SEHEMU YA 79
Walijikuta wakiangaliana kwa muda kidogo kisha kila mmoja kuendelea na mambo yake ambapo Samir alikaribishwa vizuri na kiongozi wa
darasa na kuonyeshwa sehemu ya kukaa na kuendelea na masomo.
Ila leo Samir hakumfata Angel wala nini yani ilikuwa kama vile yeye na Angel ni watu wasiofahamiana kabisa, muda kidogo Samir alikuja
kuitwa na mwalimu ambapo mama yake mzazi alikuwa amekuja tena pale shuleni, ingawa ni yeye alimtafutia Samir hiyo shule ila aliamua
kurudi tena kuongea nae, basi wakaingia ofisini na kuanza kuongea na Samir ambapo mama yake alianza kumwambia,
“Naona nyumbani nimeshasema sana hadi pumu imenishika, leo nimekuleta hapa shuleni, huwezi amini nimeenda hadi stendi ya daladala
ila sijapata hamu ya kupanda gari nimeamua kuja tu kuongea na wewe, si unajua mume wangu ana usafiri lakini leo alifungia magari yote
maana hataki kusikia huu ujinga wako. Jamani Samir, leo naongea na wewe kwenye hii ofisi kwa mara ya mwisho, naongea kama mama
mwenye uchungu na mtoto wake, Samir tafadhari sitaki ujinga, yani sitaki ujinga kabisa yani kile leo nakuhamisha shule sababu ya ujinga
wako, ile shule ya kwanza ulimshika mwalimu makalio ukafukuzwa, shule ya pili ulimpiga mwanafunzi mwenzio ukafukuzwa, sasa shule ile
ya tatu umeanza kuongea na simu shuleni jamani na skendo za mapenzi zimekufukuzisha, hivi Samir akili yako ikoje? Nani aliyekuroga?
Hebu soma mwanangu, upate kazi nzuri uone kama kuna mwanamke yoyote wa kukukataa wewe Kwakweli Samir ukifanya ujinga wako na
shule hii ujue sina dhamana na wewe, yani ufukuzwe shule basi tutabaki nyumbani tukiangaliana, ujinga sitaki jamani!”
“Sawa mama, nimekuelewa na haita jirudia tena”
“Haya nipe simu yako, yani umefanya kila mtu anitukane kuwa sina malezi bora kwako hata mume wangu kanitukana mjinga wewe
umeniletea balaa tu katika maisha yangu”
Basi Samir akaitoa simu aliyokuwa ameiweka kwenye mfuko wa suruali yake, kisha kumkabidhi mama yake ambaye aliichukua na kuiweka
kwenye mkoba wake kisha Samir akaambiwa arudi darasani, kisha walimu wakaanza kumsema mama Samir,
“Ila na wewe una makosa, utamuachaje mtoto anakuja shuleni na simu? Yani sisi tungemkamata nayo u basi tusingejari ni hela ngapi
umetoa zaidi zaidi tungemfukuza shule, inaonyesha kijana wako ni kiburi sana”
“Jamani walimu naomba mnisaidie tafadhari, naomba mnisaidie, natambua kuwa nyie pia ni walezi naomba mnisaidie yani huyu mtoto
anafanya niumwe kichwa kila kukicha jamani, naomba mnisaidie walimu. Muwe nae karibu tafadhari”
Akajitokeza mwalimu mmoja na kusema,
“Usijali mama Samir, mimi nitakuwa na huyu bega kwa bega”
“Asante sana mwanamke mwenzangu, Napata shida mimi”
“Basi usijali, yani mimi ndiye mwalimu ninayeogopewa na wanafunzi wote hapa shuleni, kwahiyo usijali wala nini”
“Asante sana”
Basi mama Samir aliaga wale walimu na kuondoka zake.
Muda wa kukaribia kutoka, mwalimu ambaye alijulikana shuleni kwa jina la madam Hawa, alimuita Samir na kuanza kuongea nae,
“Sasa Samir, mimi ndio nimeachiwa wewe hapa shuleni nikuangalie na kukulea, nasikia kichwa chako hiko ni kitupu basi mimi nitakijaza maji
na mchanga ili upande uwa kichwani. Sikia nikwambie kitu, unapokuja shuleni unatakiwa uje kuniona mimi na unapoondoka shuleni
unatakiwa kuja kuniona mimi pia. Hilo sio ombi bali ni amri, sijui tumeelewana”
“Nimekuelewa ndio”
“Haya unaweza kwenda sasa”
Katika shule hii hapakuwa na usafiri kama shule zingine, kwahiyo wanafunzi waliondoka na kwenda kupanda madaladdala kurudi nyumbani
kwao niomana hata Angel alikuwa akipelekwa na dereva na kufatwa na dereva, mama Angel hakupata nafasi ya kumpeleka Angel kwenye
shule atakazo kwahiyo ilibii ampeleke kwenye hiyo shule kwani alisikia nayo inafundisha vizuri.
Basi Samir aliondoka ili kurudi kwao ila aliongozana na yule kiranja wa darasa ambaye alimkaribisha na alikuwa akiitwa Adam basi alianza
kuongea nae,
“Naona madam Hawa alikuita?”
“Ndio, alikuwa akinipiga mikwara yake”
“Ana mikwara yule madam hatari sababu anajua wanafunzi wengi tuna muogopa, ila yule madam tatizo lake hana mume”
“Kheee kwanini?”
“Sijui alitendwa huko anajua mwenyewe, yani madam ana hasira yule sijapata kuona, ukimsogelea tu utashangaa umenaswa kofi, sasa
kama kashakupiga mikwara basi ujipange ndugu yangu”
“Aaaah sawa, nimekuelewa”
Basi waliongozana na kuongea hadi stendi ya daladala na kila mmoja alipanda daladala ya kuelekea nyumbani kwao.