Simulizi: Nawapenda Mapacha Wangu

DR SANTOS

JF-Expert Member
Mar 11, 2019
7,776
13,582
SIMULIZI; I LOVE MY TWINS (NAWAPENDA MAPACHA WANGU)
MWANZO.

Dunia nzima ilisimama kushuhudia tukio la ugawaji wa tuzo kubwa za muziki zilizotolewa na kampuni kubwa ya utangazaji ya MTV yenye makao yake nchini marekani.

Hakuna aliyeweza kusubiri wala aliyekubali kupitwa na tuzo hizo hasa raia wa Tanzania kwani macho yao yote yalikua yakimtazama kijana mtanashati na mwenye kipaji cha aina yake aliyechaguliwa kugombea tuzo hizo huku akichuana na wasanii wakubwa duniani ambabo ndio nembo za muziki duniani.

Miongoni mwa watu waliokua makini na televisheni alikua ni binti mrembo Sheila ambaye hakutaka kabisa kupitwa na tukio zima la ugawaji wa tuzo.

“omg! dont be nervous laiton”. (mungu wangu! ondoa wasiwasi laiton). Alijisemea Sheila akiwa juu ya kochi aina ya sofa nyeupe huku macho yake yakiwa kwenye televisheni.

Sheila alisema maneno hayo baada ya kusikia jina la mumewe kipenzi laiton urassa au “lai boy”. Lina maarufu sana na tamu sana pindi mtu alitajapo.

Sheila alijikuta akitamani sana kuongozana na laiton kwenye tukio hilo lakini laitonn hakutaka kumruhusu kabisa kutokana na hali yake ya ujauzito, ambapo alibakiza miezi michache tu kabla ya kujifungua.

Akiwa juu ya kochi Sheila na macho yake kwenye televisheni mawazo yalimpeleka mbali zaidi ambao alianza kukumbuka siku aliyomuona laiton kwa mara ya kwanza na kutokea kuvutia nae pini alipokua kwenye starehe katika fukwe za Ibiza nchini Hispania.

“bueno diaz?”. (habari yako) aliongea Sheila mara baada ya kumuona laiton akiwa katika mwonekano ambao watu wa uswazi huenda tungeweza kumwita bishoo.

“bien, como estas!”. (salama habari ya asubuhi) alijibu laiton japo hakuielewa vizuri lugha ya kihispania lakini salamu alizijua kidogo kwani ilikua si mara yake ya kwanza kukanyaga ardhi ya Hispania .

“bien”. (njema!) alijibu Sheila huku akimkaribisha kinywaji aina ya belaire ambacho laiton alikipenda sana na mara nyingi amekua akikitumia katika video za nyimbo zake.

“you look familiar, I hope you are lai boy”. (sura yako sio ngeni, natumai wewe ndiye lai boy) alihoji Sheila huku akitoa tabasamu pana kisha kuipandisha miwani yake aina ya tinted.

“indeed! Who are you then”. (haswaa, nawe unaitwa nani”. Alihoji laiton huku akimtazama Sheila usoni kama mtu anayejaribu kukumbuka kitu.

“wewe ndiye Sheila mwanamitindo uliyebeba tuzo ya vazi bora Africa?” alihoji laiton baada ya kufanikiwa kurejesha kumbukumbu zake vema.

“ndio mimi, nimefurahi kukuona laiton, na imekua bahati sana mimi kukutana na wewe huku”. Aliongea Sheila kwa hisia kali wakati huo walikua wameketi chini ya mwavuli uliokuepo katika eneo hilo wakiendelea kupata vinywaji.

“hakika nafikiri jambo hili lilipangwa na manani, kwani sikua na mpango wa kuja huku, lakini baada ya kumaliza kurekodi video ya wimbo niliyomshirikisha rapa wa marekani niliamua kuja Hispania nipate mapumziko ya siku chache kabla ya yurudi nchini Tanzania, hapo ilinilazimu kuuliza eneo zuri la kupumzikia ndipo lnilipoletwa hapa Ibiza”.
Aliongea laiton kwa kirefu lakini hakuna hata neno moja lililomwingia akilini Sheila kwani alikua mbali sana kimawazo, hususan nafasi ya kuwa karibu na laiton ameitafuta kwa muda mrefu na hakuwahi kuipata

“eeeeh,,….naam…umesema..ibiza, ndio Ibiza”. Aliongea Sheila kwa kuuma maneno jambo ambalo laiton aliliona kisha kuachia tabasamu pana.

Kisha akamshika mkono Sheila ambaye aliinuka na kusogea karibu ya laiton ambaye alichukua simu yake na kuingia upande wa kamera kisha kupiga shelfie ambayo iliwaonesha wote wakiwa kwenye tabasamu mwanana na wakiwa na furaha ya hali ya juu.
Baada ya muda laiton aliituma picha hio kwenye mtandao wa instagram na kuandika maneno ambayo yalitosha kabisa kuutambulisha uhusiano mpya.

Sheila pia alipiga picha akiwa pamoja na laiton na kuandika maneno ambayo yalionesha wazi kwamba alikua akimpenda sana laiton na alieleza furaha yake dhahiri.

“my dream husband! But now I can realize that am not dreaming anymore”. (Mwanaume wa ndoto zangu,lakini sasa sioti tena). Aliandika Sheila katika mtandao wa instagram. Hakika ilikua ni siku ya furaha sana kwa upande wa Sheila lakini bado laiton alikua hajasema chochote kuhusiana na mapenzi mapaka inatimia jioni ya siku hiyo ambapo walikula na kisha kila mtu alienda kwenye chumba chake kwani walikua ndani ya hoteli moja.

Jambo hilo lilimuuma sana Sheila na hakuweza kuvumilia kabisa kulala siku hiyo pasina kumwambia laiton ukweli wa moyo wake hapo alichukua simu na kumigia laiton ambapo simu iliita kwa sekunde chache kisha ikapokelewa.

“haloo laiton! Siwezi lala bila kukutakia usiku mwema, nakupenda sana laiton”. Aliongea Sheila ambapo laiton alishusha pumzi ndefu na kishs kujibu.

“nakupenda pia malkia, lakini nimechoka sana leo, tutaongea kesho, kikutakie usiku mwema”. Baada ya maneno hayo laiton alikata simu na kumuacha Sheila akiwa ameikumbatia simu yake akiwa haamini kwamba kazi imekua rahisi kuliko alivofikiri.

Siku iliyofuata Sheila na laiton walifungua ukurasa moya wa mapenzi ambapo waliandika maneno mengi yenye taswia nzuri ya upendo. Na kama kikngenkua kitabu basi mnunuzi angevutiwa na ukurasa wa kwanza wa kitabu kabla hajakinunua.

Ndoa kati ya laiton na Sheila ilifungwa punde tu baada ya wawili hao kurudi nchini Tanzania, ndoa hio iliweka historia ya kutumia pesa nyingi sana kiasi cha shilingi milioni mia tatu za kitanzania kama maandalizi.

**********************************

Akiwa juu ya kochi Sheila alistushwa na sauti ya dada wa kazi aliyekua akimuuliza sababu za yeye kulia,
“dada unaumwa?” alihoji nasra aliyekua msaidizi wa kazi za ndani

“hapana mdogo wangu siumwi, naomba maji ya kunywa”. Aliongea Sheila huku akijifuta machozi yaliyomtoka baada ya kukumbuka matukio yaliyopita.

Macho yake yalitua kwenye luninga ambapo hakuamini baada ya kuona laiton amenyakua tuzo moja ya msanii bora wa kigeni.

“oooh ahsante mungu kwaajili ya mume wangu kipenzi”.aliongea kisha kivivu alinyanyuka na kwenda ndani kupumzika.

Kulikucha na hatimaye siku zilisonga, laiton akarudi nchini Tanzania, na miezi nayo ilizidi kusonga hatimaye ulifika muda wa kujifungua.

“oooh my god, she cant undergo normal delivery”.(mungu wangu hawezi kujifungua kawaida) Aliongea daktari wa masuala ya uzazi wa hospitali ya hill side iliyopo jijini johanesberg nchini afrika kusini.

“she must undergo scissor before we coud miss them all”. (ni lazima afanyiwe upasuaji kabla hatujawapoteza wote) aliongea daktari huyo kwa msisitizo wa hali ya juu.

Kisha zilifanyika jitihada za kumuokoa Sheila pia kuhakikisha anajifungua salama na hatimaye walifanikiwa kwa asilimia zote, Lakini watoto waliozaliwa ndio waliomshangaza kila mmoja kwani walikua ni mapacha walioungana.

“these are conjoined twins, another wonder of the year, oh my god”. (hawa ni mapacha waliounga, ajabu lingine la mwaka, mungu wangu!)
Aliongea mmoja kati ya madaktari waliohusika katika kuhakikisha Sheila anajifungua salama.

Itaendelea...
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom