naye taratibu, wakati mwingine akimshirikisha mkewe, Salome, hadi akafanikiwa kumrejesha nyumbani kwake na kuachana na hawara na kuanza kuihudumia familia yake ipasavyo.

Hata ukaribu wake na Andrew uliongezeka baada ya kusaidia kuokoa ndoa yake iliyokuwa inaelekea kusambaratika. Wengi ambacho hawakujua ni kwamba elimu ya ushauri-malezi alikuwa anaipata kutoka kwa mkewe, Salome, ambaye asasi aliyokuwa akiifanyia kazi iliwahi kumpeleka nchini Uingereza kwenda kusomea masuala hayo kwa kipindi cha miezi mitatu. Mkewe pia alikuwa ameshiriki semina kadhaa ndani na nje ya nchi kuhusu masuala ya jinsia, afya ya uzazi, malezi na saikolojia ya mahusiano.

Baadhi ya wafanyakazi wa kike ndio walifurahia zaidi uvumi huo kwa sababu walikuwa na hofu sana na Bruno ambaye alikuwa akijulikana pia kwa kupenda kila mwanamke anayepita mbele yake. Kulikuwa na tuhuma kwamba mwanamke anayemkataa alikuwa hata yuko radhi ‘kumkomesha’ kwa kumnyanyasa na hata kumpa vitisho vya kufukuzwa kazi.

Pia alituhumiwa kwa uchoyo wa safari za kikazi katika mikoa mbalimbali ya nchi ambazo zilisaidia kuwaongezea kipato wafanyakazi na hasa kwa vile nyingi zilitokea ofisini kwake akiwa kama mhandisi mkuu wa Tume.

Mara nyingi mambo kama hayo yenye maslahi alitaka aende yeye mwenyewe, na kama sivyo basi alimpendelea mfanyakazi mmoja waliyekuwa na undugu naye au msichana mmoja kwenye idara yake ambaye ilisemekana ana uhusiano naye wa kimapenzi.

Hata hivyo, asubuhi hiyo kulikuwa kumezuka uvumi mwingine kwamba Baba Mchungaji alikuwa amekamatwa na polisi. Baada ya kusikia uvumi huo, Andrew aliamua kutoka ofisini kwake na kupita akiukanusha kwa nguvu zake zote ili kulinda heshima ya Jackson katika kipindi hicho ambacho alikuwa anaamini kwamba jina ambalo lingetangazwa ili kukaimu nafasi ya ukurugenzi wa Tume ni la Jackson.

Aliyekuwa amevujisha uvumi huo ni karani wa Bruno, huyo aliyekuwa akituhumiwa kutembea naye huku akiwathibitishia wafanyakazi kwamba alimwona akiwa kapigwa pingu. Ukanushaji uliofanywa na Andrew uliungwa mkono na wafanyakazi wachache ambao walikutana na Jackson kwenye ushoroba wa jengo hilo akiongozana na askari waliokuwa kwenye sare huku akiwa hana pingu zozote.

Wakati wafanyakazi wanasubiri, hamu yao kubwa ikiwa ni kujua atakayekaimu au kuchukua moja kwa moja nafasi ya ‘Mzee’, muda waliousubiri ukawadia. Akaingia Matakwali pale ukumbini akiwa ameandamana na menejimenti yake pamoja na Mwenyekiti wa Bodi na makamu wake.

Miongoni mwa wajumbe wa menejimenti alikuwepo Mhandisi Mkuu wa Tume (Bruno), Ofisa Rasilimali Watu (Andrew), Meneja wa Fedha na Meneja wa Majengo. Kidogo wafanyakazi walishituka kwa kutomwona pale Mwanasheria wa Tume, Jackson Malima.

Baada ya kuketi, mwenyekiti wa kikao hicho, Matakwali, alisimama kuwasalimia wafanyakazi, kisha akatoa hotuba yake ndefu kuhusu namna walivyopewa jukumu la kuanzisha Tume hiyo na Serikali, magumu aliyopitia, mafanikio na changamoto alizopambana nazo na zinazoendelea. Matakwali pia aliwashukuru wafanyakazi wote kwa kumuunga mkono muda wote aliokuwa ofisini na kuwaomba radhi wale aliowakosea.

