SEHEMU YA 133
Leo Vaileth akiwa mwenyewe nyumbani, alishangaa tu kumuona Prisca akiwa amefika pale nyumbani kwa mama Angel,
“Jamani Prisca, umekuja kufanya nini tena? Mbona hamnitakii mema na kazi yangu hii jamani!”
“Sio kwamba hatukutakii mema, ungejua ni muda gani nimekaa hapo nje ya geti lenu nikkisubiri hao mabosi wako waondoke hujui tu, yani walivyoondoka tu na mimi nimekuja, kwakweli Nyanda hatuhitaji kufa kwa umasikini wakati utajiri tunauona”
“Mimi nipo tayari kufa masikini ila kuharibu kazi yangu sipo tayari, yani kwa dawa yoyote unayotaka kuifanya sipo tayari. Na leo ningeenda pia Kanisani ila sijisikii vizuri ndiomana wameniacha, kwakweli Prisca naomba uende”
“Hapana, mimi siondoki hadi tufanye hizi dawa”
“Prisca, nitamuita mlinzi akuondoe yani sina masikhara kabisa kuhusu hilo ndugu yangu. Usinitanie ujue”
“Kheee yamekuwa hayo Nyanda?”
“Ndio, sitaki ujinga. Nawe katafute kazi halafu ufanye huo ujinga wako”
“Yani Nyanda unanijibu hivyo, ujue naweza nikakuharibia hata hii kazi ukaiona chungu!”
“Niharibie tu hakuna tatizo”
Kisha Vaileth akaenda kumuita mlinzi ili amuondoe Prisca, yani kile kitendo kilimuuma moyo sana Prisca na alisema kuwa ni lazima atalipiza kisasi.
Leo wakati Tumaini na familia yake wametoka kanisani wakapata ugeni na mgeni huyo alikuwa ni Derrick, basi Tumaini akamwambia,
“Kwanini umekuja bila taarifa?”
“Hapa ni kwa ndugu yangu ujue, sasa unataka nitoe taarifa, taarifa gani?”
Wakati wakiongea hayo mara mama Angel na familia yake nayo wakafika nyumbani kwa Tumaini, ila Derrick alipomuona mama Angel alionekana kufurahi sana kwani alimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha.
Wakati wakiongea hayo mara mama Angel na familia yake nayo wakafika nyumbani kwa Tumaini, ila Derrick alipomuona mama Angel alionekana kufurahi sana kwani alimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha.
Kiukweli mama Angel hakuipenda ile kitu hata kidogo na kujikuta tu akijitoa mikononi mwa Derrick ila Derrick alionekana kutaka kuendelea kumkumbatia ndipo baba Angel alipoamua kumuachanisha Derrick na mkewe huku akisema,
“Inatosha sasa”
Ila Derrick akasema,
“Dah shemeji, una wivu hadi kwa ndugu? Au umesahau kama huyu Erica ni ndugu yangu? Ni dada yangu huyu, baba yetu ni mmoja”
Baba Angel hakujibu kitu, basi mama Angel alisogea moja kwa moja kwa wifi yake Tumaini na kumuuliza,
“Umeanzaje kumkaribisha huyu?”
“Aaah mimi sikuelewa, ila ninachojua ni kuwa ni ndugu yako na sijui kama kuna mengine kati yenu na hata hivyo sijamkaribisha bali amekuja mwenyewe”
Muda huo Angel nae alikuja na kuwakumbatia ndugu zake kwa furaha sana kwani ni muda mrefu hajaonana nao.
Basi alimfata baba yake sasa na kuanza kuongea nae kwani Angel alimpenda sana baba yake, ni mara nyingi aliongea na baba yake na alijionea vizuri sana kwani baba yake pia alimpenda sana,
“Baba nafurahi sana kwani shangazi anakaa vizuri sana na mimi”
“Oooh nafurahi kusikia hivyo, ukimaliza shule utaniambia ni wapi unataka kwenda kutembea”
“Asante sana baba, nakupenda sana”
Basi Angel alikuwa akimkumbatia baba yake kwa furaha hadi Tumaini akasema,
“Haya sasa wapendanao wamekutana, maana nahisi Angel ndio roho ya mdogo wangu jamani”
Wote walikuwa wakicheka kasoro Derrick aliyeonekana yupo kimya toka muda ule baba Angel amtoe toka mikononi mwa mke wake.
Ila alikaa kimya kidogo na kuanza kumwambia Tumaini,
“Hey, Tumaini ulimuuliza Erica kuhusu lile swala”
“Swala gani?”
“Swala la mimba yangu”
Mama Angel akaona huyu anataka kumuharibia siku basi akainuka na kumshika mkono halafu akaenda nae nje na kuanza kuongea nae,
“Hivi Derrick una nini lakini? Hivi unajua kama ni muda mrefu sana umepita jamani, kwanini upo hivyo hadi leo eeeh!”
“Nisamehe ila najua mtoto wangu angekuwa ni mkubwa kushinda huyo Angel”
“Hivi wewe umesahau yote yaliyotokea kati yangu na yako? Kwani tulienda kufanya tambiko ili iweje jamani eeeh! Hivi wewe si kaka yangu jamani! Yani natamani marehemu baba angekuwepo na angerekebisha makosa yake, nina uhakika asingeruhusu uzaliwe mjinga wewe, hivi unaacha kufatilia maisha mengine ila unawaza ujinga tu muda wote jamani!!”
“Sikia Erica, kipindi naanza na wewe si kwamba nilitaka kukujaribu hapana bali nilikupenda kwa dhati sema ilitokea tu mimi na wewe tukawa ndugu, kweli huwa naumia hadi leo kwani leo hii ni mimi ambaye ningekuwa naishi na wewe na sio huyo kichaa Erick”
Mara mume wa mama Angel alitoka nje na kumwambia Derrick na mama Angel,
“Jamani, hivi kwanini sieleweki Kiswahili!! Derrick nakuomba umuache mke wangu tafadhali, ni ndugu yako ndio ila sikuamini ndiomana nakwambia uwe mbali na mke wangu”
Tumaini nae alitoka na kumshika mkono Derrick ambapo moja kwa moja alitoka nae nje ya geti na kumwambia,
“Derrick kwaheri, siwezi Kurusu uharibu amani ya nyumba yangu”
Kisha akaingia ndani na kufunga geti halafu akamfata mama Angel na baba Angel na kuwataka warudi tu ndani na waendelee na maongezi kama kawaida.