Simulizi: Penzi ama kaburi?

Sehemu ya 31.

Shadya alipofika chuoni, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumtafuta kaka yake kwa lengo la kumpa dawa ile aliyotoka kuichukua kwa Gibson, akampigia simu na kuonana katika ukumbi wa Nkurumah.

Rahim hakuamini kama dada yake alifanikiwa kuipata dawa hiyo kwani alikuwa akienda kudhalilika kama tu asingekuwa nayo. Akaichukua, akashukuru na kuondoka zake.

Alipofika bwenini, kitu cha kwanza kilikuwa ni kumpigia simu Hawa na kuanza kuzungumza naye. Akamwambia alikuwa tayari kwa kila kitu, alijipanga na hivyo alihitaji kuonana naye haraka iwezekanavyo.

“Haina shida!” alisema msichana huyo.
Kweli wakaonana katika nyumba ya wageni iliyokuwa Sinza Kumekucha na kabla ya mambo yote, Rahim akaenda mariwato na kufanya kile alichoambiwa alitakiwa kufanya na kurudi chumbani.

Alimwangalia Hawa pale kitandani alipokuwa, hakusisimka hata kidogo, hakuvutiwa hata mara moja lakini kwa sababu dawa aliyoipaka ilikuwa na nguvu, akashangaa kiungo chake kikianza kukakamaa.

Alishtuka, kwa mara ya kwanza ndani ya miaka minne alikutana na hali hiyo, alimshukuru dada yake kwani kitendo cha kuingiliwa na wanaume wenzake kilimuharibu kabisa na kukosa hisia kwa wanawake kama wanaume wengine.

Akamsogelea msichana yule kitandani, akamshika na kuanza kumbusu kila kona mwilini mwake. Kwa mara ya kwanza Rahim alifanikiwa kufanya mapenzi na Hawa, hakujisikia kama wanaume wengine, kwake ilionekana kuwa kawaida na wakati mwingine alijiuliza ni kwa sababu gani wanaume walipenda sana ngono.

Walitumia dakika arobaini na walipomaliza, wakaondoka. Kitu cha kwanza kabisa kwa Hawa kilikuwa ni kumwambia Hamisi kwamba alifanikiwa kufanya mapenzi na Rahim.

“Unasema kweli?” aliuliza Hamisi, hakuamini alichokisikia.

“Ndiyo! Tena ana nguvu ile kinoma, utafikiri alikuwa na ukame wa miaka ishirini,” alijibu Hawa huku akionekana kutabasamu.

“Hebu niambie ilikuwaje!” alisema Hamisi na Hawa kuanza kumwambia kila kitu.
 
Sehemu ya 32.

Alipomaliza, Hamisi akamlipa pesa aliyomuahidi na kumfuata rafiki yake, kwanza alipomuona tu, uso wake ulikuwa na tabasamu ambalo lilimfanya Rahim kushangaa, akahisi kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea hivyo alihitaji kufahamu.

“Kidume!” alisema Hamisi huku akimwangalia Rahim.
“Unamaanisha nini?” aliuliza Rahim huku akionekana kushangaa.

Hakufikiria kuhusu Hawa, alichokijua walikifanya kitendo hicho kwa siri kubwa na hapakuwa na yeyote ambaye alifahamu lolote lile, kitendo cha kuitwa kidume na Hamisi kilimshangaza kidogo hivyo kuhitaji kufahamu kulikuwa na kitu gani.

Hamisi akaanza kumwambia kuhusu Hawa, jinsi walivyoondoka na kuelekea Sinza, alichomwambia ni kwamba kulikuwa na watu waliowaona mpaka wakiingia kwenye nyumba ya wageni.

Rahim akanyamaza kwa dakika kadhaa, moyo wake ulikuwa na furaha mno kwani kama kweli kulikuwa na watu waliomuona ilimaanisha sasa wasingejua kama alikuwa mshiriki mzuri wa mapenzi ya jinsia moja.