“Kwanza niseme, kama alivyowahi kusema Rais Mstaafu wa Kenya, Daniel Arap Moi, kwamba wale wote walionikosea nimewasamehe kwa dhati kabisa kutoka moyoni mwangu. Lakini kwa vile mimi kama mwanadamu nina upungufu mwingi na udhaifu, ninaomba wote niliowakosea kwa kujua au kutojua mnisamehe,” alisema.

Hatua hiyo ililipua sauti kubwa miongoni mwa wafakanyakazi zaidi ya 100 waliokuwa wamejumuika siku hiyo ikisema ‘Tumekusamehe Mzee’. Matakwali aliendelea kueleza mengi kuhusu jinsi anavyoiacha taasisi, kisha akamkaribisha Mwenyekiti wa Bodi, Profesa Mwinchumu ili kutaja jina la mtu atakayekaimu nafasi ya ukurugenzi hadi hapo Rais atakapoteua mkurugenzi mwingine.

Profesa Mwinchumu alianza kwa kuwashukuru wafanyakazi wote kwa juhudi zao za kila siku na akawataka kuendelea kuchapa kazi kwa bidii na juhudi ili kuzidi kuboresha shughuli za Tume ambayo alisema ni chombo muhimu katika maendeleo ya kisasa yanayoletwa na matumizi ya TEHAMA. Na kwamba ni chombo chenye jukumu adhimu la kusaidia Serikali katika kujenga uchumi unaotegemea viwanda. Kikubwa aliwataka kutoa ushirikiano mkubwa kwa kaimu mkurugenzi ambaye ataiongoza Tume hadi Rais atakapochagua mkurugenzi mpya.

Baada ya maelezo hayo, akasema kwa sasa atakayekaimu nafasi ya ukurugenzi si mwingine bali Mhandisi wa Tume, Bruno James Mapunda. Kulitokea miguno ya chinichini baada ya jina hilo kutajwa hadi Matakwali, mtu ambaye wafanyakazi walikuwa wakimheshimu sana kulazimika kusimama na kuonya tabia hiyo kwamba haikubaliki na pia akaonya kwamba mtu anaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu katika mazingira kama hayo.

Baada ya utulivu kurejea, Profesa Mwinchumu alimwelezea Bruno kama mkongwe pia kwenye Tume tangu inaanzishwa na kwamba ametoa mchango mkubwa katika kuifikisha mahala ilipo. Hata hivyo, alitumia nafasi hiyo kumtaka Bruno kuvaa viatu vya Matakwali kisawasawa kwani vikimpwaya bodi haitakaa hivi hivi.

Akamtaka awe mwadilifu, mtiifu na mnyoofu kwa wafanyakazi wenzake ili kuhakikisha Tume inapiga hatua zaidi, ikiwezekana kuliko hata alizoita zama za Matakwali. Baadaye alimkaribisha Bruno kuzungumza na wafanyakazi wenzake na aliposimama tu miguno ikarudi tena hadi ‘Mzee’ aliposimama tena kuwatuliza. Hali ilipotulia na Bruno alianza kuwaeleza wafanyakazi wenzake kwamba atajitahidi kuwa mwadilifu na kujali maslahi yao na ya kampuni na kuomba ushirikiano.

Hata hivyo, wakati akizungumza baadhi ya wafanyakazi walianza kutoka nje kama vile wanakwenda kujisaidia wakionekana kukerwa na hatua ya bodi kumpa madaraka hayo Bruno. Hadi Bruno anamaliza kuzungumza na wafanyakazi kama alivyoombwa takribani robo moja ya wafanyakazi walikuwa wametoka nje na wengi kuanzisha vikundi kwenye shoroba za jengo hilo wakishangaa uamuzi wa kumpitisha Bruno kuwaongoza.

Idadi kubwa ya wafanyakazi waliendelea kujiuliza ni kwa nini Jackson ambaye awali uvumi ulionesha kwamba ndiye angeshika nafasi hiyo na kuonekana kuwakosha wafanyakazi wengi ameachwa. Hawakupata majibu.

* * *

Akiwa ameketi kwenye sakafu na watuhumiwa wenzake kadhaa katika kituo kikuu cha polisi, Jackson alijiuliza maswali mengi kuhusu kukamatwa kwake. Swali lililokuwa likimjia mara kwa mara ni namna polisi walivyopata habari zake kwamba anatuhumiwa kwa kosa hilo.

“Kwa nini hawa polisi wamekuja moja kwa moja kwangu? Kule Mkonge Hotel nilifanikiwa kuwakimbia lakini kumbe haikusaidia kitu. Kwa nini waseme wanakaribia kumkamata mtuhumiwa na mara wanakuja moja kwa moja kwangu?” Alijiuliza.

Alifikiria tena namna alivyofanikiwa kutoka kwenye ile nyumba ya wageni ya Twiga bila mtu kumtilia mashaka hadi chumbani kwa Andrew huku akiwa ameaga kurudisha chumba siku hiyo.

Akajiuliza ilikuwaje askari polisi wakajaribu kumsaka pale Mkonge Hotel. Je, kuna mtu aliwaambia yuko pale? Lakini akakumbuka kwamba mlinzi wa nyumba ile ya wageni alikuwa anajua kwamba yuko kwenye semina pale Mkonge Hotel na akakumbuka kumwambia kwamba semina yao ingelimalizika Ijumaa.

Endelea kufuatilia...
 
SIHUSIKI - 17

“Huyu anaweza kuwa sababu ya polisi kujaribu kunisaka Mkonge Hotel,” akajisemea. Lakini swali likabaki kwamba yule mlinzi wala mtu mwingine yeyote hakuna aliyekuwa anajua anafanya kazi wapi.

Akakumbuka kwamba hata kwenye kitabu cha wageni hakuandika ofisi yake zaidi ya jina lake, mahala anakotoka ambako ni Dar es Salaam, anakokwenda ambako ni Tanga na kisha akaandika kazi yake ambayo ni Mwanasheria. Hayo ndio maswali pakee yalikuwa yakiulizwa kwenye lile daftari kubwa la wageni.

Pale hakukuwa na kitu kama jina na ofisi anayofanya kazi. Sasa ni kwa nini polisi waje kumkamata moja kwa moja ofisini kwake? Alizidi kujiuliza. Aliamini kwamba mtu pekee aliyekuwa akijua undani wa tukio hilo ni Andrew. Je, inaweza ikawa ni yeye ndiye anayemsaliti kwa kuwasiliana na polisi? Kama ni yeye anafanya hivyo kwa maslahi gani? Pamoja na kutoamini haraka haraka kwamba Andrew anaweza kumsaliti, lakini hakuona mtu mwingine anayeweza kufanya hivyo zaidi yake. Sasa alianza kupata hisia kwamba huenda Andrew alimsaliti kwa kujua au kutojua.

“Isije ikawa alimwambia mtu akidhani ni siri lakini mtu huyo akaamua kunikaanga. Au anajifanya yuko upande wangu lakini kumbe anatumiwa na Bruno kunimaliza kwa sababu ya cheo,” aliendelea kujiuliza.

Kwamba Andrew anaweza kushirikiana na Bruno ingawa hawakuwa na uhasama wa waziwazi lilikuwa ni jambo ambalo pia lilikataa kuingia kwenye akili yake.

“Lakini siku ile pale klabu Bruno alipokuja kuungana na mimi alitokea kwenye meza yake na yeye akabaki pale hadi nilipokuwa ninaondoka. Je, walikuwa wamepanga nini? Tangu lini Bruno akawa karibu na Andrew?”

Jackson aliendelea kujiuliza na kadiri alivyojiuliza ndipo alizidi kumtuhumu Andrew kuwa nyuma ya mpango mzima wa polisi kumkamata. Sasa alianza pia kujilaumu ni kwa nini alimwachia Andrew jukumu la kumtaarifu mkewe suala la kukamatwa kwake hasa kama atakuwa na ajenda ya siri dhidi yake.

