Simulizi; Penzi kitovu cha uzembe

socket

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2014
Posts
305
Reaction score
435
Sisimulii hadithi ya Ngoswe na mazoea ila hii riwaya ilikuwa na maana kubwa pia kuna mashairi kama siharakie Maisha lakini pengine tulisoma kwa nia kujibia mitihani na kuacha baada ya kupewa vyeti.

Nimejaribu kuwaza na kuona kuna ukweli kwa asilimia kubwa kuwa mahusiano na mapenzi tunayojenga yana impact kubwa katika kuandaa maisha yetu ya kesho

Nilichojifunza kwa wenzetu weupe wengi ni kuwa hii concept wanaijua hvyo wanakuwa makini sana wakati wa kuchagua partner wake ambaye wanaendana kimalengo lakini pia wanamapenzi ya dhati kwasababu wanakuwa focused kwenye malengo lkn anakuwa na yule aliyempenda pia, michepuko kwa wanawake ni kama hakuna kwa wanaume ni mpk mdada ajisogeze na anaweza asipewe chochote.

Pia ziko tabia nyingine kama kwenye mavazi, hawa watu hawajali sana wanavaa nini yaan usister duuh na usharobaro usiokuwa na maana kwao hauna priority na kwenye chakula ukiona anakula cha gharama basi angalia origin yake na income na utagundua hatumii gharama kubwa. Sasa basi usishangae mtu huyu mweupe akawa na fedha nyingi kwenye account yake yaan amesave kiwango kikubwa sana cha fedha.

Mbongo sasa mwenzangu na mm hapa ndio kazi ipo ya kulalamika kipato kidogo maana alitaman angekuwa na kadem kila mtaa ila salary inakuwa limit kwake, anataman angevaa kila siku toleo jipya la nguo ili watu wamuone, na hapa atapiga selfie akiwa na pizza na wine na kupost ili watu wajue na yye anaweza kuishi above standards.

Namalizia kwa kusema Mahusiano yetu sisi waafrica yanatugharimu sana badala ya kuandaa future zetu, kitendo cha kubadili wanawake au wanaume kinatufanya tufanye mambo ambayo yako nje ya uwezo wetu ili kumuonesha mwenzako kuwa unaweza.

Ni rai yangu kwetu vijana kuwa na mpenzi mmoja utakayejenga nae future sasa kazi kwetu kula ujana au kuja kuwatishia watoto kuwaachia laana kuwa hawakulei na pengine hukuwatunza.
 
Umenena mkuu.
 
Khaaaak kwamba ntakupa nchi, huyu jamaa atajiua mda sio maana hana tena cha kuhonga kama alifikia hatua ya kuhonga nchi
 
Khaaaak kwamba ntakupa nchi, huyu jamaa atajiua mda sio maana hana tena cha kuhonga kama alifikia hatua ya kuhonga nchi
Watu wanahonga migodi ya almasi bunacheza na penzi?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…