“Kwa maana hiyo watu waliniona?” aliuliza Rahim huku akionekana kutabasamu.

“Ndiyo! Dunia haina siri hata kidogo! Kamera zetu ndogo zilikuona,” alisema Hamisi huku akichia tabasamu pana, alimpongeza rafiki yake huyo, yaani ule ustaadhi wake usingekuwepo tena.

*** Mapenzi yalianza kimchezomchezo sana, Shadya taratibu akaanza kuwa bize na Gibson na kusahamu kama kulikuwa na mwanaume mwingine aliyeitwa kwa jina la Ngwali.

Alitokea kumpenda kijana huyo, kwa jinsi alivyofanya naye mapenzi chumbani ilimshangaza mno na kujiuliza kama kweli kulikuwa na mwanaume wa Dar aliyekuwa na nguvu kama alizokuwanazo mtu huyo.
Walikuwa wakichati, moyo wake ulibadilika kabisa, kama ambavyo alikuwa akijisikia raha alipokuwa akichati na Ngwali, sasa ile raha ikahamia kwa Gibson.

Mwanaume huyo alijua kuchati naye, kumfurahisha na kumfanya kujisikia kama malkia fulani kwenye ulimwengu wa peke yake. Walizungumza mambo mengi na kuandikiana meseji zilizomchanganya zaidi Shadya.
 
Sehemu ya 33.

“Nakupenda sana,” aliandika msichana huyo.
“Nakupenda pia! Wewe ni msichana wa tofauti sana kwenye maisha yangu. Unajua kupenda, unanukia vizuri, unapendeza mno, ni msichana ambaye kama kuna siku nitampoteza, nina uhakika nitalia maisha yangu yote,” aliandika Gibson, Shadya alipousoma ujumbe huo, tabasamu pana likachukua nafasi yake.

“Kweli?”
“Niamini mpenzi! Kwa kipindi kirefu sana nilitamani kumpata msichana kama wewe, mwisho wa siku umetokea katika maisha yangu, kipindi ambacho nilionekana kukata tamaa,” aliandika Gibson.

“Nashukuru kwa kunipenda!”
“Na wewe nakushukuru kwa kukubali kuwa mpenzi wangu! Utapenda nikupeleke wapi ukale leo?” aliuliza Gibson.

“Popote upendapo!”
“Basi nakuja kukuchukua! Jiandae, vaa ile nguo nzuri kipenzi!” aliandika.
“Sawa!”

Shadya akasimama kutoka kitandani, moyo wake ulibadilika na kuwa mtu mwenye furaha kubwa, akaelekea bafuni, akaoga na alipomaliza akarudi na kuanza kuvaa nguo zake huku tayari ikiwa ni saa saba mchana.

Akaichukua simu yake na kuangalia, kulikuwa na missed calls tatu kutoka kwa Ngwali, alimtafuta alipokuwa akioga. Kwa mara ya kwanza akahisi kumdharau mwanaume huyo, hakuwa na hamu ya kumpigia kwa sababu tayari moyo wake ulianza kuchukuliwa na mwanaume mwingine.

“Missed calls tatu utadhani ananidai figo yake...mxiiiiuuuuu...” alisema msichana huyo na kusonya, huo msonyo wake si wa nchi hii, halafu akaifunika simu.
Penzi jipya liliuchanganya moyo wake na hakutaka kusikia la yeyote yule.

Alipomaliza kujiandaa, akampigia simu Gibson ambaye alimfuata na gari chuo na kumchukua kuondoka nay kuelekea katika Mgahawa wa Samaki Samaki kwa ajili ya kula.

Muda wote Shadya alionekana kuwa na furaha tele, alitokea kumpenda Gibson na kuhisi angekuwa naye muda wote katika maisha yake.