Wakati bado akiwaza, alitolewa ndani ya selo kwamba alikuwa na wageni na kupelekwa selo nyingine ambayo ingeruhusu kuongea na wageni wake. Alihisi ni mwanasheria wake kaja, pengine akiwa na mtu mwingine kwani aliambiwa ana wageni na siyo mgeni. Alipofika akakuta waliokuwa wamekuja kumtembelea ni Mhandisi Ibrahim Matakwali akiwa ameandamana na Mwenyekiti wa Bodi, Profesa Aboubakar Mwinchumu na makamu wake, Josiah Mafumu.

Kutokana na kesi aliyokuwa akituhumiwa nayo kuwa ya aibu alijikuta pia akihisi aibu kukabiliana na mabosi wake hao. “Malima, pole sana. Tumelazimika kuja baada ya kumaliza kikao na wafanyakazi kujua hasa kilichokusibu. Maneno tunayosikia ni kweli?” Aliuliza Profesa Mwinchumu.

Lilikuwa ni swali gumu kujibu. Je, alitakiwa kueleza ukweli kwamba alikuwa na msichana huyo chumbani lakini si yeye aliyemuua au kukana? “Kwa kweli sihusiki abadani,” hatimaye alijibu baada ya kufikiri kidogo na akawa anajiuliza kama swali likija lingine la kumtaka aeleze anachokijua yeye atajibu nini.

“Hata mimi ninaamini hivyo. Niliposikia tu hizi habari nikajua ni suala la mistaken identity. Kijana wangu ninayemjua hawezi kuua mtu, achilia mbali hata kuchukua baamedi kwenda naye chumbani,” alisema Mhandisi Matakwali.

“Ni kweli bosi... Lakini ninaamini ni suala la muda tu, ukweli utajulikana muda si mrefu. Sihusiki kabisa na hili jambo,” alisema huku akijipa matumaini.

“Kwani ilikuwaje hadi ukatuhumiwa na hili?” Akauliza Profesa Mwinchumu.

“Wala sielewi chochote. Ninadaiwa kuua mtu ambaye wala simfahamu,” alijibu Jackson.

“Kwa hiyo umejipangaje katika kushughulikia hii kesi?” Akauliza Matakwali.

“Nimeshawasiliana na mwanasheria wangu na ninamsubiri. Hata nilipoambiwa nina wageni nilidhani ni yeye.”

“Lakini usiwe na wasiwasi. Kwa sababu jambo hili limekupata ulipokuwa ukifanya kazi ya kuwakilisha kampuni, tulikuwa tunajadili na Mwenyekiti hapa wa Bodi kwamba ikiwezekana kampuni igharimie gharama za wakili. Mimi sina wasiwasi pia na hii kesi kwa sababu wewe mwenyewe ni mwanasheria,” alisema Matakwali.

“Nitashukuru sana kwa hilo bosi.”

“Usiendelee kuniita bosi. Hivi nimekuja kukuaga rasmi kwa sababu muda mfupi uliopita nimekabidhi ofisi kwa Mapunda. Kwa kifupi tukio hili limetuharibia sana mimi na mwenyekiti wangu hapa kwani ofisi tulidhamiria kukukabidhi wewe.”

“Kwanza ninawashukuru sana kwa kunifikiria kwamba ningeweza kuongoza Tume. Lakini mambo yote hupangwa na Mungu na hivyo Mwenyezi Mungu alipenda Bwana Mapunda ndiye awe Mkurugenzi wetu na mimi ninamtakia kila heri na kumwombea mazuri. Hata Waswahili wanasema kisicho riziki hakiliki.”

Profesa Mwinchumu aliingilia kati: “Lakini kuanzia sasa jiandae pia kwani tutaanza harakati za kumshawishi waziri na hatimaye Rais kuhusu wewe. Jiandae hata kisaikolojia tu kuja kuwa Mkurugenzi mpya labda kama wawili hao (Rais na Waziri) watakuwa na mtu mwingine watakayeona anafaa zaidi. Lakini mimi kama Mwenyekiti mapendekezo yangu ni wewe.”

“Ninashukuru sana Mwenyekiti kwa kuweka imani yako kwangu. Hii ni heshima kubwa sana kwangu. Ninakushukuru sana.”

“Tuna habari zako kwamba unafaa sana. Nikueleze tu kwamba hatua ya kumkabidhi ofisi Mapunda hata imewaudhi wafanyakazi wenziyo. Karibu wanizomee nilipotaja jina lake na Mhandisi hapa ndiye kaniokoa. Nitajitahidi sana mchakato wa kumpata mkurugenzi mpya wa Tume ufanywe haraka. Lakini hili tafadhali ibaki kuwa siri yako na litategemea kadri kesi hii itakapomalizika mapema. Lakini kwa bahati mbaya hii ni kesi ya mauaji, inaweza kuchukua siku nyingi,” alisema Profesa Mwinchumu.

“Hamna taabu Mwenyekiti. Hili hutolisikia kwa mtu yeyote hata mke wangu. Binafsi ninaamini polisi wataniachia muda si mrefu baada ya kufanya uchunguzi wao. Nina hakika kuna mahala wamekosea,” alisema Jackson.

“Hata mimi ninaamini hivyo…” akasema Matakwali.

“Kama alivyokwambia Mkurugenzi… Bado mimi namwita hivyo, kesho nitamwagiza Bruno ashughulikie malipo ya wakili wako. Tutajadili zaidi namna ya kuliweka hili ili isije ikaonekana ni jambo binafsi. Tutajitahidi lionekane ni la Tume pia,” alisema Mwenyekiti.

Kabla hawajaondoka, wakili wake, Hussein Magabhanya aliwasili na hivyo wakamuaga kuondoka.

“Kabla ya kuja kwako tumeongea na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (MUM) ambaye ameniahidi kwamba utapatiwa huduma zote za msingi kisheria. Huyo MUM alikuwa mwanafunzi wangu wakati nafundisha sekondari kabla sijarudi shule kusoma,” alisema Profesa Mwinchumu ambaye mbali na kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTM, ni mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Wakati wanaanza kuondoka, MUM alifika eneo hilo na kumsalimia Jackson na kumpa pole. Akaagiza askari waliokuwepo kumwangalia mtuhumiwa huyo kwa jicho tofauti, jambo ambalo lilizidi kumpa faraja Jackson ambaye kabla ya hapo alikuwa katika hali kama ya kuchanganyikiwa.

Safari hii, Jackson hakupata upinzani mkali alipoomba kukaa faragha na wakili wake. Alimsimulia kila kitu kilichotokea na hivyo akataka kusikia ushauri wake kabla ya kuandika maelezo.

Endelea kufuatilia...
 
SIHUSIKI - 18

"Kabla sijakushauri, labda tuyapime haya mambo mawili. Kukubali kwamba ni kweli ulikuwa na huyu binti chumbani au kukana. Ukikana najua polisi watafanya gwaride la utambuzi na hawa wahudumu wa gesti ulimokuwa watakutambua na ukikubali itakuwa vigumu kuthibitisha kwamba huyu binti alikufa kwa ugonjwa kwa sababu kuna maelezo ya daktari kwamba alitiliwa sumu kwenye bia,” alisema wakili.

Akaendelea: “Halikadhalika, kitendo cha kukubali kuwa na huyu binti chumbani, hatua ulizochukuwa za kutelekeza mwili wa marehemu na kunyofoa taarifa zako kwenye kitabu cha wageni zitaonesha kwamba ulikuwa na nia ovu. Hapo tuangalie linaloweza kutusaidia."

"Binafsi natamani kusema ukweli tu kwamba nilikuwa naye. Siku zote huwa ninaamini kwamba ukweli humuacha mtu huru. Hata jambo hili ninaamini limekuwa gumu kwa sababu nilipindisha ukweli. Nadhani sikutakiwa kufanyia kazi ushauri wa Mambo.

Lakini tatizo linalonitisha ni hayo uliyoyasema kusababisha ugumu kama nitakubali, ingawa kubwa zaidi namhofia mke wangu. Ile hali tu ya kujua kwamba nilifikia hatua ya kuwa chumbani na msichana huyu itamwathiri sana kisaikolojia na kuondoa uaminifu wake kwangu.

