SEHEMU YA 41
“Yaani tunakuwa marafiki, siku nikiwa na hamu ya kufanya mapenzi, nakupigia simu, tunaonana na kufanya, hata wewe ukiwa na hamu, unanipigia nakuja na kufanya.
Tukiwa na shida tunasaidiana, tusiwe wapenzi, ukipata mpenzi, nitambulishe, sitojisikia wivu, hiyo ndiyo maana yake,” aliniambia.
Unajua nilishtuka sana! Sikuamini kama duniani kulikuwa na kitu kama hicho. Yaani uwe na msichana, awe rafiki yako halafu ukitaka kuduu naye, unampigia simu, anakuja na kumalizana halafu hamjuani mpaka siku ambayo mwingine angekuwa na hamu.
Nilimwangalia Nurat, sikummaliza hata kidogo, maneno yale hakutakiwa kuniambia mrembo kama yeye, kwa nini tufanye hivyo na wakati nilikuwa nampenda?
“Mbona umekaa kimya?” aliniuliza.
“Unajua nakupenda sana, sasa unaposema tuwe hivyo, kwa nini usinipe nafasi tu ya kuwa nawe?” nilimuuliza.
“Edward! Mimi ni Mwarabu, najua unajua matatizo yetu! Kuwaambia kwamba nimepata mpenzi, mweusi, halafu hauna pesa, hawawezi kunielewa. Tuwe kama nilivyokwambia,” aliniambia.
Nilijifikiria sana kwa sekunde kadhaa, nikajiona ni mjinga sana kama nisingekubaliana kuwa kama alivyoniambia.
Basi nikatingisha kichwa changu na kumwambia nilikuwa radhi kuwa kama alivyosema, akaniambia twende sehemu kutembea.
“Wapi?”
“Wewe twende tu.”
Kuanzia hapo nilimuona Nurat akiwa kwenye hali ya kawaida, alikuwa na mhemko kupita kiasi.
Niliogopa, mimi na Mwarabu wapi na wapi, halafu nilishasikia kwamba watu wahivyo walikuwa wabaridi, hawakuwa kama ngozi nyeusi, hivyo niliamini hata siku ambayo tungekuwa faragha nisingeweza kufurahia kabisa.
Wakati tukitembea, alikuwa akinishika mkono, nilijitahidi kuukwepesha lakini wapi. Akakodi Bajaj, tukapanda na kuondoka mahali hapo.
Humo ndani ilikuwa balaa, yaani ndiyo niliamini kwamba siku hiyo ingekuwa ni ya kwanza kulala na msichana wa Kiarabu. Mara aniegemee, mara anishike huku na kule, yaani akaanza kuuchaji mwili wangu hata kabla hatujafika huko.
Wakati mwingine nilitamani tu ghafla bin vuu tuwe chumbani kwani nilizidiwa nguvu na kuona muda wowote ule ningemwambia dereva Bajaj atupishe na mimi ningemlipa kiasi chochote alichotaka.