Simulizi: Scaila Michael

Bila shaka Scaila atakua anatoa hadi tigo inabidi Nyemo amwombe ndogo akirudi kutoka Maisha club
 
SEHEMU YA 48

Siku hiyo sikuwa na furaha kabisa, si siku hiyo tu bali katika wiki hiyo nilikuwa na huzuni tele, moyo wangu ulikosa furaha kwa sababu ya Scaila tu.

Nilimpenda mno, huo ndiyo ukweli kutoka moyoni mwangu. Unaweza kuniona mjinga, sina akili lakini omba sana mambo haya yasikukute, kwani yakikukuta, unaweza hata kuchukua uamuzi mgumu.

Kuna watu wengi kama mimi, tena wengine ni zaidi yangu. Hebu fikiria, sikuwahi kumfuma Scaila akiwa chumbani na mwanaume, ni maneno tu, yaani maandishi ya kwenye simu ndiyo yaliyokuwa yakinipagawisha.

Sasa hebu fikiria, kuna mwanaume anamfumania mke wake ndani, chumbani akiwa na mwanaume mwingine, uchi wa mnyama lakini bado anamsamehe, mimi ni nani? Je, nimuache Scaila kwa sababu ya meseji? Yaani nikienda kwa mama yake, nimwambie nimeachana na Scaila kwa sababu ya meseji za bando la shilingi mia tano, ni upuuzi ulioje!

Kama binadamu mwenye uvumilivu, nilitakiwa kumpa nafasi msichana ya kubadilika basi hiyo hiyo nafasi alitakiwa kuipata Scaila, ila kwanza nilitakiwa kumwambia ukweli juu ya kilichokuwa kikiendelea.

Nilijipanga na kuelekea kazini, nilipanga siku hiyo ndiyo ya kumwambia msichana huyo ukweli kabisa, yaani kama alikuwa akiyafanya mambo hayo basi aachane nayo, atulie na mimi na tujenge maisha.

Nilifika kazini na kutulia, hali haikubadilika, ilikuwa kama siku nyingine tu, nilikuwa na mawazo tele mpaka majira ya saa tatu asubuhi, simu yangu ikaanza kuita, nilipoangalia jina, alikuwa Scaila, nikashusha pumzi ndefu, kidogo mwili wangu ukachangamka na akili kukaa sawa, nikapokea.

“Halo bebi!” niliisikia sauti yake nyororo.
Kuna vitu vingi vya kuzoeleka lakini si sauti ya Scaila, kila nilipokuwa nikiisikia, ilinipagawisha mno.

Nilichanganyikiwa kupita kawaida na kila siku nilikuwa nikimuona kuwa mpya na ndiyo maana ninasema wazi kumuacha msichana huyu lilikuwa jambo gumu sana kufanyika.
“Halo mchumba...” niliita huku nikitoa tabasamu pana.

“Nimekumiss sana mpenzi!” aliniambia kwa sauti ya kudeka.
“Nimekumiss pia! Mama anaendeleaje?” nilimuuliza.
 
SEHEMU YA 49

“Anaendelea vizuri tu! Upo nyumbani?” aliniuliza.
“Hapana! Nipo kazini!”
“Oh! Okay! Mimi naenda nyumbani, utanikuta,” aliniambia.

“Haina shida.”
Nikakata simu na kushusha pumzi ndefu, bado sauti yake ilikuwa na msisimko wa ajabu sana masikioni mwangu. Nilimpenda sana msichana huyu na ninadiriki kusema katika kipindi hicho moyo wangu haukuwa na hata dalili moja ya kumuacha msichana kama Scaila.

Wanaume tumeumbiwa mateso, ipo hivyo! Mimi sikuwahi kumfuma chumbani akiwa na mwanaume, lakini kuna watu waliwahi kuwafuma wake zao na kuwasamehe, hata mimi nilitakiwa kufanya hivyo.
“Ila anatakiwa kujua kama ninajua mambo yake,” nilijiambia.

Kumsamehe mtu ni wajibu wa kila mtu, si mimi tu, kila mtu kwenye dunia hii ameagiza kusamehe, tena saba mara sabini, kama Scaila alikuwa akiyafanya hayo inamaanisha kuwa naye alihitaji kusamehewa kama wengine, lakini nilitakiwa kumwambia ukweli.

Sikutaka kumwambia kama nilihitaji kuzungumza naye, kama ningethubutu kumwambia hivyo nina imani asingekuwa na furaha, muda wote angekuwa na hofu ya kujiuliza ni kitu gani nilitakiwa kuongea naye.

Hivyo nilipotezea, nilifanya kazi zangu mpaka jioni na kurudi nyumbani. Nilipofika, kama kawaida yake alinipokea kwa mbwembwe na mabusu tele kana kwamba hapakuwa na kitu chochote kile kilichokuwa kikiendelea.

Nilimchangamkia, sikutaka kumuonyesha kama kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea. Nikaenda chumbani, kitu cha kwanza ni kuwasha kompyuta yangu na kama kawaida nikafungua WhatsApp Web kwa lengo la kuangalia kilichotokea.

Ilikuwa hivyo, ni kweli nilikuwa na wivu mkali lakini kitu cha ajabu sikuacha kuangalia mawasiliano yake kwa njia ya WhatsApp.

Niliingia na kuanza kusoma mawasiliano hayo. Hayakubadilika, yalikuwa yaleyale na yalifanywa mchana wakati nipo ofisini.

Niliyasoma, alikuwa akichati na marafiki zake akiwaambia ni kwa namna gani usiku wa kuamkia leo ulikuwa na raha yake, niliumia kupita kawaida ila sikuwa na la kufanya zaidi ya kupotezea mpaka muda wa kuzungumza naye utakapofika.
 
Wanaume wengi kama sio wote tuliwahi kupitia undezi wa aina hiyo, yes tumepitia katika nyakati na namna tofauti tofauti... Baadae mtu unakuja kujishangaa hivi nilikuwaje zoba hivi
 
nmekuta kastor kazuuur kwel yan nmefika hadi mwisho ila uko vzr mtunzi......ila huyo bodaboda amekula faida nzito na umbea katoa.....hahahaha
Mtunzi sio mm bwana mm mletaji tu Gucci
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…