Itakuwa mbaya zaidi kama hatoniamini kwamba sikuhusika abadani na kifo chake. Hilo linanisumbua sana. Hawezi kuniamini kwamba nilimwachia kitanda, nikalala kwenye kiti mithili ya mtu anayekaribisha mgeni aliyepotea njia usiku wa manane huku mvua ikinyesha. Niko tayari hata kufungwa lakini siyo mke wangu kuwa na mashaka na uaminifu wangu kwake kama ambavyo mimi namwamini kwa asilimia mia moja. Kwa hiyo nishauri nifanyeje," alisema huku akikumbuka pia kwamba wakati anamtaka Andrew kumjulisha mkewe kukamatwa kwake hakumzuia asimwambie sababu za kukamatwa kwake.

"Kama mkeo anakuamini ukimwambia ukweli kama ulivyoniambia atakuamini tu kama mimi nilivyokuamini. Hofu yangu bado ni vipi tutajinasua na nia ovu iliyokufanya ukimbie na kuondoa kitabuni details zako. Halafu kama daktari kasema marehemu alikufa kwa sumu tutakuwa na ushahidi gani wa kumpinga?" Alihoji wakili Hussein.

"Kwa hiyo unashaurije?"

"Mimi nashauri ukane halafu mahakamani tutajitahidi wasiweze kuthibitisha kesi yao kwa sababu wao watategemea zaidi ushahidi wa wahudumu ambao wewe utawakana. Huku ninaona njia ya kutokea katika hii kesi ni nyepesi kuliko upande ule mwingine."

"Nikitakiwa kuthibitisha mahala ambako siku zote nilizokuwa kwenye semina Tanga nilikuwa ninalala, hapo nitafanyaje?"

Wakili Hussein Magabhanya alibaki kimya kwa muda kisha akasema:"Hapo pagumu kidogo lakini pia tunaweza tukapata mbinu. Kuna mteja wangu mmoja Tanga anamiliki nyumba za kulala wageni mbili au tatu. Ni mjanja mjanja hivi, pengine anaweza kutusaidia. Katika hili tutamwomba ionekane kwamba ulilala muda wote kwenye moja ya gesti zake. Kufoji kitabu kikiwa na jina lako sidhani kama itakuwa shida kwake alimradi tumhakikishie malipo kwa ajili hiyo. Mimi nashauri tufanye hivyo. Wewe tumetoka mbali na kama hukumbuki ulichangia sana mimi kupata shahada yangu. Nitapigana kuhakikisha unatoka salama."

Jackson ambaye moja ya vitu anavyochukia sana ni kusema au kuambiwa ni uongo alibaki kimya kwa muda. Wazo la wakili wake aliona limekaa vyema lakini tatizo ni kwamba ni suala la kusema uongo!

"Aisee Hussein, naogopa sana uongo. Unaweza kunisumbua zaidi."

"Lakini katika hili uongo ndio utakaokuokoa Jackie... Halafu katika maelezo yako ulionesha unashangaa namna polisi walivyokujua na kukukamata, mimi sitaki kumung'unya maneno, huyu jamaa anayejua kila hatua yako atakuwa ni yeye anayekusaliti. Na kuanzia sasa nakushauri jitenge naye. Usimwambie chochote."

"Bila shaka atakuwa ni yeye. Napata hisia hizo pia na kwamba alikuja kukaa na mimi muda ule ofisini kwangu ili polisi wakinikamata nisimshuku. Alikuwa ni mtu wangu wa karibu sana ambaye katu sikumtazamia anitendee haya kama kweli yeye ndiye anayenichoma."

"Usiamini sana watu, pengine atakuwa na sababu zake za kufanya haya. Inatokea sana kwamba yule unayemwamini ndiye anayekusaliti."

"Unajua nimeshawaza sana kiasi kwamba kichwa changu kimefikia ukomo na hivyo naomba ushauri wako. Unadhani mke wangu atakapokuja kuniona nimwambie nini? Kumbuka hata yeye, kama angekuwa mtu baki, angeweza kuwa wakili wangu pia na anaweza kukusaidia katika hili."

"Kutokana na ulivyonieleza mwanzo nafikiri ungekana pia kwake kwamba huyu msichana hukuwa naye chumbani kwako na kama baadaye itabidi mimi wakili wako ndiye nitamwambia ukweli wa mambo," alisema wakili huyo ambaye pia anamfahamu vyema Salome tangu wakiwa chuo.

* * *

Andrew Mambo aliangalia saa yake ikamwonesha kwamba ilikuwa ni saa tisa na dakika 26 jioni. Kwa vile Jumanne hiyo ilikuwa ni siku ya pili kuingia ofisini, alikuwa na mafaili mengi ya kupitia na barua nyingi za wafanyakazi alizotakiwa kuzisaini kwa niaba ya mkurugenzi na hivyo kujikuta akiwa na kazi nyingi hata kushindwa kwenda kula.

Isitoshe suala la uteuzi wa bodi kuhusu mkurugenzi mpya na mkutano ambao wajumbe wa bodi walifanya na menejimenti ni mambo ambayo yaliyomfanya awe na kazi nyingi za kufanya kama ofisa rasilimali watu.

Katika mambo muhimu aliyopaswa awe amefanya ni kutekeleza kile alichoagizwa na Jackson, yaani kumwambia mkewe kuhusu kukamatwa kwake. Aliona afanye kazi hiyo ya kumpigia simu shemeji yake mara moja kisha aende polisi kumwona Jackson na kusikia alivyojipanga kuendesha kesi hiyo na kama ataweka wakili au la.

Hata hivyo, alihisi uzito mkubwa kumpigia Salome simu kumpa habari zile mbaya lakini hakuwa na namna nyingine. Mara ya mwisho kuongea na mwanamke huyo ni pale alipolazimika kumtafuta ili kuongea na mke wake walipokuwa kwenye mgogoro uliotishia kusambaratisha ndoa yao.

Alipopiga simu aligundua kwamba Salome kumbe alikuwa bado ana namba yake ya simu.

"Habari za masiku shemeji Mambo?"

"Nzuri. Unaendeleaje shemeji?"

"Naendelea vizuri... Nashukuru umepiga simu kwani hata mimi nilikuwa napanga kukupigia. Bado uko ofisini?"

"Ndio shemeji, kwani vipi?"

"Baba Hellen nimeshamtafuta sana lakini hapokei simu. Kama mko karibu naomba umwambie apokee simu yangu tafadhali."

"Kwani kuna shida yoyote shemeji?"

"Hapana, nilitaka tu kumwambia kwamba kuna simu hapa nilikuwa ninaisubiria kutoka ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa (KPM), Tanga. Wameniambia wanaweza kunipigia kwenye saa kumi na moja hivi jioni, hivyo akitoka kazini asinipitie, ninaweza kuchelewa kidogo. Nitakuja nyumbani kwa daladala au nitakodi bajaji."

"Simu kutoka kwa Kamanda wa Polisi Tanga? Kuhusu nini shemeji?"

"Ni masuala yetu tu haya ya unyanyasaji wa kijinsia. Kuna kesi fulani nimeanza kuifuatilia... Huyo baba Hellen yuko karibu hapo?" Kabla ya kujibu Andrew alijiuliza maswali kadhaa bila majibu na kusababisha Salome amuulize kulikoni amebaki kimya.

"Shemeji kuna mtu ananisemesha hapa na mimi nikawa namsemesha kwa ishara... Kuhusu baba Hellen kapata matatizo kidogo ndio maana nimekupigia."

"Matatizo? Kuna nini shemeji, mbona umenishitua hadi nasikia moyo ukinienda mbio."

"Usiwe na wasiwasi shemeji. Ni matatizo ya kawaida tu."

"Enhe, ni yapi shemeji."

"Aah ni kwamba, Malima amekamatwa na polisi."

"Amekamatwa na polisi? Kivipi?"

Je, Salome atazipokeaje taarifa hizi? Usikose kufuatilia...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom