SEHEMU YA 72
“Kaka pale ni shida. Kama una mtoto wako, acha akasome UDOM na vyuo vingine vya Tanzania lakini si pale, kwanza wajanja lazima wang’oe, yaani utake usitake,” aliniambia.
Alinichanganya sana, alisema hapo kuna mademu wakali ile kishenzi, sikuamini sana ila nilitaka kuhakikisha kwa macho yangu. Siku moja nilimwambia kwamba nataka kwenda huko, kuwaona hao mademu, ni kweli walikuwa wazuri kweli au alinidanganya.
“Hahaha! Usije kuchanganyikiwa tu,” aliniambia huku akicheka.
Na kweli tukaenda, tulipofika huko, nilishangaa sana, macho yangu hayakutulia, ni kweli niliwahi kuona mademu wakali, wenye maumbo ila wale wa pale, duuh walikuwa balaa mno.
Watoto walijua kuvaa, kutembea, kutabasamu, wapo waliokuwa wamejazia lakini pia kulikuw na wale portable, niliwaangalia na kumuuliza ni kwa jinsi gani ningeweza kuwapata kirahisi, kama walikuwa wanahitaji pesa, nilikuwanazo.
“Tufanye house party,” aliniambia.
“Ipo vipi hiyo?” niliuliza, si unajua nilitoka kwenye maisha ya kilofa hivyo hata baadhi ya mambo sikujua kabisa.
“Yaani hiyo tunaandaa party home, kunakuwa na pombe tu, tunazichanganya kwenye ndoo moja na watu wanajichotea tu," aliniambia.
“Halafu?”
“Kunakuwa na muziki, yaani watu wanacheza, wanapiga kelele lakini mwisho wa siku wanalala,” aliniambia.
“Na ukitaka mambo yetu?”
“sasa hapo nani atakunyima? Yaani unakuwa huru, unaweza kusema namtaka huyu, unamchukua, hata wanne kwa usiku mmoja, wewe tu,” aliniambia.
Akazidi kunichanganya mno, unajua mimi mtu akishaniambia kuhusu mademu akili yangu inachanganyikiwa kabisa.
Nilimuuliza jinsi ya kuwapata hao mademu, tena wawe wakali, akasema siyo tatizo, yeye alikuwa na wake na kulikuwa na mshikaji wake ambaye naye alikuwa na mademu, yaani huyo hata ungehitaji mademu ishirini, anakuletea.
Nikamwamia ampigie simu. Ikapigwa na kumuweka loud speaker.
“Oya Juvenile...nataka niandae house party,” alisema Ndimbo, alikuwa akizungumza na huyo jamaa.
“Acha masihara...upo siriazi?’ aliuliza.
“Ndiyo! Pombe zipo za kumwaga, kama vipi tuletee mademu,wapo?” aliuliza.