Simulizi: Nilinusurika kuchomwa moto 2

Simulizi: Nilinusurika kuchomwa moto 2

Joined
Apr 19, 2023
Posts
77
Reaction score
124
NILINUSURIKA KUCHOMWA MOTO 2

IMG_7722.jpg



Kelele za watu wakiongea kwa nguvu apigwe! Apigwe! Apigwe! zilizidi. Wakati huo napambana sanaa kujitetea kuwa huyu mwizi mimi simjui, na sielewi kwanini amenitaja. Sikukubali kukalishwa chini kizembe, maana walikuwa wanasema kaa chini kaa chini! Nilijetetea kwa nguvu na kuongea kwa sauti kubwa, kwa nini mnamuamini huyu bila sababu? Mm simjui kabisaa, ana sababu zake za kunitaja anajua mwenyewe lakini mimi hapa nilikuwa mpita njia tu, kwanza naelekea kuangalia mechi pale uwanja wa CCM
Sasa wakati watu wanaendelea kunivutavuta wanipige maana kinachochelewesha zoezi hilo la mimi kuanza kupigwa kama yule mwizi baada ya kunitaja kuwa nashirikiana naye wakati mimi simjui, aliulizwa tu ulikuwa unaenda kumpasia nani mzigo aufikishe sehemu nyingine yeye akanyoosha kidole kuelekea kwangu mimi nilipokuwa nimesimama nikishangaa tu watu wanavomchezeshea kipigo (kama tulivyoona sehemu ya kwanza)
Sasa mimi kwangu kipigo bado hakijaanza kwa sababu kuna wengine wananitetea ambao waliniona nikija pale wakiongozwa na yule aliyekuwa akinisimulia
kilichotokea kuhusu huyo mwizi, ila sasa point zao zinakosa mashiko kwa sababu hawana uthibitisho kuwa sio mimi, maana hata mwizi ni kawaida kufanya hivo, anakuibia halafu anakuja kukuuliza vipi nini kinaendelea? Umeibiwa? Inabidi huyo mwizi tumsake! Na wakati huo mwizi ndo yeye
Sasa katikati ya hizo purukushani, kumbe wakati watu wanapiga mwizi na wanataka kunipiga mimi kwa sababu ya hayo mashtaka ya kushirikiana na mwizi, na wao wanaiba hapo hapo, Maana kwenye hizo purukushani simu yangu nilichomolewa bila kujua, wallet pia wakapita nayo.
Mimi niko bize na kupambana na kuokoa uhai wangu, maana maamuzi wanayotaka kuyafanya ni kutuchoma wote moto kwamba ni wezi. Na kumbe na wao wakapita na hivyo vitu vyangu,
Sasa kwa sababu nilikuwa nikitumia nguvu sanaa kujitetea, maana kweli sio mwizi, hivyo ile aibu sina, Niliwaambia
nilikuwa naenda kukutana na rafiki yangu uwanja wa CCM tukacheki mechi leo kuna mpira wa timu fulani. Wakaniambia basi mpigie simu tumuulize sisi wenyewe hapa hapa, ole wako akikukana tunakuchoma moto
Sasa si nikaingiza mkono mfukoni nitoe simu tumpigie, kumbe simu sina,
nikawaambia simu yangu aisee nimechomolewa, Aloooh kile kipigo nilikula siku hiyo sitokaa nisahau kwenye maisha yangu, waliona nawaletea mzaha Nilipigwaa, nilipigwa vibaya mnooo, mpaka nikapoteza fahamu kabisaa
Nilikuja kupata fahamu baada ya siku mbili nipo hospitali.

Na kumbe yule ndugu aliyekuwa akinitetea kuwa mimi sio mwizi maana aliniona nikija na akanisimulia kinachoendelea, baada ya kuona hawa watu wako serious wataniua, maana aliona yule mwizi halisi ameshakufa tayari kwa
kipigo japo ni alikuwa amepoteza fahamu tu, alijua na mimi hawa watu wataniua vile vile, na sasa nauawa bila sababu
Aliamua kuondoka na kwenda upande wa pili huko umbali kidogo na kupiga simu polisi, akawasistiza wawahi maana hawa watu wameshaua mtu mmoja na wa pili watamuua pia
kama polisi mtachelewa.
Japo kumbe pia na yeye hakuwa wa kwanza kupiga simu polisi kumbe na watu wengine walikuwa wameshapiga, polisi ndo akamwambia tunakuja tumeshapata taarifa.
Polisi hawakuwahi kiivo lakini wakati wanakuja walikuta nimepigwa mpaka nimepoteza fahamu huku raia
wao wakijua nimekufa kama mwenzangu, polisi walifika raia wote baada ya kuona polisi hakuna aliyebaki, wakatukagua na kugundua tupo hai wakatupeleka hospital fulani chini ya uangalizi wao Hayo alinisimulia huyo ndugu aliyenisaidia kuwapigia polisi na kwa sababu roho yake
ilimuuma sana kwa kitendo nilichofanyiwa aliamua kufuatilia Usalama wangu mpaka mwisho na baada ya kupona yeye ndo alinichukua polisi. Mungu ambariki sanaa
Yule mwizi halisi nilikuwa naye kwenye wodi moja, ni vile tu nilikuwa siwezi kuamka na kumshughulikia
Nilimlaumu sanaa kila siku nilikuwa nikimwagia matusi ya kila aina kwa ukatili alionifanyia, nilitamani nipate hata bunduki nimuwashe risasi hapo alipo, polisi walipogundua kinachoendelea waliomba tubadilishwe wodi tusikae wodi moja.
Hiyo ndo ilikuwa ponea yake maana nilikuwa
nawaza kuwa nitakuja kumfanya huyo jamaa kitu kibaya mnoo kama vipi tufe wote.
Lakini yote yaliisha nilirudi nyumbani pamoja na yule ndugu aliyekuwa akishirikiana na familia yangu kuhusiana na hali yangu.
Na sasa naendelea na maisha yangu na kwa kweli sitokuja kuisahau hiyo siku

Hii story ni tafsiri tosha ya wengi walioko magerezani na cells. Wapo wengi ambao wameingia hivi hivi, hana kosa hata robo kasingiziwa mwanzo mwisho.
Tuna kitu cha kujifunza hapaa
Eeh bhana mm sina la ziada zaidi ya kukukaribisha kwa ajili ya story nyingine kali kama hii.
 
Alaah nnge wasaka kijasusi wananchi wa ilo eneo especial uyo mzee hadi wana tambue vzuri
 
Back
Top Bottom