Walikula na kunywa na walipomaliza, wakachukuana na kuelekea nyumbani kwa kijana huyo. Hapakuwa na ugumu wowote ule, alivuliwa nguo, akaanza kuguswa hapa na pale na mwisho wa siku kuanza kufanya mapenzi kama ilivyokuwa siku iliyopita.
 
Sehemu ya 34

Penzi la Shadya kwa Gibson likazidi kushamiri moyoni mwa msichana huyo, akachanganyikiwa kupita kawaida, alihisi kama katika dunia hii alikuwa akipendwa peke yake na hapakuwa na mtu yeyote yule aliyekuwa akipendwa kama alivyopendwa.

“Nitakupenda maisha yangu yote,” alisema Shadya kwa sauti nyororo, maneno yaliyoonyesha ni kwa jinsi gani alichanganyikiwa.
“Nitakupenda pia!” alisema Gibson na kumbusu msichana huyo mdomoni.
*
*

Ngwali alichanganyikiwa, moyo wake uliuma kupita kawaida, hakujua ni kitu gani hasa kilikuwa kikiendelea. Alijaribu kumpigia simu mpenzi wake, Shadya lakini haikuwa ikipokelewa.

Hakuwa na raha, moyo wake ulichoma na wakati mwingine alianza kuhisi kama kulikuwa na tatizo kubwa mno alilokuwa akilipitia mpenzi wake huyo.

Akampigia simu Rahim na kuanza kuzungumza naye. Kitu cha kwanza alihitaji kujua kuhusu Shadya kama alikuwa sawa ama kulikuwa na kitu.

Alichomwambia Rahim ni kwamba hapakuwa na tatizo lolote lile kwani siku iliyopita alizungumza naye na alionekana kuwa kawaida kama siku nyingine.
“Sasa kwa nini simu zangu hapokei?” aliuliza.

“Sijajua! Labda yupo mbali na simu!” alitetea Rahim.
“Yaani tangu jana! Ama anaumwa?”
“Sijui! Nadhani yupo mbali na simu! Endelea kumtafuta shemeji!” alisema Rahim.

“Au amepata mtu mwingine?”
“Mtu mwingine? Zaidi yako? Shadya hana hata rafiki wa kiume, achana na mpenzi tu,” alisema Rahim.

“Kweli?”
“Niamini! Mimi ndiye mlinzi wake!” alisema Rahim.
Kidogo maneno ya Rahim yakamfanya kuwa na amani ndani yake. Akamwamini kwamba inawezekana kabisa msichana huyo hakuwa karibu na simu, ama aliiacha chumbani na yeye kwenda sehemu fulani.

Hakukoma, hakuacha kupiga simu na majibu yaliendelea kuwa yaleyale kwamba simu haikupokelewa kabisa.

Siku hiyo hakuwa na furaha hata kidogo, hata madrasa hakwenda, alijiona kama mtu aliyekuwa akiumwa hivi.
 
Sehemu ya 35.

Ilipofika majira ya saa mbili usiku ndipo akajaribu tena, muda huu ikaonekana kuwa kama bahati kwake, simu ikapokelewa na sauti ya msichana huyo kuanza kusikika.

“Halo!” iliita.
“Halo mpenzi! Nimekumisi sana,” alisema Ngwali, ni kweli alimmisi mpenzi wake, huo ndiyo ulikuwa ukweli ambao haukujificha kabisa.

“Nimekumisi pia mpenzi!” alisema Shadya.
“Mbona haukuwa ukipokea simu zangu?”
“Simu niliisahau bwenini! Nimeona missed calls zako na meseji, nisamehe mpenzi!” alisema msichana huyo kwa unyenyekevu.

“Usijali mpenzi!”
Wakati huo upande wa pili Shadya alikuwa akijitahidi kuulazimisha moyo wake kumpenda Ngwali kama ulivyokuwa lakini alishindwa ni kwa namna gani angeweza kufanikisha hilo.

Ni kwa kipindi kifupi tu mwanaume huyo aliondoka moyoni mwake, hakumpenda tena, alimuona mtu wa kawaida na mapenzi yalikufa, yakazikwa na kuoza kabisa.

Walizungumza kwa dakika kadhaa na kukata simu, Shadya akakunja sura yake, katika vitu ambavyo hakuvipenda kabisa, cha kwanza kupokea simu ya mwanaume huyo, yaani alichukia kupita kawaida.

“Nitabadilisha namba! Yaani sitaki hata kuona simu zake zikiingia,” alisema msichana huyo, kile alichokisema alikimaanisha, hakupenda kweli kuona simu yak ikiita kutoka kwa mpenzi wake huyo, alichukia kupita kawaida.
*** “Imekuwaje huko?”
“Nimefanikiwa kupata uhamisho!”

“Acha masihara?”
“Ndiyo! Japokuwa ilikuwa vigumu lakini mwisho wa siku wamekubali kunihamisha, sasa nitakuja kuishi huko mpenzi!” “Bora uje, nakukumbuka sana mpenzi!”

Hayo yalikuwa ni mazungumzo baina ya Gibson na msichana aliyeitwa kwa jina la Paula. Wawili hawa walikuwa wapenzi wa muda mrefu ambao sasa walikuwa tayari kufunga ndoa.

Walipanga hilo lifanyike baada ya kufanikisha uhamisho wake kikazi kutoka jijini Arusha na kuelekea Dar es Salaam. Katika kipindi chote hicho Paula alikuwa akipambana na mwisho wa siku akafanikiwa kupata uhamisho huo na hivyo kumwambia mpenzi wake.
 
Sehemu ya 36.

Ilikuwa ni furaha zaidi kwao, kila mmoja alitamani kumuona mwenzake kwa mara nyingine. Gibson hakumfikiria Shadya kwa sababu kwake alikuwa msichana wa kawaida, wa ku-hit and run.

Maandalizi ya kumpokea mpenzi wake yakaanza kufanyika, wakati hayo yote yakiendelea ndipo akakumbuka kulikuwa na msichana aliyeitwa kwa jina la Shadya.

Huyu alikuwa Mpemba, mzuri wa sura lakini hakutaka kabisa kuona akimsababishia kutengana na mwanamke wa ndoto yake, aliyetaka kutengeneza naye maisha.

“Wanawake wa chuo huwa ni wa kupiga na kuacha, tunaishi hivyo kama wanachuo, kwani naye anataka mimi kuwa wake maishani ama?” alijiuliza.

“Na kama aking’ang’ania, kweli nitaamini hawa wasichana wa mwaka wa kwanza magumashi,” alijisemea na kuachia tabasamu pana.

Alikuwa tayari kugombana na msichana yeyote katika dunia hii lakini si Paula, huyo alikuwa kila kitu kwake hivyo kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kulazimisha kupunguza ukaribu baina yake na Shadya.

Hiyo ndiyo ilikuwa hatua ya kwanza ya kumuacha msichana ambaye hukuwa na malengo naye. Kama kwa siku ilikuwa ni lazima mpigiane simu mara tano basi ilikuwa ni lazima ipunguzwe na kufika mpaka mara mbili, kama ulikuwa na haraka mno ya kujibu meseji yake kila inapotumwa, ilikuwa ni lazima upunguze uharaka, meseji moja ichukue hata dakika ishirini kujibiwa.

“Nitaanza na haya mambo mawili kwanza. Nikijidai nipo beneti naye huyu malaya anaweza kuniharibia,” alijisemea, alianza kumuita Shadya malaya kwa sababu tu alimkubalia kumvua nguo na kufanya naye mapenzi, mara mbili, ila kwenye hayo yote, hakuwa msichana wa kumuacha moja kwa moja, yaani pale ambapo angemtaka, angekuwa akimtafuta huku akimuomba msamaha.
*
*

Je, nini kitaendelea?
 
Ahsante Shunie. Ukiwaza sana khs mapenzi unaweza kujikuta unaongea peke yako njiani.
 

Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom